𝗨𝗧𝗔𝗡𝗜𝗣𝗔 𝗡𝗜𝗡𝗜
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Sehemu ya 41
ndio daudi hiyo ndo njia sahihi ya kumpata penda’
songa nayoo,,,,,
mjeshi alijibu bira wasi wasi.
Hapo daudi ilimbidi achukue mda wa kufilikia kwanza alimuaga mjeshi kwa kusema” mjeshi ngoja kwanza nikafikilea kati ya simoni na penda” nani bora baada ya kusema hivo ” daudi aliondoka” huku ameinamisha kichwa chini na mikono kaiweka nyuma”alionekana wazi kabisa kwamba anafikilia jambo lenye uzito ndani yake” wakati huo simoni na shangazi” walikuwa wamesha fika getini simoni alipiga honi kama kawaida mjeshi akafungua” simoni akaingiza gari ndani”kisha akaipeleka sehemu husika” akaisimamisha pale, walishuka’ huku wakiwa wingi wa huraha hapo nje walimkuta Saudi yupo amesimama anawatazama,
daudi mambo vipi” simoni alimsalimia. Hivo daudi ‘ lakini daudi hakuitika salamu ya simoni”‘ shangazi nae alimsalimia” daudi hakuitikia” waliamua kumuacha tu kama alivyo” walikuja mpaka ndani’ tuliwaona jinsi wanavyo furahia”
naona mambo ni mazuri huko mtokako mama simoni aliwauliza hivo”
ndio mama simoni unazani yengekuwa mabaya tunefurahi’ shangazi alijibu huku anakaa” kwenye kiti”
penda njoo nje huku tuongea”simoni aliniambia hivo” niliinuka nikamfata”
tulitoka nje tukapishana na daudi” yeye alikuwa anaingia ndani. Nilimtaza usini, macho yake yalikuwa yanatisha mpaka nikaogopa” mimi na simoni tukaenda kukaa chini ya mti” harafu simoni akaanza kuniambia”
penda,sasa kila kitu kipo wazi * mpaka wazazi wako wamenikubali. na sasa hivi wanajua kwamba Mimi ndio Mme wako mtalajiwa nakupenda sana penda nataka nikufanye mwana mke bora duniani” simoni aliniabia hivo” nikafurahi sana, kisha nika mwambia nakupenda pia simoni wangu,” tulikumbatia”ili kufurahia penzi letu” watati tukiwa tume kumbatiana
mjeshi” alituona akawa anajisogeza sogeza kalibu alitufikia. akaanza kutuambia wapenzi haoo, mmependeza wapenzi haoo mmependeza” alisema hivo tu akaondoka” hatukujua hata alikuwa na maana gani”. Punde, tukamuona daudi ametoka ndani akapita” kalibu na sisi alienda akachua gari kisha akaanza kuitoa, alifika getini akaanza kuongea na mjeshi, waliongea kwa dakika kadhaa haikujulikana waliongea kitu gani”baada ya kumaliza kuongea”daudi aliondoka”
hivi mama simoni huyu daudi ana matatizo gani siku hizi yani hasalimii wala haitikii salamu harafu haongei na mtu yoyote humu ndani kwenini” shangazi alimuulizavhivo mama simoni ” esi hatamimi simuelewi sijui ana matatizo gani” ila ngoja nitajaribu kuongea nae’ mama simoni alijibu”
eehe vipi sasa hukusu penda” shangazi aliuliza’ esi” penda kuanzia kesho itabidi asionane na simoni yani tumueweke ndani” mpaka siku ya ndoa yao’ mama simoni alijibu” basi walielewana hivo “
Simoni twende ndani Mimi nimechoka kukaa hapa nje nilimwambia simoni”
Penda hakuna shida tende tu”
simoni alijibu hivo’. tukainuka kisha tukaenda ndani” baada ya 5 maandalizi ya ndoa yalikuwa yame pamba moto hapo nyumbani” watu wengini wa kutoka mioka mbali mbali
hata wazazi wangu nao wali kuwepo* kwa kipindi hiko simoni” alikuwa kwa baba yake mkubwa ndo alikuwa anaishi huko mpaka siku ya kufunga ndoa atarudi nyumbani”. Huku na Mimi nilikuwa nimefungiwa ndani tu nilikuwa siruhusiwi kutoka nje”. upande wa daudi alionekana anaenda kwa mjeshi’ alipo fika wakaanza maongezi”
unajua mjeshi zimebaki siku mbili tu ndoa ifungwe sasa tunafanyaje alifika akauliza swali hilo”
daudi mbona una wasi wasi sana” Mimi nimekwambia subilia siku ya ndoa
tuna muua simoni yani kabla hata hawaja fanya chochote mjeshi alijibu hivo”
haya mjeshi nakuaminia ailsema daudi” wakaendelea kuongea mambo mengine”
siku moja ikapita na sasa ilikuwa jumapili nzuri sana kwangu maana ilikuwa ndo siku ya ndoa yangu” nilikuwa siamini kabisa kama Leo naolewa kama mwajuma “
nilikuwa nime pambwa vizuri sana hakika nilipendeza kama malaika ” saa za kwenda kufunga ndoa zilikalibia” wakati huo daudi alikuwa amechanga mka sana yani alikuwa kwenye harakati zake za kumuua simoni”mbele ya watu wengi” vipi mjeshi kila kitu kinaande sawa”
ndio daudi”sasa
yuko wapi mlengaji anae kuja kumuua simoni
” mjeshi yani wewe jiandae tu simoni akipigwa lisasi wakati watu wakiwa wanapagwa” umchukue penda harafu umulete kwangu”
poa daudi usijari Mimi nipo kukusaidia lazima penda tumchukue, hatuwezi kumuacha aolewe kipumbavufu hivi, kwanza simoni ameni halibia bahati zangu nyingi” mpaka sasa hivi moyo unaniuma ni lazima nayeye nimuhalibie ikiwezekana kama nikipata nafasi kalba ya mlenaji namuua Mimi kwa kutumia mbinu ya kijeshi hawata weza kunijua hata siku moja” mjeshi alisema hivo harafu akaanza kujiweka fiti kwalijiri ya kazi maalumu ambayo anaenda kuifanya Masaa machache yajayo” daudi na mjeshi walikuwa wamezamila kweli kuuma simoni” .
wakati huo yeye alikuwa saroni anachonga nywele zake” simoni alikuwa hajui chochote kuhusu mauaji yanayo taka kufanyika” mbele ya watu wengi tena yeye ndo anatakiwa afe” natamani angejua kama anataka kuuliwa huenda ageji linda lakini ndo hivo simoni wangu alikuwa hajui”
Sehemu ya 42
simoni alipo maliza kuchongwa nywele zake. alipendeza sana hata kwa sura simoni alikuwa mzuri tu”aliondoka hapo kwenye saroni kisha akaingia kwenye gari mpya hizi wanaziita khalia ” humo ndani kulikuwa na deleva so simoni hakupata shida ya kuendesha” walirudi nyumbani, kwa baba yake mkubwa walipo fika wakapewa chakula kwanza simoni na mwenzie walikula baada ya hapo wakaoga kisha na kubadilisha nguo* kisha wakapanda kwenye gari nyingine iliyo pambwa vizuri’ wakaelekea kanisani ambako ndoa inaenda kufanyika”
wakati huo daudi na mjeshi, pamoja na mtu mwingine ambae sikumfamu jina lake”
walikuwa wamevaa vizuri wamependeza wenyewe” yani ukiwaona huwezi kuwazani kwamba wanaenda kuuwa mtu” daudi alichukua gari ya hapo nyumbani waka pakiana nawao wakaelekea kanisani”
Mimi nilikuwa bado niko ndani nilikuwa na Dada mmoja amae ni Dada yake simoni. Ikumbukwe kwamba. Mama simoni ana watoto watano” wawili wa kike na watatu madume ambao ndio hao daudi simoni na kaka yao mkubwa ambae yuko nchini kenya anasoma’ kaka yao alishindwa kuja nchini tz kwenye ndoa ya mdogo wake simoni,
kwa sababu alikuwa bize na masomo yake hivyo basi aliomba atumiwe picha tu mara baada ya ndoa kufanyika”ndugu yao mwingine wa kike ambae yupo nchini india alishindwa kuja kwenye ndoa ya kaka yake kwa sababu alikuwa hayupo vizuri kiafya yani alikuwa anaumwa” mmoja ndio alifanikiwa kuja” ambae niko nae yeye ndio alikuwa anani fundisha kutembelea viatu vilefu ambavyo ni malizawa kwa bibi harusi tu”nilipata tabu sana kutembelea kiatu kama hicho sababu nilikuwa nimezoea kanda mbili”kila siku,
hatimae mda wa kwenda kanisani ukafika”nakumbuka ilikuwa saa 7 kamili mchana tuliingia kwenye kigari kidogo kilikuwa kimepabwa vizuri kika pendeza hadi raha, humo kwenye gari tulikuwa wanne
kati yetu shangazi nae alikuwepo,
wakati tunaelekea kanisani moyo wangu ulikuwa unadunda” sana sijui ni uoga” au nilihisi tatizo” tulifika kanisani” gari ikasimama nje” harafu wengene wote wakashuka kasolo Mimi tu” nilibaki najifanya Nina maringo kama mke wa raisi kumbe sina lolote” watu walitoka ndani ya kanisa wakaja kujazana kwenye gari nilipo Mimi” kila mtu alikuwa na hamu ya kuniona” wengine ni wapiga picha tu ,
Dada ambae ndo msindikazaji wangu alifungua mlango wa gari ilinitoke” sasa, kweli nilifanya hivyo” nilishuka nikaanza kutembea mwendo wa kinyonga mbele kulikuwa na wasichana wadogo wawili walikuwa wametangulia” huku wanacheza” tuliingia kanisani vizuri nilipo tazama mbele nikamuona kipenzi changu simoni ” wakati huo sasa yule mmuuaji aliye tumwa na daudi alikuwa amesimama sehemu yake husika wakati huo alikuwa anao uwezo wa kumshuti simoni lakini mda”ulikuwa bado,
hivyo ilibidi asubuli kwanza” wakati huo mjeshi nayeye alikuwa kwenye sehemu yake ambapo alikuwa amesubilia tu apigwe lisasi simoni
ili anichukue” daudi nae alikuwa kwenye mlango wa pili anasubili kisanuke”
Mimi nilikuwa naendelea kusonga mbele talatibu simoni nae alianza kunifata tukakutana kati kati kisha simoni akanishika mkono’tukawa tunaelekea mbele kwa mchungaji” hatimae tulifika” tuka,simama watu walishangilia kwa makofi na vigere gere, wakati huo muuji alikuwa amesha muweka tageti simoni ” mjeshi nae hakuwa mbali na sisi nilimtazama nika muona anani konyeza” sikuijua maana yake, Mara ghafla nikamuona mjeshi amevuta simoni akamuangusha chini”kulikwa na mpiga picha anataka kupiga picha lakini kabla haja piga picha alipigwa lisasi ya kichwa hapo hapo akadedi
nilipo tazama pembeni nikaona kitu kama zahabu kinakuja, tena kimenilenga” nikajua Leo nakufa” lakini kabla hakijafika mjeshi alinirukia tukaanguka chini” kwa bahati mzuri au mbaya Mimi na mjeshi tuli gusana midomo”
hapo hapo akapigwa lisasi mtu mwingine”
bila kutegemea mjeshi aliruka juu kama mchina harafu akapiga bastola kule alipo muuaji kwa bahati nzuri.ilimpata kwenye bega, wakati huo daudi anashangaa nini kinaendelea” maana watu walichanya,nyikana
alipo ona mjeshi amemguka alito bastora yake akaataka kumshuti lakini wapi alikuwa amesha chelewa mjeshi alimuwahi akampiga ilsasi ya muguu” daudi akaichia bastora” kisha akapiga magoti, wakati huo watu wengi walikuwa amesha kimbia nje” police nao wali kuwepo upande wa nje walimkamata yule. muuaji baada ya dakika kumi hali ya hewa ilitulia purukushani likaisha” watu wakarudi kanisani kuja kumalizia ndoa”Mimi na simoni tuli tulifungishwa ndoa halali’ toka siku hiyo tukawa mke na Mme mbele ya
“baada ya siku mbili” kesi ya mauji yaliyo fanyikakanisani” ikachukua nafasi yake”
muuaji aliye kamatwa na police. alihojiwa”
akamtaja muhusika mkuu wa tukio ambae ni daudi”na daudi aliulizea sababu ya kutuma watu iliwafanye mauji’ akasema hivi”
Nimefanya hivyo kwa sababu nampenda sana penda ambe ndio alikuwa bibi harusi, niliona bora nimuue kaka yangu iliniweza kummiliki penda’ lakini imeshindikana”kwa sababu mtu niliye mtegemea anitimizie hili amenigeuka ghafla” Mimi sina mengi ya kusema fanyeni kama mnavyo fikilia”
Daudi alimaliza kwa kusema hivo”
Zamu ya mjeshi ilipofika kutoa maelezo yake”
alisema hivi
Mimi sijataka kusema mengi sana mimi ni mwana jeshi ambae nalinda usalama wa wana nchi wangu kweli nilikuwa pamoja na huyu kijana pia lengo langu nilikuwa sio la kufanya mauaji ndio maana nimekutoa msaada kwa sababu jeshi letu tume fundishwa kutoa misaada pale panapa tokea matatizo”na lengo langu nilikuwa ni kumaliza chuki ya kijana huyu kwa kaka yake sasa naamini amejifunza mengi” kamwe hataweza tena kushindana na kaka yake” naomba niachiwe nirudi kazini’
Mjeshi alisema hivyo”kweli akaachiwa
ila daudi na mwenzie wali pelekwa jela wakashike adabu kwanza mahojiano hayo tuliya tazama kwenye tele visheni”
mjeshi alipo rudi nyumbani tulimpokea kwa shangwe simoni alimshukuru sana kwa kumkomboa katika kifo”wazazi wa simoni walimpa mabilioni ya pesa kwa kazi nzuri aliyo ifanya” tangu siku hiyo mjeshi aliacha kazi ya ulinzi
Mimi nilimfata kwa mda wangu
Nika mwambia
mjeshi asante sana mpenzi wangu wa zamani”Nashukuru kwa kuniokoa katika kifo natamani nikupe zawadi lakini sijui nikupe nini’ penda usijiri Mimi nime jitolea kuwa saidia wewe na mmeo simoni ili muishi kwa furaha sipendi kukuona unakosa raha kwa sababu bado nakupenda” pia kitu kingine ambacho ulikuwa hujui ni kwamba Mimi Nina,mke na watoto” kwahiyo nakusihi utulia na Mme wako na,Mimi nikarudi kwa mke wangu yaliyo pita tuyasahsu ila kuanzia Leo Mimi na wewe ni ndugu kabisa” penda nitarudi kuja kuishi huku na familiya yangu iliniwe nakuona wacha Mimi niende*
mjeshi alisema hivo kisha akaondoka zake ” niliumia sana kumuona mjeshi anaondoka hivi hivi” kwa sababu nilikuwa bado nampenda” nilimwahidi atakapo rudi nitakuja kumpa zawadi nzuri sana” baada ya mjeshi kuondoka” mme wangu simoni alikuja akaniambia mke wangu twende ndani tuka pumzike
Nikaitikia sawa Mme wangu twende tu kwanza najihisi hamu ukanikuni sugue kidogo nilisema hivo tukashikana mikono” tukaingia ndani
MWISHOOOOO

