TAREHE 9 SEPTEMBER
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Sehemu Ya 3
Asubuhi palipokucha Zack alidamka mapema,, akaenda kufungua maduka yake.. kisha akawaacha wafanyakazi wakiendelea na kazi,, yeye akaingia ndani ya gari lake akaelekea kwa lafiki yake kipenzi,, ili ampeleke kwa mganga!
alipofika akamkuta rafiki yake anamsubiri! bila kupoteza muda wakaongozana mpaka ndani ya gari la Zack na safari ya kuelekea kwa mganga ikaanza!
walitumia lisaa limoja njiani, hatimae wakafika kwa mganga aitwae MANYENYE,,Nyumba ya Manyenye ilionekana kujengwa kwa miti na kuzungushiwa nyasi kavu,, na nje ya nyumba hiyo,, kulikuwa na mawe mawili makubwa kiasi yakiwa kando ya mlqngo wa kuingilia ndani ya nyumba hiyo,, lakini nyumba hiyo ilikuwa ni nyumba ya maajabu,, licha ya kuonekana ndogo kwa muonekano wa nje, lakini ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na vyumba miamoja (100) vikubwa,,Zack akaongozana na rafiki yake kuingia ndani ya nyumba hiyo,, akastaajqbu kuona ukubwa wa nyumba hiyo! tofauti ja inavyoonekana upande wa nje!!! Zack akaeleza shida yake kwa mganga,,
Manyenye akasema,, “ni jambo rahisi sana, hakuna linaloshindikana mbele yangu, mimi ndiye Manyenye wa Manyenye. aliongea hivyo huku akitingisha vibuyu viwili alivyokuwa kavishikilia mikononi mwake! kisha akasema,, “itabidi ufanye jambo la kijasiri,, Manyenye akasema chukua kisu hiki,, andika hapo chini jina lako kamili pamoja na ubini wako kwa kutumia kisu hiki,, kisha andika Jina moja la huyo adui yako unayetaka kumuangamiza..
Zack akaandika majina yake kamili pamoja na ubini wake. akiandika chini kwa kutumia ke kisu alichopewa na mganga! kisha akasita akavuta kumbukumbu,, akakumbuka kuwa aliona jina la mtu huyo kwenye simu ya Shamy ,limeandikwa SHIRIMA,, bila kuchelewa akaliandika jina hilo kwa kutumia kisu hicho!
Makanya akasimama na kunyunyizia dawa,, ghafla akasita.. kisha akamtazama Zack akasema,, “mbona umedanganya ubini wako.. hili jina la ubini wako sio sahihi,, halionekani kwenye maono yangu ya kimizimu! hilo jina lingine Shirima mbona linaonyesha kuwa ndio ubini wako! halisi na ndio chimbuko la damu yako! au umechanganya majina? Zack akashtuka mqcho yakamtoka!
zack akauliza kwa mshangao! ,,”unamaanisha nini? mbona sielewi! yani hili jina la huyu mshenzi unasema ndio ubini wangu? mimi sijachanganya majina,, umesma niandike majina yangu pamoja na ubini wangu! kisha ukasema niandoke jina moja la huyu adui yangu,, sasa yawezekana vipi jina la adui yangu liwe ubini wangu?
Mganga ajaribu tena kupiga tunguli,, akasita kisha akasema,, “jina la adui yako linaonekana ndio ubini wako sahihi,, sasa kama wewe unadanganya,, nakuomba toka uondoke zako,, naona umekuja kunijaribu!!
Zack pamoja na rafiki yake wakamuomba radhi manyenye kisha wakaondoka zao.
ilipofika saa moja za usiku Zack akarejea nyumbani,, akamkuta Shamy anajiandaa kwenda kazini(night shift)
Shamy akasema,, “pole na kazi kipenzi cha roho yangu,,
Zack hakujibubkitu chochote akabaki kimya! Shamy akastaajabu,, akauliza,, “kulikoni? mbona kama unahasira! ? nani kakukwaza?
Zack akasema,, “nahisi kama homa inaninyemelea..
Shamy akafungua droo akatoa chupa ndogo yenye kioo chepesi sana,, (Test tube) kisha akachukua bomba la sindano likiwa na sindano,, akasema wacha nichukue damu yako nikaifanyie vipimo,, huenda unamaralia!
Zack akasema,, “haina haja,, homa hii haiusiani na vipimo,,, kama kunavipimo vya mapenzi basi nahisi kipimo hicho ndio kitanifaa! Shamy akastaajabu! akauliza,, “unamaanisha nini mpenzi? mbona sikuelewi!
wakati shami anauliza hivyo,, simu yake ikaita,, alipoitazama akaona Shirima ndiye anampigia simu,, akaipokea kisha akasema,, samahani mkuu nipo najiandaa nitafika hapo muda mchache ujao.
Zack akasema,, “hivi huyo Shirima mbona huwa anakupigia simu kila siku! inamaana wewe ndiye daktari bora kuliko madaktari wengine wa hospotali hiyo! Shamy akawa mnyonge,, akasema,, “mimi ni wako tu hakuna wa kubadilisha mawazo yangu juu yako.
Zack akamtazama Shamy, kwa macho ya msisitizo.. Shamy akachukua mkoba wake akatoka nje ya nyumba akaingia ndani ya gari lake akaliwasha na kuelekea kazini!
baada ya dakika kadhaa Shamy akafika Muhimbili,,, akapitiliza moja kwa moja mpaka kwenye ofisi yake,, punde si punde Shirima akaja ndani ya ofisi ya Shamy,, wakasalimiana,, kisha Shirima akanza kumchombeza Shamy akiulizia kuhusu jibu la ombi lake! Shnamy akasema ,,”mimi nilikwambia kuwa ninamchumba na ninampenda kuliko mwanaume yeyote hapa duniani… kiukweli sina jibu zadi ya hilo,, samahani sana mkuu!
***********************************
Upande mwingine alionekana Baba yake Shamy akiwa chumbani na mkewe..
baba shamy akasema,,” kunajambo huwa nashindwa kulisahau,,jambo hilo lilinitokea miaka mingi iliyopita,, takribani miaka therathini na kadhaa,, Mama Shamy akauliza,, “jambo gani mume wangu!? mbona unanitisha! tafadhali ningependa kufahamu,.
Baba Shamy akaanza kusimulia;
ilikuwa hivi; kqbla sijastaafu nilikuwa naendeshwa kwenye gari na dereva wangu. alikuwa ni kijana mstaarabu na mwenye adabu,, jina lake nalikumbuka anaitwa SHIRIMA,, nikawa naambiwa na majirani kuwa mimi napokwenda kazi,, mke wangu anaondoka nyumbani anakwenda kwenye starehe,, alioonekana sehemu mbalimbali za starehe mara kwa mara…. nikaamua kununua mtambo maalumu wa (UCCTV) kamera za kurekodi matukio masaa24 mfululizo… kamera hizo nikazitegesha kwa kuzificha chumbani mwangu…siku moja nikapata safari ya kwenda nchini India kwenye semina ya wiki moja,, tulichaguliwa madaktari watatu watatu kutoka hoptili zote za Rufaa….
baada ya wiki moja kuisha nikarejea nchini…. nikaangalia video za matukio yaliyorekodiwa na zile kamera nilizozitegesha,,, mke wangu hakufahamu hilo,,kuhusu kamera hizo,, niliumia sana kuona anamshawishi Shirima afanyenae mapenzi,,ndani kwangu,, chumbqni kwangu mbaya zaidi kwenye kitanda ninachalala mimi na mke wangu.. nikaamua kumfukuza,,,kwa sababu alikuwa hana la kujitetea ushahidi kamili ulikuwa kwenye video zilizorekodiwa na kamera… akaamua kueleza ukweli kilichotokea akihisi huenda nikamsamehe,,, akasema,,”nilifanya hivi kwa sababu wewe hauna muda na mimi,, muda mwingi unakuwa kazini,, ukirudi unalala tu, hunipi haki yangu ya chumbani,,,sikufanya hivi kwa makusudi… mbaya zaidi ninaujauzito wake nisamehe mume wangu! Kiukweli niliumia kupita kiasi.. nikapoteza fahamu,, nikakimbizwa hospitali,, waliponifanyia vipimo nikagundulika nimepata ugonjwa wa msukumo wa damu ya kupanda,, (high blood pressure)
Niliporudi nyumbani nikaamua kumfukuza mwanamke huyo,,
mdogo wangu wa kike,, hakufurahia kitendo hicho cha mimi kumfukuza mke wangu.. akaamua kuishi nae nyumbani kwake… mimi nilifanya iwe siri yangu,, sikuwahi kumwambia mtu yeyote kuhusu hili.. mdogo wangu alinichukia sana,, akisema kuwa nimemfukuza mke wangu akiwa mjamzito.. na nimetelekeza ujauzito huo..aliishi hapo nyumbani kwa mdogo wangu,, mapaka siku ya lujifungua,, lakini baadae mwanamke huyo alikufa,, akabaki mtoto wake,, nahiso kama sikosei alimpa jina akamuita Zack…mdogo wangu aliendelea kunichukia huku akimwambia mtoto huyo kuwa mimi nilimtelekeza mama yake akiwa na mimba changa… mtoto huyo akaamini kuwa mimi ni baba yake,, lakini sivyo,,, pia nikajikuta namchukia sana mtoto huyo,, sikutaka hata kumuona,,,
Shirima akakimbia,, tangu siku hiyo sijui yupo wapi,, pia sijui kama yupo hai au ameshakufa… sana kwa kuificha siri hii lakini leo nimeamua nikwambie..
Mama Shamy akamtazama mumewe kwa macho ya huruma kisha akasema,, “pole sana kwa mkasa huu,, inahuzunisha sana….
Siku zilizidi kusonga,,Shirima hakukoma kumsumbua Shamy,,akimtaka kimapenzi..
simu za mara kwa mara zilizokuwa zinapigwa kwenye simu ya Shamy,, zilimfanya Zack,, aanze kuingiwa na mawazo ya kikatiri.. akaamua kuandaa mpango wa kumtafuta Shirima ili amfahamu kwa sura,, kisha aandae mpango wa kumuangamiza Shirima,,
Siku moja Zack alionekana kaketi kwenye hotel fulani hivi,,, akinywa mvinyo..kwa mbali akaonekana Shirima akiingia ndani ya hotel hiyo akaketi kando ya Zack.. wakasalimiana na Zack..
Zack hakuweza kutambua kuwa huyo ndiye Shirima adui yake. kwa sababu hakuwahi kumuona… punde si punde simu ya Shirima ikaita.. akatabasamu na kuipokea simu hiyo.. akasema kwa sauti kubwa kiasi,, “HALLOW SHAMY..
Zack akashtuka akajisemea moyoni,, “Shamy yupi?
wazo likamjia kuwa ampigie simu Shamy.. akatoa simu yake haraka akapiga namba ya Shamy,,, akashtuka baada ya kuambiwa,, namba ya mteja unaempigia anaongea na simu nyingine!
Zack akaingiwa na wasiwasi! punde si punde Shirima akamaliza kuongea na Shamy..
Zack akaamua kumpigia tena simu Mchumba wake( Shamy) simu iliita bila kupokelewa! Zack akahisi moyo wake unaripuka,, akajisemea moyoni,, “bila shaka yu alikuwa anaongea na Shamy wangu! watu wengine sijui wanaakili gani,,, jitu zima linatongoza mabinti… sasa kwa umri wake akijilinganisha na Shamy ni sawa na mtoto wake wa kumzaa,, zaki alijisemea moyoni huku macho yake yakionyesha amejawa na jazba,, akanyanyuka kwa hasira akaparamia meza chupa iliyokuwa na sada ikadondoka na kupasuka,, wateja waliokuwepo kando yake wakawa wanamshangaa Zack,, akazipiga hatua mpaka kule alipokuwa amelipaki gari lake,, akaingia ndani ya gari na kuliondosha kwa kasi ya ajabu… kuelekea nyumbani,
*********************************
Upande mwingine alionekana Shamy akiwa ndani ya gari lake,, akitokea kazini kuelekea nyumbani,, Shamy akajisemea moyoni,, “hii kazi ya kukesha usiku kucha,, inachosha sana mwili wangu hapa nilipo ninausingizi kupita kiasi,,
baada ya dakika kadhaa kupita Shamy akafika nyumbani, akaegesha gari lake na kuingia ndani ya nyumba! akapitiliza bafuni akaoga kisha akapanda kitandani kwa ajili ya kupumzisha mwili,
wakati huo huo alionekana zaka akiliendesha gari lake kwa kasi ya ajabu!,,,
alipofika akamkuta Shamy kajilaza kitandani,,, hata bila salamu Zack akachukua simu ya Shamy akaangalia kuwa Shamy kaongea na nani mara ya mwisho! macho yakamtoka akamtazama Shamy kwa hasira huku mwili wake unatetemeka… akasogelea na kuanza kumshushia kipigo kikali,, alimpiga bila huruma,, Shamy akapiga kelele za kuomba msaada huku akisema,, “JAMANI NAOMBENI MSAADA NAKUFAAA!
kelele za Shamy zikazidi kumpandisha hasira zack akajikuta anaachia teke kali lililompata Shamy kifuani kwenye titi la kushoto,, Shamy akadondoka chini akatulia tuli!
Zack akaingiwa na hofu,, jasho likamtoka huku anatetemeka,, akiamini huenda kauwa.
akamsogelea Shamy akamuita huku akimtikisa, uso wa Shamy ulikuwa na majeraha yna damu ilitoka kwa wingi kwenye majeraha hayo,, Zack akaanza kulia huku, haja ndogo ikimtoka ikiambatana na vijampo vya mfululizo,,
punde si punde majirani wakafika,, ni baada ya kelele za Shamy kusikika vyema upande wa nje ya nyumba,, wasiwasi ukazidi kuongezeka Zack akatamani kukimbia lakini tayari alikuwa ameshachelewa..
mmoja kati ya majirani hao waliokuja humo ndani,, alikuwepo afisa wa jeshi la polisi.. akaamua kumuweka Zack chini ya ulinzi.. kisha akapiga simu polisi akaamuru maaskari wawili waje akatoa anuani ya nyumba pamoja na mtaa..
baada ya dakika kadhaa maaskari wakawa wamefika wakamchukua Zack na kumpeleka kwenye kituo cha polisi Chang’ombe.
Shamy akakimbizwa haraka hospitali ya Muhimbili,,, manesi na madaktari walisikitishwa sana na hali aliyokuwanayo Shamy,, uso wake ulionekana kuvimba na majeraha ya mipasuko mikubwa… mbaya zaidi Shamy ni daktari tegemezi katika hospitali hiyo.. hivyo alipatiwa huduma ya kwanza kwa uangalifu wa hali ya juu!! Jopo la madaktari bingwa walihakikisha wanafanya jitihada za kuokoa maisha ya Shamy!
Taarifa hizo zikamfikia daktari mkuu wa hospitali hiyo ambaye ni Shirima.. akafanya hima kuwahi hospitali,, akakuta Shamy kawekwa katika chumba maalumu cha msaada wa pumzi,, (I. C. U) Shamy hakuweza kuvuta na kutoa pumzi yeye mwenyewe hivyo akalazimika kuwekewa mipira maalu ya kusukuma hewa safi na kutoa hewa chafu,,mwilini(Oxigen machine)
Shirima akauliza kapatwa na nini? nesi akasema ,,”bado hatujapata taarifa kamili,lakini kaletwa na mtu huenda akawa ndugu yake,, Shirima akasema yuko wapi mtu huyo! nahitaji kuonana nae sasa hivi.
nesi akaongozana na Shirima mpaka ke mapokezi,, wakamkuta mmoja kati ya wale majirani waliotoa msaada kwa Shamy,, Shirima akauliza,, “kapatwa na nini?
jirani huyo akasema,, “kapigwa na mume wake..
Shirima akakasirika sana,, akajisemea moyoni,,”hii ndio? nafasi pekee ya kumiliki Shamy,, nitahakikisha mtu huyo anafungwa miaka isiyopungua kumi,, kwanza huyu ndiye alikuwa anamchanganya Shamy mpaka asinipende mimi! sasa kaingia kwenye kumi na nane (18)zangu! ataisoma namba ya kirumi,,
Shirima akaandaa mpango kabambe,, ili Zack afungwe zaidi ya miaka kumi gerezani.. wazo likamjia akakumbuka kuwa anaye rafiki ni kamishna wa jeshi la polisi.. hivyo aongee nae wambambikie kesi nyingine ikiambatana na kosa la kujaribu kuuwa kwa kukusudia…
Baada ya kumaliza kuongea na kamishna wa jeshi la Polisi, Shirima akarudi ndani ya chumba maalumu cha msaada wa kusukuma hewa safi ndani ya mwili na kutoa hewa chafu mwilini(I.C.U) shirima alisikitika sana kumuona Shamy yupo kafika hali hiyo.
Kesho yake,, kamishna akaandaa mpango wa kesi nzito ambayo haimuhusu Zack!
wakati huo Zack aliwekwa maabusu,, pasipo mdhamana!
Siku zilizidi kusonga hatimae kesi ya Zack ikawadia,, akapandishwa kizimbani kusomewa mashtaka,,,
akaonekana wakili mmoja aliyeandaliwa kwaajili ya kusema uwongo,,, hivyo kutokana na kazi yake ya kusimamia kesi mbalimbali,,aliaminika mbele ya mahakama hiyo,
Hakimu akaanza kusoma mashtaka yanayomkabili Zack,,
wakati huo Zack alikuwa kimya huku macho yamemtoka,, hakuamini alichokuwa anakisikia kutoka kwenye kinywa cha Hakimu! alistaajabu sana makosa yote yaliyosomwa akihusishwanayo,, hakuna hata moja alilolitenda,,
akasimama wakili na kuanza kutoa ushahidi wa mashtaka yanayomkabili Zack,, wakili huyo akasema,, “Mnamo mwaka 2015 ndugu Zack alifanya tukio la ujambazi akishirikiana na wenzake,, wakavamia nyumbani kwa Daktari mkuu wa Muhimbi aitwae Shirima,,, wakapora madini ya dhahabu ambayo ni mali ya Shirima,, na baada ya kufanya tukio hilo la kuvamia na kupora kwa kutumia siraha za moto, wakatoweka eneo la tukio na kutokomea kusikojulikana!
Wakili huyo,,baada ya kuongea uwongo uliotukuka,, akazipiga hatua kumsogelea Zack akauliza je unaweza kujitetea mbele ya mahakama?
Zack alibaki kimya pasipokuongea neno lolote,,huku macho yamemtoka kama mjusi kabanwa na mlango!
kwa mbali alionekana Shirima akiwa kaketi akisikiliza kesi inavyokwenda,, uso wa Shirima ulionekana kujawa na tabasamu,,, akajisemea moyoni,, “tuvijana twingene tuving’ang’anizi,, sasa ngoja tuone jeuri yake iko wapi,, nani zaidi kati yangu mimi na yeye,,,
Wakili akasema,, “siku kadhaa zilizopita ulijaribu kumuuwa mwanamke kwa kukusudia,, pia naomba uithibitishie mahakama,, kama huyo mwanamke ni mke wako halali wa ndoa,, onyesha cheti cha ndoa,
Sehemu Ya 4
Zack akazidi kuchanganyikiwa,, akasema,, “huyo ni mke wangu lakini bado hatujafunga ndoa kuhalalisha,
wakili akadakia na kumuuliza Zack,, “je? wazazi au walezi wa mwanamke huyo wanajua kuwa wewe unaishi na binti yao?
Zack akasema hapana!
wakili akatabasamu kisha akasema,, “ni kosa la jinai kuishi na mwanamke au kumfanya mkeo pasipo wazazi au walezi wake kujua,,, je? kipindi unampiga alafu akufa,,ungewaeleza nini wazazi au walezi wake!?
wakili huyo akazipiga hatua na kumtazama Hakimu, kisha akasema, Mh:Hakimu nimemaliza maswali, naomba mshtakiwa ajibu maswali,
Hakimu akabaki mdomo wazi!! kwa sababu faili la kesi ya Zack limeandikwa tofauti na ushahidi alioutoa wakili!
Hakimu akaamua kuhairisha kesi na kuirusha tarehe, kesi hiyo isikilizwe siku nyingine!
kiwha akasema,, anahitajika mtendewa aje hapa mahakamani siku hiyo kutoa ushahidi wake! kwa sababu bado yupo hai, hivyo ataeleza mbele ya mahakama kilichotokea,,
Shirima akakasirika sana,, akajisemea moyoni,, mambo yameanza kuwa magumu,, endapo Shamy akija kutoa ushahidi,, atamtetea huyu, kwa sababu Shamy anampenda sana huyu bwege..
Zack akarudishwa maabusu,, kusubiri siku ya kesi yake kusomwa tena.
*****************************************
Siku zilizidi kusonga,, hatimae Shamy akapata nafuu,, akaruhusiwa arudi nyumbani..
siku hiyo Shirima alimchukua Shamy akampeleka nyumbani,, walipofika,, Shirima akasema,, “nimemfungulia kesi yupo maabusu,, huyu kijana si mwema kwako angekuuwa,, ebu fikiria je? asingekuja mtu hata mmoja kutoa msaada,, ingekuwaje?
Maneno hayo ya Shirima yakaanza kumuingia Shamy,, akajikuta anaanza kumchukia Zack,, Shirima akasema,, “siku ya kesi itabidi useme kuwa alitaka kukuchoma kisu,, na huwa anakutishia mara kwa mara kukuuwa!
Shamy akasema,, “sawa hakuna shida,, hata hivyo kweli angeniuwa kama majirani wasingekuja kutoa msaada,, nimeanza kuamini maneno yako Zack si mtu mwema kwangu!
siku zilizidi kusonga,, hatimae tarehe ya kusomwa kesi ya Zack ikawadia…
Shirima na Shamy wakaongozana mpaka mahakamani!
Zack akapandishwa Kizimbani,, na kuanza kusomewa mashtaka,,, kisha akaitwa muhusikia aliyefanyiwa tukio ambaye ni Shamy mwenyewe….
Shamy akapanda kizimbani kutoa ushahidi…
Baada ya Shamy kupandishwa kizimbani akamtazama Zack kwa macho ya huruma.
Shamy akasema ni kweli alinipiga nahisi ni kwa sababu ya hasira tu yule wakili muongo akadakia na kusema, “mheshimiwa hakimu mwanamke huyu atakuwa kaingiwa na uwoga baada ya kunusurika kuuawa hivyo anashindwa kunyosha maelezo.mimi kama wakili wa upande wake nitasimama badala yake, “Siku chache zilizopita mshitakiwa alimpiga mwanamke huyu pamoja na kumtishia kumuua pili, mshitakiwa huyu huyu miaka kadhaa iliyopita alifanya tukio la ujambazi akiwa na wenzake kwa kupola dhahabu ambazo ni mali ya Shirima. Hakimu akauliza mbona sijawahi kuona jalada la kesi hiyo hapa mahakamani? yule wakili aliyelipwa na Shirima ili atoe ushahidi wa uongo akasema, “ielelezo na ushahidi upo.Baada ya wakili huyo kusema hayo yote Shamy alishtuka dhamira yake ikamsuta.
Shamy akasema, “Mheshimiwa hakimu kiukweli zack nimeishi nae miaka mingi na tangu nimjue sijawahi kumuona akijihusisha na vitendo vya ujambazi na pia hana tabia hiyo. Hakimu akashtuka akajisemea moyoni, “bila shaka hapa kuna namna na kuna siri nzito inayoendelea inaonyesha wazi kuwa kijana huyu amasingiziwa.
Hakimu akasema, “mshitakiwa anaonekana hana makosa kesi hiyo ya ujambazi haina vielelezo vyenye ushahidi kuwa mshitakiwa anahusika kutokana na sheria inavyosema mshitakiwa akalipa fidia ya kumpiga na kumjeruhi mwanamke huyu,kisha ataachiwa huru. shirima alikasirika kupita kiasi akaona mpango wake umegonga mwamba…
Baada ya siku tatu zack akamlipa Shamy fidia,,, mbele ya mahakama… Zack akaamua kuondoka nyumbani kwa Shamy na kutafuta chumba cha kupanga..
Shamy akaanza kupata wakati mgumu,, kwa sababu alikuwa anampenda sana Zack,, akaamua kumtafuta na kumuomba msamaha,, Zack pia hakuwa na namna kwa sababu alikuwa anampenda sana Shamy, akaamua kurudi kwa shamy,, na maisha yakaendelea.
Siku zilizidi kusonga,, Shamy akaanza kuwa anamkwepa Shirima,, akaamua kubadilisha namba ya simu,,, hata akiwa kazini akawa hakai ofisini mara kwa mara akawa anazungukia wodi za wagonjwa ili Shirima asipate muda wa kuongea nae!
kitendo hicho kilimfanya Shirima azidi kumchukia Zack! akaamua akaamua kufanya mpango wa kumuangamiza Zack..
Siku moja Zack alikwenda kazini kwa Shamy,, ni baada ya Shamy kumuiga Zack kwa lengo la kumpa bahasha fulani iliyokuwa na nyaraka ndani yake,, nyaraka hiyo ilitakiwa ipelekwe almashauri..
Zack alipofika akaliegesha gari lake akimsubiri, Shamy alete bahasha hiyo,,, punde si punde, likaonekana gari likiingia na kuegeshwa,, kisha akashuka Shirima,,, wakati anashuka kunapicha zikadondoka amba, o Shirima hakuziona,, akazipiga hatua kulifuata jengo la hospitali,,
Zack alimuona Shirima pia aliona Shirima kadondosha picha mbili! Zack akaamua kuzipiga hatua lulifuata gari la Shirima pale lilipokuwa limeegeshwa,,, akaziokota picha hizo mbili,,alipozitazama,, akashtuka sana,, macho yakamtoka baada ya kuona picha hizo! ni picha za mama yake,, picha moja ilikuwa ya mama yake akiwa peke yake,, na ile nyingine,alionekana mama yake,, pamoja na Shirima! picha hiyo ilionekana ya kizamani,,,
Zack akahisi kuchanganyikiwa akajisemea moyoni,, “kwani mtu huyu ni nani? mbona kapiga picha na marehemu mama yangu!!!?
Zack akazichukua picha hizo akaziweka mfukoni mwake,kisha akazipiga hatua kurudi ndani ya gari lake,,
baada ya dakika kadhaa kupita alionekana Shamy,, akitokea ndani ya jengo la hospitali akielekea sehemu ya kuegesha magari,,, akaliona gari la Zack,, akalifuata na kumkabidhi ile bahasha. kisha Zack Ada ndoka zake..
Siku zilizidi kusonga hatimae,, Shirima akaamua aende kwa mganga ili amuangamize, Zack….
Shirima akaenda kwa mganga,, ni yule mganga Manyenye….. alipofika akaeleza shida yake,, Manyenye akasema,, “chukua hiki kisu,, andika hapo chini jina lako kamili,,pamoja na ubini wako.. kisha andika jina la huyo adui yako.
Shirima akafanya kama alivyoagizwa na mganga Manyenye…alipomaliza,, akaonekana Manyenye akinyanyuka na kunyunyizia dawa kwenye majina ya Shirima pamoja na ubini wake,, kisha akanyunyizia dawa kwenye jina la adui wa Shirima ambaye ni Zack.
Manyenye akashtuka na kusema! mbona umefikia maamuzi magumu kiasi hiki?? ni kweli umekusudia kufanya jambo hili? Shirima akasema,, “ndio nimekusudia, haka kakijana kashenzi sana kanasababisha mimi nisipendwe na mwanamke ninayempenda.. kwa sababu ni wapenzi,, na wanampango wa kuoana…
Manyenye akasema,, “inamaana unataka kumchukuwa mchumba wa mwanao?
Macho yakamtoka Shirima akauliza kwa mshangao,, “mwanangu kivipi?
Manyenye akasema,, “hilo jina la adui yako uliloliandika hapo chini,,, linaonyesha linashahabiana na uzawa wa damu yako.. ndio maana nikakuuliza kuwa umekusudia kufanya jambo hili!!!!”
Shirima akasema,, “akasema ndio nimekusudia…
Manyenye akamtazama Shirima kwa macho ya mshangao, kisha akasema,, “simama kisha sogelea hiyo meza,, Shirima akafanya kama alivyoagizwa na mganga Manyenye.
alipoikaribia meza hiyo,, likajitokeza boga la kimiujiza! pale juu ya meza. shirima akaingiwa na hofu,, tangu azaliwe hajawahi kuona muujiza wa namna hiyo…
Mganga Manyenye akasema,, “chukua hicho kosu kilichopo kando ya boga hilo kisha dunga kwa kuvu boga hilo kwa kutumia hicho kisu… baada ya kufanya hivyo tayari utakuwa umemuuwa adui yako!
Shirima akanyanyua kisu hicho huku mapigo yake ya moyo yakipiga kwa kasi ya ajabu! jasho lilimtoka Shirima huku mwili wake ukitetemeka!
kabla hajanyanyua kisu hicho,, ukasikika mngurumo mkubwa kupita kiasi,, mngurumo huo uliambatana na upepo mkali uliovuma kwa kasi.. Mganga Manyenye akaanza kuhisi harufu ya hatari,, pia Shirima akaogopa akakitupa kile kisu chini…
Manyenye akachukua kibuyu kimoja chenye rangi nyekundu,,akamkabdhi Shirima kisha akasema,, shikilia kibuyu hicho ni kinga ya kukulinda wewe,,, muda si mrefu kunavita kali itatokea hapa,, bila kufanya hivyo hauwezi kutoka ndani ya nyumba hii ukiwa hai, Shirima hakutaka haga kugusa kibuyu hicho akatimua mbio akatoka ndani ya nyumba hiyo iliyoezekwa kwa nyasi kavu,, yenye vyumba mia moja(100) ndani yake.. lakini ukiitazama upande wa nje inaonekana ni ndogo kupita kiasi…akatimua mbio hakutaka kabisa kushuhudia vita aliyoambiwa kuwa itatokea muda mchache ujao… kumbe mganga Manyenye aliwahi kumuuwa mtu,, kichawi! mtu huyo alikuwa katolea kwenye ukoo wenye mizimu mikali,,hivyo mizimu hiyo ilikuja kulipiza kisasi kwa kumuangamiza mganga Manyenye,, ukawa ndio mwisho wa mganga huyo.
hivyo ikawa pona pona ya uhai wa Zack,, inamaana Shirima angekidunga kisu kile kwenye lile boga basi Zack angekufa sekunde hiyohiyo..
Shirima alionekana akitimua mbio na kuingia ndani ya gari lake akaliondoa kwa mwendo wa kasi ya ajabu,, akatoka kabisa eneo hilo,, akaelekea nyumbani kwake.
alipofika aka akaliegesha gari lake kisha akaingia ndani ya nyumba yake… akapitiliza moja kwa moja chumbani kwake,, akajilaza kitandani…
baada ya sekunde kadhaa akanyanyuka na kulifungua lile begi lake dogo analoweka vitu vyake vya muhimu… akatoa picha nyingi za mama Zack,, akaanza kuzitazama…..
*************************************
Wakati huo huo alionekana Zack akiingia ndani ya nyumba anayoishi yeye na mchumba wake Shamy! akaketi kitandani huku akiwa na mawazo mazito… alijiuliza maswali mengi pasipo kupata majibu,,, akanyanyuka na kuzichukua zile picha alizoziokota kando ya gari la Shirima,, akazitazama picha hizo kwa dakika nyingi sana..
punde si punde ukasikika mngurumo wa gari likiegeshwa nje ya nyumba,, kumbe ni Shamy ndiye aliyeliegesha gari hilo, akashuka na kuzipiga hatua kuufuata mlango wa kuingilia ndani ya nyumba. akapitiliza na kuingia chumbani.. akamkuta Zack akiwa kashikilia picha mbili,,, Shamy akamsogelea Zack kisha akamsalimia,, “habari yako kipenzi changu.
Zack hakujibu salamu ya Shamy! alibaki kimya,,, hata kipindi Shamy anaingia chumbani Zack hakumuona kutokana na mqwazo mazito kuhusu hizo picha alizokuwa akizitazama!
Shamy akachukua picha moja kutoka mikononi mwa Zack.. alipoitazama akashtuka,, akasema picha ya Shirima umeipata wapi?
Zack hakujibu kitu chochote!!. Shamy akauliza tena,, “nakuiza mpenzi!
Zack akashtuka kutoka kwenye dimbwi la mawazo akastaajabu kumuona Shamy! kisha akamuuliza,, “umefika hapa muda gani?
Shamy hakujibu swali la Zack.
Shamy akasema,, “nimekuuliza hii picha ya Shirima umeitoa wapi?
Zack akasema nimeziokota kule kwenye hospitali unayofanyia kazi,, kando ya gari la Shirima,, wakati anashuka kutoka ndani ya gari picha hizi zilidondoka.. nikaziokota.. lakini cha kushangaza nilipozitazama,, nikamuona marehemu mama yangu kwenye picha hizo!
Shamy akashtuka,, akakumbuka,, kuwa kuna siku Shirima alimwambia kuwa,, alizaa na mke wa bosi wake!
bosi wake alipogundua kuwa ameshirikiana kimwili na mkewe,, ndipo Shirima akahama mji ili kulinda usalama wa uhai wake!
pia alisema hakuwahi kumuona mtoto huyo,, wala hajui mama wa mtoto huyo kama yupo hai au kafa!
Shamy akahisi kuchanganyikiwa,, akasema,, “inamaana wewe ni mtoto wa Shirima!!!?
Zack akashtuka kusikia hivyo akauliza,, “kwa nini umesema hivyo?
ndipo Shamy akaanza kusimulia kile alichokisema Shirima,,
Shamy aliendelea kusimulia kisha akauliza,, “huyu mwanamke kwenye picha ni mama yako?
Zack akajibu,,”ndiyo ni mama yangu!
Shamy akasema,, “shirima ni baab yako wa damu… inamaana yule baba yako uliyeniambia alimtelekeza mama yako kipindi anamimba changa.. ndiyo huyu Shirima?
Zack akajibu hapana sio huyu,, yani hapa nahisi kuchanganyikia nashindwa kufahamu ukweli ni upi? naomba mimi na wewe tuongozane unipeleke nyumbani kwa Shirima nikajaribu kumdadisi ili nijue ukweli, baba yangu wa damu ni yupi?
Shamy akasikitika sana akamtazama Zack kwa macho ya huruma! kisha akasema,, “sawa hakuna shaka,, twende sasahivi…
bila kuchelewa,, wakaondoka muda huo huo,,na safari ya kuelekea nyumbani kwa Shirima ikaanza.
****************************************
Wakati huo huo kule nyumbani kwa Shirima,,alionekana bado akiwa amejilaza kitandani huku,, akitafakari nini cha kufanya,, ghafla akakumbuka maneno ya mganga Manyenye,, alimwambia kuwa adui yake ambaye anataka kumuangamiza kwa kuondoa uhai wake.. ni uzawa wa damu yake!! wazo likamjia akashtuka,,macho yakamtoka,, akaongea kwa sauti ya chini chini,, “mbona sielewi? yawezekana mtoto wangu ninayemtafuta miaka yote hiyo, ndio huyo Zack.
mbona hii ni kasheshe!!! Shirima akaanza kujihisi kushindwa kupata hewa kutokana na mshtuko wa moyo! akizipiga hatua za haraka akaelekea sebuleni!! hali yake ikazidi kuwa mbaya zaidi akahisi kuishiwa nguvu,,akajitahidi kuufuata mlango ili atoke nje ya nyumba angalau apate hewa,, alipoukaribia mlango akadondoka chini akatulia tuli.
Sehemu Ya 5
Shirima akapoteza fahamu,,, pasipo kupata msaada wowote….
baada ya dakika kadhaa Shamy na Zack wakafika nyumbani kwa Shirima… wakaliegesha gari ,,wakazipiga hatua kuufuata mlango wa nyumba ya Shirima… Zack akagonga mlango,, lakini mlango haukufunguliwa! akasema,, “au katoka?
Shamy akafungua mkoba wake akatoa simu,, na kumpigia Shirima,,,
simu iliita bila kupokelewa,, Zack akasema mbona nasikia mlio wa simu ikiita ndani ya nyumba hii au atakuwa amelala?
Shamy akazungusha kitasa cha mlango ukafunguka akashtuka kumuona Shirima kalala kwenye sakafu! akaingia ndani haraka,,pia Zack naye akaingia,,
Shamy alipomtazama Shirima akagundua kuwa Shirima,, amepoteza fahamu,, akampa huduma ya kwanza kwa kumpepea mfululizo.. punde si punde Shirima akazinduka,, na kupata fahamu!! akastaajabu kumuona Shamy! alipogeuza shingo yake akamuona Zack!
Shirima akanyanyuka pale chini akazipiga hatua kulifuata jokofu,, akafungua na kutoa chupa ya maji,, akaanza kunywa,, kisha akaketi kwenye sofa,,
Zack na Shamy nao wakaketi kwenye moja ya masofa yaliyokuwemo ndani ya sebule ya nyumba ya Shirima!
wakasalimiana,, kisha Zack akatoa picha ya mama yake na kuzipiga hatua kumsogelea Shirima,, akasema,, “unamfahamu huyu? Zack aliongea huku akimkabidhi Shirima ile picha! Shirima akaipokea,,alipoitazama akasema ndio namfahamu,, huyu ni mzazi mwenzangu,, na sijui yuko wapi?
Macho yakamtoka Zack! akajisemea moyoni,, “mama yangu hakuwahi kuwa na mtoto mwingine zaidi yangu… inamaana huyu ndiye baba yangu? mbona hii ni kama sinema! sasa yule aliyenitambulisha mama kabla hajafariki kuwa ndiye baba yangu,, aghhh!!!
wakati Zack anajiuliza maswali hayo,, Shamy na Shirima walikuwa wakimtazama Zack,,alionekana yumo ndani ya dimbwi zito la mawazo pia yupo mbali kifikra!
Zack akauliza,, “unamaanisha wewe ni baba yangu? kwa sababu mama yangu hakuwahi kuzaa mtoto mwingine zaidi yangu..
Shirima akakohoa kwa sekumde kadhaa kisha akasema,, ” mnamo miaka 29 au 30 iliyopita niliwahi kuwa na mahusiano na Bi’Eliza Mushi..
Zack akazidi kuchanganyikiwa baada ya kumsikia Shirima kataja Jina kamili la mama yake pamoja na Ubini!
Shirima akaendelea kusimulia,, “Bi’Eliza alikuwa ni mke wa bosi wangu aitwae RICH.
richi alikuwa ni daktari mkuu wa hospitali ya Rufa Bugando huko Mwanza… haikuwa dhamira yangu mi; i kushirikiana kimwili na mke wa bosi wangu,, lakini Bi’Eliza alinilazimisha pia akanitishia kuwa endapo nitakataa kumtimizia haja yake.. atasema maneno ya uwongo kwa bosi wangu ambaye ni mumewe ili anifukuze kazi,,, kiukweli nilisikitika sana nikiangalia mimi ndiye tegemezi la kumlea mama yangu ambaye kwa kipindi hicho alikuwa mgonjwa sana.. pia mimi nilikuwa mtoto wake wa pekee… na hakuna ndugu wa kutupa msaada..
nilitafakari kwa kina,, nikaamua kukubali ili niendelee kufanya kazi nipate pesa ya kumuhudumia mama yangu..
siku moja Bosi Rich alisafiri kikazi.. mke wa Rich akaniita nyumbani kwake.. nilipofika akanishawishi nishirikiane nae kimwili,, nikajikuta nashindwa kuwa mvumilivu.. akaniongoza mpaka chumbani anapolala yeyw na mumewe… kumbe Rich alitegesha kamera ndani ya chumba chake pamoja na maeneo yanayoizunguka nyumba yake!!
mimi na Bi’Eliza hatukuweza kutambua kuwa kumakamera zinaturekodi…
siku zilizidi kusonga,,na baada ya wiki mbili kupita,, Bi’Eliza akaniambia kuwa anaujauzito wangu, niliogopa sana kwa sababu nilijua hii ni hatari endapo Rich atagundua!! wiki moja baadae hatimae bosi Rich akarejea nyumbani kwake…akagundua kuwa mkewe kamsaliti tena kwa kulazimisha yeye mwenyewe.. aliona tukio zima lililorekodiwa na kamera(UCCTV) akachukia kupita kiasi akamfukuza mkewe…
mimi nikaogopa kuendelea kuishi Mwanza nikaamua kuhama mimi na mama yangu nikakimbili huku dar es salaam! tangu miaka ya 80…kwa sababu nilikuwa nimesomea mambo ya uuguzi.. nikaamua kujiendeleza kielimu zaidi.. nikapata stashahada ya udaktari… serikari ikanipa mkopo wa kujiendeleza zaidi.. hatimae nikamaliza masomo yangu nikawa daktari maalumu! ndipo nikaajiliwa hospitali ya Muhimbili kama daktari mkuu… kiukweli sikuwahi kumuona tena Bi’Eliza na sijui alijifungua mtoto wa jinsia gani! kumbe wewe ni mwanangu! eee Mungu asante kwa kunikutanisha na mtoto wangu kwa namna hii! pia samahani sana Shamy! haya yote yametokea kwa sababu sikujua,, kuwa wewe ni mchumba wa mwanangu… Shamy akatabasamu pasipokuongea neno lolote!
Zack akabaki mdomo wazi huku akimtazama Shirima!,, akanyanyuka na kumkumbatia baba yake.
Siku zilizidi kusonga,,Zack akawa na furaha kumjua baba yake mzazi,, pia Shamy akafurahi mkuu wake wa kazi ni baba mkwe wake.
maisha yalikuwa mazuri kupita kiasi… waliishi kwa amani siku zote!
Siku moja Zack akaongea na baba yake(shirima) kuwa ni vyema waende kupeleka barua ya Posa nyumbani kwao Shamy,, ili ndoa ifungwe.. Shirima hakuwa na kipingamizi.. mipango na taratibu zikafanyika na safari ya kwenda mwanza nyumbani kwao Shamy ikawadia!
Shirima akalazimika kuongozana na Zack pamoja na Shamy kwenda nyumbani kwao Shamy,,huko Mwanza… Shirima akalipia usafiri wa ndege,, akapatiwa tiketi tatu….
Shamy akawajulisha wazazi wake kuwa anakuja huko nyumbani kumleta mchumba wake amtambulishe kwao!
wazazi wa shamy wakafurahi sana,, wakafanya maandalizi kwaajili ya wageni hao.
Shamy Zack pamoja na Shirima wakaelekea uwanja wa ndege(Air poart) tayari kwa safari.,,,,,
baada yaasaa kadhaa wakawa wamefika mwanza,,, wakakodi taxii kutoka kwenye kiwanja cha ndege Mwanza mpaka Nyakato nyumbani kwao Shamy….. walipofika wakapokelewa,,, Mama Shamy akafurahi sana kumuona mwanae pia akafurahi kumuona mchumba wa Shamy pamoja na baba wa mchumba wa Shamy..
wakati huo Baba Shamy hakuwepo nyumbani… alikuwa katika shughuri zake.
Chakula pamoja na madikodiko yakaandaliwa… tayari kwa chakula cha mchana.
walipomaliza kula,Shamy akaandaa Sehemu ya kulala wageni wake…
ilipofika majira ya saa mbili za usiku……Shirima akaenda kupumzika katika moja ya chumba cha wageni katika nyumba yao Shamy!
Akabaki Shamy Zack pamoja na Mama Shamy wakiwa sebuleninwakitazama taarifa ya habari….. Shamy akasema,, “mama wacha sisis tukapumzike,, naona leo baba kachelewa kurudi,,, hivyo wageni wangubwataongea nae kesho Mungubakipenda,
Maam Shamy hakuwa na kipingamizi,, akasema,, “hakuna tatizo mwnangu..
Shamy akamuongoza Zack mpaka chumbani… wakapumzika…
ilipofika saa nne za usiku Baba Shamy akarejea nyumbani… lakini akakuta wageni tayari wamelala vyumbani….
**************************************
Asubuhi palipokucha Baab Shamy alidamka mapema kama kawaida yake.. akajiandaa kuelekea kwenye shughuri zake…. kabla hajatoka akamwambia mkewe,, “wacha mimi niwahi kusimamia miradi yangu,,lakini nitawahi kirudi japo nisalimiane na wageni..
Mama Shamy hakuwa na kipingamizi,, Baba Shamy akatoka nje ya nyumba akaingia ndani ya gari,,, na kuondoka zake.
Whamy akadamka akaandaa Chai kwa ajilibya wageni wake…
kisha akawakaribisha katika meza ya chakula…
Bnaada ya masaa sita lupita Baba Shamy alirejea nyumbani… alipoingia sebuleni akastaajabu kumuona adui yake yumo mdani ya nyumba yake! ambaye ni Shirima
Baba Shamy akapigwa na butwaa… lakini akawa mvumilivu,,, wakati huo Shirima macho yalimtoka hakuamini anachoshuhudia mbele ya macho yake!
Baba Shamy akaketi kwenye Sofa….punde si punde Shamy akaja sebuleni akitokea chumbani….. akamsalimia baba yake na kumkumbatia kwa upendo.
kisha Shamy akaanza kutoa utambulisho kwa baba yake.
akasema,, “baba hawa ndio wageni wangu.. huyu anaitwa Zack ni mchumba wangu.
na huyu anaitwa Shirima ni baba mzazi wa Zack… nimechukua jukumu jili kuwaleta nyumnani kwa lengo la kufahamiana pande zote mbili.
Macho yakamtoka baba shamy.. akabaki mdomo wazi! wakati hio Shirima alikuwa akimtazama bana Shamy kwa macho ya aibu,, huku akijisemea moyoni,, “hii ni fedheha laiti kama ningejua nakuja kwenye nyumna ya huyu mzee nisinge thubutu lakini hakuna namna,, hayo yalishatokea na yamepita,, lakini sijui atachukua maamuzi gani juu ya jambo hili!
Shamy aliendelea kutoa utambulisho kisha akaketi kando ya baba yake..
Maam Shamy akasema, kwa ulande wangu mimi sina kipingamizi…. kwa sababu wao wamependana na wameamua kulifikisha swala hili kwa wazazi mimi sioni tatizo lolote.. labda baba Shamy,, unalo la kuongea??
Baba Shamy akabaki kimya huku kainamisha uso wake chini….. ajambo hilo lilimfanya Shamy akose furaha ghafla,, akahisi huenda baba yake akakataa ndoa isifungwe!
pia watu wote wakastaajabu!
Baba Shamy akanyanyuka pasipokuongea neno lolote akazipiga hatua kuelekea chumbani….Shamy na Zack wakatazamana!
utu uzima dawa, Shirima akahisi jambo baya litatolea muda mchache ujao.. akaketi kwa taadhari huku mkono wake mmoja kauegesha kiunoni… kumbe Shirima alikuwa na bastola….
punde si punde Bana Shamy akaonekana akitokea chumbani huku kaweka mikono yake nyuma… alipofika sebuleni akachomoa bastola akamnyooshea Shirima,, wakati huohuo pia Shirima akachomoa bastora kumnyooshe Baba Shamy!
Watu wote waliokuwepo pale sebuleni wakapigwa na butwaa!!! wakabaki wanajiuliza maswali yasiyokuwa na majibu… punde si punde ukasikika mlio wa risasi!!!!
Baba Shamy akaamua kupiga risasi juu ya dari.. kutokana na hasira alizo kuwanazo.. kisha akaitupa bastola juu ya sofa.. akaketi kando, akasema,, “hivi wewe shirima unatafuta nini katika maisha yangu? wewe uliharibu ndoa yangu miaka ya 80,,kwa kushirikiana kimwili na mke wangu wa kwanza,,ukaona haitoshi ukaamua kumpa ujauzito,, mshukuru mungu wako ulikimbia,, bila hivyo ningeondoa uhai wako kwa mikono yangu mwenyewe… haya leo umekuja kuivuruga tena familia yangu… hivi wewe unahitaji roho yangu ndio uridhike?
Shirima akahisi fedheha,, akamtazama Baba Shamy kwa macho ya aibu…kisha akasema,, “haikuwa kusudio langu,,, Mungu pekee ndiye shahidi wa hilo… mkeo alinilazimisha nifanye hivyo… akanitishia kuwa nisipomtimizia haja yake atasema uwongo kuwa mimi namtaka kimapenzi… ili wewe unifukuze kazi…. na kwa kipindi hicho mama yangu alikuwa mgonjwa sana,, anahitaji matunzo pamoja na mahitaji kama dawa na chakula,,niliamua kukubali ombi la mkeo kwa sababu moja tu… niendelee kufanya kazi nipate fedha za kumtunza mama yangu… lakini haikuwa kusudio langu… pia ilikuwa ni siku moja tu… na kwa mipango ya Mungu,, mkeo akapata ujauzito!! na mtoto mwenyewe ni huyu Zack… samahani sana,,naomba haya mambo yaishe… kwa sababu tayari wewe unafamilia nyingine.
Shamy akashtuka akahisi kuchanganyikiwa,,, macho yakamtoka!
Pia Zack akabaki mdomo wazi!
Mama Shamy akasema,, “kwa upande wangu mimi sioni kama kunatatizo… huwezi jua kusudio la Mungu,,punguza hasira Baba Shamy!
Baba Shamy akamtazama mkewe,,, kisha akashusha pumzi; akasema,, “kiukweli Shirima wewe sijui nikuweke katika historia ipi ya maisha yangu…. umekuwa gumzo kwenye ubongo wangu… SITOSAHAU KAMWE..
Shamy akazipiga hatua za taratibu akamsogelea baba yake,, akapiga magoti kisha akasema,, “tafadhali baba yangu kipenzi naomba umsamehe,, ameshakwambia ukweli.
pia nampenda sana Zack,,yeye ndiye mwanaume wa maisha yangu… naomba baraka zako baba yangu… Shamy aliongea maneno hayo huku machozi yakimtoka.
maneno ya Shamy yalimfanya baba yake aingiwe na roho ya huruma,, akamkumbatia binti yake(Shamy) akasema,, “ondoa shaka mwanangu,, nawatakia kila la heri wewe na mchumba wako.
Shamy akafueahi sana..
baba Shamy akazipiga hatua akamsogelea Shirima akashikana mkono na Shieima ishara ya amani.
*****************************
baada ya siku nne kupita.. Shirima,, Zack pamoja na Shamy wakarudi dar..
mipango ya harusi ikafanyika na ndoa ikafungwa.
Maisha ya Shamy na Zack yakawa na amani na furaha,,,kutokana na furaha na amani aliyokuwanayo Shamy,.,utendaji wake wa kazi ukaongezeka hatimae akapata tuzo ya daktari bora katika sherehe za tuzo za hospitali hiyo… daktari mkuu(shirima)
akaamua kumpandisha cheo..na mshahara wa Shamy ukaongezwa kwa aslimia kumi ya mshahara wake aliokuwa analipwa mwanzo.
baada ya miezi mitano(5) kupita,,Shamy akapata ujauzito.
Zack akafurahi sana,, upendo ukazidi kuongezeka kila kukicha,,
baada ya miezi tisa (9) kupita Shamy akajifungua mtoto wa kike,, mtoto huyo alikuwa mrembo kama mama yake,,, hatimae Zack akawa na familia…. alihakikisha familia yake inakuwa na amani siku zote…. pia Shirima alifurahi sana kumpata mwanae wa pekee(Zack) pamoja na mjukuu wake…
Familia hiyo inaishi kwa amani na upendo mpaka leo.
***MWISHO***

