HAINA MABEGA
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA KUMI NA SITA
Phia alikuja kwa kasi na kunipokonya simu yake, kitendo cha mimi kuwa makini na simu pasipo kusema jambo kilimfanya kuhisi kuna jambo halijakaa sawa ndio maana akaamua kuchukua maamuzi hayo ya haraka, nae alipoangalia video ile alijikuta anaziba mdomo alijiona mjinga kwa kuzificha video nyingi na hiyo kuisahau mpaka kupelelea mimi kuiona, video ilimuonesha Phia akifanya mapenzi na mwanaume ambae umri umesogea kidogo alikua ni mbunge wa bunge la nchi.
“Kumbe mdogo angu unacheza miguu yote?” nilimuuliza swali hilo Phia nikimaanisha alikua anafanya mapenzi mpaka kinyume na msumbile.
“Ni huyo mshenzi ndie aliniharibu, sikua na hiyo tabia alipofanikiwa kunirubuni kwa pesa zake siku tuliyokutana faragha akanilazimisha kuniingilia kwa mtindo huo imesababisha mpaka nimezoea, najitahidi kuacha ila inanipa wakati mgumu sana, Mungu anisaidie tu” Phia alinisimulia namna alivyoanza kucheza michezo mibaya.
“Pole sana unahitaji tu maombi kwakweli maana wote tunatenda dhambi lakini hiyo ya kwa mpalange imezidi hata moto wake utakua mkubwa zaidi, ukiamua kuacha utaweza”
“Sawa kaka” nilimfariji fariji pale Phia giza lilipoingia nilimdanganya kwamba naenda kulala nyumbani wazee wameniita hiyo ilikua mbinu ya kumkwepa Phia ambae alianza kuonesha dalili ya kutaka pale ili nimfariji usiku mzima, nilimsindikiza mpaka barabarani akapanda bodaboda ambayo ilimchukua kumpeleka chuoni.
Jumatatu kama kawaida niliingia kazini na oda zangu ni mwendo wa kucheza nazo nilipeleka kwa Dr Furaha pia nilipeleka kwa madam Brigita huko alinidaka akitaka nisitoke.
“Kama kufanya mapenzi nitakudanganya sina mzuka kabisa leo” nilijihami mbele ya madam Brigita yeye aliipenda sana hiyo michezo ya ngono.
“Gaa pana sio kufanya mapenzi mimi nataka nikuulize mambo ya msingi kuhusu maisha yako ujue ile kazi ya mgahawani hutakiwi kuifanya mpaka unazeeka kwasababu kuna kipindi utakua na watoto na wajukuu lazima ujue ulipo, unapokwenda pia kuna siku uliniambia kwamba umewahi tamani kufanya kazi kwenye hivi vyombo vya ulinzi na usalama sindio”
“Ndio ndio nilitamani huko nyuma lakini sioni kama litawezekana tena kwenye maisha yangu, labda dunia nyingine huko”
“Hahaha eti dunia nyingine usinichekeshe mbona unakata tamaa na unajua hakuna lisilowezekana chini ya jua”
“Nikweli lakini umri wangu unakaribia miaka ishirini na tano, elimu yangu ni kidato cha nne huoni nimeshatoka kwenye vigezo vya kujiunga na hivyo vyombo” nilijielezea kwanini niliona ni ngumu sana kwa ndoto hiyo kutimia.
“Aah ni sawa ngoja nijaribu kukupambania kwa nguvu zangu zote nione nitaishia wapi kwenye kuikamilisha hiyo ndoto yako”
“Ooh sawa hamna shida ukifanikiwa itakua furaha kubwa sana kwangu” nilikubali na kuibariki michakato hiyo ya kunitafutia nafasi kwenye vyombo vya ulinzi na usalama.
Siku hiyo ikapita na siku mpya ilipoingia tulifanya kazi na usiku nilirudi kwangu nikiwa kwangu nilipigiwa simu na Dr Furaha alinipa taarifa kwamba tufanye matembezi ya kwenda zanzibar tukale raha kidogo za maisha hiyo ilikua jumatano nikamweleza kwamba nitaendaje halafu kuna swala la kazi akanijibu hilo nimuachie yeye atanilipia mara tano ya posho yangu ya siku pia ataniombea ruhusa kwa mama shirima hilo la ruhusa niligoma, nilimwambia kama ruhusa nitaomba mwenyewe na sio kuombewa, sikutaka namna mama shirima alivyonipenda na kuniheshimu, heshima hiyo ishuke kwa kunihisi mimi kutembea na wamama kama Dr Furaha, nilimwambja nitashughulikia mwenyewe halafu yeye nitampa mrejesho, asubuhi ilipofika niliingia kazini kama kawaida, nilifanya jazi ilipofika usiku nilimwomba ruhusa mama shirima ya kutokuwepo mpaka junatatu nilimdanganya naenda kijijini na familia kujengea makaburi ya ukoo, hivyo ilikua muhimu kuhudhuria tukio hilo kwani kulikua na ibada nyingine zitaendelea, bila kuuliza zaidi boss wangu aliniruhusu. Ijumaa tuliingia kwenye ndege na kupaa mpaka visiwa vya marashi ya karafuu ndio mara yangu ya kwanza nakanyaga zanzibar na pia ndio ilikua mara yangu ya kwanza kupanda ndege.
SEHEMU YA KUMI NA SABA
Tukiwa ndani ya zanzibar tulilala kwenye hoteli kubwa yenye hadhi ya kipekee mandhari ya kuvutia initwa Jaz Elite Aurora humo ndani ndio nilicheza mechi ya ugenini lakini ilipigwa kwa kiwango kikubwa sana, nilimpa haki yake Dr Furaha hakupaswa kukosa raha wakati safari iligharamikiwa kwa pesa ndefu sana, hatukulala pekee bali tulizulura haswa tulitembelea Nugwi beach, tulienda kisiwa cha Mnemba, hatukupoa tulifika mpaka the rock restaurant huu ni mgahawa uliojegwa juu ya mwamba uliokua katikati ya bahari, tulitembelea mji wa kale kiufupi maeneo yote mazuri tuliyafikia, tulifurahia sana maisha, sikuona ajabu kufurahia maisha na Dr Furaha japo nilionekana kupitwa miaka mingi kwangu nilijari furaha ya moyo wangu tu hayo mengine hayakunishughulisha kabisa, jumapili usiku tukiwa hotelini baada ya chakula cha usiku Dr Furaha alikua anapiga wine taratibu na mimi nilikua nakunywa maji tu, usiku huo sikutaka kunywa kitu kingine.
“Umefanya sana kazi pale mgahawani nazani inatosha, mwezi ujao nitakufungulia biashara ya duka la nguo kwakua wewe ni mzuri sana kwenye kupendeza nazani utalisimamia vizuri, japo tutaanza kwa kugawana asilimia, zako sabini zangu zitakua thelathini tu, tutaenda hivyo na baadae utamiliki zote mia moja” Dr Furaha aliongea maneno mazuri nilimsogelea na kumkumbatia maneno yake hayakutakiwa kuachwa yapeperuke bure kwakua alikua amejifunga kataulo kilichoishia mapajani nilipenyeza mkono katikati ya mapaja yake, zilipoanza ashiiii nikajua ngoma imeswitch nilimvuta kitandani.
“Ga ga mwenzako nataka nikwambie vingine jamaaaani”
“Nataka useme nikiwa katikati ya mapaja yako”
“Oooosh jamani utanimaliza weee Ga Ga sijamaliza niachie bhasi” Dr Furaha aliongelea puani nami sikutaka kumwachia.
“Nagusisha kichwa tu hapo juu mimi siingizi ndani” nilimchapa uongo wa kiume.
“Ga gaaa haina mabega inazama ashiiiiiiii hapo ichape babaa ichaapeeeeeeee” nilipopata ruhusa ya kuichapa niliichapa kisawa sawa, tulilala, nilikua wakwanza kuzinduka, kabla ya kumuamsha Dr Furaha niliikagua simu yangu kwanza niliona meseji kutoka kwa madam brigita.
“I have very goooooood news, fanya tuonane leo” nilijisikia furaha sana yaani habari njema zinajiongoza tu nilijiona ni kijana mwenye bahati sana. Niliifuta jumbe hiyo ili kupunguza maneno baadae kwa bibie aliekua bado kalala fofofo, shughuli yangu ilikua kwa damu changa yeye damu zee ilikua inamzidia sana na mimi kwa sifa sijawahi mpunguzia dozi nilimpa yote apambane nayo. Nilimpiga busu la mdomo, lilikua busu matata sana la asubuhi, nilimuamsha tukaenda wote bafuni huko tuliogeshana si unajua miili miwili yenye jinsia tofauti, nikamwambia aokote sabuni hilo ni kosa aliponiachia kiuno nami nilikiwahi na kukikamata hapo hapo nilimpump vya kutiosha baada ya vurugu za bafuni tulitoka tukajiandaa tukapata kifungua kinywa, gari lilikua nje likitungoja tukapanda mpaka uwanja wa ndege saa sita tukapanda ndege ya kurudi dar, baada ya kutua tu kila mmoja alielekea upande wake saa nane kamili nilikua nyumbani kwangu nimejipumzisha nilikua nalifijiria duka la nguo atakalonifungulia Dr Furaha nilijiona mjinga kwa kulazimisha kumpa ahsante wakati kuna vingine alitaka kuniambia nikajiambiza kwamba kama ipo ni ipo tu ataniambia, akili yangu ilihama haraka na kuiwaza good news ambayo ambazo alikua nazo madam Brigita, muda ulisogea ilipofika saa moja usiku nilikua tayari nimejiandaa nilipanda bolt ya gari safari ilienda kuishia kwenye hotel moja nzuri humo ndipo ambapo Madam Brigita aliniambia nitamkuta nilipofika mapokezi na kujitambulisha, aliulizwa mwenyeji wangu alipotoa idhini nilioneshwa chumba alichopo, nilienda nilivuta kitasa kilitii na kuingia ndani nilimkuta Madam Brigita akiwa mtupu, mguu wa kushoto upo kule wa kulia huku, aliniita kwa kidole chake kimoja akitaka kabla ya yote nimshughulikie niliona sasa wanawake hao wataniua maana wananitumia kupitiliza nilipomfikia nilipiga magoti kichwa changu kilikua usawa wa kisima cha Madam Brigita nilitumia ulimi kuzama chumvini, baada ya hapo nilipeleka vidole viwili na kuvipitisha kwenye kisima nilitaka kumridhisha kwanza kwa vidole ili nisishughulike sana kwani ningezidi kuchoka, mchezo ulilipa kwani nilimuingilia kidogo tu tayari aliomba maji ya kunywa na kuniambia amechoka, tukaenda kuoga tuliporudi, kiliagizwa chakula tulikula, nilikua tayari kuipokea hiyo good news ambayo kuipata ilikua na kikwazo cha kuzama chumvini, baada ya kukamilisha kazi nilikaa kitako kusikiliza upendo huo ambao nilijua lazima utanifurahisha kwa vyovyote, wanawake hao walishindana kunifurahisha.
SEHEMU YA KUMI NA NANE
“Guess what”
“Oooh come on baby just tell me”
“Nimeomba nafasi ya moja ya jeshi la uhamiaji nchini, nimeipata ni swala la wewe kuleta vyeti tu ili hiyo connection ikupitishe moja kwa moja”
“Weeeee unanitania au kweli mpenzi” nilimuuliza madam Brigita, sikuamini amini yaani ndani ya muda mfupi amefanikisha jambo la kuniombea nafasi kwa mtu wa ngazi za juu.
“Sitaniiiii babe, ni kweli tukitoka hapa kanitumie vyeti vyako softcopy then mimi niwasilishe huko kwa connection yenyewe”
“Mmmh connection kweli au mtu wako”
“Heee yamekua hayo, uniamini sasa na wewe sina mtu mwingine zaidi yako mpenzi wangu, ukweli ni kwamba baba yangu ni askari ndani ya jeshi la uhamiaji, sitokutajia anacheo gani lakini ujue ni mtu mkubwa, kwakua kipindi hiki ndio watu wanaomba nafasi ya kujiunga na jeshi la uhamiaji ndio maana na mimi nikapenyeza ajenda kuhusu wewe, kwakua baba ananisikiliza sana binti yake amekubali moja kwa moja kwahiyo babaa jiandae na mafunzo ya kambini hapo tu”
“Ooooh nakupenda nakupenda wewe mwanamke” niliongea kwa hisia kali huku nikimkumbatia kwa nguvu Madam Brigita, swala la kujiunga na jeshi la uhamiaji ilikua ndoto yangu ya muda mrefu sana pia nilitamani siku moja niwe na kazi yangu ya uhakika nikiajiriwa serikalini, kingine kilichonipa mzuka zaidi ni kwamba jeshi la uhamiaji halikua na mambo mengi kama majeshi mengine, furaha ikaturudisha katikati ya mchezo kaka enu nilicheza sana ile mechi kwa uwezo wangu wote, ilipofika mishale ya saa tano usiku kila mmoja alipita upande wake nilipofika gheto kwangu nikaviscan vyeti vyangu vyote kuanzia cha la saba, kidato cha nne na cheti cha kuzaliwa, nilienda kwa mjumbe na kumgongea mlango nilimwomba barua ya utambulisho kwamba mimi ni mkazi wa ule mtaa, alinipatia barua, niliporudi kwangu nilivituma vyote kwa Madam Brigita nikimsisitiza asisahau kuvituma kwa mzee, kweli baada ya siku tatu niliitwa kwenye interview ya jeshi la uhamiaji, nilifanya ile interview kwa uwezo wangu wote nikapita, mwezi uliofuata nikaelekea kambi ya mafunzo ya jeshi la uhamiaji huko Tanga, kabla ya kuondoka niliaga mgahawani kwa mama Shirima pia nilimuaga Dr Furaha, wote walifungua moyo na kunitakia kila la kheri huko kwenye mafunzo yangu.
Mafunzo yalichukua miezi kumi, yalikua mafunzo mazito na magumu kwakua nilikua na nia na moyo wangu ulikua wazi kuvumilia kila kitu kwa uwezo wa Mungu nilifanikiwa kuwa mhitimu wa mafunzo hayo, siku ya mahafali wazazi wangu walifika kwenye mahafali yangu, nilimtambulisha madam Brigita kama rafiki angu kwakua umri wetu haukua umepishana sana wazazi walimuelewa na pengine walihisi ni mchumba angu, ukweli mzito ulikua moyoni mwangu nilifanya maamuzi magumu kwa namna ambavyo Madam Brigita alinisaidia kuipata hiyo kazi niliazimia moyoni kwamba mambo yote yatakapotulia nikiwa na kipato cha uhakika bhasi nitaenda kwenye familia ya Brigita na kuomba ridhaa ya kumuoa, mbali ya kuwa ni agemate lakini nilijua kwamba ni mwanamke mwenye kujitambua, mwenye utii na nidhamu pia mambo yote mazuri ambayo nilitamani awe nayo mke wangu niliyaona kwa madam Brigita, kuna wakati tulikua wawili tu tunazungumza.
“Gasper unajua nini, sisemi kama nimejitoa sana kwenye maisha yako ila nachotaka uone na kukipima ni kuhusu huu upendo wangu, baada ya kutendwa na kuumizwa na Ali, moyo wangu ulikufa ganzi mazima sikuona kama itafika siku nitapenda tena nilijiona ni mtu mfu ninaesukuma siku duniani, kitendo cha ajabu ni kwamba siku ambayo nilikuona wewe kwa mara ya kwanza kila kitu kilibadilika kwa upande wangu, uliumwagia maji ya upendo moyo wangu ukazinduka upya, nikapata hisia za kupenda tena, nilikuhitaji zaidi ya kawaida, sikujali kuumia tena, nilichotazama kwenye akili yangu ni kuwa na wewe siku zote, haijalishi utanioa au tutakua hivi hivi moyo wangu uliridhika kwa kila kitu. Leo nikuombe jambo moja ambalo ukiridhia nitafurahi sana” Madam Brigita alitiririka namna moyo wake ulivyokua unanizimikia mpaka kufikia hatua ya kutoona wala kutosikia kabisa. Sikutaka kutia maneno mengi kwani ningeharibu pishi hilo la ubwabwa liliojaa nazi nyingi.
“Naam nieleze mama angu ni jambo gani hilo” nilimpa uwanja atiririke zaidi.
“Nataka nizae nawewe, moyo wangu utafurahi sana nikiipata damu yako, sijioni kama furaha yangu kwenye haya maisha itakamilika bila kuwa na kiumbe chako, usiwaze kuhusu malezi na mambo mengine, mimi nitamlea mwanangu ila ninachotaka ni kuzaa na wewe” Madam Brigita aliongea kwa hisia sana, hisia zile zilinigusa haswa, moyo wangu nao ulishaanguka kwenye mapenzi yake sikutaka awe mwenyewe katika wimbi hilo nilimkumbatia na kumwambia kwa sauti ya upole.
“Sio mtoto mmoja ni watoto wengi natamani kuishi na wewe katika siku hizi za uhai zilizosalia, natamani kufurahia na wewe, natamani tupendane zaidi ya jana, nataka kufurahia na wewe kama mke wangu na mtu wangu wa karibu sana, nakupa ahadi hii nitakuoa Brigita nitakufanya mama wa watoto wangu na msingi kwenye kizazi changu kijacho” wapendanao wawili tulikua tunaongea maneno yenye kugusa mioyo kama unamtu unapendana nae utanielewa kama huna bhasi itakua ngumu sana kunielewa. Tulipeana ahadi nyingi sana. Ilipofika jioni wazazi pamoja na madam Brigita wote waliaga kuondoka. Walikua na ticket za mabasi tofauti hivyo kila mmoja aliondoka kwa mpango wake, kwa upande wangu tuliitwa kwa taratibu nyingine za kupangiwa vituo, nilimshukuru Mungu kwani nilipangiwa makao makuu ya jeshi la uhamiaji Dar es salaam, nilifurahi sana kwakua nilikua narudi nyumbani nitakua karibu na wazazi na kipenzi cha moyo wangu Brigita. Wengine walipangiwa mikoa ya mbali huko kama mpakani Kagera na maeneo mengine mengine, baada ya ratiba zote tuliruhusiwa kwenda kupumzika, kabla ya kulala niliingia mtandaoni kuperuzi kidogo ndipo nilikutana na habari ya kushtua moyo.
“Basi la abiria Vick Luxury limepata ajari baada ya kugongana uso kwa uso na roli la mizigo kwenye kijiji cha Mkenge, abiria wote waliokua ndani ya gari wamefariki wote baada ya gari kulipuka moto, tunatoa pole kwa wafiwa wote, Mungu azilaze mahali pema roho za marehemu wote amina”
Kuona taarifa hiyo moyo ulipiga paaaaaa, mapigo yakaanza kunienda kasi nikaanza kazi ya kumtafuta mama niliipiga namba yake ya simu haikua ikipatikana, niliipiga ya baba nayo vile vile, nikamtafuta Madam Brigita nae hakua akipatikana nilihisi kuchanganyikiwa, hofu ya kuwapoteza watu ninao wapenda ilinivaa, jamani nilikua kwenye wakati mgumu sana katika maisha yangu, kutoka furaha ya kuhitimu mafunzo mpaka uchungu wa kuwapoteza ninao wapenda, kweli mstari unaotenganisha furaha na huzuni ni mwembamba sana.
SEHEMU YA KUMI NA TISA
Nilisubiri kwa masaa mawili, hali yangu haikua sawa kabisa hali ilizidi kuwa mbaya baada ya jeshi la polisi kutangaza majina ya abiria waliopoteza maisha kwenye ajari hiyo, niliposikia jina la Brigita Komba nilihisi kuishiwa nguvu, niliona giza mbele yangu sikujitambua tena, nilizinduka siku ya pili nikiwa hospitalini, nimewekewa madripu hapo nilikaa kwa siku moja japo kila nilipokumbuka juu ya kifo cha mpenzi wa maisha yangu Brigita nilikua nalia sana, niliruhusiwa siku hiyo kutoka hospitalini, niliwatafuta wazazi wangu niliwapata wakiwa salama na walisafiri salama nilimshukuru Mungu kwaajili yao, nilisafiri na kuelekea Dar es salaam kwanza niliripoti kazini kwangu makao makuu ya uhamiaji, hapo nilipewa ruhusa ya siku tatu kwakua walikua na ripoti nimetoka kulazwa, sikurudi nyumbani bali nilielekea msibani nyumbani kwa kina Brigita.
Wakati napita kuaga na kutoa salamu za mwisho nilishindwa kujizuia kulia, eti mwanaume halii, nilishindwa mimi nawezaje kuacha kulia wakati nimempoteza mtu muhimu sana, nimempoteza mwanamke ambae niliamini nitamuoa kabla hajafaidi matunda yangu licha ya yeye kunisaidia kwa kiasi kikubwa eti anafariki, anaendaje ananiacha na nani nililia sana sikujali watu watanichukuliaje ila mimi nililia kupooza uchungu wangu japo sikujua ni lini haswa uchungu huo utapona moja kwa moja kwakua aliniachia kidonda kikubwa moyoni mwangu. Tulimpumzisha Brigita kwenye makazi yake ya milele mpaka kufikia hapo niliamini sasa sitoweza kumwona Brigita wangu, siku tatu zilipokwisha niliendelea na majukumu yangu ya kazini, sikujibu jumbe wala kupokea simu kutoka kwa Dr Furaha wala mwanamke yeyote niliewahi kuwa nae huko nyuma, niliupa moyo wangu utulivu kwanza mpaka pale nitakapo msahau kabisa Brigita miezi sita ilikatika angalau nilipata ahueni ya kumsahau Brigita na maisha yangu yalikua yanaenda kama kawaida.
Jumamos moja nikiwa off, off ilikua inaendelea kwa weekend nzima, hivyo ulikua utawala mwanzo mwisho, nilipata wazo la kwenda chuoni kwenda kuwasalimia wafanyakazi wenzangu ambao tuliishi kwa upendo na kufanya kazi pamoja pale Cafe kwa mama Shirima jambo lingine ambalo lilinipa nguvu ya kwenda jumamosi ni kwamba siku hizo Dr Furaha hakua akienda chuo kwahiyo kwavyovyote nisingepata usumbufu kutoka kwake.
Nilimcheki Troy mtoto wa kishua nikamwomba aniazime pikipiki yake moja kali la kinyamwezi, nilivaa na kupendeza kama kawaida yangu nilipitia supermaket nikanunua vikolo kolo kadhaa vya kutafuna, nilipofika chuoni kabla ya kwenda mgahawani nilimpigia simu Phia, nikamkabidhi hivyo vikolokolo nilivyombebea alifurahi sana kuniona na zawadi niliyompelekea kwa wakati huo hakukua na mapenzi mengine kati yetu ni ukaka na udada tu alipoondoka nikaenda mgahawani, wafanyakazi wenzangu walifurahi sana kuniona kwani ulipita muda mrefu pasipo kuonana, niliongea na mama shirima anipe kitengo cha kusambaza msosi kama kawaida sikutaka kuacha asili yangu na kujifanya boss eti kisa nimepata kazi mahali pengine. Siku hiyo nilifanya kazi ya kusambaza chakula hakukua na oda ya kupeleka chakula ofisini kwa Madam Brigita hilo liliniuma kwa kiasi fulani lakini nilijikaza kubwa zaidi hakukua na oda ya kupeleka chakula ofisini kwa Dr Furaha hilo lilinipa furaha zaidi kwani sikutaka kuonana na huyo mwanamke kwa vyovyote vile. Nilipokea oda ya kupeleka chakula kwa Director of Student Services huyu ni mkurugenzi wa kushughulika na mambo ya wanafunzi chuoni hufanya kazi kama mlezi wa wanafunzi wakiwa chuoni, nilimfahamu vyema yule mama hivyo sikupata wasiwasi wa kupeleka chakula. Nilichukua oda njiani nilisalimiana na watu wengi niliokua nakutana nao nikweli kipindi ambacho nilikuwepo pale mgahawani nilipata kuzoeana na waru wengi sana, nilipofika mlangoni niligonga mlango nikaruhusiwa kuingia, ile kufika ndani sikuamini niliemkuta ndani nilifikicha macho yangu ili kuona vizuri, alikua Dr Furaha nilishangaa imekuaje kuaje tena nilikitazama chumba vizuri kama nimekosea mlango au vipi.
“Hujakosea ofisi bro karibu sana” Dr Furaha alinikaribisha huku akiwa mwingi wa tabasamu.
INAENDELEA

