KAHABA MLOKOLE
Sehemu ya 16
“ nitaoa mama kuna mwanamke ninae so tukiwa tayar tutafunga ndoa, akawa anajibu Julius nikamuomba mlinzi akaniitie Julius, kweli aliingia ndani na baada ya dakika chache Julius alitoka nje, na kumbe mama yake nae alitoka nae kutka kujua ni nani alimuita, ndio akaniona ni mimi…
Aliponiona akanikaribisha ndani kwa bashasha, kisha akaniletea kinywaji kisha akasema “ naomba unambie kwanini haufungi ndoa na mwnangu mpaka sasa, naomba unambie ni jambo gani ambalo linawazuia nyie kuoana? Akauliza mama yake Julius , nikabaki nimetoa macho ila Julius akanionesha ishara kuwa natakiwa kukubaliana na mama yake, ikabidi nijichekeshe kisha nikasema kuwa “ kuna mambo tulikuwa tunamalizia ila tutafunga ndoa soon…..
“ wewe ni dhehebu gani mamaa, amama yake Julius akaniuliza…
“mimi ni mlokole mama, nikajibu, nikashangaa mama yake Julius anacheka kisha akasema “ ndio maana maana kijan a wangu kila wakat anasema kuwa anataka kuwa mlokole, kumbe ni kwasababu yako, ila hongera sana bint yangu ila naomba unambie kwnai siku hizi umegombana nae, kwa maana amebadilika sana kipindi hichi amekuwa mtu ambae hana raha kabisa, akasema mama yake Julius ..
“ ni kweli mama tulipishana kauli kidogo ila tumeshaweka mambo sawa tayar, nikajibu na mama yake Julius akawa anataka niwe naenda pale mara kwa mara, nikawa naogopa kukubali au kukataa kwa maana kisirani cha Julius sijawah kukielewa hata mara moja …
Ila akanionesha ishara ya kukubaliana nae , so nikakubali anachosema… basi baada ya hapo mama yake Julius akaniaga na kuniomba kesho yake kuwa anaomba niende pale, nikaitia tu kisha nikaondoka zangu, sasa wakat naondoka Julius akanifata nyuma kisha akasema “ kesho uhakikishe unakuja ila usije ukafikiria kama mimi nakupenda sana au ntakoa, njoo umtumikie mama yangu na mimi nitakulipa…
“ nimeshachoshwa na dharau zako, na kwa taarifa yako sina shida ya pesa zako, sasa uanze kutafuta uongo ambao utamuambia mama yako kwa maana sipendi hata mimi kuonana na wewe, na wala sina shida na hivyo vipesa vyako, nikasema kisha nikaondoka zangu na kumuacha Julius akiwa ananiangalia…
Kesho yake asubuh Julius akawa ananipigia simu ila sikumjibu kabisa na mwisho nikazima simu, kwa maana anajifanya anajeuri sana, sasa ngoja tuone mwisho wa jeuri yake ni wapi?….
Ila sio kweli kama sikuwa naenda kwao, kwa maana nilidamka na kumaliza majukum yangu na kuongea na japhet kwa maana alitaka tukutane nikampa udhuru, na hapo kazi ya baa nilikuwa nimeshaacha, kisha nikaanza safar ya kwenda nyumban kwa akina Julius na kumbe wakat mimi naenda Julius nsio alikuwa anatoka…
Nikagonga hodi ila Julius hakuniona maana nilisubiri mpaka gari lake lipotelee ndio niende kugonga mlango, nikamkuta mama yake maskin anafanya usafi, basi nikamsaidia pale na mara baada ya kumsaidia nikaingia jikoni na kuanza kupika, sasa yalipiya masaa matatu toka nifike pale, kumbe Julius alienda kunitafuta bila mafanikio, akaenda mpaka ninapoishi ila napo hakunikuta…
Sasa akiwa anarudi nyumban kwao, akiwa ameshakata tamaa ndio akamuuliza mama yake , ‘ nasikia vinanukia sana , embu nambie umepika nini…
“ sio mimi mwanangu ni mpenzi wako, akajibu mama yake na wakat huo huo Julius akaja jikon kuangalia kama ni kweli nilikuwa jikoni aliponiona ni kama alishindwa kuzuia tabasamu lake, akajikuta anatabasamu kisha akasema kwa sauti ya juu kumuambia mama yake ‘ nilitaka kushangaa, kumbe ni mke wangu mtarajiwa, huyu namuamin sana kwenye secta ya jikoni….
Sehemu ya 17
Basi nikawa natenga pale chakula na muda wote Julius anatabasamu tu, yaan alikuwa anaraha balaa, nikapakua chakula , mama yake alikuwa ananisifian sana, akawa anasema “ kama ulikuwa na mwanamke bora kama huyu kwann usingefunga nae ndoa tu, kwa maana wanawake kama hawa ni kazi sana kuwapata, ni kazi sana kupata mwanamke ambae anapenda kupika na akapika chakula amabcho kinaeleweka, akawa anasema mama yake Julius ..
Julius muda wote alikuwa kimya kana kwamba hakuwa anamsikia mama yake anasema nini…
Basi tukala pale , lakin muda wote Julius alikuwa anakula huku ananiangalia kisha anatabasamu, basi kuna muda mama yake Julius alisema kuna sehemu anataka kwenda na anaweza asirudi kwa siku kadhaa ila hazitozidi siku tatu, kisha akaenda kupanga vtu vyake kisha akaondoka zake….
Julius akawa ananiangalia kisha akasemas “ kumbe sio kitandani tu, hata jikoni unayaweza hivi, akawa anasema Julius ..
Nikatabasamu kisha nikasema kuwa nilifanya vile kwa sababu ya mama yake na sio kwaajili yake…
“ lakin mama yangu kafurah sana na furaha ya mama yangu ndio furaha yangu, asante sana aneth akasema Julius na mimi nikatabasamu kisha nikaenda jikoni na kuanza kuosha vyombo kisha baada ya hapo, nikaingia chumba cha kubadilishia nguo nikavaa, kuna nguo ambayo japhet alininunulia, nikaivaa, kisha nikajipaka makeup yangu moja pambe, na manukato ya kitajiri, kisha nikawa najiangalia kwenye kioo na baada ya kuona kuwa nilikuwa bomba, nikanyonga kitasa cha mlango na kuanza kutoka kwenye chumba ambacho nilikuwepo, sasa wakat ambao nilikuwa natoka , nikamkuta Julius amekaa ukumbini, na aliponiona ni kama alishindwa kuyazuia macho yake kunitazama….
“unaenda wapi? Akaniuliza…
“ naenda kwenye shughuli, kuna party nimealikwa, nikajibu…
“ unaenda na nani? Julius akauliza ila kabla hajaongea neno lingine mara mlango ukagongwa, nikatabasamu, ila alinikata jicho hilo, hata sikujali….
Nikaenda kufungua mlango kwa shauku, alikuwa ni japhet, na yeye ametupia suti flani hivi ameizing, nikaona kabisa Julius amekosa utulivu kabisa….
“ mnaenda wapi? Akauliza Julius kwa sauti flani ya kutokuwa na amani kabisa…
“ nilimuomba aneth anisindikize kwenye shughulin ya rafiki yangu na namshukuru Mungu kuwa amekubali, so kama unaswali lingine uliza haraka haraka maana tunaondoka na tumechelewa sana, akasema japhet…
Julius akatabasamu kisha akasema “ haya safar njema, kisha akakaa zake kwenye kochi akawa anaendelea kucheza zake gamu, kwa maana muda wote alikuwa anacheza game…….
Kumbe baba akili yake iligoma kabisa kukubali kuwa mimi naweza kukaa na japhet hivi hivi bila hatujafanya kitu, yaan alipohakikisha tumetoka, kwa maana japhet alikuwa na gari nay eye vile vile akatoka na yebo zake, kwa maana aliona kama akiendelea kupoteza muda tutaendelea kufanya yetu, na tulijua ni lazima Julius atatufata kwa maana hatukuwa tunaenda hata kwenye party au wapi, tulikuwa tunamtoko wet utu wakawaida…
Tukafika sehemu tukakaa, na baada ya muda mchache tukamuona Julius anachungulia chungulia, tukaona ehee dawa inaanza kumuingia …
Japhet akaanza kunimiminia kinywa tukawa tunapiga story huku tunacheka hatuna habar, mara hjaphet aanze kuninywishwa kinywaji, na kila kitu tulikuwa tunafanya makusudi mara simu yangu ikaanza kuita, kuangalia ni Julius, nikatabasamu kisha nikamuambia japhet kuwa Julius anapiga, akanambia nipokee, kweli nikapokea…
‘ upo eapiu, akauliza Julius kwa sauti ya ukali kidogo..
“ si tulikuaga kuwa tuko kwenye party, nikajibu…
‘ sipo vizur kiafya unaweza kurudi nyumban sasa hivi, akasema Julius ..
‘ mimi sio house girl wako, so tatuta mtu wa kuja kukuhudumia, nikasema kwa sauti ya kujiamin, kwa maana nilikuwa najua kuwa alikuwa eneo lile ambalo mimi na japhet tulikuwa tumekaa
Sehemu ya 18
“ mbona sehemu imetulia hivyo ni kweli upo kwenye party ? akauliza Julius mara baada ya mimi kupokea simu …
“ kwani paerty zote zinamakelele, ni kweli nipo kwenye party au na wewe unataman kuja? Nikamuuliza…
‘ nije kumfata nani? Akauliza kwa sauti ya dharau…
“ huku kuna mademu, unaweza kujiopolea mmoja, nikajibu, akacheka kwa dharau kisha akasema “ mimi sio Malaya kama wewe,..
“ kwa hio umenipigia simu ili kuniuliza kama nipo kwenye party au laa, au unajambo lingine kwa maana kwa kumbukumbu zangu, nakumbuka kuwa nilikuwaga kuwa naenda kwenye party, so sijategemea kabisa kama unawea kuniuliza swali kama hilo, nikasema…
Nikashangaa amekata simu…
Basi nikakaa pale na japhet, kisha japhet akanambia kuwa natakiwa kwenda kulala kwa julius ili asije akajinyonga bure …….
Basi akaenda kunishusha kwenye nyumba ya Julius alafu yeye akaondoka zake, nimefika ndani nikamkuta Julius bado anaendelea kucheza game,. Anajifanya kama vile hajatioka, hata sikuongea nae nae, nikapitiliza kwenye chumba ninacholala kisha nikafunga mlango kwa ndani, kwa maana sikutaka vurugu za Julius, kwanza nilikua nimechoka zangu…
Kuna muda nilikuwa nasikia kama kitasa kinanyongwa, nikajua lazima Julius alikuwa anajaribu kuja chumban kwangu, baada ya hapo nikasikia tulivu, nikalala zangu mpaka asubuh na asubuh nikaamka mapema sana, nikaanza kufanya morning prayer na hio ndio kawaida yangu, kwa maana hata kama tunamkosea mungu kiasi gani hatutakiwi kuacha kumuabudu….
Nimemaliza morni ng prayer nikaanza kujiandaa kwa ajili ya kufanya usafi, nilifanya usafi kisha nikapika chai, na mara baada ya kupika chai nikatenga, kisha nikaenda kumgongea Julius, akataka niingie chumban kwake, ila sikutaka, nikamuambia kwa pale pale mlangin kuwa chai tayar na mimi naenda zangu kazin…
Akakurupuka kisha akaniuliza “ unaenda kufanya kazi gani, au ndio umepata mteja..
Sikutaka kumjibu hata, kwa maana sikuona haja ya kumjibu, nikawa naondoka zangu…
Nikashangaa anakuja kunishika kisha akasema “ n i kweli umepata mteja? Kwa hio ndio unaenda kumhudumia? Akawa ananiuliza…
“ sio mteja , kuna kazi ambayo japhet ameniafutia ndio naenda kufanya, nikasema …
“ naomba nikupeleke, akasema sikukataa, basi akajiandaa haraka haraka nay eye akanywa chai kwa maana nay eye alitakiwa kwenda kazin kwake, akan ipitisha mpaka kazin, ndio akaamin kuwa nafanya kazi, kisha akaondoka zake…
Tumerudi nyumban tukamkuta mama, Yule mama akanipongeza kisha akasema kuwa nitahakikisha mwanangu anakuoa, kwa maana nyumba sasa hivi inaonekana kabsia anakaa mwanamke, nikijaga hapa nakutanaga na vumbi mpaka nweye tv, akasema Yule mama na mimi nikatabasamu…
Alikuwa amechoka sana, so akaenda zake kupumzika, mara akaja Julius, na wakati huo huo akaingia japhet, wakasalimiana ila ni kama Julius hapendi kabisa kuona ukaribu wangu na japhet ….
Tukasalimiana pale kisha japhet akaja nilipo akanishika kiuno kisha akasema “ samahan Julius nataka kukuibia aneth kidogo, na kingine nataka kwenda kufunga ndoa na aneth so nataka wiki hi nifanye tukio la kumvisha pete na baada ya hapo anaenda kuwa official mrs japhet, so kwa ruhusa yako naomba niondoke nae, akasema japhet , na Julius akatuangalia kisha akasema ni juu yenu na mimi hainihusu, kwa sababu najua mnapendana haya Nawatakiwa Baraka kwenye maisha yenu, kisha akaondoka zake na kwenda chumban kwake….
Sehemu ya 19
Tukaondoka zangu na japhet ila hapo ni tulikuwa tunampima tu Julius, lengo ni kuwa Julius adhihirishe hisia zake kwangu kwa maana alikuwa anaonekana kama ananipenda sana ila ujeuri ndio ulikuwa unamponza, s o tulitaka aache ujeuri kisha aseme kuwa ananipenda na tuanza harakat za ndoa, kwa maana hata mimi nilikuwa nampenda sana, na japhet alikuwa na mwanamke wake, ambae alikuwa ni mwanachuo na so muda mwingi hakuwa nae zaidi ya kuongea kwenye simu tu…
Mama yake Julius alikuwa ananipenda sana , na alikuwa anamsihi mwanae anioe kwa maana aliona maihs ambayo nilikuwa naishi, kila siku asubuh nilikuwa nafanya morning prayer, siku za mwanzo nilikuwa nafanya mwenyewe ila mama yake akataka ndio uwe utaratibu ,pya wa ile nyumba, so asubuh, mimi , Julius pamoja na mama yake Julius wote tulikuwa kwenye maombi..
Yule mama akaniona kama ni mwanga na nuru kwenye ile nyumba, alikuwa anampongeza sana Julius kwa kuchangua mwanamke kama mimi, na hapo anajisikia vzr na kumuambia mama yake kuwa “ ndio maana hakuwa anataka kuharakishwa kwa maana alikuwa anatafuta mwanamke sahihi, na mama yake alionekana kumuelewa na alikuwa kila wakat anatuombea tuwe na maisha mazuri na tuishi kwa furaha kwa maana aliamin kuwa furaha yetu ndio mwangaza na nuru kwenye maisha yetu…
Japhet hakuacha kabisa kuja kunisalimia na wakat mwingine alikuwa anashinda kabisa pale ila Julius hakuwa na amani kabisa akimuona japhet , siku moja japhet alikuja, nikashangaa Julius kavuta mdomo, sasa nilikuwa sijamaliza kufanya kufanya usafi, nikawa naelekea kwenye vyumba kusafisha nikasikia Julius anaongea na simu, akawa anasema ‘ unakuja lini jaman shemu maana japhet analalamika kuwa amekumiss sana, embu urudi hata umpe kampan maana siunajua wanaume anaweza hata kukusaliti, akawa anasema Julius ..
Nikaona kama Julius anataka kumuondoa japhet karibu yangu, nikaenda kumuambia japhet, akacheka sana kisha akasema , jenipher anajua kila kitun so hawez kuja, basi japhet akataka kumuumiza zaidi Julius akaanza kunisaidia kufanya usafi…
Akaanza kunisaidia, sasa Julius anatoka akamkuta Julius anadeki nyumba, alitoa macho kisha akasema ‘ unafanya nini wewe?…
“ huoni kama nafanya usafi au, akasema japhet ..
“ kuna gamu nilikuwa nacheza, kama hutajal naomba ukanipe kampani kwa maana kwanza sijawah kuwaza kama unaweza kushika hata fagio, au ndio unampenda sana aneth? Akauliza Julius, japhet akacheka kisha akasema “ mimi huwa sina msaidizi wa kazi na chochote kile unachokiona kwenye nyumba yangu ujue kuwa nafanyaga mwenyewe, napikaga mwenyewe, natandikaga mwenyewe na nafua mwenyewe, hivyo mimi nimezoea sana kufanya kazi zangu pekee yangu, akasema japhet , Julius hakutaka kubishana nae akajifanya hajali, akaenda zake kucheza zake gamu…
Nikawa nafanyan usafi, huku tunataniana na japhet, kumbe Julius hakuweza kufamya chochote akawa anajibanza anatufatilia, alafu akihisi tunaenda upande ambao alikuwepo, akawa anajifanya anacheza zake gamu..
Basi tukmaliza kufanya usafi, na baada ya kumaliza kufanya usafi, tukaingia jikon na kuanza kupika wote, tukapika na mara baada ya kumaliza kupika tukasaidizana kwenda kutenga chakula kisha nikasema “ karibu chakula bwana Julius, kwa maana mama yake hakuwepo siku hio…
“ japhet na wewe njoo ule pamoja na mimi, akasema Julius…
“ kuna kazi namalizia na nitakula na aneth tukimaliza shughuli zetu, akajibu japhet, nikama julius alishindwa kuvumilia, akasimama na kjuondoka wakat huo huo, akawa anasema anaenda kufanya mazoezi,…..
Sehemu ya 20
MWISHO WA MSIMU WA KWANZA
Akaondoka kama nusu saa, kisha akarudi akakuta tumeshamaliza kula na nilikuwa najiandaa kana kwamba nataka kutoka…
“ mnaenda wapi? Akauliza Julius …
“ tunatoka ofcoz si unaona, akasema japhet …
“ tumekula na aneth mungu kambariki vitu vingi, sikuwa najua kama na jikoni ni fundi hivi, akasema japhet, hapo Julius akakunja sura sijui hata alikuwa anawaza nini..
“ chakula chako kiko jikoni bro, so kama utataka kula naomba usiacvhe kujihudumia, akasmea japhet
“ alafu nilitaka kukuambia kitu bro, kwa maana naona kama chelewa chelewa mwisho nitakuta mwana sio wangu, nilishaachana na jeniher , na kutokana na tabia nzuri za aneth nimeona nisijicheleweshe nimuoe aneth, so nadhan wiki hii tutaanza harakat za uchumba wiki hii, na namshukuru sana aneth kwa maana nilipomuambia nia yangu akakubali, so nashukuru sana Julius kwa kunikutanisha tena na mwanamke wa ndoto zangu, akaendelea kusema japhet…
Julius akatoa macho kisha akatuangalia kwa sekunde kadhaa kisha akasema “ ni sawa, nyinyi ni watu wazima na nina uhakika kuwa mnajua mnachokifanya, haya nawatakia bara njema na uchumba mwema, akasema Julius kisha akaondoka zake, jpahet akajifanya kama amepokea simu, akanambia kuwa atakuja kunichukua baada ya kama nusu saa, so akanitaka nibaki pale…
Julius alipoona japhet ameondoka akarudi kukaa na mimi pale ukumbini ila kila mtu alikuwa busy na mambo yake, nan i kama Julius alikuwa ananiangalia kwa wizi wizi hivi…
Muda ukawa unaenda, akaenda jikoni , sijui alikuwa anataka nini, mara nikashangaa sms inaingia kwenye simu yangu, kusoma ilikuwa inatoka kwa Julius, akisema njoo mara moja jikoni…..
Nikasimama na kwenda mpaka alipo…
“ aneth ,akaniita…
“ abeee umeniitia nini, au kuna kitu unataka….
“ hapana kuna jambo nataka kuongea na wewe, kwa maana naona kama uvumilivu unaanza kunishinda, akasemA JULIUS …
“ kitu gani hicho? Na mimi nikauliuza…
“ aneth samahan kwa nitakachokuambia, ila naomba unisikilize kwa makini ninachotaka kukisema, akasema Julius …
“ sitamani uolewe na japhet, na sio japhet, sitaman uolewe na mwanaume yoypote Yule, aneth, kwa maana nilikuwa nakupenda kuanzia siku niliokuona, na nilikuwa nahasira kidogo wakat ambao nilihisi unanidanganya, ila ukweli ni kwamba hata kama nilikuwa na hasira sana ila sijawah kuacha kukupenda na nakupenda sana aneth, naomba usiwe karibu na japhet kwa maana unanitesa…
Nikamsogelea, nikamgeuza kwa maana alikuwa amenipa mgongo kisha n nikasogeza lips zangu kwenye lips zake kisha tukaanza kukiss, na sio siri Julius huwa anahisia sana na mimi, so tulikiss mwisho nikamuachia na kusema “ sijawah kuwa na mahusiano na japhet, na siku zote tulikuwa tunapambana ujikaze na useme wazi kuwa unanipenda, tulikuwa tunataka tukuone unajivunia kuwa na mimi, na sio kunitoa kasoro kwa maana huenda kweli nilikuwa Malaya, ila kuanzia nilipoanza kuwa na wewe sijawah kulala na mwanaume mwingine,n ajaphet hakuwa kuwa mwanaume wangu hata mara moja, nikasema…
Mara tukasikia mlango unafunguliwa kisha japhet akaingia na kusema “ ulikuwa unanichukia bure bro, mimi sio adui yako bwana na sijawah kukuchukulia mwanamke wako hata mara moja, basi wakaanza kucheka , kwa maana Julius alijiona boy asana kuwa na hasira na kisirani dhidi ya japhet ….NA HUU UNAKUWA
MWISHO WA SEASON YETU YA KWANZA
INAENDELEA