UJI MZITO
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA 1
Waswahili husema ni bora kukata kiuno kuliko kukata tamaa kwenye maisha, kila mtu huwa na ndoto yake, sio ile inayotawala ukiwa umelala bali ile inayokufanya usilale. Katika chombezo hili tutamzungumzia kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Mbosoni Kakei. Ni mhitimu wa chuo cha veta mahiri kwenye masuala ya umeme. Alitoka na cheti kizuri sana lakini ndio hivyo nchi yetu basi la ajira limepotelea kusikojulikana.
Juhudi za kutafuta kazi mjini ndizo zilizomwokoa na kuufanya mkono wake uende kinywani. Alipanga chumba ambacho hakikuwa katika hali mbaya sana. Hata kama siku akiwa hana uhakika wa kupata kazi, hakukaa nyumbani, alitoka kutembea akiamini mkaa bure sio sawa na mtembea bure.
Kila siku alfajiri lazima Mbosoni aamke na kwenda uwanjani kufanya mazoezi, huko hukutana na watu mbalimbali, vijana wa kike kwa wa kiume, kinamama na kinababa, mpaka wazee, hivyo hujumuika nao. Siku zote alikuwa akifanya mazoezi na kuondoka lakini siku hiyo aliamua kuwashirikisha wanamazoezi hao juu ya ujuzi wake akiamini riziki popote. Walipomaliza mazoezi aliwakusanya pamoja wengine walikuwa kama wazazi wake. Mbosoni alishangaa baada ya kuwaambia walimpongeza na wakakubali kuchukua mawasiliano yake, hilo likawa jambo jema sana kwa Mbosoni.
Hisia ni kitu cha ajabu sana, siku hizo zote alizokuwa akienda mazoezi, alikuwa akimtamani sana mama Fulani wa kikubwa ambaye alikuwa akija mazoezini na mume wake. Mama huyo ni kweli Mungu alimbariki umbo la kutochoka mapema, alikuwa ni mzuri kupita maelezo, “enzi za ujana wake alikuwaje?” lilikuwa ni swali alilojiuliza Mbosoni asipate jibu. Hakuwahi kumsemesha wala kumsogelea kwa karibu hata siku moja, aliishia kumpiga kijicho Fulani cha matamanio, na kuna muda walikutanisha macho yao, huyo mama na Mbosoni kisha kupotezeana.
Zilipita wiki mbili bila kuona simu yeyote kutoka kwa wale aliokuwa akifanya nao mazoezi. Sifa mojawapo ya wale waliokuwa akifanya mazoezi nao, ni pochi nene. Hawakuwa watu wa shida, kwanza walikuja uwanjani na magari yao, bado Mbosoni hakujua kwanini hawaendi ‘gym’ wanakimbilia uwanjani kufanya mazoezi, au hata nyumbani kwao isingeshindikana kutenga sehemu ya kufanyia mazoezi.
Siku hiyo mchana nikiwa kwa mchaga Fulani nikimfanyia ‘wayaringi’ nyumba yake. nilipigiwa na namba ngeni, kwangu namba ngeni huwa ni muhimu kama mwandishi wa hadithi kupitia mitandao ya kijamii maana asilimia kubwa huwa ni wateja, nilipokea,
“Sasa, unaongea na mzee Lomo hapa,”
“Ndio baba yangu heshima yako!”
“Ahsante, nyumbani kwangu kuna shida, nakuomba uende halafu utasaidizana na huyo fundi utakayemkuta hapo,”
“Sawa, nashukuru sana,”
“Nimeona nikushirikishe ili upate riziki na wewe ndugu yetu,”
“Ahsante mzee wangu ubarikiwe, nitumie maelekezo ya kufika kwako na sitachukua muda.” Basi mzee huyo aliyejitambulisha kuwa ni mzee Lomo, alimtumia maelekezo kisha akamtoroka mchaga wake na kuelekea alipopigiwa simu, hisia zake zilimtuma atakuwa ni mmoja kati ya wale matajiri anaofanya nao mazoezi alfariji.
Mpaka kwa huyo mzee, Mbosoni aliwasili, kilichomwezesha kuwahi katika kazi zake ni usafiri wa pikipiki aliyokuwa nao ambayo ilikuwa katika hali mbaya kweli. Kwanza hata kuingia ndani ya hilo geti haikuruhusiwa, yeye pekee ndio alifanikiwa
kuingia. Ilikuwa ni nyumba ya kifahari, kwanza hiyo mitaa yenyewe ni ya kifahari kweli.
Alhamdulilahi! Hamadi bin vuu! Huyo hapo yule mama aliyekuwa akitamaniwa sana mazoezini na Mbosoni. Hakuamini macho yake, na hapo ndipo alipozihakikisha hisia zake kuwa ni kweli simu hiyo ilitoka miongoni mwa matajiri aliokuwa akifanya nao mazoezi,
“Khe! Karibu mwanamazoezi,” alisema huyo mama,
“Ahsante, shikamoo mama,”
“Marhaba, karibu sana Jamani, jisikie huru,”
“Ahsante,” kwa maongezi hayo, yalimsogeza Mbosoni mpaka sebuleni na kuketi. Masikini Mbosoni wa watu sijui hisia zilimpeleka wapi, alipoona tu chura ya huyo mama ikipigana vikumbo ndani ya khanga, tayari msumari wake ulishajiandaa kugongelea…
SEHEMU YA 2
Mama la mama alirejea sebuleni akiwa na glasi ya juisi ya embe iliyotoka kwenye jokofu. Alimpa Mbosoni kisha yeye akaketi kwenye sofa la jirani, mama hakuwa haba, alijaaliwa weupe usiokuwa hata na doa, umbo halisi la kiafrika, huo uso ndio usiseme, yaani kama mtoto kumbe ni mtu mzima. Hilo umbo lilijaa ushawishi kuliko hata ulivyoweza kumfikiria, sasa kama wakati alipokuwa akiketi sofani, kile kikhanga chake kilifunuka na kumfanya Mbosoni afanye utalii wa ndani uliozidi kuutia msumari wake joto la hasira.
“Hivi ndio unaitwa nani?” alimhoji
“Mbosoni,”
“Ooh! Karibu sana, ila mimi napenda sana kuwaita watu majina yao kifupi,”
“Aah! Mimi kifupi huwa sina, watu huwa wananiambia kifupi cha jina langu ni jina la msanii maarufu huku wengine wakisema wakilifupisha zaidi itakuwa sio jina zuri japo ndio watu wengi wananiita hivyo,” Mbosoni aliongea hivyo, basi huyo mama alicheka ile ya kushtukiza kisha akamkata kijicho Fulani Mbosoni
“Hiko kifupi ndio wanakuitaje?” Alihoji huyo mama huku sura yake ikiwa katika hali ya kutaka kuangua kicheko
“Yaani mama we acha tu,”
“Haya bwana.”
Mbosoni hapo sebuleni unafikiri ile juisi ilikuwa inashuka! Ni kama kulikuwa na kitu kimemkaba kooni, alimtamani huyo mama mpaka kuna muda alitaka amtongoze ila roho ikasita kufanya hivyo.
Kabla hata ya kupita sekunde thelathini, honi ya gari ilisikika. Mlinzi akafungua geti,
“Huyo atakuwa fundi mwenzako,” alisema mama huyo
“Samahani mama, hivi unaitwa mama nani?” swali hilo lilimfanya awe mpole ghafla usoni, ni kama lilikuwa na ganzi iliyomwingia mama huyo, ilinibidi Mbosoni ajirudi
“Samahani mama kama nimekukwaza,” alilimtaka radhi, mama huyo hakumjibu kitu bali aliingia ndani.
Mbosoni alichukua kama dakika moja kuwaza kitendo hiko, aliona atoke nje. Alipotoka tu alikutana na rafiki yake wa muda mrefu sana waliyesoma wote shule ya msingi na sekondari. Kwa jina aliitwa Sadick, walikumbatiana kwa furaha na kuanza kushangaana kwanza, kila mmoja alimshambulia mwenzake kwa maswali yaliyolenga kukumbushana enzi hizo wakiwa shuleni.
Basi walifanya kazi wote kwa ushirikiano kutatua tatizo kwenye eneo hilo, walikuwa watu wa utani sana,
“Naona sasahivi unang’aa tu, maisha mazuri gari ya kufanyia kazi,” aliongea hivyo Mbosoni
“Tulia mbo, mbona unasimama na hujaonyeshwa utamu,”
“Sio hivyo Dick, maisha magumu ujue!”
“Hayo tutaongea, kwanza nikuulize kitu,”
“Huo mkao lazima uulize kuhusu wanawake,” wote walicheka kwasababu walijuana sana
“Huyu mama namtamani tangu kitambo ila ni muoga na hapendi mambo ya kuzoeana, sasa…”
“Sasa nini?”
“Nimekuona ukitokea ndani, sijawahi kukaribishwa ndani, na muda mwingine nikifanya kazi hapa kwake huwa hata hatuonani, anajifungia ndani,”
“Yaani wewe hunizidi mimi, huyu mama mimi nampenda yaani kabisa! Hata angesema amwache bwana wake mimi nimuoe niko tayari, yaani pale kukaa naye tu tayari msumari ulishaanza kakamaa kama mgonjwa wa kifafa rafiki yangu,”
“Kwahiyo umeongea naye kabisa?”
“Ndio, mpaka juisi amenipa,”
“Juisi kabisa! Wewe (tusi..) ameshakupenda,”
“Ni ukarimu wake tu nadhani ila sikufichi Dick, huyu mama nimempenda kuliko masihara, huwa najizuia kila siku ninapokwenda mazoezi lakini wapi! Halafu kibaya zaidi kila ninapomwona sikufichi, hata kama nina shida zinaisha kaka!”
“Wewe umpende mtu! Wewe kabisa! Sema unataka kuhudumiwa nitakuelewa!”
“Kitu kingine ujue hajazaa,”
“Kweli?”
“Ndio, halafu huyo mzee anapiga vitoto vya seko asikwambie mtu,”
“Daah! Yaani mwanamke mzuri vile halafu unamsaliti, kweli hata ukifa utaunguzwa kwa kuchochewa na ile kuni kubwa kuliko zote iliyoko jehanamu,” wote wakacheka sana.
Kumbe wakati wote wanaongea, mhusika aliyekuwa akizungumziwa alikuwa akiwasikia kwasababu eneo walikofanyia kazi halikuwa mbali na dirisha. Kutoka ndani ya moyo wake alifarijika sana kusikia anapendwa tena na kijana, na amekiri kuwa sio pesa ndio lengo lake…
SEHEMU YA 3
“Kumbe kijana wa watu alikuwa amesimamisha muda ule? Kha! Ina maana bado nalipa eeh!”
Alijisemea hivyo moyoni huku akiendelea kumwangalia Mbosoni na kuzidi kumweka akilini. Mbosoni na Dick walipomaliza kurekebisha tatizo ambalo ilikuwa ni shoti ya kawaida tu, ilibidi wamuage huyo mama.
“Sitaki kukujazia nzi, wewe nenda,” Dick aliongea hivyo
“Twende wote bwana,” alisema Mbosoni
“Ngoja nikamtongoze!” Dick aliposema tu hivyo, Mbosoni alimzuia na kumtaka abaki
“Kumbe una wivu! Utakufa kumpenda mke wa mtu,”
“Kwa huyu mama acha nife tu!” maneno yote aliyoyaongea mbosoni, mama aliyasikia na yakamwingia akilini. Alibaki akitabasamu tu, aliwafaidi kwasababu vioo vya madirisha vilimwezesha kuona nje bila yeye kuonwa ndani.
Mbosoni alisogea mpaka mlangoni na kubisha hodi, alikaribishwa mpaka ndani, akakuta meza imechafuka, palikuwepo na chipsi pamoja na kuku wa kukaangwa.
“Mezani inabidi ushiriki,”
“Ahsante mama,” alijibu Mbosoni akijifanya ameshiba
“Wewe ni mchoyo eeh?”
“Kwanini mama unasema hivyo?”
“Ukila ndio nitajua wewe sio mchoyo, kwahiyo unatufundisha tukija kwako tusile sio?”
“Hapana,” basi alitoka nje kisha akamwambia Dick kuwa Mbosoni ana kazi nyingine kwahiyo anaweza akaondoka
“Sawa mama.” Dick alipojibu hivyo aliwasha gari kisha akaondoka
Sasa huku ndani Mbosoni alianza kutilia shaka ukarimu huo wa huyo mama, akahisi kupendelewa ila hakuwa na uhakika. Kwa muda huo mama alijisitiri kidogo japokuwa ndani ya kichwa cha Mbosoni ugonjwa haukumtoka. Alivalia sketi Fulani ujiuji iliyomkaba chura yake, huku juu alivalia blauzi iliyokuwa ikimwacha kidogo eneo la mgongo. Kitu kingine ambacho mama huyo alibarikiwa ni uvaaji wa mavazi yaliyomuweka kwenye chati, yaani ndio kabisa alizidi kuonekana ni mdogo. Hiyo miguu yake Jamani utadhani aliomba kibali kwa Mungu cha kujiumba mwenyewe.
Mbosoni alishambulia msosi huku mama huyo akiwa pembeni yake akila matunda aliyoyaandaa kwenye sahani. Mama huyo akawa anamwangalia Mbosoni kwa umakini jinsi anavyokula kwa ustaharabu, maneno yake ya ucheshi, hazikupita sekunde ishirini bila mama huyo kicheka hali iliyomfanya amwone ajihisi amepewa kampani ya kutosha.
“Mbo!” mama aliita, Mbosoni hakutegemea, ilibaki kidogo apaliwe chakula
“Naam mama,” aliitikia Mbosoni na kumwangalia mama huyo kwa sura ya kutaka kucheka iliyochanganyikana na aibu
“Chakula kitamu!”
“Saaaanaaaa yaani hata hakielezeki,”
“Kitamu kama nini,” hilo swali lilimsisimua Mbosoni na kujikuta akishindwa kumeza kuku huku msumari ukijipigiza ndani ya suruali yake
“Mbo!” alishtuliwa kwa sauti hiyo
“Hamna cha kufananisha kwa kweli,”
“Una uhakika?”
“Ndio,”
“Ila mimi ninajua cha kufanana na huo utamu wa chakula,”
“Nini?”
“Mbo!”
“Umesema?”
“Nimekuita, itika,”
“Abee mama,”
“Umekuwa mwanamke mpaka uitike hivyo?” Mbosoni na huyo mama wakajikuta wamecheka kwa pamoja. Kuna mambo ambayo yalishaanza kumpa ishara za ushindi Mbosoni alizoonyesha huyo mama, moja ni kukubali kumwita Mbo, ikiwa ni kifupi cha jina lake, pili ni kumwandalia chakula ambacho alihitaji ashiriki Mbosoni bila ya kuwa na yule rafiki yake Dick, tatu ni maswali Fulani ya kimtego aliyokuwa akiyauliza mama huyo. Kwa ishara hizo alitamani avunje ukimya lakini alipokumbuka huyo ni mke wa mtu, tena mtu mwenye pesa zake, mwenye uwezo wa kutumia pesa zake kukufanya chochote atakacho, mdomo ulikuwa mzito.
Baada ya chakula kidume kikaribishwa sahani ya matunda, wala hakuvunga, aliishindilia ipasavyo, kitendo kilichomfurahisha yule mama kupita maelezo mpaka mbosoni alishangaa, wakati akiwa anakula matunda, mama alimtaka radhi Mbosoni kwa muda ule alipokaa kimya pindi alipoulizwa anaitwa mama nani,
“Hilo halina shida mama,”…
INAENDELEA

