MTOTO WA AJABU
Part 1
Ama kweli ukistaajabu ya Musa basi utayaona ya Firauni. Ni ngumu kuamini lakini ukweli ndo huu hapa.
Karibu katika simulizi hii ya kusisimua kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Ilikuwa siku ya jumatano huko wilayani kakonko mkoani kigoma, ndipo Sarah mke wa Braison aliyekaa kwenye ndoa kwa takribani miaka 3 hivi bila kuona dalili yoyote ya kupata mtoto alipomwambia mmewe,
“Mme wangu…” alimwambia kwa tabasamu.
“Naam…”
“Nina habari njema…”
“Zipi hizo mke wangu ?”
“Nikwambie au nisikwambie?” Alimshika kwenye bega.
“‘Sasa kwanini usiniambie..?” Alimuuliza.
“‘Ayaa ngoja niseme,!. Najihisi kuwa mjamzito…”
“Hee! acha utani ..! ” aliongea kwa mshutuko.
“‘Kweli kabisa mme wangu…”
“Umejuaje?”..
“Yaani sijaona mwezi wangu kabisa afu najisikia mwenye kichefuchefu..”
“Mhh..mwezi ndo kitu gani?” Alimuuliza
“Jamani kwani hujui, yaani sijaona siku zangu..”
“Hee!, sipati picha kama nami naweza kupata mtoto na wewe. Kikubwa iwe siri yetu na kesho asubuhi na mapema twende hospitali”
“Sawa mme wangu yaani ninafuraha kweli…”
“Hahah ebu punguza furaha tukapime kwanza”
Kesho yake asubuhi na mapema, waliongozana kuelekea hospitali huku wakijihisi wenye aibu mara baada ya kuongozana bila mtoto.
Braison baada ya kukaribia hospitali, alisimama kisha akageuza shingo nakumwambia mkewe,
“‘Mke wangu, nakupeda sana tena sana lakini nakuomba nibaki hapa nikusubiri maana sijisikii kwenda hospitalini hapo..”
“Mhh kwanini ?!, “
“Naona aibu mke wangu kuona hata vijana walioa juzi tayari wana watoto..”
“Mme wangu usijali kuhusu hilo na mtoto ni mpango wa Mungu. Nina imani na matumaini makubwa tutapata mtoto..”
“Nenda kwanza nakusubiri hapa…”
Baada ya kauli hiyo, Sarah akiwa amekunja uso alielekea hospitali.
Aliketi kwenye benchi ndipo aliposikia tangazo kutoka kwa nesi kuwa,
” Wote mliokuja kupima ujauzito kwa mara ya kwanza , mnatakiwa kuja na wenzi wenu”.
Sarah bila kuchelewa, alinyanyuka na kumfuata Braison.
“Wanakuhitaji…” alimwambia.
“Hee! Wananihitaji ili nifanye nini sasa!. “
“‘Bwana ndo utaratibu uliopo sasa hivi…”
“‘Kwahiyo namimi wananipima ujauzito au?”
“‘Bwana we twende kwani unaogopa nini?. Kuna wanaume wenzio wengi nimewaona..”
“Ni vizuri kujua wanataka kunifanya nini maana..” alikatisha maneno kisha Sarah akamvuta na kuongozana naye.
Braison alikuwa anatembea kwa kutetemeka kwelikweli huku akiwa kama anataka kutimua mbio.
Alijikaza mdogomdogo na hatimaye wakafika hospitalini hapo kisha Sarah akaingia chumba (Nesi).
Kabla hajamsikiliza, alimuuliza.
“Umekuja na mwenza wako?”
“Ndiyo…”
“Ebu kamuite aingie ndani..”
Sarah alimfata Braison kisha akamwambia kwa sauti ya chini.
Braison alijikuta mwili mzima unatetemeka lakini alikubali kwenda.
“‘Karibu…” Nesi aliwakaribisha.
“‘Asante…” Braison aliitikia.
“Samahani kwa usumbufu lakini ndivo mwongozo unavyotaka kila mama anayetaka kupima ujauzito kuja na mwenza wake…”
“‘Sawasawa. “
“Sasa kabla ya kuendelea, tutapima afya zetu hasa kuona kama tupo salama juu ya VVU au la”
“‘Hee! Yamekuwa hayo tena!, kama ni hivyo basi..basi…”Braison alifoka.
“‘Kuwa muelewa, kupima afya yako inasaidia kuishi kwa matumaini na kujikinga zaidi. Kikinge inamsaidia mtoto mtarajiwa kuweza kuwa salama” Nesi alimwambia Braison.
Baada ya kuambiwa hivo, Braison alitulia kidogo huku akikimbuka ni miezi mitatu imepita tangu binti wa kinyarwanda aliyetembea naye (Guest house), afariki .
Mapigo ya moyo yalipanda na kushuka kwa Braison hali iliyomuogopesha sana Sarah.
Nesi aliwapeleka kwenye chumba cha maabara ambapo walitolewa damu kwa ajili ya vipimo.
“‘Subirini kidogo kama dakika 5 nawapa majibu” aliwambia.
Bila kupoteza hata dakika 1, Nesi alimuita Braison aje peke yake ili ampe majibu.
“Braison….”
“Naam…”
“Nakuomba…”
Kwa hofu kubwa alienda kupokea majibu.
“Relax, jisikie huru…” alimwambia….
PART: 02
ILIPOISHIA,
Braison aliitwa na Nesi ili kupokea majibu ya vipimo …
SONGA NAYO…
Mwili mzima ukiwa unamtetema, Nesi alimwambia,
“Relax…” Nesi alimwambia
Kwa umakini mkubwa sana, alitulia kama maji ya mtungi huku Nesi akiwa ameshika kalamu.
“Hongera kwa hatua hii.” Nesi alimwambia.
“Majibu yakoje?” Alimuuliza.
“‘Uko vizuri kikubwa endelea kuwa muaminifu kwenye ndoa na zingatia kutumia kinga”
Braison alishusha pumzi na kuachia tabasamu kisha akatoka chumbani humo.
Baada ya dakika kama 1 hivi, Sarah aliitwa kisha akaingia ndani na kupatiwa majibu.
Katika majibu hayo, vipimo vilionesha yuko salama huku akiwa na ujauzito wa wiki 3.
‘” Hongera uko salama na tayari mpaka sasa wewe ni mama kijacho “
“Waohhh…!, kweli ?” Alimuuliza kwa mshangao.
“Vipimo vinaonesha hivo zingatia mlo kamili lakini pia utaanza kuhudhuria clinic”
“Asante…”
Sarah alitoka chumbani humo akiwa na tabasamu kisha akaambatana na mme wake kuelekea nyumbani.
” Mme wangu mambo yameiva sasa. Tumesubiri kwa mda mrefu sasa hatimaye ombi letu limejibiwa…” Sarah alimwambia kwa tabasamu.
“Kwakweli nina furaha isiyo na kifani . Leo lazima tuchinje kuku maana nilikuwa sijisikii vizuri kukosa mtoto..”
” Hahaha, lakini mme wangu mbona ulikuwa unaogopa kupima” alimwambia huku akiachia cheko laini
“‘Hahaha hapana bwana ebu tuongee mengine”
Baada ya mazungumzo hayo, waliendelea na safari na walipofika nyumbani, jogoo mkubwa alimwagwa damu na kukaushwa.
Ni furaha iliyokuwa ya aina yake kwa wawili hao.
Baada ya mambo kuwa mazuri, utaratibu wa kwenda clinic kila mwezi, ulianza, mpaka ilipotimia miezi 9.
Cha kushangaza, baada ya miezi 9 kutimia, Sarah alienda hospitali kujifungua lakini uchungu hakuwa nao ndipo alipokaa wodini kwa wiki moja bila kujifungua.
Maneno ya chinichini yalianza kusambaa mtaani mara baada ya Sarah kushindwa kujifungua.
Daktari alimfanyia vipimo kuona kama anaweza kufanyiwa upasuaji lakini cha kushangaza, mtoto alionekana bado mchanga yaani hajatimiza mda wa kuzaliwa.
Sarah alipewa taarifa hiyo kisha akaambiwa arejee nyumbani.
Alirejea nyumbani huku tumbo likiwa limetuna kweli.
“Mke wangu kulikoni?” Braisona alimuuliza mke wake.
“‘Nimeambiwa mda haujafika….”
“Hee!, mbona miezi 9 tayari?”
” Nami nashangaa lakini yatupasa kufuata maelelezo ya daktari..”
Maisha yaliendelea hivohivo mpaka hapo alipotimiza miezi 15 ndipo alipohisi uchungu.
Ilikuwa ni mida ya saa 4 za usiku hivi, ndipo hali ya Sarah ilipobadilika huku uchungu ukiongezeka.
Braison alimbeba mkewe kwenye baiskeli kisha akampeleka hospitali.
Baada ya kufika, walimpokea kisha akakimbizwa kwenye wodi ya kinamama wajawazito.
Ndani ya mda mfupi, Nesi alianza shughuli ya kumsaidia kujifungua huku kwa pembeni akiwa na mwenzake kujua ni mtoto gani ambaye amemaliza miezi 15 ?
PART: 03
ILIPOISHIA
Nesi akiwa na mwezake kwa pembeni, alianza kumsaidia Sarah kujifungua huku wakiwa na taharuki ya kumuona mtoto huyo aliyebebwa tumboni kwa miezi 15..
SONGA NAYO..
Nesi huyo ambaye anajulikana kwa jina la Mariatabu pamoja na mwenzie anayejulikana kwa jina la Dokta Asia walifanya kila jitihada lakini ilishindikana ndipo walipomwambia Sarah ambaye alikuwa anajigalagaza kitandani..
“Sukuma…!..acha uvivu tutakutia kisu..” walitamka.
Sarah aliyekuwa amechoka kama jogoo waliotoshana nguvu, alijitahidi kusukuma lakini hakuwa na nguvu tena.
“Hapa hamna namna nyingine tofauti na kumtia kisu” Dokta Asia alimwambia Mariatabu
“‘Wewe dada!, umekuja na mme wako?” Walimuuliza Sarah.
“‘Ndiyo…” kwa sauti iliyoambatana na uchungu mkubwa aliwajibu.
“‘Anaitwa nani?”
“‘Braison…”
Baada ya mazungumzo hayo, walikwenda mpaka ukumbi wa mapokezi na kumkuta Braison akiwa ameshika tama.
Walimuita na kwenda naye ndani kisha wakamwambia,
”Samahani, wewe ndo mme wa Sarah ?”
“Ndiyo..” aliitikia kwa wasiwasi.
“‘Sasa mkeo imeshindikana kujifungua kwa kawaida hivo atafanyiwa operation ndogo ili kuokoa maisha yake pamoja na mtoto..”
“Ohhh mke wangu jamani…mtoto wangu jamani…kwanini hivo?” Alitikisa kichwa huku machozi yakimlengalenga
“Hee! Sasa unalia nini?, tunakuomba ukasaini fomu hii ili tuanze kazi maana mkeo hana nguvu .Afu ni kawaida sana kujifungua kwa aina hiii…”
Braison akiwa anatetemeka, alijaza fomu ya kiapo kwa niaba ya mke wake kisha akatia saini.
Baada ya kumaliza, alitakiwa kulipa kiasi cha Tsh laki 280 ndipo aliposhika kichwa nakubembeleza kwani hakuwa nayo yote..
“Jamani hela tena!, mbona tumeambiwa kujifungua ni bure?” Alitamka kwa huruma.
” Kujifungua ni bure kwa wale wanajifungua kawaida ila wa operation ni laki 280.” Walimwabia.
“Naombeni msaada wenu maana nimekiwa na laki 2 na nusu tu..” aliwaomba
” Kalipie hiyo afu utaandikiwa deni ” walimwambia
Braison alilipia kiasi cha sh laki 2 na ñusu na kubaki hana chochote mfukoni kisha akaandikiwa deni la elfu 30.
Baada ya mchakato wa malipo kukamilika, Dokta Asia akiwa na Mariatabu, walimpeleka Sarah ambaye alikuwa hoi kwa uchungu kwenye chumba maalumu tayari kwa kumuweka kisu tumboni ili kumtoa mtoto.
Kwa wakati huo, Sarah hakuwa na utambuzi wowote hivo alisukumwa kwenye kiti cha wagonjwa mpaka chumbani humo.
Baada ya kumfikisha humo, walimbeba kisha wakamvua nguo zote na kumvalisha vazi maalumu.
Wakati wanamfanyia hivo, Sarah hakuelewa chochote ndipo walipomdunga sindano ya ganzi na ile ya usingizi.
Haikuchukua mda mrefu, Sarah alisinzia kama mtu aliyepoteza uhai huku akiwa haisi chochote.
Dokta Asia akingozana na Nesi Mariatabu, alichukua kisu chake kisha akalisogelea tumbo la Sarah na kuanza kukataka ngozi moja baada ya nyingine kwa uangalifu mkubwa.
Zoezi hilo liliendelea kwa takribani dakika 30 hivi ndipo walipofanikiwa kumtoa mtoto akiwa salama kabisa.
Mtoto huyo alikuwa wa kike huku akiwa ameota nywele kichwani kama mtu mzima.
Walizidi kumshangaa ndipo walipomuachamisha kinywani na kukuta tayari ameshaota meno.
” Hee! Huyu mtoto ameota mpaka meno!” Asia kwa mshangao alimwambia Mariatabu.
” Sijawahi kuona mtoto wa namna hii tangu nianze kazi yangu hii…” Akiwa anashangaa, Mariatabu aliongea.
” Mhh lakini katoto haka ni kazuri sana yaani utadhani malaika. Sidhani kama mama yake au baba yake wana mbegu za kuzaa mtoto mzuri namna hii..” Dokta Asia aliongea huku akiendelea kumsafisha mtoto.
Mtoto huyo alikuwa na sura ya aina yake kama ni uzuri basi alijariwa kiasi cha kuwashangaza wahudumu.
Baada ya kumaliza kumsafisha, walimpeleka kwenye kitanda kisha wakampa namba ili wasimchanganye na kuanza kumshona Sarah.
Wakati wanaelekea kummalizia kumshona Sarah, Mariatabu alishangaa kuona mama mmoja aliyekuwa amejifungua mda huohuo ambaye anajulikana kama bonge akitoa machozi.
” Umekuwaje?!” Alimuuliza kwa mshangao.
“Mtoto wangu kafariki huyo hapo…”
” Hee!” Mariatabu alienda kumuangalia mtoto na kukuta kafariki kweli.
” Pole sana..”
” Samahani dokta, nipo tayari kuwapa chochote kile ila mnipatie mtoto huyu afu yeye mwambie mtoto wake amefariki. Nimehangaika sana licha ya kuwa na mali nyingi lakini sijabahatika kupata mtoto. Leo hii mme wangu kajipanga kufanya sherehe lakini mtoto kafariki sasa nifanyeje?, huyu mtoto nimempenda sana tena sanaa.” Bonge alimwambia Mariatabu kwa uchungu..
“Hee! Kazi zetu zinakataza sana na hairuhusiwi!, ukibainika ni kifungo jela cha maisha wala hakuna msamaha..” alimjibu.
” Najua hilo lakini mnisaidie hapa nina milioni 8 kwenye mkoba afu nyingine milioni 8 ntawaletea kwa siri lakini nimpate mtoto huyu…”
” Hela hiyo ni nyingi lakini ngoja niongee na Dokta ili tuone itakuwaje japo sidhani kama itawezekana…”
Mariatabu alimuita Dokta Asia kisha akasogeaa naye kwa pembeni na kuanza kunena huku Sarah akiwa bado hajazinduka kwenye ganzi….
JE WALIKUBALIANA NINI?
JE BONGE ALIONDOKA NA MTOTO?
JE SARAH AKIZINDUKA ITAKUWAJE?
PART: 04
ILIPOISHIA,
Mariatabu alimuita Dokta Asia kisha wakasogea pembeni na kuanza kuongea kwa sauti ya chini sana. .
SONGA NAYO…
“‘Dokta kuna ujumbe tunaweza jadiliana?” Alimuuliza
“‘Sawa ngoja nimmalizie kumshona maana ganzi inaweza kukata mda wowote” alimjibu kisha akaenda kumalizia kumshona Sarah kwenye jeraha lake tumboni
Baada ya mda mfupi, Asia alimsogelea Mariatabu huku akionesha sura ya shauku,
” Ehee nipe habari. .” Alitega masikio
” Samahani kuna dili la fulani nimepewa na lina hela nyingi sana lakini ni gumu kwelikweli”
” Lipi hilo?”
” Huyo mmama bonge mtoto wake kashafariki hivo kanambia ikiwezekana tumpe tumbadilishie mtoto achukue wa Saral afu Sarah tumwambie mwanae kafariki..”
” Hee!, ni hatari sana. Kumbuka kabeba ujauzito kwa mda mrefu afu isitoshe ni hatari sana. Huwezi jua kama katumwa kututega au la..”
“Hapana hajatumwa wala nini bali anauchungu wa kumpoteza mwanaye..”
“Makubwa sasa ina maana mwili wa mtoto bado upo kitandani au umeupeleka mochwari?”
“‘Hapana hatuwezi kuupeleka mochwari.., tutaufunga vizuri afu tujifanye hatujamuona..”
“Duuh moyo wangu nasikia bado unakakaa..'”
“‘Dokta kuwa mwelewa, hata mimi nilianza kukataa mwanzo lakini kwa kazi yangu na mshahara wangu, siwezi kupata kiasi hicho labda nikistaafu. Tukiacha hela hizo tutakufa maskini..”
“Ni kweli vipi kuhusu hesabu yetu mbinguni?”
“‘Hahah..kwani tunamuua, hatumuui , tungekuwa tunamuua ndo tungetenda dhambi..”
“Mhh lakini…”
“‘Usiogope tena ana milioni 8 keshi mda huu…”
“‘Ni kweli ana keshi lakini mwanadamu hawezi thaminishwa kwa kiasi chochote…”
“‘Kwahiyo vipi sasa maana nataka ikiwezekana atupe hela afu tumruhusu aondoke usiku huu..”
Dokta Asia mapigo yake ya moyo yaliongezeka huku akiwa hajui nini akifanye kwa mda huo.
Wakati wanaendelea na mazungumzo, Braison alikuwa ameshika moyo wake huku akiwa hajui kama mke wake kipenzi kanusurika au la maana kwenye upasuaji kuna mengi.
Alijaribu kuulizia kwa wahudumu lakini hakupata majibu kwani chumba alokuwemo Sarah ni maalum na hakihitaji muingiliano.
Aliendelea kuomba mpaka hapo alipomuona Mariatabu akiwa anatembea kwa haraka.
Bila kujali, alinyanyuka kwenye benchi kisha akamkimbilia na kumuuliza,
“‘Samahani Nesi, nahisi unanikumbuka…”
“‘Ndiyo we ndo mme wa Sarah?”
“‘Ndiyo, naomba mrejesho maana nimekaa hapa bila kujua nini kinaendelea..”
“‘Tumefanikiwa kumsaidia kujifungua kwa njia ya operation na mtoto yupo salama..”
“Asante baba wa mbinguni..” Braison aliinua mikono yake juu kisha akarudi kuketi kwenye benchi .
**
Huko chumbani, Asia pamoja na Mariatabu walizidi kuongea kwa sauti ya chini sana na hatimaye walifikia hatua ya kumuita bonge..
“Una uhakika utatunza siri?” Mariatabu alimuuliza bonge.
“‘Siwezi kutoa siri kwa mtu yeyote. Niamini …!” Bonge aliongea huku akiwa anatetemeka.
“‘Umesema hapo una shilingi ngapi keshi?” Alimuuliza.
“‘Nina milioni 8 nyingine ziko benki.”
“Tunataka milioni 20 keshi kama unayo maana dokta kakataa hizo…”
“‘Ngoja nihamishe pesa kwa simbank..”
Bonge alishika simu yake kisha akavuta milioni 5 kwa njia ya simbank mara 3 yaani milioni 15 kisha akamtumia Mariatabu kweye namba zake za tigo na Voda kisha akamuongezea na milioni tano.
Mariatabu alijikuta anatetemeka kwa kiasi hicho kwani hakuwahi kukishika.
Harakaharaka waligawana kila mmoja akabeba milioni 10.
Nyuso zao zilibadilika gafra na kuwa zenye furaha huku vichwani mwao wakianza kupanga mipango.
“‘Kifuatacho sasa, maana nataka niondoke…” Bonge aliongea.
“‘Ingewezekana kukuruhusu mda huu lakini vipi kuhusu usalama wako?”
” Usalama hakuna shida kwani nimekuja na mlinzi wangu pamoja na dereva bila kusahau house girl wangu..”
“Ok sawa…”
Mariatabu alikwenda moja kwa moja mpaka kwa mtoto huyo wa Sarah kisha akamuandaa vizuri.
Wakati anamuandaa, alishangaa kusikia mtoto anaongea,
“Mama…mama…” sauti hizo ziliwatisha sana huku wakibaki wameangaliana.
Kadri mda ulivyozidi kusogea ndivyo mtoto huyo alivyozidi kuwa mzuri ( mrembo) mpaka Mariatabu akatamani awe wake.
Maandalizi yalikamilika kisha wakampatia Bonge mtoto huyo na kutaka kuondoka naye.
Wakati anakaribia kuondoka, Sarah alianza kuzinduka kwenye ganzi ndipo alipojishangaa kujihisi maumivu makali tumboni.
Alifunua shuka na kujikuta ameshonwa nyuzi tumboni hapo.
Dokta Asia alimuona kama kazinduka ndipo alipomfuata kisha akamwambia,
“‘Pole na hongera kwa kupata mtoto. Usijitingishe maana utatonesha kidonda…”
“Asante..” Sarah licha ya uchungu wote, alionesha sura ya tabasamu mara baada ya kuambiwa kuhusu mtoto.
“Hongera tena na tena, hiki kidonda utapona mda mfupi…”
“‘Asante mtoto wangu jinsia gani na ninaweza kumnyonyesha?”
“‘Niwakiume…, kuhusu kumnyonyesha ngoja tuone ila unatakiwa kuwa makini asikutoneshe kidonda. Kwa mara ya mwisho alikuwa amesinzia ngoja nimlete..”
Asia akiongozana na Mariatabu, walifuata maiti hiyo kisha wakataka kumletea Sarah anyonyoshe.
“Vipi lakini kuhusu hili au tumwambie kuwa kafariki?”
Asia alimnong’oneza Mariatabu.
“Hapana hatoamini hivo tunajifanya hatujui kama kafariki afu yeye atagundua mwenyewe”
“Mhh..mie naogopa….” Asia aliongea.
“Ngoja mie nimpelekee…”
Mariatabu alibeba Maiti hiyo ya mtoto huku ikiwa imefunikwa vizuri kisha akampelekea Sarah ambaye alitabasamu na kuibusu bila kujua ni maiti. Huko upande wa Bonge, alianza mwendo wa kutoka chumbani humo akiwa amembeba mtoto wa ajabu…
JE ILIKUWAJE MARA BAADA YA KUJUA KABUSU MAITI?
JE BONGE NAYE ALIFANIKIWA KUMCHUKUA HUYO MTOTO WA AJABU?.
PART: 05
Sarah kwa sura ya tabasamu iliyopoteza maumivu yake kwa mda, aliendelea kuibusu maiti hiyo ya mtoto huku akiigeuza huku na kule.
Wakati anazidi kufurahia, alishangazwa na hali ya ukimya kwa mtoto huyo.
Alimsogeza machoni mwake na kuona kama amefumba macho huku mwili wake ukiwa wa baridi sana.
Kwa bahati mbaya, Sarah hakuwahi kupata mtoto wala kushuhudia mtoto akizaliwa ndipo alipobaki njia panda.
“‘Huyu mtoto mbona hajitingishi wala kulia ?” Alijisemea mwenyewe.
Aliendelea kumchunguza ndipo alipoamua kuomba msaada.
“‘Nesi nakuomba maana sielewi hapa .” Alimwambia Mariatabu aliyekuwa anaongea na simu kwa kujificha huku akionesha uso wa furaha.
Bila hiyana yoyote, Mariatabu alifika sehemu hiyo kisha akamuuliza Sarah,
“‘Kuna nini?”
“‘Mtoto wangu kanishangaza ..”
“‘Kivipi?”
“‘Yaani hajitingishi wala nini…”
“‘Ohh huwa inatokea wakati mwingine ni uchovu kwa mtoto hivo atakuwa sawa..”
“‘Ebu njoo umuangalie vizuri..”
Mariatabu alisogea na kumchunguza kisha akatoa maneno machache,
“‘Bwana ameleta na ametwaa, jina la bwana lihidimiwe. Kashapoteza maisha hivo mda huu nikufanya mchakato wa kuhufadhi mwili wake mochwari au kama kuna uwezekano wa kuondoka na mwili mtatujulisha.” Mariatabu aliongea
“Hee’!’mama…mama!..mwanangu jamani…mwanangu!, kwanini mapema hivo, hujaliona hata jua mwanangu, baba yako hajakuona hata mie sijakuona kumbe ulilala mapema. Mola wangu nimekukosea nini mie mpaka wananitesa namna hii?!, . Yoooh!…yooo…yuuuh!!..:’Mariatabu alipiga kelele huku akijiviringisha na bahati mbaya alijitonesha kwenye kidonda na kuanza kutokwa damu tena.
“‘We mwanamke vipi?, hapa ni hospitali!, nyamaza kulia. Unaona sasa, umejitonesha kidonda na kimeanza kuvuja damu. Unapolia unasababisha mishipa ya tumbo kuwa (tight) nakufanya nyuzi kuvuta nyama za jeraha. Nakuomba utulie kwanza nimekuheshimu maana kwa utaratibu sikupaswa kukwambia..”
Sarah alianza kulilia tumboni kama speaker za kwenye kibuyu ambazo sautu husikika kwenye kibuyu na nje unasikika mdundo tu.
Alichukua dawa na pamba kidogo kisha akamsafisha kwenye kidonda hicho.
Wakati anaendelea naye, maiti tayari ilikuwa imeshasafishwa na kutunzwa kwenye jokofu ili isiharibike.
Mnamo mida ya saa 6 na nusu za usiku, Braison akiwa ameanza kupitiwa na usingizi, aliamshwa na mlinzi kisha akaambiwa,
” Unahitajika mapokezi..”
Akiwa na uchovu wa usingizi ulioambatana na mawazo, Braison alifika mapokezi kisha akakaribishwa,
“‘Karibu tena..”
“‘Asante..”
“‘Kweli umevumilia mpaka mda huu…”
“‘Eeh sasa nitafanyaje?, huyu ni mke wangu na mtoto ni wangu..”
“‘Hahaha hongera…”
“‘Asante…”
“‘Sasa kuna taarifa imetufikia naomba uipokee..”
“‘Ipi hiyo?!” Braison aliitikia kwa mshangao kidogo.
“‘Mtoto wetu mpendwa katutoka hivo nikupe pole kwa hilo lakoni utapata …”
Kabla hajamaliza kuongea, Braison alidondoka chini na kunyanyuka kisha akauliza,
“‘Unasema?”
“‘Mtoto katutoka yaani kapoteza maisha..”
“Hee mwanangu aliyezaliwa leo..!”
“Ndiyo…”
“Basi..basi…sina ujanja tena..”
“‘Pole kwa sasa mwili wake uko mochwari na gharama zake ni elfu 80 ukijumlisha na deni la elfu 30 jumla inakuwa laki na 10 ndo upewe mwili wa marehemu”
Braison alimwaga chozi kwa mara ya kwanza mithiri ya mtoto mdogo.
Mfukoni mwake alikuwa amebakiwa na elfu 5 tu .
Akiwa anamwaga chozi la kiume, aliondoka usiku huo kwa usafiri wa boda.
Kutokana na mazingira ya barabara waliyokuwa wanapitia huku kukiwa hakuna hata taa za barabarani, walijikuta mikononi mwa vijana wanne waliokuwa wamefunga kamba barabarani huku kwa pembeni kukiwa na msitu mkubwa kidogo.
” Simama na leteni kila kitu mlichonacho! Kama huna kitu jua wewe ni nyama yetu leo” Walitoa amri huku wakiwa wameshika mapanga na Rungu.
Braison pamoja na dereva bodaboda, walijikuta hawana ujanja kwani walishutukizwa ndipo walipolishwa chini na kuanza kupigwa ( Search).
Wakati mambo yakiwa hivo, huko kwa upande wa bonge , alifanikiwa kufika salama nyumbani kwake usiku wa manane akiwa na mtoto .
Baada ya kushuka kwenye gari, walishangazwa na mtoto huyo kushuka mwenyewe kwenye gari yaani kwa kutembea huku akisema,
” Hapa mnanipeleka wapi?” Mtoto aliongea huku akiwa amejishika kwenye nyonga
” Hee!, hivi huyu ni mtoto wa aina gani!” Bonge aliongea kwa mshangao mkubwa huku mlinzi pamoja na mfanyakazi wakibaki wameduwaa…
JE NINI KILIENDELEA?