CHUMBANI KWETU
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Episode 10
Nilifurahi sana❤😘nikaletea mtoto wangu nikamuona nililia kwa furaha nikamshukuru sana Betty maana amekuwa msaada sana kwangu🙏❤
asubuhi ya siku iliyofuata mume wangu nae akaja kumuona mtoto nae alifurahi sana 🥰 akampa jina mtoto wetu kuwa aitwe faith🥰🙏 akasema anaenda kazini akirudi atapitia na tutarud nyumbani,basi nkaletewa chakula nikapiga👌💃
wifi zuu hakuja maana alivyoenda home akapata kahoma, nikasema sababu ya kukaa hospital siku zote hizo,sio mbaya tukirud nyumbani atamuona huyo alotuweka hospital wiki nzima🤣🤣🤣
mama mkwe ilibidi aende kwenye majukumu yake maana mume wangu alisema atatupitia kurudi nyumbani
basi ilivyofika jioni nilikua nishapewa ruhusa maana hatukuwa na tatizo lolote mimi na mtoto, tukawa tu tunamsubiri mume wangu aje ikafika mpaka saa kumi na mbili nikasema labda foleni😫
mama mkwe akapiga nkamwambia bado ajatufata mpaka saivi anawakalisha tu ngoja niwafate nyie mpaka mama mkwe amefika pale ilikuwa saa moja mume wangu akawa tulipiga hapatikani😳
nikaanza kuwa na waswas😭 tukarud nyumbani roho hainipi kabisa😿kila tukipiga hapatikani mama mkwe akajaribu kumtafuta rafik ake akamwambia walivyotoka kazini waliachana akasema anakuja hospital😫
usiku huo ata nililala sasa kila nikipga simu jibu ni lile lile haipatikani🥺 mama mkwe akasema nisiwe na waswas tulale asubuhi tutajua la kufanya,siku iliyofuata wakaenda ripoti polis kuwa mume wangu kapotea ,nikawaza kwahiyo mume wangu kaniacha hivi atakuwa mzima kweli😭😭😭
betty akasema usijali atakuwa salama tu,betty akaondoka kurud anapofanyia Kazi maana aliomba tu ruhusa,mamangu hakuondoka maana asingeondoka wakati hatujajua muafaka wa mume wangu,ikapita wiki hatujapata taarifa zozote za mume wangu😭😭😭
zaidi tu lilipatikana gari eti lilikutwa limepakiwa pale hospital🤔polis wakasema tutulie wanaendelea na uchunguzi roho inaniuma jamani nikikaa chumbani nawaza mwenyewe uko wapi mume wangu mtoto wetu tulompambania umeniachia mwenyewe hivi u mzima au ushakufa😭chumba nakiona kikubwa mimi nimemiss ucheshi wako😿
nikabaki kumuombea dua njema🤲awe salama uko aliko na arudi salama🥺 usiku nikawa nimembembeleza mtoto alivyolala na mimi nikalala , sasa usingizi umenikolea😴nikasikia simu inaita🤔nikaamka ni betty anataka nini usiku huu mamy mbona usiku hivi kuna tatizo?
hamna ila nimeota ndoto mbaya ebu naomba usali Kwa imani yako na mimi uku nasali hili jambo niloota liepushwe sasa niombe nini si uniambie niombee nini?
au unihadithie hiyo ndoto jamani😫weee muombee mtoto tu kesho nitakutumia voice note nkuhadithie sawa basi nikabidi nimuombee sana mtoto wangu🤲😔
nikalia sana Mungu amlinde betty sijui kaota nini…!!! niliomba kama lisaa nikamaliza nikapanda nilale betty akanipigia tena umesali? ndio sawa uyo mtoto ni moto haguswi ng’o Amina mama, tukalala asubuhi nikaamka nikawasha data nikute betty kanitumia hyo voice na nisipokuta nitampigia kawaida mbona😹😹😹
nikakuta kanitumia tu picha na maelezo mama faith mwenzio nimekabwa leo sasa Ile picha alinitumia ilikuwa ya shingo yake yaani nikaona Ina alama maana yeye ni mweupe pee basi alama ilikuwa inaonekana😳
nikampigia umekutwa na nini jana nimekabwa sana Kwa akili zangu timamu nimeshuhudia napigana na mtu ila sikumfahamu makubwa mwaka huu acha tu lakin usijali naenda job tutaongea bde ..
mama lakini kama huna waswas rafiki angu khaa ulopigana nae si itakua ni mchaw eeeh ndio sasa niwe na waswas wanini hata usiwaze bhana ya kawaida tu👌👌sawa dear baada ok siku njema msalimie faith sawa mama kalala saiv akiamka timbwili lake si mchezo
nikaamka sasa nifanye usafi ndani , ntoe na nguo chafu mama anifulie,nikaamka mama nae akawa amekuja akanipeleka kuoga,akatoka aende kufua na kazi zingine , nikachukua simu nijaribu kumpigi aman tena ikawa inaita🥲lakin haipokelewi🥲
nilipiga kama mara nne zote kimyaaaaa🤨 nikatoka nikaenda waambia kina mama simu ya amani inaita leo ila ndo hapokei🥲 aaah jamani angepokea tujue🥺
au twende polis tukaseme simu inapatikana wanaweza jua jinsi ya kumtafuta,mama na mama mkwe wakasema wanajiandaa waende wifi zuu akawa ana vihomahoma tangu tumerud hospital au una mimba shoga angu ata sielewi leo ndo najisikia vibaya sana ukapime kama unatuletea kitoto tujue wee naogopaje😭 si ulikuwa unancheka mimi😹😹😹
ngoja nikalale tu🏃🏃sawa mama
basi mimi nikabaki pale nje najaribu kupiga simu tena na tena lakini wapi😫 nikabidi niingie ndani tu nmuangalie na faith kama kaamka sasa nakaribia mlango wa chumbani nasikia faith analia sana😭😭😭
afu nasikia vishindo vya mtu kama anakimbia mule chumbani🏃🏃nikawahi kuingia nakuta yupo mwisho wa kitanda ananing’inia kwenye net nusu aanguke, kafikaje jamani mtoto mdogo hivii😳nikawahi kumchukua kuanza kumbembeleza😭😭
Episode 11
basi ikabidi nianze kumbembeleza akanyamaza,baadae wakina mama wakarudi walivyofika polis wakapiga simu mara mbili haikupokelewa baadae ikawa haipatikani tena, kwahiyo polis wakawaambia warud tu nyumbani lakini njiani wakapigiwa simu kuwa Mzee jabir kaumwa kichwa ghafla kafariki😳🥲
afu sorry nilisahau kuwaambia,wifi zuu ni mtoto wa mzee jabir ila mimi nilikua simjui kabla ya kuolewa maana yeye alizaliwa mama tofauti na watoto wa mzee jabir wa kule kijijini,sasa aliposikia babake kafariki aliliaje😭😭 pole wifi ,alilia vibaya mno😭😭😭
mama akasema wajiandae waende yeye na wifi zuu mimi, mama na dada wa kazi tubaki tu , kidogo simu yangu ikaita ilikuwa namba ngeni nkapokea;
hallo mke wangu mume wangu ni wewe? ni mimi mke wangu😭uko wap babangu mke wangu acha tu apa navyoongea na wewe nipo dodoma na sijui nimefikaje,hivi mlishatoka hospital? ujui umefikaje?
mbona sisi hospital tushatoka muda sana ndio naomba msaada wako tu Kwa sasa hapa nilipo sina ata cent sina chochote naomba plz nitumie hela Yani kesho nipande gari asubuhi nirudi nyumbani ujui umefikaje dodoma?
kivipi ebu nielezee vizuri mke wangu huu sio wakati wa kuuliza mengi mimi mwenyewe hapa nimechanganyikiwa naomba ntumie hela nije nyumbani ntaelezea hukohuko na hapa nilipo sina simu sina nini ntumie kwenye hii namba nimefanya kuomba tu hapa, asee sikuamin kama nimeongea na mume wangu😭
nilitamani nipae niende alipo nikabidi nitoke nje fasta kuwaambia nkatuma elfu 80 nkapiga Ile namba akapokea akasema ameipata basi nikampa na mama ake aongee nae pia akasema kesho anakuja🙏🙏
tukamtakia safari njema ila hatukumwambia kuna msiba,tuliomba tu kwanza afike mama mkwe akapga simu kule msiban kuwaambia kuwa aman amepatikana kwahiyo watachelewa kidogo kwenda Ili wajue nae alipatwa na nini,ila wifi zuu akasema mimi naenda asee nikamzike babangu utaendaje mwenyewe na unaumwa na kule huna wenyeji napo vumilia tutaenda ote keshokutwa,
akakataa kata kata, ikabidi nami nimtaarifu betty kuhusu aman akasema kesho nikitoka kazini mbona sirudii nyumbani nitapita kwanza huko nipate habari kamili💃
basi asubuhi mume wangu akanitafuta kwa namba nyingne akanambia ndo anapanda gari ,nkamtakia safari njema mida ya jioni mama mkwe akaenda mpokea alivyofika nyumbani tulikumbatia kwa furaha😭😭😭
tulilia sana tukamuacha aoge ale afu aanze kutuambia kilichomsibu ,
akasema mara ya mwisho mimi nilitoka kazini vizuri nikaja mpaka hospital nikapaki gari afu sikumbuki tena kilichoendelea zaid jana ndo nikapata fahamu najikuta eneo silijui sina sina nini zaidi ya nguo nilizovaa tu ndo kuuliza kwa watu hapa wapi nikaambiwa ni dodoma🙌🙌
sielew nimefikaje yaani sijui dah…! ikabidi nasi tumuelezee kuwa amepotea wiki sasa akashangaa akasema mbona mimi nilidhani ni jana tu😳kwahyo wiki nzima mimi nilikua wapi? unatuuliza sie tutajuaje?😹😹🙌
dunia Ina mambo tukamwambia na habari za msiba wifi zuu kashaondoka na asubuh inabidi twende polis pia kutoa taarifa mtu kapatikana basi balaa tupu akasema mimi msibani siend asee kichwa changu hakipo sawa🥲
mama mkwe nae akasema mimi ntaenda ata kama wakiwa washazika basi ila tumalize kwanza mambo ya polisi nmemmiss mtoto wangu 😭
tumemuhangaikia sana😭😭😭 nikampa mtoto wake akambeba,usiku wote nilimkumbatiaje asije akapotea tena😹😹 kesho yake walienda polisi kutoa taarifa lakini polis si hawaamini kuhusu ushirikina wakasema au kijana ulijichimbia sehemu na kamchempuko🤣🤣🤣kesi ikaisha
mama mkwe akaenda msibani sisi tukabaki,saa mbili usiku tukasikia hodi dada akafungua alikuwa wifi zuu eeeh wifi umerud alikuwa hoi akajibwaga chini🥺 naomba wifi niitie yule rafik nataka kusema mmh rafiki angu betty ndio naombeni mumuite jamani😭😭😭
usiku huu wifi kweli? naombeni mumuite jamani nakufa mwenzenu akawa analalamika kichwa kinamuuma tukupeleke
hospital hapana jamani niitieni tu yule dada au nitawaambia tu nyinyi peke enu kama hamtaki nikabid nimpigie betty
akasema anakodi boda anakuja basi tukawa tunamwambia tumpe chakula hataki tukampigia mama kumwambia kuwa zuu karudi nyumban akasema hata uko pia walikuwa wanamtafuta hawakumuona tangu asubuh kama yuko nyumban basi tunashukuru maana nae si mnajua hayuko sawa anaumwa aman akashauri tumpeleke hospital nkamwambia ngoja Betty afike tujue ana shida nae gani🤔
INAENDELEA

