SHUSHA NYEGEZI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Chapter 1
“Ahsante Mungu umepokea Simu,”
“Nani?”
“Mimi Dorini, sijui utakuwa umenisahau! Ni shemeji yako kwa Renatusi,”
“Ooh! Mbona usiku sana sasahivi, kwema?”
“Kwema, nipo hapa barabarani nakuomba uje unifuate jamani, nitakulipa hata mara kumi ya nauli,”
“Uko barabarani peke yako?”
“Ndiyo, nimeshuka muda si mrefu, naogopa sana,”
“Sawa nakuja,”
“Ahsante sana,”
“Dakika tano tu nitakuwa hapo,”
“Mungu akubariki, nashukuru sana.”
Dorini alikata simu. Alikuwa akiongea na dereva bodaboda aliyekuwa akiitwa Kiboro.
Kabla Kiboro hajaenda kumfuata Dorini, alimtafuta Renatusi maana mchana wake alikuwa na mwanamke mwingine. Simu haikupokelewa, alimtumia jumbe fupi nyingi lakini pia hazikujibiwa, yalikuwa ni majira ya saa saba na robo. Wakati huo Renatusi alikuwa amekumbatiwa na simu zote waliweka katika hali ya ukimya (Silent).
Kiboro alimfuata Dorini akiwa ameuvaa ujasiri mkubwa maana usiku kuna mambo mengi. Dorini alifurahi kumuona Kiboro maana alikuwa akiogopa sana.
Wakati wakiwa wanashuka huku stori zikiendelea baina yao, Kiboro alikuwa akimpigia Renatusi mara kwa mara, alikuwa akiendesha pikipiki kwa mwendo wa taratibu ili Renatusi ajibu maana ilikuwa ni msala.
Dorini alikuwa ni msichana mrembo, alikuwa mweupe, mwili wa wastani lakini hapo panapomteka mwanaume ndio usipime, umbo fulani la kichokozi, lile gauni la mpira alilovaa lilimshika vizuri sana. Hakuwa na makalio makubwa lakini yalitosha kumtamanisha mwanaume.
Kiboro akampitisha Dorini nyumbani kwake, yote hayo ni kumchelewesha ili Renatusi aseme jambo lolote,
“Amehamia hapa?” alihoji Dorini
“Hapana, kuna kitu nilisahau nataka nimpelekee mtu,
“Usiku huu?”
“Sio mzigo mkubwa, yuko jirani na kwa Renatusi,”
“Sawa.”
Renatusi aliingia ndani kwake na kuanza kumpigia simu tena, Renatusi wala hakushtuka, huyo mwanamke aliyelala na Renatusi alishtuka na kuona mwanga, akakata simu na kuzima kabisa, laiti kama angesoma jumbe zilizoingia ingekuwa hatari ya mapema.
Renatusi aliona kwa jitihada alizozifanya ameshajitoa kwenye lawama. Lakini aliwaza sana, laiti kama akimpeleka lazima utatokea ugomvi. Alirudi akiwa na koti mkononi na kumpa Dorini avae,
“Shemeji, unaonaje ukapumzika hapa halafu kesho ndio twende kwa Renatusi,”
“Kwanini?”
“Nimewaza tu hivyo,”
“Au ana mwanamke mwingine?”
“Sijajua,”
“Maana wanaume hamkawii, mkiachwa kidogo tu hamuwezi kuvumilia,”
“Hamna.”
Basi Kiboro alimpa koti Dorini kisha ikabidi amwambie ukweli kuwa Renatusi ana mwanamke mwingine.
“Kiboro una uhakika?”
“Nina uhakika ila tangu nakufuata nilikuwa nashindwa nikwambie nini, naomba uvumilie na huyo mwanamke mlikuwa mnapishana sana, yaani ukitoka wewe anaingia yeye,”
“Kwanini usingeniambia kama Renatusi ananisaliti,”
“Sikuwa na namba yako,”
“Naomba unipeleke nikashuhudie,”
“Sawa, lakini naomba usiwe na jazba.”
INAENDELEA

