MCHEPUKO WA RAISI
Chapter 1
Ilikuwa ni mwaka 1995. Binti mmoja anaitwa Monica Lewinsky, mbichi kabisa ana miaka 21, alitua Washington DC akitokea California. Alikuwa amepata shavu la kuwa mwanafunzi wa mafunzo hapo White House.
Kwa Monica, huu ulikuwa mchongo wa uhakika, kuingia ndani ya mjengo mweupe na kumuona Rais ilikuwa ina raha kubwa sana.
Ukicheki umbile lake, alikuwa amejaliwa kile tunachoweza kusema ni umbile la kimahaba. Hakuwa mwembamba sana, alikuwa na nyama kiasi na haiba iliyojaa uanamke fulani wa kuvutia. Hiyo ilimfanya awe na presence kubwa, yaani akipita sehemu, lazima ugeuke.
Hata Bill Clinton, ambaye amezungukwa na wanawake warembo na wenye akili kila siku, alishindwa kujizuia kwa Monica. Macho yake na jinsi alivyokuwa anajirembesha vilikuwa kama sumaku. Unajua tena mambo ya mjini, binti anajua akivaa nini atamtega mzee, na anajua akitupia lile tabasamu lake, mzee lazima alainike.
Hicho ndicho kilichomponza Clinton, alishindwa kutofautisha kati ya majukumu ya ofisi na yale “macho ya mahaba.
Macho ya mahaba na lile umbile lake lilozidi kumchanganya mshua, mke wa Rais, Hillary Clinton, alikuwa bize na mishemishe za kiserikali.
Unajua mwanamke yeyote mwenye akili anakuwaga na radar fulani hivi. Hillary hakuwa mgeni na tabia za Bill; alijua mume wake ni mtu wa watu na anapenda sifa, lakini hakuwahi kufikiria kuwa mwanafunzi mdogo kama Monica anaweza kupenya mpaka chumbani kufanya mapenzi na Bill.
Kuna kipindi Hillary alikuwa anamuona Monica kwenye hafla za White House, lakini alimchukulia kama binti mwingine yeyote anayetafuta maisha. Hakujua kuwa huku nyuma, mzee Clinton alikuwa ashazama kwenye lile penzi…
Kuna muda watu wa karibu wa Clinton walianza kushtuka. Waliona Monica anajipitisha pitisha sana maeneo ya Ofisi ya Rais kuliko inavyotakiwa. Walijua mzee Bill ana udhaifu wa warembo, hivyo wakaanza kuona huyu binti ni hatari kwa usalama wa kisiasa wa Rais.
Ndio maana, bila Hillary hata kujua, wakapanga mchongo wa kumhamisha Monica haraka iwezekanavyo. Wakampiga transfer ya nguvu mpaka Wizara ya Ulinzi Walijua wakimuweka mbali, moto utazima. Lakini wapi! Clinton na Monica walikuwa washapigwa na radi ya mahaba; wakaanza kupigiana simu za siri usiku kucha.
Hapa ndipo sasa yule mama mbea, Linda Tripp, anapoingia kazini. Monica alikuwa na upweke, anamkumbuka mshua wake , na alikuwa anahitaji mtu wa kumhadithia vile Clinton anavyomjali. Akawa anampigia Linda simu na kumpa full data Wee Linda, unajua leo mzee kanipigia simu? Anasema ananikumbuka sana…
Linda, akiwa amekaa zake sebuleni, alikuwa ameweka kinasa sauti tape recorder pembeni ya simu. Alikuwa anarekodi kila neno, kila kicheko, na kila siri ya mahusiano yao. Monica alikuwa anadhani anajenga urafiki, kumbe anajichimbia kaburi.
INAENDELEA

