NILISHEA PENZI NA MAMA YANGU, TAZAMA KILICHOTOKEA
Chapter 2
Nikaanza kufuatilia meseji, nikakuta chati za mapenzi na mahaba, ukweli sikuamini..kidogo ikaingia meseji inasema, Leo nimemiss penzi lako we mama, vipi nije hotelini Baadae?
Jina la hotel aliotaja ni hotel ya baba yangu mzazi ambae kwasasa yupo Afrika kusini Kikazi..Nguvu ziliniisha aisee ikabidi nirudishe simu, Nianze fuatilia kama kweli atatoka..
Jioni mama akatoka, na akafika kweli Hotelini pale, Nikiwa nachungulia pembeni, Akaja mpenzi wangu, ni kijana ndogo tu wa miaka 27, mama anamiaka 46, Daaah chozi lilidondoka palepale, ikabidi nirudi home.
Kwa hasira mama aliporudi nikamchana ukweli anachokifanya sio heshima, hapo ndio vita ikaanza, akatoa laana zote na kusema nitafute pakukaa hana radhi namimi, na amenitisha nikimuambia baba juu ya Hili hatoniacha salama.
Jamani Huyu ni mama yangu mzazi wa kunizaa, Natamani nipate amani nae na upendo kama ulivyo kua zamani, lakini hii tabia yake nashindwa vumilia,Je nifanye maamuzi gani?

