π πͺππππ π¨ π πππππππ‘π
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi.
EP 04
ILIPOISHIA…..
Magdalena alikimbia huku akipiga kelele bila kujua anakokimbilia angepata msaada ama la! Alishaanza kuchoka na ilikuwa giza sana, lakini alichoambulia kugundua ni kwamba mtu aliyekuwa akimkimbiza alikuwa amevaa kinyago na nguo nyeusi ili asitambulike…………
SONGA NAYOΒ
GHAFLA mwalimu Magdalena akajikuta akikamatwa na kufumbwa mdomo, alikukuruka ili ajitoe katika mikono iliyombana vema, lakini hakuweza kuitoa, alijitahidi kujitoa mbele ya mtu huyo aliyemfumba mdomo, sauti pia miguu yake havikumsaidia kufanya chochote kujikwamua kutoka eneo hilo Mwenyekiti alishangaa kutosikia sauti ya mwalimu Magdalena, akaangaza huku na kule, lakini hakuweza kutambua wapi alipo mwalimu Magdalena, alinyanyua macho huku na huko, lakini hakufanikiwa.
Taratibu Mwalimu Magdalena alikuwa akipoteza nguvu kutokana na kubanwa na asiyemjua, mtu yule alimvuta eneo lingine ili kumkwepa mwenyekiti aliyekuwa akimsaka mwalimu Magdalena ili atimize ahadi yake.
Mwenyekiti alianza kuhamaki alipojificha mwalimu Magdalena, akavua kinyago alichokivaa kuficha uso wake, akaingia katika majani anayohisi mwalimu Magdalena amefichwa.
Mwenyekiti alikanyaga majani yale akiamini mwalimu Magdalena amejificha na yupo peke yake, akazidi kusogea ghafla, naye akashtukia amekabwa na kitu asichokijua.
Mwenyekiti alipiga kelele huku akijitahidi kutoa mkono uliomkaba, lakini hakuweza, akatumia akili za kuruka sarakasi na kujidondosha huku na huko, akapata nafasi ya kujinasua katika mkono huo, hakuwa na ulazima wa kupambana na mtu asiyemjua, akaamua kutimua mbio.
Mwalimu Magdalena taratibu akanyanyuka na kutaka kukimbia, lakini yule mtu aliyemkamata na kumziba mdomo akamkamata kisha akajitambulisha kwake.
βSitaki, sitaki, sitaki mwenyekiti,ββ
βMwenyekiti, mwenyekiti ndiyo nani mi siyo mwenyekiti, nimekusaidia ulikuwa katika hatari nimekuokoa,ββ walishindwa kuelewana kutokana na giza lililotanda siku hiyo, mwalimu Magdalena alianza kupunguza woga lakini hakutambua sura ya mtu huyo aliyemweleza kuwamba amemuokoa.
Alijitahidi kumtazama lakini hakuweza, mtu huyo alitambua kwamba mwalimu Magdalena anataka kumtambua ni nani, akaingiza mkono wake mfukoni kwake akatoka na simu akawasha tochi kisha akajimulika usoni na kumtaka mwalimu Magdalena amwangalie.
βWewe ni nani? Umesema ni mwalimu, mwalimu gani na huku umefuata nini?ββ alihoji. βMimi ni mwalimu Jokam, wengi wanapenda kuniita Joka.ββ
βJokaββ alihoji kwa hofu mwalimu Magadalena.
βNdiyo ni Joka kwa kuwa ni mtaalamu wa hisabati, huwa sishindwi chochote katika hisabati na nililetwa kijiji hiki muda mrefu lakini sikupenda lakini kuna jamaa yangu aliniambia aliwahi kufika huku na kuna fursa nyingi huku ndiyo nimekuja kuangalia kama ni kweli nije kufanya kazi huku.ββ Alifafanua mwalimu Joka.
βTatizo ni nini hadi huyu mwenyekiti akukimbize hivyo.ββ βWe acha tu ni story ndefu.ββ
βNisimulie nitakusaidia.ββ
βNajua utanisaidia, ila turudi kwanza nyumbani kisha kesho asubuhi nitakuhadithia kama unataka.ββ
βSawa ila mimi ni mwenyeji wa mwenyekiti.ββ
βSasa mwenyekiti mwenyewe ndiyo huyo umemtimua.ββ βKazi ipo kweli kweli sasa nifanyeje?ββ
βTwende kwangu mambo mengine yote utajua asubuhi, maana ni usiku na umenisaidia sana kuniokoa, ila mimi sihitaji hata fursa zilizopo, kesho mapema nitaanza safari ya kurudi mkoani kwetu bora nikawe mama wa nyumbani huko kuliko kuteseka hapa na mwenyekiti,ββ alilalama mwalimu Magdalena.
βAhaaa! Huyu mwenyekiti ndiyo akusumbue wewe nitadeal naye we niachie mimi tena nitamweka wazi kwa watu wote, kwani hana mke.ββ
βHata sijui,ββ alijibu mwalimu Magdalena.
Mazungumzo yao yaliendelea, wakafika nyumbani kwa mwalimu Magdalena, wakapitiwa na usingizi, kutokana na uchovu waliokuwa nao mwalimu Magdalena na mwalimu Joka wakajikuta wakiamka saa 4 asubuhi, tena baada ya John kuwagongea kutokana na kutomuona mwalimu Magdalena shuleni.
βSasa itakuwaje, nje kuna hodi inagongwa na sauti ya huyo mtu namjua ni wa shuleni, kama akikuona itakuwa balaa upya, watahisi kuna kitu kimefanyika kati yangu na wewe, sasa naomba ujifiche humu humu ndani mi natoka kumsikiliza.ββ
βSawa.β
EP 05
Mwalimu Magdalena alipotoka nje akakutana na John,
mwanafunzi anayempenda, John hakutaka kuhoji chochote hadi aingie ndani lakini mwalimu Magdalena alionyesha hofu kama ya kusita, lakini akakubaliana na yote, John akaingia akakaa kitandani huku mwalimu Joka akiwa amejificha chini ya uvungu wa kitanda cha mwalimu Magdalena.
βMwalimu mbona hadi sasa hujafika shuleni kila mtu anahofu nawe, hakuna anayeelewa somo lolote hadi wakuone, mwalimu unanujua wanafunzi wa shule ile tulivyokuzoea na pia kuna taarifa kwamba mwenyekiti alikubaka jana ni kweli mwalimu Magdalena,ββ alihoji John huku uso wake ukionyesha kukasirishwa na kitendo hicho βHapana John hakunibaka, ni kweli lengo lake lilikuwa hilo maana alinikimbiza kichakani usiku mzito lakini alishindwa kufanikiwa.ββ
βAlishindwaje wakati mlikuwa wawili? Mi nilijua mwalimu Magdalena huwezi kusubiri unaona sasa, mwenyekiti namchukia maisha yote,ββ alilalama mwanafunzi John huku
mwalimu Madgalena akibubujikwa namachozi akishangaa nani katangaza habari hizo akatambua kwamba atakuwa ni mwenyekiti.
βJohn hapana hakufanikiwa kufanya hicho kitendo ingawa alinikimbiza lakini niliokolewa na mtu mwingine huko msituni alimpiga mwenyekiti akakimbia mimi bado nipo vizuri na nakusubiri John wangu usiwe na hofu,ββ alijibu mwalimu Mgadalena huku wote wawili John na mwalimu Mgdalena wakitokwa na machozi.
Walifutana machozi pale wakajikuta nao wakipitiwa na usingizi. Muda ulipita walipokuja kusituka ilikuwa jioni.
John alistuka kuona muda umekwenda hivyo kwa haraka akaelekea kwao akimwacha mwalimu Magdalena ajiandae kujibu maswali kuhusu John.
Lakini alipoita hakuna aliyeitika na alipochungulia uvunguni hakumuona mwalimu Joka, akashangaa kwa nini hakumuona, alijiuliza maswali mengi asijue alipoelekea mwalimu huyo lakini akili ilimtuma kuamini kwamba mwalimu huyo alitoka wakiwa wamepitiwa na usingizi na John.
Jioni ya saa 12
Mwalimu Joka alifika kwa mwenyekiti na kujitambulisha kwamba yeye ni mwalimu aliyetakiwa kufika katika kijiji hicho kusaidia kuokoa somo la hisabati lililokuwa likielekea kupotea kwa kuwa hakuna mwanafunzi aliyekuwa akilipenda somo hilo kutokana na kutokuwa na mwalimu wa somo hilo kwa miaka mingi zaidi ya wanafunzi wa kujitolea ambao walifika kijijini hapo kwa mafunzo.
Mwenyekiti alionyesha kutofurahishwa na mwalimu huyo aliyekuwa na umbo la wastani lenye nuru angavu, sura yenye mvuto.
Hofu ya mwenyetiki ni kwamba ujio wa mwalimu huyo ni pigo kwake kumfuatilia mwalimu Magdalena kwa kuwa tayari atapata mlinzi na kwa vyovyote watapendana kwa kuwa wote wametoka mjini, hivyo watakuwa wanapenda maisha yao yaendelee….
EP 06
Katika hali isiyotarajiwa, wakati mwalimu Magdalena akimaliza kipindi chake cha historia kipindi kilichofuata ni hisabati, kilichofuata hapo ni hali ya mshangao uliotoka kwa mwalimu Magdalena.
Kitendo cha mwalimu Magdalena kumuangalia kwa muda mrefu mwalimu Joka kilitafsiriwa tofauti na John, lakini hakikuleta fikra tofauti kwa kuwa imani ya wanafunzi ni kwamba walimu hao ndiyo kwanza walikutana………
Haikuwezekana kunyamaza kimya licha ya mwalimu Joka kuonyesha kuchukizwa na jambo, lakini hakuweza kutoitikia salamu ya mwalimu Magdalena.
βMwalimu Joka ndiyo umefika? Maana sikukuoana ofisini asubuhi,β aliuliza Mwalimu Magdalena.
βHapana nilikuwepo,β alijibu kwa mkato mwalimu Joka, sauti iliyotumika kujibu hilo swali ilimuonyesha dhahiri kwamba amekasirika hivyo mwalimu Magdalena alihama kuondoka darasani na kumuachia aendelee na kipindi chake.
βSawa naomba ukimaliza kipindi tuzungumze jambo kidogoβ
βSawaβ alijibu huku akielekea mbele ya dawati lililowekwa mbele kama meza ya mwalimu wa kipindi na kisha akajitambulisha kwa wanafunzi hao kwamba, yeye ni mwalimu wa kipindi cha hisabati huku akiwaasa wafuate anachowaelekeza ili waweze kulipenda somo hilo.
Mtihani ulibaki kwa mwalimu Magdalena alikwenda moja kwa moja hadi ofisi ya walimu, alisogea kwenye kiti chake akatulia kimya bila kuanzisha mada wala kuchangia chochote kilichokuwa kikijadiliwa na walimu wenzake katika ofisi hiyo.
Mazungumzo ya chini kwa chini yaliendelea katika chumba hicho cha walimu, wapo waliodhani kwamba mwalimu Magdalena ametulia kimya kutokana na kashfa iliyozagaa ya kubakwa na mwenyekiti wa kijiji hicho lakini pia wapo waliodai mambo mengine lakini kilichokuwa kikimuumiza kilikuwa moyoni mwake.
βNajua kanikasirikia kwa sababu ya John, hakuna lingine ni hilo tu maana wanaume kunisaidia siku zile keshachukulia βadvantage any wayβ lakini nisimzungumzie inawezekana
amekasirishwa na yake ngoja atoke nizungumze naye nitajua,ββ alijisemea mwalimu Magdalena huku akiwa anapitia daftari la mahudhurio ya wanafunzi lililokuwa mezani kwake.
βNdiyo mwalimu Magdalena, nimeitikia wito,β alikuwa mwalimu Joka baada ya kutoka darasani alifika kwa mwalimu Magdalena kama alivyomtaka afanye hivyo baada ya kipindi chake.
βNashukuru umekuja lakini hatuwezi kuzungumza hapa ofisini twende nje.β
βNje tena, mi sitaki mambo ya kitoto maana nasikia una mpenzi mtoto wa hapa shuleni.ββ
βHayo ya nini Joka, hayo maisha yangu nataka tuzungumze mambo mengine hayo niachie mwenyewe nitamaliza.β
βNa ya Mwenyekiti, utayamaliza vipi na kubakwa kwako.β
βJoka usinifedheheshe, unajua ukweli wote wa mwenyekiti lakini kama umeamua kuniharibia sikukatazi unaweza kufanya hivyo maana wewe ndiye unayejua ukweli wa tukio zima la usiku ule,β alijieleza mwalimu Magdalena akimtazama mwalimu Joka akiwa amesimama mbele ya meza yake ndani ya ofisi ya walimu.
Walizungumza mengi wakafikia mwafaka wa kwenda kuzungumza nje ya ofisi hiyo, lakini wakiwa katika harakati za kutoka ofisini hapo, wanasikia kelele kutoka nje ya ofisi huku wanafunzi wa madarasa mbalimbali wakitoka darasani.
Walimu nao wakashangazwa na tukio hilo wakachungulia nje kuona kwanini wanafunzi walikuwa wakitoka nje ya madarasa yao na kukimbilia nje.
Akiwemo mwalimu Magdalena na Joka walichokiona hawakuamini kwani alikuwa baba wa John aliyekuwa akimchapa John bakora huku akimtaka akamuonyeshe mwalimu Magdalena.
Mwalimu Magdalena alifedheheka hakuweza kutoka nje ya ofisi, alijisikia vibaya kumsikia mzee huyo aliyeonyesha kukasirika akiwa na bakora mkononi akimtaja jina lake huku akirusha baadhi ya maneno ya kufedhehesha.
Wanafunzi walizidi kushangilia kila mzee huyo alipomcharaza bakora mwanaye huku akimtaka kuzingatia masomo badala ya mwalimu Magdalena.
Haikuwa siri tena kila aliyekuwepo katika eneo hilo alisikia kila kitu kilichokuwa kikizungumzwa na baba huyo wa John, maneno makali na yasiyosimulika yalimuumiza Joka akamtazama mwalimu Mgdalena aliyekuwa ameanza kutokwa na machozi akiwa amejiinamia katika meza yake ofisi ya walimu akaingiwa na huruma.
Akatoka moja kwa moja hadi kwa mzee huyo akamtaka wakazungumze katika ofisi ya mwalimu mkuu, mzee huyo akaleta mzozo
Je baba yake john atazua mzozo gani, je atakubali kwenda ofisini?,Aibu kwa mwalimu Magdalena ataficha wapi uso wake jambo hili likifika kwa mwalimu mkuu?
INAENDELEA

