JOIN US WHATSAPP
CLICK HERE
JOIN US TELEGRAM
CLICK HERE
MAJAMBAZI WAMTEKA MWALIMU MKUU, WAKATI AKITOKA BENKI NA PESA ZA SHULE – WAMNYANG’ANYA PESA NA KUMTUPA PEMBENI YA BARABARA.
Wakaazi wa Kibugu kaunti ya Embu walibaki na mshangao baada ya mwalimu mkuu wa shule ya upili kutekwa nyara na kuibiwa KSh800,000 mchana kweupe.
Pesa hizo zilikuwa zimetolewa kutoka kwa benki ya eneo hilo ili kulipia huduma zinazotolewa shuleni.
Kwa mujibu wa mashuhuda, mkuu huyo wa shule alibanwa muda mfupi baada ya kuondoka katika benki hiyo. Washambuliaji walimlazimisha kuingia kwenye gari na kuondoka.
Saa kadhaa baadaye, alipatikana akiwa ametelekezwa kando ya barabara, akionekana kutikiswa na kuchanganyikiwa. Wapita njia walimkimbiza hospitali kwa matibabu.

