MREMBO JASUSI ALIYEMNASA RAISI KIMAPENZI, NA RAISI AKAMATWA
Chapter 2
Wakati Rais amelala fofofo, Alicia alikuwa anachukua muda huo kupekua makaratasi ya siri, kusikiliza mazungumzo ya siri ya biashara za silaha, na kujua ramani nzima ya jinsi almasi zinavyochimbwa na kuuzwa nje ya nchi. Kila kitu alichokiona usiku, asubuhi kilikuwa mezani kwa mabosi wa CIA.
Lakini unajua maisha ya kijasusi ni kama kutembea kwenye kamba? Baada ya muda, walinzi wa Taylor wakaanza kujiuliza “Huyu mzungu mbona anauliza sana maswali?” Hali ikawa tete.
Alicia akaanza kuhisi kuwa Charles Taylor anaanza kumshtukia. Siku moja usiku, akapokea ujumbe wa dharura kutoka kwa mabosi wake.
“Ondoka hapo mara moja, mchezo umegundulika!”
Ilibidi atumie mbinu za hatari kutoroka Liberia usiku wa manane kabla ya makomando wa Taylor hawajamkamata. Alirudi Marekani akiwa na siri zote ambazo baadaye zilitumika kumfunga Charles Taylor maisha kule mahakama ya The Hague kwa makosa ya kivita.
MWISHO

