JICHO LA TATU
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Sehemu Ya 5
***ilipoishia***
walipoangaza macho yao kumtazama mtu huyo kafika wapi..wakastuka!!! hawakumuona tena….wakiwa bado wanatahamaki…ghafla alionekana Joshi akitokea kwenye kichaka kilichokuwa karibu kabisa na gari hilo………..walipojaribu kufyatua risasi kumlenga Joshi..tayari walikuwa wameshachelewa..Joshi aliwafyeka shingo zao kwa kutumia upanga wake… .wakafa papohapo,,,kumbe wakati wanapiga simu mtandao ukakata…. hawakukuta simu ile ilibaki hewani ikisikika kule makao makuu..
Kule ndani ya Hema,,alionekana Makala….akinyanyuka kutokea ile sehemu aliyokuwa amejificha,,akazipiga hatua za tahadhari…kuufuata mlango ili achungulie upande wa nje,,wakati huo mapigo yake ya moyo yalikiwa yakipiga kwa kasi,,huku jasho linamtiririka kama kamwagiwa maji….alipochungulia upande wa nje,,kwa mbali akaona kuna gari limesimama…akafurahi,,akajua atapata msaada wa kutoka kwenye msitu huo…..akaangaza macho yake kwa kutazama huku na kule,,hakuona dalili yoyote ya mtu kuonekana eneo hilo…akatoka ndani ya hema akazipiga hatua za haraka haraka huku akitazama kushoto kulia……alipolikaribia lile gari,,akastuka kuona watu wamo ndani ya gari hilo,,,akatazama kwa umakini akagudua watu hao..walikuwa hawana vichwa…vilionekana viwiliwili tu…..hofu ikatanda juu yake….akatimua mbio kulifuata gari hilo akafungua mlango wa upande wa dereva akamvuta yule askari aliyekuwa dereva wa gari hilo na kumtoa nje…akaingia ndani ya gari hilo akafunga mlango…akazungusha ufunguo ili gari liwake….lakini gari halikuwaka….macho yakamtoka….akaamua kufungua mlango kutoka nje….akaingia uvunguni, mwa gari hilo kwa ajili ya kujificha…
***********************
Upande mwingine kule makao makuu,,alionekana askari anayehusika na mawasiliano ya moja kwa moja na maaskari wakiwa huko porini kwa ajili ya kulinda wanyama, akajaribu kufanya mawasiliano kwenye ile simu iliyopigwa kutokea kule msituni
Makala alisikia mlio wa simu ikiita ndani ya gari hilo, kutokana na hofu kubwa aliyokua nayo hakuthubutu kutoka chini ya uvungu kuipokea ile simu….. simu iliita mpka ikakata na baaada ya sekunde kadhaa simu ikaita tena!!lakini Makala aliiacha hivyo hivyo ikiita, wazo likamjia akajiona yeye ni mjinga akajisemea moyoni,,”wacha nipokee simu hii huenda nikaweza kupata msaada..akanyanyuka haraka kutoka uvunguni mwa gari akafungua mlango wa gari akaangaza macho yake ndani ya gari hilo,, akafanikiwa kuiona simu,,alipotaka kuipokea simu ikakata
kumbe tayari alikua amekwisha chelewa!!! akajarbu kuipigia hiyo namba…lakini simu ikamwambia kuwa hakuna salio la kutosha kuweza kupiga simu hiyo….akaamua kuichukua simu hiyo akaiweka mfukoni mwake..akarudi chini ya uvungu wa gari…….akajificha.
baada ya dakika tano simu ikaita tena…akaitoa mfukoni haraka,,alipobofya kitufe cha kupokelea..simu ilikuwa imeishiwa umeme(charg) ikazimika,,Makala akajutia kwa kusema,,”USIPO ZIBA NYUFA UTAJENGA UKUTA..sasa wacha nijenge ukuta…..mimi ni mjinga kiasi gani,,,kwa nini mwanzo sikupokea simu ilipokuwa ikiita!!!
ghafla akasikia vishindo vizito vya mtu akitembia..
akastuka..hofu ikazidi kuongezeka….akasikia gari linatikiswa….akafumba macho….ili asishuhudie akiuwawa…. alipofumbua macho ghafla akaona gari linavurutwa….akaamua kulishikilia kwa nguvuzake zote…
kumbe Josgi alirudi na kulivuruta gari hilo aende akalifiche kwenye vichaka vilivyokuwa mstuni humo,,kama kunamtu anayetaka kutoroka,,basi atoke mstuni humo kwa kutumia akili zake mwenyewe,,..Makala aliendelea kushikilia kwanguvu…vyuma vilivyokuwa chini ya gari hilo…
Joshi alilivuruta gari hilo umbali mrefu sana….kwa mbali akaona kuna korongo kubwa,,akatabasamu….akazipiga hatua za haraka haraka huku akilivuruta gari hilo akalitupe kule chini ya korongo…..Makala alipotazama ni wapi Joshi anaelekea,,akaona Joshi anaelekea kwenye korongo lililokuwa na mteremko mkali…akastuka macho yakamtoka…..akajilaumu kwanini asingebaki palepale lilipokuwa limesimama gari….
*************************
upande mwingine kule makao makuu…alionekana mkuu anayehusika na kitengi cha wanyama pori…akiamuru….askari waende kwenye msitu UNGEBO kuwaokoa maaskari waliokuwemo ndani ya msitu huo……..
akamteuwa MICHAEL awe kamanda mkuu aongoze kikosi kitakachokwenda msitu UNGEBO..
zikaruka ndege mbili..zilizokuwa na maaskari watatu kila ndege moja…kuelekea msitu Ungebo
Michael na maaskari saba wakaingia ndani ya gari na kuianza safari ya kuelekea msitu Ungebo..
***********************
kule mstuni,,Joshi alionekana akiendelea kuliviruta gari akakaribia kabisa kwenye korongo…Ghafla akasikia mngurumo wa ndege….akanyanyua shingo yake kutazama angani…..
wakati huo huo..kule angani..alionekana askari mmoja..akiwa ameshikilia Darubini(BINOCOLUS)
Akitazama upande wa chini kwa kupitia darubini hiyo..akastuka kumuona mtu mrefu anavuruta gari..alipotazama kwa umakini..akaona viwiliwili vya maaskari vikiwa havina vichwa..ndani ya gari hilo….akazungusha (ZOOM)darubini ili kumuona yule mtu ni wa aina gani..ananguvu gani za kulivuta gari zito aina ya JEEP!!!akastuka kuona mtu huyo…hana sura…usowake ulionekana kama nyama mbichi……akasema,,”WEKA SHABAHA,, SHAMBULIA….bila kupoteza muda Rubani wa mdege hiyo ya kijeshi..aliweka shabaha akaanza kumshambulia Joshi kwa kubonyeza kitufe cha kufyatulia risasi mfululizo….
risasi hizo zilitoka nyingi nyingi kama mvua….
Risasi hizo ziliingia kila mahali kwenye mwili wa Joshi….akaamua kuliachia gari na kutimua mbio akatokomea mstuni…hapo ndipo walipoamsha hasira za Joshi!!! alikasirika sana……akaanza kung’oa miti kwa hasira huku akipiga kelele zilizotoa mngurumo mkubwa wa kutisha….akachukua mti mkubwa alioung’oa akauvunja katikati..akaurusha angani kuilenga ile ndege iliyokuwa ikimshambulia…..mti huo uligonga pembeni ya ndege…na kung’oa injini moja ya ndige hiyo..ikapoleza uelekeo na kudondoka kuelekea chini kwenye korongo ikaripuka…..wakati huo Makala alikuwa bado yupo kule chini ya gari….akitetemeka kwa uwoga…haja kubwa na ndogo zilimtoka mfululizo……
*****************
Upande mwingine alionekana Michael akiwa pamoja na maaskari saba(7) wakianza kuingia ndani ya msitu huo…. wakasikia sauti ya mripuko mkubwa!!!!….wakati bado wanataamaki..ghafla kuna mti mkubwa uliong’olewa ukarushwa na kutua mbele ya gari lao njia ikaziba na mti huo….
Michael pamoja na wale maaskari saba..wakastuka…wakashuka kutoka ndani ya gari haraka….wakaweka sawa bunduki zao..tayari kupambana na chochote kitakachotokea mbele yao…Michael akasema,,”Hakuna kurudi nyuma tusonge mbele kuhakikisha tunawaokoa maaskari waliokuwemo kwenye msitu huu..SAWA??
wale maaskari saba hawakuwa na budi kutii amri ya kamanda mkuu wa kikosi hicho…..wakaanza kuzipiga hatua kusonga ndani zaidi ya msitu huo…
walizipiga hatua kwa tahadhari…huku wakiwa katika mstari mmoja..
walitembea mwendo wa lisaa lizima,,lakini hawakufanikiwa kumpata askari hata mmoja…wakazidi kusonga mbele zaidi…..wakatokezea kwenye lile Hema….wakalifuata na kuimgia ndani ya Hema hilo kwa tahadhari huku maaskari watatu wamebaki nje..kwa ajili ya kulinda usalama…
miongoni mwa wale maaskari wanne(4) alikuwemo kamanda mkuu Michael…wakaona vitu vimevurugika huku matone ya damu yakiwa yamedondoka chini…wakastuka!!! Michael akasema kunatatizo ndani ya msitu huu..akafanya ishara ya kuondoka,,kisha wakatoka nje huku bunduki zao wameziwaeka tayari kwa kupambana. wakasonga mbele….
***********************
Upande mwingine alionekana Makala akiwa bado yupo kule chini ya gari…akatazama pande zote..akaona ukimya umetawala..akaamua kutoka chini ya uvungu wa gari hilo..na kuanza kutimua mbio..wakati anakimbia akatereza na kuanza kuserereka kuelekea chini ya korongo….alijigonga kwenye mawe mpaka akafika chini kabisa ya korongo hilo akajingonga kwenye jiwe upande wa kichwani akapoteza fahamu……
*********************
Upande mwingine walionekana watu wanaoishi mstuni…watu hao walikuwa wametoboa masikio yao na kuweka vipande vikubwa vya miti…yakaonekana kuvutika na kuwa marefu…walikuwa wameshikiria mikuki ikiambatana na upinde mishale….watu hao walijulikana kwa jina la jamii ya WAKOLOLO…walikuwa wamevalia ngozi za nyani!!! kufunika sehemu zao za siri…kwenye jamii hiyo..hakuwahi kukanyaga binadamu wa kawaida na akatoka akiwa hai katika ardi hiyo…watu hao waliishi kwa kula matunda na wanyama pori….
siku ya leo wawionekana vijana shupavu wa jamii hiyo ya WAKOLOLO wenye umri wa kuanzia miaka kumi na minane na kuendelea…wakizipiga hatua kwenda kutafuta kitoweo…..kutokana na ukame mkali..wanyama walilazimika kwenda mbali kutafuta majani mabichi pamoja na maji…hivyo jamii ile walipata vitoweo kwa tabu..walikuwa wakitembea maili nyingi kwenda kutafuta vitoweo..
Sehemu Ya 6
Upande mwingine alionekana Joshi akizidi kusonga mbele zaidi kuingia ndani kabisa ya msitu huo huku kashikilia upanga wake mrefu…akiwa anatembea akakutana uso kwa uso na mnyama chui..Joshi akapandwa na hasira akakumbuka kapoteza jicho lake kwa kuraruriwa na chui…akarusha upanga wake..ukaenda moja kwa moja mpaka ubavuni mwa chi huyo…chui akalia kwa sauti kali….kutokana na maumivu makali aliyoyapata..akatimua mbio huku upanga huo ukining’inia huku sehemu ya upanga huo ikiwa ndani ya ubavu wa chui huyo…alikimbia lakini hakufika mbali akadondoka chini…Joshi akamfuata,,alipomkaribia akauchomoa upanga huo..akazamisha vidole vyake kwenye jicho moja la chui huyo akalinyofoa jicho…na kulipachika katika lile sehemu iliyokuwa wazi ya jicho lake moja…kisha akachana kipande cha nguo yake akajifunga kichwani kuizungu sehemu ya paji la uso mpaka jichoni…akazipiga hatua na kusonga mbele zaidi…..
**************************
upande mwingine alioneka Michael akiwa na wale maaskari saba(7) wakizidi kusonga mbele huku macho yao yakitazama kwa tahadhari kubwa…wakakutana na Fisi wengi kiasi wakiwa wamezunguka wakionekana wanakula….wakawastua wale fisi kwa kuponda jiwe,,,lile eneo ambalo fisi hao walikuwa wamelizunguka,,
wale fisi wakatimua mbio na kutokomea mstuni…
Wakastuka kuona maiti ya askari ikiwa haina kichwa ndiyo ilikuwa chakula cha fisi hao….wakasikitika sana pia hofu ikaanza kuwaingia wakaanza kuwa makini zaidi…wakati bado wakiwa wanaitazama maiti hiyo…….kunaupanga ukarushwa kutokea kwenye kichaka..upanga huo ulikwenda moja kwa moja mpaka kifuani mwa askari mmoja…..akapoteza maisha papohapo hata bila kuvuta pumzi…..
wale maaskari wengine sita wakatimua mbio wakamuacha Michael akiwa kasimama..
*****************
Upande mwingine,,alionekana Makala…akiwa bado yupo pale chini alipodondoka na kupoteza fahamu……yale matukio ya mauwaji ya wafanyakazi wezake yalizunguka katika ubongo wake!! ghafla akizinduka akapata fahamu,,hakutazama kushoto wala kulia…alinyanyuka na kutimua mbio….akapanda korongo kuelekea upande wa juu..na baada ya nusu saa alifanikiwa kutoka ndani ya korongo hilo….akaanza kutimua mbio….kabla hajafika mbali akakutana uso kwa uso na wale watu jamii ya WAKOLOLO. wakiwa wameshikilia mikuki,,wengine wakiwa na upinde na mishale……
watu wale wakamtazama Makala kisha wakaanza kuwasiliana kwa lugha yao……wakati huo Makala alibaki kasimama akitafakari nini cha kufanya…mara ghafla watu wale wakaanza kumfuata huku wakipiga lele na kuongea lugha yao…….Makala akaingiwa na hofu kubwa akaanza kutimua mbio ghafla akajikwaa na kudondoka chini………..
akanyanyuka haraka akaendelea kutimua mbio….
akaonekana mtu mmoja wa jamii ya WAKOLOLO..akiweka mshale kwenye upinde..akauvuta…ghafla ikasikika sauti ya mkuu wa vijana hao akiongea kwa lugha yao,,akimaanisha,,”Muache hawezi kukimbia na kufika mbali…wengine piteni upande huu,,na wengine piteni upande mwingine…mumzunguke…
lile kundi la vijana wa jamii ya wakololo wakatii amri ya mkuu wao,,wakatimua mbio huku kila mmoja akipita njia yake….kwenda kumnasa Makala..
*******************
upande mwingine,,kule alipokuwa amesimama kamanda Michael…alistshajabu kumuona Joshi akija upande wake huku akizipiga hatua za kikakamavu…Michael akaanza kumshamburia kwa kufyatua risasi kuelekea upende ambao joshi alikuwepo!! akashangaa risasi zilingia kwenye mwili wa Joshi lakini bado akaendelea kumfuata..
Michael akaona mambo yamekuwa magumu akaamua kutimua mbio na kutokomea mstuni..
Joshi akaendelea kuzipiga hatua mpaka pale alipokuwepo yule askari aliyechomwa na upanga..
alipomkaribia akachumua ule upanga…kwenye mwili wa askari huyo…
akazipiga hatua kwenda kumnasa Michael pamoja na wale maaskari waliokuwa wamekimbia na kutokomea mstuni humo…..
***********************
wakati huo huo walionekana wale maaskari wakiendelea kutimua mbio ili kunusuru uhai wao..
wakaona kichaka kikubwa kilichozungukwa na miti mingi iliyo ota kwa karibukaribu…wakaamua kuingia ndani ya kichaka hicho na kujificha…
Upande mwingine alionekana Kamanda Michael akititua mbio….akaamua kupanda juu ya mti akatazama huku na kule huenda akaona njia ya kutoka ndani ya msitu huo…..alipotazama kwa mbali aliliona lile gari walilokuja nalo mstuni humo..akakumbuka kuwa,,ndani ya gari hilo walibeba silaha nzito za kivita….akashuka haraka kutoka juu ya mti akatimua mbio kulifuata gari hilo….baada ya dakika kadhaa alifanikiwa kulifikia gari hilo akafungua mlango akachukua silaha maalumu kwa kutungulia ndenge angani…ROCKET RANGER(RPG) akaweka kombora moja ndani yake pia akabeba kombora jingine akaliweka ndani ya begi..
wakati huo alionekana Joshi akija upande huo huo…safari hii Joshi aliongeza kasi ya kutembea….
*******************
upande mwingine alionekana Makala akiendelea kutimua mbio…..ghafla wale wakololo wakajitokeza mbele yake wakamuweka katikati yao……Makala akapagawa…..akajiuliza nini cha kufanya…
akaonekana yule mkuu wa vijana hao..akizioiga hatua kumfuata makala,,,lipomkaribia akaongea lugha ya Kikololo,,,Makala aliweza kuelewa baadhi ya maneno yaliyotamkwa..kwa sababu Makala alikuwa akisoma vitabu kudadisi na kutaka kujua makabila pamoja na jadi zao….akajibu kwa kuongea Lugha yao!!! yule mkuu wa vijana hao wa wakololo akastuka akamtazama Makala kwa macho ya msisitizo….akanyoosha mkono wake juu akiwafanyia ishara wenzake,,wasimdhuru Makala…wale wakololo wengine wakastahajabu….lakini hawakuwa na budi kutii amri ya mkuu wao….wakamchukua Makala kumpeleka kwenye kijiji cha Wakololo…..Makala akaanza kuingiwa na imani kiasi…akajipa moyo kuwa yupo katika mikono salamaa…..wakololo
walipofika kwenye kijiji chao wakampeleka Makala moja kwa moja mpaka kwa MTEMI wa jamii hiyo..
yule mkuu wa vijana akaanza kuongea na Mtemi kwa lugha yao….mtemi akanyanyuka nakumtazama Makala kwa umakini huku akimzunguka……….akaamuru Makala apelekwe kwenye nyumba iliyotengenezwa kwa miti awekwe humo…..
************************
upande mwingine alionekana Michael akizipiga hatua za tahadhari…kumuwinda Joshi huku akiwa amebeba begani ile silaha maalumu ya kutungulia ndege(RPG) alimuwinda Joshi lakini hakufanikiwa kumpata….hatimae usiku ukaingia….
upande mwingine walionekana wale maaskari sita waliobaki hai miongoni mwa wale maaskari saba aliokujanoa Michael….maaskari hao waliendelea kujificha ndani ya kichaka hicho tangu mchana….
**************************
Upande mwingine,,kule kwenye kijiji cha Wakololo alionekana Makala ameketi kwenye ngozi ya simba,,iliyokaushwa ndani ya ile nyumba iliyotengenezwa kwa miti…
kwa mbali alionekana mwanamke mmoja akizipiga hatua,,huku akiangaza angaza macho yake huku na kule…
mwanamke huyo aitwae,,,VIDA kumbe ni bimti wa pekee wa MTEMI wa Wakololo,,,,mwanamke huyo aliinekana kuvutiwa kimapenzi na Makala Tangu alipomuona mchana akiletwa na vijana wa jamii hiyo ya wakololo….
mwanamke huyo alizipiga hatua akafungua mlango wa nyumba aliyokuwemo Makala…
Makala akastuka kumuona mwanamke ameingia ndani ya nyumba hiyo iliyokuwa na vyumba viwili..vilivyotenganishw…..Vida alikuwa kavalia ngozi ya nyani iliyokuwa imefunika sehemu zake za siri huku makalio yakiwa wazi pamoja na matiti..akamsogelea Makala…
wakati huohuo alionekana Mtemi akiwaamuru walinzi wake wa karibu wakamuite Vida anamaingezi nae.
wale walinzi walipoingia chumbani kwa Vida hawakumkuta,,wakamtafuta kila kona..hawakufanikiwa kumuona vida.. wakarudi kwa Mtemi kutoa taarifa kuwa Vida hayupo..Mtemi akastuka akahisi huenda binti yake hayupo katika sehemu salama!!! akaamuru vijana wote wamtafute Vida usiku huohuo..na popote watakapomkuta…wahakikishe wanamrudisha haraka iwezekanavyo…..akasema,,”mtu yeyote atakayekutwa na binti yake…akamatwe…na kunyongwa hadharani…..
msako ukaanza……….
Sehemu Ya 7
Upande mwingine alionekana Michael,akiwa bado yumo ndani ya kichaka kajificha…..upepo ulikuwa ukivuma kwa kasi kutokana msitu huo ulikuwa na miti mikubwa….
upepo huo ulisababisha baridi kali..na mbu pamoja na wadudu watambaao/siafu walimng’ata Michael lakini hakuwa na namna alivumilia.akakumbuka mafunzo na mateso kipindi amejiunga na jeshi…ghafla zikaanza kusikika ngurumo za radi…..wingu likaanza kutanda na kuzifunika mbaramwezi na nyota…giza likatanda ghafla Mvua ikaanza kunyesha….
ilinyesha mvua kubwa kupita kiasi…
*******************
Upande mwingine walionekana wale maaskari sita waliobaki…wakiwa bado wamo ndani ya kile kicha walichokuwa wamejificha tangu mchana..mvua iliwanyeshea…ikiambatana na baridi kali sana..wakaanza kutetemeka……mmoja kati yao..kumbe alikuwa anasumbuliwa na kifua…..huwa kinambana na kushindwa kumpumua,,,,akipigwa na baridi kali…….ghafla akaanza kushindwa kupata pumzi…akahangaika sana..wenzake walijitagidi kumsaidia kwa kumkumbatia kwa pamoja wakamuweka katikati,,,lakibi haikusaidia…na baada ya dakika kadhaa..askari huyo alikata Roho….wale maaskari wenzake waliskitika sana wakajikuta wanadondokwa na machozi bila kutarajia,,wakabaki maaskari watano.
mvua iliendelea kunyesha kwa kasi kubwa…walitamani ardhi ipasuke watumbukie ndani yake…..
*************************
Upande mwingine alionekana Vida akiwa ameketi kando ya Makala huku akimtazama kwa macho ya kimitego mitego(kimahaba) vida alishindwa kuongea na makala kutokana kila alichomwambia Makala,,,Makala alibaki kimya bila kujibu…kutokana na lugha aliyokuwa akiitumia Vida kuongea nae,,,Makala aliweza kuyaelewa maneno machache…lakini akaagundua kuwa Vida anamtamani kimapenzi….uzalendo ulimshinda Vida akaanza kumtomasa Makala….
Makala alijizuia,,kwa sababu alikuwa anampenda sana Norega…hakuwahi kufikilia kumsaliti mkewe.
Kumbe wakati Vida anatoka chumbani kwake kuelekea kwenye nyumba aliyokemo Makala…
SUBI alisikia mlango wa chumba cha Vida ukifunguliwa….Subi ni mama mzazi wa Vida….akaamua kufatilia ili abaini binti yake anaenda wapi usiku huo!!! akamuona binti yake anaingia kwenye ile nyumba alipomokuwemo makala…..Subi akazipiga hatua za kunyatia…akazunguka nyuma ya nyumba hiyo…
kutokana nyumba hiyo ilitengenezwa kwa miti…..Mama Vida aliweza kuchungulia na kuona kila kitu kilichokuwa kinaendelea mule ndani……macho yakamtoka…kumuona binti yake anamlazimisha Makala kufanya nae ngono….akaamua kuondoka aende akamshtaki Vida kwa Baba yake…lakini alipoingia upande wa ndani ya nyumba…akamkuta Myemi ambaye ni mumewe anafanya matambiko yake……na alishasema tangu mwanzo..kuwa kama akiwa anafanya matambiko….asiongeleshwe na mtu yeyote hata mkewe……
Mama vida akaingia chumbani akaketi kumsubiri Mumewe amalize kufanya matambiko,,ili amueleze kile alichokiona vida anakifanya..
********************
wakati huo huo kila kijana wa jamii ya wakololo alikuwa kashikilia kitani cha moto..kilichotengenezwa kwa mti,,huku upande wa juu kumefungwa kwa kuzungushiwa kamba zilizochunwa kwenye magome ya miti..na kupakwa mafuta ya wanyama…
vijana hao wakaingia mstuni zaidi kumtafuta vida,,binti Pekee wa Mtemi…walitafuta kwa muda mrefu sana mpaka majira ya saa nane za usiku,,lakini hawakuweza kufanikiwa kumpata vida,,wala hawakuona dalili yoyote ya vida kuwepo maeneo hayo..wakaamua kurudi kule kijijini kwao,,ili wakatoe taarifa kwa Mtemi kuwa,,hawajafanikiwa kumpata vida…..wakiwa njiani wanarudi alionekana mkuu wa vijana hao wa kikololo,,,akiwa nwenye mawazo mazito,,alikuwa akitafakari neno la kumwambia MTEMI….kwa sababu Mtemi wao huwa hataki kusikia kauli ya kushindwa….endapo akitoa agizo….ni lazima litekelezwe na endapo wakishindwa kufanya walichoagizwa,,huwa anawachinja bila huruma vijana kadhaa wa kikololo……waliendelea kuzipiga hatua kurudi kule kijijini…..hatimae wakafika,,,lakini yule mkuu wa vijana hao..akasema,,”kabla sijaenda kutoa taarifa kwa Mtemi,,,itabidi tukague nyumba moja hadi nyingine..huenda Vida yupo hapa hapa kijijini….wakaanza kufanya msako kwenye nyumba moja baada ya nyingine…..walimtafuta vida bila mafanikio….mkuu wa vijana hao akapagawa….lakini hakuwa na namna ya kufanya….akazipiga hatua kuufuata mlango wa Mtemi ili akatoe taarifa….ghafla wazo likamjia akasita kutembea akageza shingo yake na kuitazama nyumba iliyo kuwa mbali kidogo na hapo alipo……akajisemea moyoni,,”hiyo nyumba hatujaikagua..yawezekana vida akawemo ndani ya nyumba hiyo….
pia akawaza kuwa,,huenda Makala katoroka na vida….
akapaza sauti,,”akaongea kwa lugha yao akimaanisha waende kufanya msako kwenye ile nyumba iliyotengenezwa kwa miti,,
nyumba hiyo ndio ile nyumba aliyokuwemo MAKALA pamoja na VIDA……
wale vijana wa Kikololo wakatii amri ya mkuu wao,,wakazipiga hatua kuifuata nyumba hiyo.
wakati huo huo alionekana Vida akiendelea kumpapasa Makala.,
Makala akaongea kwa sauti ya ukali nakusihi acha hilo jambo unalotaka kulifanya Vida akastuka ingawa hakuelewa lugha aliyoitumia Makala lakini akagundua kuwa makala hataki yeye afanye jambo hilo.
kitendo hicho kilimfanya Vida akose furaha kwa sababu mwili na hisia zake zilikua tayari kufanya ngono na Makala ,Vida akachukia akanyanyuka kwa hasira .
Upande wa nje wa nyumba hiyo walionekana vijana wa Kikololo wakiizunguka nyumba hiyo huku wakipiga kelele za mayowe kwa lugha yao, Vida akastuka akaingiwa na hofu baada ya kujua mayowe hayo yakiashiria hali ya hatari akamtazama makala kwa macho ya mshangao!! Vida akatimua mbio huku akinyata akaingia kwenye kile chumba kingine akajificha chumba hicho kilikua na makololo mengi yakiambatana na ngozi pamoja na pembe za wanyama mbali mbali
******************
Upande wa nje ya nyumba hiyo….alionekana yule mkuu wa vijana hao wa kikololo akiwaamuru vijana watatu kuingia ndani ya nyumba hiyo wafanye msako…ni kitendo cha sekunde wakafungua mlango na kuingia upande wa ndani..wakamkuta Makala…..ameketi wakaanza kuangaza angaza macho huku na kule….hawakumuona Vida!!! Makala akaanza kuingiwa na hofu…wale vijana watatu wakaingia kwenye kile chumba alichokuwemo Vida..wakaangaza angaza macho lakini hawakumuona vida…
kijana mmoja kati ya vijana hao watatu,,akazipiga hatua kuelekea kwenye zile ngozi zilizokuwa zimepangwa…..akaangaza angaza macho lakini hakumuona Vida,,,kumbe Vida alikuwa amejificha kwenye kona ya chumba hicho na kujifunika ngozi ya chui iliyokuwa imekaushwa……
Sehemu Ya 8
wakati anazipiga hatua kutoka hapo…akasita akahisi kitu,,,akawaita wenzake kwa lughatq yao….akimaanisha waje wasaidiane kuzitoa ngozi hizo ili watazame huenda Vida kajificha chini ya ngozi hizo……
wale vijana wawili wakaja haraka…wakaanza kutoa ngozi moja moja…..lakini kijana mmoja akasema kwa lugha yao akimwambia yule yule kijana aliyewaita,,akimaanisha,,”utakuwa umeona vibaya hakuna mtu hapa…..wakarudisha haraka ngozi hizo…..kwa kuzipanga.
walipomaliza wakazipiga hatua kutoka nje ya chumba hicho…….
Vida aliendelea kujificha lakini uzalendo ukamshinda kutokana na joto na harufu kali ya ngozi hizo za wanyama pia alianza kukosa pumzi..akakurupuka akanyanyuka huku akikohoa kwa nguvu….
sauti ya Vida ikasikika…vyema kila mtu aliweza kusikia sauti ya vida akikohoa…..
wakarudi haraka ndani ya chumba kile..wakamkuta Vida wakamsisitiza atoke aende kwa baba yake anamaongezi nae…..
hawakuweza kumgusa wala kumkamata Vida..kwa sababu ni mwiko kumgusa binti wa Mtemi…isipokuwa Mwanaume atakae kuwa Mume wake…..Vida akatoka ndani ya chumba hicho,, akazipiga hatua kuelekea kwa baba yake huku akilindwa kwaulinzi mkali……
Yule mkuu wa vijana hao akaingia ndani ya nyumba hiyo akamfuata Makala..akamtazama kwa macho ya huruma kisha akamuingelesha makala kwa lugha yao akimaanisha,,”Nasikitika sana kwa sababu unamasaa machache ya kuishi,,,alipomaliza kuongea hivyo akaondoka zake akimuacha Makala bado kaketi..lakini kitu kilichomshangaza zaidi Makala,,,alipomuona mkuu wa vijana wa kikololo akifunga mlango huo kwa nje…….Makala alistuka akajaribu kukumbuka Hayo maneno yanamaana gani? kwa sababu alishawahi kusoma historia ya jamii hiyo katika kitabu…hivyo alikuwa anaelewa baadhi ya maneno ua lugha hiyo…..ghafla akastuka akanyanyuka haraka..baada ya kukumbuka maana ya manenk hayo kwa kiswahili..macho yakamtoka akaingiwa na hofu kubwa kupita kiasi,,mapigo yake ya moyo yakaanza kupiga kwa kasi huku jasho linamtoka…akajisemea moyoni,,”Inamaana nitakufa!!!!????
*****************
upande mwingine alionekana Subi(mke wa Mtemi)
akijilaza kwenye kitanda kilichotengenezwa kwa miti kikiwa kimetandikwa kwa manyoya mengi ya ndege….na upande wa juu zikatandikwa ngozi mbili za mnyama simba.. Subi alikuwa akisubiri mumewe amalize kufanya matambiko ili amueze kile alichokuwa anakifanya binti yake wa pekee..
akajikuta amepitiwa na usingizi akasinzia kabisa bila kuongea chochote na mumewe..(Mtemi)
wakati huo alionekana Vida akiingia ndani ya nyumba…akamkuta baba yake(Mtemi) ameketi kwenye kiti baada ya kumaliza kufanya matambiko….Mtemi akasema,,kwa lugha yao akimaanisha,,”ulikuwa wapi?Binti yangu kipenzi!
nilikuwa na wasiwasi huenda umepatwa na jambo baya….kabla Mtemi hajamaliza kuingea,,akaja yule mkuu wa vijana wa kikololo..akatoa heshma kwa Mtemi kisha akasema,”tumemkuta kwenye ile nyumba tuliyomuhifadhi yule mtu tuliemkuta kule mstuni….
Mtemi akakasirika sana,,,akajisemea moyoni…yani huyu mwanaharamu anathubutu kumgusa binti yangu….hii ni Fedhea!! akaongea kwa ukali kwa kusema,,”nenda kamfunge kamba…na awekewe ulinzi wa kutosha ili asije akatoroka…..na itakapofika kesho asubuhi Anyongwe hadharani mlaka kufa ….
****************
upande mwingine kule mstuni alionekana Joshi akizipiga hatua za kikakamavu usiku huohuo akisonga mbele zaidi….aliweza kuona vyema kutokana na lile jicho la chui alilolipachika kwenye jicho baada ya kulilinyofoa.. jicho lake….
kwa sasa akawa na uwezo mkubwa wa kuona vizuri hata akiwa mbali….
alizidi kusonga mbele ….alitembea umbali mrefu mpaka pakakukucha…..kwa mbali akasikia kelele za watu wakiimba kwa kilugha akaamua kuelekea upande huo ambao kelele hizo zinapotokea……alipokaribia akaona watu wamekusanyika kumzunguka mtu aliyekuwa amesimama juu ya meza iliyotengenezwa kwa miti…huku kafungwa mikono yake kwa kamba. pia akamuona kijana mmoja wa kikololo akimvika kamba shingoni yule mtu aliyesimama juu ya meza hiyo…Joshi akatabasamu akazipiga hatua za haraka haraka kuwafuata watu hao….
Alionekana yule kijana wa kikololo akiendelea kuifunga kamba balabala juu ya mti ikitokea kwenye shingo ya Makala. watu wa jamii hiyo ya wakololo walikusanyika kushudia tukio hilo huku wakiimba nyimbo kwa lugha yao, Makala akavuliwa nguo zote nakubaki uchi wa mnyama tayari kwa kunyongwa….watu hao waliendelea kuimba kwa lugha yao huku wakipiga kelele wakimsubiri mtemi aje kutoa amri Makala anyongwe..
Ghafla ulionekana upanga mrefu uliorushwa kutokea msituni, upanga huo ulikwenda moja kwa moja mpaka kwenye shingo ya yule kijana aliyekua anamfunga kamba Makala….akandondoka chini na kupoteza maisha papo hapo .,wale watu jamii ya wakololo wakashtuka na kutazama ule upande ambao ule upanga umetokea, wakamuona mtu mrefu mwenye sura ya kutisha akizipiga hatua kuja huo upande walipo .Wakaanza kurusha mikuki huku wengine wakirusha mishale, walirusha mikuki na mishale mingi mfululizo .
Mishale na mikuki iliingia kwenye mwili wa Joshi lakini Joshi aliichomoa na kuitupa chini pia alichomoa mikuki na kuirusha kule walipokuwepo wakololo.,
Wakati huo huo alionekana Makala akihangaika kujinasua kutoka kwenye kitanzi akafanikiwa kukata kamba zilizofungwa mikononi mwake ,akazua kitanzi (kamba iliyokua imefungwa shingoni mwake), akaanza kutimua mbio. Kutokana na mwili wa Makala kua mnene na kitambi ,Makala alipata wakati mgumu kukimbia kwa kasi akajikuta anadondoka mara kwa mara, kwa mbali alionekana Mtemi akiwa amesimama nje ya mlango wake macho yalimtoka akastaajabu kumuona Joshi.
***********
Upande mwingine kule msituni walionekana wale maaskari watano wakichimba shimo ndani ya kichaka hicho kwaajili ya kumzika mwenzao ….walipata wakati mgumu sana kutokana walikuwa hawana vifaa vya kuchimba shimo…wakaamua kuchimba kwa kitumia panga zao fupi..walizokuwa wamezifunga kwa mkanda…kwenye viuno vyao,huku wakiutoa udongo nje ya shimo hilo kwa kutumia mikono yao. iliwachukua masaa manne mfululiizo mpaka wakachimba shimo la urefu wa futi nne(4) walipomaliza wakamzika na kulifukia shimo hilo..wakatoka kwenye kichaka hicho na kuanza kutafuta njia ya kutoka kwenye msitu huo..walizipiga hatua huku macho yao yakitazama kwa tahadhari kubwa..na bunduki zao zikiwa tayari kupambana na chochote kitakachotokea mbele yao…..walitembea umbali mrefu sana..bila kupata uelekeo wa njia ya kutoka mstuni humo…wakaanza kupatwa na njaa….wakajikaza kwa kupoza njaa kwa kunywa maji yaliyokuwemo ndani ya vibuyu vyao vya plastiki….
*******************
Upande mwingine alionekana Michael akiwatafuta wenzake ili ahakikishe kama wapo salama..kwa sababu yeye ndio mkuu wa kikosi hicho,,,wakati huo,Michael alikuwa hajui kuwa kapoteza askari mwingine,,yeye aliamini bado wapo sita……akaendelea kuwatafuta wenzake…..aliwatafuta kwa muda mrefu bila mafanikio yoyote…akaanza kuhisi njaa…akaamua kuwinda angalau mnyama ili aweze kujipatia mlo.
haikuwa kazi ngumu kwa Michael kwa sababu alizaliwa katika familia ya Uwindaji…Baba yake alimfundisha kuwinda kwa kutumia mbinu mbali mbali za uwindaji….akachomoa upanga wake akakata Fito kadhaa (miti mwembamba sana) akachonga miti hiyo..ikatengeneza ncha kali….akachimba mashimo mafupi manne..akaichomeka miti hiyo..akachuna kamba za magome ya miti na kuifunga kwa kuivuta akafunga kamaba hizo kwenye mti mikubwa miwili..kwa kuegesha….akawa tayari katengeneza mtego wa kumnasa muama ueyote atakaye katiza eneo hilo….. akazipiga hatua na kujificha kwenye kichaka…….
**********************
Upande mwingine kule kwenye kijiji cha jamii ya Wakololo,,,hali ilikuwa tete…Joshi aliendelea kufanya mauwaji ya kikatiri bila huruma….
Mtemi….alipo ona watu wake wanauwawa akaingia ndani kufanya jambo fulani……akachukua mshale akaupaka dawa maalum kwenye ncha ya mshale huo… dawa hiyo ni sumu kali sana ya kichawi,,ya mila za Wakololo…. ambayo inauwezo wa kupenya kwenye Mzimu….hata kama Mzimu huo umevaa kiwiliwili cha Binadamu …….akachukua upinde akazipiga hatua akatoka upande wa nje….
Wakati huohuo Joshi aliendelea kuwaangamiza wale vijana wa Jamii ya wakololo…akachukua ule upanga wake kwa kuuchomoa kutoka kwenye shingo ya yule kijana alimchoma kwa kuurusha upanga huo…..akaanza kuwafyeka shingo zao vichwa vikaruka kando….Joshi aliuwa watu wengi kwa muda mchache…
wakololo waliobaki wakaanza kutimua mbio na kutokomea mstuni..baada ya kuona mambo yamekuwa magumu…….
Mtemi alionekana akutafuta sehemu nzuri ya kujificha ili aweze kuufyatua mshale huo kutoka kunako upinde huku akiwa ametulia…….na kulenga shabaha kwa umakini mkubwa ili mshale huo uingie katikati ya kifua cha..Joshi.
akafanikiwa kupata sehemu ya kujificha vyema…akachukua ule upinde akaweka mshale na kuuvuta vyema…akawa tayari kwa kuufyatua….lakini alikuwa akisubiri Joshi ageuke ili afyatue mshale huo kifuani mwake…
Ghafla Joshi akageuka ili kutazama nani kabaki ili amuangamize………
Mtemi akavuta upinde huo kwa nguvu zake zote akauachia mshale huo…………
INAENDELEA

