ALINIACHA KWASABABU SIZAI
Sehemu 11 – 12
💙🤎💙🤎💙🤎💙🤎
Kwanza sikuamini kumuona baba yangu yangu akiwa katika hali kama hiyo, baba yangu ni mtu wa serious sana sana Kwahiyo ili tendo la yeye kupiga sarakasi kaama hivi Lilinishangaza sana.
“Aaaah Mungu Mwema sana na Mimi Nina mjukuu sasa, Mungu Mwema na Mimi naitwa babu “
Alizungumza baba Angu uku akijichezeza kWa furaha Sanaa kisha akanigeukia na kuniuliza.
“Mjukuu wangu anaitwa Nani ?”
Haraka nikajibu.
“Anaitwa Daniel baba”
“Aaaaah Kwahiyo Mimi naitwa babu Daniel kwa sasa, we mama Zayana Kuanzia Leo sitaki kukusuikia ukiniita Sijui mume wangu, Sijui laazizi niite babu Daniel “
Kwanza pia nilishangaa na kuniuliza hivi baba ajastuka kusikia Kuwa Jina la Mtoto ni la Kristo, je ni Sawa kwa upande wake au, aaah Walahi baba alijua kunichanganya.
Baada ya muda nilitulia na kuanza kuzungumza.
“Aaaah baba na mama, najua hapa katikati tumekuwa na mambo Mengi sana, tumekuwa na kila aina ya nikwaluzano ambayo imepelekea sisi kutengana kwa Namna moja au nyingine, hii hali imekuwa ikiniumiza sana ila Sijui kWa upande wenu, hii hali ni zaidi ya pigo kWa upande wangu, mpaka sasa naashindwa kujua kosa langu ni nini lakini niko hapa kuomba radhi kWa kosa lolote lile ambalo mimi niliwakosea”
Nilimaliza kuzungumza na kupiga goti.
Baba yangu akaniwai na kunikumbatia kisha akaniambia.
“Siku zote Binti anayeomba radhi kwa wazazi wake uwa anastahili kumbato Kubwa sana kutoka kWa wazazi wake, Zayana unatakiwa kuelewa Kuwa haukuwai kutukosea ni Mimi nilipumbazika na Maneno ya mume wako ambayo sikuwa nimeyafanyia uchunguzi wa Namna yoyote ile, kWa sasa Nimejua makosa yangu na niko tayali kuomba radhi na unisameehe Binti yangu “
Aaaaaaah hii ni zaidi ya release kwenye moyo wangu jamani, nilijikuta nikilia sana na mwisho nikatulia, kWa upande wangu nikachukua nafasi hiyo hiyo na kumtambulisha dokta Joel kWa wazazi wangu na kuwaambia Kuwa yeye ni mume wangu Mtalajiwa.
KWa upande wa wazazi wangu Wala awakushtuka zaidi kila mtu Alimkaribishaa baba wa Mtoto wangu na kutupatia kila aina ya baraka.
Siku hiyo ilikuwa ni siku ya furaha sana sana kwenye maisha yangu, kitu ambacho nilikuwa nakiogopa sana ni baba yangu kumkataaa mzee Joel lakini kwa uwezi wa Mungu amekubaliwa bila vita.
Siku hiyo dokta Joel akaondoka na kuniacha Mimi na wazazi wangu, kWa upande wa wadogo zangu walivyorudi kwenye mizunguko yangu walifurahi sana, Siku hiyo kumshika Mtoto wangu ilikuwa ni nadra sana, Yaani nikimshika ujue ni kumnyonyesha tu baada ya hapo anachukuliwa Kama sio na baba Basi na mama, Kama sio mama na baba Basi ni ndugu zangu.
******
Nilikaa Nyumbani kwetu siku Kama Tatu au nne kisha my wangu akanifuta Nami nikarudi mjengoni kwangu ambapo Daniel wangu alikuwa akisubiliwa sana na ndugu zake wengine, kiufupi Kijana wangu alikuja na Bahati ya kupendwa Bwana, Yaani alipendwa sana.
Baada ya muda dokta Joel akaanza process za uchumba Nyumbani kwetu, mwisho akatoka mahali na kila kitu, na mwisho kabisa Mimi na dokta Joel tukafunga ndoa kanisani kabisa.
Ndoa yetu Bwana haikuwa Kuwa kiivyo kwenye macho ya watu lakini kwa upande wangu ilikuwa ni zaidi ya ndoa, kWa upande wangu ilikuwa ni kila kitu na Rasmi kabisa nikawa Mrs Joel.
Maisha yaliendelea kusonga na kila siku nilimuomba Mungu anitunzie hii furaha ya familia maana mambo ni Mengi sana duniani.
Siku moja nikiwa ofisini, secretary wa ofisini kwetu, akaja ofisini kwangu na kuniambia.
“Zayana kuna mgeni wako hapo nje, amejitambulisha Kama Amina, nimeshindwa kabisa kumkaribisha ofisini kwako maana Sijui Kama mnafahamiana”
“Oooooh Mwambie NAKUJA”
Nilijua tu Kuwa ni Amina mke mwenzangu kwenye ile ndoa yangu ya Kwanza.
Niliweka vitu vyangu vizuri kabisa kisha nikatoka nje ambapo Nilimkuta Amina akiwa amejiinamia tu kwennye benchi la mapokezi na alionekana kutokuwa Sawa kabisa.
“Amina “
Nilimuita baada ya kumfikia.
“Eeeeh da Zayana, shikamoo, shikamoo dada Angu, nisamehe sana mwaya Nimekuja ofisini kwako “
Yaani ukimuangalia tu Amina unaona kabisa Kuwa hayuko Sawa, nilimuangalia kwa muda mwisho nikamshika mkono na kwenda nae kwenye restaurant ya pale Jilani.
“Agiza chochote kile ambacho unaweza ukala kWa amani “
Nilimwambia amina.
Basi akaagiza chakula na kuanza kula, akiwa anaendelea kula nikamuuliza.
“Kwanini umekuja kunitafuta ?”
“Aaah da Zayana Naomba kwanza Nile kwa amani halafu tutazungumza, sikumbuki Mara ya mwisho lini kupata msosi mzuri Kama huu “
Nilijikuta nikizidi kumuonea huruma Binti wa watu mwaya.
Baada ya kumaliza kula akashushia na maji kisha akaanza kuzungumza.
“Kwanza kabisa Nimekuja kukuomba radhi, unajua siku ile tulivyokutana sikuwa nimekuomba radhi ata kidogo kWa sababu pia atukupata muda mzuri wa kuzungumza, da Zayana dunia imenifunza na Inazidi kunifunza”
“Amina kila mtu Ana mapito yake Mdogo wangu, kWa upande wako bado ujachelewa kabisa, bado wewe ni Mdogo Sanaa, Una nafasi kubwa sana ya kurekebisha makosa yako nakuomba Mungu akuinue Tena “
“Ni kweli lakini upande wangu ni Kama nimeshafeli, unajua da Zayana Mimi ni Binti ambaye natokea kwenye familia yenye shida sana lakini pia Mimi ndio nategemewa na mama yangu kwenye kila kitu, mama yangu sio mtu mzima sana ila ni amepata na shida ya akili, kwetu tumezaliwa wawili lakini dada yangu ametutelekeza sisi”
“Ooooh pole sana amina “
“Asante sana, Abbas bado ananisumbua sana, anakuja Nyumbani muda wowote ule na kuniumiza anavyotaka kisha anaondoka , Mara ya mwisho Amekuja pale ninapokaa na mama yangu na kuharibu genge langu ambalo nilifungua kupita Pesa ambayo Ulinipatia, kWa sasa Sina ata mtaji wa kutembeza mboga kwenye beseni, Abbas amewatangazia watu Kuwa Mimi ni mgonjwa na kufanya watu kunitenga pale Mtaani kwangu”
Ila Abbas ni Kama shetani jamani, Sijui ata Kwanini niliwai kumpenda huyu kaka kwenye maisha yangu, Sijui nilikuwa ni kipofu wa mapenzi mwaya.
“Kitu ambacho nilikuwa Naomba ni mtaji tu dada angu, najua Mimi na wewe atujawai kuwa na ukaribu mzuri lakini Nimeona wewe ndio mtu Pekee ambaye naweza nikazungumza nae “
“Usijali Amina nakuelewa sana, Mimi Nina wadogo zangu Kama wewe hivyo naelewa sana ile foolish age ilikuwa ikikudanganya, aaah kwanza kabisa nitakupatia Pesa ya kodi ili uende mbali kidogo na abbas, lakini pia nitakupatia na huo mtaji ambao utakusaidia Kama Utakuwa na akili nao”
Kwakuwa sikuwa na cash, Mimi na Amina tukaongozana na kwenda kwenye ATM na nikamtolea kiasi cha Pesa na kumpatia.
“Eeeh da Zayana Asante sana, huu ni zaidi ya msaada kwa upande wangu”
Tukiwa Tunaendelea kuzungumza simu yangu ikaita na Mage ndio alikuwa akipiga haraka nikapokea.
“Aaaah mama Sijui Daniel ana nini Leo, Yaani analia sana sana ni masaa mawili sasa analia pasi na kunyamaza.
Alizungumza mage akiwa na wasiwasi sana.
My zangu uchungu wa mwana aujuaye mzazi weeeh kWa jazba nikamuaga amina.
“Aaah kwaheri Amina, hi simu niliyopokea inaonesha Kuwa Mtoto wangu hayuko Sawa uko Nyumbani “
“Da Zayana Una Mtoto ??”
Sikuweza ata kujibu swali lake nikamuacha na kuondoka.
*******
Hatimaye Mtoto wangu akafikisha mwaka mmoja na miezi Kama 8 hivi na muda huo Zayana Mimi nilikuwa na tumbo kubwa tu la miezi 7 😂🙌 Yaani hakuna kupumzika ni bandika Bandua Mungu si amefungua kizazi changu lakini 😅.
Siku moja nikiwa Mimi na Mtoto mkubwa wa kiume wa mume wangu lakini pia na mke wake, tuliingia zetu sokoni na kununua mazaga zaga, gafla nikakutana uso kWa uso na Abbas akiwa na mama yake nika……..
SEHEMU 13 na 14
💙🤎💙🤎💙🤎💙🤎
Niliganda nikiwashangaa lakini pia na wao waliganda wakinishangaa aswaaah tumboni kwangu, Walahi hakuna mtu aliamini Kuwa Mimi ni mjamzito, Abbas na mama yake walihisi kaama wako ndotoni hivi.
Muda huo huo akaja Mtoto wa kiume wa mume wangu na Kunikabizie Daniel na kusema.
“Aaah huyu Mtoto wako analia hatari tunaonekana Kama tumemuiba hivi “
Hapo Abbas na mama yake ndio walizidi kushangaa zaidi Yaani inawezekanaje mimi Kuwa na Mtoto mmoja halafu saa hizi Tena Nina tumbo kubwa zaidi, bado wakazidi kushangazwa na mkononi kwangu ambapo nilikuwa Nina Pete Mbili moja ya uchumba nyingine ya ndoa.
“Hii inawezekanaje ??”
Mama mzazi wa
Abbas alijiuliza uku akimuangalia Kijana wake usoni.
“Ahaha mama Bwana, hivi kumbe bado ujamjua Zayana vizuri eeeh, Yaani hii ni michezo
Yake tu, Yaani ameamua kuweka manguo tumbo na Mtoto wa kuigiza ili anirushe roho, najua Kama Zayana Unanitaka Leo kesho lakini siwezi Kuwa na wewe mgumba “
Nilitabasamu kisha nikazungumza.
“Itependeza Kama mtaniachia njia ili niweze kupita halafu mkaendelea na opinion zenu vichwa maji nyie”
Mama mzazi wa Abbas akanyoosba mkono wake na kushika tumbo langu, nilijitaidi kukwepa lakini mwisho akafanikiwa kushika.
“Weeeh mimba kweli “
Mama Abbas alilipoka kWa sauti ya juu sana na Kuwafanya watu wa Jilani kitu Angalia 😂🙌 Yaani ukisikia kilio cha watesi ndio iki sasa, Yaani awaamini Kuwa Leo hii ni mjamzito.
Walibaki wakinishangaa Nami nikawapita na kuondoka zangu, moja kwa moja nikaenda sehemu ya parking na kutulia maana nilichoka sana Kuwaacha watoto wangu wa kubwa wakiendelea kununua zagazaga.
Nikiwa bize muda huo huo Abbas na mama yake Wakaja, mwanzo Nilihisi Kama wameamua kunifuata hivi, lakini sio kweli walikuwa wamepaki gari Yao Karibu na gari yangu.
Kwa wakati huo tayali nilikuwa Nina Ndenga moja Matata na wao walikuwa na gari ile ile ambayo niliwaacha nalo.
Abbas akanisogelea na kuniuliza.
“Kwahiyo umeolewa??”
Niliishia kumuangalia tu sikuona umuhimu wa kimisini mpuuzi Kama huyu.
“Zayana nakuuliza wewe ni umeolewa eeeh ? Zayana Kwahiyo ulikuwa ikipata mimba zangu unatoa si ndio ??”
Ila huyu baba ameanza kupata uchizi 😂🙌 sikuwa nataka kumjibu lakini kWa utulivu wa hali ya juu nikamuuliza.
“Hivi ni lini Abbas uliwai kumpa mwanamke mimba ? Ni lini mmoja kati ya wanawake zako alishika mimba na ikawa kubwa au ata ikaharibika uku ukishuhudia ??”
“Unataka kumaanisha nini Zayana eeeh, Yaani unataka kusema me Sina uwezo wa kuzalisha au ? Zayana mimi ni mwanaume na nusu Sawa”
“Kila la kheri mwanaume na nusu “
Nilijibu na wakati huo wenzangu wa kafika kWa pamoja tukapanda kwenye gari na kuondoka uku nikiwaacha wakiendelee kunishangaa.
“Ni kina nani wale mnaonekana kufahamiana ??”
Kaka wa Mwanangu akaniuliza maana hakuwa Amesikia maongezi yetu.
“Ahaha Yule ndio Abbas na Yule ni Mamaa yake, Nina Uhakika Leo atesi chakula akitashuka mwilini mwao”
Nilijibu uku nikicheka.
“Kumbe ndio Yule 😁 eeeh mtanisamehe lakini khaaaaah hamkuwai kuendana Bwana kaka mweusi Kama lami ni kitu gani kile 😅 aka kwanza afadhali ujazaa nae maana mngezaa usiku wa manane “
Walahi sikuwa na plan ya kucheka lakini huyu Kijana wa dokta Joel alijua kunichekesha.
“Babe sio vizuri ujue”
Mke wa Kijana huyo akamwambia mwanaume wake uku akijitaidi Kubana kicheko chake.
Basi tulirudi Nyumbani na maisha mengine kuendelea, nyieeeh Yaani Kama ku move on me niliondoka na kila kitu kwenye maisha ya Abbas Yaani sikuwa na kumbukumbu yoyote ile kumuhusu yeye, Yaani nimekutana nae lakini Kama Sijakutana nae Yaani sikuwa nikikumbuka kitu chochote kile.
Majila ya usiku nikiwa na my wangu chumbani, dokta Joel akaniuliza.
“Ni kitu gani unataka nikufanyie mke wangu ??”
Niligeuka na kumuangalia vizuri na kuzungumza.
“Umeshafanya kila kitu kwenye maisha yangu,umefanya kila ninachokiitaji”
“Hahaha muone kwanza, Ila Zayana unanifanya nijione Kijana kila iitwapo Leo, Yaani kuna muda naona Kama watoto wangu ndio wa kubwa halafu Mimi ndio mchidreni 😂🙌.
“We mzee wewe Ebu muogope Mungu Basi “
Nilimwambia uku nikaingua kicheko, Yaani huyu mbaba ana vituko kama Binti yake mage.
Siku iliyofuata ilikuwa ni weekend, aaahh siku hii Bwana tulitembelewa na baba na mama yangu, baba yangu alionekana Kuwa na wasiwasi sana.
“Uko salama kabisa Binti yangu ??”
Baba aliniuliza.
“Ndio baba Mbona Kama huamini hivi au kuna ndoto mbaya umeota ??”
“Hapana Binti yangu, unajua Jana usiku alikuja Abbas Nyumbani na alikuwa akilia sana, Amelia sana mwisho akataka kujua unaishi wapi, lakini pia Alizungumza Maneno ambayo haya Kuwa mazuri “
Hapo dokta Abbas akamuangalia na kuniambia.
“Huyu mwanaume wako nitamkata masikio awe Kama toinyo “
“We baba tuheshimiane Sina mwanaume anaitwa Abbas mimi “
“Sawa mke wangu mrembo, sasa baba nikutoe hofu kabisa kabisa, Zayana yuko katika mikono salama salimini na huyo Abbas akitaka kutangulia mbele za haki acheze na mwanamke wangu “
Alizungumza dokta Joel akiwa serious sana.
“Kiukweli napata wasiwasi sana, akili ya huy Kijana sio nzuri ata kidogo, sasa hivi amekuwa na maisha ya kishetani kabisa, pale Nyumbani kwake anaishi na wanawake Wapatao Sita wote anawalipa, Yaani ni Kama ametengeneza mashindano kwamba atakayepata Mimba anabaki na kuolewa kabisa “
KWa haraka nikajibu.
“Mwaya amepaniki Kijana wa watu”
********
Siku ziliendelea kusonga na hatimaye siku ya kucheza sebene la pili iliwaidia, nyieeeeeh maumivu ya uchungu hayazieleki kabisa kabisa, Yaani uwiiiiiiiih .
Finally nimajipatia Katoto kangu kwa kike, Yaani Mungu ni Kama alijua kunibadilishia uzazi, familia ilikuwa na furaha sana kWa kupata mwana familia Mpya.
Binti yangu niliamua kumuita Anath ili kuenzi Jina la Mtoto wa kwanza wa mume wangu, Yaani Yule Binti wa dokta Joel ambaye Alifariki.
SEHEMU 15 na 16
💙🤎💙🤎💙🤎💙🤎
Kama ni furaha Basi ujio wa Binti yangu ndio uliongeza furaha Mara dufu, Kiukweli familia nzima ilifurahi sana aswaaah niliposema kuaa Mtoto huyu ataitwa Aneth kwaajili ya kumuenzi dada mkubwa wa familia.
“Zayana nini nikupe mama Angu ili uelewe ni kiasi gani umenifurahisha nambie mpenzi chochote na fanya kwaajili yako “
Alizungumza dokta Joel Tena mbele ya wazazi wangu, Ila huyu baba nae jamani 😂🙌 hivi anajiona yeye bado ni mchidreni eti, Yaani mbele ya mtu ambaye wanapishana miaka mitatu tu anaanza kuonesha mahaba.
Walahi nilijikuta nikiona aibu na kushindwa kujibu Maneno yake aliyoniambia.
Baada ya kila mtu kumuona Mtoto, wote wakatoka nje na kuniacha Mimi na mume wangu chumbani kwetu kwani tulisharudi Nyumbani.
“Joel ujue unazeeka vibaya wewe mume wangu “
Nilimwambia my wangu uku nikimcheka.
“Kwanini ??”
“Yaani baba Angu alivyokuwa Anakuangalia unavyojobebisha 😅 uwiiiih nilijikaza tu nisicheke, Nina Uhakika pale baba Angu alikuwa Anajiuliza hivi huyu aoni kama sisi tupo hapa “
“Aaaaah mzee nae aache ukololoni kwakweli, mke wangu Yaani Mimi Likija suala la kudeka na kukudekeza Walahi Sitaacha, nataka watu wavimbe na wapasuke maana sina huo muda kwakweli “
“Wachaaaaah weeeh, huyu ndio my wangu sasa, tuache utani, Ila
We baba me nakupenda mwenzio”
“ Nakupenda mke wangu”
Hatimaye Binti yangu akatimiza mwezi mmoja na upande wa Daniel wangu aliendelea kukua na alikuwa Mjanja sana muda wote alikuwa bize na dada yake Mage. Yaani mage na Daniel walikuwa na bondi kubwa sana utazani mage ndio mama mzazi wa Daniel wangu.
Bwana bwanaaaah, baada ya miaka mingi kupita pasi na kukutana na rafiiki zangu wa chuo uko, hatimaye kulikuwa na meet up party 🎉 ambapo tulitakiwa kukutana sote na kulikuwa na Michango kadhaa.
KWa upande wangu kwanza kabla ya kufanya chochote nikamshirikisha mume wangu ambaye alinijibu hivi.
“Kikubwa uwe na furaha lakini pia uwe salama, Nafikili hii ndio chance yako ya kwenda kukutana na Rafiki zako ambao Abbas alikutenganisha nao, hii ndio nafasi yako ya kuonesha ulimwengu Kuwa kila kitu ni mipango ya Mungu “
Aaahh my zangu mume ninae na ninatamba nae nyie wenzangu mkikasilika mkajitundike mie sijali loloseeeeeeh mbwa nyie 😂🙌.
Hatimaye siku ya tukio lilifika nyieeeeeeh maandalizi yangu yalikuwa sio ya kitoto kwanza familia nzima ilishiriki kuniandaa, siku hiyo nilipendeza sana nilikuwa kama msichana vile kumbe ni mama wa watoto wawili lakini pia Nina miaka ya 30’s uko 😅.
KWa mwendo wa madaha nikatoka nje nikiwa na Aneth wangu princess wa familia, uwiiiiiiih kwanza nilishtuka sana baada ya kukutana na gari aina ya G wagon lakini pia ilikuwa na preti Namba ya Jina langu full uwiiiiih hii familia inanipa raha jamani.
“Happy birthday mama “
Walizungumza watoto wa mume wangu na hapo ndio nikakumbuka Kuwa siku hii pia ni siku yangu ya kuzaliwa.
Niliwakumbatia kWa nguvu sana na kujikuta nikianza kulia, hawa watoto sina kikubwa nilichowafanyia lakini upendo Wanaonionesha ni level nyingine kabisa.
“Aaaah hatutaki mambo ya kulia, ata hivyo utaharibu make up bure “
Aliniambia mage na kuanza kuniweka vizuri.
“Sasa Leo Bwana ladies mtatoka pamoja na sisi tunamtoko wetu “
Alizungumza mume wangu kisha wakapanda kwenye gari na kuondoka, kWa upande wangu Mimi na mage na Aneth Mdogo , Tukapanda kwenye gari yetu Mpya na kuondoka, siku hiyo niliondoka na mage kwenda kukutana na marafiki zangu wa shule.
Kwanza nilivyofika tu kila mtu akawa anaangalia ndinga
Yangu na kujiuliza ni Nani anashuka kwenye ndinga Kama hiyo, Kiukweli hakuna mtu ambaye alikuja na ndinga Kali kama yangu.
KWa furaha ya hali ya juu nikashuka chapu na kuwakimbilia Rafiki zangu ambao walikuwa wakinikumbuka kidogo ata kwenye simu.
“Uwiiiiiih Zayana I can’t believe that it you “
Alizungumza shemeji yangu Yule ambaye kipindi kile alikuwa ananinisaidia kuweka mambo Sawa kwa Abbas.
“Aaaah Mungu Mwema kwakweli”
Muda huo huo Mage akaja akiwa na Mtoto wangu, kwanza kabisa nikamkutansha mage mkaka huyo ambaye tangu nimemfahamu sikuwai kumsikia akiwa na sekendo chafu lakini pia ni mstaarabu sana.
“Aaah victor huyu ni Binti yangu Mtoto wa mume wangu anaitwa Mage, na huyu ni Binti yangu Mwenyewe kabisa anaitwa Aneth “
“Subili kwanza, Yaani huyu ni Mtoto wako kabisa kabisa Yaani umemzaa wewe ??”
“Ndio Mbona Kama uamini ? Victor nakumbuka ni wewe uliwai kuniambia Kuwa wakati wa Mungu ni wakati sahihi sana. “
“Daaaaah kweli Mungu Mwema”
Basi victor akamchukua Aneth na kuanza kuzunguka nae akiwa na mage lakini kwa upande wangu nilikuwa bize kusalimia watu wengine maana ni wengi sana.
Kila mtu hakuwa akiamini muonekano wangu Mpya, Yaani nilikuwa Kama Ka Binti Afu Mbili kumbe ni mshangazi wa kwendaaaa 😂🙌.
Nikiwa naendelea kuzunguka uku na uku, niliweza kufika kwenye bustani moja nzuri sana ambayo ilikuwa imejaa sana gafla nikavutwa na kujikuta Nikiingia Ndani ya Bustani hiyo pasi na kutalajia.
“Abbas ni nini jamani kuvutana eeeh unataka kuniumiza au ??”
Nililalamika baada ya kuona Kuwa anayenivuta ni Abbas.
“Naomba tuzungumze mke wangu”
Eeeeh Makubwa haya , mke since when ? 😁 baba bure ili jamani
“Ebu Niache kwanza akhaaaaah, mambo gani haya, halafu tuneshimiane, hiyo mke vipi ndugu yangu eeeh hiyo mke ni ya nini class mate ?”
Nilimuuliza kwa kumkejeri kabisa mama yeye si alijifanya Chizi wacha nimuoneshe Mimi ni Nani.
“Zayana najua ni kiasi gani unanipenda, Angalia jamani, najua umekubali kuja uku kwakuwa umejua kabisa Mimi nitakuweo, Zayana ndoa yetu iliandikwa na Mungu ujue”
“Abbas Rafiki yangu amka mwaya Yaani sasa hivi unajikokolea”
Muda huo huo sauti ya kiongozi wetu ikasika na sote tukaenda kwenye sehemu husika ambayo iliandaliwa kwaajili ya mazungumzo.
“Kiukweli kwa upande wangu hii siku nilikuwa naona Kama inachelewa sana, unajua ni muda mrefu snaa umepita na mambo Mengi yanetokea, Nafikili Leo ni siku ya kurudisha furaha zetu tulizikuwa nazo kipindi iko, lakini pia Nina imani Kuwa bado upendo upo Ndani yetu maana daaaah muitikio umekuwa mkubwa sana.
Muda huo huo akaja Mage akiwa na Aneth ambaye alikuw aakilia sana.
“Mama mnyonyeshe tu ili niende nae kule hapa atakusumbua”
Kila mtu akaganda asielewe kitu, kWa kifupi hakuna ata Rafiki yangu mmoja Aliyekuwa akijua Kama Nina Mtoto au watoto, lakini pia hakuna mtu alikuwa anajua Kama Mimi nimeolewa wa kWa Mara nyingine ingawa wengi walikuwa wanajua kuwa nimeachana na Abbas na sababu ikiwa ni kutokumzalia.
“Wait guys naona yuko na surprise hap, Zayana nini kinaendelea? “
Kiongozi wa hiyo even aliniuliza maana ata yeye alikuwa aamini anachokiona.
Nikatanasamu na kunyoosha mkono wangu wa Pete juu na kuzungumza.
“Mnachokiona ndio iko hivyo , aaaah nimeolewa ndoa ya ki Kristo, lakini pia Nina watoto Sita, ambapo wanaume watatu na wanaume watatu “
“Sitaaaaah “
Kila mtu akashtuka sana maana ni miaka miwili tu na miezi kadhaa imepita tangu kuachana na Abbas.
“Yaaah Sita, watoto wa nne ni watoto wa mume wangu na wawili ni kwangu, huyu mbele yenu anaitwa Mage ni Binti wa mume wangu “
“Oooooh jamani so lovely 🥰 kwanza nimependa amekuita mama”
KWa hasira Abbas akanyanyuka na kutoka eneo ili.
INAENDELEA….