
za Mapenzi, Maisha na Uchawi Mautundu Kitandani
ALINIACHA KWASABABU SIZAI
Sehemu ya Sita
💙🤎💙🤎💙🤎💙🤎
Habari ni Kama zilikuwa njema kwangu hivi, kWa shauku nikamsogelea shemeji yangu na kumuuliza.
“Weeeh unasoma kweli au ??”
“Shemeji naweza je kukudanganga lakini, huyu msichana simjuagi lakini Mara yanngu ya kwanza kumuona ni Leo na Nimemuona kWa mshikaji wangu, aaaah Walahi Abbas amekurupuka kumuona huyu msichana Yaani hapa ni anapigwa tukio demu anaweza huyu kwanza anaonekana kabisa Kuwa ni Binti wa mjini huyu “
“Aaah ila shemeji ni habari njema sana kwangu lakini Abbas awezi kunielewa kabisa na sio tu kunielewa Yaani kunisikiliza atotaka, Naomba sana masada wako “
“İli limeisha shemeji yangu, Yaani nitatafuta muda wa kuzuungumza na Abbas lakini pia ikiwezekana na ushaahidi kabisa “
“Utakuwa umenisaidia sana shemeji yangu “
Basi tukaagana kisha huyo nikarudi Ndani.
İle nimeingia tu sebuleni nikakutana na Kidomo domo cha Amina.
“Hivi Zayana uoni aibu kuingiza wanaume Ndani ya Nyumba yako ya ndoa ??”
Nilimuangalia Amina kWa kumpandisha na kumshusha kisha nikamuuliza.
“Unaweza ukaniambia ulienda wapi ?”
“Zayana acha kubadilisha masa hapa, nikuulize swali la muhimu, hii nguvu ya kuingiza mwanaume kwenye nyumba ya mume wako umetoa wapi ? Yaani ndio nazidi kuamini Kuwa wewe mwanamke ni wa Ovyo snaa Walahi, Yaani kuondoka muda mfupi tu tayali umeshaita Kibenteni Sijui ndio kinani iko mwaya”
Walahi nilijikuta nikipatwa na hasira sana na Kutamani ata kukachapa ambao lakini nilitulia baada ya kujua Kuwa yeye ni mjamzito.
“Kaa mbali na Mimi Amina Utakuwa kunichikia nakuambia ukweli “
Basi baada ya hapo nikapitiliza na kwenda chumbani kwangu, moja kWa moja nikashika simu yangu na kukutana na missed call nyingi sana za dokta Joel ambazo ziliniyosha kuliko kawaida maana hakuwai kunipigia kiasi iki hivyo haraka nikampigia.
“Umenishtua sana dokta Joel shida nini ?”
Nilimuuliza pale tu alipopokea simu.
“Aaaah mambo yamejikuta Bwana, nimezoea kutibu watu lakini Leo siwezi ata kumtibu Binti yangu Mwenyewe “
“Unamaanisha nini ??”
Nilimuuliza nikiwa na wasiwasi wa hali ya juu.
“Nipo aghakan hospital kama unapata muda usisite kuja yapı Mengi ya kujifunza hapa”
“NAKUJA “
Nilijibu na kukata simu kisha nikajiandaa na nilipomaliza tu nikashika simu na kumpigia Abbas kwaajili ya kumuomba ruhusa.
Nilimpigia simu Abbas zaidi ya Mara 5 lakini hakupikea ata simu yangu moja, mwisho nikaamua kumtumia tu ujumbe Kuwa nataka .
Moja kWa moja nikafunga safari na kwenda hospital ambayo nimeelekezwa an dokta Joel , dokta Joel amekuwa ni mtu wangu wa Karibu sana, amekuwa mtu wa kusikiliza mambo yangu yote na muda wingine kusikiliza kilio changu na kunibembeleza ata Kama kwenye simu.
Nilifika hospital na kumkuta dokta Joel akiwa amekaa kwenye benchi la mapokezi, miguu yake haikutulia ata kidogo alibaki akiipiga piga chini kWa style ya kuitetemesha.
“Dokta”
Nilimuita na kWa haraka tukakumbatiana.
“Nini shida jamani ujue umenitisha sana kwenye simu ?”
Nilimuuliza baada ya kumaliza kusalimiana.
Dokta joel akashika mkono wangu kWa nguvu sana na moja kWa moja tukaelekea kwenye wodi moja hivi ambayo ni private, tulifika na kukuta msichana akiwa amelala, mwilini akiwa na bandeji za kutosha, lakini pia alitumia mipira ya gesi kwaajili ya kupata Pumzi.
“Ni Nani huyu ??”
Nilimuuliza.
“Ni Binti yangu wa kwanza anaitwa Aneth”
“Amepata ajali au ??”
“Nafikili tungekaa chini tupate kuzungumza vizuri.
Basi Mimi na dokta Joel tukaaa chini na kWa uchungu wa hali ya juu dokta akaanza kuzungumza.
“Huyu ni Aneth na ni Binti yangu wa kwanza Kama ambavyo nimekuambia, ajapata ajali Kama ambavyo unatalajia Bali ni kipigo kutoka kwa mume wake, Yaani mumewe amemchalanga na viwembe kila kona pasi na kujali maumivu ya Binti yangu “
Aaaah Walahi niliogopa sana, Yaani mwanaume anawezaje kumtenda mkewe Kama hivi.
“Zayana ili ni Funzo tosha sana kWa upande wako, Binti yangu hakuwai kuniambia ndoa yake Ina hali gani lakini Nina Uhakika haikuwa nzuri hata kidogo, na sababu ya Binti yangu kupigwa ni baada ya kumfumania mumewe na mwanamke mwingine Ndani kwake, Binti yangu amejaaliwa watoto wawili ambao kWa sasa wako likizo pale Nyumbani kwangu hivyo hawakuweza kushuhudia kipigo cha mama Yao “
Aaaah nguvu ziliniisha kabisa, nikabaki nikimuangalia tu msichana wa watu ambaye alikuwa na maumivu makali sana kWa wakati huo ni vile tu hakuwa aiiyasikia kwaajili ya Sindano ya usingizi aliyochomwa.
Nilikaa na dokta Joel Kama masaa matatu hivi na hatimaye Giza Likashika nafasi yake hivyo nikamuaga na kuondoka.
Nilifika Nyumbani kwangu Majila ya Saa 2 kasoro usiku, Picha linaanza nilifika na kukuta mlango umefungwa lakini Ndani kuna Mbili mkubwa sana na sauti ya Abbas na Amina zilisikika kWa mbali sana, nilijaribu sana kugonga mlango lakini sikufunguliwa mlango, nilimpigia simu Abbas lakini pia hakuokota simu yangu.
Aaah siku hiyo nilijua kuteseka pale nje, nilikaa sana mpaka Saa 7 ikanikutia nikiwa hapo nje na mwisho nikapitiwa na usingizi.
********
Hatimaye siku Mpya ikashika nafasi na nililala mlangoni imagine jamani 🥹😭.
Muda huo huo Abbas akatoka nje na alikuwa anaelekea kazini.
“Umelala wapi Jana ??”
Abbas aliniuliza kwa hasira mno kana kwamba sio yeye Aliyekataa kunifungulia mlango.
Nilimuangalia kWa dharau sana mwisho nikamsukuma na kuingia zangu Ndani , kWa muda huo nilijua kabisa Kuwa Abbas awezi kipigizana Kelele na Mimi kwani Anawai kazini.
KWa wakati huo mwili wangu haikuwa Sawa kabisa kutokana na baridi lililonipiga usiku kucha, hivyo moja kWa moja kwanza nikapitiliza jikoni na kuanza kujiandalia chai ili niweze kupasha mwili wangu joto.
“Naweza usiku wako ulikuwaje usiku wa Jana 😂 imagine mume wako Mwenyewe kaniambia usije ukamfungulia mlango huyo panya mweupe, mwanzo nilijua Kuwa Anatania kumbe alikuwa akimaanisha Bwana na huyo ndio Furaha yangu, Zayana nataka kukuona ukiteseka umu Ndani mpaka unyanyue midabwada yako na uondoke “
Alizungumza Amina Tena kwa kujiamini sana kisha akatoka nje.
KWa upande wangu niliweza kupata chai na moja kwa moja nikaenda kuoga, Walahi nilikuwa na usingizi sana hivyo nikachukua simu yangu ili niweke alam nipate kulala ata masaa mawili tu, lakini nilikutana na ujumbe ambao ulinishtua sana na ilitoka kwa dokta Joel, ujumbe huo ulitumwa tangu saa 10 alfajiri lakini ndio nauona Saa 3 hii na ulisomeka hivi.
“Aneth amefanikiwa kuamka na nimeweza kuzungumza nae, Kiukweli Binti yangu ameteseka sana na sasa anaitaji Kuwalinde sana watoto wake, atalı kabisa watoto wake wake Karibu na baba Yao, Nashukuru Mungu Kuwa nimefanikiwa kuzungumza na Binti yangu before umauti haujamchukua, lakini kWa sasa Jina la Binti yangu Aneth linaanza na marehemu “
Aaaah Walahi nilishtuka sana sana, nilijikuta nikitetemeka Sana kwa woga Yaani Binti wa watu ni Mdogo sana yaaani daaah wanaume hawa 😭🥹.
Haraka nikampigia simu dokta Joel na kuzungumza nae kisha nikajiandaa na kwenda msibani.
Mwendo ni ule ule, Mimi siwezi kuondoka Nyumbani kwangu bila kuaga, nilimpigia mume wangu hakupokea hivyo nimamtumia ujumbe.
Majila ya saa 10 jioni nikarudi Nyumbani kwangu na kumkuta mume wangu akiwa Nyumbani, Picha linaanza ile nafika tu nikapikelewa na mabao Mvua, unayajua mabao mvua wewe 😂 Yaani nilipigwa mabao ambayo hayana idadi 😂.
“Zayana nimekuchoka sana kwakweli na kunakoelekea utafia kwenye mikono yangu Walahi, Ingia chumbani paki kila kilichokuwa chako na uondoke, kuhusu taraka zote Tatu Zipo kitandani kwako.
kwnza nika……
SEHEMU YA SABA
💙🤎💙🤎💙🤎💙🤎
Walahi nilishtuka sana mambo ya taraka Tena jamani Tena zote Tatu kWa pamoja 🥹 hii inawezekana vipi, Yaani huyu mwanaume ananiachaje kWa mfano🥹.
“Abbas unaongea kuhusu nini ??”
Nilimuuliza nikiwa nalia maana sikuwa naamini kwamba ndio tumefikia level ya kuachana kabisa.
“Wewe mgumba Sijui tasa, beba kila kilichokuwa cha kwako na uondoke Sawa ? Sitaki kukuona Wala kukusikia kwenye maisha yangu laana mkubwa wewe “
Weeeh haraka nikapiga goti chini na kuanza kuomba radhi maana kuachika sio mchezo tena na mtu ambaye unampendaaa weeeh 🥹 hapana jamani huyu kaka mimi nampenda sana.
Abbas na Amina wakashirikiana na kunisukumia nje kisha vitu vyangu na taraka vikafuatia kWa nyuma.
Mpaka hatua hiyo sikuwa na Namna sikuwa na chaguo, Yaani Nipo official single kabisa kabisa, Yaani nimeachika na taraka Tatu🥹.
Nikabeba kila kilichokuwa changu na kurudi Nyumbani kwetu ambapo nilikutana na Kisanga cha baba yangu ambaye alikataa kabisa kunipokea.
“Hivi Unafikili hii aibu ni ndogo kwetu wewe mbwa wewe “
Baba yangu alinifokea uku akifinya masikio yangu na peni, eeeeh hii wanaelewa wanafunzi wa Santi kayumba tu, wale wa magari ya njano mtuache kidogo.
“Baba Zayana Mtoto ataenda wapi jamani eeeh, ata hivyo Giza linaingia mume wangu”
Mama mwaya akajaribu kunitetea.
“Unataka kuondoka na Binti yako au ? Haya paki na wewe uondoke, na ukinyanyua miguu yako hapa hakikisha Kuwa unaishi na Mimi Kama watu ambao hatujuani kabisa unanielewa ?? “
Eeeeh nikaona huu nao Msala sasa, Yaani mama yangu miaka yote hiyo ya ndoa Leo hii aje kuachika kisa Mimi aaah sio Sawa kabisa.
“I’ll go daddy “
Nilizungumza kwa huzuni sana uku nikifuta machozi maana nimeshalia vya kutosha.
KWa wakati huo kwakweli sikuwa Sawa kabisa imagine, kupewa taraka Tatu na mume halafu kufukuzwa Nyumbani na baba yako mzazi ambaye anaamini kabisa Kuwa Mimi ndio nimevunja ndoa yangu.
Kitu cha kushukuru ni kwamba nilikuwa na Pesa kidogo hivyo nikaingia uswazi kwenye zile Nyumba za wageni za bei rahisi na kujipatia Ka chumba kangu Ka moja na kujistili.
*******
Week nzima ilipita na ndio akili yangu ilianza Kuwa Sawa hivi, Maana week nzima mimi nilikuwa ni mtu wa kulia tu na Kuwaza sana kuna muda nilikuwa natamani ata kujiua lakini nafsi yangu ilinisuta sana.
Siku hiyo nilifunga safari na kwenda kwa dokta Joel maana mambo yalivyoingiliana sikuweza ata kuudhulia Mazishi ya Binti yake laki pia sikuweza ata Kuwasiliana nae.
Nilifika Nyumbani kwake na kukuta watoto zake kadhaa na wajukuu zake, lakini yeye hakuwepo .
Walahi watoto wake ni watu wakarimu sana, imagine wameniona siku moja tu siku ya msiba wa dada Yao lakini Leo hii wamenichangamkia utazani ni watu ambao Tunafahamiana.
“Yaani baba alikuwa akikuulizia sana, muda mwingine alionekana kuchanganyikiwa baada ya kuona Kuwa simu yako haipatikani”
Oooooh my zangu sikuwaambia Bwana, Abbas alinipokonya na simu kabisa na kila kitu eti kWa Kuwa yeye ndio alininunulia hivyo akaichukua, hapa ndio tunaweza kuomba ule Wimbo wa kanununa simu kampa demu walivyoachana kampokonyaa 😂🙌.
Baada ya muda dokta Joel Aliweza kurudi Nyumbani kwake Walahi baada ya kuniona alifurahi Sana, uku akiwa na furaha ya hali ya juu, akaniuliza.
“Zayana where have you been? Nimekutafuta sana umenipa wasiwasi sana wewe Binti “
Aaah kwakuwa bado Nina maumivu makali , nilijikuta nikimkumbatia kWa nguvu sana na Kuangua kilio cha hali ya juu kama mwanafunzi aliyekutwa na ujauzito.
“Nisamehe sikuweza kuudhulia Mazishi ya Binti yako, Nisamehe sikuweza Kuwa Karibu na wewe ingawa uliitaji sana kampani yangu, dokta yamenikuta mimi, yamenikuta mwenzio “
Aaah nilimuelezea dokta Joel kila kitu, kwanza akaniomba nitulie na kWa muda huo mwili wangu ulikuwa wa moto sana, kwanza nikapatiwa dawa ambazo ata Mimi sikuwa nazifahamu, baada ya dakika kama 10 hivi, nilijikuta nikipata usingizi Mzito sana sikuweza ata kustaimili macho yangu mwisho nikalala.
Nilikuja Kuamka Majila ya saa 2 usiku, kWa wakati huo nilikuwa Sawa kabisa sikuwa nikisikia ata maumivu ya kichwa Yaani kuna Namna Nilihisi ni Kama nimekuwa mtu Mpya hivi,
Walahi Sijui huyu mzee alinipa dawa gani lakini amenisaidia sana.
Nikatengewa maji ya kuoga na kwenda kuoga kisha nikarudi kwenye chakula, nyieeeh kuna muda nilitamani ata familia ya dokta Joel ndio ingekuwa familia yangu, Yaani ni familia ambayo Ina upendo sana na Inajali sana.
Baada ya kumaliza kula, niliweza kukaa na dokta Joel na kuzungumza.
“Zayana, Mimi na wewe kwa sasa tumekuwa ni watu wa Karibu sana, mimi na wewe tumekuwa ni watu ambao tunaongea Mengi sana, kWa upande wangu nimekaa na familia yangu yangu na tumeona tukusaidie, Yaani Kuanzia sasa wewe Utaishi hapa na sisi mpaka pale utakapopokelewa Nyumbani kwenu “
Nyieeeh sikuamini kabisa, haraka nikapiga magoti na kushukuru, maana sikuwa na uwezo wa kuendelea kulipia Nyumba ya wageni lakini pia ata Pesa ya kupanga chumba sikuwa nayo.
“Sijui niseme nini lakini nashukuru Sana, Yaani ujui ni kiasi gani najisikia amani, Mungu akubariki sana dokta Joel, lakini pia awabariki na watoto wako ambao wamekubali mimi kuishi nanyi hapa “
“Wewe ni familia yetu Zayana Sawa ? Wewe ni wa kwetu “
Aaaah my zangu, dokta Joel amebarikiwa
watoto wanne na wakike walikuwa wawili lakini sasa hivi amebaki mmoja tu, na wa kiume ni wawili ambao tayali Wanamaisha Yao uko, huyu wa kike ndio Anaishi na baba yake hapa kwao.
******
Siku nyingine ikashika nafasi na Majila ya saa 4 usiku, Mimi na Mtoto wa kiume wa dokta Joel tukafunga safari na kwenda kwenye Nyumba ya wageni kwaajili ya kuchukua mizigo yangu.
Tukiwa njiani tunarudi Mtoto wa dokta Joel akaniuliza.
“Hivi Zayana uliweje kuvumilia ndoa chungu kmaa hiyo ikiwa wewe hauna shida ??”
Kwanza nilishtuka sana kisha kimoyomoyo nikajiuliza.
“Inamaana anajua story yangu yote au ??”
Kabla Sijajibu kitu Kijana huyo akaendelea.
“Aaaah kuhusu story yako ni baba ndio alitusimulia, kwanza nimuombee msamaha mzee wangu maana Nina Uhakika akuomba ruhusa kuhusu story yako,
Lakini pia nikutoe Ofu kabisa, Lengo la baba yangu ni zuri sana na anatengeneza mazingira ya maisha Mapya kwaajili yako “
“Oooh usijali, sijachukia kabisa, aaah dokta Joel Nimemjua muda mfupi sana lakini amekuwa mwalimu wangu mkubwa sana,
Lakini pia ni amekuwa kama baba yangu vile nashukuru Mungu kwakweli “
Story za hapa na pale ziliendelea na hatimaye tukafika Nyumbani.
Rasmi nikaanza maisha yangu mapya kwenye Nyumba ya dokta Joel Walahi hii Nyumba ilikuwa kurudisha furaha yangu iliyopotea KWa muda mrefu sana.
Dokta Joel akaingia ghalama nyingine na kunilipia huduma ya psychology ili kuhakikisha kuwa akili yangu unakuwa Sawa kabisa .
Baada ya miezi Kazaa nikapata na kazi kabisa Tena kwenye ofisi nzuri sana na hii yote ni msaada wa dokta Joel, Yaani huyu baba ndio anasimamia ndoto zangu kWa sasa maana yeye ndio ana nielewa zaidi.
******
Hatimaye miezi kadhaa ikakatika na kuna Kahisia nikaanza kukapata juu ya dokta Joel, Yaani kuna Ka hali Fulani hivi nilijikuta nikimpenda dokta Joel ambaye yeye alinichukulia kama Binti yake.
Ikiwa ni Majila ya saa 4 usiku, niliamka na kwenda kukaa sebuleni kwani nilishindwa kabisa kupata usingizi, nilikaa sebuleni kWa muda wa Kama dakika 15 hivi, kisha dokta Joel akaja na kunikuta hapo.
“Oooh Zayana uko Sawa Mbona usiku huu uko hapa ??”
Dokta Joel aliniuliza akiwa na wasiwasi sana.
“Ata Sijui lakini nimeshindwa kulala “
Basi dokta wa watu akanisogelea na Kunikumbatia kWa nguvu sana, shida ikaanzia kwangu ambaye nilijikuta nikishindwa kabisa kujizuia na kuanza kumpapasa mbaba wa watu.
SEHEMU YA NANE
💙🤎💙🤎💙🤎💙🤎
Yaani nilikuwa bize kabisa kWa wakati huo niliendeshwa na hisia jamani na sio akili na ukizingatia Nina muda mrefu sana Sijakutana na mtu Yaani daaaah.
Cha ajabu Bwana ata dokta akushtuka zaidi akaanza kunipa Sapoti kiaina 🙌😂 hapa niligundua Kuwa wawili sisi tulikuwa tukiviziana Bwana, na ukizingatia sisi sote tupo single sasa kosa liko wapi jamani.
Aaah dokta kama dokta akaona ndio muda wa kunitibu Binti yake Bwana, akaninyanyua na pasi na kuulizana maswali akanipeleka chumbani kwake.
****
Nilikuja kuamka Majila ya saa 11 jioni na nilikuwa nimekumbatiwa kisawa Sawa na mzee huyo, Ila sio mzee Bwana ni my handsome wa kwenda huyu baba jamani.
“Unataka kwenda wapi ??”
Dokta Joel aliniuliza baada ya kuona Kuwa naangaika kutoka kwenye mikono yake.
“Nataka kwenda chumbani kwangu, sizani Kama ni Sawa kutoka kukiwa kumepambazuka, sitaki Binti yako mage anione kabisa”
“Ooooh Sawa “
Alijibu dokta Joel kisha akanikiss kwenye paji la uso.
Tangu hapo Bwana Mimi na dokta Joel tukaingia kwenye mahusiano Rasmi, Ila mahusiano yetu yalikuwa ya kujificha sana sana, kwa upande wa dokta Joel Bwana hakuwa na shida kabisa alikuwa tayali kuwaambia watoto zake kuhusiana na mahusiano yetu, lakini kWa upande wangu sikuweza kabisa, Yaani kuna ya hali Ka uwoga kalinitawala na kunifanya nisiwe huru kabisa.
Siku moja nikiwa kazini mimi na Rafiki zangu, ilikuwa ni muda wa kupata kifungua kinywa, hivyo tukaenda kunywa nje ya ofisi,nilishtuka sana kumuona Amiina Yaani mke wa pili wa mume wangu, Amina alikuwa amepauka hatari na ameleta Mboga za majani kwenye restaurant ambayo tulikuwa tunakula.
Niliganda nikimshangaa na kujiuliza ni kitu gani kimempata maana ni muda mfupi tu lakini ni amepauka kuliko kawaida Walahi.
“Zay unawaza nini ??”
Mmoja kati ya marafiki zangu akaniuliza…
“Aaaah namuangalia tu huyu msichana ni Kama namjua hivi lakini sikumbuki nimewai kumuona wapi “
Niliamua kudanganya tu maaana hapo kazini hakuna mtu alikuwa akijua historia yangu ya maisha, hakuna mtu ambaye alikuwa anajua Kama Mimi niliwai kuelewa.
“Aaah huyu labda umemuona hapa hapa, ni Binti Mdogo sana lakini anapitia Makubwa sana baada ya kuachika kwenye ndoa ambayo mume wake alikuwa akimzalilisha sana, hii restaurant ndio imempa Ofa ya kuleta mboga za majani kila siku kwaajili ya kumsapoti “
Kuna muda nilitamani ata kushangilia kutokana na matukio ambayo amenifanyia huyu Binti lakini kwa upande mwingine nilimuonea huruma sana, ni Binti Mdogo sana lakini ndio hivyo Alijiingiza kwenye tanuli la moto pasi na kuwaza joto lake.
Baada ya muda Amina akabeba beseni lake la mboga na kutoka nje, kWa upande wangu haraka nikanyanyuka na kumwambia shoga yangu.
“Nakuja sasa hivi “
Haraka nikatoka nje na kumsimamisha Amina.
KWa kipindi iki Walahi nilipendeza sana, nilikuwa navaa mavazi ya bei lakini pia muonekano wangu ndio ulikuwa so nice 👌 Yaani mtu lazima uniangalie Mara Mbili Mbili.
Amina alishtuka sana kuniona nikiwa na hali nzuri Kama ile maana daaah sote tumeachika lakini upande wangu nuru ilikuwa ni ya hali ya juu.
“Eeeeh da Zayana jamani “
Amina alinichangamkia utazani tuliwai Kuwa watu wa Karibu.
“Mambo “
Nilimsalimia uku nikimuangalia kwa makini sana Walahi huyu msichana ata Ngozi imechoka sana.
“Shikamoo da Zayana jamani kitambo “
Alizungumza uku akijichekesha.
“Marahaba Unaendeleaje? “
“Mmmmh Kama unavyoniona dada Angu, Yaani hali tete kwangu Yaani muonekano wangu tu unaelezea hali ya maisha yangu, da Zayana umependeza sana “
Basi Mimi na amina tukasogea kwenye Kivuli na kuzungumza.
“Aaaah ndoa ilinishinda dada Angu, unajua sikuwai Kubeba Mimba ya Abbas, kipindi kile nilimdanganya uku nikiamini muda na saa yoyote ile naweza nikapata mimba, Abbas aliniaminisha Kuwa wewe ndio unashida, lakini kila siku zilivyozidi kwenda ndio niliona Kuwa Abbas ndio Ana shida, kwanza ni anaishi kwenye maisha ya kizamani alinikataza kufanya kazi hivyo Nikabaki Nyumbani, sasa hivi Abbas Ana mke mwingine, nimeachika kWa kuzalilishwa sana na hatimaye now nauza mboga mboga kwaajili ya kuendesha yangu na Ugonjwa nimetoka nao kWa mwanaume Yule sasa hivi Mimi ni mtu wa dawa tu 😩”
Daaaaah Abbas jamani ameshamuumiza Binti wa watu, sasa hapa Sijui ni Nani kamaletea mwenzie shida maana wote ni awajatulia, Yaani wote ni waangaikaji walikuwa.
Nilimpa ushauri kadhaa mwisho nikampa kiasi cha Pesa na kumuaga.
“Mungu akubariki sana da Zayana, nakumbuka uliniambia Kuwa Mimi bado Mdogo sana lakini sikuwa nimekuelewa lakini kWa sasa naelewa “
“Kila la kheri usikate tamaa Mdogo wangu “
“Haya dada byeeeeh “
Daaaah Yaani Leo hii Amina ndio ananipa heshima kubwa Kama hivi, daaah kasichana Ka watu ni kadogo sana lakini ndio hivyo alivamia mambo.
Basi nikarudi zangu kazini na kuendelea na majukumu ya kazi.
Majila ya jioni, nilienda kwenye restaurant nyingine ambayo ni nzuri sana, siku hiyo Bwana nilikuwa Nina appointment na mama yangu mzazi, Yaani Sawa baba amenifukuza Nyumbani lakini Mimi na mama
Yangu Tunwasiliana vizuri kabisa na siku hii mama aliomba tuweze kukutana kwani aliniambia Kuwa amenikumbuka sana.
Kweli mama yangu alinikumbuka maana Nilimkuta akiwa ameshafika Yaani alifika mapema na kubaki akinisubili Binti yake, ukisikia damu nzuri kuliko maji ndio hii, mama yangu alinikumbatia kWa furaha kubwa sana uku Akitamani ata kulia.
“Eeeeh Binti yangu, 30 years imekupendeza sana jamani yaaani uwiiiiih you look so mwaaaaah, eeeh husda za Wana wa adamu zikae mbali na wewe Binti yangu “
Alizungumza mama yangu baada ya kuona Kuwa Binti yake nimenawili sana.
“Nimekumisi sana mama Angu, na sio wewe kiufupi nimemisi familia nzima, nimemmisi baba lakini pia na wadogo zangu “
“Yaani Acha Binti yangu, ata baba yako anakukumbuka sana lakini Naomba kWa sasa Kaa mbali na baba yako, naona anawasiliana sana na mumeo Abbas ni Kama anataka kukurudisha kWa Abbas”
Kwanza nilishtuka kisha nikajibu.
“Kwanza Abbas sio mume Angu na awezi Kuwa Ameshapita na hana nafasi kwenye maisha yangu, mama Mimi ni mtu Mpya sana, tazama Nina maisha ya amani kabisa “
Muda huo huo simu yangu iliita na dokta Joel ndio alikuwa kipiga, muda huo nilimbadilisha Jina na Kumsave hivi “HUBBY WA DUNIA 💙💜”
Aaaah huyu baba amejua kunikamata, haraka nikapokea kisha nikazungumza nae kWa muda na kukata simu.
“Eeeh ndio mkwe yangu nini naona mambo ya hubby hapo “
Aliuliza mama yangu ila huyu mwanamke ana mambo jamani 😂🙌 khaaaaah.
Ila my zangu hivi ni Sawa Kuwa na mahusiano na mtu ambaye umri wake ni Sawa na baba yako ? Yaani umri wa mr Joel na baba yangu ni wemepishana miaka mitatu tu ambapo baba yangu ni mkubwa, lakini kuonekano wa dokta Abbas ni Kama Kijana wa mika 35 na kidogo hivi, na hii yote ni kutokana na mazoezi.
Baada ya kumaliza mazungumzo na mama yangu nikampatia kiasi cha Pesa kisha tukaagana, baada ya mama kuondoka tu dokta Abbas akafika kwaajili ya kunichukua na kuweza kurudi wote Nyumbani.
******
Siku iliyofuata ikiwa ni Majila ya mchana na Nipo kazini , sikuwa Nilihisi Kia powa kabisa hivyo sikuweza kutoka nje kwaajili ya chakula cha mchana nilichokifanya ni kumtuma shoga yangu aniletee sausage maana ndio kitu Ninachopenda sana.
Siku hiyo Bwana ilikuwa tofauti sanna, baada ya kuniletea sausage Nilihisi Kuwa Zina harufu mbaya, kichefu chefu cha hali ya juu gafla nikatapika juu ya meza ya yangu na baada ya kumaliza kutapika nikajikuta nikianguka chini na kupoteza fahamu.
Nilikuja kuamka nikiwa kwenye chumba cha hospital na dokta Joel alikuwa Alizunguka tu kwenye chumba iko.
“Babe “
Nilimuita kwa sauti ya kichovu.
“Ooooh jamani umeamka mama kija wangu”
Eeeeeh 😱😳 majilani Mbona Kama ameniita mama kija au sijasikia vizuri ??
SEHEMU YA TISA
KWa haraka nikanyanyuka pale nilipokuwa nimelala, nilinyanyuka utazani sio Mimi ninayeumwa, Yaani niliamka Kama jetiliii 😂 Sijui niwaambiaje ili mnielewe kisha kwa mshangao zaidi nikamuuliza dokta Abbas.
“Umeniitaje !!”
“Mama kijacho wangu”
“Unamaanisha Mimi ni mjamzito au ??”
Nilimuuliza ili kuelewa zaidi na kuelewa maana hali ya Jina lake.
“Aaaah umeweza Zayana wangu, Yaani umeweza bila vita mama, Walahi mke wangu una kizazi cha house girl “
Nyieeerh huyu baba ameniita mke mjue 😂🙌 uwiiiiiiiih majilani Sijui niwaite kWa style gani ili mnielewe, Yaani niwaite kWa sauti yani ili muweze kusikia, eti niambieni, au nitumie balagumu ndio mtaweza kunisikia.
KWa furaha nikamkumbatia my wangu na kuanza kumkiss kila kona, Yaani huyu baba ameweza halafu anaweza Tena, Yaani yeye ndio ameniaminisha Kuwa kweli sikuwa na shida na hii ni wazi Kuwa Abbas ndio alikuwa na shida.
“Eeeh Mungu weeeh umejua kunitendea Mungu wangu nikushukuru Vipi Mimi “
Nilizungumza uku nikiwa nimepiga goti na mr joel alikuwa amenikumbatia tu kWa nguvu sana.
Kwakuwa sikuwa Naumwa ugonjwa wowote ule, niliruhusiwa na kurudi Nyumbani, hapo niliwakuta mpaka watoto wa kiume wa dokta Joel.
“Nini shida baba, umenishtua sana kuniambia Kuwa Zayana ameanguka kazini “
Alizungumza Mtoto mkubwa wa kiume wa dokta Joel.
“Aaaaah ni mambo ya kawaida tu, muda ule nawatumia ujumbe Walahi nilikuwa nimepaniki sana maana alifikishwa hospital akiwa ajitambui kabisa lakini kWa sasa yuko Sawa”
Alijibu dokta Joel na kujitupia kwenye kochi.
“Hivi unajua we mzee unazeeka vibaya sana, Yaani unajitupia kwenye kochi mama Mzigo na kumuacha mgonjwa kasimama”
Kama kawaida wakaanza kumtania baba Yao, Yaani hawa watoto na baba Yao ni Kama mtu na Rafiki zake tu ni watu ambao wamejengeana ukaribu mzuri snaa sio Kama Mimi na baba yangu 🥹.
Basi Mage na dada wa kazi wakaandaa chakula na kuweka mezani kWa upande wangu kila kitu Kilikuwa kibaya, kitu ambacho nilikuwa naitaji ni chai tu ya moto ambayo aina sukari sana.
“Baba Nafikili kesho tumrudishe Zayana hospital tu bado hayuko Sawa huu utapikaji sio wa kawaida “
Walizungumza vijana hao uku wakinionea huruma sana pasi na kujua Kuwa Mdogo wao ndio analeta shida kwenye tumbo langu.
“Msijali atakuwa Sawa, kuna dawa amepatiwa zitamsaidia sana “
“Aaaah baba hapana Bwana, Yaani ninavyomuangalia tu naona Kuwa hayuko Sawa mmempima vizuri kweli huyu jamani “
“Aaaah jamani Tulieni Basi, Mimi nilikuwa pale na nimesimamia vipimo vyake vyote, Zayana aumwi chochote kile, zaidi ni huyo mwana familia Mpya ambaye anataka kutuletea ndio analeta shida kwenye tumbo lake”
Weeeh hapo nilishtuka sana na kuanza kutetemeka ni Kama anataka kusema ukweli huyu mbaba jamani uwiiiih si aibu hii jamani 🥹 maana watoto zake na Mimi tumepishana kidogo sana ingawa bado Mimi ni mkubwa.
KWa pamoja watoto wake wakanigeukia na kuniuliza.
“Zay wewe ni mjamzito ??”
Nyie nilikuwa naona Kama wananiatakii hivi, kabla sijajibu swali Lao mage akaendelea.
“Natamani ata nichukue Tarumbeta niende Nyumbani kWa Abbas nimfikishie taarifa ili awai hospital chap akafanye vipimo 😂🙌”
Ila huyu mage nae akili zake sio nzuri Yaani akili zake muda mwingi ziko juu juu, sasa Abbas amefuata nini hapa, Ila ni Kama Anakitu Ndani yake 😂.
“Ebu acha uswahili wako hapa, “
Dokta Joel akamtuliza Binti yake ambaye alikuwa na miemko ya Kiswahilini.
“Sa si nasema ukweli, aaah kwanza nimekumbuka, da Zayana huyo mwanaume mwenyew Bahati ya kukupata wewe ni Nani ??”
Uwiiiiiiih huyu Binti Mbona kama anataka kunichimba sasa, muda huo hali ya kutetemeka iliziidi kuongezeka na muda huo huo dokta Joel akazungumza.
“Aaah huyo lucky man ni Mimi baba yenu”
Kila mtu alishtuka Saana na kWa pamoja wakanigeukia mimi, Yaani mpaka wajukuu wakanigeukia Mimi Saa ngapi nisizimie maana sio kwa kunipa presha hawa watu. 😁🙌
Watoto wa huyu baba Sijui watalipokeaje ili jamani daaah Mbona Kama napata wasiwasi mkubwa sana.
KWa haraka Wakanikimbiza hospital na nilivyofika tu nikaanza kupewa huduma ya kwanza na kuwekwa kwennye chumba cha mapumziko.
Sawa nilipoteza Fahamu lakini nilizinduka kitambo tu lakini niliogopa ata kufungua macho yangu maana nilikuwa na wasiwasi sana.
“Aaaah mmekuwa wengi sana kwa sasa jamani, aaaah Naomba kila mtu atoke nje na abaki mtu mmoja ambaye atakuwa akimuhudumia mgonjwa wetu”
Alizungumza daktari mwingine kisha akatoka nje, muda huo mr Joel na watoto wake alibaki wakiangaliana mwisho dokta Joel akawauliza.
“Kwani dokta amkamsikia au ? Tokeni nje ikiwezekana nendeni Nyumbani mke wangu kitabaki nae Mwenyewe”
Weeeeeh huyu baba jamani ndio anajiachia kabisa ananiita mke wake, niambieni kuzimia mwisho masaa mangapi isije ikawa najiova dozi hapa. 😅
“Akhaaaaah me nabaki na Zayana ata hivyo Mimi ndio mwanamke mwenzie “
Alijibu mage na kusogelea kochi na kukaa si unajua Tena hospital za private.
“Me pia nabaki na Zayana kwanza ni mama yangu, anaitaji ulinzi “
Jamani me nataka ulinzi wa nini lakini, hawa watoto wa huyu baba Mbona wanataka kuniingiza majaribuni 😂🙌.
“Mimi pia nabaki”
Yaani watoto wote Wakagoma kuondoka, dokta Joel Akanyanyuka na kwa sauti ya kuchukia akazungumza.
“Haya bakini nyie sasa ili mfurahi na mioyo yenu, mwanamke wangu lakini nakuwa Kama nimemuazima “
Ila hawa Sijui watakuwa lini na baba Yao. 😂
“Safari njema baba, hakikisha usalama wa wajukuu zako uko Nyumbani sisi Tunahakikisha usalama wa mama hapa maana huyu Abbas anaweza akamvamia ata ndotoni”
Alizungumza Mage na hapo Aliniweza kabisa nikajikuta nikicheka sana, Yaani imagine mtu unajulikana umezimia halafu gafla tu unaanza kucheka.
SEHEMU YA KUMI
💙🤎💙🤎💙🤎💙🤎
Kila mtu alishtuka sana, haraka dokta Joel akatoka nje na kurudi akiwa ameongozana na daktari na kwa sauti ya wasiwasi akamwambia dokta.
“Dokta imekuwa gafla sana, Yaani ajaamka kWa kufungua macho yake Wala kujinyoosha Yaani ni gafla tu Ameanza kucheka Kama. Unavyomuona”
KWa muda huo Walahi kicheko kilinibana sana nilishindwa ata kuacha kucheka Yaani Vituko vya hawa watu ndio vilikuja mfululizo na kunifanya nizidi kucheka.
“Nafikili amepata shida ya afya ya akili “
Alizungumza dokta, hapo haraka mage akanyanyuka na kulopoka.
“Washamloga jamani “
Yaani hapo ndio nilizidi kucheka, mwisho nikajiambia Kuwa nisipokuwa makini natajikuta napelekwa milembe hivi hivi 😂🙌.
Nikijikaza na kuzungumza.
“Jamani me mzima tu Ila hawa watu wamenichekesha sana, ata hivyo nilizindukankitambo tu “
Hapo kila mtu akashusha Pumzika Ndefu sana maana Niliwashtua sana.
“Niko Sawa jamani, niliamka muda mrefu sana lakini nilikuwa Nina wasiwasi sana juu yenu, niliwaza mtazipokeaje hizi taarifa za Mimi kumzalia baba yenu, lakini Nimeona upendo wa dhati sana kutoka kwenu, nawapenda sana jamani nawapenda “
Nilijikuta nikianza kulia jamani, Yaani sikuwai kufikilia Kuwa kuna siku nitakuja kupendwa na mwanaume na watoto zake wote.
“Aaaah tunakupenda sana Zayana, oooh sorry mama”
Alijibu Yule ambaye nilienda nae kufuata begi kule kwenye Nyumba ya wageni.
“Aaah Ila hapo kwenye kukuita mama ni kazi sana 🥹 Utakuwa Tayali sisi kuendelea kukuita Zayana ??”
Dokta Joel akawageukia vijana wake na kuwauliza.
“Na Kwanini mumuite Zayana ? “
Haraka Nikadakia.
“Kuniita Zayana sio shida, kikubwa Kuwa amani na upendo na heshima vipo kati yetu, nakumbuka mama yangu wakati niko Mdogo alikuwa ananiambia niite Faidha na sio mama, nilivyokuwa Nilimuuliza Kwanini anataka Mimi nimuite jina lake na sio mama, akanijibu Kuwa imekuwa kazi sana kWa watoto kujua majina ya wazazi wao, Mara nyingi watoto wanapotea lakini ukiwauliza mama anaitwa Nani Anakujibu mama yangu “
Dokta Joel Akajibu.
“Hii ni mijitu mizima, hapo walipo ni wana meno yote kinywani mwao, Zayana ni mama yenu na mtamuheshimu Kama
Mama “
“Sawa baba”
Yaani kama ni watoto tu huyu baba jamani amejua Kuwapata na alijua Kuwalea kwenye maadili mazuri na hizi pongezi za malezi mazuri zimfikie mama Yao mzazi ambaye ameshafariki kWa miaka kadhaa sasa.
Life style ya maisha yangu ilibadilika kabisa, Yaani Mungu alijua kunitoa kwenye kilio na kunieleta kwenye mideko, nyieeeeh familia ninayo na Ninatamba nayo.
Muda mwingi nilijiangalia kwenye Kioo,
Kila siku nilikuwa nikifatilia ukuaji wa tumbo langu, yaani kuna muda nilikuwa naona Kama linachelewa kukua hivi 😂🙌 Ila iki ni kiherehere sasa maana daaah.
Yaani kila stage ya ukuaji wa tumbo langu nilikuwa nikijisnap kuna muda nilikuwa Nashindwa ata kuamini Kuwa na Mimi naenda kuitwa mama, nyie Mimi hii hali nimeisubili sana kwenye maisha ya Abbas lakini ndio hivyo haikuwa Riziki.
Dokta Joel wa watu akawa Kama mtumwa kwangu, nikiwa kazini alihakikisha Kuwa ananiletwa chakula cha asubuhi na mchana, Sijui ata kazini alikuwa anatoka kWa style gani lakini alihakikisha Kuwa ananiletea chakula kWa wakati.
KWa upande wangu Walahi mambo ya Msosi yalinipitia Kushoto kabisa, Yaani Mimi ni chai tu na maji ya baridi na matunda Tunda na sana sana ni Matango na matikiti maji.
Dokta Joel alihakikisha Kuwa kila clinic tunakuwa wote.
KWa upande wa watoto zake wa kiume ambao tulikuwa atukai nao pale Nyumbani, walihakikisha Kuwa wananipigia video call kila siku na walihakikisha Kuwa wananiita mama na walinipa heshima ya mama na niliwapenda Kama watoto wangu lakini pia marafiki zangu.
KWa upande wa huyu mage ndio kabisa, Yaani huyu Binti ni zero plus sifuriii 😂🙌 Yaani ninawasiwasi na akili zake, kuna muda nilikuwa najiuliza huyu ni comedian tu au ni Mtoto wa mume wangu , Yaani muda wote alihakikisha naacheka.
********
Aaaah siku zilikimbia Bwana na hatimaye siku ya kucheza segele ikafika Bwana , uwiiiiih nilijua Kusakata rumba uku mume wangu Yaani dokta Joel akiwa pembeni yangu akishuhudia kila kitu.
Hatimaye Bwana nikawa blessed na Mtoto wa kiume nyieeeeh kuna muda nilishindwa kuamini kabisa Kama na Mimi Leo hii naanza kuitwa mama Fulani kutokana na uzazi wangu Mwenyewe, Yaani nilikuwa nikimuangalia Mtoto wangu muda wote na nisiamini Kuwa ni Mimi nimembeba miezi Tisa na nimempushi kWa nguvu zangu.
Aaah mwanangu Bwana akapatiwa Jina la Daniel, hapo na Mimi Bwana nikaanza kwenda kanisani kwani ndio nimeshapata familia ya ki Kristo ata hivyo Mungu ni mmoja na imani ndio Nguo kuu.
Baada ya Kijana wangu kufikisha miezi minne mimi na Dokta Joel, tukapanga safari ya kumpeleka Daniel kwenye familia yangu ili aweze kukutana na familia yake nyingine, ikumbukwe Kuwa ata mama yangu hakuwai kujua Kuwa Binti yake ni mjamzito.
Basi tulifika Nyumbani na baba akifurahi sana kuniona na kWa furaha akanikumbatia, kWa wakati huo Daniel alikuwa kwenye mikono salama kabisa ya baba yake mzazi dokta Joel.
“Karibuni sana jamani “
“Asante”
“Ebu subili kwanza, Picha ninayoiona Niipokee hivyo hivyo au nisubili maelezo maana naona Kama mnachelewa hivi “
Alizungumza mama yangu na swali lake ni juu ya huyu Mtoto.
“Yaaah mama Binti yako sio mgumba Kama ambavyo walikuwa wakiniita, Binti yako nimeweza kusikia kilio cha kwanza kabisa cha mtoto wangu, Binti yako nimeweza kubeba Mtoto huyu tumboni mwangu miezi Tisa”
Walahi nilijikuta nikilia sana, hapo nilikumbuka ata jinsi ambavyo baba yangu alikuwa akimsapoti abbas na kuniacha Mimi Binti yake.
“Zayana unaitwa mama ??”
Baba aliniuliza kwa sauti ya kutokuamini kabisa.
“Ndio baba “
Weeeeh nyieeeh baba yangu Alipata furaha ya hatari mpaka akajikuta akipiga beki mbele ya mkwe yake 😂🙌 Ila kumbe baba yangu nae akili zake ni fupi.
INAENDELEA…..