MWANAFUNZI ALIYESEMA “SITAKI SHULE – NATAKA MUME” AFARIKI DUNIA
Wakaazi wa kaunti ya Machakos walisalia katika mshangao mkubwa baada ya mwanafunzi wa kidato cha pili kudaiwa kujitoa uhai kufuatia kutofautiana na mamake kuhusu kuhudhuria shule.
Kisa hicho cha kusikitisha kilitokea baada ya mama huyo kuripotiwa kusisitiza kuwa bintiye arejee shuleni kuendelea na masomo.
Kulingana na ripoti kutoka kwa marafiki wa msichana aliyekufa, ambao walikuwa wanafunzi wa shule moja, kijana huyo alikuwa ameacha kuhudhuria masomo kwa muda. Wanafunzi wenzake walipomuuliza kwa nini haendi tena shule, aliwaambia kwamba amepata mwanamume ambaye alikuwa akimtimizia mahitaji yake yote. Mwanamume huyo alisemekana kuwa mzee zaidi yake.
Marafiki hao pia walidai kuwa msichana huyo alisema waziwazi kuwa haoni umuhimu wa shule tena.

