USIKU WA KAFARA
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Sehemu Ya 1
USIKU WA KAFARA!
31 DICEMBER
Ilikuwa bado masaa sita siku igeuke kisha mwaka 2016 upite na kuupisha 2017, macho mengi ya watu yalisubiria kwa hamu hayo masaa machache yaliyo bakia waweze kuushuhudia usiku mpya wa mwaka 2017 ,wengi wali subiria masaa yale wakiwa sehemu za starehe wakipata moja moto na nyingine baridi na baadhi waliusubiri mwaka mpya katika nyumba za ibada na wengine majumbani mwao.
Shamra shamra kutoka kwenye kila kona ya dunia zililindima kutoka kwa watu walio usubiri huu mwaka kwa hamu ya ajabu .
JUA ndo kwanza lili kuwa linazama likizungukwa na rangi ya wekundu na kulifanya liwe la kuvutia kulitazama.
Pembezoni mwa kijiji cha muvila nje kidogo ya mkoa wa pwani kulikuwa na msitu ambamo humo kuna viumbe vilivyo changamana na baadhi ya binadamu navyo vikiusubiria huu mwaka 2017 , lakini wao wali usubiri kwa hali tofauti na yaa ajabu sana!
Naam! ni pembezoni ya pango liliopo ndani ya kimsitu kile ndipo kulikuwa na watu waliokaa mistali miwili iliyo tazamana wakiwa wanevalia nguo za ki mila na tena zilikuwa nyeusi na watu hawa hawa kusema wala kunong’ona !
Ulikuwa ni mkao wa kustaabisha sana pembeni ya pango lile.
Ndani ya pango kulikuwa na mwili uliofanana na maumbile ya kibanadamu wenyewe ulikuwa mrefu ya pata futi nane kasoro na urefu huo ndio ulio tambulusha kuwa ule haukuwa mwili wa bina damu wa kawaida!
mwili huu ulikuwa umelala juu ya jiwe ambalo lilikuwa limefanywa kama kitanda jiwe hili lilikuwa limechongwa kwa mikono na bila shaka lili tengezwa na jamii isiyokuwa ya binadamu wakiwa na nia ya kulipendezesha!
Pembeni ya mwili huo kulikuwa na kizee kikongwe kilichokuwa kimeshika fimbo iliyo kunjwa sehemu ya kushikia , kikongwe alionekana kuwa jinsia yakike!
japo alikuwa ni mzee na kupinda mgongo (kibyongo) ila bado nae alionekena kuwa ni mrefu kama mwili uliolazwa juu ya jiwe.
Niwazi wote wawili hawakuwa binadamu wa kawaida..
“Ni kwa miaka mingi tumiishi kwenye hii dunia ya binadamu wenye uhai mfupi …na leo GOROZA atafurahi tutampa zawadi nyingi kisha atakurudisha kutoka kifungoni na wewe GUNZANI utarudiwa na uhai kisha utandeleza utawala huu” yule bibi kizee aliongea huku akitazama sanamu iliyo kuwa pembeni yao na sanamu hiyo ndio iliitwa goroza ,
kisha akaushika mkono wa ule mwiliwa kiume ulio lazwa juu ya jiwe
“GUNZANI….” alimuita na kujaribu kuongea nae kwa hisia mwili ule ambao haukujitikisa hata kidogo !
Nje ya pango wale watu waliokaa kwa kutazamana sura zao ghafla ziliijiwa na furaha baada ya kumuona mtu ambae kwa hakika hakuwa mtu wa kawaida akitokea nyuma ya pango akiwa amembeba msichana mdogo begani akiwa kamviringisha kwenye kitambaa cheusi
“Aabudiwe goroza na aheshimiwe msaidizi wa gunzani kwa kuleta sadaka ya leo usiku” watu wale ambao kwa hakika kabisa walikuwa ni binadamu wenzetu walitamka kwa pamoja…
Wakainuka kumlaki huku mmoja akimpokea msichana kutoka begani kwa mtu yule
“mzee juma mfungue na umwandae kwa ajili ya sadaka ” yule mtu ambae ni msaidizi wa gunzani mwenye urefu takribani futi saba kasoro aliongea…
Mzee juma alimchukua yule mtu alie vingirishwa kwenye shuka jeusi gubi gubi , akamuweka kati kati yao na kuanza kumfungua na kila mmoja akiwa na hamu ya kumshuhudia msichana yule ambaye kwa hakika anahitajika kufa kifo cha kunyonywa damu usiku.
Mzee alifungua msichana yule na hapo urembo wa msicha yule ukadhihrika kwenye macho ya kila mmoja, ila macho mawili kati ya watu wale hawa yalikumbwa na mshangao na hali ya kuto amini.
“Mkuu huyu ni mwanangu..diana” sauti ya mama moja kati ya watu hao ilisikika huku akimtazama mwanae juu ya shuka jeusi akiwa hana fahamu.
“Ah mama DIANA siku ya leo kijijini nime kosa kabisa vigoli kwa ajili ya goroza wasichana baadhi wapo makanisani na wengine likizoni kwa ndugu zao hivyo ni kigoli diana pekee ndie nilie mkuta kijijini…. leo goroza atakunywa damu ya mtoto wa mwanachama mwenzetu” yule msaidizi wa gunzani alifahamika kwa jina la gola aliongea huku akitabasamu na kumchukiza mama diana
“HAIWEZEKANI GOLA” mama diana ali maka
“ah nini tena mama diana? sisi sote tunaishi ndani ya moyo wa goroza japo nyie ni binadamu na sisi ni majini tunao jivisha miili na taswila za kibinadamu acha goronza anywe damu ya diana ili mkuu gunzani arudi kwenye madaraka” gola alifafanua na wale wengine waka afiki kwa kutingisha vichwa…
Mama diana hakutaka kukubali kwani alijua ni wazi kwamba nitamaa za kimwili zilizompelekea gola kumkamata diana mwenye sifa za urebo kwani kabla ya damu ya kigoli kumfikia goroza hua lazima gola amuingilie kimwili kigoli huyo mpake apoteze fahamu kisha huawawa..
“wewe mpuunzi na jua ni tamaa za kumtamani mwanangu nasema sikubali” mama diana alipinga vikali
“Umeniita mimi mpuuzi” gola aliuliza huku akisogelea mama diana huku akiwa kachukia kama mbongo
“ndio matamanio yako unaleta kwa mw”.. kabla hajamaliza sentesi yake mama diana alipigwa kifuani pigo zito kutoka kwa gola na kutupwa hewani na kuanguka nyuma hatua kadhaa … yowe kali lili mtoka mama diana na kusababisha magwi ndani ya msitu ule. yowe lile lifika mpaka pangoni alipokuwepo kuwepo yule bibi kizee na mwili wa gunzani.
*************——***********
Gari aina ya land cruser iliyo kuwa ya kampuni la utalii ikiwa ime pakia wasichana watatu na wanaume wawili pamoja nadereva jumla walikuwa sita ndani ya gari ile iliyotumika kubeba watalii kutoka nje ya nchi lakini siku hii ilikuwa haina raia wa kigeni hata mmoja gari ile ilikuwa imepakia vijana wa kitanzania waliokuwa na urafiki mkubwa.
Safari yao ilikuwa ni ndefu sana walikuwa wametokea mbuga za mikumi na sasa walikuwa wameipita morogo wakielekea kuuikalibia msata ambapo walipanga wange katisha na kuifuata bara bara inayo elekea KIWANGWA kisha wapasue msitu na waingie kijiji cha MVILA ambapo wange shika bara bara inayo ilekea bagamoyo ambako huko walisubiriwa na wana chuo wenzao kwenye hotel mpya iliyokuwa pembezoni mwa mwa ufukwe maridhawa.
Wote waliokuwa kwenye gari hili walikuwa ni wanafunzi wa chuo kasoro dereva yeye alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni la utalii.
dereva aliendesha gari kwa mwendo usio wa kawaida alihitaji awahi kufika ili waanze kusherehekea usiku wa mwaka mpya.
Ghafla wakati akiendelea kukimbiza gari aliwaona asakali wa barabarani hatua kadhaa mbele wakimpugia mkono na kumsimamisha hakuwa najinsi ikamlazimu kupunguza mwendo.
“Aisee unaendesha gari kwa fujo tumezipata habari zako kutoka kijiji ulicho kipita sehemu ya kuendesha speed hamsini wewe umeendesha speed zisizo pungua mia… ongoza gari kwenye kile kituo chetu tukague gari yako” asakali wa bara barani aliongea huku kichwani mwake akiwaza kuwa lazima apate dollar nyingi kama hongo kwani alijua gadi ile imebeba watalii wa kizungu…
Dereva aliendasha gari mpaka kituo kile kidogo kisha akashuka akifuatiwa na wenzake..yule askali uso ukamshuka baada ya kujua wote mule ndani walikuwa ni watanzania wazo la kupata dollar likamyayuka ghafla…
“kagueni mizigo yote humo ndani” akawaamulisha wenzake yeye akawa ana muhoji dereva
“unaitwa nani?”
“baraka “
“unatoka wapi?”
“mimi ni dereva wa watalii ndani ya nchi natoka mikumi na watalii wangu” baraka alijibu na kumkabizi liseni yake pamoja na nyaraka za watalii wake..
askali akawa anazipitia mara ikasikika sauti kutoka kwa askali waliokuwa wanashusha mizigo na kuikagua gari
“afande kuna bunduki ndani ya gari lao” sauti ilimshitusha askali alio kuwa anamuhoji hadi watalii wale walihamaki macho yao yakimtazama askali alie shikilia bunduki ilio kutwa ndani ta gari.
“kha! wewe nini jangili..?” askali alimuhoji baraka huku kichwani akiona ameshapata deal
“kila dereva ana kabidhiwa bunduki na kampuni kwa ajili ya kujitetea anapo kutana na matatizo safarini” baraka aliongea bila wasi wasi akaingiza mkono mfukoni na kutoa hati miliki ya bunduki ile.
Askali akachoka..
“ok unapigwa faini ya kuendesha gari kwa mwendo usio salama kijjini hivyo unatakiwa kulipa faini ya elfuthelathini” askali aliongea na baraka akatoa waleti na kumuhesabia pesa ile.
“pakieni vitu vyao waondoke.. ila kijana muda umeenda ni hatari kusafiri na watalii usiku” askali alitimiza wajibu wa kiusalama
“tunaenda kulala chalinze” baraka aliongea uongo kumdanganya afande
“ok safari njema …naona vijana wameweka mambo sawa”
Baraka na wenzake wakaingia kwenye gari na kuondoka bila kujua pale chini walisahau kidumu chao cha maji cha lita tano kilicho sahaulika kupakiliwa na wale askali…
hili lilikuwa tatizo kwenye safari yao!
Baraka aliendasha gari na kuingia msata kisha akaiacha bara bara inayoelekea mbezi yeye akaelekea bara bara inayo katiza kijiji cha mvila kuelekea bagamoyo na jua lilikuwa lina zama!
**********;*;;*;;;****************
Yule bibi kizee aliuacha mwili wa gunzani na kutoka nje ya pago ili kujua yowe lile lilikuwa la nini hasa
“kuna nini wana wa gozola” kikongwe yule aliuliza
“huyu mjiga mama diana hataki mwanawe kuwa zawadi kwa gozola” gola alidakia
“Hatuna haja ya kuuana sisi kwa sisi leo usiku mtapata damu ya kutosha na gozola atalizika…. kuna watu wanakuja kupitia ukanda huu leo leo wote sita watakuwa chakula chetu usiku huu” bibi yule kizee aliongea kwa sauti ya juu huku kichwani mwake akiwaona wale watalii wakiendeshwa na baraka….!
“ndio wanakuja kupitia barabara jirani leo tutafurahia damu zao” aliongea tena kwa msisitizo.
USIKU WA KAFARA.
Wote walikuwa kimya hata gola nae hakusema kitu.
“haya kila mtu arudi mahali pake na binti wa mama diana ahifadhiwe mpaka nitakapo rudi kutoka ndani” yule Mzee ali waamulu
“sawa malikia” wote walijibu na kuanza kurudi sehemu waliyo kaa mwazo huku mzee juma akimuhifadhi vizuri yule binti kigoli diana.. na yule malikia kikongwe akarudi tena pangoni aakanene na gunzani.
*****************
Baraka aliendesha gari kwa speed tena kwa umakini mkubwa
“Dah hawa askali wametupotezea muda mwingi sana” baraka aliongea na kuvunja ukimya wa punde
“Ah ila mimi niliogopa sana nilipo muona yule askali katoa bunduki kwenye gari yako ” sauti ya msicha mmoja kati ya wale watatu aliongea
“Umeonae dolla …halafu wewe baraka unatabia mbaya kumbe una bunduki humu muda wote huja tuambia” msichana mwingine alidakia kumuunga mkono msicha dolla namsichana huyu alie dakia aliitwa Neema
“AH vitu vidogo sana kumiliki bunduki kama ile kwangu kama fimbo tu” baraka aliji gamba
“ehee ulisha anza kujisifu mr misifa …sio ajabu hata hajui kuitumia bunduki yenye” sauti ya kiume kati ya wanaume watatu ndani ya gari ile ili msanifu baraka kwa kumtania
“Umeonaeeh john kaishaanza kujisifu” kijana wa tatu aliimuunga mkono john . nahuyu aliemuunga mkono john aliitwa Gadyson huku
wote wakicheka…
Kabla kicheko chao hakijaisha baraka alikanyaga brek ya ghafla kisha wote wakayumba kwa kwenda mbele na kurudishwa nyuma na muda huo baraka akashuka na kwenda kuufungua mlango wa nyuma kabisa kulipo kuwa na mizigo akaipekuwa na kuichukua ile bunduki akarudi nayo kwa wenzake akaingiza mkono mfukoni akatoa mfuniko wa simu akamkabidhi john na kumwambia auinue juu mfuniko ule..
“ENHEEE hivyo hivyo uinuie juu nataka ni ulenge niupige risasi huo mfuniko” baraka aliongea huku akirudi nyuma akawa anaikoki kwa kuvuta kitasa kichoopo juu ya bunduki ile
“ahh acha boya wewe” joh alimaka huku gadyson akitaka kuingia chini ya kiti na muda huo baraka akaanza kuwacheka
“mbona mmeogopa si mmesema sijui kuitumia” baraka aliongea huku maneno yake yakiambatana na kicheko….muda huo wasichana walikuwa wakicheka kwani wanayajua masihara ya hawa vijana watatu..
“haya tazameni jinsi ya kuitumia ” aliongea na wote wakamtazama
“ukitaka kupiga una vuta hiki chuma cha standby kisha hii triger unaibonyeza kwa kidole cha shahada …” aliongea kisha akageuka akailekezea bunduki mstuni na kufyatua risasi na mlipuko mkubwa ukasikika pale na wale wote watano waliziba masikio
“HAPPY NEW YEAR” baraka alilalama kwa sauti ya kusherehekea
“Oya mzee wa manchester tuondoke naona ushaanza sifa zako” gadyson aliongea baraka nae akarudisha ile bunduki huku akicheka
“kumbe wa oga .. ” aliongea huku akifungua mlango wa nyuma akaiweka juu ya mizigo akafunga mlango akaingia kwenye uskani..
“Yani huyu jamaa kila kitu chake anacho penda kibaya hilo bunduki lake bovu bovu sauti yake mbaya hata mwizi akija na mshale ana kutagisha… bado timu unayo shabikia mbovu….unavyo penda vyote vibovu kasoro demu wako neema” john aliendeleza tena utani huku wale mabinti wakicheka
“acha wewe huyo movic ana goli kumi na moja bado mbili amkamate coasta then spurs man city asanal tupo nyuma yao tuna wakimbiza na baiskel lao la miti..nyie acheni timu yangu noma “baraka aliongea huku akianza kuchochea speed
“Ila hawa watu wana masihara sana wamenifanye niwe na furaha sana huu umekuwa mwaka mpya wa furaha sana nime enjoy kupita kiasi” ilikuwa ni sauti ya sarah msichana wa tatu ambae muda mwingi alikuwa kimya akicheka na kufurahia ucheshi ulio endeshwa na kina baraka.
“Hata mimi nime furahi sana NASHUKURU MWAKA HUU NIMEUMALIZA SALAMA! kuanzia mwanzo wa 2016 mpaka mwisho sija sumbuliwa na homa maradhi wala matatizo yoyote nimevuka mwaka salama thanks god” gadyson aliongea akiwa kwenye furaha.
Sehemu Ya 2
NAAMU ! gadyson alihesabu kuwa amesha umaliza mwaka 2016 ! ama kweli usio lijua ni usiku wa giza mpenzi msomaji…
Safari ya furaha ilizidi kusonga huku maongezi ya kiucheshi yakitawala ndani ya gari lile..
Wakati baraka anaendelea kuendesha mara ghafla aliutambua muungurumo tofauti kwenye gari yake na hapo akakunja sura akilaani
“Ah chuma kilishaanza kuchemsha acha niweke maji ili ipoe mdogo mdogo” baraka aliongea huku akifunga brek na kuchukua touchi na kushuka nayo akazunguka kwenye mlango wa mizigo akaufungua na kulitafuta dumu la maji lakini hakuliona..
“ujinga huu hili dumu limeenda wapi” aliongea peke yake huku akizidi kupanga na kupangua mizigo lakini ilikuwa kazi bure…
“wadau kidumu cha maji tume kitupa wapi” aliwauliza wenzake na wao hawakujua
“kwani wale maafande walikirudisha kweli? maana walikishusha ule muda walipokuwa wana kagua” sarah aliwakumbusha wenzake..
“aah pumbavu zao watakua hawakukipandisha” baraka aliwalaani wale askali wa barabarani… baraka akafunga mlango wa mizigo na kurudi kwenye uskani.
“Hapa ina bidi niendeshe mwendo mdogo mdogo kwani gari inakaribia kuchemsha… ila kilo meta kazaa kutoka hapa kuna sehemu ina mashine ya walter wind hapo kuna kisima tutapata maji” baraka aliongea na wenzake wakaafiki na safari iliendelea kwa mwendo wa speed hamsini.
Kila walipo zidi kutokomea ndipo gari nayo ilizidi kuchemsha na baraka nae akapunguza speed hatimae gari ikawa inatembea taratibu kabisa kana kwamba ilikuwa kwenye foleni za tanzara.
Na mwishoe kabisa gari ile ilizima kabisa na baraka alijaribu kuwasha lakini haikuwaka hata kwa kujaribu…
Wakawa wamekwama katikati ya msitu na hapakuwa mbali sana na lile pango la goroza!
******–*********;**************
Malikia wa viumbe wale yule mzee kikongwe alikuwa ndani ya pango akisubiria kwa hamu muda ufike na kwenye taswila yake aliwaona jinsi kina baraka walivyo hangaika na gari lao ..!
kikongwe yule aliwasha mshumaa mkubwa uliokuwa pembeni ya sanamu la goroza na kupunguza kiza ndani ya pango..
“Sadaka imefika …” aliongea na kuanza kutoka nje ya pango lile huku kichwani mwake akiliona lile gari la kina baraka linavyo jikokota kwa mwendo dhaifu…
“Haya muda umefika mbweha mtaenda kuchukua sadaka sita zipo barabarani ….mzee juma njoo nikuoneshe ukawachukue tuje tufurahie damu zao” malikia kikongwe aliongea baada ya kutoka nje na mzee juma haraka akamsogelea mzee yule..
Kwa hisia na maajabu malikia akamuelekeza mzee juma sehemu waliyo kwama akina baraka.. na mzee juma kwa muujiza mkubwa aliwaona wale marafiki sita waliokuwa ndani ya gari .
“Haya chukua mbweha sita uwaongeze mkalete hiyo zawadi ” malikia alimuamuru mzee juma…
Wakatoka vijana sita kwenye kile kikundi cha washirikina wakiongozwa na mzee juma wengine wakiwa na mishale mashoka na wengine mikuki huku wengine mapanga ambayo hutumika na kikosi hiki cha mbweha kukutolea sadaka .
jumla walikuwa saba wakaanza kuondoka kwa kukimbia wakielekea barabarani kuwachukua akina baraka ….huku mioyo yao ikiwa imetawaliwa natamaa ya kumwaga damu…
“gola mchukue diana mrudishe kwao haraka kwanjia ulio itumia kumleta” mzee yule akamuamuru gola ambae hakupendezwa na amri ile kwani nia na matamanio yake ilikuwa kwa msichana diana usiku wa leo.
Gola akamuinua diana ambae hakuwa na fahamu kabisa akamuweka begani kisha akamtazama mama diana kwa macho ya chuki.
gola akageuka na kutikomea akiwa na diana begani…
“Haya mliobakia anzenu ibada ya kukaribisha sadaka ya usiku huu wa kafara”….. yalikuwa maneno ta malikia….
31December.
Baraka alishuka na kwenda mbele ya gari na kufunua lile bati linayo ifunika injini na hapo macho yake yaka kutana na moshi kutokea kwenye injini.
“Dah gari imechemsha tukisema tuisubiri ipoe inabidi tukae saa zima ….ila kutoka hapa hadi kwenye mashine ya wind walter ni kama dakika kumi na tano hivyo napendelea tukachukue maji huko ili tusichelewe sana” baraka aliongea huku akiliangalia gari lake lilio fuka moshi…
baraka alikuwa mzoefu wa barabara hii mara nyingi alishawahi kuitumia na kutembea sana eneo la wind walter
“dah hii ilishakuwa mbaya na mama nilimuahidi nitampigia jioni mpaka sasa hivi saa mbili usiku sijampigia na hapa naona mtandao haukamati” sarah alilaani maana alijua muda ule wazazi wake wanamtafuta kwenye simu…
“Ah usijal chukua tablet yangu uwa pigie kwa namba yangu ya zantel maana zantel hapa ina kata kwa njia ya satelite” baraka alio ngea kisha akawageukia gadyson na john
“oya wazee wa kazi tufanye maamuzi ya haraka” baraka aliwasihi
“ok kama vipi hawa bibie tuwaache sisi tukachukue hayo maji haraka” john aliongea na muda huo baraka akafungua mlango wa mizigo na kuchukua dumu lisilo na kitu ndani kisha akamsogelea neema.
“sasa jamani tunawaacha humu kwenye gari sisi tunakuja haraka” baraka aliongea na kumbusu neema kwenye paji la uso(neema na baraka walikuwa na mahusiano ya kimapenzi”
John nae alimsogelea msichana dolla na kumbusu kwenye midomo yake…”kuwa na amani sawa mpenzi” john aliongea baada ya kumpiga busu na dolla alitikisa kichwa kuafiki. ..pia john na dolla walikuwa ni wapenzi
Ni sarah pekee ndie alikuwa msichana asie kuwa na mpenzi kwenye safiri ile yeye mpenzi wake alikuwa akimsubiri kwenye ile hotel walio panga kwenda kushrehekea mwaka mpya pale bagamoyo.
Gadyson nae hakuwa na mpenzi kwenye safari ile ila kuna wakati alijaribu kumchombeza sarah walipo kuwa mbugani mikumi, lakini sarah alionesha msimamo na gadyson akawa kalifutilia mbali lile swala.
Baraka akachomoa ufunguo wa gari yake na kuutia mfukoni akiwa na kidumu aliwasha touch yake yenye mwanga mkali akaaanza kuongoza njia akiwaongoza john na gady kuelekea kwenye maji wakiwaacha wasichana watatu ndani ya gari.
Tayari ilikuwa ni saa mbili usiku na upande wa magharibi mwezi mkubwa wa kuvutia ulikuwa una chomoza.
Kile kikosi cha vijana mbweha kikiongozwa na mzee juma kilikuwa kime wasili eneo lile kwa usiri na ukimya wa hali ya juu na wao walikuwa upande wa pili wa barabara na waliwashuhudia akina baraka wakiwaacha wasichana ndani ya gari na wao wakitokomea ndani ya msitu.
“sasa watu watatu wafuateni hao wa kiume sisi tunaenda kuwakamata hao wasichana wao tuna wapeleke kwa goroza” mzee juma aliongea na muda huo vijana watatu wakainuka na kuwafuata kina baraka …vijana watatu hao walifuata kwa kuwazunguka na kwa mwendo wa ukimya mkubwa.
“dalu wanyatie kimya kimya na wasikuone ukifika jaribu kuufungua mlango wa gari” mzee juma aliongea na kijana dalu akiwa na panga aliondoka akiwa kajikunja kuanzia kiunoni huku aki hama mti hadi mti akihofia ule mwanga wa mbala mwezi usije kumfanya aonekane.
Ilimchukua dakika kumi na mbili kufika pale kwenye gari ali kokota kokota akiwa anatembele magoti aliufikia mlango na kujaribu kuvuta kile kitasa lakini haukufunguka akauwacha na kutambaa tena ili akajaribu kufungua mlango wa upande mwingine..
Ndani ya gari wasichana hawakutambua lolote dolla na neema walikuwa wakisikiliza mziki kwenye ear phone na sarah alikuwa busy na tableti akihamisha namba za wazazi wake ili awapigie…..
Baraka na wenzake walitembea kama dakika kumi kisha akasita kichwani kwake akiwa kuna kitu amekumbuka
“ah nime fanya ujinga ujue humu ni mstuni na kuna wadudu wa na wanyama siku paswa kuiacha bunduki” baraka aliongea huku akisimama
“ilo nalo neno” gadyson alijibu
“ok ikimbilie sisi tuna kusubiri hapa” john aliongea na baraka akaweka dumu chini akaanza kukimbia kuirudia bunduki yake huku touch yake ikimulika msituni mule ipasavyo .
Dalu wakati ule ana zunguka ghafla aliona mwanga wa touch kwa mbali ukija kueleke kwenye gari akahamaki na haraka akajua kina baraka wana kuja… haraka dalu akaingi uvunguni mwa gari…
Sarah alijaribu kumpigia mama yake lakini mama yake alipo pokea simu sarah aliisikia sauti ya mama yake lakini mama yake hakumsikia sarah..
“dah mtandao una sumbua kweli” sarah alisema na hapo akaona mwanga wa touch ukija upande wao “oh mara hii wamesha pata maji… ngoja nishuke nimpigie mama huenda nje ya gari nitaongea nae vizuri” sarah aliongea na kutoa lock ya mlango na kushuka akakifuata kisiki cha mti wa mbuyu akakipanda mara moja na kuanza zoezila kumpigia mama yake..
na muda huo baraka nae alikuwa ameisha ifikia gari…
31December
“haloo nani mwenzangu” sauti ya mwanamke upande wa pili iliuliza na hapo moyo wa sarah ukachanua kwa furaha na akazidi kusimama imara juu ya kisiki kile
“mama mimi ni sarah simu yangu imeisha chaji ila moyo wangu hujaridhika mwaka 2016 upinduke bila kusikia sauti yako” sarah aliongea kwa furaha
“asante mwanangu tumekupigia sana ukawa hupatikani upo wapi muda huu” sauti ya mama sarah iliuliza kutokea upande wa pili
“Ah nipo bwenini muda huu najisomea” sarah aliongea uongo kwani wazazi wake walijua yupo chuo hakuwashirikisha chochote kwenye safari hiii
“haya mwanangu nimemtuma dereva wetu akuletee zawadi nilizo kuandalia kwa pongezi ya kuvuka mwaka 2016 salama …ni zawadi nzuri sanaa mwanangu acha nimtumie na hii unayoitumia ili asipate tabu” mama sarah aliongea kwa wahka mkubwa na kukata simu.
moyo wa mariamu ulipiga kwani alijua ataumbuka akiwa pale juu ya kisiki akashindwa afanye nini ili kumdanganya tena mama yake… na simu ilikuwa imekatwa!
Baraka alisogea mpaka kwenye kioo cha gari walipo kuwepo neema dolla kisha akagonga na wasichana wale wakafungua
“mbona upo peke yako ” neema aliuliza
“nilisahau bunduki si unajua njiani tunaweza kukutana na swala …akawa bahati yetu” baraka aliongeakwa utani huku kumtupia sarah alie simama juu ya kisiki ..
Ghafla yowe kubwa lilimtoka baraka kurunzi alioshika ikimdondoka huku akihisi kitu chenye ncha kali kikimcho kwenye paja lake…
Naamu ulikuwa ni mshale ulio fyatuliwa ki ustandi ukitokea kwenye upinde wa mzee juma ndio mzee juma alikuwa ameamua kuanza kazi na hilo lilikuwa shambulizi lake la kwanza.
Dolla na neeama walishtuka sana hawakujua nini kimemtokea baraka ambae alikuwa chini akigaagaa huku kilio cha maumivu kikimtoka.
Yowe lile lilimshtua sana sarah hadi kufikia hatua ya kuichia ile tablet bila kujua akageuka kuangalia kule kwenye gari.
“nini baraka” neema alipaza sauti huku akisukuma mlango
“nimechomwa ….. ni mshale” baraka alilalama muda dolla alikuwa kwenye bumbu wazi ya aina yake..
Neema alijaribu kushuka amuangalie mpenzi wake lakini hapo hapo kwa kihoro kikubwa alishuhudia watu watatu wakiwa na siraha za kienyeji wakija mbio kuelekea upande wao ikawa zamu ya neema kupiga yowe la kuhitaji msaada
“mamaaa aaaa!” nema alijikuta akimuita mama yake huku akifanya jitihada za kurudi ndani ya gari wajifungie..
Sarah alikuwa anapiga hatua kusogelea gari “kuna nini ” alijiuliza moyoni huku fikira zake zikidhani alitamka kwa sauti na ghafla macho ya sarah yali mshuhudia dalu akitoka uvunguni mwa gari akiwa na panga … na muda huo akasikia yowe la neema.
Hapo sarah alihamanika na upeo wake ukatambua roho zao zilikuwa hatarini , sarah aligeuka na kuanza kutimua mbio akitokomea msituni huku akijaribu kuita ba kupiga kelele za kuomba msaada msaada na nyuma ya yake dalu alimkimbiza kwa mwendo wa ajabu…
Upende wa gadyson na john********kabla ya yowe*********
“Dah kimsitu kimetulia hadi raha” john aliongea wakati wakimsubiri baraka..
“mazingira yapo poa simu yangu ingekuwa na flash light ninge..” gadyson alionge kisha akaacha huku macho yake yakiwa yame ona kitu kwa mbali kitu hicho kikiwa kama kimehama kutoka mti hadi mti mwingene na kisha haku kiona tena.
“Ebwana nimehisi kama kuna kitu ama mtu alikuwa kule” gadyson aliongea
“wapi….”john aliuliza na gady akamuonesha lakini wote hawakuona kitu…
“hizo pombe ulizo kunywa mchana bado hazija kutoka kichwani”john aliongea huku akicheka
“dah kweli acha nikakojoe huenda bado nipo kwenye hangover” gadyson aliongea huku akisogea kama hatua kumi na na akawa ana kojoa akimuacha john akibonyeza bonyeza simu yake….
Nyuma ya john waliibuka watu wawili walio mnyatia kwa kumvizia na muda ule walikuwa nyuma kabisa ya mgogo wake …
Ghafla john akijikuta akikabwa kwa roba kali akahamanika vikali simu yake ikamdondoka akawa analeta purukushani akitupa mikono hovyo huku akikosa nafasi ya kupiga kelele kwani roba kali ilikuwa imebinya koromeo lake ipasavyo… na muda ule ule mikono yake ika kamatwa na kufungwa kamba ..
Gadyson alihisi purukushani na alipo geuka alimuona john akiwa kakabwa na mtu mmoja huku mwingine akimfunga kamba mikononi….
na muda huo huo macho mawili yalishudia mtu mwingine wa tatu akija upande wake akiwa na gongo mkono wa kulia huku mkono wa kushoto ukiwa na shoka …
wakati akiwa kwenye kihoro kikubwa hapo hapi akasikia yowe la baraka kwa mbali….
Tume vamiwa. !!!neno hili lilipita kichwani na muda huo gady alipiga hatua kadhaa na kuanza kukimbia ..
Lakini kabla hata ya kukimbia hatua ishirini gongo lilio rushwa na yule bweha wa goroza lilitua kichwani kwake na kumtupa chini kama mzigo huku akihisi kupoteza fahamu……
Alijiinua tena na kukimbia safari hii alikimbia bila tahadhari na huku giza dogo ukichanganya na kupigwa kichwani na lile gongo hakuona vizuri mbele na hatimae aliuvaa mti na kuanguka chini na muda huo huo aliona mtu mwenye shoka akimsogelea sehemu ile aliyo anguka!
“pumbavu usijitikise shoka hili litaka kata shingo yako” yule mtu alimfokea….
INAENDELEA

