ALIKUBALI KUOLEWA NA MIMI KWA SABABU YA KITAMBI TU
Habari yako Raha Special.
Naomba unipostie huu mkasa wangu ili nipate ushauri.
Nilikua kwenye mazungumzo ya kawaida na mke wangu kuhusu jinsi tulivyo oana.
Sasa yeye akasema kuwa,hapendagi sura yangu maana mimi Nina sura mbaya ila alikubali kuolewa na mimi kwasababu ya kitambi changu tu na kimo changu halafu na mwili mkubwa, maana yeye hapendagi mwanaume mwembamba(mkonde).
Akaongezea kusema,Niko na sura mbaya,hakika hakunipendea sura,kwa sura asingeli olewa na mimi ila alikuwa anavutiwa na wanaume wenye muonekano mzuri wa sura na kimo.
Sasa mimi nikamuuliza, kwanini ukubali kuolewa na mwanaume mwenye sura mbaya,Sasa ikiwa Siku moja kitambi kikiisha,utanipendea nini kingine?, je,haukuwaonaga hao wanaume wenye sura nzuri ?.
Alijibu kwa kusema,
– kuolewa ni hivyo tu,
– pia,alisha ingia kwenye ndoa, hawezi fanya lolote tofauti na kukaa na mimi.
Sasa ndugu,huyu mwanamke ana maanisha nini kuniambia hivyo bila kumkosea kwa lolote ,maana apendaye hajali lawama na upendo husitiri wingi wa mabaya.
Hivi Kuna mtu ampendaye mwenzie,awezae kumvunjia heshima na kumdharau kiasi hiki kwa kumwambia maneno kama haya?,

