BOSS AISEE MI SIWEZI KUBWA MNO
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Episode 1
Nilikuwa zangu kwenye toyo nawahi kazini, ile nimeshuka tu hivi nikampamia kaka mmoja ilibidi nimuombe samahani huku natembea nikashangaa kanivuta, “wewe dada kuwa na heshima, umenidondoshea simu yangu, then unaomba samahani huku unatembea hata hujatazama kama umeniharibia simu yangu wala kutumia uombe kwa adabu hio samahani, niligeuka kwanza nikamtizama uku nimekasirika mno, wewe kaka mbona hufanani na huu ujinga unaofanya mkaka smart unalilia samahani🤔, huoni aibu, ebu niache samahani namwahi boss wangu asiejua nini maana ya muda, nataka nikamfundishe boss wangu kujali muda weee nae unaanza kunichelewesha ili nifanane na boss, ivi viumbe wengine mkoje jamani, ulivyovaa unaonekana kama zimo ila sasa ukiongea tu mtu anatahamaki afu ni mwanaume dah, au ndo nyie vyakula vya wakubwa ee? Niliona yule kaka anatunisha misuri yake kwa hasira…
Nikajua ehee itakuwa nimempatia, nikacheki pembeni yake kuna gari ya bei chafu, kwa harakaharaka hii gari si chini ya ml 800, napenda magari hivyo najua mpaka bei, apo nilivyoijua tu, moyo ukashtuka hii gari, inasemekana boss wetu pia anayo, huenda huyu akawa analiwa na boss Mungu wangu 🧐, nilimsikitia yule kaka nakumwambia kaka pole sana yani na uzuri wote huo kweli una pakuliwa? 😃😃, dah ebu niache niwahi mimi sijazoea kuchelewa mwalimu wangu wa sekondari, alinifundisha thamani ya muda tena kwa viboko vya miguu, nimelambwa vipoko mpaka nikajua thamani yake, na kazini kwangu naheshimika kwa sababu ya muda, sasa usifanye nikapoteza thamani, kama hio simu yako imeumia shika no yangu hii hapa, nitakulipa kwa muda mwingine huu ni muda wa kazi, naenda kumpokea my Boss, Boss ambae hajitambui sema namshukuru kwa kuwa tu analipa mishahara kwa wakati ila kuhusu muda mwalimu wake alifeli sana, sasa acha niwahi nitakucheki demu wa wakubwa byee,niliongea uku natimua mbio kazini kwangu, nilimuacha kaka wa watu kavimba…
Nilifika kazini wa kwanza, nikaweka mambo sawa hii ni kawaida yangu,kuwahi kazini, Boss wa hii kampuni hatujawahi kumuona tunakutana na msaidizi wake tu, kila akisema anakuja tutajiandaa anasema anafika saa tatu, ajabu lazima atachelewa na kukutana na viongozi wakubwa tu, sisi tutapewa tu taarifa alichelewa ni mwaka sasa anakuja na kutoonekana, huu ni mwisho wa mwaka sasa anataka kuja kutupongeza na kufanya part na sisi tumefanya kazi nzuri sana, tumeipandisha kampuni kwa kasi sana, ameahidi pia kutuongeza mishahara hivyo nilikuwa na kimuhe muhe mno, apo nawaza tu nyongeza ya mshahara, nishaanza na kupiga budget kabisa ya matumizi🚶…
Wenzangu pia walianza kuingia, apo nikabadilisha nguo, huwa sitembei na nguo za kazini, huwa nakuja kuvalia kazini sare za kazi, kwa sababu sare zangu sio ndefu,na nyumbani ukionekana na nguo fupi aiseee utajuta siku io, ili nisikatazwe kufanya kazi nikaamua kuwa navaa nguo tofauti, nikifika kazini nabadirisha…
Nilibadirisha mimi ni kazuri ka shep, nikipita kama nimevaa nguo ya kushep lazima unitizame tu, tulisubiri huyo boss chumba cha mkutano, leo akawa kachekewa kwa saa moja, ila hatimae alifika, aliingia nilikuwa nimeinama nikasikia anakaribishwa si ndo nikainua uso, namimi uku nasalimia, saa ngap nisimuoe yule kaka, ila yeye alikuwa hajaniona, uwiii ninekwisha mimi, nilijikaza kama sio mimi, kila mtu akawa anainuka anapita mbele, anajitambulisha uku anatoa maelezo ni kwa namna gani, kajiandaa kuikuza kampuni kwa mwaka ujao, na anaahidi kuifikisha hatua ipi kampuni…
Ilifika zamu yangu, nikainuka, Boss akashtuka akakaza uso, watu wakaanza na jina la utani miss time, nyie hawakujua tu wanavyozidi kuharibu, nilijikaza nikatoa point zangu, sema kwenye kazi mimi nimenyooka kama rula, ninapiga kazi mno, na najua kukuza soko, kampuni inaniaminia huwa siferi kwenye mawazo yangu…
Nilivyomaliza watu walinipongeza, Boss hakulaza damu,pale pale akaniuliza “ndo wewe ee? Nikavunga sijui, samahani boss sijaelewa unamaanisha? Akasema utambulisho umefika mwisho tutaendelea kesho, wewe miss time nifate, nilimfata ila mikono imeshaswet ni ninaogopa mno, nilimfata tulivyofika ofisin kwake, akaniambia niandike maelezo kwa nini nilimtukana, lakini pia nisain makubaliano yakulipa simu yake imevunjika kioo na kioo cha simu yake ni ml 8,nisain mkataba wakukatwa mshahara mpaka pesa yake itimie, tena hataki simu iliyokanyaga kwa fundi, simu yake kanunua ml 35, kwenye kiwanda, kwa kuandaa logo ya jina lake na maelekezo yake hakuna simu kama yake sokoni hiyo yake ni special oda…
Nilimtizama uku nimekaza, samahani sana boss, mimi sikuelewi mbona? Mimi na wewe tumekutana wapi? Na saa ngap? Na kama ni kwenye utambulisho mbona Boss sijakutukana? Au hauko sawa? Mimi ndo nakuona kwa mara ya kwanza boss…
Boss alisimama akiwa na hasira, uku ananiambia, “usinifanye mimi mpumbavu kubadirisha nguo hakunifanyi nikusahau, sasa si unakana, napiga no uliyonipa uzuri uko na simu yako hapa, ikiita mikononi mwako, naandaa mkataba, unasain sasa hivi, nyie jamani huyu Boss mbona kichefuchefu khaaa😭…
Episode 2
Alitoa simu tofauti na ile iliyodondoka, kidogo niropoke nikakumbuka nineshajikana, nikafunga mdomo, alipiga simu, ikaanza kuita, bahati ilikuwa kwangu, sikutoa no yangu nilitoa no ya dada angu mkubwa lengo anilipie huo msala, nilishazoea kesi zangu huwa nalipiwa na dada mkubwa 🫣, ananielewa sasa hii ya leo ninauhakika hawezi kulipa atachanganyikiwa dada angu maskini, Boss alishangaa kuona haiiti kwangu alipokea dada angu na sauti zetu zinafafa, tofauti dada angu sauti yake ni ya ukarimu hata ukimkosea anakujibu tu vizuri ila mimi sasa, unavyokuja ndo ninavyokupokea…
Dada angu alipokea haloo, Boss akanitizama kwanza kisha akajibu, “bila shaka naongea na Juliet binti wa thamani ya muda, dada alivyosikia tu ivo akajua nishaharibu hakutaka kujibu ndio au hapana akajibu tu, sema hio bill tumalizene kaka, Boss akahamaki kwanza, si ndo kumtajia bill na maelezo kama aliyonipa, weee dada apo apo akapiga ukunga, wee kama uko sawa, yani simu tu ndo bei ya gari na nyumba uko serious kweli ama hutaki kulipwa?..
Boss akajitambulisha nakutuma taarifa za simu yake, kama haamini aingie Google akacheki, dada akakata simu,akaingia kucheki akakuta kweli, alichoka muda huo Boss akaniomba samahani huenda yule akawa ni ndugu yangu, mimi hapo naomba tu aniruhusu nitoke tu, make najua dada angu atanipigia tu, na kweli hakukawia akapiga Boss akaniruhusu nipokee simu, ila uoga, akahisi huenda ni boy wangu, ” pokea usiogope najua wewe ni kijana kuwa huru, dada simu imekata akapiga tena, ikabidi nitoke nikapokee tu nje, nilimchana ukweli wote dada, na jinsi nilivyokana, kumbe uku wakati na toka boss kaona wowowo, mwanzo hakuwa amenicheki vizuri kwa sababu ya hasira, alijikuta anadata na mzigo, akawa anajizuia, shit nawaza ujinga gani huu tena mimi, mbona sio kawaida yangu…
Upande wangu, dada alilalamika sana, sasa tutafanyaje hio pesa ni nyingi mno, ml 35, ata duka lake halifki, tulikubaliana tutaongea nikitoka kazini, alikubali nikakata simu, kumbe Boss bado alipata mashaka sauti zilikuwa zinafanana sana, akaunganisha na maneno niliyokuwa na sema boss kutokufika, matukio yalikuwa yananilenga mimi, alivyopata utata mchana, akamuita msaidizi wake na kumuuliza kama mimi nina pacha wangu, msaidizi wake alikataa, akasema hapana, ananijua vizuri, ikabidi aulize kuna nini?, Boss alimpa mkasa ulivyokuwa, msaidizi wake alicheka akamwambia tu aendelee kumtafuta, aliogopa kunisema make anadet na dada angu…
Ila na yeye alianza kuogopa kuhusu hio ml 35, ikabidi kwanza amuulize, “unataka kumlipisha kweli ama unamtisha tu, Boss akasanuka ila hakutaka msaidizi wake ajue, kwa sababu kwanza ni mkubwa kwake, wanaheshimiana sana, pili alihisi kuna sababu ya msaidizi wake kumficha, akaona asijibu lile swali amruhusu tu aende ila apo tayari alishaamini, lazima tu ninahusika, muda wa chakula cha mchana, tulitoka kula, kumbe yeye kaenda kuweka kinasa sauti, kwa msaidizi wake na mimi pia, msaidizi wake alikuwa na kitete, alichukua chakula akaniita ofsini kwake, nilifika, nikamuita shem…
Akaitikia na kuniuliza leo tena nimefanya tukio gani, nilimsimulia na kumwambia nimekana, sijui tunafanyaje kulipa dada angu hilo deni ni kubwa hawezi, “ivi Juliet huwa unamhurumia kweli dada ako? Sasa kesi kama hii unamtesa mke wangu, umekuwa unamtupia kesi zako, anakulipia sasa hii utailipa na sijui Boss anamango gani, mbona Juliet hukui jamani, apa utafanya harusi yangu isifanikiwe kisa hili deni, aliongea kwa uchungu, adi nikaumia, shem nisamehe mimi sikujua kama kutatokea hili, ila naomba msiingilie tena nitaenda kusema ukweli atanikata tu kama alivyosema kwenye mshahara wangu, uzuri mimi na kaa nyumbani nakula nyumbani, na kuhusu nauli, nitakuwa natembea naweza nitakuwa nawahi kuamka, niliongea nikiwa namaanisha kabisa, kumbe maongezi yetu yote Boss anasikia, alitabasamu, kisha akakaa kusubili nikajisalimishe mwenyewe…
Nilitoka ofcn kwa shem, nikaingia ofsin kwangu, lakini leo ata kula nilishindwa, sijawai kushindwa kula toka nijitambue napenda mno kula, lakini hili jambo lilijua kuninyoosha, nilijikuta nakosa raha, nikaweka chakula pembeni, ata kazi nikashindwa kufanya nikaanza kulia, upande wa boss akawa anasikia nalia, alitamani kuja ila akajizuia, kidogo simu yangu ikaanza kuita, alikuwa ni dada, nilipokea, dada alikuwa na hofu mno na mimi,nilijikaza asijue lakini alijua tu, akataka aje kazini nilimzuia nakumwambia nitaomba ruhusa nije…
Aliuliza kama nimekula, dada mimi nimeshindwa kula kwa mara ya kwanza dada anaogopa, Juliet omba ruhusa mdogo wangu utanikuta nje ya kampuni yenu nakusubiri twende wote, nilikubali nikaenda kuomba ruhusa kwa shem, aliniruhusu nikatoka, nafika ivi nje nikamkumbatia dada angu, uku nalia, na yeye akaanza kulia, wakati tumekumbatiana tunabembelezana saa ngap tusishtuliwe na Boss yani tumekamatwa kama utani vile…
Episode 3
Boss alitushtua kwa kutuita, miss time, naona mko wote, mda huo anaongea uku anampigia dada simu, na sauti inatoka kwenye simu ya dada, nyie niliogopa nikapiga magoti haraka, Boss naomba unisamehe ni mimi dada angu hahusiki nitasaini mkataba niko tayali, nikiwa najitetea dada nae aliingilia akidai atalipa kila mwezi apewe muda, “kwahiyo kila mtu anahitaji kulipa ok nipeni muda nifikirie nitachagua kwa leo sina majibu, acha nikatafakari zaidi, aliongea ivyo kisha akasepa aisee nilichoka, nikiwaza uko nyumbani mzee awezi kuelewa na hata hizo pesa hana, sitaki kumpa hofu, tulienda dukani kwa dada angu, ili nikabadilishe nguo na kutuliza kichwa kidogo, niliona niongee tu na dada, nilikumbuka shemeji alivyonilaumu sana leo, nilimbembeleza dada asilipie mimi ndo nilipe, ila yeye atanisaidia tu nauli za kazini, dada alinielewa na kukubali japo alinihurumia sana, alijua kabisa hili deni litanichukua miaka kulimaliza ila hatukuwa na jinsi…
Dada alinimbembeleza nikala, kisha akanipeleka nyumbani, yeye alikuwa anajitegemea aliolewa ila, mme alifariki akaachwa mjane na mtoto mmoja ni miaka 13 sasa,toka mmewe amuache, nilifika nyumbani nikamkuta mdogo wangu anapika, kwetu tuko watatu tu, wakike wawili na huyo wa kiume wa mwisho, yuko chuo, ananipenda mno, japo kuna muda tunatibuana sana, anatabia yakuiba soks zangu, tshart yani nguo yangu akiipenda tu, basi nitaikuta kwenye nguo chafu, hujui ata kavaa saa ngap 🙌, nashukuru alizaliwa wakiume, vinginevyo ningekoma, aliniona akanichangamkia, ila akagundua siko sawa, ni bonge la muelewa, alinishika mkono akanipeleka chumbani, akaniambia nipumzike afu nikiamka nimwambie uyo mpuuzi aliyenitibua akamnyooshe, nilimkubalia tu, nilioga nikalala,mama na baba walikuwa bado kwenye biashara yao ya vyombo…
Nililala kiasi kwamba wamerudi ata sina habari, mama alishtuka na kuniulizia, dogo akajibu nimelala,mama alishangaa sio kawaida yangu,alikuja chumbani kuniamsha ili nikale chakula, niliamshwa nikaamka kivivu nikamsalimia mama, alinitizama nakuniuliza unaumwa? Nilijibu hamna mama nimechoka sana leo, sitokula mama, ngoja tu nimsalimie baba, mama alishangaa sana..
“Juliet unatatizo gani binti yangu, mbona sio kawaida yako, ata ukiumwa huwa hauachi kula, leo kulikoni, au ni siri sipaswi kujua unataka mpaka baba ako aje kukubembeleza ndo utajibu? Jamani mama sio hivyo mimi sina tatizo leo nimechoka sijawai kuchoka hivi toka nizaliwe, mama alinitizama akasikitika na kuanza kimuita baba, Baba aliitika uku anakuja, alifika akagonga hodi, mama akamruhusu, nilimsalimia akaitikia, ata salam haijafika vizuri moyoni, akaingiziwa mada nyingine na mama, aya malikia wako leo kwa mara ya kwanza anasema hali chakula namuuliza anashida gani kagoma kuniambia, naomba umuulize wewe kipenzi chake labda ataongea make sisi wengine ni kunguni sio watu, hatufai kujua matatizo yake, nilichoka jamani mama mbona mimi sina tatizo, baba nae alihisi huenda naficha jambo,na anajua mimi nikipenzi chake siwezi kumficha, akamwambia mama atoke ili tuongee, mama alitoka kwa hasira akabamiza mlango, Baba akaanza kunibembeleza, dar mpaka akataka kulia ilibidi nimwambia baba kuna jambo nimekosea kazini na kesho ndo nitapata mwafaka, naomba usimwambie mama mimi kesho nikipata mwafaka nitawaambia wote kwa pamoja ili asijisikie vibaya…
Baba alinielewa akatoka, utazani ajajua chochote, mama alishangaa ilaaa akahisi tu tumemzunguka, alikula uku anagomba, ikabidi mdogo wangu amtulize na kumwambia atuache tu yakitushinda wenyewe tutaropoka, walikula tukalala, kumekucha nikajiandaa kama kawaida kiwahi ni kawaida sana kwangu, niliwahi kazini, ila cha ajabu leo, ile natoka tu hivi kubadirisha nguo, nakutana na Boss, alitabasamu kisha akaniomba nimfate…
Episode 4
Nilimfata huku naogopa, tuliingia ofisin,alinitizama sana, kisha akaanza kuniuliza, msaidizi wake ninani yangu, “usinidanganye tena, kama utadanganya utaongeza kosa endapo utasema ukweli basi nitakupunguzia deni lako nusu nitalilipia, nilimeza kwanza mate, nikasema tu ukweli ni shemeji yangu, kamchumbia dada angu, “vipi kuhusu wewe? Mimi nini Boss sijaelewa, “kwenu mpo wa ngapi?, nilimtizama nakujibu watatu, wawili wakike na wakiume mmoja, “na huenda wewe ndo last born? Hamna boss, “basi ulitakiwa tu kuwa lastborn kwa mambo yako, sio mbaya na wewe umechumbiwa, nilitamani ata kucheka kwanza, ila kesi iliyokuwa mbele yangu niliona kabisa itaniponza, mbavu zangu kaza nisijeongezewa deni, bahati nzuri zilinitii nikajibu bado, “ok sasa Leo hapa nahitaji msaada wako, naomba no ya mzazi wako niongee nae anipe ruhusa kuna part unisindikize,nitakurudisha, lakini pia ujiandae kuna safari ya kikazi kesho kutwa tutaenda South Africa, na wewe ndie naona unafaa hio nafasi,niliitikia tu ila nikiwaza kuhusu baba angu mmh, sijui nikapata wazo ampigie tu dada, afu dada atajua cha kuongea nyumbani, aligoma nakuhitaji no ya mzee, nilipiga magoti kwanza, Boss naomba usimwambie baba angu kuhusu deni atachanganyikiwa, hio pesa ni kubwa…
“Juliet kwani kwenye mazungumzo yangu, nimezungumzia swala la deni? Hapana “sasa mbona unaleta deni,kwenye topic tofauti? Aliniomba simu yangu, nilimpa kwa uoga, na kimbembe haikuwa hata na pasword, aliingia akatafuta no ya mzee, aliniuliza nilivyomsave, nilimjibu, akachukua nakupiga,alipiga akajitambulisha, kuwa ni Boss wangu, mzee akasema yuko nje ya kampuni yetu, nikaona kama Boss kashtuka, wakakubaliana kuongea live, nilishtuka nikamuuliza mbona live, “nikuulize wewe umemwambia nini mzee wako, mpaka kaja kazini asubuhi yote hii, kamuacha mke wake kitandani na baridi looooote hili, huu muda ni wamasingle kukimbia vitanda sio wanandoa, nilimtizama kama namshangaa, anaongea kiutani, akati nje ni bonge la kauzu la kutisha, hazoeleki tulikuwa tunapewa vitisho kumbe mtu mwenyewe simple tu, nilianza kuondoa ata ile hofu kiasi…
Nikamuomba lakini usimwambia kama nadaiwa pesa kubwa, mwambie tu niliharibu kazi, tayari mmesharekebisha, “mwanamke unanifundisha uongo sasa, niliona aibu nikakaa kimya, alitoka na mimi nikatoka, nilijua wanaenda kuongelea hapa hapa ofsin, lakini nikashangaa mzee wangu, katiwa kwenye gari, sijui anapelekwa wapi jamani,nilibaki kuwaza tu, mda ulizidi kwenda naona kimya tu, nikaamua kupiga kazi, saa 5 ivi asubuhi, nikapigiwa simu na baba, haloo, nilimsalimia baba akaniambia, “binti yangu usiwaze, Boss wako nimwelewa, kasema hilo tatizo kashapata njia rahisi atakupa maelekezo nini cha kufanya kila kitu kitakuwa sawa, niliwaza mbona kama mtego, “na pia kasema wewe ni mtu anaekuamini, kanihakikishia usalama wako, kaomba leo kuna kazi usiku ila itaisha saa 6, atakurudisha, nimemuomba uende na mdogo wako au dada ako, kakubali, tumeongea na dada ako kasema atakusindikiza, usiku siwezi kukuruhusu kwenda na mwanaume bila uangalizi, nilikubali tu nikafurahi huenda deni nimesamehewa, baba hakuishia hapo, akasema kampa boss chakula aniletee nile, nisije tena nikalala njaa kama jana…
Nilicheka nikamshukuru baba, nikasema nitapitia tu kwa dada sasa, mzee akakubali, nikakata simu, haukupita muda dada akanipigia kunipa ubuyu, namimi nikatiririka, dada akaguna, ikabidi nimuulize, kulikoni?
“Apana ila kuna jambo nahisi, kama ni kweli tutakuwa salama,hakutaka kusema nilichukua, ila akasema kapigiwa simu na Boss wangu, ajiandae tukachague nguo, kaogopa kusema kama anauza nguo, namimi nikasema ila kweli dada sasa kama mtu ananunua simu ya mamilio aya utamvalisha nini apo dukani kwako, au ndo hizo suti za laki 3 na nusu, make ndo suti peker yenye bei uliyonayo, tukajikuta tunacheka tu na dada, ila dada kwa nini kama kasema anaenda kutununulia na sisi, tusimuombe bajet yetu, ili sisi tujinunulie apo kwako?, “apana dogo kwa mara ya kwanza hatupaswi kuwa na viherehere, kwanza hatujui huko tunakokwenda pakoje, tukasome kwanza vitu anavyochukua ili tujifunze na sisi tuwe tunaleta dukani, siku nyingine akituambia tunakuwa tushajua nini kinahitajika kwanza tumjue vizuri saiv shona mdomo kila kitu iwe sawa…
Nilimuelewa dada nikakata simu,Boss alifika akapitiliza ofisn kwake, akapiga simu niende, nilifika nikagonga, akaniambia niingie, alionekana kuwa bze sawa, aliniambia nichukue chakula mzee kampatia, nilichukua nikaondoka,nilivyofika ofcn nifunue sasa nikakutana na kuku wa foil na ndizi, nyie nilikula nikashushia na juice awee nilimpigia baba nikamshukuru mno, baba akasema yeye akutoa pesa alitaka kunichukulia chips tu, ndo boss akasema atanichukulia nisijali…
Mmh nilikausha, make adi baba alianza kuhisi kuna kitu kati yetu,nikiwa naendelea na kazi nikasikia kama Boss anamtimua mtu kazi, ilibidi nitoke sikuwa peke yangu, kuna dada mmoja uyo anamashauzi balaa, kajipeleka uko uku kapandisha skert kumbe jana pia alienda akapewa onyo, hakukoma leo karudia tena apo kachana vifungo vya shart yake, ni kifua kiko wazi mno kwa juu, sema ni kadada kazuri jamani, sijui tu kwa nini kamejidhalilisha…
Boss alitupiga mkwala wote, “sihitaji mapenzi apa ni kazi tu, ole mwingine arudie, atakuwa kapoteza kazi muda huo huo mikataba, ikatolewa amri irekebishwe, kuwepo na hio amri ukijirengesha kwa Maboss ushahidi ukapatikana, huna kazi wala huna haki yoyote, na kwa Boss ivyo ivyo, ila kama ni nje na kazini hio mtajuana wenyewe, isiletwe kazini…
Mikataba ikaletea tukapitia nakupitisha wote, Boss alionekana kuwa na hasira mpaka anatisha, kila mtu alimuogopa, yani ata kupita karibu yake tulikuwa tunaogopa…
Episode 5
Nilirudi ofisin kwa hofu,nikawaza huyu mtu hatabiriki niwe makini sana, alipiga simu ikaniondoa kwenye mawazo, apo ilikuwa saaa 8 mchana, akaomba nitoke yupo kwenye gari ananisubiri, niweke mambo yangu sawa sitorudi tena ofisin, kwa sababu kesho nitakuwa off kwa ajili ya maandalizi ya safari, nilitamani kuuliza, ila kwa jinsi anavyotisha awee nilifunika mdomo wangu,nikakausha tu nakukubari, nikiwa naweka mambo sawa alikuja shemeji na kuniambia niende yeye atanisaidia kumalizia, nilikubali..
Nikatoka nilimkuta kakaa nyuma mbele kuna dereva, siti ya mbele jirani na dereva haikuwa na mtu, nikatamani kukaa mbele, nilimsalimia dereva, akanipa tu maelekezo nikae nyuma, nilitamani kumtukana, nikabana ila kichwani tayari nilishamtukana mpaka, nilifungua mlango wa gari taratibu ili nisimshtue Boss, nilifungua nikaingia nakufunga mlango ila nikakaa mbali nae, niliona nyuma pia kuna siti nikataka nikakae za nyuma zaidi, Boss akaniambia, “J kaa tafadhari, sitaki usumbufu saiv, nilikaa kwa uoga akanitizama kama ananishangaa hivi…
Akaniuliza mbona kama hauna uhuru, kichwani nikamjibu, unataka niwe huru useme nimekutaka unifukuze kazi ama unazani sijui🤔, mwenzako akinyolewa zako tia maji, nikashtukia Boss ananiuliza, “we J huo ukimya hunitukani kweli kichwani mwako umo? Jamani kwani huyu Boss ni mchawi jamani khaa, nilimtizama uku naogopa, nikajibu amna,mda huo nimekaa pembeni kabisa nazidi kubana mlango wa gari tu, uku Boss nimemuachia nafasi kubwa, gari ikaanza kuondoka, Boss akasogea karibu na kuniuliza mbona kama umejibana sana uko na akati nafasi kubwa iko hapa, wee nashukuru mlango ulikuwa umelokiwa vinginevyo ningejikuta nje ya gari…
Boss aliniambia tu usiogope tuko nje ya kazi Bwana, apo nikapumua, aliniambia nikae vizuri, lakini bado nikawa namashaka sana, nilimuelekeza dereva dukani kwa dada,tulikuta yuko anafunga atusubiri nje hakutaka aibu kwa madai yake, nilitamani kucheka nikajizuia, dada alimalizia kufunga, tukaingia wote, Boss akasema tumweke katikati, mimi nikawa naogopa, Boss akanikazia macho nikakosa ata chance yakumpanga dada…
Yeye aliingia akakaa tu vizuri mimi sasa nikawa najibana haswaa, mpaka dada akaniuliza, “wewe mbona kama hujakaa vizuri, “afadhali umenisaidia kuuliza huenda wewe ukapewa majibu, kwa sababu mimi mwenyewe wakati tunakuja alikaa kama vile nimempa mpaka, simuelewi mdogo wako, dada akahisi tu kuna jambo, hakutaka tuendele na mada, tulifika dukani duka ni la kishua haswaa, nguo ni za gharama, tulinunuliea nguo gauni langu lilikuwa la ml 5, bado kiatu,blacelet,heren, saa,poch, nyie bado dada nilihisi kuzimia,mpaka nikawa nashindwa kupumua vizuri, tulivyomaliza mahemezi…
Boss akatoa mkataba wa deni, nguvu zikanisha, nikawa naogopa ata kuusoma, “J nimetoa mkataba mbele ya dada ako, nahitaji tu majibu leo, sihitaji kupoteza muda kwenye hili,tulifungua na dada tukasogeleana, kucheki mkataba unasema nichague kuolewa na Boss deni liishe, ama aongee na mzee wangu, wakubaliane malipo ndani ya mwaka mmoja…
Inaendelea…..

