YAMENIKUTA; Watoto wawili na mimba juu, aliniachiasha kazi serikalini sasa anaoa Mwanamke mwingine?
Naomba ushauri wako. Mimi ni mama wa watoto wawili na sasa hivi nina ujauzito mwingine. Watoto wa kwanza ni mapacha. Miaka minne iliyopita, huyu mwanaume alikuja kwetu kujitambulisha, akanitolea mahari na kuwaomba wazazi wangu tuishi pamoja kwa kuwa suala la ndoa lilikuwa halijajulikana. Aliniambia kuwa hajajipanga bado.
Kweli nilikubali, tukaanza kuishi pamoja. Nilibeba ujauzito na kujifungua mapacha. Kila kitu kilikuwa vizuri, ananijali na kunihudumia kwa kila kitu. Nilikuwa na kazi, lakini aliniambia kwa kuwa wote tuko serikalini, niache kazi ili tufungue biashara, kwani kutegemea sehemu moja si sawa.
Niliona kweli ni wazo zuri. Niliacha kazi na tukaanza biashara, na kweli ilifanya vizuri mwanzoni. Ila mwaka jana mwishoni alibadilika na kuacha kuhudumia familia. Nikimuomba pesa hatoi, na akiniambia kila kitu kipo dukani. Duka lilianza kushuka mpaka tukalifunga kabisa. Kweli nilihangaika sana, lakini ndiyo hivyo – sasa hivi niko nyumbani bila kazi.
Kuna nyumba tuliyokuwa tunajenga, lakini yeye ndiye aliyekuwa anaenda huko. Sasa, kama wiki mbili hivi zilizopita, nikaona dada mmoja akanifollow Instagram. Niliangalia na kuona amepost picha akiwa kwenye site ya nyumba yetu na akasema ni kwake. Nilimfuata na kumuuliza yeye ni nani, akanijibu, “Mimi ni mchumba wa fulani, na wewe ndiye mama wa watoto wake?” Nilishangaa sana na nikaamua kumwambia kuwa mimi ni mke wake.
Yule dada, kwa mshangao, alikua na namba yangu na akanipigia simu akaniambia, “Hapana, mimi najua kila kitu. Wewe ni mama wa watoto wake na sasa hivi una mimba yake. Mwanaume alisema utoe mimba lakini hutaki, unamng’ang’ania kwa sababu unadhani atakuja kukuoa.” Sikugombana naye. Mwanaume aliporudi, nilimuuliza kuhusu hilo. Alikanusha na kusema hakuna kitu kama hicho, lakini nilipomwonyesha picha, tuligombana sana na akaondoka bila kurudi.
Juzi alinitumia meseji na kuniambia kuwa anaenda kufunga ndoa ujao, hivyo tutalea tu watoto, na kama nitaamua kutoa hiyo mimba, ni uamuzi wangu, lakini hawezi kuwa na mimi tena. Sasa nina ujauzito wa miezi mitano, na mwanaume hataki hata kupokea simu zangu.
Kanaicha na watoto wawaili! Nimejaribu kumpigia mama yake, lakini amesema hawezi kumlazimisha kijana wake amuoe mtu asiyemtaka. Nimechanganyikiwa na sijui nifanye nini?

