UKINIPA SISEMI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Sehemu Ya 26
Huduma bado tuliendelea kupata kwa hali ya juu na watu ambae walikuwa wapo kwenye kile chumba walionekana kutujali sana. Ile hali ya wale watu kutujali sana na walikuwa wanaongea kwa Heshima ya Hali ya Juu mimi ilinishitua na kuamua kuongea na mtu mwingine.
Ingawa walikuwa wamejazia miili yao sikuona tabu kumuuliza maana heshima ambayo alikuwa ananionyesha ilikuwa inaonyesha wanatuheshimu sana. Yule mtu nilipomfuata na kumuuliza kwa nini Wanatuheshimu na kutuhudumia vizuri hivi wakati sisi ni Maaduni wa boss kwanza alininishangaa sana. “Hapana wewe siyo adui wa Tajiri wetu masanja hata siku Moja. Ungekuwa adui wa Masanja usingekuwa kwenye hiki chumba kabsa. Labda ngoja nikwambie tu kitu ingawa najua unataka kunipima akili maana unajua kinachoendelea humu. Nitakwambia kwa kuwa mimi ni mfanyakazi wa humu na nikikujibu vibaya akasikia boss wangu nitakuwa nimekosa kazi kitu ambacho sitaki kukisikia kwenye maisha yangu. Maana kupitia Hii Kazi ingawa Mungu anaipinga kwa kiasi kikubwa Nawatunza wazazi wangu, mke wangu na nasomesha watoto.
Hiki Chumba bwana ni Chumba Special kwa Wafanya biashara wakubwa wa Masanja. Kama Unavyoona Hata Huduma humu mnapewa ya hali ya juu sana hii ni kutokana na Thamani yenu. Siyo kwamba hii nyumba kuna chumba hiki tu kizuri ambacho kinawahudumu wazuri na wakalimu vyumba vipo zaidi ya kumi na kila Chumba na biashara yake. Kwenye hiki chumba ambacho mmeningia Nazani mtakuwa na Mzigo mzuri tu wa Madawa ya kulevya mmeyaleta. Hivyo Karibuni sana hii Ndio kazi ya Boss wangu nazani mnajua kama aliwaambia kuwa yeye nje ni mchungaji mzuri tu lakini ndali ni mfanyabiasha na Muuaji mzuri.
Pia Ndugu biashara yako ikienda vizuri nikumbuke hata kidogo”Aliongea Yule mtu kwa ulefu maelezo yaliyonifanya kuniacha hoi. Usiku kwa kweli sikupata Usingizi nilikuwa nawaza ni namna gani naweza kutoka kwenye kile chumba salama na jinsi gani naweza kupambana na Masanja mtu ambaye alikuwa ananizidi kwa kila idara. Kwenda kupambana kingumi Masanja alionekana mzuri, nguvu ya pesa ndio kwanza alikuwa anatisha, kwa kutumia maneno ya dini ili kuwafanya watu wamchukie hicho kilikuwa hakiwezekani maana misaada ambayo alikuwa anatoa mchungaji masanja ningeyaongea kwa watu ningeonekana kichaa. Hadi saa Kumi usiku ndio Usingizi ulinipia na kula hadi Saa mbili asubuhi nilipoamshwa na kelele mihudumu akituamsha. Nilipoamka na kutoka kwenda kumsikiliza Muhudumu alikuwa anasemaje nilibaki nikishangaa nilipomuona Klinita. “Boss Jitaidi Kuongea haraka maana baba yako akigundua upo huku itakuwa hatari sana maana haturuhusu wewe kuingia huku”Aliongea muhudumu kumwambia Klinita.
Kwa kweli kitendo cha kumuona Klinita amekuja angalau kilinipa ahueni kidogo na kufikilia yeye huenda atakuwa msaada mkubwa wa sisi kutoka pale tukiwa salama salimini “Sam sina muda wa kupoteza sana hapa ila nimekuja kuwasaidia nyinyi ingawa msaada ambao nitautoa kwenu itakuwa kama sijawasaidia tu. Ila kabla sijafanya hicho kitu naomba unithibitishie kwa Mdomo wako tena ni kweli baba yangu siyo mtu mzuri . Ninaposema baba yangu siyo mtu mzuri nikiwa na maana ndiyo kafanya mauaji ya kumkata mama yako kichwa kama ulivyoniambia pia naoma unithibitishie ni kweli maneno ambayo aliongea Magreth kabla ya kufa ni sahihi. Ni kweli Magreth ni dada yangu na wazazi wake waliuawa kinyama na baba yangu. Naomba nieleze kwa makini na tumia muda mfupi sana niweze kukuelewa”Yalikuwa ni maswali ambayo aliniuliza Klinita huku akiwa na wasiwasi hali iliyonifanya kugundua huku aliingia kwakuibia lengo aweze kuyaokoa maisha yetu. “Klinita kabla ya kujibu maswali yako kwanza kabsa nataka utambue kuwa nakupenda sana na sitaki nikupoteze. Nataka kutimiza kile ambacho dada yako magreth aliniambia kabla ya kufa kuwa nikuokoe upo sehemu mbaya. Hivyo kama mimi nakupenda sana hata hiki ambacho naenda kukwambia ni kitu cha kweli kabsa wala siwezi kuongea uongo wa aina yeyote ile. Kwanza kabsa nataka utambue kuwa magreth ni dada yako ambae mmechangia damu chafu ya baba yako. Kama nilivyokwambia mwanzo baba yako alikuwa ni Padri na alikuwa Yupo shule ya Seminary kama masimamizi hivi. Wakati baba yako akiwa Padri mama yake na Magreth alikuwa ni Mwanafunzi wa seminary hiyo akisomea Usister. Kutokana na Uzuri wa mama yake na Magreth ulimfanya Baba yako amtake kimapenzi mama yake na Magreth bila kujali kama ni kinyume na matakwa ya Dini yake. Mama yake na Magreth alipoambiwa vile kwa kweli alikataa. Licha yakukataa baba yako alimbaka Mama yake na Magreth. Alipombaka hatimae Mama yake na Magreth naye aliona kama hana sifa ya kuwa Sister tena alilidhika na Masanja na kuanza kufanya mapenzi hatimae akamtia Mimba. Masanja alimpompa mimba mama yake na Magreth alimdanganya kuwa asimtaje kama yeye ndio kampa mimba. Aliendelea kumwambia kuwa yeye ataacha upadri siyo muda na kumuoa yeye. Kwa kuwa mama yake na Magreth alishamzimia masanja alikubaliana na kumtaja mtu mwingine then walifukuzwa shuleni. Lakini baada ya Mama yake na Magreth kufukuzwa shuleni masanja hakufanya kama alivyomwambia mama yake na Magreth bali alienda kuwauwa wazazi wote wa mama yake na Magreth lengo amuue na Mama yake na Magreth ilikupoteza ushaidi. Bahati nzuri wakati anawauwa wazazi wa Mama yake na Magreth yeye mama yake na magreth hakuwepo. Baada ya wazazi wa mama yake na Magreth kuuawa. Mama yake na Magrethalitoroshwa na babu yake hadi kijiji cha mbali na kwenda kuifadhiwa huko. Alikaa huko hadi akajifungua Mtoto ambaye ndio alikuwa Magreth huyu aliyouawa hapa. Baada ya kupata mtoto mama yake na Magreth alipanga mpango kulipiza kisasi kwa Masanja kufukuzwa upadri. Lile waliweza kufanikiwa lakini liliwapa matatizo mengi sana kwani siku hiyo hiyo mama yake na Magreth aliuawa na baba yako masanja. Kisha baba yako aliamrisha mwanae ambae ni Magreth kuchomwa sindano ya Sumu ambayo itapoteza kumbukumbu yake na kwenda kuuzwa brazil. Sasa baada ya mageth kufanyiwa vile na mpango ukafanikiwa baba yako alikosana na yule mzungu wa kike ambae alimchukua magreth kwa kumdhurumu pesa ndipo yule mzungu aliamua kumtibu magreth kurudisha fahamu zake ili kuweza kujakulipiza kisasi kwa baba yako
kiufupi tu ndio hivyo ndio maana hata Magreth visasi alianza kulipiza kwenye shule ya seminary maana hata mtu aliyemfanyia unyama wa kumchoma sindano ya sumu alikuwa ni mtu mkubwa ya shule ile. Pia baba yako ndio amemuua mama yangu na baba yangu. Ile siku uliyeniletea zawadi ulibeba kichwa cha mama yangu bila wewe kujua”Nilimweleza klinita kwa uharaka wa hali ya juu maana hata yeye alikuwa na wasiwasi. Kwa maelezo yale tu mafupi Klinita alishanielewa na kutambua ubaya wa baba yake. Hii niliweza kubainisha kutokana na machozi ambayo yalikuwa yanamtoka. “Nitawasadia mtatoka salama hapa ingawa nilishawaambia kuwa msaada ambae nitautoa mimi utakuwa siyo mzuri. Sina njia nyingine ya kuwatoa hapa zaidi ya ile ya baba ya nyinyi kukubali kuwa mumemuua Magreth ili muweze kutoka salama. Nimekuja huku kwa Haraka maana nimemsikia baba yangu akiwa anapanga kabsa sehemu ya kuwapeleka kwenda kuwauwa. Hivyo mimi nitafanya kila mbinu kwenda kumshawishi baba yangu awabebeshe kesi ya Kumuua Magreth”Aliongea Klinita.
Sehemu Ya 27
Kwa kweli yale Maneno ya Klinita yalinipa wasiwasi kidogo maana kama baba yake tayari alikuwa ameshapanga kutuua sisi ilikuwa vigumu yeye kumshawishi aweze kumsikiliza mwanae maana baba yake na Klinita kwa kweli hakuwa mtu wa mchezo mchezo. “Klinita Mpenzi wangu sitaki nikupoteze mimi kabla ya mimi kupotea.
Ninachokuomba nataka mimi kwenye hii dunia niwe wakwanza kuondoka ila isiwe wewe wakwanza. Naongea Hivi kwa sababu haya ambayo unataka kuyafanya yanaweza yakawa na Msaada mkubwa sana kwangu na yakakuletea matatizo ambayo yanaweza kughalimu maisha yako kabsa. Hivyo fanya vitu kwa akili sana na isizidi uwezo wako wa kufikili maana Ukifanya vikazidi uwezo wako wa kufikili kitakachofata ni kukupoteza wewe. Labda Klinita nikwambie kitu kimoja ambacho hukijui kutoka kwa baba yako. Baba yako hana Huruma kabsa na pindi anapoona mtoto wake anaenda tofauti na yeye anavyotaka hashindwi kumfanyia kitu kibaya. Magreth ingawa alikuwa mtoto wake wa kumzaa lakini alimbaka kisha kumuamlisha Mzee jonasi kumchoma sindano ya kumpotezea Kumbukumbu kisha kumuuza kwa mzungu ili akafanyiwe biashara ya Ukahaba na wala hakumkosea itakuwa wewe ambaye utakuwa umemkosea kabsa. So nenda fanya kile ambacho unahisi hakitakuletea matatizo kwenye maisha yako zaidi ya hapo naomba usifanye kitu kingine”Yalikuwa ni Maneno ambayo nilimwambia Klinita ili kumsisitizia maana Mtu ambaye alikuwa anaenda kumshawishi kutusamehe alikuwa siyo wa kawaida. Baada ya Kuongea yale Maneno Klinita alitoka kwenye kile chumba kwa Haraka sana. Alipoondoka Klinita kwenye kile chumba nilimwita yule mzee ili kumuulizia kama kuna Njia nyingine ambayo inaweza kututoa kwenye kile chumba. Mwanzo sikuwa nachachalika kabsa kuhusu kutoka kwenye kile chumba. Ila baada ya kusikia kama Masanja anapanga mbinu ya kutuua ndio nilianza kuchacharuka. Sikuwa naogopa kufa hata kidogo kwa Muda ule ila pia sikutaka kufa kwa Muda ule maana nilikuwa na Jukumu kubwa ambalo nilitakiwa kulifanya Dunia kabla ya kufa. Jukumu la kwanza ambalo nilitakiwa kufanya ni kulipiza kisasi cha kifo cha mama yangu na baba yangu ambaye mfanyaji mkuu alikuwa masanja. Kitendo cha Masanja kumuua mama yangu kwa kumkata shingo kisha kichwa kunitumia mimi kama zawadi ndicho ambacho kilikuwa kinanipa wazimu kila nilipokuwa nakumbuka. Bora kifo cha baba yangu nilisimuliwa tu pia unyama aliofanyiwa Magreth nao nilisimuliwa hivyo maumivu yalikuwa siyo kama yale ambayo nilikuwa nimeyapata kutokana na kifo cha mama yangu. Nilipomuuliza yule mzee kama kuna njia nyinge ya kutoka pale kwenye kile chumba kisha kuambiwa hakuna ndio nilizidi kuchoka zaidi. “Sam Najua utakuwa unawaza Kufanya mambo mengi sana kwa huyu Mwanaharamu Masanja. Ila nachokuomba Muda huu hauna uwezo kabsa wa kupambana na huyu mtu. Wakati naondoka Blazil mama yangu alinituma kuja kumwambia Magreth afanye haraka amuue Masanja kabla yeye hajafa maana alikuwa anamwamini maana alipitia mafunzo makali. Pia mama yangu aliniambia kama Magreth atafeli kumuua Masanja basi mimi nisithubutu kufanya kitu chochote maana Masanja siyo mtu wa kawaida kabsa. Sam ambacho nakuomba sasa hivi usikurupuke kufanya kitu chochote maana tutakufa kitu ambacho mimi sitaki kutokea. Mimi siyo kwamba kisasi nataka kulipiza kwa ajili ya kifo cha Magreth tu hapana. Kuna kitu kikubwa sana ambacho wewe hukijui Kwa nini Mama yangu Cutherbet alimtuma Magreth kuja kummaliza Masanja. Najua Magreth alikwambia tu kuwa Ametumwa kuja kumuua Masanja kama kulipiza kisasi chake pia Kumlipizia mama yangu kisasi kwa kuwa alidhurumiwa pesa. Mama yangu anapesa nyingi sana hivyo asingekaa kuwaza kulipiza kisasi kwa mtu hatari kama masanja et kisa tu kudhurumiwa pesa. Sasa siyo hayo tu lipo jingine kubwa ambalo ndio hata mimi lilinitoa Brazil kuacha kazi ili kuja kushuhudia kifo cha Masanja. Labda ngoja nikupe Mdokezo kidogo ili ujue ni kiasi gani tunatakiwa kubaki wazima ili kuweza kulipiza kisasi kwa Masanja. Baada ya Mama yangu kudhurumiwa pesa na Mchungaji masanja kwa kweli hasira zilimbana sana Baba yangu na kuamua kusafiri kuja hadi Tanzania kumuonya masanja alipe pesa. Kwa kuwa baba yangu alikuwa ananipenda sana na kila kitu ambacho kilikuwa kinafanyika alikuwa anataka mwanae nishuhudie aliamua kusafiri namimi pamoja na walinzi wake watatu. Alipokuja Tanzania baba yangu naye wala hakupoteza Muda siku hiyo hiyo ambaye alienda kumuonya masanja usiku huohuo aliuawa mbele yangu na alikatwa kichwa kabsa na mimi nilipewa kichwa cha baba yangu nimpelekee mama yangu kama wewe ulivyopewa kichwa cha mama yako. Sema Masanja amenisahau tu maana kipindi nimekuja nilikuwa na umri mdogo sana. Hivyo mimi ninahasira sana na huyu Mtu ndio maana nashindwa hata kuongea. Ila point tunatakiwa kumuomba Mungu tutoke wazima hapa”Aliongea Mzungu matonya kwa lugha yakiswahi kilichoenda shule utafikilia alikuwa Mbongo.
Kiswahili ambacho aliongea Matonya kwa kweli kilikuwa kinaeleweka vizuri sana hali ambayo ilinifanya kunishitua kidogo. Ingawa kiswahili chake kiliambatana na Lafudhi ya Kizungu lakini alionekana ni mtu ambaye alikuwa anaongea sana kiswahili hali ambayo ilinifanya kushindwa kuvumilia na Kumuuliza hii lugha yeye ameifahamia wapi. “Sam kuna mambo mengi sana nimepitia mimi tena kwenye hii hii nchi ya Tanzania na ukitaka kuyajua hutayamaliza maana kwanza hatuna muda wa kuyakumbuka haya ila tunamuda wa kujadili ni namna gani tutatoka salama humu. Mimi kiswahili nilifahamia hapa Hapa Tanzania tena Magerezani nilifungwa. Ninaposema nataka kumuua Masanja ninahasira naye ndio maana navunja hata baadhi ya Amri za mungu kwa Mpumbavu mmoja. Baada ya Masanja kumuua baba yangu na walinzi na kuwatoa vichwa na kunipa mimi aliniambia niondoke. Kwa kuwa nilikuwa nampenda sana baba yangu kweli niliamua kubeba vile vichwa ili kupanga namna ya kusafiri navyo au kwenda kuvizika mahali pazuri. Nilipotoka Pale Kwa Masanja wala haikunichukua hata Dakika kumi nilishangaa Gari ya Polisi inakuja kusimama na polisi waliniambia kuwa wanawasiwasi na mimi wamepata taarifa kwa wasamalia wema kuwa mimi nimehusika na mauaji ya watu wanne kisha vichwa vyao nimevibeba. Yale maneno ya polisi yalinishitua maana kweli nilikuwa na vile vichwa. Waliponikagua kweli walivikuta na walinipeleka Kituoni. Baada ya wiki Mbili nilihukumiwa kifungo cha maisha jela na kilishonishangaza sikupewa uhamisho wa kwenda kufungwa nyumbani kwetu na ilisemekana ni ni raia wa Tanzania hali iliyonifanya kugundua kuwa Masanja kanichezea game. Hivyo kiswahili mimi nimejifunzia jela Naomba tuishie hapa Sam sitaki uniulize tena kama nilifungwa Kifungo cha Maisha nilitokaje jela maana hiyo ni Story ndefu sana”Yalikuwa ni Majibu ambayo alinipa Matonya na sikuwa na swali tena kuhusu kiswahili amefahamia wapi. Kwa maelezo mafupi tu ambayo alinipa Matonya nikajumlisha maelezo aliyonipa Magreth na yote yalikuwa yanahusu unyama wa masanja kweli nilijiona kupambana na Masanja sitaweza na nilitamani kuacha kabsa hata kulipiza kisasi maana nilikuwa kama nakitamani kifo hivi. Wakati nikiwa natafakali maneno ambayo aliniambia Matonya mlango wa chumba ambacho tulikuwepo ulianza kugongwa. Kama kawaida maana ilibidiniende kufungua maana chumba ambacho tulikuwepo ilikuwa chumba ndani ya chumba. Yani chumba kilikuwa kikubwa sana ambacho kilikuwa hadi na watumishi lakini ndani ya kile chumba kulikuwa na chumba kingine ambacho ndio tulikuwa tunakaa kule. Nilipoenda kufungua kwa kweli Moyo wangu uliruka sana nilipoona mtu ambaye alikuwa anaingia Mle alikuwa masanja huku wakiwa na watu ambae walikuwa wamejazia sana. “Nimefikilia sana kuwafunga lakini nimeona kama nitakuwa naongeza uadui tu. Maana najua mnavisasi na mimi na mnauwezo wa kutoroka hata jela na kuja kutaka kuniua. Ingawa najua hakuna mtu ambaye ataniua mimi ila kujihami lazima. Hivyo kitu ambacho nimekiamua mimi ni kuwaua nyinyi ili mfatane na magreth. Ila wewe Sam naomba umsalimie Sana mama yako na mwambie nimemisi sana na kifo chake ambacho nilimuua kwa kumkata shingo nakiota kila siku ndotoni. Pia wewe mzungu Mjinga utamsalimia Sana Mwanangu Magreth mwambie baba yake nimemisi sana maana nakumbuka ile siku ambaye nilimtoa usichana wake alikuwa analia sana.
Pia mnatakiwa muwahi huko mkaamulie maana najua kutakuwa na Ugomvi mkali kati ya Mwanangu magreth na Mzee Jonasi maana yeye ndio alimchomaga sindano ya sumu. Sasa mtatoka hapa kwenye nyumba yangu tukufu na nitawapeleke kwenye makazi yangu ambae ni bucha ya kuchinjia watu wajinga kama nyinyi”Yalikuwa ni maneno ambayo aliongea Masanja kwa mapozi ya hali juu sana.
Sehemu Ya 28
Yale maneno ambayo aliongea Masanja kwa kweli yalinifanya kujisikia vibaya sana na kujilaumu kwa nini tulikubali kizembe kizembe kumsindikiza Magreth kuja kumuua Masanja hatimae amefanya Makosa makubwa sana ambaye wote sasa tunaenda kufa na kumuacha adui yetu anaendelea kutamba Duniani. “Masanja kabla ya kutaka kuniua nataka nikuulize ni kweli unauwezo huo. Mimi nahisi unatuogopa sana ndio maana hata kutuua unatuzungusha sana hadi utupeleke mafichoni. Wewe kama kweli muuaji hatari kwa nini unamuogopa Mwanao. Kama kweli Gangstar hebu tuue wote hapa haina haja ya kutupeleka sehemu nyingine”Nilimwambia Masanja huku nikiwa nimemkazia Macho. Nilichokuwa nataka muda huo ni kuweza kumchelewesha kidogo masanja ili asitutoe mle huenda tukapata masaada maana Klinita alituhaidi kuwa anatusaidia. Hivyo kama tungeondolewa tu kwenye ile nyumba tutakuwa na wakati Mgumu sana maana Klinita wala asingetuona. “Wewe kijana kumbe ni Mjinga na akili zako zinafanana na baba yako vilevile. Yani leo nimesibitisha kuwa siku zote mtoto wa chura nichura tu wala hata siku moja hawezi kubadilika kuwa mtoto wa papa. Inamaana wewe mjinga unataka kuniambia kuwa mimi nashindwa kukuua hapa na naogopa sana hadi nikusafirishe kwenda mbali. Sasa ili nikuonyeshe kama Masanja anaweza kufanya kitu mahali popote bila kuwaza nakuua hapa hapa namaiti yako sitaibeba bali Masikini Police ndio watakuja kukutoa hapa”Aliongea
Masanja kisha alisogea hatua tatu kurudi nyuma kisha alitoa Mguu wake wa kuku tayari kwa kutaka kunitoa dunia. nilipoona bastora kwa kweli sikumbuki jasho lilitoka wapi ambacho niliona uso tu umebadilika na kitu kama maji yakiwa yanatiririka. Woga ambao ulinikumba ulikuwa wa aina yake na hakuna siku ambayo niliogopa kama hiyo siku. Kifo bhana kisikie tu ila kamwe usikwepo kwenye tageti ya kifo hata siku moja. Kwa muda ule ambae Masanja alikuwa amekoki bastora yake huku akijiandaa kuifyatua nilikuwa nawaza neno tamu fupi lakuongea ambalo litamfanya masanja kurudisha Bunduki yake mfukoni lakini sikuwa naliona kabsa. “Hapana baba hurusiwi kufanya hivyo maana wewe ni mtu wa Mungu na Mungu anatukataza kufanya hivyo. Baba najua hawa wamekukosea sana na hata Magreth umemuua kwa kuwa ulikuwa unajilinda. Baba hawa naomba usiwauwe maana utapata dhambi kubwa sana. Ili hawa dunia iwahangaishe wabebeshe kesi ya kumuua Magreth na mimi nitakuwa mstari wa mbele kukusaidia kama watakataa hii offa ambayo utawapa ndio uwaue”Yalikuwa ni Maneno ya Klinita akiongea mara tu alipoingia chumba ambacho tulikuwepo. Masanja alipomuona mwanae kaingia kwenye kile chumba huku akiongea yale maneno alionekana kunyongonyea sana na kurudisha bastora yake kiunoni hali iliyonifanya masanja hataki mwanae ajue unyama ambae anafanya. “Mwanangu nimekusikia na nitafanya kile ambacho wewe unataka ila hawa watu wakikaidi tu kile ambacho nitawaambia nitawaua kabsa. Nikiwaacha bila kuwafunga hawa maisha yangu yatakuwa matatani sana maana watanisaka tena ili wanimalize sijui nani anawatuma. Lakini Mwanangu umejuaje kama mimi nipo kwenye hiki chumba na mimi mbona nilikukataza kuingia vyumba kama hivi”Aliongea Mzee Masanja. Maneno ya Mzee Masanja kwa kweli yalinifanya kupumua pumzi ndefu sana maana ilikuwa hafadhali kufungwa maana ipo siku nitatoka ila siyo kufa wakati bado sijafanya kile ambacho nilimuhaidi mama yangu wakati nazika kichwa chake pia bado nilikuwa sijafanya yale ambao aliniagiza magreth kabla ya kifo chake. “Baba naomba unisamehe kwa kuingia huku wakati ulikuwa umenizuia.ila baba nilipoona mimi unawatu wenye nguvu kama hawa wanaingia huku nilijua tu kuna kitu kibaya ambacho ulikuwa unawaza kufanya ndio maana nikaamua kuja kukukumbusha usifanye hivyo maana ni vibaya sana”Aliongea Klinita maneno ambayo yalimfanya baba yake kutikisa kichwa cha kukubaliana na yeye. “Sasa nyie wendawazimu Mungu bado alikuwa hajapanga nyinyi kufa na mnatakiwa kumshukuru sana mwanangu. Sasa ili kifo kiendelee kuwakosa mnatakiwa kukubaliana na mimi kwa hiki ambacho nitakisema. nitawatoa hapa hadi nje ambae kuna Gari lenu tayari nimeshalileta hadi hapa. Kwenye hilo gali nitafunga Bom ambalo nitakuwa nalimoti pia kwenye hilo gari kutakuwepo kichwa cha mzee Jonasi, kichwa cha mama yako maana wakati unakizika mimi nilienda kukitoa pia utakuwepo mwili wa magreth. Hivyo nyinyi mtapanda kwenye hilo Gari na kwenda mbali kidogo ambapo mimi nitaenda kusimama sehemu mbali na nyie na nitawapigia police kuwa kunawatu wanavichwa vya binadamu alafu mtakuja kukamatwa. Sasa mkipanda kwenye lile gari sitaki kuona mtu yeyote anashika hata mlango wa gari Ukigusa tu nalipua pia kwenye hii gari naweka microchip ambazo zitanifanya kusikia kile ambacho mtakuwa mnaongea na wale afande ambapo mtakamatwa mkipindisha tu sijui mnataka kutaja jina langu nawalipua pia”Aliongea Masanja.
************************************************************************** Kwa kweli maneno ambayo aliongea Masanja yalinishitua mbaya. Kwanza maelezo tu aliyotoa ilikuwa ya aina yake alafu bado anasema tena kuna kichwa cha Mama yangu kitakuwepo mle. Moyo wangu kwa kweli ulianza kuuma na kujikuta machozi yenyewe yananitoka. Yani Masanja pamoja na kumuua mama yangu kwa kumkata kichwa kisha akaniletea mimi kile kichwa na kukienda kukizika lakini bado alienda kukichimbua na kukiweka sehemu nyingine. Kwa kweli katika vitu ambavyo vilinitoa machozi katika maisha yangu ni ile hali. “Masanja kama kweli kichwa cha mama yangu kitakuwepo kwenye lile gari mimi kwa kweli siwezi kukusumbua tena nitaingia kwenye gari na kufanya kile ambacho wewe unakitaka. Ila wakati nafanya hili Jambo naomba unihaidi kitu kimoja kuwa mimi nikikamatwa na Police naomba kichwa cha mama yangu kikazikwe kwenye kaburi ambalo alizikwa mama yangu. Naomba sana hiki kichwa kisiendelee kukaa sehemu kama vile makumbusha ya kale. Pia Masanja naenda Jela kabsa ila jua nitarudi kumuoa Mwanao pia ningependa wakati naenda kumuoa mwanae huku wewe ukiwa unakata roho bila kupenda maana kabla ya Magreth kufa aliniambia kuwa mama yake alitaka wewe ufe huku ukiwa bado na hamu ya kuendelea kuishi duniani”Yalikuwa ni
Maneno ambayo yalikuwa yanatoka Mdomoni kwangu huku machozi yakiwa yananitoka. Kwa kwa kweli Muda ule nilikuwa na hasira ambazo zilikuwa hazipimika na hasira ambazo nilikuwa nazo ningeshikiwa Mzee Masanja na mtu kisha niambiwe nimuhukumu pale pale nilikuwa sina hukumu nyingine zaidi ya kuutafuna mwili wake kama nyama ya mbuzi iliyorostiwa. Maana kupiga ningehisi wala nisingeonea. “Hahaha Kijana naona unajidanganya sana kuna mambo nilikuwa naogopa kukwambia mwanangu alikuwa karibu. Hivyo kwa kuwa Mwanangu ameshatoka labda ngoja nikwambie ukweli. Wengi sana waliongea maneno kama yako lakini hakuna ambaye alitekeleza hata Mmoja mimi ndio Masanja ambae nafanya kila ninachotaka hapa Duniani na Hakuna ambaye ananihukumu. Labda ombi ambalo umeniomba nitetekeleza maana ukikamtwa kichwa cha mama yako kitachukuliwa na Police hivyo lazima wakakizike. Naomba kijana acha maneno yako kijinga ongoza twende kwenye Gari nisije kupasua Kichwa chako”Aliongea Masanja baada ya Mwanae kutoka Nje. Masanja aliposema tutoke nje wala hatukuwa na Ubishi. Tulitoka hadi Nje na Kukuta Gari ambayo tulikuwa tunatumia kweli ipo kwa Mzee Masanja wakati tulikuwa tumeiacha nyumba. Nilipanda mimi kwenye gari kisha Matonya nae alipanda kisha Masanja alienda kupandakwenye gari nyingine. Masanja alipopanda kwenye ile gari aliongea akiwa ndani ya gari yake na sisi kweli tulisikia alichokuwa anakiongea kupitia Micro chip ambazo alitegesha kwenye gari. Pia kwa mbele pia nilipoangalia vizuri baada ya masanja kunielekeza nilikuta kweli kuna Boom ambalo lilikuwa limetegeshwa tayari. “Naomba muwashe Gari wewe sam mwelekeze huyo Mzungu mwenzako hadi sehemu ile nilipokupigia simu wakati ulipofungua boksi ambalo lilikuwa kichwa cha mama yako kama zawadi na mimi nawafatilia kwa nyuma.”Aliongea Masanja na sisi tulikuwa tunamsikiliza kwa Micro chip. Matonya aliposikia Maneno ya Masanja aliwasha gari na safari ilianza. Kutoka Nyumbani kwa masanja Safari ilianzishwa ya kwenda eneo lile ambalo nilikuwa napenda sana kukutana na Klinita maana ilikuwa nje kidogo ya Manispaa ya Tabora. Mwendo kama wa dakika kumi na tano tayari tulikuwa tumeshafika kwenye lile eneo. Masanja naye gari yake nilikuwa naiona kupitia kioo ambaye alipaki mbali. Kwenye lile eneo tulisimama kama muda wa dakika tano tu ghafla nilianza kusikia Ving’ora vya gari la polisi bila shaka walishapewa taarifa
Kwa kweli kitendo cha kusikia gari za polisi zinakuja huku zikipiga ving’ora vya kutisha ndio hofu ya Kukamatwa ilizidi kuongezeka. “Sam inabidi tutoroke hawa Polisi wasitukamate. Hii kesi Sam tukikamatwa unafikilia kuna kupona kweli lazima tutafungwa Maisha na kushindwa kufanya kile ambacho wewe na mimi tunataka kukifanya. Sam wewe unajua unalipa visasi vya watu wengi sana hadi sasa na hakuna mtu ambaye utampa Jukumu la Kulipa kisasi kama utashindwa kutoroka. magreth kabla ya kufa alishapata watu wa kumsaidia kulipa Kisasi. Sasa sisi tukifa unafikili nani ambaye ataweza kufanya kitu kama hicho”Aliongea Matonya huku akiwa amechanganyikiwa mbaya. Hapo kweli niligundua Mzungu alikuwa amechanganyikiwa kweli maana alishasahau hata yale maneno ambayo alikuwa anaongea Masanja alikuwa anayasikia kupitia Micro chip na ilikuwa hatari sana kwa maisha yetu maana angelipua boom. “Wewe Mzungu unataka kuleta balaa gani hapo. Hivi umesahau tulivyokubaliana kuwa mnatakiwa kukamatwa na Polisi kuliko kufa. Sasa utaamua wewe ufe kwa mimi kulipua Bom pindi utakapotaka kutoroka au ukamatwe na Polisi ukafungwe Jela”Aliongea Masanja kwa Sauti ya Nyodo. Wakati Maongezi yote hayo yanendelea tayari Gari za polisi zilishakaribia sehemu ile ambayo tulikuwepo. Idadi ya Gari ambazo zilikuwa zinakuja kwa kweli zilikuwa nyingi sana huenda polisi waliposikia kama ndio wauji wa kutisha ambao waliwakata shingo mzee Jonasi na mama yangu waliogopa sana maana Hakuna vifo vya kutisha kama vile ambavyo vilikuwa vimetokea tabora. Kwanza vifo vile vilitikisa nchi nzima. “Sam tunatakiwa tusife kijinga mimi ni Mtaalamu wa Mabom sana hivyo Humu hakuna Mtu ambaye ametega bom hata kidogo. Pindi tu nilipopanda kwenye Hili Gari nilianza kuchunguza hili boom lakini nimegundua siyo boom original ambalo linaweza kulipuka. Sasa kama wewe unaamini boom mimi nakurusha ili masanja kama atalipua nife mimi ili mmoja abaki kulipiza kisasi maana hatuwezi kufa kizembe. Pia kama halitalipuka na mimi nitakamatwa na polisi wewe ndio utakuwa Msaada mkubwa wa kuhakikisha natoroka gerezani maana siyo kusema kunitoa. Nauhakika nikikamatwa mimi nitafungwa tu kifungo cha maisha”Aliongea Tena Mzungu kwa haraka sana na kipindi anamalizia kuongea maneno yake tayari alishafungua mlango kwa kasi ya ajabu alinisukuma. Kwa kuwa alinisukuma bila mimi
kujiandaa hakupata upinzani kutoka kwangu hivyo nilienda kuanguka nje ya gari. Nilipoanguka nje niliamka kwa kasi ya ajabu na akili zangu zilishahama kabsa maana niliamini kwa Asilimia mia lazima huo ndio utakuwa mwisho wa kumuona Mzungu tena hivyo macho yangu yalikuwa kuangalia Gari jinsi ambavyo litalipuka. Nilishajisahau kabsa kama Mzungu amenisukuma vile ili niweze kukimbia. Cha ajabu hata Mzungu aliponisukuma na kutua nje bado gari haikulipuka. Wakati nashangaa ile hali nilimuona Mzungu akichomoka na yeye kwenye gari kisha alitoka nduki bila hata kunisemesha. Nilipoona Matanya na yeye kachoma kwenye gari na kutimua mbio ndio kumbukumbu na mimi zilinijia na kukumbuka kama kuna kesi ya ajabu tunatakiwa kubebeshwa. Niligeuka kwa kasi na kuiangalia njia kisha mbio ilianza. Wakati natimua mbio nilianza kusikia milioa ya Risasi huku sauti ya kutuamrisha tusimame ikitawala. Nilipoisikia ile sauti ni kama ilinipa mzuka wa kukimbia zaidi maana sikutaka kabsa kukamatwa na Polisi. Wakati nikiwa nakimbia nilihisi kitu cha baridi kikipenya kwenye Mguu wangu hali iliyonifanya nianguke chini kama mzigo. Nilipoanguka chini kwa kasi ya ajabu nilitaka kuamka kuendelea kukimbia lakini Mguu wangu wa kushoto nilihisi hauna Nguvu. Ilibidi niangalia kuna nini kimefanya niwe vile. Nilipoangalia ndipo moyo wangu ulishituka zaidi maana nilikutana na Damu inatoka mbaya bila shaka nilikuwa nimepigwa Risasi. Pamoja na kujikuta nipo vile sikutaka kukata tamaa. Nilijitaidi nikaamka vile vile na kuanza kukimbia kwa Mguu mmoja. Ile haikuwa kukimbia tena bali ilikuwa kurukaruka. Kwa hali ile sikuweza hata kufika mbali polisi wakanikamata.
Kwa kweli kitendo cha mimi kukamatwa na Polisi kiliniuma Sana na kuamini sasa kazi ya kulipa kisasi inazidi kuwa Ngumu. Ingawa wakati tunatoka kwa Masanja nilikubali kukamatwa na Polisi ili tusiuawe kama Masanja alivyosema ila kwa Muda ule sikupenda tukio kama lile litokee.
Sehemu Ya 29
Polisi waliponikamata kwanza nilianza kuambulia kichapo cha kuwasumbua. Yani hawakujali hata kama wamenipiga Risasi Mguuni wao waliponifikia kilifuata kipigo takatifu sana. Hawakuwa wanachagua watumie nini kunipigia walikuwa wanachanganya wengine walikuwa wanatumia lungu wengine makofi yani walikuwa wamenisakama sana. Maneno ambayo nilikuwa nasema kuwa siyo mimi niliyofanya hilo tukio huenda ndio yalizidi kuwapa hasira na kuzidi kunidunda zaidi. Maana walichokuwa wanahisi wao haiwezekani nikawa na mwili pamoja na vichwa vya watu kwenye gari alafu niseme siyo mimi nimefanya lile tukio. Wao hawakujua kama kuna mchezo ambao ulikuwa umechezwa na Mzee Masanja. Kipigo kiliendelea pale kama cha muda wa dakika tatu tayari nilikuwa nimeshatapakaa damu sasa maana damu ilikuwa inanitoka mguuni ambapo nilikuwa nimepigwa Risasi na nyingine puani na Mdomoni ambayo ilitokana na kipigo cha Makofi ambacho nilikuwa nalipata kutoka kwa wale Afande. Afande walipolizika na kichapo ambacho walikuwa wanakitoa kwangu yani wakahakikisha nimechoka ndipo walinibeba kwenda kunipakia kwenye Defenda kupelekwa hospitali ya Mkoa wa Tabora Kitete kwa ajili ya Matibabu kabla ya kupelekwa kituoni maana hali yangu ilizidi kuwa mbaya kutokana na damu ambazo zilikuwa zinanitoka. Wakati wakiwa wananibeba moyoni nilikuwa naomba kwa Mungu matonya awe ametoroka maana nilihisi ndio atakuwa msaada mkubwa kwangu. Kile ambacho nilikuwa nakiomba nahisi Hakikufanyikiwa maana Hazikupita hata dakika mbili tangu nipakiwe kwenye Gari matonya nae nilimuona akiletwa huku akiwa ametapakaa damu hafadhali ya mimi. “Jamani hakuna kitu kibaya ambacho tumekifanya sisi naomba tusikilizeni kwanza mtatuelewa na mtu ambaye amefanya hili tukio mumkamate”Yalikuwa ni maneno ambayo alikuwa anaongea Matonya huku damu zikiwa zinamtoka mdomoni na puani na kushuka kwenye shati lake maana hakuwa na uwezo wa kuzizuia maana tayari mikono yake alifungwa pingu. Maneno ya Matonya hakuna afande ambaye alimsikiliza zaidi ya kuongezewa vibao na kuambiwa hayo maelezo ataenda kutoa Kituoni. Baada ya Matonya kupakiwa Defender iliondoka kwa kasi kuelekea Tabora Mjini kupelekwa hospitalini. Kutoka Sehemu ambayo Tukio lilitokea hadi tabora mjini kulikuwa na umbali kidogo. Kwa Gari ilichukua kama Muda wa Dakika kumi na saba ndio tulifika. Tulipofika Tabora Mjini tulipelekwa kwanza Kituo cha polisi cha line polisi hapo Tabora mji vikatolewa vibari kisha tulipelekwa Hospitali ya kiteto kwenda kutibiwa huku tukiwa kwenye Ulinzi Mkali wa Polisi. Pale Hospitalini Matibabu yaliendelea kwangu kwa Muda kama wa wiki moja ili kuhakikisha kidonda ambacho nilipigwa Risasi mguuni kinaonyesha dalili ya kupona ndio niruhusiwe. Uzuri ile risasi kwa kweli iliweza kupiga nyama na haikuwa na nguvu sana hivyo haikuweza kudhuru mifupa. Mwenzangu siku ile ile tulipofikishwa alitibiwa na kurusiwa na alipelekwa Polisi huko sikujua alikuwa amepelekwa kituo gani cha polisi. Baada ya wiki kwisha tayari nilishapona Mguu wangu na kuweza kutembea ingawa ilikuwa kwa shida sana. Nakumbuka ilikuwa siku ya Juma Mosi nikiwa nimetulia Kitandani Hospitalini nikiwa nasubilia Hurusa kutoka kwa Dactari ili niweze kutolewa hospitalini na kupelekwa kituoa cha polisi tena. Nikiwa pale mgeni mmoja ambaye alikuwa ni Muhimu sana kwangu aliingia. Nilipomuona yule Mgeni kwa kweli nilishituka sana maana sikutaka kumuona akija pale. Huyu Mgeni hakuwa Mwingine bali ni Klinita. Klinita alipoingia na kuniona alishindwa kujizuia na kunikimbilia Kuja kunikumbatia huku machozi yakiwa yanamtoka. “Sam Najua upo kwenye wakati Mgumu sana ila vumilia utatoka tu. Huu wakati Mgumu unaopitia ni moja ya Mipango ya Mungu hivyo yeye mwenyewe ndio atakusafishia kwa kila kitu. Usiwe na wasiwasi kabsa utatoka Salama wala hautofungwa na utafanya kile ambacho dada yangu alikuagiza kabla ya kufa” aliongea Klinita kwa uchungu huku akiwa analia. “Klinita kama unanipenda naomba iwe mara yako ya mwisho kuja hapa. Namjua baba yako ni mtu ambaye hana huruma hata kidogo kama atagundua kuwa unakuja kuniona hapa anaweza kukufanyia kitu kibaya sana ambacho kitanifanya nikukose duniani.
Hebu fikilia kama baba yako aliweza kumbaka mwanae Magreth ambaye hakumkosea kisha kumpeleka Brazil kumuuza na baadae kufanikiwa kumuua wewe unafikili anashindwa kukufanyia unyama zaidi. Nakupenda sana klinita sitaki nikukose kabsa hivyo kwa sasa kaa mbali na mimi”Nilimwambia Klinita.
Sehemu Ya 30
Kwa kweli yale maneno ambayo nilimwambia Klinita ni kama yalimuongezea huzuni na kuzidi kulia zaidi. “Sam Najua kama baba yangu ni mtu mbaya sana lakini Kamwe siwezi kukaa mbali na wewe. Sam nipo tayari kupoteza maisha ila siyo kuwa mbali na wewe. Nazani unafahamu na unakumbuka vizuri kuwa niliacha kusomea Usister kwa ajili yako wewe lengo niwe karibu na wewe leo utaniambiaje nikae mbali kisa baba yangu. Kiufupi Sam labda elewa tu kamwe siwezi kukaa mbali hata siku moja kwa mtu ambaye nampenda kama wewe. Nakupenda Sam na nipo tayari kufanya kila kitu kwa ajili yako wewe hata kile ambacho kitasababisha maisha yangu kupotea nipo tayari”Aliongea Klinita huku Muda ule tayari alishafuta Machozi ambayo yalikuwa yanamtoka na kuongea kwa Usiliasi wa hali ya juu. Maneno ambayo alikuwa anaongea Klinita mimi nilibaini kuwa hatanii hata kidogo maana Klinita mimi nilikuwa namjua. “Nimekuelewa Klinita tena nimekuelewa sana. Klinita nimekwambia usinifatilie sana kwa kuwa wewe kuwa hai ndio furaha yangu hapa Duniani. Mama yangu na baba yangu wamekufa nimebakiwa na wewe tu wa kunifariji sasa na wewe ukifa utafikili nitabaki na nani. Klinita Nahitaji uwe nuru katika maisha yangu hasa kwenye mitihani migumu kama hii. Hivyo kwa sasahivi wewe ndio umetuokoa kwenye kifo cha kuchinjwa na kuja jela hivyo subilia uone hukumu yetu ndio utaanza kutoa Msaada tena”Nilimwambia Klinita. Kwa maneno yale Machache ambayo nilimwambia Klinita kidogo alinielewa. Klinita alinisogelea na kuja kunipiga busu la Mdomoni ambalo lilifanya Mwili wangu kushituka kama nimegusa waya wa Umeme. Baadae Klinita ilibidi aondoke na kuniacha pale Hopstalini nikisumbilia kutolewa. Muda wa Saa sita Machana Dactari ambaye alikuwa anahusika kunitibu mimi Aliniruhusu nakutolewa Hospitalini ili nipelekwe kituo cha Polisi. Nilipotolewa Hospitalini kwa kweli nje nilishangaa nilikutana na watu wengi sana ambae sikujua walikuja kufanya nini. “Alafu jamaa mwenyewe ukimwangalia hafananii kabsa na matendo ambayo aliyafanya. Kwa kweli nimeamini pesa ni mwanaharamu na Ndugu yake ni shetani. Angalia kijana alivyo mzuri lakini huwezi amini huyu ndio ambae alikata kichwa cha mama yake pamoja na kichwa cha mzee wa kanisa mzee Jonasi kisha kumuua Sister Magreth lengo tu kusaka utajiri”Nilisikia Moja ya Maneno ambayo kijana mmoja alikuwa anaongea na mzee Flani. Yale Maneno ya yule kijana kwa kweli yaliniumiza mbaya na kupata picha kumbe wale watu walikuwa wamekusanyika ili kuja kumuona Jambazi ambaye alichinja watu wawili na kuwatoa vichwa mmoja akiwa mama yake. Sikuwa na kitu cha kujibu kwa muda ule kwa yale maneno ambayo nilikuwa nayasikia zaidi ya kumuomba Mungu anitoe kwenye wakati mgumu kama ule. Nilipanda Gari na Safari ilianza ya kuelekea kituo cha polisi . Hapo Polisi line niliandikishwa vitu ambavyo nilikuwa navyo kisha nilipelekwa Gerezani Uyui ambako niliwekwa Rumande Kusubilia Kesi ambayo ilikuwa inatukabili. Huko Gerezani kwa kweli nilipofika hadi nilitamani kulia maana Nilimuona na Mwenzangu Mzungu hali yake ndani ya wiki kama moja na sehemu alikuwa amekonda hadi anatia huruma. “Sam hafadhali Umekuja hivyo muda wa kuondoka nahisi umewadia. Kwa kesi hii tulionao hakuna haja hata ya kuisikiliza maana lazima tufungwe. Hivyo muda tulionao ni kutoroka Gerezani kitu ambacho nahisi kitakuwa cha hatari sana kwetu lakini hakuna jinsi. Tuna siku chache sana za kupanga namna ya kutoroka Hapa Gerezani hakuna haja ya Kusubilia kesi”Aliongea Matonya.
Maneno ya Matonya kusema kuwa tunatakiwa kutoroka Gerezani bila kusubilia kesi yetu kusomwa mimi nilimuunga Mkono. Nilikuwa najua jinsi Ugumu wa kesi jinsi ulivyo hivyo kufungwa ilikuwa Muhimu tu hali ambayo ingenikosesha mimi kulipa kisasi kwa Muda muafaka. Mwenyezimungu nilikuwa najua kabsa kama anapinga vikali mtu kuua ila Kwa Muda ule nilikuwa na Hamu ya kumuua Mchungaji masanja tena kifo cha kinyama sana. Kwa Jinsi ambavyo alimfanyia mama yangu kisha simulizi ambayo nilipewa na Magreth ukijumlisha na kifo cha Magreth mbele ya macho yetu nilitokea kumchukia Sana Masanja. Kwenye Lile Gereza uzuri tulikuwa tunalala chumba kimoja na Matonya. Chumba ambacho tulikuwa tunalala kilikuwa kizuri tu maana tulikuwa hatuchanganywi na Wafungwa wengine maana bado tulikuwa hatujafungwa tulikuwa Rumande kusubilia Kesi yatu. Ulinzi ambao Ulikuwa unatulinda sisi kwa kweli ulikuwa wa aina yake na kama Ungeendelea vile ilikuwa Vigumu sana kuweza kutoroka kwenye lile Gereza la Uyui. Kwa Muda ule prosses za kutoroka pale Gerezani zilikuwa zinaendelea kama kawaida maana uzuri mimi na Matonya tulikuwa tunalala chumba kimoja hivyo ilikuwa Rahisi kuweza kupangilia mambo yetu. Siku zilizidi kukatika pale Gerezani bila kupata nafasi kabsa ya kutoroka maana ulinzi ulikuwa Mkali sana. Tulikaa pale Gerezani kwa Muda wa mwezi mmoja na nusu bila Mafanikio hatimae siku ya kusikiliza kesi yetu ilifika. Hiyo Siku asubuh muda wa Saa nne ndio tulikuja kuchukuliwa. Hiyo Siku pili ndio tulipanga kutoroka hata kwa kuruka kutoka kwenye gari wakati tunapelekwa mahakamani gari ikiwa inakimbia. Ila hicho kitu tulipanga kitafanyika endapo askari ambao watakuwa wanatupeleka huko hawatakuwa wengi. Kwenye ile Defender Askali kwa kweli walikuwa wakutosha na wote walikuwa na siraha. Hata wakati tunapelekwa tulikuwa tumefungwa pingu na bado tulikalishwa chini ya Gari. Hadi pale kutoroka hiyo siku tulikuwa tumefeli. Tulifika Mahakamani muda wa saa nne asubuhi tulikuta watu wengi sana walikuwa wamerundikana lengo watuone sisi maana taarifa zilikuwa zimezagaa kuwa ni majambazi sugu. Tulipofika mahakamani tuliingizwa hadi ndani kisha bila kupoteza Muda hakimu alianza kusoma kesi zetu ambazo zote zilikuwa zinafanana. Hakimu alitusomea kesi kuwa tunahusika na Mauaji ya mama yangu pamoja na magreth na Mzee jonasi lengo kujipatia utajiri. Walikuwa na ushaidi kabsa kama walitukamata na vitu hivyo na bado vilikuwepo. Hakimu aliposema hata vitu vile bado vipo na viliwekwa kwenye Friji ili vikae kama ushaidi ndio niliumia zaidi. Kwa kweli kitendo cha kusikia hadi muda ule kichwa cha mama yangu bado kilikuwa kinazunguka kama pambo niliumia vibaya mno. Hakimu alipomaliza kusoma kesi yetu alitupa Muda wakuongea ambao ilikuwa kukubali au kupinga ile kesi. “Asante sana Hakimu Mtukufu kwa kunipa hii nafasi. Hakimu hata nikiongea neno gani nahisi itakuwa vigumu nyinyi kuweza kunielewa ambacho nawaomba hakimu pindi naondoka hapa mahakamani kichwa cha mama yangu naomba mkakizike kwenye kaburi la mama yangu ili kisiendelee kuteseka hivyo. Kwa kweli mimi ndio nilimuua mama yangu pamoja na hawa watu. Haya nayathibitisha kupitia mdomo wangu na hii sauti inatoka kwenye koo langu na siyo ndani ya moyo wangu. Nikisema kuwa mimi sijafanya hivi ni vigumu kunielewa kwanza mmenikamata na ushahidi na pili mmepandikizwa vitu na watu wenye uwezo wa juu kushinda mimi. Nakubali kuwa nilimkata mama yangu kichwa ili niwe tajiri. Nimekubali haya yote ili kichwa cha mama yangu mkakipumzishe salama kisiendelee kuteseka. Mama yangu yupo kaburini haoni, haiskii, hanusi, hapumui wala hapigi chafya kwani kitu ambacho kinamfanya kufanya hayo mambo bado mmekizuia huku duniani tafadhari pelekeni hicho kitu kwa mama yangu”Niliongea yale Maneno kwa sauti ya juu na yaukali kidogo hadi machozi yalianza kunitoka. Hakimu alipoona nimemaliza kuongea yale maneno alimkaribisha na Mzungu. “Najua kuwa Tanzania ni nchi ambayo inanuka rushwa hivyo mliponikamata nilijua kabsa lazima mtufunge. Nikiongea ukweli wa mambo naona sitamaliza siku mbili tayari nitakuwa nimekufa tena naweza kuuawa na polisi kabsa. Ila nathibitisha na Mungu ananisikia hicho kitu hatujafanya na aliyefanya hiki kitu muda utafika mtakuja kumjua tu. Mimi nipo tayari kwa Hukumu yeyote ambaye mtaitoa ila mtakapo nirudisha gerezani mpelekeeni salamu Mchungaji masanja atufanyie ibada sana tuweze kufia huku Jera tusitoke tena”Yalikuwa ni Maneno machache ambayo aliongea Matonya nakutulia kimya. Baada ya kumaliza kuongea yale Maneno hakimu alisema turudi wiki ijayo kwa ajili ya Hukumu.
********************-************************************************ Baada ya kesi yetu kusomwa ikaisha pia sisi kupewa nafasi ya kujitetea tukajitetea hatimae hakimu kutoa wiki moja ndio Hukumu itapita ilibidi kurudishwa tena Rumande kusubilia Hukumu yetu. Kutoka Mahakamani hadi Gerezani Uyui defender ilitumia muda wa dakika tano tu tayari tulishafika. Tulipofika tulishushwa na kuwekwa Sello tena kama kawaida. Ile hali kwa kweli mimi ilikuwa hainipendezi kabsa maana bora tungehukumiwa tungekaa huru bila kulindwa muda wote. Tungehukumiwa ingawa ulinzi ungekuwepo lakini usingekuwa wa hatari kama muda huo. “Tunatakiwa kukaa miezi minne mbele ndio tutoroke inaonekana ulinzi kwetu Bado mkubwa sana. Ila kama tukihukumiwa Angalau ulinzi kwetu utapungua na kufanya maandalizi ya Kutoroka. Kiufupi siwezi lazima nitoroke kwenye hili gereza hata kama kutakuwa na ulinzi mkali wa aina gani. Nahitaji kulipiza kisasi cha kifo cha baba yangu ambae aliuawa bila hatia na Masanja kisha kesi nilitupiwa mimi. Kifo cha Magret pia ninajukumu la kulipiza kisasi hivyo kutoroka humu ni lazima”Aliongea Matonya. Yale Maneno ya Matonya kwa kweli yalinipa Amani sana na mimi kupata malengo ya kutoka Gerezani ingawa tulikuwa na kazi Kubwa sana. Kwa Gereza la Uyui ambalo lilikusanya wafungwa Watukutu wote wa Mkoa Wa Tabora kulikuwa na ulinzi Mkali kutoroka pale ilikuwa siyo kitu cha Mchezo mchezo. Maisha yaliendelea Pale Gerezani hatimae Wiki moja ambayo tulikuwa tunaisubilia iliisha na Kuja kuchukuliwa Tena Kupelekwa Mahakani. Hiyo Siku Mahakamani kila Mtu alikuwa anaingoja kwa Hamu kujua Stakabali ya maisha yake. Saa nne kamali tulishafikishwa Mahakani na nilipoingia Mahakani moyo wangu ulishituka sana nilipomuona Mzee Masanja pamoja na klinita walikuwepo. Uwepo wa Klinita pale haukunishitua maana nilijua anakuja kujua mumeo nahukumiwa miaka mingapi. Ila uwepo wa Masanja pale ilimaanisha Hukumu ambayo tungepewa ilikuwa kali. Baada ya kesi kukumbushiwa kidogo hatimae Hakimu alisimama ili kutoa hukumu “Kutokana na Sheria namba 103 inayohusu makosa ya Njinai kama kuua kwa kukusudia, kubaka pamoja na mashambulizi ya Ugaidi hukumu yake huwa kunyongwa au Kuhukumiwa kifungo cha maisha jela. Hivyo Basi namuhukumu Samweli Kifungo cha maisha Jela kwa kosa la kumuua mama yake na watu wengi kinyama tena kwa kukusudia ili apate mali. Pia namuhukumu Matonya kunyongwa kwa kosa linalofanana na kosa la Samweli ingawa katika kumbukumbu zetu Matonya siyo mara yake ya kwanza kukutwa na Hatia kwenye nchi yetu ya Tanzania. Kosa la Kwanza alimuua Baba yake Mzazi ambaye alikuwa rafiki yake na mchungaji wetu kipenzi Mzee Masanja. Sheria ya Kunyongwa bado haijapitishwa Hapa Tanzania kuwa Rasmi Hivyo ataendelea kutumikia kifungo Gerezani na Siku sheria itakapopitishwa na Rais Matonywa atatakiwa kunyongwa mara moja”Yalikuwa ni maneno ya Hakimu aliyaongea ambayo yalinifanya mapigo yangu ya Moyo kuanza kwenda mbio. Nilimwangalia Masanja yeye alionekana mtu mwenye furaha sana. Nilimwangalia Klinita nilimuonea Huruma maana yeye alikuwa anatokwa na machozi. Masanja yeye alikuwa anacheka kwa kuwa alishaona kazi imemalizika kamwe hata pata Usumbufu tena kutoka kwetu. Upande wa Matonya yeye alikuwa kimya ametulia wala hakuongea kitu chochote. Baada tu ya Hukumu kutolewa tulifungwa Pingu tena tukabakiwa kwenye Defender safari ya kupelekwa Magerezani Uyui kuwa wafungwa Rasmi ilianza
INAENDELEA

