KAHABA MLOKOLE
Sehemu ya 21 na 22
‘ ila umeninyanyasa sana kisaikolojia wewe kijana mpaka nikawa nahisi kuchanganyikiwa, yaan mlikuwa mnanitesa sana, kuna muda nilikuwa nataman hata nimfate nimpasue, kwa maana niliona kama ananifanyia makusudi, ila muda mwingine nikawa najipooza, kwa maana sikuwah kumtamkia anitha kama nampenda, tangu nilipogundua kazi zake, ila japhet ubarikiwe sana kwa kunitesa, akasema Julius na tukajikuta wote tunacheka, ila ukweli ni kwamba nilikuwa najikaza ila nilikuwa nataman kukutimua nyumban kwangu, akaendelea kusema …
“ sasa kwanini hukuwa unataka kudhihirisha hisia zako na wakat tulikuwa tunakuona hutoboi kabisa, nilikuwa nakuona namna unavyonikata jicho la wivu, nilikuwa nakuona unavyoniona nuksi, ila kiburi bana ndio kimekutesa, usinilaumu mimi bana, akasema japhet na Julius akaanza kucheka kisha akasema ‘ mimi ni wakiume nilikuwa najiona kama mwanamke atanioanda kichwan kumbe ndio nilikuwa nazidi kuharibu, akasema Julius na tukajikuta tunacheka …..
Basi tulipiga story pale na japhet , mwisho akaaga zake na kwenda nyumban kwake, nikabaki mimi na Julius, sasa safar hii akawa kama ananionea aibu flani hivi, sikutaka kusema nae, kwa maana nilijua kuwa siku hio ni shoo shoo, natoka bafuni nikamkuta Julius amekaa kitandani kana kwamba alikuwa ananisubiri..,.
Nikataka kuanza kujipaka mafuta, akawa ananizuia anataka kunipaka yeye, basi akaanza kunipaka huku akiwa anasema “ mamaa kwanini uliamua kwenda kujiuza na unaonekana kama unatabia nzuri na maadili mazuri sana…
Nilikuwa nimelala na Julius nikamtaka aache kunipaka mafuta, nikamuangalia kisha nikasema “ mimi mwenyewe sikuwa nataman kabisa kujiuza, kwa maana nilikuwa naona kama ni kazi ya kujidhalilisha, mtu yoyote Yule ambae ananijua anajua ni kiasi gani alikuwa nalitumikia kanisa, na namna gani niliokoka, sasa mama yangu akaanza kuumwa, na kiukweli mimi nipo na dada yangu na mama pakee, na mama akawa anatakiwa kwenda india, kutokana na hali yake, akapata mzamini wa kumpeleka ishu ikaja kwenye huduma zake za kila siku…..
Deni limefika million kumi, mimi na dada yangu tukaanza kutafuta, nimesoma ila nimepambana sana kutafuta kazi, ila sijawah kupata kazi, dada akaamua kujiuza, akawa anaeweza kurudi na elfu hamsin au laki, ilikuwa ni pesa nyingi sana kwake….
“ akawa anataka na mimi nikajiuze, ila mpaka wakat huo nilikuwa sijawah kulala na mwanaume, na nilikuwa naogopa sana kuvunja amri ya sita, na alikuwa anaujua msimamo wangu, akawa ananihusia sana kuwa nikajiuze ila sikuwah kukubali, basi dada akanitafutia kazi kwenye ile baa ambayo ndio ulikuta nafanya kazi, na siku ya kwanza kazin nikaambiwa nikalale na mwanaume, sikutaka kwa maana sikuwah kulala na mwanaume kabla, ila sijui ni waliniwekea kilevi, nimekuja kuamka asubuh nikakuta bikra yangu imeshatoka, na badala ya kunipongeza kwa kuitunza akaanza kunitukana, akawa anasema kuwa “ ingawa walikuwa wameniwekea kilevi ila bado nilikuwa namsumbua sana, anajuta kunichagua mimi, nilikuwa katika maumivu makali, nimerudi nyumban nikamuahadithia dada akanipongeza na kunambia karibu chaman, na kusema alikuwa anaogopa kunitafutia mabwana kwa sababu bado nilikuwa bikra, ila kwakuwa imeshatoka niache kubana bana, sikumuelewa na sikutaka kuendelea kulala na wanaume, ila sijui alinipa nini, nikawa nataman wanaume mwenyewe, na kuanzia hapo nikawa nalala na wanaume mpaka nilipokutana na wewe, ila nilipokutana na wewe nilianza kuhisi upendo na nikawa naomba kuwa wewe ndio uninunue kila siku, kwa maana ulikuwa unanipa rah asana na ulikuwa unafanya ya mapenzi na mimi kwa upendo mkubwa sana, nikawa nasema na wakt wote Julius alikuwa ananisikiliza kwa makini sana…….
Sehemu ya 23 na 24
“ sio siri nlikuwa nakuoenda sana Julius , na nilikuwa namuomba mungu sana siku moja uwe mwanaume wangu, ila tatizo likaja pale ambapo ulikuwa unanifatilia na ukaja mpaka mtaani kwetu, niliogopa sana kuharibu taswira yangu mtaan, ndio maana nikaamua kukuigizia, mara ya kwanza nilifanya kama utani, nilipojifanya kama sikujui ila baada ndio nikaja kugundua kuwa unajua kuwa mimi wa club na mimi wa mtaan ni watu wawili tofaut, na vile mimi ni msomaji mzuri wa bibilia, so maigizo yangu hayakunianguasha, mpaka nilipokutana na japhet na kwakuwa ananijua akataka nikuambie ukweli, ila ubaya ni kwamba ulipojua ukweli ukawa na hasira sana na mimi, kiasi kwamba haukuwa hata unataka kuniona………………
“ nilikuwa najua kuwa bado una hisia na mimi na ndio maana ulikuwa unataka kunitumia mimi tu na sio mwanamke mwingine yoyote, ila kilichokuwa kina nipa wasiwasi ni lini utanisamehe na kuamua kuacha mambo yapite na tuanze maisha yetu kwa raha mustarehe, nikawa naendelea kusimulia….
“ siku moja japhet ndio akanipa wazo la kukutia wivu mpaka ukiri upendo wako kwangu, tulikuwa tunakuona namna ambavyo unatufatilia, ila tulikausha kwa sababu tulitaka ukiri upendo wako, na uwe tayar kunisamehe na kuwa na mimi kwenye maisha yako, tumefanya mambo mengi na japhet ya kukutia wiu, naomba unisamehe sana kama yalikuwa yanakuumiza, ila angalau yamefanya kazi, nikasema na Julius akaanza kucheka kisha akasema ‘ hakika mmeniweza sana, ila angalau nimempata mwanamke ambae nimempenda mwenyewe, akasema Julius kisha akanisogelea na kusema kuwa anataka kuendelea kunipaka mafuta kwa maana anasikia rah asana kuishika ngozi yangu laini………..
Basi akanipaka mafuta pale, ila ni kwamba alikuwa anajikaza, mwisho akataka na mimi nimpake mafuta, “ unataka kupaka mafuta kwani umeoga, nikamuuliza, akacheka sana kisha akasema “ nilitaka kumpima mke wangu kama yuko makini na mimi, najua umeshaoga ila nimemiss sana kuogeshwa mamaa, akasema Julius na sikuwa na hiyana, ingawa nilikuwa nimetoka kuoga muda mfupi uliopita ila nikasema kuwa nikamuogeshe na n yeye, kwa maana nisimnyime raha anazozitaka …..
Tumeogeshana pale, mwisho akanibeba na kuja kunilaza kitandani na tukaanza kupeana burudan zile za miguso, na mipapaso ya hapa na pale mwishon tukazama kuleee….
Siku hio nadhan ndio siku ambayo nilijituma zaidi kuliko siku zote kwenye maisha yangu, kwa maana nilitaka nizidi kumpagawisha Julius , yaan nilikuwa nataka anipende mpaka anipendelee ….
Tumemaliza hapo, akanikumbatia kisha akasema ‘ asante sana aneth kwa kuja kwenye maisha yangu, hakika wewe ni Baraka na mwangaza wangu…
Nikacheka tu pale, na akaanza kunipa sifa zangu kuhusu juhudi zangu kitandani, mwisho kabisa akaniuliza, “ mama bado anadaiwa kiasi gani….
“ tumeshalipa million mbili mimi na dada, zimebaki nane, nikasema Julius akaniangalia kisha akasema kesho nataka mtume pesa zote kwa maana nataman kumuona mama yangu mkwe, nataman aje aone kuwa Yule bint yake mrembo mdogo nataka kumuoa na nitamuoa, tena nikishakuoa kila mwaka unataka uwe na mimba , yaan unabeba mimba mwezi wa kwanza, mwezi wa tisa unajifunga, unapumzika mwezi wa kumi alafu wa kumi na moja unabeba mimba nyingine, akasema julius nikaanza kucheka, kisha nikasema kuwa ‘ unaona mke au kifaa cha kuzalisha watoto..
“ vyote, akajibu..
“ aweee mimi siwez kuzaa kama nina mashindano ya mwanamke ambae anazaa zaidi asee, nikaanza kujilalamisha..
“siwez kukutesa bwana mke wangu, na kwanamna ninavyokupenda, usishangae nikakuomba kukusaidia kubeba na mimi hio mimba, akasema Julius , basi nikatabasamu na kumuambia kuwa “ nashkuru sana kwa kunipenda kwa maana niliamin kutokana na kazi ambayo nilikuwa nafanya basi nisingepwa ila mungu kaamua kunipa mwanaume wangu, na mwanaume wa maisha yangu….
Sehemu ya 25 na 26
Basi siku hio ilikuwa ni burudan na Julius alikuwa anaonekana kama ana hamu na mimi sana, kwa maana ulikuwa ukikaa vibaya tu unaye, ukikaa vibaya unae, ila sikuona shida kwa maana nilikuwa pia nina hisia nae na sikuwa nataka kumbania….
Japhet hakunitafuta na hakuna mtu alijaribu kunipigia wakat wote huo ambao nilikuwa na julius, yaan ilikuwa ni raha rahani , na julius alikuwa anaenda kazin ila alikuwa anarudi mapema sana, kwa maana alikuwa anapenda sana kukaa na mimi, alikuwa anataman sana kuwa karibu yangu wakati wote, alikuwa anataman niwe pemben yake siku zote za maisha yetu……
Basi siku zilienda na siku hio japhet akatupigia simu kuwa kuna shuhuli ndogo ya kuvishana pete ya uchumba, kati yake na mpenzi wake jenipher akatutaka tuudhurie, na hatukuwa na hiyana, ila siku hio ambayo ndio ilikuwa tunatakiwa kwenda kwenye hio shughuli, ndio siku ambayo mdogo wake Julius alikuja, alikuwa ni mwanamke na alikuwa anaitwa veronica, sikuwah kumuona kabla kwa maana alikuwa ameolewa muda mrefu kidogo, na sio mtu wa kuongea sana na ndg yake, ingawa walikuwa wamezaliwa wawili, ila kila mtu alikuwa na mishe zake, maana veronica alikuwa ni mtu wa starehe, ila Julius stress ndio zilikuwa zinampeleka kwenye starehe, kwa maana kama hana stree, atashinda anafanya kazi, au ata shinda anasoma vitabu au kanisani, kwa hio aina za maisha wanayoyapenda hayakuwa yanaendana na ndio maana hawakuwa na destury ya kuwasiliana mara kwa mara, na pia vero alikuwa anaonekana kama ni wale wanawake wenye viburi sana….
“ owww Julius mama alinambia kuhusu mwanamke wako, ni mrembo sana, hakika kaka yangu unajua kuchagua, ety wifi unaitwa nani? akauliza veronica na Julius akamjibu kuwa anaitwa aneth…
“ na kama unalinine lolote ambalo unataka kumuuliza, utanitumia sms na mimi ndio nitakae muuliza na sio wewe, akasema Julius na sikuwa najua ni kwanini alikuwa anamjibu short dada yake kiasi kile, ila baadae ndio nikaja kugundua, kuwa hawa ndg wawili hawakuwah kuelewana kabisa……….
“ naweza kuongozana na nyie huko mnapoenda? akauliza vero…
“ kama ungekuja na mumeo tungeweza kwenda, kwa maana nakujua dada yangu nisije nikaambiwa nakuuza bure, kwa maana sijui una mapepo, yaan ukionaga wanaume ni kama umeona dhahabu, akasema Julius kisha akanishika mkono na tukaanza kuondoka zetu, na kumuacha vero anatuangalia namna tunavyoondoka…
Basi tukaenda mpaka kwenye hio engagement party ya japhet na jenifer , ilikuwa ni zaidi ya party kwa maana walijipanga mno, na kiukweli sikuwah kumuona jenipher kabla, ila nilipomuona ndio nikaelewa kwann japhet aliamua kutulia na kumsubiria mpenzi wake, kwa maana ni chombo haswa…
Basi part ikaisha, tukawa tunarudi zetu nyumban mimi na Julius wangu…
Tyumefika nyumban tukawa tunasikia sauti kubwa ya mziki, kana kwamba ndani kuna disco, mlinzi akatuambia kuwa amejaribu kumsihi mara kadhaa vero apunguze sauti lakin ameishia kumtuka, nikamuona Julius kakunja sura kisha akasunya na kusema ‘ ndio maana sikuwa namtaka nyumban kwangu huyu mpuuzi…
Tumeingia ndani nyumba haifai, yaan kwanza yeye amekunywa zake pombe mpaka amelala hapo hapo, alafu amekula ameacha vyombo kwenye kochi, alafu kamwaga mwaga pombe, yaan nyumba nzima ilikuwa inanuka pombe zake, na ni kama alikuwa anafanya sofa, yaan inaonekana ni kama alikuwa anakunywa huku anamwaga…
Sehemu ya 27 na 28
Julius akataka amuamshe, ila nikamzuia, nikamuomba nifaye usafi, akasema atanisaidia, basi tukafanya zetu usafi na mwisho tukaenda zetu kulala, tumekuja kushtuliwa na sauti ya ya mziki, nikamuona Julius kasunya kisha akasema “ naenda kumtimua huyu mpuuzi….
Ila wakat tunatoka, kwa maana mimi nilikuwa namzuia Julius asije akamtimua ndg yake, kwa maana sikutaka kuja kuonekana mimi ndio sipendi ndg bure, kwa maana ndg wa mume hawakawii kukuona mwanga, ndio tukashangaa amelala akiwa amelewa na ameamka akaanza kunywa pombe, aisee Julius alimfata na kumuweka kibao kisha akasema ‘ embu toka nenda kwa mume wako, kwa maana haujamaliza hata siku ila ukweli ni kwamba nimeshakuchoka…..
“ nyie wanaume mnajiona kama nyie ndio mnastahili kukosea, lakin sisi tukikosea ndio kosa, lakin yakweli yote hayajawah kuwa makosa, kwa maana nyinyi mmekamilika sana si ndio, akasema veronica kwa sauti ya kunung’unika ikichanganyikana na sauti ya kilevi…
‘ namjua shemeji yangu, kama ni makosa wewe ndio umemkosea na sio yeye, akasema Julius ..
‘ ndio mimi ndio nimekosea juzi ila yeye alikuwa ananikosea kila siku, kwa maana hakuwa analala kabisa nyumban, akawa anakuja nyumban kubadilisha nguo kana kwamba anakuja zake dukani kisha anaondoka zake, nilikuwa mpweke sana nilikuwa nataman mara kadhaa niwe nae hata kidogo ila kila wakat anasingizia yuko busy na kazi, basin a mimi siunanijua kaka, siwez kukaa muda mrefu bila kupata mwanaume wakukunyoosha, na ndio mimi nikawa hivyo, kwa maana nikatafuta kamchepuko, akakafuma kwa maana nilikuwa nashindwa kujizuia kwa raha ninazopata , kwa maana kuna wakat nilikuwa namleta mpaka nyumban na siku moja mume wangu akatufumania na ndio tatizo likaanzia hapo, kwa maana alinitimua na kwakuwa sina sehemu nyingine ya kwenda na ndio maana nikaja nyumban kwako, kaka yangu au nimekosea, akasema vero, na Julius akashusha pumzi kisha akachyukua simu yake kwaajili ya kumpigia mama yake na kumuambia kuwa aje kumchukua bint yake, kwa maana anasababisha nyumba nzima isiwe na amani kwa sababu anamakelele alafu unamjua mwanao, sio wakupika wala kuosha vyombo, akawa analalamika Julius…
Mama yake alionekana kumuelewa, ila wakat wote ambao nilikuwa nakaa nae, alikuwa anaonekana kunipenda, na kila wakat alikuwa anapambana kufanya mambo ambayo yalikuwa yananivutia , hivyo tukawa mabest sana…..
Siku moja dada yangu akanipigia simu, na kuniuliza kama nani amemlipia mama pesa yote au ni mama yangu amefariki,. Nikamuambia kuwa mwanaume wangu amenilipia, kiukweli hakuamin , akawa anataka kuja kumuona Julius, kwa maana alikuwa anajua naishi na mwanaume, na mara kadhaa alikuwa anajua kuwa kuna mwanaume ambae alikuwa ananifukuzia, ila hakuwah kumuona sura hata mara moja….
Basi siku hio akaja ninapoishi, akamuona Julius na aimshukuru sana, na tukiwa pale akapigiwa simu kuwa mama yetu atarudi nyumban siku sio nyingi kutoka nchini india, basi baada ya dada yangu kumshukuru Julius akawa anataka kuondoka zake ndio akakutana na yule wifi yangu, na akauliza huyu kafata nn hapa, kwa maana walishawahig kugombania mwanaume na hata kupigana, so veronica akiwa anajua kuwa dada yangu ni Malaya…
Vero akauliz Yule mwanamke ni nani, nikamuambia ni dada yangu, aisee alitoa macho mpaka tukashangaa kwanini kajawa na taharuki baada ya kumuambia kuwa huyo mwanamke ni dada yangu………..
Sehemu ya 29 na 30
Wifi yangu veronica akatoka nje kana kwamba anamfata dada yangu, na alikuwa kama anamfahamu, alikaa nje kwa takriban dakika 20, kisha akarudi na kicheko cha dharau, na kusema ‘ kaka na ujanja wako wote na wewe umeenda kuangukia kwenye mikono ya chagudoa kweli kaka yangu, ni kwamba wanawake wameisha au kuna mambo mengine sitakiwi kukuuliza, maana kwa namna ambavyo najua unavyochukia wadada poa, sikudhan kama unaweza ukachanganyikiwa na penzi la kahaba akasema veronica …
‘ embu chunga mdomo wako, chunga unachoongea na ujue unaongea na nani, kwa maana naona unabwabwaja kana kwamba unaongea na mjinga mwenzio, akasema Julius kw sauti ya ukali kidogo…
“ sasa unanifokea ni si nimeuliza tu, kuwa pamoja na kujifanya baba paroko, pamoja na kujifanya kuwa unachukia zinaa ila mwisho wa siku kumbe na wewe umeangukia kwenye mikono ya mdangaji, wewe wewe ambae unachukia zinaa sasa hivi umekuwa mzinifu sugu, kweli dunia inaenda kasi sana, yaan kaka anaechukia wanawake wanaojiuza, kaka anaemchukia dada yake baada ya kujua ni changudoa nay eye anakuja kuoa changudoa, ama kweli maisha yanaenda kasi sana, any way nimefurahi sana kugundua hlo, akasema veronica kisha akaingia zake chumbani….
Basi siku hio ikapita na kesho yake tunashangaa mama yake Julius huyo, na alipofika tu akaniita mimi na juulius kisha akasema “ embu nambien ukweli huyu mwanamke ni kahaba…
“ mama hata haujasalimiana na sisi, unaanza na lawama, kwani shjida ni nini, na mnamtaka nini mwanamke wangu , awe kahaba au asiwe kahaba wewe inakuhusu nini mama, kwa maana mimi ndio naenda kuishi nae, na sio mtu mwingine yoyoe Yule,akawa anasema Julius …
´naomba nijibiwe swali langu kama nilivyouliza na nimeuliza kuwa, je huyu bint ni kahaba? Akauliza mama yake Julius, na safar hii aliongea kwa sauti ya msisitizo kidogo kana kwamba amemaanisha anachokisema, nilijisikia vibaya na kuanza kuogopa kwanini anakuja na hayo maswali, kwa maana nilikuwa nampenda sana Julius, sasa hio midahalio sikuwa najua walikuwa wanaileta tena ya nini, na wakat sisi tayar tumeshapendana na tumesharidhika na mapenzi yetu, nikaangalia chini kisha nikaongea kwa sauti ya kinyenyekevu kidogo na kusema kuwa “ nilikuwa kahaba na sio sasa…\
“ aneth hukuwa unatakiwa kusema hivyo, any way ni sawa, nadhan mama umemsikia, anasema kuwa alikuwa na sio sasa, akajibu Julius…
“ yaan kujifanya kote mtu wa mungu, kujifanya anatuoongoza kwaajili ya morning prayers kumbe tulikuwa tunaongozwa na kahaba, sasa utaliupia kwa kila uongo ambao umeshawah kunidanganya wewe binti , kwa maana nilidhan nimepata mkwe mwenye maadali, mkwe mwenye hofu ya mungu , kumbe tulikuwa tunaongozwa na Malaya, akawa anaonge mama yake Julius mpaka nikawa najisikia vibaya, na wakat wote Julius alikuwa anapambana kunitetea lakin wapi, mwisho akasema “ ni kweli alikuwa anajiuza ila mimi ndio nilikuwa ninamnunua, akasema Julius ……