TANGA RAHA
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Sehemu Ya 26
Nikafanya kama mzee ngoda alivyo niagiza na kwa tahadhari kubwa na mimi nikazipandisha ngazi hadi chumbani kwa Rahma na kumkuta akiwa amelala pamoja na Hilda.Nikaigeuza kwa nyuma kofia yangu ya jeshi niliyo ivaa na nikamshika shavuni Rahma na akaanza kupepesa macho akihisi kama mdudu ndio anamtambalia
“Rahma”
Nikaita na akafumbua macho yake na kunitazama kwa muda na akastuka kidogo kuniona ila kabla hajazungumza kitu nikamziba mdomo
“Ni mimi Eddy nimekuja kukuchukua mpenzi wangu wa maisha”
“Kweli Eddy”
“Ndio ninakuomba twende pamoja mbali na hapa mpenzi wangu”
Nikamuona Hilda akinyanyuka na kwa haraka nikamnyooshea bastola yangu na alipo niona ni mimi akawa kama anawewesekea kwa woga ulio changanyikana na uwoga
“Nyanyua mikono yako juu kabla sijakufyatua huo ubongo wako”
Akatii na kwaishara nikamuamuru kushuka kitandani na anyooshe mikono yeka juu na atangulie mbele,Rahma akashuka kitandani huku akiwa amevalia gauni jepesi linalo muonyesha nguo yake ya ndani.Kisha nikamshika kiuno kwa mkono mmoja huku mwengine ukiwa umeishika bastola nikimuelekezea Hilda ambaya gafla akachomoka haraka huka akupiga kelele za kuomba msaada na nikamaucha akimbie huku akishuka kwenye ngazi na kukutana na mzee ngoda akiwa ameshika bastola na kumnya kasi yote kumuishia kweye ngazi
“PITA HUKU KWA WAJINGA WEZAKO”
Hilda taratibu akapita kwa wezake na kufanya kama walivyo fanya huku akiwatazama watu waliopo kwenye adhabu hii.Rahma akaniendelea kunikumbatia huku akiwatazama wazazi wake kwa macho makali
“Baba na Mama……najua siku zote kwamba mulifanya njama za kila namna ili nisiweze kuwa na Eddy…ila tambueni kuwa sijali kama yeye ni mtu mweusi au anapesa au hana pesa mimi ni-memkubali jinsi alivyo…”
Rahma alizungumza kwa sauti ya kufoka na yenye uchungu na kwafanya wazazi na ndugu zake kubiki wakimtazama pasipo kujibu kitu cha aina yoyote.Kwa kuwadhiirishia wazazi wake na ndugu zeka akanishika midomo yangu na kuinyonya kama dakika mbili kisha akawageukia ndugu zake.
“Japo baba ulijaribu kumuua Eddy kwa kumpiga risasi ila ikanipata mimi nakuufanya ujauzito wangu kutoka ila ukweli ni kwamba ana uwezo wa kunizalisha tena na tena na tena na tukawa na watuto wafamilia kubwa “
Nikamuona baba Rahma akitemeka kwa hasira huku macho yake yakiwa mekundu kupita mae-kezo,kwa upande wa mama Rahma nikayashuhudia machozi yakimwagika huku akitetemeka kwa uchungu kwani hawakuamini kama mtoto wao ndio anaondoka mbele ya macho yao
“Eddy hembu fungua begi unitolee redio ndogo”
Nikafanya hivyo na kufungua na kukuta kijiredia kidogo kinacho tumia kanda na kimetenge-nezwa na kampuni ya Panasonic.Mzee Ngoda akakiwasha na kuminya kitufe cha rangi ya kijana kilicho andikwa ‘record’
“JE UMEKUBALI KUMUUOZA MWANAO RAHMA KWA BWANA EDDY?”
Mzee Ngoda alimuuliza baba Rahma huku bastola ikiwa juu yakichwa cha baba Rahma ambaye bila ubishi akajikuta akijibu
“Ndio nimekubali”
“Je Rahma umekubali kuolewa na Eddy?”
“Ndio nimekubali tena sana”
“Na wewe Eddy umekubali kumuoa Rahma”
“Ndio nimekubali”
“Je mama Rahma umekubali binti yako aolewee na Eddy”
“Ndio nimekubali”
“Wanandugu wote wajomba mashangazi na mababu je mumekubali mtoto wenu Rahma kuole-wa na Eddy?”
“Ndioo”
Walijibu kwa sauti za unyonge japo ndio hivyo wamekubali kwa kulazimisha.Akairudisha nyu-ma tepu iliyo kuwemo ndani ya redio hiyo kisha akaisikiliza na sauti zikawa zimeingia vizu-ri,akaizima redio na kuiingiza mfukoni mwake.
“Toa kamba na kisu ndani ya begi”
Nikatoa kamba ina ya manila pamoja na kishu kisha akawaamuru wote kulala chini na idadi yao wapo kumi na nne.Nikaanza kuwafunga kamba mmoja baada ya mwengine na mtu wa mwisho kummalizia kumfunga ni Baba Rahma ambaye akaanza kuleta ubishi nikatandika kofi moja la usogo akatulia,hasira ikaanza kunipanda na nikaikumuka siku alipokuwa akinitesa ikanilazimu na mimi kumhindilia mateke mawili ya makalio baada ya kumaliza kumfunga kamba
“Jamani asanteni kwa ushirikiano wenu mulio tupa sawa”
“Samani jamani ngoja kuna kitu ninataka kwenda kuchukua ndani mara moja”
“Dakika mbili zinakutosha”
Rahma akapandisha ngazi na kurudi akiwa amevalia suruali ya jinzi pamoja na sweta lenye ko-foa na akamfwata mdogo wake mmoja wa kike ambaye kwa makadirio ana miaka kama mitatu akambusu na wakazungumza kiarabu na tukaondoka.Tukamkuta mlinzi getini akiwa amesinzia na alipo stuka na kumuona Rahma akanywea
“Wewe una kazi ya kulala lala?”
“Ahaa ni ni samehe dada Rahma”
“Nyoo ingia ndani ya kibanda chako”
Mlinzi akaingia na Rahma akamuomba funguo za geti kisha akamfungia mlizi kwa nje na kabana mlango kwa kufuli kisha tukaondoka.Tukaingia ndani ya gari huku saa yangu ikinionyesha ni saa saba usiku na tukaanza kuelekea katika njia ya Horohoro inayoelekea mpakani mwa Kenya na Tanzania.Mzee Ngoda akakunja kushoto na tukaingia kwenye barabara ya vumbi na safari ikaendelea na tukavipita vijiji kama vinne na katikati yam situ Mzee Ngoda akasimamisha gari na sote tukashuka
Mzee ngoda akanza kumtazama Rahma kwa macho ya kuiba kuanzia juu hadi chini na kwa jinsi Rahma anavyo nikumbatia kumbatia nikamuona kabisa mzee Ngoda akiumia moyoni mwake kwani ikafikia kipindi hadi sura yake ikawa inajikunja na kitu kinacho nikaanza kunipa wasiwasi.Gafla tukastukia akiichomoa bastola yake na kutonyooshe sisi na Rahma na kwastory nilizo wahi kuzisikia mtaani kweni ni kwamba huyu mzee anatabia ya kutembea na wasichana wadogo japo sikuwahi kumshuhudia na kwa story nyingine nilizo zipata mtaani ni kwamba alimuua mke wake kwa kumpiga rasasi baada ya kufumaniwa akiwa na binti mdogo
Mlio wa bastola ya mzee Ngoda ukanifanya nifumbe macho huku nikisikilizia ni wapi risasi yake ilipo tu,Swali nililo nalo kichwani kwangu ni kwamba ni wapi risasi ilipo tua kwa maana mwilini mwangu sikusikia maumivu ya aina yoyote na kama imempiga Rahma wangu mbona sijasikia sauti yoyote ya yeye kutoa maumivu.Kwa haraka ni kafumbu macho na kumtazama Rahma na kumkuta akitetemeka kwa woga
“Angalieni nyuma yenu”
Tukageuka na kukuta nyoka mkubwa akining’inia kwenye tawi la mti huku kichwa cheke kikiwa kimetawanywa na risasi aliyo pigwa na Mzee Ngoda
“Mwanajeshi anatakiwa kuwa na hisia za kitu chochote cha Atari kitakacho kuwa karibu yake ila nakushangaa Eddy wewe nyoka yupo nyuma yako wala hustuki kwa kitu cha ina yoyote”
Kutokana na mstuko wala sikujua nimjibu kitu gani mzee ngoda,Rahma akanishika mkono na kunikumbatia huku akiendelea kutetemeka.Mzee Ngoda akapanda kwenye gari na kutuomba na sisi tupande,taratibu nikamshika Rahma mkono na tukapanda kwenye gari na safari ikaendelea ambayo tayari nilisha anza kuitilia mashaka na sikujua ni wapi tunapoelekea.Tukafika kwenye moja ya jumba kubwa lililo jegwa vizuri na Mzee Ngoda akasimamisha gari nje ya jumba hili na akatuomba tushuke kwenye gari
“Karibuni sana wanangu hapa ni nyumbani kwangu”
Mzee Ngoda alizungumza huku akitoa funguo nyingi na kufungua geti la chuma lililopo kwenye jumba hili,kisha akafungua na mlango mwengine na tukaingia ndani japo kuna giza ku-ba.Akawasha swichi na taa za ndani zikawaka
“Hapa ni kwangu huwa nikiwa na mawazo sana huwa ninakuja huku kupumzika kama wiki ki-sha ninarudi tena mjini”
“Unakuja kupumzika peke yako?”
“Ndio ninakuja peke yangu na niwatu wengi hawaijui hii nyumba yangu kwa maana ipo porini sana”
“Ni kubwaa”
“Yaa ina eneo kubwa kwa huko nyuma kuna bustani za maua ya kutosha sema sasa hivi ni usiku sana….Hii nyumba niliinunua kwa rafiki yangu alikuwa ni mwanajeshi wa kijerumani kipindi cha miaka ya semanini”
“Ahaa sawa”
Mzee Ngoda akatuonyesha chumba cha kulala ambacho ni kikubwa sana na kina vitu vichache vya dhamani pamoja na kitanda kikubwa cha duara ambacho tangu nizaliwe sikuwahi kula-la,nikakichunguza chumba kizima na kuridhika na mazingira yaliyopo humu ndani.Nikavua nguo zangu na kupanda kitandani na Rahma akafanya kama nilivyo fanya mimi na ikawa ni siku nyingine ya furaha katika mahusiano yetu baada ya kupitia kipindi kigumu cha maisha.Baada ya kupeana haki ianyo stahili kila mmoja akapitiwa na usingizi mzito
Jua kali kiasi linalopita kwenye dirisha na kutupata kitandani ndilo lililofanya niamke na kushuka kitandani na kumuacha Rahma aendelee kulala,Nikaoga na kutoka na kuvaa nguo zangu na kutoka nje na kumkuta Mzee Noda akifanya mazoezi
“Shikamoo mzee”
“Marahaba ila Eddy hilo jina la mzee nilisha kukataza”
“Ahaa samahani baba yangu
Mzee Ngoda akamaliza kufanya mazoezi na akaanza kunitembeza kwenye kila sehemu ya jumba lake la kifahari na kusema kweli wajenzi wa hili jumba waliweza sana kulijenga kwa maana lina vyumba hadi ardhini na maeneo makubwa ya michezo pamoja na sehemu ya kuhifadhia magari ya kutembelea
“Hizi ni Ford za mwaka gani?”
“Aaaa hizo gari ni za mwaka 1932 mimi jamaa alikuwa akizitumia zamani sana ndio kaniachia mbili za ukumbusho”
Tukaendelea kutembea tembea kwenye bustani zenye maua mazuri ya kuvutia
“Haya matunda yote unayo yaona hayana mlaji mengi yanaiva na kuanguka chini”
“Ina maana huku hakuna watu wanaofika kwenye hii nyumba?”
“Hakuna kwa maana hapa ni katikati ya msitu isitoshe kuna ukuta kubwa umezunguka hili jumba upo mbali sana na hapa hadi kuufikia kwa kutumia miguu ni mwendo wa masaa matatu na nusu hadi mane”
“Ehee kumbu ni kukubwa hivyoo?”
“Ahh wee acha tuu wezetu zamani walikuwa na akili sana na hata hii miti yote unayo iona asili-mia 90 ameipanda yeye mingine ni miti ya asili kama ulisha wahi kusoma kuwa kuna misitu ya kutengenezwa huu ni mmoja wapo”
“Ahaa kweli alijitahidi ndio maana nikawa ninashangaa ni kwanini hii miti imepandwa kwa mistari ila nikashindwa kukuuliza tuu”
“Ni yeye jamana alikuwa anaitwa Muller Shostaiger Manzuchuk”
“Ehee kweli hilo jina ni la kijerumani”
“Yaaa”
Tukaendelea kuzunguka maeno ya karibu na jumba lake na baada ya kumaliza tukarudi nyum-bani na kumkuta Rahma akiandaa kifungau kinywaa.Kutokana na upendo nilio kuwa nao juu yake nikamsaidia kupika piaka anacho kipika,tukaandaa chakula mezani na sote tukajumuika kwa kula.
“Jamani mimi leo nitarudi mjini sasa nyinyi sijui mutakaa kwa kipindi gani huku?”
“Kama wiki hivi?”
“Eddy wiki…….baba yangu sisi tutakaa zaidi ya wiki sitamani kurudi mjini kwa maana ninajua ni lazima baba atakuwa ananitafuta”
“Sasa Sheila tutakaa kwa kipondi gani huku?”
“Kwa muda wowote hadi nichoke mwenyewe ndio nitarudi mjini?”
“Na shule jee?”
“Shule ya kazi gani?”
“Lakini Eddy wewe si mwalimu…..? Utakuwa unamfundisha huku huku mke wako”
“Ahaa jamani haya hapo sina ubishi mumeshinda nyinyi”
“Yeaa kila ninacho kifanya lazima nikishindee”
Raham alizungumza huku akinyanyuka na kuelekea jikoni
“Mmmm mwangu huyo mkwe wangu anavutia sana kwa maana mmmm hongera sana”
“Asante”
“Ila kitu ambacho ninapenda kukuambia usije ukaja kumuacha huyu msicha ua kumsaliyi kwa maana utakuja kupata matatizo makubwa sana utakayo yajutia kwenye maisha yako”
“Mmmm matatizo gani?”
“Hapa hakuna cha kuuliza ni matatizo gani ni wewe tuu kuwa makini na kumlindia penzi lake….Kindi ninamuoa mke wangu nilikuwa ninampenda sana tena sana ila hadi ikafikia hatua ya mimi kumuua ilinilazima kufanya hivyo ili kuondoa dukuduku nauchungu ulio kuwa moyoni mwangu”
“Alikufanyaje?”
“Ni historia ndefu tena sana”
Rahma akarudi na kukaa kwenye kiti alicho kuwa amekikalia na Mzee Ngoda akamtazama sana Rahma kisha akatabasamu na kumalizia na kicheko
“Baba mbona unacheka?”
“Ninacheka kutokana mke wangu alikuwa ni muarabu kama huyu mkwe wangu hapa na tabia za waarabu ninazijua vuzuri kwa maana wazazi wake nao hawakupenda sana mimi nimuoe na kipindi kile ndio ninatoka zangu depo bado kijana mbichi mbichi ninavutia ahaa basi mtoto alidata sana sema wazazi wake baada ya kugundua mimi ni mwanajeshi walipiga sana kelele nikaamua nimtoroshe kinguvu na kuja kumuweka huku msituni hadi alipo pata ujauzito na alipo karibia kuzaa ndio nikamrudisha mjini na akajifungua yule mwanangu wa kwanza na wapekee…..”
“Basi kadri miaka ilivyo zidi kukatika ndivyo jinsi nilivyozidi kumpenda mke wangu ila kuna kipindi nilichukuliwa na serikali nikapelekwa Cyuba nakumbuka ilikuwani mwaka 1999 na kule nilikaa miaka mitano mbali na yumbani kwangu.Ila nilipo rudi nikamkuta kijana mmoja ambaye alidai kuwa ni mhuhudumu wa ng’ombe…..aaah kuntokana sikuwa na mud asana sikuweza kumfwatilia sana mke wangu ila tabia yake ilianza kubadilika”
“Alibadilikaje?”
“Jamani mimi mwezenu wala sijui hta munazungumzia kitu gani?”
“Subiri nitakuaadisia wakati wa kulala”
“Mmmm jamani mbona munanitenga au mimi sistahili kuielewa story yenu”
“Lakini mpenzi wangu mbona unakatisha utamu hembu tulia kwanza baba amalizie”
“Mwaya mweke ni kwamba story ninayoizungumzia ni kuhusiana na mke wangu ambaye kaburi lake lipo nyuma yah ii nyumba”
“Ina maana baba wewe huna mke?”
“Ndio sina mke kwani alisha kufa siku nyingi sana”
“Ahaa masikini pole baba yangu”
“Asante”
“Alikuf a na nini?”
“Rahma unakatisha utamu wa story hembu nyamaza bwan”
“Kwani nimekuambia wewe Eddy…….hembu litazame lile komo leke”
“Ndilo ulilo nipendea”
Sote tukajikuta tukicheka kwa furaha
“Kwa ufupi mke wangu nilimuua kwa kumpiga risasi”
“Haaaa….!!”
“Dawa ya meno hiyo si ulikuwa unataka kujua sasa unashangaa nini…..mwaya baba endelea na story”
“Kwa makelele yenu mumenifanya pia nimesahau ni wapi nilipo ishia?”
“Umeishia pale uliposeme tabia yake ilianza kubadilika”
“Eheee basi kila nilipokuwa nikimuomba chakula cha usiku basi akawa ananinyima kiasi kwamba nikaanza kupata wasiwasi lakini kipindi cha nyuma yeye ndio alikuwa anakiomba tena kwamachozi pale nilipo kuwa nimechoka alikuwa akilia kama mtoto”
“Mmmm chakula cha usiku ndio nini baba?”
“Rahmaa ahaa utaniboa sasa”
“Mkwe wangu chakula cha usiku hata wewe jana ninaimani umekila”
“Rahma usijifanye hujui wakati kila kitu unakijua…..watu wamefunga bwana usiropoke mambo mengine si yakuyazungumza”
“Wewe umefunga wakati jikoni ulikuwa ukidokoa dokoa soseji”
Ikanilazimu nimzibe Rahma mdomo kwa kiganja ili mzee Ngoda aendelee na Stori ya ma ishayake
“Basi ile tabia mimi ikaanza kunipa mashaka na mbaya zaidi mwanangu alikuwa bord kwa maana nilimpeleka tangu akiwa chekeche”
“Eddy nikizaa mwangu swala la bord sitaki kulisikia”
“Haya nimekusikia nyamaza”
“Kuna siku nilimuaga mke wangu kuwa ninakwenda Congo kikazi na haikuwa hivyo nikachukua chumba hotelini na kukaa siku mbili bila kutoka njee na siku ya tatu usiku wa manane nikaelekea nyumbani kwangu nikaruka ukuta na kuingia……Sikuingia ndani kabisa ila nikazunguka kwenye chumba cha dirisha ninalo lala…..katika siku nilizo umia moyoni mwangu ni siku ile kwa maana nilimshuhudia mke wangu akishuhulikiwa na yule mtunza ng’ombe tena nilikuta kipindi anapigwa makofi ya makalio na yule mchunga ng’ombe huku akiamrishwa anitukane tusi ambalo hadi kesho naingia kaburini siwezi kulisahau ni lile alililokuwa anaalizungumza kwa sauti ya kejeli…..MUME WANGU NI FALA HAWEZI CHOCHOTE….iliniuma sana”
Rahama akaanza kucheka kichini chini na akashindwa kuvumilia na kuaanza kucheka kwa nguvu na kunifanya na mimi nijikaze kucheka huku nikimuliza Rahma
“Kinacho kuchekesha ni nini sasa….”
Nikajikuta na mimi nikicheka sana hadi nikahisi Mzee Ngoda anaweza akachukia ikanibidi niji-kaze japo sura yangu imejaa tabasamu la kucheka
“Wee acha tuu niliitwa Fala mimi na kuambiwa siwezi kabisa….hilo ni tusi dogo kuna mengine makubwa sana alinitukaa tungekuwa sisi wawili ningekuambia sema huyo mkwe wangu hapo ninalinda heshima yangu”
Rahma akainama chini ya meza kwani kila anapomuangalia Mzee Ngoda anashindwa kukizuia kicheko chake hadi machozi yanamwagika
“Niliondoka zungu huku nikiwa mnyonge sana ila nikaataka kumfanyia kitu kibaya mke wangu ila nikaona nimsamehe na kesho yake asubuhi nikarudi na kumuambia safari imehairish-wa……kutokana ninampenda mke wangu niliamua kumuambia tabia yake ila alikataa kata kata”
“Aaaah kweli hata kama ni mimi ningekuwa mwanaume huyo mwanamke ningemua kwa njia yoyote ile”
“Basi nilifunga kamera za ulinzi za siri siri nyumbani kwangu pasipo kumjulisha mke wangu cha kushangaza sasa wakawa wanaendelea kufanya vitu vyao kama kawaida…..nikaamua na mimi nianze kwenda nje ya ndoa na nikaanza kumfanyia kubuhu nikawa sirudi home nalala siku mbila tatu nje ya nyumba…kumbe na yeye akawa ananifwatilia na kunakitu nilimfanya yule mkata majani hadi kesho huko alipo kama yupo hai nahisi anajutia”
“Ulimfanya nini?”
“Nilimchoma sindano yenye dawa ambayo itamfaya mika yake yote hadi anakufa mashine yake isisimame hata kama anatumia dawa za namna gani haiwezi kusimama”
“Duuu”
“Tena ngoja nikawaonyeshe kaburi lamke wangu muda kidogo umekwenda”
Tukasimama na tukatoka nje na kuzunguka upande wa pili wa nyumba na gafla nikaanza kumuona Rahma akianza kubadilika sura yake baada ya kuiona picha iliyo wekwa juu ya kaburi la mke wa Mzee Ngoda
Sehemu Ya 27
“Huyu ndio mke wangu ambaye alinifanyia mambo mengi ya ajabu sana”
Rahma akapiga magoti taratibu na kuitazama picha kwa kwa umakini huku akiifuta futa vumbi na mimi nikajikutana nikiikazia jicho kwani picha iliyo kuwepo pale inafanana sana na Olvia Hitler ambaye siku zote ninaamini ni shetani ambaye alikuwa akinifwatilia
“Baba huyu ni mke wako?”
“Ndio na nimezaa naye mtoto yule mmoja”
Nikataka kuuliza jina lake ni nani ila kwenye msalaba ulio tengenezwa ukanipa jina kamili am-balo ni Olvia Abdukarim,kajasho kembamba nikahisi kina nimwagika kwenye uso wangu huku kwa mabali mapigo ya moyo yakienda kasi kiasi
“Huyu dada mimi mbona kama ninamjua”
Rahma alizungumza na kutufanya sote tumtizame na mimi wasiwasi ukazidi kunijaa na kujikuta nikikishindwa hata kuzungumza
“Umemonea wapi?”
“Sikumbuki ni wapi nimemuona ila hata majuzi nilikuwa naye ila sikumbuki ni wapi?”
“Utakuwa umeota huyu mke wangu nilimuua miaka miine ya nyuma”
“Labda watu wanafanana na pia alinielezea mambo mengi sana ila ahaaa siyakumbuki”
Nikamtazama Rahma jinsi anavyo ishika shika picha iliyopo kwenye kaburi hata hamu ya kui-tazama ikaniishia
“Jamani mimi nipo ndani”
Nikaondoka taratibu huku nikiwaacha wakiendelea kuzungumza kuhusiana na maisha ya mke wa Mzee Ngoda,Amani yote ikatoweka moyoni mwangu ila nikaanza kujifariji kimya kimya ku-tokana nina pete mkononi ambayo alinipa Yudia.Wakaingia na kunikuta nikiwa nimejilaza kwenye kochi na Rahma akajiusha na kunikalia kwenye mapaja yangu
“Tutaumizana bwana”
“Jamani eti baba mimi ninauzito gani?”
“Ahaa nyinyi malizaneni wenyewe…..mimi ngoja niwaache nirudi zangu mjini kati yenu si yupo mwenye simu”
“Yaa mimi ninasimu baba naomba namba yako”
Mzee ngoda na Rahma wakapeana namba kisha akatomba tumsindikize nje na akaingia ndani ya gari lake na kutuahidi atarudi baada ya siku tano kutuletea chakula kwa maanakilichopo kwenye mafriji makubwa yaliyomo ndani kinatutosha kwa siku zaidi ya tano
“Mkwe ukiwa na mhitaji ya chakula utanitumia meseji ni nini unahitaji ili nije nacho”
“Sawa baba wala usijali kwa hilo”
“Eddy mtunze mkwe wangu bwana si unajua nimewafungisha ndoa ya kijeshi”
“Ndio kwa hilo usijali baba yangu”
Nilimjibu mzee ngoda kwa unyonge na akawasha gari na kuondoka,tukarudi ndani huku moyoni nikijutia kwa nini nimekuja
“Eddy mbona huna raha mume wangu?”
“Mbona ninaraha tuu”
“Mmm unaonekana huna raha kabisa kuna kitu nimekuudhi?”
“Hapana baby”
“Ila mbona upo hivyo…..? mimi sipendi bwana”
Rahma akaanza kunitekenya huku akizungumza kwa sauti ya kudeka,nikajikuta nikicheka ila kusema ukweli moyo wangu haukuwa na furaha hata kidogo,kwa bahati mbaya katika kumi-nyana minyana na Rahma nikamkwaruza kwenye mkono
“Baby kucha zako ndefu ngoja nikachukue kiwembe nije nikukate”
“Kiwembe wewe umekiona wapi?”
“Kuna kimoja nilikiweka kwenye wallet yangu ndogo”
Rahma akaelekea chumbani na mimi nikaendelea kujilaza kwenye kochi na baada ya dakika kadhaa akarudi akiwa na wallet yake na akaifungua nikaona kadi nyingi za benki
“Makadi yote hayo ya benki ni ya nani?”
“Nimechukua kadi ya baba,mama na zangu na zote ninazijua namba zao za siri…..Mungu akibariki tukirudi hivi nataka tokatoe pesa zote kwenye akaunti zao kisha twenda mbali na hapa”
“Unataka twende wapi?”
“Oman popote ambapo tunaweza kwenda kupata uraia wa kutuwezesha kuishi kwa amani na furaha katika maisha ya ndoa yetu”
Rahma alizungumza huku akiendelea kunikata kucha taratibu mkono wa kulia
“Ahaa mume wangu una kucha nzuri”
“Mmmm umeanza”
“Sio nimeanza kwani mtu kumsifia mume wake ni vibaya kama hutaki unamakucha mabaya ka-ma zombie”
“Ahaa haya bwana kama mimi zombi basi wewe mama zombi”
“Jamaani baby….”
“Hakuna cha jamani tena wewe mazombi yake yanayo fanya khaa”
Nilipo kuwa nikijitingisha nikimuonyesha Rahma jinsi ya aina ya mazombi anayo fanana nayo kwa bahati mbaya akanikata kwenye kidole na damu zikaanza kunimwagika
“Umeona sasa na kuigiza kwako uzombi umejitingisha hadi nimekukata”
“Hembu nenda kaniletee kitu cha kuizuia hii damu kutoka”
“Ila pole mume wangu”
Rahma akanibusu kwenye uso na kuingia jikoni na mimi nikabaki nikiwa nimejishika kidole huku damu zangu zikimwagikia kwenye sakafu iliyo tengenezwa kwa mbao ngumu sana.Akarudi akiwa ameshika pakti ya chumvi na bakuli lenye maji.Akaanza kuninawisha taratibu kisha akanipaka chumvi ya kutosha ili kuizuia damu isitoke kwa wingi
“Eddy hiyo pete amekuvalisha nani?”
“Nimevaa tuu”
“Sipendi nakuomba uivue”
“Baby hii si ninapendeza nikiivaa”
“Sitaki ninakuomba uivue kwa maana pete yangu ndio inapaswa nikuvalishe ila sio wewe kujivalisha mapete pete yako ya ajabu”
Rahma alizungumza kwa hasira huku akiushika mkono wangu wa kushoto na kuanza kuicho-moa pete,
“Babay ila hiyo pete ni ya dawa”
“Kwenda zako huko tangu lini pete zikawa dawa……au umevalishwa na mwanamke wako huko unajidai ni ya dawa”
“Sio hivyo baby ila kuna…”
“Sitaki kusikia cha kuna wala nini….Hivi Eddy mashani mwako umesha wahi kupata mwanamke ambaye yupo tayari kujitoa maisha yake kwa ajili yako?”
“Hapana?”
“Kwa hiyo mimi nilikuwa mjinga sana kusimama mbele yako ili risasi inipate mimi si ndio?”
“Hapana mpenzi wangu ninakuomba upunguze jazba….hiyo pete mimi nimeivaa kutokana na matatizo yangu binafsi na kuna dada mmoja ndio alinipatia ili nijikinge nayo”
“Dada ehee dada eheee….kwahiyo mukavalishana?”
Rahma alizungumza huku machozi yakimwagika taratibu na akanyanyuka kwa hasira na kutoka nje akiwa na pete yangu mkononi na mimi ikanibidi nitoke nje kumfwata na kumkuta akiwa amekaa kwenye moja ya mabembea yalipo kwenye bustani za hili jumba
“Rahma”
Nilimuita huku nikimshika mkono na akaitoa mikono yangu kwa hasira
“Eddy sitaki uniguse nakuomba uniache”
“Siwezi kukuacha kwa sababu wewe ni mpenzi wangu”
“Eddy mimi sio mpenzi wako na unikome na kuanzia sasa hivi Eddy ninakuapia sitaki kuwa na wewe tena…..Mimi napigwa risasi na baba yangu kwa ajili yako,ninawakimbia wazazi wangu kwa ajili yak oleo hii unanimbia eti kuna mwanamke alinipa eti nijikinge unadhani mimi ni mtoto mdogo kiasi cha kunidanganya”
“Rahma mke wangu nakuoma uniamini hiyo pete mimi inanisaidia kuona mauza uza yanayo nitokea usiku”
Nilizugumza kwa sauti ya uyonge na ya upole ila sura ya Rahma haikubadilika na kwajinsi ni-navyo mjua Rahma hasira yake huchukua mud asana kuondoka
“Eddy hivi unajua ni dhamani gani ambayo mimi ninakupa,unajua ni jinsi gani mimi ninavyo kuchukulia wewe kama kiongozi wangu wa maisha…..ila kwa nini unafanya hivyo lakini?”
“Mke wangu ninakuomba unisamehe kama nitakuwa nimekuudhi kwa hilo ila kusema kweli hiyo pete mimi sina nia nayo mbaya kama unavyo nichukulia ila ukweli ni kwamba kuna majini yananisumbua sana usiku yanapelekea ninashindwa kuishi kwa amani mke wangu ninakuomba unipatie hiyo pete”
“Ahaa basi na mimi ninataka niyaone yakikusumbua na nikama pete yako nimesha itupa”
“Haaaa wapi…!!?”
“Sijiu na niankuomba uniache”
Ni kweli mikono yaRahma haikuwa na pete yangu mkoni na nikaanza kuitafuta katia sehemu ambayo Rahma amekaa ila sikuiona
“Mke wangu niambie basi ni wapi umeitupa?”
“Si nimekuambia usinihusi na mambo yako nenda kamuulize huyo Malaya wako aliye kupa akuchongeshee nyingine”
“Rahama usizungumze hivyo utanikasirisha”
“Kasirika kwani nimekuzuia kukasirika wee vipii”
Nikaachia msunyo mkali na kuendelea kuitafuta ni wapi ilipo na kwa dharau Rahma akanyanyuka na kuingia ndani,Sikufanikiwa kuipata pete baada ya kuitafuta kwenye kila sehemu ambayo nilihisi kuwa anaweza kuitupa,Nikarudi ndani sikumkuta Rahma sebleni,nikaingia chumbani na kumkuta akiwa amekaa kitandani huku akiwa ameukumbatia mto machozi yakiendelea kumwagika hadi sura yake ikatawaliwa na uwekundu fulani.Akanitazama kwa jicho kali hadi ninakaa kitandani akaendelea kunitazama
“Mke wangu hembu niambie ni wapi ilipo hiyo pete”
Rahma hakunijibu zaidi ya kuendelea kunitazama na machozi yakazidi kumtoka,gafla nikastukia akianza kunipiga na mto alio ushika
“Eddy kwanini kwanini unanifanyia mimi hivi…..?”
Rahma aliendelea kunipiga na mto wake anaona haitoshi akantupa na kuanza kunipiga kwa mi-kono yake huku akiwa amenikalia kiunoni huku nikiwa nimejilaza chali.Nikawa na kazi ya kui-zuia mikono yake isisiendeleaa kunipiga kwani nilimuachia apunguze hasira zake kwa namna hiyo ya kunipiga,Taratibu akaanza kupunguza nguvu na kasi ya kunipiga na taratibu akajishusha na kulilaza kichwa chake kwenye kifua changu na kuendelea kulia kwa sauti ya kudeka
“Eddy”
“Naam”
“Unanipenda?”
“Ndio ninakupenda mke wangu tena zaidi ya kukupenda”
“Kwa nini unanisaliti?”
“Mke wangu sijakusaliti na siwezi kufanya hivyo ndio maana niliamua kuja kukuchukua kwenu japo baba yako alinitena na kuninyanyasa kutokana na weusi wangu na kuto kuwa kwangu na pesa”
Nilizungumza kwa sauti ya uchungu huku machozi yakinilenga lenga
“Rahma nipo tayari kufa kwa ajili yako….alama zote za mistari niliyo chanwa na kisu yote ni kwaajili yako,Damu yangu nyigi ilimwagika kwa ajili yako.Baba yako alitaka kunizika hai ila kwa uwezo wa Mungu nikafanikiwa kuokoka laity ingekuwa ni mtu mwengine angakuja kwenu tena eheee…?”
“Eddy ninakuomba unisamehe mume wangu najua ni jinsi gani unanipenda na kunihita-ji,natambua umeteseka kwa ajili yangu”
Rahma alizungumza huku akinifuta machozi ambayo yalisha anza kunimwagika,Rahma akaishusha midomo yake na kuikutanisha na midomo yangu na ndani ya dakika chache tukajikuta tukiingia kwenye dimbwi kubwa la mapenzi huku kila mmoja akijitahidi kumfurahisha mwenzake kwa jinsi anavyo jua yeye mwenyewe.Tukamaliza na kuingia afuni huku nikiwa nimembeba Rahma,tukaanza kuoga na kurudi chumbani na kujitupa kitandani
“Eddy unataka kula?”
“Nimeshiba mke wangu au wewe una njaa?”
“Hapana nilitaka kujua kama unanjaa basi tutapika jioni”
Masaa yakazidi kukatika huku na jjioni tukasirikia kupika chakula cha usiku na tukala kwa pa-moja huku tulilishana na tukamaliza na sote kwa pamoja tukajilaza kwenye kochi moja
“Baby hivi ile pete uliitupa wapi?”
“Umesha anza unataka nikasirike eheee”
“Basi yaishe mke wangu kwa maana ukianza kukasirika utaanza kurusha makofi yako”
“Yaa kama Sensia vile”
“Toka huko Sensia uwe wewe umelegea hivyo”
“Nimelegea wapi wakati nimekupiga zakichina china”
“Hahaaa haya mwaya mke wangu ila na wewe ni baunsa”
“Twende tukalale ninahisi usingizi”
“Zima taa za sebleni”
Sote tukaingia ndani na kujilaza kitandani,usingizi mzito ukanipitia nakulala fofofo.Kwa mbali nikaanza kuhisi ngoma kubwa ikipigwa na watu wakishangilia.Kwa mara ya kwanza nikaipote-zea nikijua ni ndoto zangu za kawaida,ila kadri muda unavyo zidi kwenda ndivyo jinsi sauti za watu na mlio wa ngoma hiyo ulivyo zidi kuongezeka kupigwa.Nikachukua mto na kujiwekea kichwani na kuziba masikio ila nikahisi kitu na kujikuta nikikurupuka na pembeni yangu siku-muona Rahma.Na mlio wa ngoma nikausikia ukizidi kuongezeka ilanibidi nichungulie dirishani ila sikuona watu wanao cheza ngoma hiyo kwa maana dirisha la chumba chetu linaelekea kwenye bustani ya nyuma
Nikaingia bafuni na sikumuona Rahma ikanilazimu kujifunga taulo na kwenda sebleni ambao mlio wa ngoma na kelele za watu zikazidi kuniumiza masikio yango.Taratibu nikafungua pazia la dirisha la sebleni na nusu nipoteze fahamu ila nikajikaza kuendelea kutazama.Kundi kubwa la watu wenye asili ya kijerumani wamewazunguka Rahma na jamaa mmoja wa kizungu huku Rahma akiwa amevalia shela la harusi huku na jamaa suti ya harusi na Rahma ameishika pete yangu aliyo itupa akitaka kumvalisha jamaa kwenye kidole kama nilicho kuwa nimekivaa mimi na nikazidi kuchanganyikiwa baada ya muongozaji wa harusi hiyo akiwa ni Olvia Hitler
Taratibu nikalifunga pazia na kukaa kwenye kichi huku nikijiuliza ninacho kiona ni kwelia au ni ndoto,Kelele za ngoma zikanifanya niweze kuamini kama ni kweli kwa ujasiri mkubwa nikasimama na kuufungua mlango na kuwafanya watu wate waliopo kwenye eneo nje kunitazama kwa macho makali ambayo si ya kawaida kama ilivyo kwa sisi binadamu.Macho yao yametawaliwa na rangi ambazo si za kawaida kwa haraka haraka ninaweza kuzifananisha na mwanga wa moto wa gesi.Rahma akabaki akinishangaa kama mtu asiye jitambua aliye kamatwa na bumbuazi kali,Nikaanza kupiga hatua mbili mbele na kuwafanya vijana wawili wa kijerumani kusimama mbele yangu na kunitazama kwa umakini kisha nao wakaanza kunisogela huku taratibu wakianza kubadilika maumbo yao kwa kutoka manyonya kama ya mbwa.Nikaanza kurudi nyuma kwa haraka na nikausukuma mlango ila kwa bahati mbaya nikaukuta mlango ukiwa umejifunga kwa ndani.
Jamaa wakazidi kunifwata na sikuwa na jinsi zaidi ya kaanza kupiga hatua za hakanyaga maua yaliyopo pembezoni mwa ukuta na kuanza kukimbia kuelekea sehemu yenye msitu,Vijana wa kijerumani naa wakanza kunikimbiza na kadri wanavyo kimbia ndivyo miili yao ikabadilika na kuwa kama mbwa aina ya Bweha(FOX) na kuzidi kunikimbiza.Sikuwa na namna nyingine yoyote zaidi ya kuuparamia mti kwa haraka cha hadi nikakaa juu ya moja ya tawi huku nikihema na jasho jingi lilimwagika.Mwanga wa mbara mwezi ukanisaidia kuwaona jamaa wakiuzunguka mti huku wakinguruma kwa sauti za kutisha sana.Mbwa watu wakaanza kutoa vilioa vya ajabu na kadri mawingu yanavyozidi kuufunika mwezi ndivyo wao wanavyozidi kupata shida katika miili yao na ambayo ikaanza kurudi katika hali kawaida hadi wa kawa binadamu wa kawaida ila hakuna aliye kuwa na nguo miomgoni mwao
Kila kitu ambacho kinaendelea sikuwa ninaamini ni kweli na ninayo jionea,nikajilaza kwenye tawi huku nikiendela kuwatazama jamaa na wakabaki chini ya mti wakiwa wananitazama huku wakinisubiria nishuke.Masaa yakazidi kwenda na kidogo nikaanza kushindana na macho yangu kitika swala zima la usingizi na kila nipojaribu kuyafumbua kwa nguvu zagu zote ndivyo jinsi macho yalivyo zidi kunikatali nakujikuta taratibu nikiyafumba na kausingizi kakanipi-tia.Nikaanza kuisikia sauti kwa mbali ya Rahma ikiniita na kunilazimu kuyafumbua macho na kukuta mwanga ukiwa umetawala kila sehemu na jamaa sikuwaona,Nikashuka kwenye mti taratibu hadi ninakanyaga ardhi na Rahma akawa amefika kwenye sehemu nilipo
“Eddy ulikuwa wapi?”
Nikamtazama Rahma kwa macho makali yaliyo jaa hasira na sikumjibu kitu cha aina yoyote zai-di ya kuondoka pasipo kumkibu.Nikapitiliza moja kwa moja hadi sehemu walipo kuwa wakicheza ngoma zao usiku na kuyakuta mazingira yakiwa kama jana mchana tulivyo yaacha na hapakuwa na hata jani linalo onyesha kuwa limekanyagwa.
“Eddy mume wangu si nimekuuliza ulikuwa wapi hujanijibu kitu au hujanisikia?”
“Pete yanguipo wapi?”
“Ila baby jana si nilikuambia kuwa nimeitupa”
“Nisikikilize wewe mwanamke usitake nikufanyie kitu ambacho sijapanga kukufanyia ninaomba unipe pete yangu kabla sikakuvuruga.”
Nilizungumza kwa hasira huku macho yangu nikiwa nimeyakaza hadi Rahma akaanza kurudi nyuma
“Eddy kwahiyo mimi unanikasirikia?”
“Ninaomba pete yangu”
Nilizungumza kwa hasira huku nikiwa nimemsogelea kwa karibu Rahma hadi akaanza kutete-meka kwa woga.Nikamuacha na kuingia ndani,kitu cha kushangaza sehemu ambayo jana damu zangu zilimwagika sikuzikuta ila kila kitu tulicho kiacha nikakikuta kama kilivyo ikiwemo dishi la maji na kiwembe.Wasiwasi ukaanza kunijaa na sikujua ni nini kinacho endelea,nikapitiliza moja kwa moja hadi chumbani na kujitupa kitandani na baada ya muda Rahma akarudi akiwa amechoka na kukaa pembeni yangu
“Baby nimeitafuta ila sijaiona”
“Huo ujinga usiniambie ila kikubwa ninaihitaji peta yangu umenielewa?”
“Ila baby kwani swala la pete si tulisha lizungumza jana na likaisha”
“Nitakunyonga Rahma au ndio umemvisha yule bwege wako jana usiku?”
“Eddy mbona sikuelewi hayo yote yametokea wapi?”
“Sasa hivi unielewei eehee?”
“Ndio Eddy sikuelewi ninaona unanichukia pasipo kuwa na sababu ya msingi….”
“Nisikilize Rahma mimi sio mjinga na kama unahisi kuwa mimi ni mjinga tambua ya kuwa ume-kosea na kamwe usitaraji kuwa mutaweza kuniteka akili zangu wewe na hao mashetani wezako sawa?”
“Eddy mimi shetani?”
“Ndio wewe nishatani tena Shetani mwenye mguu mmoja”
Rahma akaanza kulia kwa uchungu huku akinitazama kwa unyonge
“Tena usijilize kinafki kiasi hichi mimi ninadhani nina mwanamke mtu kumbe unakwenda ku-funga ndoa na majini watu wala wasio eleweka ili sasa iweje au unavyo ona mwenyewe umeni-komoa si ndio?”
Nilizidi kupayuka kwa hasira
“Eddy laiti kama mimi ni jini basi Mungu anilaani sasa hivi na nife ninaapa kwa jina leke mimi siwezi kukufanyia hivyo unavyo fikiria”
“Ahaa kwahiyo jana mimi niliota si ndio….hadi mashemeji zako wakaamua kunilaza juu ya mti?”
“Eddy naomba unisikilize mpenzi wangu……..mimi jana usiku niliamka na kwenda jikoni kunywa maji ila nilipo rudi huku chumbani sikukuta kutokana na usingizi mwingi nikajua utakuwa upo bafuni mimi nikaamua kujilaza zangu sasa asubuhi ndio nikaanza kukutafuta na kukukuta ukishuka juu ya mti ila unapo nihukumu nakuniita mimi jini la mguu mmoja unakuwa hujanitendea haki mume wangu….Unavyo niambia hivyo unanipa mimi uchungu mwingi inaonekana kuwa mimi si chaguo lako sahihi.”
Sehemu Ya 28
Rahma akaendelea kuzungu kwa uchungu huku machozi yakimwagika
“Kwa hiyo niliye muona pale nje sio wewe?”
“Nje wapi mume wangu mbona unaninyanyasa kiasi hicho au kukupenda kwangu ndio kosa?”
“Koma sijazungumzia maswala ya kupendana,mimi ninacho taka kukijua ni kwamba ipo wapi pete yangu”
“Eddy sijui nimetafuta sehemu nilipo itupa jana ila sikuiona”
“Ahaa powa niache nilale….ila kabla sijalala nahitaji kujua mbona jana ulipo iona picha ya mke wa Mzee Ngoda ulistuka?”
“Eddy yule dada nilimuona siku moja nikiwa sijielewi pale nilipo pigwa risasi na baba,alikuwa akinijia katika mazingira ya kuogopesha sana kiasi kwamba nikawa ninaogopa sema sikuwa na uwezo wa kusema kuwa ninaweza kupambana naye.”
Nikajikuta nikikaa kimya huku nikimuangalia Rahma akizungumza huku machozi yakimtiririka
“Kuna vitu ambavyo alikuwa akinionyesha vya ajabu ajabu na akaniambia kuwa mimi ni mfu na sito weza kuishi tena,ila akaniambia kuwa nisipo weza kukubaliana na sharti lao moja basi sino weza kurudi kuishi tena duniani”
Mwili mzima ukazizima huku nikiusikilizia jinsi unavyo nisisimka na kujikuta nikikaa kitako nakumtazama Rahma vizuri na kumsikiliza kwa umakini
“Walikupa Sharti gani?”
“Waliniambia kuwa nifanye juu chini niweze kukuvua pete ambayo ulikuwa umevaa mkononi,na walinipa siku saba za kuishi ndio maana ile siku ya kwanza ulipo kuja nyumbani mimi mwili wangu ulikuwa umesimama nyuma ya mlango na pale kitandani alikuwa amelala Rahma mwengine anaye fanana na mimi na ndio uliye zungumza naye na baada yaw ewe kuondoka mimi mwili wangu ukaingui kwa yule Rahma uliye mkuta kitandani.”
Maelezo ya Rahma yakanichanganya kiasi kwamba nikabaki nikiwa kimya nimemtumbulia mi-macho huku akilini mwangu nikijiuliza kwa maana huyu niliye kuwa naye ni Rahma mfu au asiye mfu
“Kwa hiyo wewe hapo upo upo vipi?”
“Eddy mimi ndio Rahma wako halisi ila Rahma mwengine yupo anaye fanana na mimi na endapo akiingia mwilini mwangu ninakuwa na hasira kama niliyo ishika jana nilipokuwa ninakulazimisha kuweza kuivua pete yako.”
Nikajikuta nikichoka pasipo kufanya kazi,hali ya mashaka ikaanza kunitawala juu ya Rahma huyu ambaye ninaonge.
“Ila Eddy kwa nini ulinificha?”
“Nilikuficha na nini?”
“Hujui kuwa wewe ndio chanzo cha haya yote”
Nikabaki nikiwa ninamtazama Rahma huku nikikosa la kunzungumza na sikjua nimwambie nini juu ya kitu anacho dai mimi ni chanzo
“Rahma unaposema kuwa mimi ni chanzo sijakuelewa una maana gani?”
“Eddy tambua ya kuwa kila ulilolkuwa ukilifanya haya ndio matokeo yake”
Moja kwa moja nikaanza kuhisi Rahma ameingundua tabia yangu ya zamani,ikanibidi niibadi-lishe mada kuepukana na mizozo ya kelele.
“Fanya basi upike msosi baby ninanjaa?”
“Sawa mume wangu ila hiyo mada tutazungumza baadaye vizuri”
“Mume wangu unanichekesha sana”
Rahma alizungumza nyuma yangu na kunifanya nigeuke na kumtazama
“Kwa nini?”
“Kwa maana wewe unajing’ang’aniza kupanda juu ya huo mti wakti unauona ni mkubwa na tangu kule ndani niliikuwa nikikuangalia jinsi unavyo paramia parami”Rahma alizungumza huku akicheka
“Kinacho kuchekesha wewe haswa ni nini?”
“Ninakucheka wewe unaye nga’angana kuapanda hapo”
Nikamtazama Rahma kwa macho ya umakini na kujikuta nikiachia msunyo ulio mnyamazisha kuchela
“Baby jamani mbona unanisunya?”
“Nenda ndani kaniletee maji ya kunywa”
“Sawa mume wangu au umechukia nilivyo kucheka?”
“Hapana”
Rahma akanisogelea na kunibusu shavuni na kuondoka kwa mwendo wa madoido,Sehemu ni-liyo simama nikaanza kuhisi mtetemeko ulio nifanya nitazame chini kwa muda.Nikajaribu kupakanyaga nikasikia mlio unao ashiria chini yangu kuna shimo.Nikaanza kuyasogeza majani mengi ya mti yaliyo kauka na nikakuta mfuniko ulio tengenezwa kwa chuma na niimara sana na juu yake ukiwa na mnyororo chakavu ulio unganika kwa pamoja
“Kuna nini hapo?”
Rahma aliniuliza huku akiwa ameshika jagi lenye maji pamoja na kikombe
“Humu ndani sijui kuna nini,ila ninahisi kuna viu muhimu sana”
“Mmmmm hembu”
Rahma akapiga hatua hadi sehemu niliyopo mimi na akanyaga mfuniko kama nilivyo ukanyaga mimi kwa kutumia mguu kisha akanitazama machoni.
“Baby iseje kukawa na madudu ya ajabu ikala kwetu?”
“Madudu gani?”
“Madudu tuu ya ovyo ovyo”
“Hakuna kitu…..Fanya hivi nenda kule jikoni kalete kile kijishoka kilicho ning’inizwa pale ukuta-ni”
“Sawa”
Rahama akakimbia kuelekea ndani na baada ya muda akarudi akiwa ameshika kijishoka nilicho muagiza na kunikabidhi.Nikaanza kuukata mnyororo kwa kutumia nguvu nyingi ila haukukatika karahisi kama nilivyo tegemea.Nikaendelea kuukata na Rahma akanipokea kishoka na yeye akaanza kukata,mpaka inafika jioni hatukuweza kuukata mnororo tukaamua kurudi zetu ndani kila mmoja akiwa amechoka kwa kiasi chake.
“Eddy pale wewe uanhisi kuna nini?”
“Mmm sijajua ila kwa historia ya Mzee Ngoda aliniambia kwa hili jumba alikuwa anaishi rafiki yake wa kijerumani so huwezi jua kuna nini?”
“Mmmmm Mungu akibariki kesho asubuhi na mapema tunamkia kwenye ile sehemu”
“Sawa mke wangu”
Tukapika chakula cha usiku na kula,kutokana na uchovu kila mmoja akalala upande wake wa kitanda huku akilini mwangu nikifikiria ni kitu gani kilichopo ndani ya shimo lenye mfuniko wa chuma.Sikuweza kupata usingizi nikiwa ninashahuku kubwa ya kutaka kujua,masaa yakazidi kukatika hadi inatimu majira ya saa nane usiku nikaanza kuhisi watu wakizungumza nje ya dirisha la chumba chetu.Nikamtazama Rahma na kumkuta amelalal fofofo,kwa ujasiri mkubwa nikasimama na kuchungulia dirishani na sikuona kitu.Nikajianza pembeni kusikilizia kama wataendelea kuzungumza wanacho kizungumza kwa lugha zisizo eleweka ila sikusikia tena.Nikarudi kitandani na kujilaza hata kabla sijajiweka vizuri nikasikia tena mazungumzo yao wakiyaendeleza na nikaanza kujiuliza ina maana wananiona ninapo karibia kwenye dirisha au ila nikakosa jibu.
“Nyinyi washenzi hapo nje ninaimani munanisikia hembu niachieni kelele zetu za kijinga”
Nilizungumza kwa kujiamini huku woga kwa mbali ukininyemelea kusikilizia jibu nitakalo pe-wa.Ukimya ukatawala kama dakika tano hivi nikaamini wameondoka gfla nikaanza kusikia kengele kubwa lenye mlio mithili ya makengele yanayofungwa kwenye minara ya makanisa likaanza kusikika likigongwa kwa nguvu kubwa.Rahma mwenzangu hana hili wala lile,kwa hasira nikanyanyuka na kuchungulia dirishani sikuona mtu zaidi ya kusikia milele ya kengele.Nikaanza kupiga hatua za kwenda nje gafla kwenye kona ya chumba akajitokeza bibi ambaye alinitibu kipindi nilipo okotwa msituni,sikustuka sana japo moyo ukanipasuka na kuyabadilisha utaratibu wa mapigo yangu ya moyo
“Shikamoo bibi”
“Marahaba……haikuwa ratiba yangu ya mimi kuja huku ila inanipasa kuja huku kukupa maagizo haya.”
“Mmmmm”
Niliguna huku nikimtazama bibi machoni mwake
“Kwenye lile shimo munalo lifungua mule kuna fugwa majini ambayo yakifuguliwa yatawadhuru walimwengu waliopo ndani ya huu mkoa hata nje ya mkoa kwa maana yanahasira na njaa kali na majini haya yanakula nyama za watu pasipo kuwa na huruma…”
“Ila kuna dhahabu nyingi ambayo ukiipata ni lazima uwe tajiri maisha yako yote wewe na kizazi chako ila sharti ni moja”
“Sharti gani?”
“Mupo wawili ila mmoja wenu ni lazima afa?”
“Nini wewe?”
“Ndio la sivyo mukifanikiwa kila kiumbe mutakacho kizaa au atakacho kibebe mke wako kitakufa tumboni mwake kwani hiyo ni kama sadaka ya majini hayo”
“Sasa bibi hakuna njia nyingine?”
“Njia nyingine ipo ila hiyo ni ngumu sana”
“Niambie tuu”
“Hiyo njia njingine ni kuweza kupata damu ya Ngamia mzee tena mwanamke…..sasa jiulize huyo Ngamia kwa hapa Tanzania utamtolea wapi?”
“Mmmmm sasa ni boara niachane na hio ishu”
“Huwezi kuacha kwa maana mumeshaanza ndio maana unazisikia kelele kama hizo huko nje hao ni watoto wa majini hayo ambao wanaweza kutoka kwenye lile shimo wakakupigia hiyo kelele ili ukawatoe wazazi wao”
“Sasa…..ahaaa bibi….”
“Na laiti ukiacha kuwafungulia matatizo ambaypo ulipia mwanzoni yataongezeka mara kumi zaidi ya ulivyo yapata”
“Ahaaa sasa bibi inakuwajee hapo”
“Ila usijali nitakupa dawa ambayo nitahitaji ujipake wewe na mwenzio usoni na mikononi pale mutakapo kwenda kukata ule mmnyororo”
“Je hao majini wakitoka itakuwaje?”
“Nitakupa fimbo ndogo yenye mamlaka ya kuwaamrisha kwa kila jambo utakalo wewe”
“Wapo wangapi hao majini?”
Bibi akakitazama kiganja chake cha mkono wa kulia sikujua anaangalia nini kisha akanitazama usoni
“Mmmmm wapo majini milioni moja,laki sina na hamsini”
Nikashusha pumzi kama nimetoka kukimbizana mbio ndefu
“Humo ndani walikuwa majini wachache ila kutokana na kuishi kwa muda mrefu wakazaliana na na kufikia hiyo idadi na kama wote hao ukishindwa kuwaongoza inakula kwako kwani watakutafuna wewe na uzao wako wote”
“Ohooo basi bwana bibi wewe nipe tuu dawa itakayo nisaidia kurudi zangu mjini na mke wangu ila si kuendelea na hiyo biashara mimi ni binadamu siwezi kuwaongoza viumbe wa ajabu kama hao”
“Mbona mfalme Suleima aliweza kuwaongoza majini na kuwaamrisha kwa kila kitu……Nahisi si mara ya kwanza kusikia neno hili kuwa nyota yako ni kubwa na inanguvu kubwa sana na inau-wezo mkubwa wa kuongoza chochote unacho kihitaji………Pia majini hao watakusaidi kupamba-na na maadui zako ambao ukiwapa nafasi tuu ya kuiteka nyota yako huo ndio utakuwa mwisho wa maisha yako”
Nikatulia kama dakika tano nikimtazama bibi huku akilini mwangu nikiwaza ni jinsi gani nina-weza kufanya kazi hii ambayo tayari imesha nipa doa katika maisha yangu kwani sikuweza ku-tegemea kama ipo siku nitakuja kufikiria kumiliki jini
“Usiogope kwani kuna mambo mawili?”
“Kuifanya nchi na dunia kuendelea kuishi katika amani au kuifanya nchi kuingia kwenye matatizo makubwa na kila kiumbe aishie ndani ya nchi na nchi zote nazo zijua ndani ya ubongo wako watapata shida kubwa sana kwani ni lazima watafumwe”
“Mmmmm sasa mke wangu atakufa?”
“Hawezi kufa pale utakapo amua kuwaongoza hao majini ila ukikataa tuu atatafunwa”
“Bibi itakuwaje na hao majini wametokea wapi?”
“Wewe ndio utakuwa ni mridhi wa Mfalme Suleiman katika hilo hii ni baada ya karne nyingi kupita pasipo kupatikana kwa mridhi wake”
“Sasa bibi hawakuona mtu mwengine zaidi ya mimi kwa maana mimi kazi yangu ni ualimu”
Nilijitete nikimsikilizia jibu atakalo nipa bibi kwa maana ni hichi kikombe cha dhambi kilichopo mbele yangu ni zaidi ya kubebe sufuria lenye uji wa moto tena kwenye kichwa chenye upara
“Kuhusu ualimu wako weka pembeni….kilichopo hapa mbele yako ni kuangalia ni nini unapaswa kukifanya”
Nikasikia sauti ya kujinyoosha nyoosha kwa Rahma kitandani na kumfanya bibi kumtazama Rahma kisha akatabasamu
“Una kitoto kizuri ila usipo kiangalia kitatafunwa na hao majini ni kazi yako kukilinda”
“Daaaaa…..bibi inakuwaje sas?”
“Hapo hakuna ya itakukuwaje kazi ni kwako kulinda nchi,mke na kizazi chako”
“Nimekubali”
Bibi akatabasamu na kunipa kichupa kidogo chenye unga unaofana na poda nyeupe,Akanipa maelekezo yote yanayopaswa kufanywa kwenye dawa hiyo ambayo ni kuipaka usoni na miko-noni kwa kiasi kidogo,pia akanipatia kifimbo ambacho ni chakuongezea hao majini
“Kitu kingine nilitaka kusahau…usije kumuambia mke wako kuwa kwenye hilo shimo kuna ma-jini kwa maana kama unavyo wajua wanawake wenu wa kisasa walivyo waoga na ataaribu kazi yote namwisho wa siku katatafunwa mbele yako”
“Sawa bibi…..ila ngoja kwanza ile pete yangu imepotea”
Bibi akanigeukia na kunitazama kwa macho makali yaliyo jaa mshangao
“Umeipeleka wapi?”
“Anivua mke wangu”
“Utakufa kwa ujinga wako nisubirie”
Bibi akaondoka kwa njia aliyo jia na mimi nikarudi kitandani huku kelele za kengele zikinyama-za kimya.Akili nzima ikawa imevurugika kila nilicho kiwaza hakuna ambacho nilikifikia maamuzi katika mawazo yangu.Baada ya muda bibi akarudi na nikanyanyuka kitandani na kumfwata alipo simama na akanionyesha pete yangu
“Umeipata wapi?”
“Si mulikuwa mumeitupa kwenye hizo bustani zenu kwa ujinga wenu”
Bibi alizungumza huku akinivalisa kwenye kidole ilipo kuwawepo
“Kumbuka hao majini hawaitaji kelele zozote za binadamu hadi ukiwaweka chini ya mamlaka yako ndio utakuwa huru kuwaongoza la sivyo watawatafuna”
Bibi akamaliza na kuondoka na kuniacha nikiwa na sinto fahamu hata kujilaza kitandani nilijilaza kama mgonjwa.Hadi kuna pambazuka sikupata usingizi wa aina yoyota.Rahma akanigeukia na kunitazama kwa macho yaliyo jaa usingizi huku akipiga miyayo
“Mume wangu umeamkaje?”
“Nimeamka powa tuu”
Nilizungumza kinyonge kwani kazi niliyo nayo si ndogo,Rahma taratibu akajisogeza kifuani kwangu na kunikumbatia na kuanza uchokozi wa hapa na pale na kuufanya mwili wangu kunisisimka.
“Mume wangu naitaji tutafute mtiti wa asubuhi asubuhi”
Rahma alizungumza huku akiaendelea na uchokozi ambao moja kwa moja ninajua ni ugonjwa wangu,ndani ya dakika kadhaa tukawa ndani ya dimbwa zito la mapenzi hadi tunamaliza mechi yetu kidogo nikawa kwenye amani
“Alafu baby kuna kitu nilisahau kukuadisia?”
“Kitu gani?”
“Kipindi ambacho nilipigwa risasi na baba si nilikuwa nina ujauzoto japo mima ilikuwa ni chan-ga?”
“Ehee”
“Basi yule Olvier Hitler alikichukua kile kiumbe chenye changu na kukiingiza kwa msicha mwengine amabaye ni jini wakidai watanirudishia tumbo langu litakapo pona”
“Mamaa weee sasa ni kwanini na wewe ulikubwali?”
“Ahaa baby unadhani ningekataa vipi wakati watu wenyewe wale ni majini”
“Mmmmm sasa mke wangu aaahaa”
Ikawa ni taarifa nyingine mbaya kwangu kwa maana moja ya njia mbazo Olvia na majini wake wanataka kunifanyia ni kuipata kwanza damu yangu.Na moja kwa moja endapo kiumbe changu kitazaliwa nilazima wataitumia damu ya mwanangu kuiangamiza dunia
“Sasaw wewe unadhani huyo mtoto atakuwa wetu kweli?”
“Hata mimi sijui mume wangu ila tumuachie MUNGU kwani si tutamzaa mwengine”
“Laiti ungejua kinacho endelea wala usinge zungumza hilo”
“Ni nini kinacho endelea”
“Utajua siku ila si kwa sasa cha msingi hapa ni kumtafuta mwangu kwa juhudi zangu zote”
“Mmmmm utampataje wakati wale ni majini na wewe ni mwanadamu?”
“Nitajua tuu jinsi ya kuwapata”
Nikanyanyuka kitandani na kuingia bafuni na Rahma akafwatia kwa nyuma na sote tukaofa ba-funi na kuvaa nguo zetu ambazo ni kauka nikuvae kwani hatuna nguo nyingine za kubadilisha zaidi ya makti tuliyo yakuta ndani ya hili jumba.Tukashirikiana kupika kifungua kinywa na baada ya kumaliza kila mmoja akawa tayari kwa kazi.Nikakimbia chumbani na kuchukua kichupa chenye dawa pamoja na kifimbo changu na kurudi sebleni na kumkuta Rahma akiwa ameshika kishoka.Nikatoa unga kidogo kwenye chupa na kujipaka usoni na mikononi kama alivyo niambia bibi
“Ni nini hiyo?”
“Wewe tulia nikupake”
Nikachuka tena unga kidogo na kumpaka Rahma kwenye uso na mikono yake na sote tukatoka nje.Tukafika kwenye sehemu lilipo shimo na kulikuta kama tulivyo liacha
Sehemu Ya 29
“Hivi Eddy kwa mfano humu tunakuta mahela cha kwanza tuakwenda kuishi wapi?”
“Mbinguni”
“Jamani Eddy ndio jibu gani hilo mume wangu?”
“Niikuwa ninakutania mke wangu,tutaishi popote ambapo wewe utahisi panafaa”
“Mimi nataka tuishi kwetu Dubai”
“Hakuna shida mke wangu”
Rahma akakaa pembeni na mimi nikaanza kazi ya kuukata mnyororo kwa kutumia nguvu zangu na kila ninapo ukata ndivyo jinsi unavyo katika,nguvu nilizo nazo leo ni tofauti sana na nguvu nilizokuwa nazo jana kwani leo ninanguvu nyingi sana kupita maelezo.Mnyororo ukakatika na kumfanya Rahma kuanza kupiga makofi akifurahia
“Baby leo unanguvu nyingi kama John Cena”
“Kwenda huko nyoo tusaidine kuufungua huu mfuniko”
Rahma akanifwata na tukaanza na kazi ya kuuvuta mfuniko huu ambao ni mzito sana na kuto-kana na kuwa na kutu nyingi ukasababisha kushikana kwenye maeneo ya pembezoni kwa mfu-niko huo.Taratibu yukaanza kuufunua kwenda juu,tukiwa tumeufunua kwa kiasi fulani tukasikia sauti ya Mzee Ngoda ikutuita huku akija katika eneo tulilopo
“Munafungua nini wanangu”
“Njoo utusaidieee”
Nilizungumza kwa sauti ya kujiminya kwani mfuniko ulituzidi nguvu,Mzee ngoda akajiingiza katikati yetu na kutusaidia kuufungua mfuniko na kwa pamoja tukafanikiwa kuufungua.Gafla tukastukia kumuona Mzee Ngoda akirushuwa juu kama kifaranga kilicho nyakukiliwa na Mwewe mwenye njaa kali na kitendo cha kutua chini hakuwa na kichwa na damu nyingi zikawa zinaruka kila sehemu na kumfanya Rahma kupiga ukulele mkali
Nikabaki nikiutazama mwili wa mzee Ngoda jinsi unavyo rusha rusha miguu,Sauti kali nikaisikia kwenye masikio yangu ikiniambia
“Mmoja wenu ni lazima afee”
Nikayakumbuka yalikuwa ni maneno ya bibi,kwa haraka nikamuwahi kumziba mdomo Rahma.
“Shiii nyamaza”
Nikaendelea kumziba mdomo Rahma kwa nguvu kwa kutumia kiganja cha mko-no.Tukayashuhudia majini yakitoka na kulizunguka eneo tulilopo sisi huku wakiwa wanaelea elea angani.Nikakitoa kifimbo mfukoni na kuwanyooshea majini yaliyojaribu kwenda mbali,
“RUDINI HAPA”
Nilizungumza kwa sauti ya ukali na majini hayo yakatii,hadi na mimi nikaanza kushan-gaa.Rahma akanikumbatia kwa nyuma,mwili mzima ukiwa unamtetemeka mithili kama ame-pigwa shoti ya umeme.Eneoa la anga zima katika eneo tulilopo limefunikwa na majini haya am-bayo ni mengi sana na yana sura za kila aina
“Tunakushukuru sana kwa kututoa”
Niliisikia sauti kwenye masikio yangu ambayo ni tofauti sana usikiaji wake kama tulivyo sisi wanadamu,Kwani sauti niliisikia ndani ya masikio yangu na si kama ile inayo ingia kwenye ma-sikia yangu.Nikawatazama kwa umakini na kuwashuhudia wakiwa akatika makindi tofauti to-fauti,Wazee sana,wazee kiasi,vijna na watoto
“Munataka nini?”
“Tulikuwa tunauhitaji uhuru,tumeupata kutoka kwako asante sana,tupo tayari kukusikiliza wewe kwa kila kitu”
Hata jini ambaye ananijibu simjui ni yupi kati ya kundi kubwa ambalo limetuzingira mimi na Rahma
“Kwa leo tunakuomba tutoke tukatafute japo kitu cha kula,kisha saa kumi na mbili tutakuwa tumerudi”
“Eddy ukiwaruhusu hawa huko kwengine mambo yatakuwa si mazuri”
Rahma aliniambia
“Kumbe hata wewe unawasikia?”
“Ndio”
“Sasa munaniahidi nini nikiwaruhusu kwenda kuchukua chakula?”
“Amani itakuwa juu yetu”
“Hamuto wadhuru wanadamu wengine kama huyu?”
“Hatuwezi fanya hivyo,tunakuahidi”
Nafsi moja inaniambia niwaruhusu na nyingine inaniambia nisiwaruhusu.Nikamtazama Rahma akatingisha kichwa nisiwaruhusu.
“Acha wakatafute kitu cha kula,unadhani hapa wakikaa watakula nini?”
“Haya kama umeoamua hivyo”
“Haya nendeni ila saa kumi na mbili jioni nawahitaji hapa”
“Turuhusu tuanze na mwili huu.”
“Khaaa”
Nikautazama mwili wa mzee Ngoda kisha nikawatazama Majini,sura zao baadhi zimejaa upole na masikitiko makubwa,wengine wapo kwenye rah asana.
“Kwanza ni nani aliye fanya hivi?”
Akajitokeza jini wa kiume mwenye mwili wa kawaida tuu na kushuka chini kitendo cha kuka-nyaga ardhi mwili wake ukakamilika kama wa binadamu wa kawaida,kwani wote anao elea elea angani miili yao imekaa kama donge kubwa la maji.Akapiga magati mbele yangu na kuinama
“Nisamehe mkuu haikuwa dhamira yangu ufanya hivi ila nilimuona kama adui yetu ndio maana nikamdhuru”
“Sawa nimekusamehe”
Akanyanyuka kwa furaha na kurudi juu na mwili wake ukafanana sawa sawa na we-zake.Nikawaruhusu na ndani ya dakika mwili wa Mzee ngoda haukuwepo mbele ya macho ye-tu,walisha utafuna.Wakaondoka kwa furaha huku wakishangilia na kutuacha mimi na Rahma
“Eddy nahisi kama nipo kitandani,naota vile?”
“Mmmm upo kwenye maisha halisi mke wangu”
“Eddy wewe umewezaje kuwaamrisha hawa viumbe kwa maana hawaeleweki”
“Wee acha tuu mke wangu”
Tukaanza kushuka kwenye ngazi zilizopo kwenye handaki tulilo lifungua,Tukakuta mafuvu mengi ya vichwa vya watu pamoja na mifupa ikiwa imesambaa chini,Mwanga wa bluu uliopo ndani ya handaki ukatusaidia sana kuyaona mazingira yaliopo humu ndani
“Baby huu mwanga unatoka wapi?”
Rahma aliniuliza kwa sauti ya kuninon’oneza
“Hata mimi sijui unatokea wapi?”
Tukaendelea kutembea kwenye eneo la handaki,lililo na eneo kubwa sana.Tukaingia kwenye moja ya ukumbi na kukuta kila kitu kilichomo ndani ya ukumbi huu kimetengenezwa kwa dha-habu,kuanzia viti,meza ukuta sakafu vipo kwenye namna hiyo.Nikataka kuokota kikombe cha dhahabu ila Rahma akanizuia
“Ona kule”
Rahma akanionyesha mzee aliye keti kwenye kiti cha dhahabu akiwa ameshika fimbo ndefu ya dhahabu huku mikononi mwake akiwa amevalia pete nyingi.Nikashika kifimbo changu vizuri na kuanza kuoiga hatua za taratibu huku Rahma akiwa nyuma yangu akinifwata.Tukafika eneo alilopo mzee huyu ambaye ni wamakamo sana,hata macho yake yanafumbuka kwa shida.
“Nikipindi kirefu sana nilikuwa ninakusubiria wewe,na leo nimekuona”
Mzee alizungumza kwa sauti ya kukwaruza kwaruza
“Nani….Mimi?”
Nilijiuliza swali na kujijibu mwenyewe na kumfanya mzee kutingisha kichwa chake
“Ndio,Imepita karne na karne nikiwa namtazamia atakaye shika falme yangu ya kuwaongoza hawa majini.Tangu ulip kuwa tumboni mwa mama yako niliweza kukulinda hadi ukafika hapa.”
“Samahani mzee wangu wewe ni nani?”
“Mimi ni mfalme wa wafalme”
Nikakaa kimya kwani jibu alilo nipa sikujua kama ndio jina lake alisi au ni mbwembwe tuu,Akasimama akisaidiwa na fimbo yake,vazi zima alilo livaa nimepabwa na dhahabu.
“Sogea karibu,Usiniogope”
Rahma akanishika mkono,nikamtazama na kumkazia macho hadi akaniachia mko-no.Nikamsogelea mzee na akaninyooshea mkono wake ulio valia pete na bangili nyingi zilizo tengenezwa kwa madini ya kila aina.Nikampa mkono wangu na kitu kama shoti kikautetemesha mwili wangui kwa sekunde kadhaa na kikaachia
“Wewe ndio mridhi wangu,Utaifanya dunia kuwa katika uwezo wako,waongoze wanadamu ka-tika njia ya kumtafuta MUNGU.Ila unakazi kubwa sana ambayo mimi niliishindwa na kujifungia humu ndani kwa siri”
“Kazi….kazi gani hiyo?”
“Nitakuambia,Jina langu ni Suleima Mfalme wa wafalme,Nilipewa uwezo mkubwa na MUNGU katika kuvitawala viumbe vyake,vya baharini na nchi kavu.Watu wengi wanatambua kuwa sasa hivi nimefariki,ndiovyo maandishi yalivyo katika vitabu vitakatifu vya MUNGU.Ila nimepewa nafasi hii ya kuonana na wewe ili roho yangu ikalale mahali salama,nikiwa nimekuachia kazi yangu ya kuendeleza mapambano dhidi ya majini 72 yalio niasi”
“Ehee nitawezaje?”
“Vizuri,Uwezo wako ni mkubwa kuliko mimi.Unasauti kubwa katika viumbe hivi kuliko mimi.”
“Mungu alinipa uwezo mkubwa sana wa kuwatawala ila hao 72 waliniasi na niliwafungia kwenye Gudulia la Shaba na kuwadumbukiza mtoni,Baada ya mimi kufa katika enzi zile wakaja kufunguliwa na watu wa Babilon ambao walikuwa wakitafuta mali na kusababisha majini hayo kuwa huru na kuleta tabu kama unayo iona katika dunia ya sasa”
“Baada ya BARBATOS na wezake kurudi katika mamlaka yao,Ndipo nami MUNGU alipo niruhusu nirudi duniani na kuwa katika handaki hili lenye udongo ulio jaa Baraka za Mungu nikisubiria wewe kuzaliwa na kuja kuwa mridhi wangu na laiti nisinge rudi basi Dunia ingezidi kuangamia”
Nikashusha pumzi na kubaki nikimtazama Mfalme Suleiman,ambaye kwa kipindi chote nilim-soma kwenye histori za vitabu tuu.
“Majina hao ni BARBATOS ambaye ni mkuu wao au Mungu wao,BAAL anamiliki mashariki mwa duni,BUER anawapa umashuhuri watu,AGARES huyu husababisha mitetemeko ya ardhi,ni mzee anatumia mamba katika kusafiria,AMON ananguvu nyingi na anamwili wa mbwa mwitu ila anakichwa cha joka lenye ndimi zinazo tema moto ila anabadilika na kuwa kama binadamu anatumika katika upatanishi wa marafiki”
“Sasa hao wote wapo wapi?”
“Duniani”
“Hao walio salia ni wafuasi tu,Kikubwa ni kupambana nao kwa kutumia hekima ambayo ume-pewa”
Mfalme Suleima kwa ishara akaniamrisha nipige goti moja chini wa mguu wa kushoto huku mguu mwengine wa kulia nikiunyanyua kidogo na kuuwekea kisuku cha mkono wa kulia na ngumi ya mkoni wikiwa imegusana na paji la uso na kuangalia chini.Akanishika kichwa na kuanza kuomba kwa lugha ambayo sikuitambua,akatumia dakika zaidi ya kumi katika kufanya maombi yake.Akavua pete mbili kidoleni mwake na kunivalisha,kwenye vidole vyangu vya mkono wa kulia,kisha akaniinua na kunivisha joho lake.
“Nimekukabidhi mamlaka yangi juu ya majini wote wema ambao nilikuwa nao humu ndani,Ila hakikisha hawatekwi na majini waliomo dunia.”
“Nitalihakikisha hilo hakuna linalo tokea”
“Kazi unayopaswa kuanza nayo ni juu ya wale wote wanaotumia nguvu za giza,kuwateka watu wa Mungu katika majengo yao waliyo yaanzisha duniani kote”
“Sawa”
Mfalme Suleiman akamuita Rahma kwa ishana,akaja na kusimama kando yangu.Akachukua pete yake nyingine na kumvisha Rahma kwenye mkono wake wa kushoto
“Pete hii inanguvu ya ushawishi na ikusaidia kumtuliza jazba pale mume wako atakapofanya maamuzi yaliyo kinyume palipo na ukweli”
“Sawa” Rahma alishukuru kwa sauti ya unyenyekevu
Mfalme Suleiman akatukumbatia kwa pamoja huku akinipiga piga mgongoni,akasogea nyuma kidogo,
“Utajiri wangu upo juu yako”
Gafla mwanga mkali ulio ambatana na radi ukjatawala ndani ya ukumbi na kusababisha teteme-ko kubwa la ardhi.Mfalme Suleiman akanyoosha mikono,wau wawili wenye mavazi meupe pee na madawa mawili mgongoni mwao wakasimama pembeni yake na kumnyayua kwenda juu hana kupotea naye na mwanga ukarudi kama kawaida.
Kila kitu kinacho endelea kwenye maisha yangu ninaona kama mkanda wa kuigiza,Tukatoka nje ya handaki na sote tukaelekea ndani.Mida ya saa tisa jioni tukasikia vishindo nje ya nyumba ikatulazimu tutoke nje kuangalia ni nini kinacho endelea.Nikakutana ana kundi la majini ninao waongoza wakikatiza katiza nje wengine wakiwa wanaelea angani.
“Kuna nini?”
Nilimuuliza mmoja wa majini ambaye alisimama mbele yangu
“Mkuu kuna hali mbaya imetoke?”
“Hali gani?”
“Wezetu wapatao 250 wametekwa”
“Wametekwa….!!? Na nani?”
“Tunakuomba utupe ruhusa tukawakomboe”
“Wapi?”
“Sehemu ambayo wapo ni kwenye kisiwa kimoja kipo karibu na bandari ya Tanga”
“Ngoja unaweza kuniambia ni nini kimetokea?”
“Mkuu twende ukajionee”
“Eddy unataka kwenda wapi?”
“Ngoja nikaone mke wangu”
Jini la kiume ambalo ninaongea naye akaniishika mikono na gafla kufumba na kufumbua nikaji-kuta nikiwa katika anga na sikuamini macho yangu baada ya kuukuta mji mzima wa Tanga uki-wa umetawaliwa na damu nyingi lizilizo tapakaa maeneo mbalimbali ikiashiria watu wengi wa-metafunwa na majini yangu.
Nikabaki nikihamaki kwani hali ilizidi kuwa mbaya,watu walikimbizama hovyo kuyaokoa mai-sha yao.Jini aliye nishika akanishusha juu ya gorofa moja la bandari.Kwa kutumia uwezo wa fimbo nilio nao nikaamaru majini wote kutulia,Wakatutii kwani maamlaka niliyo nayo juu yao yamezidi kuongezeka.Wakalizunguka eneo ambalo mimi nipo wakisubiri nini nifanye.
“Nani aliye waamuru kufanya huu upuuzi wakati niliwaachia kwa roo njema?”
Niliwauliza kwa ukali na majini wote wakaa kimya
“Aliye jijua kuwa amefanya tukio la kumla au kumdhuru binadamu yoyote ambaye ni mwema akae upande wangu wa kushoto”
Majini wakajigawa hadi mimi mwenyewe nikashangaa kwa jinsi wanavyo nisikiliza kwa umakini wa hali ya juu.
“Mkuu sisi ni wachache kati ya wale ambao wametekwa na wanadamu wenye nguvu zinazo en-dana na wewe.”
Jini mmoja alizungumza kwa sauti nzito akiwa katika kundi la majini walio watafuna watu.
“Hiyo sio mada niliyo nayo,nimeuliza ni kwanini mumewala watu wasio na hatia?”
“Mkuu wezetu ambao wametekwa walipandikizwa roho ambazo ni mbaya ndio maana wakawala watu na sisi tulio nusurika tukajua tumeruhusiwa kuwala watu ndio maana hata sisi tukawala”
Nikaangalia chini na kuona jinsi ukimya wa sehemu tuliyopo ulivyo tulia,Magari mengi yaliacha milango wazi huku mengine yakiwa yameangushwa na kuwashwa moto.
“KUMBUKA KUNA WATU WANAHITAJI MAJINI ILI KUYATUMIA KATIKA KAZI ZAO ZA KICHAWI NA WAGANGA,KUWA MAKINI NA HAO WATU.”
Sauti ya taratibu ilisikika masikioni mwangu,na ninauhakika hakuna jin lolote aliye weza kuisi-kia
“Sasa nifanye nini?”
“UNATAKIWA KUWAREJESHA KWANZA HAO 250 KAMA WALIVYO KISHA UANZE LILE AGIZO LA KWANZA ULILO PEWA.”
“Nitawarudisha vipi?”
“CHAGUA WAFUASI KUMI,NANE WAAMRISHE WAENDE KWENYE KILA KONA YA DUNIA WA-KIWA WAWILI WAWILI,KISHA WAWILI WABAKI KATIKATI YA MKOA WAKO”
“Sijakuelewa,hao nane waende pende za dunia mzima au kwa huu mkoa tuiopo?”
“KWEENYE DUNIA,WANAKWENDA KUZUIA KUBADILISHWA KWA WEZAO,NA ENDAPO WEZAO WAKIBADILISHWA ZAIDI WATAWEZA KUKUANGAMIZA KWA MAANA WANAJUA SIRI ZAKO ZOTE”
“Sawa ila wewe sijajua ni nani?”
“MIMI UTANIJUA,NI KIONGOZI WAKO NILIYE AGIZWA KUFANYA KAZI HII”
“Asante”
Nikawatazama majini na kuona wakiendelea kusubiria kitu cha kuwaambia,Nikaaamrisha jinsi nilivyo ambiwa na nikapata majini kumi vijana wenye nguvu za kutosha na wenye miili mikub-wa.Mara moja wakaanza kazi niliyo wapa,wengine nikawaruhusu warudi nyumbani na nikabaki na wawili wa kunilinda.Nikamuagiza jini mmoja kunishusha chini na akafanya hivyo.Nikaanza kukatiza maeneo ya Club Lakasa Chika na kukuta damu nyingi ikiwa imetawala sehemu nyingi za barabara.
“Mkuu,mimi ninaitwa Khadan huwa ukoo wangungu asili yetu kubwa ni ulinzi kwa binadamu wanao tuhitaji”
“Sawa”
Sehemu Ya 30
“Sawa”
Tukazunguka karibu mji mzima kuna maeneo yamesalimika kwa watu kutafun-wa.Wakanichukua hadi nyumbani,Na kumkua Rahma akiwa katika hali ya majonzi.Baada ya kuniona akanikumbatia huku akimwaga machozi
“Baby una nini?”
Nilimuuliza Rahma kwa wasiwasi huku nikiwa ninamashaka
“Eddy viumbe vyako vimeua ndugu zangu.”
Nikastuka kidogo sikujua ni vipi amezipata hizi habari
“Nani amekuambia?”
“Nimehisi tu mume wangu”
“Utahisi vipi wakati kitu haujakiona?”
Nikamtazama Rahma machoni,nikamvuta karibu na kumpiga busu la mdomoni na kuingia naye ndani.Hadi inafika jioni majini ambao walikuwa wametekwa wakawa wamerudishwa kwenye himaya yangu.Siku mbili zikapita nikiwa ninaendelea kupata kuwatamua majina na kazi zao wanazo zifanya majini ninao waongoza.Siku ya tatu alfajiri na mapema nikaanza kuwaagiza kazi husika ambayo mimi ninahitaji waweze kuifanya
“Agizo la kwanza ninahitaji muwalete hapa viongozi wote wa dini ambao hawamchi MUNGU wanamtukuza BARBATOS na wezake”
Majini wapatao hamsini nilio wakabidhi kazi ninayo hitaji wakanisujudia na kuondoka zao.
“Eddy mume wangu hao viongozi watakao letwa utawafanyaje?”
“Nitajua ni nini cha kuwafanya”
“Ila kuwa makini katika maamuzi yako”
“Usijali kwa hilo”
Ndani ya masaa mawili wakaanza kuletwa watumishi mmoja baada ya mwengine na wengine nikabaki nikiwashangaa kwa maana ni maarufu sana nchini na duniani.Idadi yao ikazidi kuon-gezeka hadi wakafikia watumishi zadi ya elfu moja.Nikamuomba Rahma kwenda ndani aniache niwashuhulikie hawa wapumbavu
“WAKATI WA HUKUMU UMEFIKA” Niliisikia sauti ikiniambia masikioni mwangu
“Niwafanye nini?”
“WAWEKE KATIKA MAKUNDI NA KILA MMOJA ATAPATA ADHABU YAKE KUTOKANA NA UDANYANYIFU ALIO UFANYA KWA WATU”
“Sasa makundi hayo yawe vipi?”
“NITAKUWEKEA KILA MWENYE KUSTAHILI ALAMA YA X NAWE UTAWEZA KUCHAGUA NI NINI CHA KUWAFANYA”
Ndani ya muda mchache watumishi wadanganyifu wengi wakawa wamewekewa alama ‘X’ kwenye mapaji ya nyuso zao.Katika kupita pita na kuwachunguza macho yangu yakakuta na baba mchungaji ambaye anashirikiana na Olvia Hitler na nimiongoni mwa waliotaka kuniangamiza,akatabasamu huku akitingisha kwa dharau nikatamani nimzabe kofi ila askari wangu akanishika mkono na kuionya nisifanye hivyo.Hakuweza kuzungumza chochote kwani nimewaamrisha majini wangu kuwafunga kauli,hii ni kuepuka kuomba misamaha isiyo na msingi wa aina yoyote.Nikawatazama kwa umakini wakiwa katika mistari ya kunyooka kama wanajeshi wa Adolf Hitler
Gafla nikaanza kuona madonge makubwa mawili ya moto yakija kwa kasi kubwa kutoka anga-ni,Majini baadhi yanayo nilinda yakapaa angani kwenda kuyazuia ila wakashindwa na kuun-guzwa miili yao
“NI WAKATI WAKO KUPAMBANA WEWE KAMA WEWE,HAO WANAO KUJA NI MAJINI WABAYA AMBAO UMEWACHUKULIA WATU WAO” Sauti iliniambia
“Nifanye nini?”
“TUMIA FIMBO KUYAZUIA”
Nikainyoosha fimbo ya dhahabu niliyo powa,Mwanga mkali ukatoka mbela ya fimbo na kusababisha madonge ya moto kujibadilisha na kuwa katika hali upepo unaokwenda kwa kasi midhili ya kimbunga cha Katrina.Upepe ukaanza kunizunguka kwa kasi na kujikuta nikiaanza kunyanyuliwa kwenda juu
“USIOGOPE ENDELEA KUPAMBANA”
“Mbona nakwenda juu sasa?”
Niliiuliza sauti ninayo isikia ila haikunijibu kitu chochote,Nikazidi kwenda juu na jinsi ninavyo-zidi kwenda juu ndivyo nguvu za mwili wangu zilivyoaanza kuniishia.Kufumba na kufumbua nikajikuta nipo katikati ya usawa wa bahari.Nikaanza kwenda chini kwa kasi kuelekea yalipo maji
Fimbo yangu ikatoweka mkononi mwangu,nikaanza kuchanganyikiwa.Nikashtukia nikigeuwa kichwa chini miguu juu na kuingizwa kwenye maji kwa kasi ya ajabu,Nikaendelea kupelekwa chini hadi nikajikuta nipo katika mji ambao siuelewi na watu waliopo ndani ya mji huu wanasura za kutisha sana.Gafla upepo ukaniachia na ukabadilika na kuwa watu wenye mikono miine mikubwa inayo tisha.Vichwa vyao vikiwa na mapembe yenye ncha kali sana
Ikaninyanyua juu na kunidumbukiza kwenye kisima chenye giza totoro,Nikaanza kushuka kwa kasi kwenye kisima hichi pasipo kufika chini.Sikuweza kuona chochote kwenye kisima kutokana na giza kali.Nikastukia nikipigwa kikumbo kikali kilicho nipeleka chini zaidi.Galfa nikaanguka kwenye ukumbi mkubwa ulio jaa watu wasio eleweka na wakaanza kushangilia,Chakushangaza sikuweza kuumia sehemyu yoyote
“KARIBU KUZIMU BWANA EDDY,NIMEFURAHI KUKUONA KWA MARA NYINGINE”
Sauti ya Olvia Hitler ilinifanya nigeuke nyuma yangu na kumkuta akiwa amekalia miili ya majo-ka mawili makubwa yanayotoa moto midomoni mwao.Akasimama huku akipiga makofi kwa dharau
“EDDY,HUWEZI KUPAMBANA NA MIMI KAMWE.MIMI SASA CHAGUA MOJA KUACHIA WATU WANGU HURU AU MKE WAKO RAHMA NA KIUMBE CHAKO HICHI NIVIANGAMIZE”
Olvia alizungumza huku akiwa amemshika mtoto mchanga ambaye sikuweza kumuona vizuri sura yake.Olvia Hitler akanyoosha mkono wake kwenye moja ya lango kubwa,ukafunguka na yakatoka majitu mawili yakutisha yakiwa na vishoka vikubwa na kuwafanya watu waliopo hapa kuanza kushangilia
Nikabaki nikiwa nikiyatazama majamaa yanayo kuja kwa mwendo wa taratibu ulio jaa vishin-do.Nikatazama vishoka walivyo vishika na kujikuta mwili mzima ukiingiwa na hufu
“NIMERUDI”
Nikaisikia sauti ambayo mara kwa mara huwa inanielekeza nini cha kufanya,
“Muda wote ulikuwa wapi hadi umeniacha nimekuja huku chini?”
“NILIKUWA NINAMANA YANGU”
“Maana gani?”
“MANAA KUU NI KWAMBA UJE KUICHUKUA DAMU YAKO KABLA HAWAJAKUDHURU ZAIDI”
“Sasa nitamchukuaje?”
“USIJALI KWA HILO”
Sauti ninayo zungumza nayo kidogo ikanipa matumaini ya kuweza huku kizimu nili-po.Nikastukia kuona watu watu wapatao sita,walio valia mavazi meupe wakiwa wamenizunguka.Mwanga mkali mweupe ukaanza kumulika katika eneo zima lililo kaa watu wanaoshangulia.Mwanga ukasababisha miili ya watu hao kuanza kupasuka vipande vipande.Majiu yaliyokuwa yakinifwata nayo yakaanza kupasuka vipande vipande.Olvia Hitler akabaki akiwa amenitazama kwa macho makali.Sikuweza kujua ni kwanini mwanga haukuweza kumdhuru,
“Mbona yule msichana audhuriki na huu mwanga”
“TUNAUA KWANZA WATU WAKE”
Watu walio nizunguka,wakaanza kazi ya kukimbia huku wakinizunguka kwa kasi kub-wa,Nikajashangaa nikianza kupanda kwenda juu hadi nikafika sehemu alopo Olvia Hitler,
“USIMUOGOPE MSOGELEE”
Nikaanza kupiga hata za taratibu huku nikiwa ninajiamini sana,Olvia Hitler akabaki akinitazama kwa macho makila
“MCHUKUE HUYO MTOTO,HAWEZI KUKUZUIA TUMEMFUNGA MWILI WAKE”
Nikaupeleka mkono wangu wa kulia alipo mtoto,Olvia hakuweza kunifanya kitu chohote zaidi ya kubaki akinishanga,Nikamchukua mtoto wangu,Jambo ambalo linaniogopesha juu ya huyu mtoto ni jinsi alivyo.Sura yake haijaendana kabisa na mimi hata mwili wake si wakawaida kama watoto wengine
“Hivi huyu ni mwanangu kweli?”
“WEWE MCHUKUE HUYO MTOTO TUONDOKE”
Sikuwa na lakuuliza zaidi ya kumchukua mtoto,Nikajistukia nikivutwa nyuma,watu walio nizingira kwakanishika na kuanza kwenda juu.Tukiwa katikati kuna sehemu nikaiona ikiwa na moto mwingi sana
“Pale ni wapi?”
“NI KWENYE ZIWA LA MOTO,WALE WOTE AMBAO WANAFANYA MAOVU WANAPELEKWA KULE.NA SIKU YA MWISHO WA DUNIA MOTO UTAONGEZEKA MARA DUFU”
“Mmmmm naweza kwenda kupaona?”
“UNA MOYO WA KUVUMILIA?”
“Kwa nini unasema hivyo?”
“KUNA HALI YA KUTISHA JE UTAWEZA KUVUMILIA?”
“Ndio”
“NITAKUZUNGUSHA KWA DAKIKA KUMI NA TANO TUU”
“Sawa”
Wakanichukua na kunipelea sehemu yanye giza kuwba,Galfa nikasikia kelele za ajabu ambazo siwezi kuzifananisha na kiumbe cha aina yoyote duniani.Kila tunavyozidi kwenda mbele ndivyo jinsi kelele zilivyo zidi kuongezeka.Gafla nikamuona mnyama mkubwa sana mwenye pembe kumi na vichwa saba na mfano wake kidogo anaendana na chui na mdomo ya vichwa vyake vimefanana na Simba.Mwili kigogo ukaanza kunitetemeka,Pembeni ya mnyama huyu nikaliona jijoka likubwa lenye vichwa kumi na mbili.Unene wa mwili wake sikuweza kuupatia mfano.Mkiwa wake unaendana na mkia wa Tai
“HILI JOKA NDILO LINALO TAWALA HUKU KUZIMU NA LINA MAMLAKA KUBWA SANA NA NDIO SHETANI MWENYEWE”
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio kiasi kwamba nikatamani kuwaambia kuwa tuondoke
“Akituona itakuwaje?”
“HATUONI KWA MWAANA SISI NI TOFAUTI SANA NA WAO,ILA ITAFIKIA KIPINDI WATATUO-NA”
“Leo?”
“HAPANA”
“Na lile jinyama?”
“Na lile jinyama?”
“LILE NDIO MKE WA LILE JIJOKA NA PALE HUWA ANAPEWA MAMLAKA NA LILE JOKA”
Tukaipota sehemu na kutokea sehemu ambayo kuna eneo kubwa lenye moto mwingi.Watu wengi wakiwa wamo kwenye bwawa la moto.Miili yao inatobolewa na funza wakubwa walio nenepa sana na wana midomo inayo fanana na nng’e,Nikabaki nikijaribu kutazama kama nita-weza kujaa baadhi ya watu ila sikuweza kuzitambua sura zao kutokana ni nyeusi sana,Vilio vili-tawala katika kila sehemu ya bwawa la moyo
“Hawa nao wamefanya nini?”
“HAWA NI WALE WOTE WANAO ENDENDA KINYUME NA TARATIBU ZA HUKU KUZIMU”
“Kivipi?”
“KUNA WATU AMBAO WANAMUABUDU SHETANI,SIKU AMBAYO WANAVUNJA MASARTI YA SHETANI BASI HULETWA HUKU,NA HUWA WANAKUFA KWA SIKU ZAO WAO WENYEWE ILA SI ZILE ALIZO ZIPANGA MUNGU”
“Mmmmm,sasa ikifika siku zao za kufa inakuwaje?”
“WANATOLEWA HUMU NA KUPELEKWA KATIKA SEHEMU AMBAYO YUTAIENDELEA”
Kila sehemu ya ziwa la moto kunamiminika uji uji wa moto kutoka juu sana,sehemu ambayo ukiitazama huoni mwisho wake.Uji unafanana sana na uji wa volcano inayo toka kwa wingi.
“UNAWAONA WELE”
Mmoja wa watu wangu walio nizunguka aliunyoosha mkono kwenye upande wa kushoto wa sehemu tuliyopo.Nikaona kundi kubwa watu wakiwa wanalia kwa vilio vya ajabu sana na miili yao ikidonolewa na mandege makubwa mawili,yenye sura za kutisha sana.Midomo yao ikiwa ni mirefu sana na inafanana na misumeno mikubwa ya kukatia mbao
“WALE NI WATUMISHI WAONGO,KAMA WALE AMBAO UMETOKA KUWAKAMATA.NA WALE WANAPATA ADHABU TOFAUTI SANA NA WEZAO”
Hali ya mandege makubwa ikawa na kazi kunyofoa nyofoa nyama za miili ya watumishi hao,kiasi kwamba kila ninapowatazama nikajijihisi ndio mwili wangu ndio unavyo nyofole-wa,Tukaendelea kwenda mbele hapo ndipo nilipokutana na mavitu ya kutisha yenye minguru-mo mizoto kiasi kwamba nikabaki nikiwa nimeyatazama,
“Ni manini haya?”
“HAO NI MAJESHI WA HUKU KUZIMU,ENDAPO SIKU KUTATOKEA VITA KATI YA MALAIKA WA MUNGU GABRIEL AKIWA NA MAJESHI YAKE BASI UJUE ANAPAMBANA NA HAYA MA-DUDE.HAPA YAMELALA ILA YAKIPEWA NGUVU NA LILE JOKA NDIO UTAONA JINSI YANAVYO FANYA KAZI”
“Mmmmm…..!!”
“USIGUNE NDIO HALI ALISI”
“Na vita hivyo husababishwa na nini?”
“UTAJUA,DAKIKA ZETU ZIMEKWASHA TUNARUDI DUNIANI”
Tukaondoka zetu na kuanza kwenda juu kwa mwendo wa kasi,Tukatokea sehemu ya bahari ambapo tuliingilia mara ya kwanza.Wakanikabizi fimbo yangu ya dhahabu,wakanirudisha hadi nyumbani huku mkono mmoja nikiwa nimembebe mwanangu.Rahma akanishangaa baada ya kuniona nikiwa nikitokea kwenye msit ulipo karubu na nyuma yetu
“Eddy ulikuwa wapi?”
“Kuna sehmeu nilikwenda mara mara moja”
“Huyo mtoto umemtoa wapi?’
“Nimemuokota huku porini”
“Mmmmm mtoto mwenyewe mbona wa maajabu ajabu hivyo?”
“Hata mimi mwenye ninashangaa,Ndio maana niliamua kuja naye”
“Eddy,hembu wape hao viumbe vyako kumla huyo mtoto”
“Ili iweje?”
“Eddy ninamashaka kabisa na huyo mtoto.Nafsi yangu hainipi jibu kabisa juu ya huyo mtoto”
Nikataka kumjibu Rahma kwamba huyu ndio kiumbe wake aliye tolewa tumboni mwake Olvia Hitler kwa madai ya kumsaidia katika kumlea
“USIDHUBUTU KUNYANYUA KINYWA CHAKO KUMWAMBIA KWAMBA HUYO NI MWANAE”
Sauti ilinionya,Nikampita Rahma na kungia zangu ndani.Nikamlaza mtoto kitandani japo ni-meambiwa kuwa ni mwanangu ila hata mimi mwenyewe nikaanza kupata mashaka juu ya mto-to.
“Eddy,yaani huyu mwanao ndio umeamua kumlaza kwenye kitanda ambacho tunalala mimi na wewe?”
“Si mtoto jamani”
“Ahaaa hembu mtafutie sehemu umuweke.kumbuka kuwa mimi ndio mshauri wako mkubwa na hii pete nilivalishwa kwa kazi hiyo.Hembu naomba unisikilize mume wangu fanya hivyo”
Nikamnyanyua mwanangu na kumpeleka chumba cha pili na kumlaza kitandani,Nikamtazama kwa muda,kichwani kwachangu sikupata jibu la kueleweka.
“Labda ni kutokana na jinsi alivyo kaa tumboni mwa jini”
Nilijisemea mwenye kimoyo moyo.Nikaufunga mlango na kutoka nje.
“NI MUDA WA KUWAHUKUMU HAWA WOTE,AKGIZA WAPELEKWE KULE KWENYE LILE ZIWA LAMOTO.ILA HAWA WATAPATA MATESO MAKALI KULIKO WENGINE KWA MAANA WANAKWENDA KULE WAKIWA HAI”
“Wote”
“WOTE NDIO”
“Hawa viumbe vyangu watarudi kweli?”
“NDIO NITAKUWA PAMOJA NAO”
“Nahitaji siku na wewe nikuone,kwa maana tunazungumza pasipo mimi kukujua”
“UTANIONA”
Nikafanya kama suti ambayo inanishauri muda wote akilini mwangu,Nikawaagiza majini kuwachukua watumishi wote.Ndani ya dakika moja watumishi wote wakapotea mbele ya macho yangu.
“Eddy wanakwenda wapi wale?”
“Kutoswa baharini.”
“Eddy mbona unafanya kazi nyingine pasipo kunishirikisha?”
“Ahaa wacha wakafe”
“Sawa,twende ukashuhudie hicho kiumbe chako huko ndani”
“Si amelala?”
“Wewe twende ukajionee”
“Ngoja nitakuja”
Rahma akaondoka akiwa amenuna.Majini walio salia nikawaamuru kuingi kwenye handaki ambalo walikuwa wakiishi na sikuufunga mlango.Nikiwa ninarudi kwenda ndani nikastukia kumuona bibi aliye nitibu akiwa amesimama mbele yangu
“Bibi nini tena?”
“Kuna tatizo?”
“Tatizo gani?”
“Umewatoa sadaka viumbe vyako.Pili unaongozwa na roho potofu na huyo unaye zungumza naye ni yule mwanaume jini uliye tembea na mke wake?”
“Nani?”
“Hilda,Si unamkumbuka vizuri?”
Mapigo ya moyo yakanienda mbio kiasi kwamba nikawa sijui nifanye nini.Bibi akabaki akiwa ananitazama
“Bibi mbona sikuelewi?”
“Utanielewa,Kumbuka nilikupa kifimbo ambacho kingekutambulisha kwa kila ambaye unazun-guumza naye kama ni mbaya kwako au si mbaya kwako,ila umekiweka na kutumia hiyo fimbo kubwa japo ina uwezo ila si wautambuzi kama ilivyo kile kifimbo changu kidogo”
INAENDELEA

