MUME WANGU ALIVYONIACHA NA KUMUOA MDOGO WANGU
PART: 07
ILIPOISHIA,
Mnamo mida ya saa 5 za asubuhi, tulishuka stendi ya Makumbusho huku tukiwa tumebebelea vizawadi hali iliyowafanya dereva bodabda waanze kutukimbilia.
Tulisimama pembezoni kidogo mwa barabara kisha tukaanza kujipangusa vumbivumbi. Ndipo nilipopatwa na mshangao na mshutuko mkubwa sana huku nikiwa siamini nini macho yangu yanaona.
Nilidondoka chini kwa mshutuko huo huku mama Suzi akibaki na mshangao ..
SONGA NAYO….
Mapigo ya moyo yalinienda mbio sana mpaka nikaona kama roho yangu inataka kuchomoka.
Ni.kama nilikuwa naota vile lakini nilichokiona hakukuwa ndoto.
Nikiwa bado najitambua, niliwaona watu wakiwa wamenizunguka huku wakinipepea .
Kadri mda ulivyozidi kusonga mbele, ndivyo kumbukumbu zilivyozidi kuruka kichwani mwangu.
Mnamo mida ya saa 12 za jioni, nilijishangaa kijikuta nimelazwa kwenye hospitali ya Mwananyamala huku kwa pembeni nikimuona mama Suzy.
Nilimuuliza,
“Nimefikaje hapa?”
“We acha tu, yaani bora umezindukaa!, nilikuwa natetemeka kweli sijui ulipatwa na nini!”
“Mhh!..pole shoga angu …sasa hivi niko vizuri tunaweza kuondoka…”
“Ngoja nikamuite nesi maana aliniambia ukizinduka nimuite…”
“Sawa mimi niko vizuri..:
Mama Suzy alifungua mlango kisha akaondoka chumbani humo na baada ya dakika kama 5 hivi, aliambatana na Nesi mpaka nilipokuwa.
“Unajisikiaje?” Nesi aliniuza
“Niko vizuri…”
“Sawa. Sasa unatakiwa kupumzika nyumbani na upunguze mawazo kichwani mwako. Inaonekana ulipata mshutuko wa moyo . Huu siyo ugonjwa bali ni hali ambayo humpata mtu yeyote punde aonapo kitu cha kushangaza “aliongea.
“Asante nimekuelewa..” nilimjibu kisha tukaondoka na mama Suzy kurejea nyumbani.
Wakati tuko njiani , mawazo makali yalinijia kichwani mwangu mpaka nikashindwa kutembea na kujikuta namwaga machozi.
“Shoga umekuwaje? , au turudi hospitali” aliniuiza huku akiwa amenishika mkono.
Nilikosa nguvu za kumwambia chochote. Nilipangusa machozi yangu kisha tukaanza kutembea mpaka kituo cha daladala za kuelekea Posta.
Mda si mrefu, tulifika kivukoni kisha tukayakata maji mpaka makazini kwetu kigamboni.
“Shoga umepatwa na nini mbona hutaki kunambia?” Aliniuliza.
Nilitamani kumwambia lakini roho yangu ilisita kwani nilikuwa bado siamini kabisa. Nilishika simu yangu kisha nilkampigia mme wangu Daudi lakinì hakupokea kwa mda huo.
Kwa machungu makali sana, nilirusha kisimu changu chini mithili ya tenesi ndipo mama Suzy alipozidi kunishangaa.
Sikuona umuhimu wowote wa kuwepo duniani kwa uchungu niliokuwa nao siku ile mpaka kinywa changu kikawa kichungu.
“Niache kwanza nipumzike..” nilimjibu huku mschozi yakiwa yananitiririka.
“Shoga! kwanini hutaki kuniambia?, usikae na kitu moyoni mwako ni bora ukanishirikisha tuone tunafanyaje. Kumbuka we ni mjamzito hivyl hutakiwa kuwa na huzuni wala mshutuko wa namna hii..kwani utamuathiri mtoto tumboni..:”
“Shoga mimi nilo vizuri wala usiwe na shida…”
“Haya!, ngoja nikuache upumzike nami nikawapikie watoto wangu”
“Sawa ila naomba unisamehe kwa kutokusindikiza..”
“Wala usijali haina shida..” tuliagana kisha akaondoka kuelekea nyumbani kwake.
Nikiwa peke yangu nyumbani humo, nilijiuliza maswali mengi kipi nafaidi duniani hapa?, hasira zangu zilinipeleka mbali sana lakini nikakumbuka usemi usemao ” usifanye maamuzi yoyote wakati una hasira sana au wakati unafuraha sana”.
Nilijituliza kisha nikaenda kitandani kulala kwani siku hiyo sikuwa hata na hamu ha kula chakula.
Nililala mapema sana sikupata usingizi hata kidogo kwani kila nilipojaribu kusinzia, niliijiwa na taswira ya kile nilichokiona mchana.
Niliamka mnamo mida ya saa 4 za usiku kisha nikampigia mme wangu kwa mara nyingine ndipo alipokata kisha akanitumia meseji,
“Nitumie meseji nipo kwenye kelele kidogo..”
“Sawa upo wapi mpenzi wangu?”
“Si nililkwambia mchana kuwa nimesafiri kikazi kwa mda wa siku 3 mpaka 4!?, au unamatatizo ya kumbukumbu…:
“Hujaniambia uko mkoa gani”
“Nipo Morogoro kwani kuna shida gani”
“Hapana hakuna shida yoyote…”
“Sawa unalingine?, maana nataka nilale mapema leo..”
“Hivi mme wangu unanipenda kweli?”
“Maswali gani unauliza kila siku?, ningekuwa sikupendi ningekuoa!, nilliwaacha wangapi tena warembo kuliko hata wewe lakini nikakuchagua wewe. Nimechoka sasa!, unataka nikupende kwa namna ipi?, au nichomoe moyo wangu nikupe ndo uamini kuwa nakupenda?.
“Siyo hivyo mme wangu, nakupenda sana ndo maana nakuulizia maswali hayo…”
“Asante mke wangu kipenzi nami nakupenda sana. Nikuletee zawadi gani nikirejea?”
“Asante kwa sasa sihitaji zawadi yoyote ile”
“Kwanini tena mke wangu?”
“Basi tu!, ila nikwambie kitu?”
“Sawa niambie…”
“Au ngoja niache nitakwambia ukirejea..”
“Niambie mda huu kipi hicho”
“Basi tu ila nit…”
Nilishindwa kuendelea na kuchati ndipo nilipoamua kufanya maamuzi magumu sana ambayo hayatosahalika wala kufutika.
Nilichukua kalamu na karatasi kisha….
PART: 08
ILIPOISHIA,
Nilishindwa kuendelea na kuchati ndipo nilipoamua kufanya maamuzi magumu sana ambayo hayatosahalika wala kufutika.
Nilichukua kalamu na karatasi kisha….
SONGA NAYO…
Wakati naanza kuandika wosia wangu na chanzo cha kifo changu, gafla roho yangu ilinusuta ndipo nilipiweka kalamu chini na kuchana kikaratasi hicho.
Bila kupoteza mda, nilianza kukusanya nguo zangu na vitu vyangu vyote kisha nikavufungasha katika sehemu moja.
Kesho yake asubuhi na mapema, nilienda kumuaga mama Suzy ambaye kiukweli ni rafiki yangu wa kufa na kuzikana .
Baada ya kufika kwake, alinikaribisha huku akionesha kama kuna jambo anataka kuniuliza hivi.
“Shoga hujaniambia tatizo lako ni nini?” Aliniuliza.
“Nitakwambia kwa simu. Mda huu narudi nyumbani sijui kama nitarudi tena hapa nyumbani..”
“He!, jamani shoga!, kwani shida nini?” Aliniuliza kwa sauti ya huruma.
“Ebu naomba simu yako nione kidogo maana ya kwangu haina mtandao wowote wa kijamiii”
“Kuna mtu kakutukana kwenye mitandao?” Aliniuliza kisha akanipatia simu .
“Wala siyo hivyo…” nilimjibu kisha nikasevu namba ya mme wangu kwenye simu yake.
Baada ya hapo, niliingia whatsap status ndipo nilipokuta amepost picha ya mdogo wangu Delila wakiwa wote
Niliishiwa nguvu kabisa lakini niliendelea kupekua kwenye akaunti ya instagram ya Delilla ndipo nilipokutana na picha nyingi za mme wangu akiwa amepost wakiwa maeneo mbalimbali.
“Shoga angu!, hivi kama ni wewe unaweza kufanyaje?” Nilimuonesha picha zile huku machozi yakinidondoka
“Hivi huyu si mdogo wako?!” Aliongea kwa mshutuko.
“Ndiyo ni mdogo wangu wa tumbo moja na baba mmoja”
“Makubwa! Anavaaje hivi mbele ya shemeji yake! Halafu wanaenda mpaka beach bila wewe kujua!, hapa kuna kitu…” alitamka.
“Juzi alinidanganya kaenda kazini morogoro lakini ile jana nilimuona kwa macho yangu akiwa anaongozana na Delila halafu amevaa kinguo kidogo mpaka aibu. Nilishindwa kuangalia ndo maana nilipatwa na mshutuko”
“Jamani pole sana. Duniani kuna mengi,. Hakika waliosema kua uyaona hawakukosea..”
“Sasa mimi nataka niondoke ili akae naye kwa amani. Kama kanichoka siwezi kumlazimisha. Kinachoniuma sana, ukweni wananipenda sana na nyumbani wanampenda sana..”
“Shoga usifanye hayo makosa!. Utavunja ndoa yako!, hapa kaeni muyamalize. Haya ni mambo yakawaida kwenye ndoa..”
“Sasa unataka nifanyeje?”
“Tulia nyumbani afu jifanye hujui chochote. Atakaporejea, usimwambie chochote kile halafu mshawishi mwende nyumbani kwenu..”
“Mhh!, shoga nami nina moyo! Yaani siku zote nimsubirie mtu ambaye yupo anafanya upumbavu afu aje kunipaka uchafu wake!”…
“Hapana siyo hivyo, najua atakubali kwani atataka kukuridhisha..”
“Kwahiyo nyumbani nisiende?”
“Nyumbani kufanya nini?, ukitoka hapa mnaenda kwao ndo utamwambia mama mkwe na baba mkwe wako..”
“Mhh..mbona kama naona aibu kuongea na baba mkwe?”
“Wala hakuna haja ya kuongea naye, ukishaongea na mama mkwe ujumbe utafika tu…”
“Hapo sawa…”
“Ndo hivyo shoga vumilia maana ndoa ni mtihani…”
“Ila …!, sijui…” nilitamka kisha tukaagana nami nikarejea nyumbani.
Baada ya siku 5 , mme wangu alirejea nyumbani akiwa amebebelea zawadi huku akiwa amenyoa vizuri na kuvalia nguo mpya.
“Karibu sana mme wangu!, nilimkumbatia huku nikijitahidi kuonesha uso wa furaha lakini moyo wangu ulikuwa unavuja damu ya huzuni na maumivu makali.
Nikiwa nimemkumbatia, nilishindwa kujiuzuia ndipo nilipojikuta namwaga machozi mbele yake.
Aliniangalia kisha akaniuliza,
“Unalia nini?”
“Nimekumi…si..ii s..a..an.a mme wangu” nilimjibu
“Pole mke wangu kipenzi, asante pia kwa upendo wako” alijibu kisha akanibeba kama mtoto.
Baada ya mda, niliandaa chakula huku nikiwaza kumfanyia kitu kibaya tumalizane.
Wazo la karibu, lilikuwa kumkatata mashine yake au nimwagie maji ya moto lakini nikakumbuka mtoto wangu aliyeko tumboni akiniuliza baba yuko wapi nitamjibu nini?.
Swali hilo lilinifanya nishindwe kutekeleza wazo langu.
Chakula kiliiva kisha nikapakua na tukaanza kula ndipo nilipomwambia,
“Sorry mme wangu nadhani ni mda mrefu tumeenda kuwaona wazazi ( mama mkwe na baba mkwe) unaonaje twende siku mbili tatu hizi?” Nilimuuliza.
“Umewaza nini mpaka ukanambia hivi?” aliniuliza huku akiwa na sura ya tabasamu
“Jamani kwani vibaya? , isionekane tunaenda kwetu tu halafu upande wa wazazi wako hatuendi”
“Leo umeongea point kubwa sana…”
“Jamani mme wangu! Sasa tunaenda lini? Maana natamani twende hata kesho…'”
“Kesho tena!, kweli unaharaka …”
“Yaani nimemmis sana mama mkwe..”
“Ohoo sasa twende kesho kutwa. Kesho iwe siku ya kununua vizawadi si unajua huwezi kwenda mikono mitupu?”
“Vizuri siyo mbaya…'”
Baada ya mazungumzo hayo, moyo wangu kwa mbali ulifurahi mara baada ya kuona mtego wangu unakwenda kumnasa vizuri.
Usiku tukiwa tumelala, aliaogelea kisha akaniomba mechi ya kirafiki ndipo nilipomjibu
” sorry mme wangu sijiaikii vizuri kwa leo najihisi kichefuchefu na maumivu ya mgongo”
” Haya sawa mke wangu” alitamka huku nikiwa na hasira kali sana dhidi yake na laiti angejua basi asingeweza hata kunisogelea.
Kesho yake kulipambazuka vizuri ndipo maandalizi ya kwenda ukweni yalipoanza huku niki….
PART: 09
ILIPOISHIA,
Baada ya mazungumzo hayo, moyo wangu kwa mbali ulifurahi mara baada ya kuona mtego wangu unakwenda kumnasa vizuri.
Usiku tukiwa tumelala, aliaogelea kisha akaniomba mechi ya kirafiki ndipo nilipomjibu
” sorry mme wangu sijiaikii vizuri kwa leo najihisi kichefuchefu na maumivu ya mgongo”
” Haya sawa mke wangu” alitamka huku nikiwa na hasira kali sana dhidi yake na laiti angejua basi asingeweza hata kunisogelea.
Kesho yake kulipambazuka vizuri ndipo maandalizi ya kwenda ukweni yalipoanza huku niki….
SONGA NAYO..
Mambo yote yalinyooka na kukaa sawa kama ilivyotakiwa huku moyo wangu ukiwa unavuja damu kwa ndani.
Tukiwa ndani tumekaa, mama alinipigia simu na kunijulisha kuwa tayari Delila kashafika nyumbani hivyo nisisumbuke kumuulizia.
Nilishukuru kwa taarifa hiyo ambayo sikutaka hata kuisikia kwani kama ingewezekana bora angepata ajali akavunjika miguu yote ili kabisa.
Nilitamani kumwambia mama juu ya kile kinachoendelea, lakini nilijiuzia kwani kufanya hivyo kungeharibu ratiba yangu ya kwenda ukweni na mme wangu.
Wahenga wasema, ” hakuna marefu yaso na ncha na kile lenye mwanzo lina mwisho wake” .
Hatimeye safari nilokuwa nimeisubiria kwa hamu zote, iliwadia kuelekea ukweni mkoani Dodoma.
Mnamo mida ya saa 11 za jioni, tulikuwa tumewasiri nyumbani kwa mme wangu ambapo tulipokelewa kwa mikono miwili kama ilivyokuwa siku zote.
Ama kweli mama mkwe alikuwa ananipenda sana mpaka nikawa namuona kama mama yangu mzazi.
Niliwasalimia mashemeji zangu, baba mkwe na ndugu wote wa mme wangu. Wakati natoa salamu, uchungu ulinizidia moyoni mwangu mpaka nikashiindwa kuubeba ndipo nilipomwaga machozi mbele ya baba mkwe na mama mkwe.
Hali hiyo iliwashangaza wengi mpaka wakabaki wamenishangaa. Hakika ukiona nyani mzee, jua kakwepa mishale mingi sana.
Mama mkwe alinishika mkono kisha tukaelekea jikoni ambako kulikuwa na jamvi.
Tuliketi chini huku akiniangalia kwa macho ya mshangao,
“Umepatwa na nini au uchungu wa mimba?” Aliniuliza huku akiwa amenishika mgongoni mwangu.
“Mama…!, nashindwa hata nianzie wapi kukwambia!, nina uchungu mzito sana ambao umenishinda kuuzuia..” nilimwambia
“Shida nini ! Mbona mmekuja vizuri?” Aliniuliza.
“Mama!…kwa hali ya kushangaza na kustaajabisha, mme wangu anampenda na kutembea na mdogo wangu ambaye alikuwa nyumbani kwa mda. Mara ya mwisho aliniaga kuwa kaenda kazini Morogoro lakini kwa hali ya kushangaza, nilimuona akiongozana na mdogo wangu ambaye naye alidai anaenda nyumbani. Nina ushahidi wa picha ambazo wamepiga wakiwa kwenye fukwe…na maeneo mengine ya starehe..”
“Hee!..Daudi huyuhuyu!, “?alitamka kwa mshangao.
“Ndiyo huyuhuyu na picha zake ninazo” niliongea kisha nikamuonesha picha ambazo nilikuwa nazo kwenye simu yangu.
Mama mkwe alibaki ameshika tama huku akiwa kama anatetemeka hivi.
“Tulia mwanangu!, hatuwezi kufumbia macho kitendo hiki. Katufedhehesha sana tena sana ila …atajuta..ngoja nikamwambie baba yake. ” alitamka kisha akaingia ndani.
Nilibaki jikoni nikiwa nimeshika tama ndipo mme wangu aliponifata na kuniulizia,
“Umepatwa na nini mbona unalia na kushika tama?”
Sikumjibu chochote kwani ningeweza kumtolea maneno makali sana.
Mda huohuo, baba mkwe alimuita Mme wangu Daudi ambaye kwa mbali alionekana kuanza kuwa na wasiwasi.
Nami niliitwa kisha wote tukaenda kuketi sebuleni.
Tukiwa tumeketi, niliona wazee watatu wakiwa wameshikilia mikongojo na kuingia ndani.
Niliwasalimia nao wakaitikia.
“Sasa wazee wangu nimewaita hapa ili mnisaidie balaa ambalo limetokea nyumbani kwangu” Baba mkwe alitamka.
Sawasawa…” waliitikia.
“Kuna nini …?” Mme wangu aliulizia
“Unajifanya hujui kinachoendelea!, mama ebu ongea shida yako…” baba mke alitamka.
Baada ya kupewa nafasi hiyo, niliweka wazi kila kitu huku mme wangu akiwa ameinamisha kichwa chini.
Baada ya kumaliza walimuuliza,
“Wewe mtoto!, unapata wapi nguvu ya kutenda laana hii!, unaanzaje kuwa kwenye mahusiano na ndugu wa mke wako ambaye umemuoa tena kwa kufunga ndoa!, unataka kutuletea balaa nyumbani hapa!, sasa tunataka ukiri mbele yetu juu ya mahusiano yenu na shemeji yako huyo” Baba mkwe aliongea kwa hasira
“Hee!, kwanza nashangaa sana kusikia taarifa hizi, sijui chochote kile na wala sina uhusiano wowote na mdogo wake. Anachokiongea hapa ni uongo mtupu akiwa na lengo chagu la kunichafua..” alijibu huku akiniangalia kwa jicho kali.
“We kijana!, unadhani huyu ni kichaaa!; mapenzi hayafichiki siku zote! , akuchafue kwa lengo lipi?. Umekosea sana tena sana, umeingiza ugomvi mkali sana kwa ndugu hawa lakini ebu fikiria nyumbani kwao wakijua taarifa hii utaficha wapi sura yako?!, umetuvua nguo zote!, mbona unaonekana kijana mstaarabu na mwenye heshima kumbe una mambo ya hovyo kiasi hiki…hee! We kijana” wazee walitamka kwa msisitizo huku wakiwa wamemnyooshea kidole..
“Mbona mnanihukumu kwa jambo la uongo wala nisilolijua!, aliyoyaongea yote ni uongo! , ni kweli sikuwepo nyumbani kwa siku nne ila nilikuwa kikazi Morogoro na nilimuaga sasa nashangaa kusikia taarifa hii. Kama anachoongea ni kweli, alete ushahidi hata wa picha nikiwa na mdogo wake anayemuongelea..”
Alitamka huku akiwa hajua kama nina picha zake zote tena wakiwa wamekunbatiana.
” Naomba niwaoneshe ushahidi wa picha ambazo amesema nioneshe” nilitamka kisha nikafungua simu yangu ndipo mme wangu alipobaki ameduwaa huku akiwa ametoa macho….
PART: 10
ILIPOISHIA,
“Mbona mnanihukumu kwa jambo la uongo wala nisilolijua!, aliyoyaongea yote ni uongo! , ni kweli sikuwepo nyumbani kwa siku nne ila nilikuwa kikazi Morogoro na nilimuaga sasa nashangaa kusikia taarifa hii. Kama anachoongea ni kweli, alete ushahidi hata wa picha nikiwa na mdogo wake anayemuongelea..”
Alitamka huku akiwa hajua kama nina picha zake zote tena wakiwa wamekunbatiana.
” Naomba niwaoneshe ushahidi wa picha ambazo amesema nioneshe” nilitamka kisha nikafungua simu yangu ndipo mme wangu alipobaki ameduwaa huku akiwa ametoa macho….
SONGA NAYO….
Taratubu nilifungua simu yangu sehemu ya Gallery kisha nikaweka picha zote hadharani. Nilimkabidhi mama mkwe ili awaoneshe kwani nilijihisi aibu kwa jinsi picha zile zilivyokuwa.
Mama mkwe aliwapatia simu hiyo na kuwaonesha picha hizo ndipo walipopigwa na butwaa kwa mshangao mkubwa sana.
“Hee!, mwanangu!..mwanangu!..haya njoo uangalie ulchokifanya” Baba mkwe alitamka kwa sauti ya juu.
Waliendelea kuangalia picha moja baada ya nyingine huku wakiishia kutikisa vichwa. Kwa pembeni, mme wangu alionekana akitetemeka kwa mbali huku akiwa ameinamisha kichwa chini.
“Njoo uangalie mbegu uliyoipanda…” wazee walimwambia.
Licha ya kumwambia hivyo, alishindwa hata kuamka sehemu alipokuwa ameketi. Aibu kali ilimuandama usoni mwake mpaka kwa mbali nikamuonea huruma kwa jinsi alivyokuwa anaonekana.
“Sasa nadhani tusipoteze mda wala kuendelea kujadili jambo ambalo liko wazi. Kijana huyu anatakiwa kukiri mbele yetu kwa kosa lake alilolifanya nasi tutaamua adhabu ipi tutampatia. Hatuwezi kufumbia macho tabia hii ya hovyo kabisa. Nilikuwa nakuona kijana mwenye heshima kubwa kumbe hovyo kabisa.Sasa nataka utamke kwa kinywa chako una mahusiano gani na shemeji yako?” Mzee mmoja aliyekuwa ametinga miwani, alitamka.
“Naomba mnisamehe!, ni kweli picha ni zangu lakini sina uhusiano naye wowote. Ilitokea tu tukapiga picha..” mme wangu alitamka kwa sauti ya chini mithili ya mtu aliyebanwa koo.
“Hee!, unatuchukulia sisi watoto wadogo!, ebu kuwa na heshima kwa mvi na upala wetu. Mwanamke huyu kakuheshimu sana ndo maana kaja kukushtaki hapa ili muyamalize kwa amani. Sasa unapoendelea kukataa unamaanisha nini! Nakuuliza unamaanisha nini? Alitamka
“Naomba msamahq mnisamehe sitorudia tena..” mme wangu alijibu
“Kwanza kabla ya kuomba msamaha tunataka kujua unamahusiano yapi na shemeji yako?” Wazee walizidi kumuuliza maswali.
“Kwakweli niwe tu mkweli, ni shetani alinipitia wala sikuwa mimi kabisa..” alijibu.
“Shetani yupi huyo!, huyu ni nani?” Walimuuliza.
“Ni mke wangu…” alijibu
“Unampenda humpendi?”
“Nampenda sana tena nayeye analijua hilo…”
“Ulichomfanyia unahisi anajisikiaje mpaka sasa”
“Naomba mnisamehe, nimetenda kosa ila naapa mbele yenu sitorudia tena..”alitamka.
Baada ya kutamka hivyo, wazee walitoka nje kama dakika 5 hivi kisha wakaendelea na mazungumzo,
“Sasa unatakiwa kupiga magoti mbele ya mke wako halafu uombe msamaha kwa kukiri makosa yako” walimwambia.
Kinyonge sana, alinyanyuka kisha kisha akapiga magoti mbele yangu na kuanza kutamka,
“Nimekukosea sana, nakuomba unisamehe sitorudia mke wangu” alitamka lakini sikumjibu chochote.
“Mama umepokea msamaha au bado?” Waliniuliza.
“Namjua vizuri, haya aliyotamka hapa , kaongea ili yaishe lakini ukweli dalili nilianza kuziona mda mrefu japo sikuwahi kumuwazia hivyo. Kusema eti ameomba msamaha, haitoshi bali hata mdogo wangu anapaswa kuwepo ili naye aulizwe kama kweli wanapendana au la” nilitamka.
“Umeongea pointi nzuri, hatuwezi kumaliza tatizo kwa upande mmoja tu. Tutakuwa tumejidanganya na tutakuwa tumefanya kosa kubwa, wanatakiwa kukalishwa wote sehemu moja ili tumalize tofauti zao” mzee mmoja aliongea.
“Mhh…yakifika huko si itakuwa aibu tena!” Mama mkwe alitamka.
“Kama ni aibu tayari ishatokea!, lengo letu ni kuhakikisha tofauti zao zinamalizika kwa amani. Hakuna namna yoyote ile yakumaliza mzozo huu bila kwenda kukaa na wazazi wa mwanamke …” Mzee alitamka.
“Samahani naomba tusifike huko kwani naheshimika sana ukweni. Mtakuwa mmenipa adhabu kubwa maishani mwangu ambayo itanishinda kuibeba:” mme wangu alitamka
“Kama unaheshima ukweni kuna mtu kaivunja? umeivunja mwenyewe! lazima twende tena bila kupoteza mda twende kesho kutwa na nauli ya kwenda na kurudi utalipia kama faini. Kama utashindwa kufanya hivyo! , utatengwa moja kwa moja na wanaukoo wote katika maisha yako yote” Mzee alitamka.
“Lakini mimi sioni kama kuna haja ya kwenda huko, kwakuwa mmeshaliongelea na yeye kakiri, ;basi yaishie hapa” mama mkwe alitamka.
“Unatetea nini! , unamuhurumia nini!, wewe ndo unamkingia kifua!. Sina huruma wala msamaha kwa mambo ya fedheha na kipuuzi kama haya. Lazima liwe funzo hata kwa wadogo zake.” Baba mkwe alimfokea mama mkwe.
Mama mkwe alikaa kimya na kushika tama mithili ya mtu aliyefiwa.
“Sasa unatakiwa kutoa kiasi cha sh. Laki 7 kama adhabu na nauli ya usafiri wa kutoka Dodoma mpaka Tanga” mzee alitamka.
“Jamani naomba msamaha wenu!, sitorudia tena naapa mbele yenu…” aliongea
“Hakuna aliyekutuma kufanya ujinga wako! wala hakuna mtu anayetaka kukukomoa bali ni kwa nia njema yakuhakikisha ndoa yenu inakuwa na amani. Ongea na mke wako kama atakubali yaishie hapa au mpaka mwende kwao ila kwa upande wangu kwenda lazima”Mzee alitamka.
Baada ya kauli hiyo, mme wangu alinyanyuka na kunifuata ndipo nilipowaza uamuzi gani nitoe….
PART: 11
ILIPOISHIA
“Sasa unatakiwa kutoa kiasi cha sh. Laki 7 kama adhabu na nauli ya usafiri wa kutoka Dodoma mpaka Tanga” mzee alitamka.
“Jamani naomba msamaha wenu!, sitorudia tena naapa mbele yenu…” aliongea
“Hakuna aliyekutuma kufanya ujinga wako! wala hakuna mtu anayetaka kukukomoa bali ni kwa nia njema yakuhakikisha ndoa yenu inakuwa na amani. Ongea na mke wako kama atakubali yaishie hapa au mpaka mwende kwao ila kwa upande wangu kwenda lazima”Mzee alitamka.
Baada ya kauli hiyo, mme wangu alinyanyuka na kunifuata ndipo nilipowaza uamuzi gani nitoe….
SONGQ NAYO….
Hakika ulikuwa wakati mgumu sana juu ya uamuzi gani nichukue kwa wakati huo kwani mme wangu alikuwa anatia huruma kwelikweli.
Nikiwa bado najifikiria nini niamue wakati huo, alinifuata na kukaa pembeni mwangu lakini wazee walimwambia asogee mbali na mimi,
“Usimlazimisha acha aamue mwenyewe!, mama tunakusikiliza .” Walitamka.
“Samahani naomba nijifikirie kidogo ..” niliwajibu.
“Sawa haina shida hata ikiwa kesho kikubwa amani itawale..”walitamka.
“Asante…”
“Sasa sisi tunaondoka, baada ya majibu mtatuita tuone umeamuaje..” walitamka kisha wakaondoka huku nikibaki na mama mkwe pamoja na mme wangu Daudi.
Baada ya mda mfupi, mama mkwe aliniita kisha akanipeka jikoni na kuanza kuniambia,
“Sasa kwakuwa amekiri na kuomba msamaha kwanini yasiishie hapa halafu hiyo pesa ambayo ingetumika kwa nauli isitumike kwa mambo mengine?”
“Mama ni kweli lakini utu na heshima yangu ni muhimu kuliko hata hizo pesa. ..” nilimjibu.
“Kwahiyo umeamuaje?”
“Halmashauri ya kichwa changu inanisukuma twende mpaka nyumbani ili mdogo wangu pamoja na mme wangu waonywe mbele ya hadhara..” nilitamka
“Mhh…!, mwanangu haya mambo ya ndoa usipende kuyaweka sana wazi kwani siyo kila mtu anakutakia mema. Wengi wao wanatamani kuwaona mkiachana halafu wawacheke.”
“Lakini mama!, tusipoongea kwa pande zote 2 ina maana mdogo wangu atakuwa tayari kuachana na mme wangu?” Nilimuuliza.
“Ebu ongea na mme wako kwanza ila nakushauri yaishie hapahapa kama ni faini alipe…” akitamka.
Baada ya kauli hiyo,
Mme wangu aliyekuwa ameegamia ukuta huku akionesha sura ya huzuni kweli, aliniita kwa sauti ya chini,
Sikukataa wito, nami nilienda mpaka alipokuwa amesimama ndipo alipoanza kuniambia,
“Mke wangu kipenzi, nimekukosea sana tena sana!, nakuomba unisamehe maana nami ni binadamu tuliombwa kukosea.”
“Ulikosa nini kwangu mpaka unaamua kutembea na mdogo wangu?” Nilimuuliza
“Ni bahati mbaya tu ilitokea ila sikuwa na lengo hilo…”
“Bahati mbaya!..yaani mnaenda kupiga picha, mnaongozana huku mkiwa mmevaa nguo za ajabu hiyo ndo bahati mbaya..!, ” nilitamka kwa mshangao mkubwa
” Samahani lakini hivi ni nani aliyekupa taarifa hii…?” Aliuliza
“Kwo unadhani mie nilikuwa sijui?, kila sehemu mliyokuwa mnaenda nami nilikuwepo mpaka hotel mliyokuwa mnalala hapo Nakumbusho naifahamu mpaka namba ya chumba…” nilimjibu
Baada ya kumwambia hivo, alinywea mithili ya panya aliyedondoka kwenye ndoo ya maji . Aliinamisha kichwa chake chini huku akiwa hawezi kuniangalia.
Mda si mrefu, alipiga magoti mbele yangu huku kwa mbali machozi yakimlenga ,
“Kama maji yashamwagika, hayawezi tena kuzoleka, nipo tayari kukupa chochote lakini tusiende ukweni”
” Kwani unaogopa nini?” Nilimuuliza
“Hivi unahisi nitaongea nini mbele ya baba mkwe na mama mkwe?
“Kwani ulikuwa hujui wakati unakula raha zako?”
“Hapana sikujua kama mambo yatakuwa hivi, na laiti ningejua nisingefanya haya yote…nisamehe mke wangu…” alitamka.
“Bahati nzuri mama na baba ni watu wastaarabu wasio na hasira wala ugomvi hivyo haina shida tutaenda tu…” nilimjibu.
“Jamani unataka nifanye nini ili uone niluvyojutia makosa yangu?, naumia sana na najutia sana kwa hili…” alijibu.
“Nikuulize swali?”
“Sawa niulize…”
“Kwanini ulinikataza nisitumie mitandao ya kijamii?”
“Nilifanya hivyo ili wasikutongoze maana wewe ni mzuri sana..”
“Ndo lengo lako kuu hilo?” nilimuuliza
“Ndiyo….:
“Sawa, mdogo wangu umelala yane mara ngapi?”
“Mara mbili tu wala siyo nyingi…”
“Hee!..nilitaka nikusamehe lakini kwa uongo huu acha twende nyumbani…”
“Ngoja niongee ukweli mke wangu!, ni mara 4 tu huo ndo ukweli”
“Ulipata kitu gani kipya ambacho sina?
Hakujibu chochote alibaki kimya ndipo nilipomuuliza tena,
“Kama akikwambie anakupenda mpaka mda huu upo tayari kukaa na kumkana? Nilimuuliza
“Yaani mda huu sitaki kumsikia hata kidogo!, namba yake nimeshafuta na nimemwambia asinitafute tena..”
“Nitaaminije? Nilimuuliza
“Amini mke wangu siwezi kurudia makosa mara 2 “aliongea
Wakati tupo kwenye mazungumzo hayo, baba mkwe akitokea kuwasindikiza wazee, aliniita kisha akaniuliza,
“Umeamuaje?!, tunataka tujipange mapema kwa safari ikiwa ni pamoja na kuwataarifu wazazi wako”
“Nilikuwa najiuliza lakini kaniomba msamaha na kuniahakikishia hatorudia kosa..” nilimjibu
“Wanaume unawajua?” aliniuliza
Nilibaki nimeinamisha kichwa chini kisha nikamuuliza baba mkwe,
“Samahani baba, wewe unanishaurije?”
“Sinaga mjadala wala kulea tabia za kipuuzi, kawapigie wazazi wako kuwa tunakuja japo usiwambie tunakuja kufanya nini” aliniambia ndipo…..
PART: 12
ILIPOISHIA,
Wakati tupo kwenye mazungumzo hayo, baba mkwe akitokea kuwasindikiza wazee, aliniita kisha akaniuliza,
“Umeamuaje?!, tunataka tujipange mapema kwa safari ikiwa ni pamoja na kuwataarifu wazazi wako”
“Nilikuwa najiuliza lakini kaniomba msamaha na kuniahakikishia hatorudia kosa..” nilimjibu
“Wanaume unawajua?” aliniuliza
Nilibaki nimeinamisha kichwa chini kisha nikamuuliza baba mkwe,
“Samahani baba, wewe unanishaurije?”
“Sinaga mjadala wala kulea tabia za kipuuzi, kawapigie wazazi wako kuwa tunakuja japo usiwambie tunakuja kufanya nini” aliniambia ndipo…..
SONGA NAYO…
Kauli hiyo ilizidi kunichanganya kabis kwani moyoni mwangu nilikuwa nimesharidhia kumsamehe mme wangu lakini kauli ya baba mkwe , iliniacha njia panda kabisa.
“Lakini kama baba yake mzazi anasema mwanaye aende kwanini nimsamehe?, na nisipomsamehe itakuwaje?, maana mama mkwe yupo upande wa mme wangu” nilijiuliza lakini sikupata jibu lolote.
Kichwa kiliuma kwelikweli ndipo nilipoamua kufanya maamuzi magumu kama moyo na nafsi yangu ilivyonituma.
Nilipiga hatua kadhaa kutoka nyumbani hapo ili wasisikie nini naongea kisha nikampigia simu mama huku nikiwa natetemeka.
“Halloo mwanangu…” mama alitamka
“Shikamoo..mama…
“Marhaba hamjambo?:
“Hatujambo mama. Sasa nataka kukutaarifu kuwa kuna wageni watakuja nyumbani…”
“Hee!, karibuni sana!, akina nani hao !?”
“Baba mkwe na rafiki zake pamoja na mme wangu.”
“Hee!, mbona umetushtukiza!, hapa hatuna chochote sijui tutawapatia nini!”
“Haina shida mama chochote kitakachokuwepo maana hali ya nyumbani wanaijua”
“Ngoja nimwambie baba yako aandae hata mbuzi mmoja .”
“Asante mama, Delila yupo?”
“Ndiyo yupo nimpe simu uongee naye?”
“Hapana haina shida nilitaka kujua kama yupo…”
“Sawa mwanangu karibu sana ngoja nianze maandalizi ya usafi..”
“Jamani mama..siyo leo tutakuja kesho kutwa..”
“Ohoo!. .hapo sawa..”
“Msalimie baba.”
“Haya nitamsalimia nawe wasalimie huko”
(Nililikata simu)
Baada ya maongezi hayo na mama, nilishangaa kumuona mme wangu akiwa karibu yangu jambo lililonishtua.
“Heee! Kumbe ulikuwepo hapa?” Nilimuuliza kwa mshangao
“Hapana wala!, nimefika mda huu . Vipi ulikuwa unaongea na nani?”
“Nilikuwa naongea na rafiki yangu…”
“Ohoo sawa.., vipi sasa hujanipa jibu…”
“Jibu lipi?”
“Mhh umesahau baby?, si kuhusu kwenda kwenu?”
“Ohoo!, sasa sikia nikwambie kitu kimoja , mimi nimeshakusamehe wala sina shida na wewe ila usirudie tena .Lakini kuhusu kwenda nyumbani, haina shida maana nilikuwa nimeshamwambia mama kuwa nitakuja na mme wangu kutembea hivyo tutaenda hiyo kesho kutwa”
“Hujawambia chochote kabisa!” Aliongea huku akiwa anakuna kidevu chake
“Sijawambia na siwezi maana ni aibu kubwa .”
“Unaonaje tujipange twende hata mwakani? Maana mda huu pesa zimeniishia ukiangalia wazee lazima wanipige faini..”
“Mwakani tena!, yaani hata tukipeleka kilo mbili za sukari inatosha afu tutapitia huko turudi nyumbani”
“Sawa haina shida .”aliitikia kwa sauti ya chini huku akionekana mwenye mawazo
Baada ya mazungumzo hayo, tulirejea nyumbani ndipo niliponkuta baba mkwe akiwa anapangusa koti lake la suti.
Nilitamani kumsaidia lakini nikaona aibu . Aliponiona, alilitundika kwenye kamba ya kuanika nguo kisha akaniita .
Nilipiga hatua kama mbili kisha nikaweka goti langu chini kama ishara ya heshima ya kuzungumza na mkwe.
“Umeshawataarifu?”
“Ndiyo mda huu nimempigia mama “
“Umemwambiaje?”
“Nimemwambia kuna wageni tu wala sijamwambia wanakuja kufanya nini”
“Umefanya vizuri!, lengo ni kuongea na mdogo wako pamoja na mme wako ili watamke hadharani kuwa wameacha”
“Asante lakini nilikuwa naomba mme wangu asijue maana nimemwambia tunaenda mimi na yeye tu”
“Hilo halina shida. Hatojua chochote kwani akijua anaweza kumpigia mdogo wako siku hiyo asiwepo.”
“Asante..”
“Haya unaweza kuendelea na shughuli zako…”
Nilinyanyua goti langu chini kisha nikaenda kupumzika ndani.
Mnamo mida ya saa 10 za jioni , wazee walirejea tena nyumbani wakiambatana na baba mkwe ndipo nilipomuuliza mme wangu ,
“Mbona wamerudi tena wakati tumeshayamaliza?”
“Hapa wamekuja kunipiga faini…”
“Mhh…pole ila ulitaka mwenyewe”
Mda si mrefu , walikusanyika ndani kisha wakatuita. Mapigo ya moyo wangu yalianza kunienda mbio mara baada ya kuwaona
Niliwasalimia kwa mara nyingine tena kisha tukatega masikio kujua nini wanataka kuongea.
Mzee mmoja alisimama kisha akatamka,
“Kwa kitendo ulichokifanya kijana wetu!, tunakikemea na kukilaani kwa nguvu zote lakini tulikuwa tumemua tukutenge kwenye ukoo ila tukakumbuka ni kosa lako la kwanza. Tumekuja na adhabu mbadala ambayo itakuwa fundisho hata kwa wengine. Baada ya kuketi, tumeamua kukupiga faini ya laki 8 ambayo inatakiwa kulipwa mda huu kwa keshi na endapo utashindwa basi utakuwa umejiondoa kwenye familiia kwa ujumla…” alitamka.
Mme wangu pesa alikuwa nazo milioni milioni hivi kwake haikuwa shida. Alichomoa wallet yake kisha akahesabu keshi ya laki nane kisha akawapatia.
Walizihesabu na kuona kama zimetimia .
“Haya faini umemaliza lakini usirudie tena kutudhariridha wazazi wako” mzee alitamka.
Mme wangu alipiga magoti mbele yao kisha akaomba msamaha na kukiri kuwa hatorudia tena.
Baada ya mda, wazee walitawanyika huku wakiambatana na baba mkwe
Mda uliendelea kutaradadi huku akili yangu yote ikiwa inamuwazia mdogo wangu Delila kwa kile alichonifanyia.
Usiku tukiwa tumelala, nilimuona mme wangu akiwa anachati huku akinichungulia kama nimesinzia. Nilijifanya nimefumba macho japo nilikuwa naona kama mtu mwenye chongo.
Roho yangu ilianza kuvuja damu kwa ndani huku nikitamani kupasuka mara baada ya kuona picha ya Delila akiwa amevaa nguo ya ndani tu huku maziwa yake yakiwa nje yote.
“Hivi kampa nini ambacho sina mpaka anakuwa kama kichaa?!, yaani kumbe kuomba kote msamaha ni uongo mtupu!, haya ila kitaeleweka..” nilitamka moyoni mwangu.
Niliendelea kujifanya nimesinzia bila kumwambia chochote mpaka asubuhi yake.
Tulifanya maandalizi ya mwisho kuelekea nyumbani huku nikiwa na hasira kali sana.
Kesho yake mnamo mida ya 12 asubuhi, tulianza safari ya kuelekea nyumbani Tanga huku baba mkwe akiwa ameshatangulia kimyakimya na wazee wenzake wawili…..
INAENDELEA….