KAHABA MLOKOLE
Sehemu ya 11
Nilishtuka sana kwanini Julius na japhet wapo ninapoishi, yaan Julius aliponiona akaja na kunikumbatia, nikajua kila kitu kimeshaharibika, na japhet alikuwa kimya anaangalia mambo yanavyoenda , “ ulikuwa wapi mamaa, na kwanini ulihama bila kunambia, haujui umeniweka kwenye wakat mgumu kiasi gani wewe mwanamke, kwanini hata haukunambia, haya nipe hata hio namba ya dada yako ili usije ukanikimbia tena, akasema Julius
Nilishindwa kujitetea kwa maana nilikuwa sielewi kwanini japhet kafanya vule, na wakat wote ambao japhet alikuwa pale, alikuwa kimya na alionekana kama hanifahamu kabisa, akawa anaasema kuwa “ umefanana sana na rafiki yangu, hata nilipokuona sikuamin kama sio wewe, ama kweli dunian wawili wawili, akasema japhet, nikajua hapa anataka kuliendeleza gemu, nikajichekesha pale na baada ya hapo nikaanza kuongea kwa upole, kisha nikasema “ muda mwingine usipopata neema, basi bwana mungu wako anataka uhame huenda kipato chako na rizki yako ameiandika sehemu nyingine, kikubwa ni kujichunga na maovu ili uweze kuupata ufalme wa milele, nikasema mpaka Julius akatabasamu na kusema “ this is my girl na sio Yule kahaba…
“ mbona hata hautukaribishi ndani? Akauliz Julius kwa maana wakat wate ambao tulikuwa tunazungumza tulikuwa tumesimama mlangoni, niliogopa kumuingiza ndani kwa maana niliogopa asije akaona kiashiria chochote kile cha mimi kuwa ndio Yule Yule mwanamke kahaba, nikawaomba nikajiandae kisha tutoke, kweli tulienda mpaka restaurant moja, na wakat wote Julius alikuwa ananiangalia kwa matamanio, ila japhet akawa anajifanya hana hata muda na mimi, nikasema huyu lazima atakuwa na mipango yake, sasa kuna muda Julius alienda uwani, ikabidi nimuulize kwanini amemleta Julius nyumban kwangu…
“ alikuwa kama amechanganyikiwa,sasa nitafanya je? Akauliza japhet ..
“ lakin anaweza akaja ghafla akagundua kuwa mimi wa club na wa kanisani ni mtu mmoja, nikasema
“ Julius anakupenda sana, naomba umuambie ukweli, kwa maana sidhan kama atakataa kuwa na wewe, kwa upendo alionao kwako, na umuambie kila kitu ambacho unakitaka na hata hayo madeni yako atakulipia kuliko kuendelea kumtyesa hivi, akasema Jsphet …
Kabla sijamjibu japhet Julius alikuja, akawa anatuangalia pale, kisha akasema “ mmeshaanza kupia na story, japhet huyu sio Yule changudoa, nilishawah kukuambia kuwa Yule demu anaringa na wakat kuna wanawake wengi wazuri na wamefanana nae waliokuwa na maadili mazuri, si unaona hata wewe…
“ ndio bro na wamefanana sana, ila mungu awajalie mfunge ndoa mapema, siunajua mungu hapendi maasi, akasema japhet …
“ avunjae amri za mwenye zi mungu amevunja imani yake kwa mungu, mimi siwez kuvunja amri ya mungu so hatuwez kufanya madhambi, na kama hilio tunaloliona ni dhambi tutakuja kulifanya kwenye ndoa ili iwe ni Baraka kwetu, nikasema mpaka Julius akatabasamu kisha akasema “ this is my girl …
Basi tulipiga story pale na nikamtumia japhet sms kuwa nataka kwenda kupumzika, so anatakiwa kutafuta namna ya kumuondoa Julius pale maana ni kweli nilikuwa nimechoka na wakatb wote huo nilikuwa nataman kulala tu….
“ samahan Julius naomba nikafanye majukumu mengine, najua umeshajua ninapoishi so utakuwa unakuja kila unapotaka kuja kwa maana mimi ni wako tu, nikasema , Julius akatabasamu na kusema “ ndio mara ya kwanza nasikia maneno mazuri kama hayo kutoka kwenye kinywa chako, asante sana aneth…
Sehemu ya 12
Nikatabasamu na wakaniomba wanikirudishe nyumban, ila tulipofika nyumban na dada yangu nae alikuwa amerudi kutoka kenye mizunguko yake, alikuwa amevaa nguo na wigi langu, nan i kawaida kwetu sisi kuvaliana nguo, ni kama Julius alikuwa anamuangalia sana dada yangu, kana kwamba kuna kitu alihisi, ila sikutaka aendelee kumfikiria pale nikaingia ndani na kuwaomba waondoke, na watakuja kesho yake na walikubali…
Baada ya kama dakika kumi sms iliingia kutoka kwenye simu yangu ilikuwa inasema “ kuna jambo Julius amehisi, ananiuliza kuhusu dada yako hapa na anasema kama nguo alizozivaa anahisi anazitambua..
“ mwambie kuwa nguo zinafananaga na siwez kuwa navaa nguo za hovyo kiasi hicho, na mimi nikamtumia sms japhet
“ sawa ila kwanini usimuambie ukweli? Kwa maana naona ni bora ajue ukweli mapema, huenda akawa mwanaume bora sana kwako na akakubaliana na kila kitu, ikaingia sms nyingine kutoka kwa japhet …
“ sijui naanzaje kuongea nae, kwa maana mimi mwenyewe nimechoka kujifanya naishi maisha ya aina mbioli, ni bora ajue posh baby na aneth ni mtu mmoja ila hata sijui namuambiaje ukweli, na mimi nikamjibu japhet ..
“ usijal hio kazi niachie mimi, akajibu japhet kisha tukaagana kwa maana kweli nilikuwa nimechoka na wakat huo nilikuwa nataka kupumzika tu…
Bsi tukaagana na mimi nikalala zangu na usiku kama kawaida, na siku hio sikumuona kabisa Julius, ila japhet alikuja pale bar, kwa maana kuna mambo yetu tulikuwa tunapanga , ingawa nilikosa kazi ila aliniunga na biashara moja ambayo ni kweli ilikuwa inaniongezea kipato na kila mwezi alianza kunipa laki tatu, ili kunisaidia tu niweze kumpipia mama yangu na ikiwezekana niache ile kazi chafu na niendelee na huduma yangu ya kumtegemea mungu
Kumbe Julius hakuja pale club kwa kuwa alikuwa anataka kwenda kunizumbua nyumban, nimekaa pale nafanya majukum yangu, nikashangaa dada yangu ananipigia simu na kunambia metja wangu amerudi na anakuulizia…
Nilijua moja kwa moja ni Julius, nikamwambia japhet, maana sikujua nafanya je..
“ ni wakat sasa wa kumuambia ukweli, kuwa nimuambie dada yako aniongelee na aseme ninapofanya kazi, ili hata ikiwezekana Julius ajue kuwa Yule mwanamke anaemdharau na kumuona kama hana adabu, ndio huyo huyo mwanamke ambae anatangaza kila siku kuwa anataka kumuona, kwa kuwa anataka kunioa ni lazima awe ananijua, akasema japhet ila nikajikuta naanza kuogopa sana, kwa maana sikujua Julius atalichukuliaje…
Japhet basi akaniombea ruhusa pale, kisha akanambia hakuna kubadilisha nguo akanipeleka mpaka ninapoishi, sasa dada yangu akamkaribisha Julius ndani, ile naingia ndani tu, nikashanaa namuona Julius katoa macho kana kwamba mjusi kabanwa na mlango, ni kama hakuwa anategemea kama naweza kuvaa nguo kama zile, akasimama kisha akasema “ aneth …
Nikaangalia chini kisha nikaitikia kwa sauti ya chini kuwa “ abeee ..
“ umevaa nini, na kwanini umevaa kama changudoa, kwa hio wewe sio bint mlokole kama nilivyokuwa nakufikiria si ndio, wewe ni nani, na ulikuwa unataka nini kwenye maisha yangu, akasema Julius ..
“ posh baby na aneth ni mtu mmoja mwenye mionekano miwili tofauti, naomba unisamehe sana Julius kwa kutokukuambia ukweli, nikaanza kujiliza pale, ila Julius ni kama alikuwa amishiwa na nguvu akajikuta amekaa chini, huku akiniangalia kwa macho ya kutoamin anachokiona na alichokisikia
Sehemu ya 13
Mara Julius akaanza kucheka, akacheka sana kisha akasema ‘ hatimae nimekutana na mwanamke muigizaji, yaan anajifanya bikra kumbe ni kahaba, akacheka sana kisha akasema “ aneth bint mlokole, aka posh baby mnenguaji, unajua kunengua sana na mauno unayo,naona utakuwa umeshamuonjesha mpaka rafiki yangu kwa maana anakufata nyuma nyuma kila siku kama mkia, ila wewe mwanamke ni shetani, akawa analalamika Julius …
‘ sikutaka kukudanganya ila sikuwa najua kama unanipenda, so nimeona bora ujue ukweli kwa maana sikutaka uje kugundua mwenyewe kuwa mimi ndio Yule kahaba unaemtukana na ndio huyo huyo bint mlokole ambae kila siku unamuomba mungu aje kuwa mke wako, naomba unisamehe sana Julius , nikaanza kusema…
Akacheka sana kisha akaondoka zake, ikabidi na japhet amfate nyuma kisha akaanambia usijal kila kitu kitakaa sawa mamaa, huyu ni kwamba hajategemea ila najua kuwa anakupenda sana, kisha wakaondoka zao…
Nilijisikia vibaya ila nikajiambia kama ni riziki yangu basi atarudi na kama sio rizki yangu hata kaa arudi tena , nikawa naendelea na maisha yangu kama kawaida….
Nikasema kuwa nitakuwa naendelea na kazi zangu kama kawaida, na japhet alikuwa anapambana sana nisidange na akawa anapambana kunifanya niwe mwanamke mwenye hadhi, siku zilipita na kila nikimuuliza japhet kuhusu Julius anasema kuwa hataki hata kunisikia, wala kuniona, hataki hata kusikia jina langu, nikasema ni sawa kwa maana anayo haki ya kuwa na hasira kwa namna ambavyo nilikuwa namdanganya…….
Basi maisha yakawa yanaenda, nikawa naenda tu kuuza pale baa ila nikawa sitaki maswala ya kutumiwa na mwanaume, na mchana nilikuwa naenda kazin, kwa maana japhet alikuwa amenitafutia kazi na usiku nilikua naenda kuuza pale baa, ila sikuwa najiuza tena na nikaja kugundua Yule meneja ya ile baa alikuwa ni mwanaume wa dada yangu, so hata nilipokuwa nakataa alikuwa anaelewa….
Basi maisha yangu yakaanza, nilikuwa kweli navaa nguo za ajabu kwenye kazi yangu ya usiku, ila mchana nikaanza kuitengeneza heshima yangu ile ile, kwa maana ni kweli sikuwa napenda kabisa kujiuza ila ni maisha na mahitaji ya pesa nyingi ambazo alikuwa anahitaji mama yangu huko hospital ….
Basi siku moja nikiwa nauza zangu baa, nikashangaa Julius anakuja, na aliponiona akaanza kutukana, akawa anasema “ yaan unaweza ukamuona mwanamke ni mrembo sana ila kumbe ni kahaba, alafu mchana anajifanya ni church girl kweli dunia ina maajabu yake, na mimi nimeshaona maajabu yangu, sikumjibu ila akawa anataka mimi ndio nimuhudumie, ila nikimsogelea, mara anishike kalio, mara anishike ziwa, nikaona uduwanzi huu, nikaenda kwa meneja na kumuambia kuwa nimeingia period ghafla sikuwa najua, nikaomba nikajitengeneze kidogo, akanielewa na akampeleka muhudumu mwingine kwa Julius, ila Julius hakuwa anataka akawa anataka mimi ndio ni muhudumie, na meneja alipoweka ngumu akawa anaondoka zake, nani dhahiri kuwa alikuwa amekuja kunikera mimi tu hakuwa na lingine lolote…..
Basi siku hio ikapita na kesho yake japhet alinifata na kwenda kuniombea ruhusa kazin, kwa maana nilikuwa nafanya kazi kwa mshkaji wake mmoja…
Kisha akanipeleka nyumban kwake, ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kwenda nyumban kwa japhet, kwa maana tunakutanaga kwenye migahawa, au kwenye ile baa ambayo nafanya kazi au muda mwingine huwa tunakutana nyumban kwangu…..
Alikuwa na nyumba nzuri, akanambia kuwa amechoka kula kila siku chakula cha migahawan so alikuwa anataka nimpikie, na kiukweli sikukataa…
Basi akanipeleka jikoni kisha akanambia kuwa niwe huru, kisha yeye akaondoka na kunambia ameitwa mara moja kazin, ila atarudi kula chakula cha mchana, kisha akaondoka zake, sasa nikajua nipo pekee yangu, nikawa napika huku naimba, nikawa naimba zangu huku nacheza nikiwa nakata kata vitu…
Na kwakuwa nilihisi kuwa niko pekee yangu, nikaanza na kukatika kabisa, kwa maana nikiamin hawez mtu yoyote Yule kuniona, mara nikasikia kama mtu kakohoa, nikashtuka na nikawa nasikilizia, nikawa nasikia kimya, nikajua ni wenge langu tu na hakuna mtu pale…
Sehemu ya 14
Nikiwa naendelea na shughuli zangu, Mara nikaanza kusikia sauti za nyayo kana kwamba kuna mtu anatembea, “ japhet … japhet umerudi, nikawa naita ila kukawa kimya, hivyo nikanyamaza kidogo na kuanza kusikiliza, ila kulikuwa kimya nikajua labda ni wenge langu, nikiwa namalizia kupika nikahisi nashikwa kiuno kugeuka alikuwa ni Julius akaanza kunikiss …
Nikamsukuma kisha nikasema “ una shida gani wewe …
Akjacheka kwa dharau kisha akasema “ wewe ni kahaba so sitegemei kama unatakiwa kuuliza swali kama hilo kwa mwanaume ambae anataka kukununua, haya leo naongeza dau, laki tatu, yaan unipe vyote kwa maana najua ndio kazi yako…
“ samahan Julius sipo hapa kwa sababub yako, nipo hapa kwa heshima ya japhet so please naomba uniheshimu hata kidogo, nikawa nalalamika, nikashangaa anaanza kucheka kisha akasema “ kwahio umelala na mimi pamoja na rafiki yangu , ila wewe mwanamke unajua kutumia ulichobarikiwa na mungu vzr sana, hongera, akasema Julius ila hata skumjibu, nikashangaa anazima jiko kisha akasema “ lazima unipe nitakulipa, nikawa naleta vurugu ila hakuwa ananielewa, akanibeba juu juu kisha akaniingilia kwa nguvu na mara baada ya kumaliza akaniandikia cheque ya hizo laki tatu kisha akaingia kabatini na kutoa nguo kisha akasema, “ nimekuletee hii kwa sababu ya kukuomba samahan…
“ kwa hio ulikuwa unapanga ujinga wako na kitu cha kunipuuza, sina shida na nguo yako, nikasema la hata hakuongea na mimi, kwa maana aliingia bafuni akaoga kisha akawa anaondoka zake, na mimi nikainia bafuni kisha nikamsimulia kile ambacho amenifanyia, japhet akasema anakuja…
Sasa wakat ambao Julius alikuwa anatoka , ndio muda ambao japhet alikuwa anaingia “ unaenda wapi bro, vipi kwani umeshakula?, akaiuliza japhet kana kwamba anamshangaa Julius kuondoka wakat ule …
“sina njaa so naomba kwa heshima yako niondoke zangu, akajibu julius …
“ jana ulilewa sana na haujala naomba ule walau kidogo, maana ndugu zako wakijua watadhan nataka kumuuwa ndugu yao, akasema japhet na kuendelea kumlazimisha Julius na mwisho akakubali, sasa nikawa naanda kile chakula na ile nguo ambayo Julius alinipa, aisee japhet akawa ananisifia balaa, hapo Julius kanuna kama anadaiwa pesa ya mkopo..
Namna ambavyo japhet alikuwa ananisifia mpaka akakosa kabisa hamu ya kula, akawa anakunywa maji, kana kwamba alitekwa tena hajapewa maji kwa miezi kadhaa…
“ alafu aneth leo nataka unisindikize kwenye party ya rafiki yangu, naomba uvae hio nguo kwa maana umekuwa kama malikia flani ila wewe mwanamke ni chombo jaman, akawa anasema japhet ..
“ ohhhh usijal kwa maana ombi lako siku zote kwangu ni amri, yaan kesho mapema twende zetu tukaburudike, nikajibu, mara Julius akasimama na kuanza kurudi nyumban..
“ ulisema kuwa unataka kuondoka, mbona unarudi chumban tena? Akauliza japhet …
“ najisikia vibaya, akajibu Julius kisha akawa anaingia zake ndani, ikabidi mimi na japhet tuangaliane, kwa maana tulianza kuona wivu unaanza kumsumbua …
Basi muda ulienda na japhet akasema ananipeleka kwangu, ila kumbe Julius alikuwa nay eye anatufata nyuma, baada ya japhet kuondoka nashangaa mtu huyu hapa…
“ aneth nataka tuongee , akasema ..
“ eheee nakusikiliza, nikajibu…
‘ sitaki kukuona tena na japhet kwa maana najua utamsambazia vidudu vyako, akasema Julius..
Nikacheka kisha nikasema “ kizuri kula na ndugu yo kisha nikaingia zangu ndani, kwa maana niliona kama anaongea pumba tu…
Sehemu ya 15
Kumbe nimemuacha Julius kafura balaa, mara nikashangaa japhet ananipigia kisha akasema “ umemfanya nini Julius maana yuko hapa anakutukana tu kutwa nzima..
“ yaan uliponifikisha nyumban nashangaa namuona huyo hapo, ananaanza kuniletea majibu yake ya ajabu, nikamjibu hovyo nikaingia zangu ndani, nahisi ndio hasira zake zilipozaliwa hapo, nikasema japhet akacheka kisha akasema ‘ mwamba amekamatika aseee, itakuwa amependa vibaya so anatafuta na,mna ya kukuumiza kama alivy0oomua yeye, akasema japhet …
“ sasa hapa kwangu ameonga mwamba, kama hawez kutulia ataendelea kuumia mpaka achanganyikiwe, nikasema kisha tukacheka pale mwisho tukatakiana usiku mwema…
Sasa asubuh wakat naamka, nikashangaa namba mpya inanipigia, na nilipopokea nikawa nasikia sauti kama ya Julius kwa maana kwa kipindi chote ambacho nimemfahamu sijawah hata mara moja kumpa namba zangu za simu, nikajua dhahiri ni japohet huyo ndio kampa…
‘ unataka nini asubuh yote hii, nikamuuliza…
Akacheka kisha akasema “ nataka tuonane, nikamuambia kwa wakat huo hapana labda usiku, akakubali…
Kweli kwenye majira ya kama saa mbili kasoro usiku akanipigia simu na kutaka tukutane , nikaenda kukutana nae alikuwa anakunywa pombe na aliponiona akaanza kunywa pombe kwa sifa, alilewa sana, alilewa mno mpaka akawa hajitambui, sasa kwa sababu mimi ndio nilikuwa namjua ikabidi nimchukue nimtafutie sehemu ya kulala, kwa maana nisingeweza kumpeleka kwao wala kwa japhet kwenye usuku mpana kama ule…..
Nikakodi hoteli nikamlaza na mimi nikalala pemben yake, nashangaa kwenye majira ya uski mpana mtu ananivamia, na kwakuwa nilikua nimeshazoea kulala nae, sikuona hata umuhimu wa kumbania, nikampa ila nikasema akili yake akikaa sawa basi ni lazima alipie alichokifanya….
Basi kweli bana asubuh anaamka, anashangaa anajikuta hotelin na mimi, yaan alikuwa hachomoi kwangu ila ujeuri ulikuwa unamuhangaisha sana…
“ nakuona mwanamke mchawi umekuja kuniloga tena eee, akasema Julius mara baada ya kuamka….
Nikatabasamu kisha nikasema “ sina kazi ya kufanya zaidi ya kukuloga si unajua wewe ndio unaniweka mjini…
“ hivi una jiamin nini wewe/ akaniuliza…
“ kwanza mimi ni mrembo na mwanaume yoyote Yule anaweza kunipenda ten asana, na licha ya urembo pia nina nyota ya kung’ang’aniwa hauni ni kiasi gani hauchomoi kwangu, nikasema kwa sauti ya nyodo kwa maana nilijua kuwa nikongea kipole basi ataanza kunionea na maneno yake ya kejeli…..
Hakutaka hata kunijibu akawa anaondoka zake, “ unaondoka unaenda wapi na wakat haujanilipa na haujalipia gharama za hotel, haya fanya malipo chap kisha uondoke zako, nikasema …
Akanitumia pesa kwenye simu, na baada ya hapo akaingia uwani kisha akaondoka zake, kumbe alikuwa amesahau simu bana, mimi nilikuwa bado nina usingizi usingizi nikaona nilale mpaka kutakapo pambazuka vizuri ndio niondoke….
Nikiwa zangu nimelala mara simu yangu ikaanza kuita ilikuwa ni namba ngeni, nikapokea nikakutana na sauti ya Julius …
“ unataka nini wewe? Akaniuliza…
“ samahan naomba uniangalizie simu yangu kwa maana siioni, akasema kweli nikaangalia ilikuwa kitandani, nikamuambia kuwa nimeiona, akaomba nimpelekee nikamuuliza ni wapi, akasema kwao, ikabidi nifunge safar niende mpaka kwao…
Sasa nimefika nyumban kwao nikawa nasikia sauti inasema kuwa “ ni lazima uoe maana bila hatujakukazania wewe hauwez kuoa kabisa, ilikuwa ni sauti ya mama yake Julius , ndio nikagundua ni kwanini Julius huwa hapendi kurudi nyumban kumbe ni kwasababu ya kelele za mama yake, za utaoa lini…