MTOTO WA AJABU
PART: 06
ILIPOISHIA,
Braison akiwa anarejea nyumbani mida ya usiku wa manane huku akiwa amebebwa kwenye bodaboda, alivamiwa na vijana wanne wenye mapanga pamoja na rungu, huko upande wa bonge, mtoto anawashangaza mara baada ya kuanza kutembea na kuuliza wapi anapelekwa ili hali ana masaa machache tangu azaliwe…
SONGA NAYO…
Baada ya kuwekwa chini ya ulinzi mkali, Braison pamoja na dereva boda, walianza kupokea makofi huku wakiambiwa,
“‘Toa chochote mlichonancho!'” Waliwaamrisha.
Walitoa kila kitu ndipo walipokuta kiasi cha sh elfu tano kwenye Wallet ya Braison na Tsh 15 elfu kwenye Wallet ya dereva boda.
“‘Hee! mnafanya mchezo hee!, ngoja tuwaoneshe kazi kuwa hatutanii” waliinua mapanga juu
“Samahani msiniue..msiniue!, ndo kiasi nilichonacho hapa nilipo nimefiwa na mtoto wangu ninadaiwa hela ya kusafirisha maiti na mke wangu bado amelazwa hospitali.” Braison aliongea huku akiwa anatetemeka.
“Una uhakika huna hela nyingine iliyobaki!, walah tukikuta hata shilingi mia!, mtakuwa halali yetu..”
Braison na mwenzake walibaki wameangaliana.
“Vueni nguo nyote!, vua nguo ..haraka!..” waliamrisha huku wakiwapa mateke..
Kwa hofu kubwa huku wakiwa wanatetemeka, walivua nguo na kubakiza za ndani huku wakiwa hawajui lengo lao ni lipi.
“‘Huko ndo kuvua nguo!, toa zote afu piga msamba!..mnaaibu ya nini!, sie wanaume wapuuzi nyie .”
Kwa unyonge walivua na kubaki watupu kabisa kama walivyozaliwa ndipo walipokaguliwa kila sehemu lakini hawakuona hata senti.
“Ayaa vaa afu potea wapumbavu nyie!, mnatembea hamna chochote mifuko!” Walitamka kwa masikitiko.
Walinyanyuka na kuvaa . Wakati wanamalizia kuvaa, majambazi hao waliwasha pikipiki na kuondoka nayo nakuwaacha Braison na mwenzie wakiwa hawaelewi.
Kwa uoga mkubwa, walitimua mbio huku wakihema mpaka mnamo mida ya saa 9 usiku ndipo walipofika nyumbani kwao.
Braison alipofika kwenye mlango wa nyumba yake, alikosa hata nguvu za kuingia ndani ndipo alipomwaga machozi .
“‘Niliambiwaga kua uyaone !, nimeyaona lakini kwanini ni mapema sana hivi…!” alitikisa kichwa.
Taratibu alifungua mlango na kuingia ndani kisha akaanza kuumiza kichwa wapi atapata pesa ya kusafirisha maiti.
Alianza kuwajulisha ndugu jamaa na marafiki juu ya kilichompata lakini waliishia kumpa pole tu wala si kumshika mkono.
Aliweka simu chini kisha akajilaza ndipo alipata wazo.
Mnamo mida ya saa 11 za alfajiri, aliamka kisha akafungua banda la mbuzi na kuwachukua mbuzi wanne sokoni ndipo alipofanikiwa kupata laki na 80.
Alirejea nyumbani kwani soko halikuwa mbali kisha akaanza kufanya usafi kabla hajaanza kutoa taarifa kwa majirani.
Wakati mambo yakiwa hivo, huko nyumbani kwa bonge, hali ya sintofahamu ilizidi kuwashangaza na kuwaacha na maswali mengi.
Mtoto yule alianza kuongea huku akiuliza wapi alipo hapo ndipo bonge alipomuita mlinzi wake na kumwambia,
” Huyu mtoto ni waajabu kweli! Sasa sijui tunafanyeje?” Bonge akiwa anakitete aliongea.
“Sasa tufanyeje?, kikubwa ni kuwa naye karibu sana huenda ni mkombozi wako..”
” Mhh anaweza kuwa hatari sana….”
” sasa nipe maelekezo nakusikiliza boss wangu…”
” Naomba iwe siri yako….”
” Ipi hiyo siri…?”
” Usimwambie mtu yeyote…”
Wakati wanaongea hivo, mtoto huyo alikuja maoneo hayo akiwa anatambaa na kutembea huku akitabasamu kisha akasema,
” Mnapanga nini?” Aliwauliza.
Mlinzi alitokwa macho kama mjusi aliyebanwa na dirisha huku akiwa haelewi kabisa.
” Mbona balaa jingine hili na pesa zangu zote nimetoa!, sikubali mpaka kieleweke..” Bonge aliongea huku akiwa ameshika kichwa.
” Naombeni chakula nile nin njaa…” moto aliongea huku akipiga miayo..
Mlizi alimpatia chakula mtoto akaanza kula.
Wakati anaendelea kula, Bonge alimnong’oneza mlinzi ,
” Nimeingia hasara tayari lakini hamna namna, naomba umshike twende naye mpaka mtoni tukamtumbukize…”
” Hee hiyo si itakuwa kesi ya mauaji boss wangu?”
” Hakuna atakayejua kama tumemuua”..
” Damu huwa ni nzito sana na itakuwa ngumu sana kuficha siri hii…” mlinzi aliongea.
” Sasa unataka nifanyeje?”
“‘Muache hivihivi maana hana shida yoyote huenda ikawa ni Neema kwako..”
” Hapana nimeamua hivyo, ebu mshike muweke kwenye gari afu nami nitaongozana nawe tumtupe mtoni huko…”
Akiwa ameinamisha kichwa, alimfuata na kumbeba mtoto huyo kisha wakaingia mwenye gari kuelekea mto mwiruzi, mto ambao ni mkubwa kweli wenye mamba na nyoka wakubwa.
Mnamo mida ya saa 10 za usiku, walifika mtoni hapo kisha wakashuka.
Mlinzi alimshika mtoto huyo na kutaka kumrusha mtoni.
Kabla hajamrusha, mtoto aliongea,
” Usinitupe mtoni maana kuna mamba watanishambulia…” alimwambia mlinzi ambaye alibaki ameshangaa …
JE ILIKUWAJE?
PART: 07
ILIPOISHIA
Braison kaponea chupuchupu kwa majambazi na sasa yupo kwenye mpango wa kutoa taarifa kwa majirani ili wamsaide kusafirisha mwili wa marehemu, huko upande mwingine, Mlinzi akiwa ameongozana na Bonge, anajaribu kumtupa mtoto kwenye mto wenye mamba lakini mtoto anawashangaza kwa kuomba asitupwe humo..
SONGA NAYO…
Baada ya kumaliza kufanya usafi nyumbani kwake, Braison alitoa taarifa kwa jirani zake ambao walizipokea kwa huzuni mkubwa.
Ngoma ya tahadhari ililindima ndipo watu waliokuwa na shughuli zao walivyoitikia mlio huo kama ilivyokuwa kawaida yao.
Walipewa taarifa juu ya kifo cha mtoto wa Braison ndipo taratibu za mazishi zilipoanza ikiwwemo mchakato wa kuanza kuchimba kaburi.
Mnamo mida ya saa 2 za asubuhi, Braison akiongozana na jirani zake, walifika hospitali kisha akaomba kumuona mke wake .
Alirihusiwa na kuingia kisha akamkuta akiwa amelala huku akimwaga machozi.
” Mke wangu, nyamaza, kila jambo hutokea kwa mpango wa Mungu. Tuendelee kuomba ipo siku tutapata mtoto” Braison alimwambia mkewe huku akiwa anatokwa na machozi.
” Mme wangu naumia sana..yuuh!..naumia sana mimi!, kwanini mimi jamani…yuuh!, sitomzika..mwanangu…”.Sarah alilianza kulia huku maumivu ya kidonda yakiongezeka.
” Nyamaza mke wangu, hamna namna. Nami naumia sana lakini huwezi kutoka hapa kwani afya yako haijatengamaa”
Wakati wanaendelea na mazungumzo, Mariatabu akiwa na Asia waliingia ndani kisha wakashutuka ,..
” We mama una shida gani?, tumeshakwambia unapolia unajitonesha kidonda.!, utakuja kuoza bure..” walitamka kwa sauti.
Sarah alijitahidi kufumba mdomo lakini machozi yaliendelea kumtoka.
” We mwanaume!, mda wa kuona mgonjwa umeisha muage tuendelee na kazi” walimwambia Braison
Braisom aliinamisha kichwa chini kisha akampa mkono wa kwaheri mke wake.
Aliondoka chumbani humo kisha akafanya malipo aliyokuwa anadaiwa ili kuweza kupata mwili wa marehemu.
Ama kweli waswahili wasema pata pesa mtu ajue tebia zako, ndivo ilivyokuwa kwa Mariatabu pamoja na Asia ambao walionesha sura na nyuso za furaha kweli huku wakichangamka kupita kawaida zao.
Bila kuchelewa, Mariatabu alimwambia Asia,
” Shoga angu, nina ndugu yangu yuko Dar kasema gari la milioni 7 tunapata vizuri tu..”
” Mhh kweli ?” Asia aliuliza kwa sura ya mshangao
“Yes ni kweli maana huwa anafanya kazi hiyo..”
” Kwahiyo tufanyeje?”
” Kasema tutume pesa mda huu afu ndani ya siku 2 yatakuwa yamefika”
” Duhh lakini hawatatushutukia?”
“Kwa lipi?”
” kwamba pesa tumetoa wapi za kununua magari…”
” Hee!, yaani wewe!, ina maana nikinunua gari tuanze kuchunguzana pesa nimetoa wapi?!, haloo imeisha hiyo..kwani kila anayenunua gari anaulizwa?, kila mtu anamipango na siri yake ya maisha..” Mariatabu alimwambia Dokta Asia.
” Hapo sawa ngoja tumalize kukabidhi zamu tuondoke maana tuko free siku ya leo”
” Ayaa shoga yangu! , yaani ninavyopenda kuendesha gari! Alooh! Watanikoma”
” Hahahah” alicheka kisha wakaenda kukabidhi.
Ndani ya dakika 10 , walikuwa wamemaliza kukabidhi kisha wakaelelea nyumbani na kufanya mchakato wa kutuma hizo pesa.
Akiwa amekaa kijiweni, Mkali alipigiwa simu na Mariatabu kuwa kaingiziwa pesa kwenye akaunti ya benki.
” Oyooo..oyooo..!” Chiku aliruka mwenyewe kama kichaa kisha akaenda ATM ndipo alipoona tarakimu za kutosha.
Alishangilia tena kisha akamtumia text Mariatabu,
” Asante nimepata mda si mrefu nakutumia picha ya magari wasap”
” Asante”
****
Huko hospitali, Braison na jirani zake, walifanikiwa kupata mwili wa marehemu kisha wakauingiza kwenye gari.
Dereva aliwasha gari na kukanyaga gia lakini gari ilishindwa kutembea.
Alirudia tena lakini wapi ndipo konda na dereva waliposhuka na kukagua gari lakini hawakuona tatizo lolote.
Walipanda tena kisha wakawasha gari lakini halikuweza kutembea.
” Mmeingiza vibaya maiti!, gari haliwezi kutembea!,” Mzee kipara aliongea.
Kwa taratibu sana, walitoa maiti kwenye gari kisha wakajaribu kuendesha gari ndipo waliposhangaa kuona gari linatembea.
” Hee! Kuna mchezo gani hap?!” Dereva aliongea huku akiwa anaonesha sura ya uoga
Waliingiza tena mwili wa marehemu ndani kwa kubadilisha uelekeo wa kichwa lakini gari halikuwaka tena.
” Samahani naomba mtafute gari jingine maana jioni natakiwa kuleta hesabu ya boss” Dereva aliwambia
Wakiwa hawaelewi nini kinatendeka, walishusha mwili wa marehemu na gari likaondoka.
Braison alizidi kuchanganyikiwa huku akiwa na maumivu mazito moyoni mwake yasiyoelezeka.
Kwa siri kubwa, walinunua begi kubwa lenye rangi nyeusi kisha wakaweka mwili wa maiti na wakatawanyika ili isionekane kama kama kuna mkusanyiko.
Ndani ya dakika kama 10 hivi, gari dogo aina ya Tax likiwa na abiria, lilisimamishwa kisha wakaingia pamoja na begi hilo lililokuwa limebebwa na mzee kipara.
Wakati sintofahamu inaendelea juu ya kusafirisha maiti hiyo, huko mtoni bonge alimlazimisha mlinzi kumtupa mtoto mtoni mwiruzi mto wenye maamba wenye njaa.
” Usinitupe ntaliwa na mamba..” mtoto alipiga kelele.
” Jamani mimi nashindwa nini nifanye!..” mlinzi alimwambia Bonge.
” We mlinzi wa aina gani?, ebu mtupe mtoni tuondoke tuondokane na usumbufu huu..” Bonge alimfokea Mlinzi.
” Mama kwanini wataka niliwe na mamba?, sina kosa lolote nimetenda. Naombeni huruma yenu nami natamani kuishi dunia hii..” mtoto aliongea kwa hisia akiwa mikononi mwa mlinzi.
Bonge kusikia maneno hayo ya mtoto, alijikuta anakimbilia kwenye gari na kumuacha mlinzi.
Mlinzi ile anageuka, alishangaa kuona yupo peke yake ndipo ali…..
PART: 08
ILIPOISHIA,
Mzee Kipara akiwa ameshikilia begi lenye maiti ndani, alisimamishaTax na kuingia ndani pamoja na wenzake. Huko mtoni, bonge anaishia kukimbilia kwenye gari na kumuacha mlinzi akiwa amemshikilia mtoto huyo wa ajabu..
SONGA NAYO..
Baada ya kugeuka na kushindwa kumuona Bonge, mlinzi naye alisogea taratibu akiwa amemshikili mtoto mpaka kwenye maeneo lilipokuwa gari.
Alichungulia kwa makini ndipo alipomuona Bonge ambaye alikuwa anapumua kwa kasi.
“‘Naomba nifungulie mlango” Mlinzi aliongea kwa sauti ya chini.
“‘Hee! Hivi wewe unamatatizo ya akili au?” Alimfokea.
“Kwanini boss..?” Mlinzi aliuliza huku akiwa anatetemeka.
“‘Mtoto huyu unampeleka wapi!, nimesema mtupeni mtoni mara moja”
Mlinzi kinyonge alienda na mtoto huyo kwa mara nyingine mpaka mtoni hapo.
Uzuri wa mtoto huyo ulimtoa machozi mlinzi lakini hakuwa nachakufanya.
“‘Uko wapi mama..uko wapi mama..nakufa…” mtoto alipiga kelele huku akirusha miguu na mikono.
Wakati anatoa kilio hicho, mamba alitekuwa na njaa kwelikweli, alianza kuwanyatia taratibu bila wao kumuona kwani kulikuwa na kiza kwa mbali.
Wahenga wasema dunia tambara bovu na kalele za chura hazimzuii tembo kunywa maji.
Kwa ujasiri mkubwa na ulioambatana na machozi, mlinzi alifumba macho kisha akamdumbukiza mtoto huyo mtoni .
Ndani ya sekunde chache, mamba aliachamua mdomo wake na kupiga miayo ya njaa huku akimfata mtoto huyo ambaye alikuwa amelishikilia gogo ili asizame huku akilia kwelikweli.
Baada ya kutekeleza aliachoambiwa na Bonge, mlinzi alirejea kwenye gari.
“‘Umemtupa mtoni?” Bonge akiwa na sura ya mawazo, aliongea.
“Ndiyo boss…”
“Safii huu ndo ushujaa sio muoga. Sasa unachotakiwa ni kutunza siri ili mtu yeyote asijue..”
“Nitafanya hivo boss…”
“‘Sawa ondoa gari tuondoke..”
Mlinzi alishika usukani kisha wakaanza usukani wa kurudi nyumbani.
Walifika salama bila shida yoyote huku Bonge akiwa amechoka kweli kwani alikuwa hajapata nguvu maŕa baada ya kujifungua.
Walimuandalia uji wa lishe kisha wakamchemshi
PART: 09
ILIPOISHIA,
Mlinzi alimtupa mtoto mtoni na kuanza kunyatiwa na mamba. Huko nyumbani kwa bonge, mlinzi anabaki kukuna kichwa mara baada ya jirani wema kuulizia juu ya kujifungua kwa Bonge. Na kizungumkuti kinaendelea ndani ya Tax kati ya Sauda na kipara mara baada ya gari hilo kushindwa kutembea…
SONGA NAYO…
Akiwa amedumbukizwa mtoni, mamba mkubwa sana aliyekuwa na njaa, alimuweka kwenye mawindo mtoto huyo ambaye alikuwa analia huku akiwa ameshikilia kipande cha mti ili asizame.
Hakuwa amemuona mamba huyo bali alisumbuliwa na ubaridi wa maji yaliyokuwa kama barafu.
Kilio cha mtoto huyo, hakikuweza kumzuia mamba kusogea ndipo zilipobakia dakika chake kabla ya kukamatwa.
“Mama..mama..mama.” mtoto huyo alimtaja mama lakini hakutokea.
Safari ya maisha yake ilionekana kufika kikomo mara baada ya mikono yake kuanza kuchoka.
Asee ndani ya sekunde chache, mamba alijisogeza ukingoni kidogo kisha akazamisha kichwa chake nakumrukia.
Wakati mambo yanakuwa hivo mtoni, huko kwa Braison maiti bado inaendelea kuwang’ania mara baada ya gari waliloingia kushindwa kutembea
Sauda mara baada ya kupaza sauti, dereva alimwambia konda wake wakague mizigo ndipo mzee Kipara aliyekuwa na begi lenye maiti alipotoa macho kwa hofu na mshangao mkubwa.
“Utaratibu gani mnataka kuufanya huu!, mizigo ni siri ya mtu ” mzee Kipara aliongea
“Nimeshawambia huyu mzee atakuwa na ndiye mwenye mkosi. Mbona anakataa yeye peke ake?” Sauda alipaza sauti.
“‘Akaguliwe..akaguliwe…” abiria walipiga kelele
“‘Vijana hivi heshima imeenda wapi!, mnaongea maneno haya mbele yangu!, mimi si babu yenu kabisa…” akiwa anatetemeka , Kipara aliongea huku akina Braison wakiwa wamebana…
“Hata kama kwanini ukatae kukaguliwa?, una umebeba madawa ya kulevya?” Walimuuliza.
“‘Haya ngoja nishuke furaha yenu itawale…” Kipara aliongea.
“‘Oyaa akaguliwe begi lake hilo..” kijana mmoja aliongea
Wakati anaongea hivo, Mzee Kipara alipita mlangoni kwa kasi kabisa begi lake kisha akasimama kwa pembeni mwa gari.
Ndani ya sekunde chache Braison alitamka,
“‘Samahani kwa mlichokionesha kwa mzee wetu ambaye ni tunu la taifa hili itoshe kusema ni udharirishaji hivo nami nashuka”
Braison alishuka na wenzake wakashuka kwa awamu ili abiria wengine wasigundue kama wapo wote.
Kwa hasira dereva aliwasha gari ndipo lilipowaka na kutembea tena kwa speed.
Abiria walimshukuru Sauda na kumtaja mzee Kipara kama mchawi.
Mara baada ya mambo kuwa magumu, walianza Ä·ujadiliana.
“Tatizo liko wapi?” Mzee alimuuliza Braison.
“Mzee sijui chochote maana tangu jana mara baada ya kupokea taarifa ya msiba huu sijafanya chochote…”
“‘Sasa tunafanyaje?” Mzee aliuliza tena.
“Tutembee kwa mguu…” Braison alijibu.
“‘Hapana, wewe na mzee mpande gari afu sisi tutakuja na mguu” baba Sadick aliongea.
“‘Sawa .”
Safari ilianza kwa mwendo wa masaa 3 hivi kwa mguu huku Braison akiwa ametangulia kwa gari pamoja na mzee Kipara.
Mnamo mida ya saa 5 za asubuhi, majirani wakiongozwa na baba Sadick waliwasiri akiwa ameshikilia begi .
Watu waliokuwa msibani walijiuliza maswali wapi mwili wa maiti upo lakini hawakupata majibu.
Kwenye mida ya saa 6 za mchana, wazee wa kimila wakiongozwa na mzee Kipara walianza kufanya kikao cha siri juu ya kile kilichotokea.
Walikaa kwa takribani masaa mawili huku wakitambikiza kila aina ya dawa kabla ya shughuli nzima ya mazishi.
Baada ya kumaliza, walimchinja kondoo na kukinga damu waliyoimwaga kwenye mti mkubwa uliokuwa kama sehemu maalumu ya matambiko.
“‘Pokea zawadi hii kama ishara ya kuomba msamaha na msaada kwako kwa hiki kilichotokea. Tunajua unafahamu na tumemaliza siku nyingi bila kukupa zawadi lakini tusamehe …” waliongea huku wakiwa wamenyoosha mikono juu.
Baada ya kumaliza, walitawanyika na kurudi msibani mmojammoja.
Ratiba rasmi ilitangazwa na mazishi yalipangwa kufanyika mida ya saa 9 alasiri .
Wakati hatua za mazishi zimefikia hatua hiyo, huko kwa Bonge mlinzi baada ya kuulizwa juu ya Bonge kujifungua alisita kidogo na kukaa kimya kwa mda huku akiwa anakuna kichwa.
“‘Twambieni basi maana tunataka tuondoke kama bado yupo hospitali tumfate tumpelekee chakula na kumpa hongera kama utaratibu wetu” Mama Vanesa na wenzake walimwambia.
“Yupo ndani amepumzika ” aliwajibu..
“‘Ohh jamani Mungu kasaidia amejifungua mtoto wa aina gani?” Walimuuliza.
“‘Sijui maana kazi yangu inaishia nje sijui ya ndani…” aliwajibu
“‘Sawa ngoja tumuone” Mama Vannesa na wenzake waliingia ndani bahati nzuri wakimkuta Bonge akiwa anakunywa uji sebuleni.
Baada ya kuwaona, alishutuka na kubaki ameshikilia kikombe cha uji mkononi.
“Karibu…” aliwakaribisha.
“‘Asante pole na hongera kujifungua salama, “walimpongeza.
Baada ya kauli hiyo, Bonge alikosa cha kuongea na kufanya ukimya utawale kwa sekunde kadhaa hali iliyoleta taharuki kwa Mama Vannesa na wenzake na kubaki wameangaliana….
💥💥
Mamba tayari kamrukia mtoto mtoni. Huko msibani saa 9 ya alasiri inasubiriwa kwa ajili ya mazishi nyumbani kwa Braison…
JE NINI ILIKUWAJE?….