𝗠𝗔𝗟𝗜𝗣𝗢 𝗞𝗜𝗧𝗔𝗡𝗗𝗔𝗡𝗜
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
EP 19
Erick alitetemeka alishindwa hata kujibu ule ujumbe, alichanganyikiwa, alijikuta anasimama katikati ya chumba akiwa uchi wa mnyama, machozi yakimtiririka katika mashavu yake yote mawili tena akidhani kwamba yeye ni mtu ambaye sio chaguo la Mungu kabisa, alijiona ana upweke uliokithiri, alijiona mkosaji
“Mungu kwanini lakini?” aliongea kwa huzuni Erick huku akiwa ameegemea ukuta anaangalia sehemu moja kama mjinga.
Alijitazama mwilini na kusema “Kwa hiyo mimi nina ukimwi kweli daaah?” alichanganyikiwa sana.
*
Kule kazini kwa Aneth furaha ilikuwa inaendelea….lakini Aneth kwa mbali alikuwa na wasiwasi
“Haidali” alisema binti
“Nambie mpenzi wangu”
“Jana mume wangu hajalala nyumbani, tena hakunipa taarifa yoyote sikujua kipi kimemkumba, na simu alikuwa amenizimia kabisa”
“Aaah mi nimeshakuambia, uachane naye nikupangishie nyumba nzima ufurahie, huyo anaonekana kuwa na mwanamke mwingine”
“Kweli unalolisema lakini hakuwahi kuonyesha hii tabia”
“Tabia ndo umeanza hivyo kwa hiyo usishangae kile anachokifanya kwako”
“Daaah” alisema binti kwa uchungu maana hata mtu amsaliti mwenzake vipi, bado hujiona yeye hastahili kusalitiwa
“Achana na hizo habari, twende tukale” alisema Haidali huku akiifunika laptop yake na kusimama
Kumbe wakati wote wakiwa wanaongea mambo hayo, yeye Erick alikuwa katika hosptali moja, alikuwa ameenda kupima virusi vya UKIMWI, moyoni alikuwa anaamini hana UKIMWI lakini saa hiyo alikuwa kwenye foleni ameshikilia simu mkononi anatetemeka kwa uoga
Kichwani alikuwa anajisemea
“Nikikutwa na UKIMWI nitaenda kumuua yule mwanamke”
Lakini ghafla kabla hata damu yake haijachukuliwa, alipata wazo na kuinuka, akaghairi kupima ngoma, halafu akasema “SIPIMI tena” halafu akajiuliza swali peke yake “Kwanini usipime?” ndipo akajijibu “Sikubali kufa peke yangu, nitalipa kisasi changu”
Alianza kupiga hatua kuondoka kwenye hospitali kuelekea getini, watu wote wakabaki wakimshangaa.
Erick alikuwa na mpango wake wa siri, aliondoka mpaka akafika nyumbani kwake, siku hiyo alikuwa anatumia usafiri wa pikipiki maana gari aliiacha nyumbani tangu jana yake.
Alipofika nyumbani aliingia moja kwa moja maana geti la dogo lilikuwa wazi, alizama hadi chumbani kwake, ndipo akachukua simu na kumpigia Manka ambaye ni shemeji yake.
Manka alipokea simu maana muda huo alikuwa nje anafua
“Shemeji” Alisema Manka
“Shemeji unaweza kuja hapa ndani?” alimuuliza
“Kuna nini shem?”
“Kuna jambo nataka kuzungumza na wewe” alisema Erick
“Sawa” alisema binti maana alikuwa akimuheshimu shemeji yake tena ni mkubwa kwake kiumri
Erick alikata simu akawa ameweka mikono magotini anachezesha chezesha mguu wa kulia huku akiwaza mambo mengi kichwani, ndipo akasikia sauti ya Manka mlangoni “Hodi”
Akasema “Ingia”
Manka alifungua mlango na kuingia akasimama katikati ya chumba kikubwa akasema “Nimekuja shemeji”
Erick alimtazama Manka kisha akasema “tafadhali embu kaa hapo” alisema huku akinyoosha mikono kwenye kochi dogo lililokuwa eneo hilo
Manka aligeuka akalitazama kochi, huku wasiwasi ikimuingia kiasi, akaenda akaketi na kumtazama shemeji yake
Kimya kilitawala kwa sekunde kadhaa pale ndani, moyo ukamuenda mbio Manka, na kuhisi anaenda kuambiwa jambo zito linalohusiana na kitendo cha dada yake kumsaliti shemeji
Erick alivuta pumzi “Oooopssss” halafu akajikuna kichwa na kusema “Unajua nini Manka?”
“Sijui shem”
“Najisikia vibaya sana” alisema mtalaam
Manka alielewa kabisa shemeji yake anaumia kwa sababu alisalitiwa “Pole shemeji yangu” alisema
“asante, lakini embu niambie tu shemeji, kwanini dada yako yuko hivi?” alimuuliza shemeji yake
“Sijui kaka….naomba umsamehe dada”
“Nimeshamsamehe, maana kama nisingemsamehe ungekuta alishakufa muda mrefu” alisema na kuvuta pumzi halafu akasema “Unajua shemeji mimi nilikuwa na bastola lakini nimeamua kuirudisha katika eneo la usajili nifutiwe umiliki maana muda wowote ninaweza kumuua mtu, wakati mimi sihitaji hilo” alisema maneno kidogo ya kushtua, Manka akaanza kuangaza macho kule na huku akidhani labda kunaweza kukawa kuna silaha kule ndani
“Mh” aliguna
“Usigune Janeth…..nikuambie tu ukweli, sikuwahi kumsaliti mke wangu, nimempenda tangu siku aliyokubali kuwa na mimi niliahidi nafsi sitokuja kumsaliti, lakini kaniumiza sana shem” alisema Erick
“Pole shemeji, lakini kwani ilikuwaje?”
“Nimemkuta dada yako akitoka lodge na boss wake wakiwa wameshikana kiuno, halafu mbaya zaidi nimewafuatilia wakaona haitoshi wakafanya mapenzi kwenye gari nawaangalia lakini wao hawanioni”
“Mh mama Chris amefanya hivyo”
“Mbsssh…..embu usinikumbushe” alisonya huku akianza kulengwa lengwa na machozi
“Usilie shemeji” alisema binti
“Nikuambie Manka?” alisema kwa uchungu na kujifuta na leso machoni
“Niambie shemeji”
“Mimi sitolala tena na dada yako, ninataka kutafuta mwanamke mwingine, nitamnunulia nyumba, nitampa pesa na kila kitu anachotaka tutafurahia mapenzi, maana mimi ninahitaji mapenzi ya kweli na ya furaha”
“Mmmh,…..usimuache dad….” kabla hajamaliza sentensi alipata swali lililomtetemesha binti huyu
“Kwani wewe nikikupa milioni tano, nikakupa na nyumba yenye kila kitu haitafaa shemeji tuishi wote kwa siri bila dada yako kujua?”
Binti alikodoa macho akimshangaa shemeji yake kwa sababu alikuwa amesema jambo zito la kumshangaza, alishindwa kulijibu swali, huku ile sentensi ikijirudia kichwani mwake.
Kila ilipojirudia neno milioni tano na nyumba yenye kila kitu, Manka alichanganyikiwa na kushindwa kujibu
“Eti hautakubali kuwa na mwanaume ambaye anakujali hivyo?” aliuliza
“Mh” aliguna shemeji na kujikuna kwenye nywele zilizosukwa mistari mitano kichwani
“usigune, halafu hizo nywele nitakusuka hata za laki, utapendeza utakuwa na kila kitu, ila uwe na mapenzi ya kweli kwangu mimi” alisema Erick kwa kujiamini
“Mimi ni sheme……”
“Achana na hizo habari, ushemeji unatakiwa ufe, niwe wako sasa, nikupe furaha, yaani kitendo cha kuwa na mimi tu ni kama umeajiriwa, tena nitakulipa milioni moja kwa mwezi mshahara ambao hata mwalimu wa sekondari halipwi, na kazi yako wewe ni kujiosha na kunipa raha basi inatosha”
Manka alibaki mdomo wazi, anaambiwa vitu amazing ambavyo hakuwahi kuviota kabisa, alimuangalia shemeji yake kwa muda mrefu sana, akashindwa kuelewa afanye nini. Alipigwa mtongozo wa kibabe kabisa ambao ulimchanganya, yaani pesa tu inaweza kununua hadi moyo wa mtu.
“Naona umekaa kimya, inuka nenda kafikirie halafu utanipa jibu shemeji yangu” alisema Erick
“Sawa” Manka aliinuka akiwa ana mawazo, hajui akubali au akatae, lakini ahadi za Erick zilikuwa ni moto, na nia yake ni kulipa tu kwa kile mkewe alichomtendea
Akiwa anatoka mlangoni, Erick alimuita jina lake la ubatizo “Janeth” ndipo Manka akageuka na kumtazama shemeji yake, Erick akaendelea kusema “Simu yako iko wapi?”
“Hii hapa shemeji”
“Okay ishike mkononi kuna ujumbe nitakutumia”
“Sawa”
Manka aliondoka, akafika kwenda kumchungulia Katarina amelala kitandani amesinzia na mtoto Chris pia amesinzia kitandani
Manka taratibu aliurudushia mlango akaenda nje kuendelea kufua, alipoketi tu hivi, alipokea ujumbe kwenye simu, na alipoufungua ni ulikuwa ujumbe kutoka M-PESA ukisema kwamba amepokea kiasi cha shilingi laki tano kutoka kwa Erick Jackson Temu
Akiwa anakishangaa kiasi cha zile pesa ambacho hakuwahi kukimiliki kabla, alipokea ujumbe kutoka kwa Erick ukisema
“Naamini umeiona, hiyo ni mwanzo tu, ukinikubalia nitakupa pesa zaidi ya hizo”
“Mmmh shemeji” aliguna Manka kwa kuchanganyikiwa
Erick akaongeza “Nataka uwe mwanamke milionea mdogo”
“Asante shemeji ila naogopa mwenzio”
“Usiogope chochote, najua tutakavyofanya kwa siri”
“Mh.. sawa shem” alisema Manka
“Kwa hiyo unasemaje, inawezekana?” aliuliza Erick
“Hamna shida shemeji” alisema mtoto wa kike bila kujua kwanini Erick anaamua kutembea naye wakati wanawake wa mbadala wa Aneth ni wengi sana jijini Dar es Salaam
“Hapo sawa, ukumbuke kufuta hizo meseji ili zisikutwe na mtu yeyote”
“Sawa”
EP 20
Ilifika jioni saa kumi na mbili, Aneth alirejea nyumbani. Alipofika chumbani alimkuta mume wake ameketi kwenye kochi dogo lililokuwa chumbani halafu kichwa aliinamisha chini akawa anawaza mambo fulani fulani
Aneth aliweka pochi kitandani halafu akamtazama na kumsalimia “Baba Chris kwema?”
Erick akaiunua uso wake na kumtazama mkewe kisha akajibu “Ni kwema kabisa, vipi upande wako?”
“Mi siko powa hata kidogo” alisema binti
“Pole kama hauko poa” alijibu mtaalamu
“Kwa hiyo ndo uliloona la kuniambia? Embu niambie kwanza jana ulilala wapi bila taarifa yoyote na simu ukanizimia?” aliuliza binti kwa hasira na kushika kiuno
“opppssss” alivuta pumzi mtaalam huku akimtazama mkewe bila kuongea chochote, ndipo hasira zikampanda Aneth
“Unakaa kimya? Wewe mwanaume ni malaya, ulienda kulala na mwanamke mwingine….nakujua vizuri una wanawake wengi sana…ila sawa” alisema na kuketi kitandani halafu akaanza kulia kinafiki
Erick alimuangalia mkewe anavyojitahidi kujifanya hana kosa, kilichomuuma zaidi ni kwamba alikuwa anaona yule mwanamke anajifanya anaumia wakati yeye ndo anafanya uchafu wa kila aina akiwa na boss wake.
“Endelea kukaa kimya….ila Mungu wangu aliye hai atajibu yote haya” alisema binti kisha akainuka na kusema “Najuta kuingia na wewe kwenye ndoa unaumiza sana wewe mwanaume”
Erick alisonya na kusimama akaona huyo mwanamke hana akili, hakutaka kumuambia alichokiona, wala nini, yeye aliinuka na kuondoka zake mpaka sebuleni akawasha tv na kuweka chaneli moja iitwayo Trace Music halafu akawa anaangalia video za nyimbo taratibu.
Chumbani alimuacha mkewe akiwa analia, tena akilalamika “Mwanaume gani haijali familia yake, mwanaume gani hanipendi…..msaliti mkubwa….ananisaliti waziwazi….ila sawa……sawa tu” aliongea mambo mengi sana, ndipo akavua nguo na kuingia bafuni akaoga.
Erick hakutaka kumuambia ukweli mke wake kwamba alimuona akimsaliti.
*
BAADA YA SIKU MBILI
Ilikuwa mida ya saa saba mchana, Erick alikuwa kazini alikuwa ana mawazo kibao kutokana na jambo ambalo mke wake alikuwa amemfanyia, hata hivyo alisimama na kumuuliza kijana wake “Oya si unaweza kupamudu hapa kwa leo?”
“Ndio boss, kwani unaondoka?”
“Ndio ninaenda nyumbani haraka nitarudi jioni au nitakupigia simu”
“Sawa hamna shida”
“Okay”
Erick alichukua ufunguo wa gari yake akazama kwenye gari, akawa anataka kumpigia Manka, lakini kabla hajampigia Manka alipata wazo akatabasamu na kusema “Ili ajue mi ni muhuni, nitamlia mdogo wake pale pale kitandani nilipokuwa nikimlia yeye”
Aliweka simu pembeni kisha akawasha gari kisha akaanza safari yake mpaka mitaa ya daraja la kijazi ambapo aliingia katika duka moja la nguo akaamua kumchukulia shemeji yake zawadi ya nguo, ambaye ni Manka. Alinunua magauni mawili pamoja na nguo za ndani.
Baada ya kununua aliwasha gari lake na kuelekea nyumbani kwake, bado mtu huyu alikuwa na stress sana, hata kitendo kilichomfanya asiwe makini sana barabarani.
Baada ya kufika salama nyumbani kwake, alipaki gari nje ya geti kisha akaingia ndani akiwa amebeba mfuko wa zawadi aliyokuwa amemchukulia shemeji yake ambaye tayari walishakubaliana kuwa wapenzi kwa mbadala wa dada yake.
Alipoingia ndani kwa bahati mbaya au nzuri alimkuta Manka akiwa nje anajisnap kwa simu yake aliyomnunulia siku kadhaa zilizokuwa zimepita.
“Manka” alisema Erick kwa furaha
“Pole shem” alisema mtoto wa kike huku akiacha zoezi la kupiga picha na kupiga hatua kumfuata shemeji
“Asante sana” alisema Erick huku akimnyooshea mfuko ule Manka
Manka aliupokea kisha akaanza kuelekea ndani, Erick naye akamfuata nyuma ndipo binti akampelekea chumbani kwake ule mzigo akijua ni wa shemeji yake lakini alipofika katika mlango wa chumba cha Erick alimuuliza
“Umekuja kutafuta nini chumbani kwangu?”
Manka akamjibu “Si nimekuletea huu mzigo niliyokupokea pale nje?”
“Hahaha…huo ni zawadi zako” alisema Erick huku akifungua mlango wake na kuingia nusu ndani halafu akamgeukia Manka ambaye alikuwa akiutazama ule mfuko ndani
“Asante shemeji” alisema huku akimshangaa
Erick alipokuwa amesimama na yule binti kimya kilitanda ndani ya nyumba ndipo akamuuliza Manka “Kwani leo Katarina yuko wapi?” alimuuliza binti wa kazi
“Ameenda sokoni”
“Mh na mtoto??”
“Yuko amelala chumbani kwetu”
“Katarina alienda muda mrefu sokoni?” aliuliza Erick
“Sio sana, kama dakika 20 zimepita tu” alisema mtaalam
Erick kusikia ile habari, aliona ni habari njema kwake ndipo akasogea nje na kumshika mkono, Manka akaangalia chini kwa aibu
“Manka” alisema Erick
“Nini shemeji” binti aliuliza huku akipata mshtuko maana alishawahi kupewa taarifa kwamba jamaa anamtaka kimapenzi siku moja iliyopita
“Naomba uingie chumbani tuongee kidogo” alisema Erick
“Shemeji mi naogopa”
“Usiogope” alisema mtaalam huku akimvuta kwa nguvu Manka akatua ndani ya chumba cha shemeji pamoja na dada yake.
“Naona tumepata nafasi nzuri”
“Hapana, shemeji hapa chumbani kwako hapana bhana labda tutoke nje na nyumbani”
“Hapana ni busu tu shem wangu” alisema Erick na kuufunga mlango halafu akamkumbatia
“Shem sio vizuri, dada akinikuta huku itakuwa sio vizuri” alisema binti
“Hawezi kuja saa hizi” alisema Erick akizidi kumpapasa shemeji yake
“Shem….bhana huyu Katarina ni mbea akij….”
Ghafla Erick alimnasa shingoni kwa lips zake akaanza kumnyonya taratibu binti akajikuta anaachia ule mfuko wenye zawadi na kulegeza macho, haamini kile kilichotokea, hata akujua saa ngapi ametupwa kitandani na kulaliwa huku akitomaswa katika chuchu na kiuno
Erick hakuwa haba, alimuonyesha yote, ndani ya dakika tano walikuwa katika mahaba mazito huku binti akihema kama gari bovu kila aliposikia akiguswa taratibu na Erick Jackson
“Auwiii sheem…..aaaagh” alisema mtoto wa kike huku akimpa busu la kifaransa taratiibu na mpaka walipofika juu ya mlima Kilimanjaro pale juu kabisa.
Mshindo mmoja tu ulimtosha Erick, maana walikuwa katika hatari ya kufumwa na mke au binti wa kazi.
Manka alichukua mfuko wake wa nguo na kutoka nao taratibu mpaka chumbani kwake, akajifungia na kujipima nguo, zilikuwa ni nzuri sana yaani shemeji alijua kuchagua
Huku nyuma Erick akijisemea moyoni kwamba hii ni trela tu kwani muvi haijaanza bado”
EP 21
Zilipita zaidi ya wiki mbili mapenzi yakizidi kukolea zaidi kati ya Erick na Manka, hii ilipelekea Manka kunogewa na kujikuta anajisahau anataka kuona shemeji akiwa naye hata kule ndani.
Ile tabia ya kuchelewa nyumbani ilianza kuzidi kwa Erick, alikuwa hawahi tena, halafu muda wote huo hakuwahi kumuambia mkewe kwamba alimuona na mwanaume mwingine, halafu hakutaka kufanya naye kitu chochote kitandani maana alikuwa anamuona ni msaliti kwake, na aliona kinyaa kabisa kulala na mwanamke ambaye amemsaliti.
Ikiwa ni usiku saa saba, familia ya Aneth ilikuwa katika usingizi mzito, lakini Manka bado alikuwa macho akichati na shemeji yake ambaye hakuwepo nyumbani
Manka na Erick walichati sana, kitendo kilichofanya Manka kupandwa na hamu ya kufanya mapenzi hadi akamtumia message Erick na kumuambia
“Shemeji unanipa hisia, natamani hata kichwa tu kingie”
“Ninakuja hapo muda sio mrefu, si unaweza kutoka tufanye hata ndani ya gari?” aliuliza shemeji
“Mmmmh….” aliguna binti
“Kweli vile, mwenyewe nina hamu unajua ni siku tatu hatujafanya” alijibu Erick
“Ngoja nitajaribu kutoka ila sasa ufunguo wakiutafuta wa geti itakuwaje?”
“Usijali mi nina ufunguo, nitafungua halafu nitakushtua, sawa?” alisema mtaalam
“Mh sawa hamna shida”
“Poah”
Erick alikuwa kwenye gari anaendesha taratibu huku akichati bila kuogopa ajali, wala hakuwa na wasiwasi maana foleni haikuwepo mida hiyo ya usiku.
Saa nane kasoro, Erick alikuwa nje ya geti lake, akamtumia ujumbe Manka ili kujua kama ameshalala au bado yuko macho
“Uko macho au ushalala?” aliuliza Erick
“Siwezi pata usingizi mpaka niliwe” alisema bila hata kujali
“Okay niko nje ya geti, toka sasa nishafungua” alisema Erick lakini alikuwa hajafungua bado, alifungua mlango wa gari akatoa ufungua na kufungua geti dogo.
Manka taratibu naye alishuka kitandani, akatoka kwa kunyata na kufungua mlango wa chumbani akaenda mpaka sebuleni ndipo akafungua mlango wa sebuleni na kutoka nje kabisa, akaurudishia.
Manka alikuwa na hamu hatari, yaani aliwahi haraka getini akatoka lakini alikuwa anatetemeka kwa uoga mkubwa. Alipofika nje ya geti, Erick alifunga geti kwa ufunguo halafu wakaingia ndani ya gari na kuliwasha.
Erick aliliendesha taratibu mpaka mbele kidogo na nyumbani, ndipo akalipaki kando ya barabara inayoenda eneo liitwalo Mivumoni halafu akamvuta Manka na kuanza kukulana ndimi.
Mdogo mdogo walihamia siti ya nyuma ya gari akaanza kumkung’uta, walikung’utana haswa, mpaka saa kumi ni kupeana tu mahaba ndani ya gari.
Kwa furaha aliyoipata Erick, alimpa shilingi laki moja shemeji yake, na mpenzi wake mpya kisha akamrudisha nyumbani.
Erick na Manka waliingia kwa pamoja, hakuna mtu aliyeshtuka kwani wote walijua ni Erick kaja kumbe kafuatana na shemeji yake.
Ubaya ni kwamba wakati gari imetua nje, Katarina alishtuka kutoka usingizini na kutazama akagundua kuwa Manka hayuko kitandani, akashtuka kidogo lakini akajua labda binti kaenda uani.
Ilipita dakika kama tano hivi lakini Katarina hakuona mwenzake akirejea, sasa kwa namna alivyokuwa mbea, aliamua kushuka kitandanI na kutoka chumbani akaangalie Manka anafanya nini….alipofika sebuleni……
INAENDELEA

