
za Mapenzi, Maisha na Uchawi Mautundu Kitandani
ALINIACHA KWASABABU SIZAI
Sehemu 17 na 18
💙🤎💙🤎💙🤎💙🤎
Kila mtu akabaki akimuangalia Abbas ambaye hakuonekana Kuwa Sawa kabisa.
“Don’t mind him kwa sasa”
Alizungumza kiongozi kisha akaendelea.
Kila mtu siku hiyo alinipingeza, wa kunipa zawadi ananipa zawadi na wengi walikumbuka Kuwa ni siku yangu ya kuzaliwa hivyo zawadi zilikiwa Kama zote.
Ila Mimi Sijui Nina moyo wangu, watu wote walikuwa bize na kuinjoy lakini Mimi nilianza kumtafuta Abbas maana nilijikuta nikipata wasiwasi mkubwa sana juu yake.
“Mama unatafuta nini “
Mage aliniuliza baada ya kuona Kuwa nazunguka uku na uku.
KWa utulivu nika Kaa pembeni ya mage na kumwambia.
“Namtafuta Abbas, Abbas hayuko Sawa kwa sasa na Nafikili anaitaji mtu wa kuzungumza nae, Sawa Mimi na Abbas tumepitia mambo mabaya Mengi lakini sizani Kama ni wakati sahihi wa kumuacha kwenye kipindi Kama iki ni wazi Kuwa Ana depression “
“Mama Unafikili ni Sawa kuzungumza na Abbas ? Una Uhakika Kuwa awezi kukuzuru ??”
Mage aliniuliza akiwa na wasiwasi sana.
“Nitakuwa Sawa, please Ka na Mtoto lakini pia sogea pale kWa victor nimemwambia Kuwa akuchukulie chakula “
“Oooh sawa “
Basi kWa upande wangu nikaendendelea na zoezi la kumtafuta Abbas, Nikimtafuta kila kona mwisho nikakumbuka pale kwenye ile bustani haraka nikaenda na kweli nilimkuta abbas akiwa amejiinamia na analia sana. 🥹
“Abbas jamani “
Nilizungumza kWa sauti ya huzuni sana na mwisho nikamkumbatia ambapo Abbas alishindwa kabisa kushikiliammaumivu yake na kujikuta akilia kwa sauti sana.
Baada ya muda alitulia na kuzungumza.
“Miaka yote nimeishi nikiamini Kuwa wewe ndio una matatizo, mama yangu aliniaminisha Kuwa Mimi ni mwanaume kamili kabisa Ila wanawake zangu ndio Wana shida, Maneno ya mama yangu na kila kitu kilinifanya nijiamini sana na kudharau kila mwanamke ambaye alishindwa kunizalia, siku zote sikwenda hospital kuangalia AFYA yangu ya uzazi nikiamini Kuwa Mimi niko Sawa kabisa kutokana na mama yangu “
Abbas akafuta machozi yake na kuendelea.
“Hakuna Siku bora na ya maumivu Kama siku ambayo nilienda hospital kuangalia AFYA yangu, na nilienda hospital baada ya kukuona wewe ukiwa mjamzito, siku hiyo ndio daktari akaniambia Kuwa Nina shida Kuwa siwezi kuzalisha kwani nilivyokuwa Mdogo nilifanyiwa upasuaji ambao ulionesha Kuwa Sitakuja Kuwa na nguvu za kumpatia mwanamke ujauzito, Zayana uwezi amını mama yangu alikuwa anajua kila kitu, Zayana mama yangu anası karatasi zote za hospital lakini hakuwai kuniambia, aliniacha niyateketezea maisha yangu, alikutesa wewe uku akijua kabisa Kuwa shida ipo kwangu, am sorry Zayana “
Daaaah Abbas jamani mshikaji wangu huyu mjue.
“Abbas kila kitu kina sababu, Nafikili ni muda wa wewe kusimama imara, ni muda wa wewe Kuwa mwanaume sasa na. Kufanya Maamuzi sahihi katika maisha yako, ujachelewa make yourself happy au usahau maumivu yote “
Tuliiongea Mengi mwisho Abbas akaniaga na kuondoka.
Kwakweli event ilikuwa powa sana na Majila ya jioni Mimi na my zangu tukarudi Nyumbani na mambo mengine kuendelea.
Majila ya usiku nilipata muda wa kuzungumza na my wangu na nilimuelezea kila kitu kilichojilimkwenye event, yaaani sikumficha ata kitu kimoja hadi maongezi yangu na Abbas nikamwambia.
“Abbas Ana kipindi kigumu snaa kWa sasa na anaitaji mtu ambaye anaweza akamuelewa yeye kWa kina “
“Aaaah nilisahau kitu mume wangu, nakumbuka Nilimwambia hii hudumu ya psychology na akakubali are if you don’t mind unaweza ukamuunganisha nae ??”
“Nilitaka kukuambia hivyo hivyo lakini ni vyema Kama ameitaji Mwenyewe”
******
Siku ziliendelea kwenda na mume wangu akamuangunganisha Abbas na huduma hiyo ya akili na akaanza kupayı wa matibabu ili kumuweka Sawa.
Ikiwa ni siku ya weekend, Nyumba nzima tulibaki Mimi na mage tu, siku hii ilikuwa tofauti sana, muda wote mage alikuwa bize na simu yake, Nilimuita Mara kadha lakini hakuwa ata akinisikia haraka nikatoka na kwenda chumbani kwake ambapo nilimkuta akigalagala tu kitandani uku anazungumza na simu.
“Mmmmmmh unaongea na mkwe nini ??”
Nilimuuliza na hapo ndio akashtuka Kuwa chumbani kwake kuna mtu , haraka akakata simu kisha akaniuliza.
“Umeingia saa ngapi umu ??”
“Ahahaha kitambo sana nimesikia kila kitu “
Niliamua kumdanganya tu Walahi maana sikuwa ata ni kitu gani alikuwa akizungumza.
“Please usimwambie baba atanitoa masikio Walahi “
Kwanza nilishangaa sana na kujiuliza huyu Binti ni mkubwa sana lakini inakuwaje anamuogopa sana baba yake, kWa utulivu nikakaa pembeni yake na kumuuliza.
“Kwamba baba atalı uwe na mahusiano ??”
“Yaaaah ataki, Yaani baba yangu ampoteze da Aneth ataki kabisa kusikia habari ya Mimi kuolewa na kWa sababu hiyo nimeamua kujiweka mbali na mahusiano, lakini tangu nimekutana na huyu victor Nafikili ni Kama naangukia kwenye penzi lake”
Eeeeh kumbe anazungumza na Rafiki yangu victor 😁 eeeh me sikuwatambulisha ili wafoli ini lavuuu jamani, ila kama wamependana kweli me victor nampitisha ni mwanaume na nusu.
“Unajua baba yenu Anawapenda sana sana na ndio maana anawajengea njia nzuri sana za maisha, aaah kitu ambacho anacho ni wasiwasi yangu kifo cha dada yako lakini usijali atakuwa Sawa, na kuhusu mahusiano yako please Mage Achana na miemko ya mapenzi na umfahamu mtu vizuri Kabla ukawa serious kiasi iki”
“Sawa mama “
“Hata twende ukale maana muda wote upo na simu tu “
Basi Mimi na Binti yangu mkubwa tukaongozana na kwenda kupata chakula.
*******
Siku moja nikiwa chumbani kwangu usiku, niliweza kupokea ujumbe wa simu na ulitoka kWa victor na ulisomeka hivi .
“Mama mkwe nataka kumposa Binti yako lakini ni Kama ni muoga sana Sijui shida nini “
Victor aliongea na mimi kushkaji kabisa kwani tulizoeana sana.
Haraka nikampigia na kuanza kuzuungumza nae.
“Victor, mage ni Binti mmoja Mtulivu sana, ni Binti ambaye Ana maisha mazuri sana lakini hana hufska kabisa na maisha yake, nazani mage ni ndoto ya kila mwanaume”
Hapo nilianza kumpa victor historia ya dada yake mage Yaani Aneth mpaka alivyosababishiwa kifo na mume wake.
“Oooooh sasa naelewa ni Kwanini Mage anaiogopa ndoa, lakini pia mage anatakiwa kuelewa Kuwa yale ni maisha ya dada yake na yeye anaya kwakwe, anatakiwa kujua hakuna story za kufanana kila mtu Ana story yake ya maisha, Mwambie Kuwa nampenda sana na nitamtunza kama ambavyo baba yake anakutunza wewe”
Mimi na victory tuliongea Mengi sana kisha tukaagana.
Ikiwa ni usiku sana mimi na my wangu tumetoka kumalizana na mipinduko nikamwambia mume wangu.
“Baba Daniel Naomba tuzungumze kitu “
“Aaaaah wee mwanamke Sijui lini utakosa Jambo la kuzungumza kwenye maisha yako “
“😂😂🙌 Niache na wewe labda nataka Kuwa RAISI “
“Kama ni RAISI wa hii familia Sawa Ila wa nchi my wangu Kaa chini kuna nazi unenepeshe shavu “
Ila nyie me na my wangu tunapendana sana mjue Yaani yani kama wote.
“Aaaah ni kuhusu Mage, mage amepata mchumba ambaye yuko serious sana na mahusiano Yao, ataki kumchezea Ila anataka kuja kabisa Nyumbani na kufata taratibu zote “
Hapo mume wangu Ali Angalia chini kwa muda kisha kWa sauti ya chini akazungumza.
“Naogopa sana kumpoteza na mage kwenye maisha yangu, lakini pia umri wa Binti yangu unaenda, Anapaswa Kuwa mama lakini pia mie wa mtu, niko njia panda future ya mage inanitatiza sana”
Mume wangu , mage ni mtu mzima na amejifunza kupitia kifo cha dada yake, Nina imani Kuwa awezi kukaa kwenye ndoa ya mateso kama dada yake alivyokaa”
Aaaah mwanamke ni mwanamke mwisho nikashinda na mume wangu akakubali.
Baada ya week moja kupita, mume familia ya victory ilikuja Nyumbani kwangu na kuleta posa kwaajili ya mage, siku hii Bwana ndio niligundua Kuwa Victor na mume wangu Wanajuana.
“Kumbe mume ndio huyu aaah nimempokea, huyu Kijana nampenda sana, Mara nyingi uwa anajitolea kufanya usafi pale hospital kila jumamosi na jumapili, lakini pia ata kuhudumia wagonjwa kwenye mambo madogo madogo ni Rafiki yangu sanna.
Aaaah hali hii ndio ikarahisisha kabisa uchumba wa mage na victor .
Majilaniiiiiiiiiih ndoa Tunayo na tunatamba nayo…..
SEHEMU 19 – 20
Mambo ya victor na Binti yangu mage yalifanywa haraka haraka sana Walahi, Yaani ilikuwa ni zaidi ndoa.
Dokta Joel alihakikisha Kuwa ndoa ya Binti yake unakuwa ni ya kukumbukwa kila kona, alihakikisha Kuwa Binti yake Anafunga ndoa moja pambe sana na Jambo likaenda Kama lilivyo pangwa.
Ikiwa ni siku ya harusi, Mimi na mage tulikuwa zetu saloon, nilihakikisha Kuwa Binti yangu anapendeza Yaani sikutaka awe na stress ya aina yoyote ile katika siku yake nzuri.
“Siwezi kuomba mama bora ikiwa Mungu amenipa wewe, kitu ambacho naweza kumuomba Mungu ni kunitunzia wewe kwenye maisha yangu yote kunitunzia wewe ili uweze Kuwa kwenye kila Jambo langu nakupenda sana mama Zayana “
Alizungumza Mage na kunikumbatia muda huo tulishamalizana na mambo ya mapambo.
Sawa Mimi sio mama mzazi wa mage lakini niliweza kwa upande wangu, nilihakikisha Kuwa mage awazii kuhusu mama yake mzazi.
Baada ya muda gari ilikuja na safari ya kwenda kanisani ikaanza.
Baada ya Lisaa limoja tu tayali Mage akaaa mke halali wa victor. Hii ndoa ilikuwa na watu jamani imagine, Rafiki zetu wa chuoni wote walikuwako na Abbas pia hakukosa, lakin pia Abbas hakuna peke yake Bwana alikuja na Amina na walipendeza sana.
KWa wale ambao mmemsahau amina jamani ni Yule mie wa pili wa Abbas ambaye waliachaana pia.
Siku hiyo sikuweza kuzungumza nao kwani nilikuwa Nina mambo Mengi.
KWa upande wa ukumbini tulibaruza bwanaaaah Yaani kila kitu kilikuwa ni mtelemko tu.
Siku hiyo nililia sana Yaani ndio hivyo Tena mage wangu anaenda kuishi mbali na Mimi, mage wangu atakuwa akija Nyumbani kutembea tu, nilimuwazia Kijana wangu danie ambaye alikuwa akipendana sana na Mage uwiiiih niliona ni kiasi gani kijaana wangu atateseka pasi na Kuwa na mage.
Hatimaye kila kitu kilikamilika na kila mtu akarudi majumbani kwao uku Maharusi wetu wakienda hotelini.
*******
Week moja ilipita baada ya ndoa ya mage na victor kupita, Kila mtu akarudi kwenye majukumu yake ya kila siku.
Nikiwa ofisini, niliweza kupokea ugeni ambao ni Amina na Abbas ambao ilionesha wazi Kuwa tayali walisharudiana na kila mtu Alisha mfunzwa na maisha.
“Karibuni sana”
Niliwakatibisha.
“Asante sana da Zayana “
Alijibu amina na kunikumbatia.
“Waoooooh naona umenawili Tena Mdogo wangu “
Nilimwambia amina.
“Aaaah pongezi zije kwako dada angu kwasababu yako nikawa jasili na kusimamia furaha yangu “
“Kila kitu kinawezekana kWa uwezo wa Mungu”
“Sasa da Zayana, aaah time kuja Mimi na mwenzangu hapa tunaitaji msaada wako wa uzamini “
“Uzamini ??”
Nilishtuka sana Yaani hawa watu wameanza mambo ya Mikopo sasa halafu Mimi niwazamini, haraka Abbas akadakia.
“Aaah ni uzamini wa kuchukua Mtoto kisheria na kumlea kama wa kwetu, tumeshafuta process zote na sasa tüme baki na wazamini tu ambao wanaitajika lakini lazima wawe Wana ndoa “
“Lakini ili ni Jambo kubwa sana Nafikili mlipaswa kuniomba nikiwa na mume wa wangu na sio peke yangu “
“Naelewa sana ila Nimekuja kwanza kuongea na wewe. Nanikiwezekana utukaribishe na kutupatia nafasi ya kuzungumza na mumeo pia, Zayana najua nimekukosea sana lakini naitaji sana msaada wako “
“Tutawasiliana nikishamuomba mume wangu kWa sasa Sina majibu sahihi”
Basi maaji ya jioni nikapata kuzungumza na mume wangu ambaye anaga makuu kabisa na bila complication akakubali.
Siku ya weekend tukamualika abbas na amina Nyumbani ambapo pia walikuja na mama zako wa Abbas, Ila huyu mama hapana kwakweli ni kama namchukia sana hivi kitendo cha kumuona tu nikajikuta nikikosa amani.
Tulifanya mazungumzo na mume wangu akakubali sisi Kuwa wazamini wa process ya ku adopt Mtoto Mdogo.
Baada ya kila kitu kukaa Sawa tukasaini makaratasi na kila taarifa muhimu ambayo iliitajika.
Baada ya hapo mama mzazi wa Abbas akaanza kuzungumza.
“Mimi mwanangu Nimekuja kuomba radhi, Sura imeumbwa na haya lakini Sina Namba kwakweli. Zayana Binti yangu. Najua nilikukosea sana sana Yaani mpaka nahisi Kuwa sistahili msamaha wako lakini Nipo hapa Naomba msamaha Binti yangu “
Mama huyo akapiga na goti kabisa, haraka nikamnyanyua na kumwambia Kuwa nimemsamehe .
*******
Majila ya usiku baada ya kupata chakula nikamwambia mume wangu.
“Unajua moyo wangu umekataa kabisa kumsamehe mama Abbas, Najitaidi sana lakini mashindwa “
“Ni Jambo la muda tu nje wangu na Utakuwa Sawa, just relax and live your life “
*******
Siku ziliendelea kwenda na hatimaye mwaka mmoja ukapita na Mage na victor Wakajaaliwa katot kao kamoja uku wakiwa na happy marriage.
Siku moja nikiwa ofisini nilipokea siku simu kWa Abbas Ba alikuwa na furaha sana akaniambia.
“Ma mkubwa Mtoto wetu Amefika Nyumbani jamani ni wa kike na tumefanikiwa kupata Mtoto Mwenye miezi minne tu “
Walahi ilikuwa ni habari njema sana na Abbas nae akapata kuitwa baba kWa Mtoto ambaye ame adopt kWa njia halali kabisa.
Kuanzia hapo maisha yakabadilika. Kabisa, pande zote sikuwa na amani na furah na kila mtu alimuheshimu mwenzie kWa nafasi yake.
…………MWISHO………