Wanaume Wajanja Huwavutia Wanawake Kwa Kukataa Haya Mambo
Mwanaume makini na mjanja hutakiwi kukimbizana sana na mwanamke uliyempenda, huku ukionyesha kumng’ang’ania sana na wakati yeye haonyeshi ushirikiano wowote kwako. Kuna mambo ukikataa kuyafanya au kuyakubali basi huyo mwanamke atakuheshimu na atakupenda sana tu.
Kataa kabisa kufanya au kuyakubali haya mambo yafutayo:
1. Kuvumilia dharau: Usikubali kabisa kuvumilia dharau kutoka kwa mwanamke hata kama umempenda kiasi gani, mwanamke anayeweza kukuonyesha dharau tangia mmeanza mahusiano ni hatari sana huko baadaye. Ukikubali dharau umepoteza heshima yako kwa mwanamke, na ipo siku atakuonyesha dharau hata mbele za watu.
2. Kutafuta kuthibitishiwa thamani: Hauhitaji kupewa sifa au uthibitisho kutoka kwa mwanawake ndio ujione unafaa. Wanaume wanyonge mara nyingi hujikuta wakiwauliza maswali wanawake wanaoteswa nao kama vile: Hivi tupo pamoja kweli?, Unanipenda kweli?, Nipo mimi peke yangu?. Mwanamke hapa atakuona wewe ni kama hauna pa kwenda.
3. Kupoteza malengo yako: Kupoteza malengo, pesa au mali yako kisa mwanamke fulani uliyempenda, huku ni kujichimbia kaburi lako wewe mwenyewe. Mapenzi ya kweli sio ya kuumizana kiasi hicho.
4. Kutoa maelezo kupita kiasi: Kama kuna jambo limetokea liwe la kweli au sio la kweli, jitahidi umwelezee Mwanamke wako kwa kiasi na kwa uhakika kuhusu hilo jambo. Ikitokea hataki kukuelewa amekomaa na misimamo yake, basi epuka kutoa maelezo mengi huku ukinyenyekea weee, hapa mwanamke atakuona wewe ni mnyonge kwake.
5. Kupatikana muda wote: Epuka kupatikana muda wowote mwanamke akikuhitaji kana kwamba hauna kazi za kufanya, hii itakuondolea thamani. Onyesha wewe ni mtu ambaye una mambo yako ya kufanya, na mwanamke aheshimu ratiba zako.
Mwisho: Ukikataa kuyafanya hayo mambo tajwa hapo juu, basi tegemea kupata upendo na heshima kutoka kwa Mwanamke yoyote yule Duniani, labda kama hakupendi tu.
TAZAMA PIA VIDEO

