TAREHE 9 SEPTEMBER
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Sehemu Ya 1
Mnamo mwaka 2007,,alionekana binti mrembo kupita kiasi akitokea bafuni,, akazipiga hatua kuufuata mlango wa chumba chake,,,binti huyo anaitwa shamy! akaufungua mlango wa chumba chake akaingia ndani,, Shamy alikuwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu,,maarufu ka MLIMANI/UDSM….huu ulikuwa mwaka wake wa mwisho chuoni,,, akichukua shahada ya udaktari…
Shamy akajifuta matone ya maji yaliyokuwa mwilini mwake kisha akavaa gauni lililoshikilia mwili wake na kuonekana vyema uhalisia wa umbile lake lililokuwa linamvuto wa aina yake! wanaume wengi walimtaka Shamy kimapenzi,, lakini Shamy alikuwa na msimamo mmoja tu,,,,, akili na mawazo yake yaliwaza masomo,,,
Shamy alipomaliza kuchana nywele zake akachukua mkoba uliokuwa na madaftari pamoja na Laptop,, kisha akazipiga hatua kutoka nje ya chumba chake akaufunga mlango wa chumba chake,,, kisha akazipiga hatua kuelekea chuoni!
baada ya dakika kadhaa Shamy akafika chuoni akaingia darasani kwa ajili ya somo maalumu kwa siku ya leo!
baada ya masaa saba kupita, muda wa masomo ulikuwa umekwisha, Shamy akazipiga hatua kurudi kule anapoishi! akiwa njiani akakutana na kijana,,,kijana huyo alikuwa ni mtu wa kawaida sana! akamsimamisha Shamy!
Shani akaendelea kuzipiga hatua bila kugeuka! ingawa alisikia kuwa kunamtu amemuita,, Kijana huyo aitwae Zack, hakukata tamaa akaendelea kumuita shamy,, huku akimfuata kwa nyuma! Shamy aliposikia kijana huyo anamuita mfululizo akaamua kugeuza shingo yake kisha akasimama!
Zack akamsalimia Shamy,, ‘habari yako dada.
Shamy akajibu salamu kwa uchangamfu,, “Safi mambo vipi?
Zack akasema,, “kwanza nimefurahi san kuongea na wewe,, pili nilikuwa ninaombi,, je? naweza kupata namba zako za simu?
Shamy akasita akabaki kimya kwa sekunde kisha akasema,, “bila shaka.. lakini nipe sababu mbili je? kwa nini unataka namba yangu?
Zack akatabasamu kisha akaongea kwa kauli ya kujiamini!,, “nitakueleza jambo lakini
si vyema kuongea hapa barabarani! Shamy akasema ,,”hakuna tatizo lakini nakusihi usipige simu usiku huwa sipendelei kuongea na simu usiku!
Zack akatoa simu yake ndogo iliyoonekana kuchakaa kupita kiasi huku ikiwa imefungwa kwa rababendi!! maarufu kwa jina(KIMEO), Shami akaipokea simu hiyo kisha akaandika namba zake za simu na kuirudisha simu hiyo kwa Zack,, kisha akasema,, “kwaheri.
Zack akabaki anamtazama Shamy kwa macho ya matamanio.
Siku zilizidi kusonga,, Zack alihakikisha haipiti siku pasipokumjulia hali Shamy!
kutokana na bidii ya Zack kuwasiliana na Shamy mara kwa mara wakajikuta wamekuwa marafiki,,
Siku moja Zack alimpigia simu Shamy, siku hiyo ilikuwa ni jumamosi. Zack akasema,, naomba nije kukutembelea siku ya leo,, Shamy akasema,, “bila shaka unakaribishwa.. siku ya leo huwa sitoki nakuwepo tu nyumbani.. nikijisomea,, Shamy akatoa maelekezo jinsi ya kufika anapoishi, Zack akapafahau akasema,, “maeneo hayo huwa nakuja mara kwa mara.. kuna rafiki yangu anaishi maeneo hayo!
Baada ya lisaa limoja Zack alifika nyumbani kwa Shamy,, Shamy akamkaribisha…
Zack akaonekana kama anataka kuongea jambo lakini alikuwa anasita.. akaamua kubakinalo moyoni!
ilipofika saa moja za jioni Zack akaondoka na kurudi nyumbani kwake!
********************************************
Siku zilizidi kusonga,Zack akawa na ukaribu zaidi kwa Shamy,, akawa anampelekea zawadi,, Shamy akajikuta anaanza kumpenda Zack kwa sababu Zack alionyesha kumjali,, ingawa hana kipato,,,
Siku moja Zack akajikaza kiume,, akaamua kutoa dukuduku lake moyoni,, akamtamkia Shamy kuwa anampenda!
Shamy akawa hana jibu la kumjibu Zack….lakini vitendo vyake vilimfanya Zack apate matumaini ya kumiliki Shamy!
miezi ilizidi kusonga,,wakajikuta wamezama kwenye penzi zito!! watu wengi walimshangaa Shamy,, kwa nini kajiingiza kwenye mapenzi na mtu ambaye sio hadhi yake! kutokqna na hali duni ya maisha ya Zack,, alionekana kutokupendeza,,mavazi yake yalionekana kuwa ya kizamani(Old fasion)
lakini Shamy alionekana kuzama kwenye penzi la Zack kwa sababu Zack alikuwa anamjali,, na kumthamini,, pia alimpa ushauri mbalimbali, ambao ulimjenga Shamy!
Wanaume wengi waliokuwa na kilato walimsumbua sana Shamy kutokana na urembo aliokuwanao! Shamy alikuwa anauzuri wa asili,, hata asipopaka urembo usoni/kujirmba bado alionekana ni mrembo kuliko!
Siku moja Shamy akamwambia Zack ahame kule anapokaaa ahamie nyumbqni kwake,, Zack hakuwa na kipingamizi,, akakubali kuhamia nyumbani kwa Shamy!
******BAADA YA MWAKA MMOJA KUPITA*******
Shamy alimaliza masomo yake,,ya shahada akisubiri ajira! maisha ya Shamy yalikuwa mazuri kwa sababu alipewe kila kitu alichokihitaji kutoka kwa wazazi wake..
Siku moja Zack akamsimulia Shamy historia ya maisha yake,, akasema,, “baba yangu alimtelekeza mama yangu akiwa na mimba changa…
maam alipojifungua akanilea yeye pekee… ingawa alinionyesha baba yangu.. lakini bado baba yangu hakuonyesha upendo kwangu! nilipoanza elimu ya sekondari.. nikiwa katika kilindi cha mitiahani,, maam yangu alifariki,, nikalelewa na mama yangu mdogo,,, lakini kwa sasa ni mlemavu,, kapooza upande mmoja… pamoja na hayo nawatambua baadhi ya ndugu zangu upande wa baba! kuna shangazi yangu mmoja hapatani kabisa na baba baada ya kumwambia kuwa hajafanya jambo jema kumtelekeza mwanamke akiwa na mimba,, mama yangu alikuwa na urafiki wa karibu na mdogo wake baba ambaye ni shangazi yangu…. mara nyingi huwa nakwenda kumtembelea anaishi KIGAMBONI.
Shamy akamtazama Zack kwa macho ya huruma, kisha akasema,, “usijali mpenzi Mungu atasimama na wewe mja weke! mimi pia nipo pamoja na wewe,, nimekupenda na nitaendelea kukupenda hivy ulivyo!!
Siku zilizidi kusonga,, Siku moja Shamy akapigiwa simu ikitokea nyumbani kwao kuwa aende kwenye harusi ya kaka yake huko Jijini mwanza!
Shamy akalazimika kuondoka kesha yake kuelekea Mwanza! kwa ajili ya maandalizi wiki moja kabla…. akamuacha Zack ndani ya chumba chake kisha akasema,, “baada ya harusi nitarejea,,
baada ya siku mbili kupita Zack akaenda kumtembelea shangazi yake..alipofika shangazi yake akasema,, jiandae wiki ijayo tutasafiri mimi na wewe tutaelekea Mwanza…..kunandugu yako ulande wa baba yako anaoa..
Kauli hiyo ikamfanya Zack afurahi sana kwa sababu anajua kuwa Shamy pia yupo mwanza hivy wataonana!
baada ya wiki moja kupita safari ikawadia.. Zack na shangazi yake pamoja na mjomba wake ambaye ni mume wa shanga yake,, wakaingia ndani ya gari na safari ikaanza..
siku ya leo ilikuwa ndio siku ya harusi. hivyo walichelewa wakakuta tayari watu wapo ukumbini na sherehe inaendelea,,,, Zack akaketi meza moja yeye na shangazi yake!
alipoangaza angaza macho yake akamuona binti mmoja kavalia gauni refu lililoshikiria maungo ya mwili wake vyema.. na kuonyesha uhalisia wa umbo lake.. binti huyo alifanana sana na Shamy….
Sherehe ikaendelea……ukafika wakati wa utambulisho wa ndugu….. wakatambulishwa wazazi wa bwana harusi……. Zack akafurahi kumuona baba yake lakini hawezi hata kumsalimia kwa sababu baab yake alimtelekeza wala hataki kumuona!
Zack akamuuliza shangazi yake,, “inamaana huyo anayeoa ni kaka yangu wa damu?
shangazi yake akajibu,, “ndio ni kaka yako wa damu,, pia unamuona yule binti aliyevaa gauni la bluu? huyo pia ni dada yako! wa damu… kisha akamuita mmoja kati ya wahudumu wa sherehe hiyo.. akauomba amuite yule binti aliyevaa gauni labluu….
baada ya dakika moja kupita alionekana binti huyo akija kwenye meza hiyo…. kumbe binti huyo ni mpenzi wa Zack,, hakuwa mwingine bali ni Shamy!
Wakati huo Zack alikuwa kanyanyuka pale kwenye kiti, alikuwa chooni,, Shangazi yake Zack akamwambia Shamy,, “nimekuita nikusalimie mwanangu…. Siku hizi mbona hauji kunitembelea! tatizo ni nini?
Shamy akatabasamu kisha akazema,, “samahani shangazi nilikuwa natingwa na masomo! lakini kwa sasa nimeshamaliza chuo nakuahidi nitakuwa nakuja kukutembelea mpaka utanichoka! Shamy aliongea maneno hayo huku uso wake ukionekana kuwa na tabasamu muda wote, kisha akasema,, wacha nikawaambie wahusika wa upande wa vinywaji wawaongezee vinywaji!
Shamy akazipiga hatua na kuondoka zake,,
Wakati huo huo alionekana Zack akitokea chooni akija pale kwenye meza! alipofika Shangazi yake akasema, umechelewa dada yako alikuwepo hapa,, lakini utamuona tu na mtafahamiana!
Zack akawa na shauku ya kutaka kufahamiana na dada yake,,, akasema,, “sawa shangazi kwani tunaondoka lini?
Shangazi yake akajibu,, “kesho mchana!
Zack akasema,, “sawa,,kisha akatoa simu yake,, akaandika ujumbe mfupi wa maneno(sms) akautuma kwenye simu ya Shamy… akimuuliza kuhusu sherehe inaendeleaje! baada ya sekunde kadhaa kupita Shamy akajibu ujumbe wa Zack akisema,, “huku sherehe imependeza sana natamani ungekuwepo,, lakini sina namna,, vipi sherehe yenu? alafu nilisahau kukuuliza,upo mwanza sehemu gani?
Zack akataka kumuuliza Shangazi yake, kuwa hapo walipo panaitwaje lakini akamuona shangazi yake yupo qnaongea na mumewe! akaona si vyema akikatisha maongezi ya watu wazima! akabaki kimya huku akiendelea kuchezea simu yake!
wakati huo huo alionekana Shamy akiendelea kuwasiliana na Zack kwa njia ya meseji(sms)
baada ya lisaa limoja kupita sherehe ilikaribia kufika ukingoni,, akaonekana maam yake Shamy akimfuata Shamy akamkabidhi ufunguo wa gari akasema,, “itabidi utangulie na wageni wale… Shamy akatazama ule upande alioonyeshwa na mama yake.. akaona ni bibi na babu yake… Shamy akamtazama mama yake huku akitabasamu kisha akasema,, “hakuna shaka mama,, kwanza wale ni wazee sio vyema wakae macho mpaka muda huu,, usiku umeenda sana,, wacha niwapeleke,,, Shamy akanyanyuka na kuzipiga hatua mpaka pale alipokuwa ameketi bibi na babu yake… akawachukua akaongozana nao mpaka nje ya ukumbi,, wakalifuata gari na kuingia ndani ya gari hilo!
Zack alimuona dada yake akitoka nje ameongozana na wazee wawili,, akaamua kuwafuata kwa nyuma,, ili angalau akafahamiane na dada yake kwa sababu tayari alionyeshwa kuwa huyo ni dada yake.. lakini hawakuweza kuongea..
Zack alipofika upande wa nje akaangaza angaza macho yake,, lakini hakumuona tena dada yake!! alipotazama upande ambao yameegeshwa magari akaliona gari moja likiondoka,,, akajisemea moyoni,, “bila shaka wameondoka na gari hilo!
Zack akazipiga hatua na kurudi ndani ya ukumbi! lakini akawa anajisemea moyoni! dada yangu anafanana sana na Shamy!! lakini dada ni mweupe kupita kiasi kuliko Shamy,….. Zack hakuweza kutambua kuwa huyo ndiye Shamy mwenyewe! kwa sababu hakuwahi kumuona Shamy kajiremba usoni kiasi hicho….. yeye anaamini kuwa Shamy huwa hapendi kupaka vipodozi usoni wala kuchora kope,, na kuchora midomo yake kwa rangi..
Zack alipofika pale kwenye meza, shangazi yake akasema,,” muda mchache ujao tutaondoka kwenda kupumzika kwa sababu sherehe imekwisha….
baada ya lisaa limoja kupita wakanyanyuka kutoka kwenye meza hiyo wakazipiga hatua kutoka nje ya ukumbi wakaingia ndani ya gari,, na safari ya kuelekea VIZANO HOTEL ikaanza,,,
wakati wanatoka ndio muda Shamy alikuwa anarudi kuwafuata wazazi wake waondoke pamoja kurudi nyumbani,,, magari hayo mawili yakapishana pale getini,, Shangazi yake Zack akasema dada yako huyo amerudi! kisha wakaendelea na safari..
hapakuwa na umbali mrefu,, walitumia mwendo wa dakika kumi mfululizo wakawa wamefika VIZANO HOTEL,
zack akapatiwa chumba chake kwa ajili ya mapumziko,, pia Shangazi yake na mumewe walichukua chumba kingine!
*********************************************
kule chumbani alionekana Zack akiwa amejilaza kitandani,, akachukua simu yake akampigia Shamy,,,
Shamy akapokea simu kisha akasema nivumilie kipenzi cha moyo wangu,.,nipo naendesha gari nikifika nyumbani nitakupigia simu! kisha akakata simu hiyo.
Shamy alipofika nyumbani,, akaingia chumbani kwake akaingia bafuni kuoga kisha akajilaza kitandani,, akachukua simu yake Akampigia Zack,,,,
katikati ya maongezi Shamy akamuuliza Zack kafikia sehemu gani?
Zack akajibu,, “VIZANO HOTEL….nimo kwenye chumba namba 57.
shamy akafurahi sana akasema sio mbali na nyumbani kwetu.. kesho mapema,nitakuja, wewe unatarajia kuondoka lini?
Zack akajibu,, “kesho mchana,
Shamy akasema,, “nitajitahidi kuwahi kabla haujaondoka.
***************************************
Asubuhi palipokucha,,. Zack akaletewa chai,, mule ndani ya chumba chake..
ilipofika mida ya saa tano za asubuhi,, Shangazi yake Zack akampigia simu Zack akimsisistiza ajiandae kuwa wanaondoka muda mchache ujao.. Zack akachukuwa simu yake akapigia Shamy akamsisitiza awahi,,
Upande mwingine alionekana Shamy akiwa ndani ya taxi,, akimsisistiza dereva aendeshe gari kwa mwendo wa kasi ili Shamy amuwahi Zack kabla hajaondoka..
awalipofika maeneo ya MWANZA HOTEL wakakuta kunamsongqmano wa magari.. kulikuwa na msafara wa chama cha siasa.. Shamy akaamua kumlioa dereva taxi,, kisha akashuka na kukodi bodaboda…..
baada ya dakika kadhaa akawa amefika VIZANO HOTEL… akamuuliza muhudumu aliyepo upande wa mapokezi,,, muhudumu huyo akachukua kitabu cha orodha ya majina ya wateja waliolala hapo,, akaona jina la Zack limewekewa alama ya tiki.. alama hiyo inamaanisha kuwa mteja huyo ameshatoka ndani ya HOTEL hiyo!!!
Shamy akatoa simu yake kwenye pochi,, akampigia Zack,,
Zack akapokea simu ya Shamy,, akaongea kwa unyonge akimlaumu Shamy!
Shamy akajikuta anakuwa mnyonge,, akaomba samahani kwa kuchelewa kufika! Zack akamuelewa Shamy kisha akamuuliza wewe unarudi lini Dar es salaam?
Shamy akasema itabidi nije kesho kutwa,, kwanza nimekukumbuka sana kipenzi changu! siku nilizokaa huku zinatosha!
Zack akafurahi sana kusikia taarifa hiyo!
Ilipofika majira ya saa saba za usiku,, wakawasili Dar es salaam,, Zack akaamua kulala nyumbani kwa shangazi yake kwa sababu ni usiku sana…
Sehemu Ya 2
Asubuhi palipokucha Zack alidamka akakuta kijakazi wa nyumba hiyo ameshaandaa chai,,akanywa chai kisha akamuaga shangazi yake na kuondoka kuelekea kule kwenye nyumba anayoishi yeye na Shamy!
baada ya siku moja kupita; Shamy akarejea nyumbani akitokea Mwanza,, Zack akafurahi sana,,msiku zilizidi kusonga hatimae Shamy akapata kazi, akaajiliwa katika hospitali ya Muhimbili,, Maisha ya Shamy na Zack,,yakabadilika wakahama katika nyumba hiyo,, wakapanga nyumba nzima huko Mbezi,, Shamy akaamua kumpa Zack mtaji aanze kufanya bihashara kuliko kukaa tu nyumbani pasipo kujishughurisha kutafuta kipato!!
Shamy akampa Zack mtaji wa milioni kumi(10) zlZack akafungua duka la vifaa vya umeme,, duka hilo lilimpa kipato kizuri kila siku zilivyozidi kwenda.. Zack akabadilika akawa kijana mtanashati kuliko,, maisha yao yakawa yenye amani na furaha kila kukicha!
Siku moja Shamy akamwambia Zack,, “jumapili hii tutakwenda nyumbani kwa shangazi yangu,, anaishi kigamboni,,, nataka nikakutambulishe kwake! Zack akafurahi sana..kisha akasema hata mimi pia shangazi yangu anaishi kogamboni,, tukitoka huko tutapitia nyumbani kwake pia nikakutambulishe!
jumapili ikafika,, siku hiyo wakadamka na kujiandaa kwenda nyumbani kwa shangazi yake Shamy! kutokana na elimu aliyokuwanayo Shamy,, alikuwa ni daktari maalumu kwa kufanya upasuaji wa Moyo… hivyo alikuwa ni mtu muhimu sana na tegemezi katika hospitali hiyo….
Shamy na Zack wakaingia ndani ya gari la Shamy. na safari ikaanza..
baada ya lisaa limoja walifika kigamboni!! Shamy akaliongoza gari lake kukatisha kwenye barabara ya vumbi, akiiacha lami.. Zack akastaajabu! akauliza,, “huku ndipo shangazi yako anapoishi?
Shamy akatabasam kisha akajibu,, ndio,, kwa nini umeuliza hivyo? hujayapenda mazingira haya?
Zack akasema,, “barabara hii pia inaelekea nyumbani kwa shangazi yangu! yawezekana wakawa majirani! Shamy akaendelea kuliendesha gari lake… Zack akazidi kustaajabu kuona wanakatisha kwenye njia inayoelekea kwa shangazi yake! akauliza kwa mshangao,, “haa! yani huku tunapoelekea ndipo nyumbani kwa shangazi yangu… nyumba ileee..wakati Shamy anatazama ile nyumba anayo onyeshwa na Zack,,, punde si punde,,, simu ya Shamy ikaita,akaacha kuendelea kutazama kule anapoonyeshwa na Zack.. akaitazama simu yake kisha akaipokea..simu hiyo ilikuwa inatokea Muhimbili.
Shamy akaambiwa kuwa kunadharura, hivyo anahitajika Hospitali haraka kwa ajili ya kufanya upasuaji wa moyo w mgonjwa aliyekuwa mahututi,, akageuza gari lake huku akimwambia Zack,, nahitajika kazini haraka iwezekanavyo..Zack hakuwa na kipingamizi!
akabaki kimya,, Shamy akaliendesha gari lake kwa kasi kuelekea Muhimbili.
walipofika Shamy akambusu shavuni Zack kisha akasema,, “samahani kipenzi naomba unisubiri hapa kwa dakika kadhaa wacha nikawajibike! Zack akasema sawa mpenzi utanikuta… Shamy akashuka kutoka ndani ya gari,,,akazipiga hatua za haraka haraka. kuingia ndani ya jengo la hospitali….. wakati anazipiga hatua kuelekea kwenye chumba cha upasuaji akastaajabu kukutana na shangazi yake kwenye korido..akiwa kaongozana na mumewe akizipiga hatua za taratibu kupita kiasi kwa sababu alikuwa kapooza upande mmoja! Shamy akawasalimia kisha akasema,, nilikuwa nije kukutembelea nyumbani kwako,,kumbe tungepishana? hata hivyo niliishia njiani baada ya kupigiwa simu kuwa nahitajika kazini,, Shangazi yake akasema,, “kumbe unafanya kazi hapa?? hongera sana mwanangu!! Mungubakutangulie kwenye kazi yako.. ghafla simu ya Shamy ikaita alipoitazama ilikuwa ni daktari mwenzake anampigia.. Shamy akamwambia shangazi yake,, “tutawasiliana,, aliongea maneno hayo huku akazipiga hatua za haraka haraka kuufuata mlango wa chumba cha upasuaji!
wakati huo huo kule nje ya hospitali alionekana Zack akiwa bado yumo ndani ya gari,, akimsubiri Shamy amalize kazi iliyomleta kisha waondoke… alipoangaza angaza macho yake akamuona Shangazi yake akiwa na mumewe!! akashuka kutoka ndani ya gari akawafuata.
alipowakaribia akauliza,, “kulikoni nani mgonjwa? Shangazi yake akajibu.. nilikuja kwenye mazoezi maalumu,, pia kunadawa nilikuja kuchukua….pia nimemuona dada yako,,ni daktari wa hospitali hii…
Zack akasema,, “itabidi unipe namba zake za simu kama unazo”
Shangazi yake akachukua simu yake ili ampe namba za simu za dada yake! alipobofya simu yake,, akagundua kuwa imezimika,, akasema,, “ooh kumbe simu imezimika chaji.. nitakutumia kwenye ujumbe wa maneno(sms) Zack akasema hakuna shaka,,pia mchumba wangu ni dakatari katika hospitali hii..
kabla hajamalizia sentensi…. kwa mbali akamuona Shamy anakuja akitokea ndani ya jengo hospitali akija ulande wao.
Wakati Shamy anazipiga hatua,,, simu yake ikaita,, akaipokea akaambiwa kuwa arudi kusaini(signature) ili alipe malipo ya ziada kwa ajili amefanya kazi wakati ni siku ya kupumzika! Shamy akaamua kurudi ndani ya jengo la hospitali,,, akasaini.. kisha akazipiga hatua kuelekea kwenye ofisi ya muhasibu wa hospitali hiyo.. akapewa pesa.. kShamy hakutaka kupoteza muda,,akazipiga hatua kutoka nje ya jengo la hospitali hiyo! kumbe wakati Shamy yupo kwenye ofisi ya muhasibu,, ndio wakati shangazi yake alikuwa anaagana na Zack kule nje. kisha akaingia ndani ya gari akiongozwa na mumewe.. wakaondoka kuelekea nyumbani!
Shamy alipofika nje kabisa ya Jengo hilo,,akazipiga hatua za taratibu kulifuata gari lake kule alipoliegesha! akafungua mlango akaingia ndani ya gari.. akasema,, “samahani mpenzi kwa kuchelewa.
Zack akajibu,, “usijali mpenzi mimi nipo kwa ajili yako! alafu umechelewa kidogo nimekutana na shangazi yangu dakika chache zilizopita!
Shamy akasema,,”hata mimi pia nimekutana na shangazi yangu,wakati naingia kwenye chumba cha upasuaji! lakini hatujaongea sana nilikuwa namuwahi mgonjwa.. kumbe tungeenda nyujmbani kwake muda ule tusingemkuta,, tungepishana.
lakini usijali mpenzi tutakwenda siku nyingine.
Shamy aliongea maneno hayo huku akiliwasha gari lake,, na safari ya kuelekea nyumbani ikaanza…
baada ya lisaa limoja kupita wakawa wamefika Mbezi.. Shamy akaliongoza gari lake mpaka nyumbani..
**********************************************
Siku zilizidi kusonga na Maisha yakaendelea biashara ya Zack ilizidi kukua siku hadi siku akafungua duka la pili,,duka hilo likawa kubwa mara tatu ya lile la kwanza, Zack akawa ana muda mchache wa kupumzika na mchumba wake(busy). Kitendo hicho kilimfanya Shamy aanze kuhisi huenda Zack kapata mwanamke mwingine hivyo anamsaliti, siku moja Shamy akaamua kumuuliza Zack kwanini umebadilika? Zack akajibu, “hivyo unisikiliavyo sivyo ni msongo wa kazi wataki mwingine narudi nyubani usiku sana ,Shamy akakubali kishingo upade lakini bado akawa na wasi wasi kuhusu Zack.
kadri siku zilivyozidi kusonga,,,mapenzi yao yalizidi kukuwa.. pia bihashara ya Zack ikazidi kuongeza kilato kadri siku zilivyozidi kusonga.. hatimae akaacha kuagiza mizigo,akawa anasafiri mwenyewe kwenda China na Dubai kufata bidhaa za kuuza kwenye maduka yake!
Siku moja Zack alisafiri kwenda China, kufata bidhaa,, baada ya wiki moja,,akaunganisha safari akaelekea Dubai!
siku aliyoondoka Zack kwenda China.. Usikubwa siku hiyo Shamy alipigiwa simu kuwa Shangazi yake ni mgonjwa mahututi.. kalazwa hospitali ya rufaa Muhimbili.. Shamy akawasha gari lake haraka akaelekea Muhimbili.. alipofika akawa amechelewa akakuta shangazi yake ameshakufa! Shamy akaangua kilio kwa uchungu wa hali ya juu.. akajitahidi kumpigia simu Zack ili ampe taarifa.. lakini Zack a
akawa hapatikani kwenye simu!
Taratibu za mazishi zikafanyika wakazika kesho yake…
Baada ya wiki moja kupita Zack akarejea nchini Tanzania..,,,alipofika nyumbani,, Shamy akampa taarifa kuwa shangazi yake amefariki, wiki iliyopita na tayari walishazika!
Zack alisikitika sana akampa pole mchumba wake!
Zack alikuwa kamletea zawadi Shamy,, simu pamoja na viatu.. Shamy akafurahi sana.
miongoni mwa zawadi alizoleta pia zilikuwemo zawadi za shnangazi yake….
kesho yake akazichukua zawadi hizo ili ampelekee sahangazi yake kule kigamboni!
alipofika akastaajabu kuambiwa kuwa shangazi yake amefariki, wiki moja iliyopita! akasikitika sana,, akalia kwa uchungu!
akampogia simu Shamy, akamwambia,, “shangazi yangu pia kafariki,, wiki moja sasa imepita,, Shamy akampa pole mchumba wake,,kwa kumwambia maneno ya kumfariji!
siku zilizidi kusonga… safari za Zack kwenda nje ya nchi.. zikazidi! kitendo hicho kilimnyima Shamy furaha! wakati mwingine akawa anahisi kuwa Zack atakuwa na mwanamke mwingine!
Siku moja Shamy akiwa kazini,,, akaingia daktari mkuu, kwenye ofisi ya Shamy,, dakatari huyo,, mwenye umri wa makamo kiasi akaanza kumtongoza Shamy kwa kumrubuni kuwa atampandisha cheo…. Shamy akakataa kata kata akisema,, “mimi tayari ninamchumba,, tunatarajia kuoana hivi karibuni.. Daktari mkuu,, akaondoka huku akimwambia,,naomba uendelee kutafakari najua nimekushtukiza ndio maana unashindwa kunila jibu sahihi..
Shamy akabaki na maswali mengi kupita kiasi,, akaanza kukumbuka matukio ya mchumba wake(Zack) zile safari za mara kwa mara tena za kushtukiza…pia hata akirudi nyumbani analala anasema amechoka! Shamy akajisemea moyoni,, “wacha nifanye uchunguzi ili nibaini ni nani anayemchanganya mchumba wangu mpaka anashindwa kunipa haki yangu ya chumbani ipasavyo!
Shamy aliporudi nyumbani akaandaa chakula cha usiku kisha akamkaribisha Zack,, wakaanza kula chakula… walipomaliza wakaenda kuoga kisha wakapanda kitandani.. shami akaanza kumdadisi Zack kwa kumuuliza maswali,, Zaki akaishia kusema hayo unayoniwazia hakuna hata mojawapo lenye chembe ya ukweli ndani yake,, mimi siwezi kukusaliti nakulenda sana,,, tatizo ni wingi wa majukumu ya kazi… Shamybakabaki kimya bola kuuliza swali lingine! baada ya nusu saa kupita Zack akasinzia kabisa.. Shamy akanyanyuka kitandani akachukua simu ya Zack akaanza kukagua.. lakini hakupata ushahidi wowote.. punde si punde ukaingia ujumbe mfupi wa maneno(sms) ni mwanamke alikuwa amemtumia ujumbe huo Zack.. alipousoma.. akastaajabu ulikuwa ni ujumbe wa mapenzi! akajisemea moyoni! siamini hili ninachokiona! akaamua kuichukua namba hiyo akapiga simu kwa kutumia simu ya Zack… kumbe aliyetuma ujumbe huo alikuwa kakosea namba.. alikuwa anamtumia mtu mwingine!! Shamy akakubali lakini akawa bado na wasiwasi kuhusu mwanamke huyo!
Shamy akaitazama namba hiyo lakini hakuiona katika orodha ya namba zilizohifadhiwa kwenye simu ya Zack!
akaamua kulala,,
asubuhi palipokucha akaenda kazini,, akiwa ndani ya ofisi yake, daktari mkuu akaingia ofisini kwake.. kisha akaketi akamwambia Shamy kuwa anahitaji wale chakula cha mchana pamoja!
Shamy akasema,, “bila shaka kama ni chakula usijali.
Daktari mkuu akatabasamu kisha akafungua mlango na kuelekea kwenye ofisi yake.
ilipofika mida ya saa saba za mchana Daktari mkuu akaongozana na Shamy mpaka ndani ya gari lake,, akaliwasha wakaelekea LEGENCY HOTEL kwa ajili ya kupata chakula cha mchana! walipofika,,Daktari mkuu aitwae SHIRIMA akachukua begi dogo la plastiki(breefcase) akashuka kutoka ndani ya gari huku kalibebelea begi hilo… akaongozana na Shamy mpaka kwenye viti, kisha wakaagiza chakula cha aina moja!
kabla chakula hakijaletwa.. Shirima akaanza kusimulia historia ya maisha yake!
akasema,, “miaka ishirini na nane (28) iliyopita.. nilikuwa dereva wa daktari mkuu huko mwanza kwenye hospitali ya BUGANDO,, lakini mke wake alitokea kunolenda sana.. mimi nilikataa lakini alinilazimisha kisha akanitishia kuwa endapo nikiendelea kumkatalia atamwambia mumewe kuwa mimi ndiye nimemtongoza nivyo atanisimamisha kazi.. wakati huo nilikuwa kijana mdogo.. nikalazimika kukubali ili kulinda kazi yangu… sikumoja Daktari huyo alisafiri,,
mkewe akaniita nymbani kwake… akanishawishi hatimae tukashirikiana kimwili… kumbe ndani ya chumba hicho kulikuwa na kamera(UCCTV) zikarekodi tukio zima… kamera hizo zilitegeshwa na mumewe kwa siri pasipo mke wake kujua…siku hiyo akapata ujauzito,,,
Daktari huyo aliporudi akaona tukio zima kupitia video iliyorekodiwa na kamera hizo.. akaamua kumfukuza mkewe.. kiwha akasema ataniuwa… mimi nimatoroka na kukimbilia Kenya.. nikaishi huko kwa miaka mingi sana…. Shirima akasitisha kuongea kisha akafungua lile begi dogo la plastiki (breefcase)
akatoa picha akamuonyesha Shamy, kisha akasema,, “hii ni picha ya mwanamke huyo na sijui yuko wapi? pia huyo mtoto wangu sijawahi kuiona hata sura yake Shamy akaitazama picha hiyo,, kisha akasema,, “pole sana kwa mkasa uliokupata.. hii ni kati ya sehemu ya maisha ya binadamu..
kisha akaiweka picha hiyo juu ya meza,,, punde si punde chakula kikaletwa wakaanza kula huku wakibadilisha mawazo!
walipomaliza kula,, Shamy akanyanyuka akasema,,”nisubiri kwa dakika kadhaa narejea..
Shirima akauliza,, “unakwenda wapi Shamy akasema naenda chooni, aliongea hivyo huku macho yake yakionekana kuwa na aibu.
Shirima akasema utanikuta ndani ya gari turudi kazini.
Sahamy akazipiga hatua kuelekea chooni!
Shirima akachukua begi lake akazipiga hatua kuelekea kwenye gari lake akaingia ndani ya gari akawa anamsubiri Shamy!
baada ya dakika mbili kupita Shamy akarejea akastaajabu kuikuta ile picha bado ipo juu ya meza! kumbe Shirima aliisahau.. Shamy akaichukua na kuiweka ndani ya mkoba wake kisha akazipiga hatua kulifuata gari la Shirima.. akafungua mlango na kuingia ndani ya gari… Shirima akawa anaongea mfululizo mpaka Shamy akasahau kumpa Shirima ile picha..
walipofika Muhimbili.. Shamy akashuka kutoka ndani ya gari kisha akalifuata gari lake.. na kuliwasha akaelekea nyumbani!
alipofika akajilaza kitandani.. alipodamka ilikuwa ni majira ya saa moja za jioni.. akaandaa chakula cha usiku.. punde si punde Zack akarejea nyumbani!
alipofika akamsalimia mchumba wake kwa furaha kisha akaingia chumbani… akakuta simu ya Shamy inaita ndani ya mkoba! akapaza sauti,, “SIMU YAKO INAITA.
Shamy akasema,, “samahani kipenzi naomba uniletee,,, nitaunguza mboga opo jikoni..
Zack akafungua mkoba akatoa simu! akaona kunapicha akaichukua picha hiyo.. alipoitazama,, macho yakamtoka akashtuka kuona picha ya mama yake ipo ndani ya mkoba wa shamy!
akajiulizaaswali mengi yasiyokuwa na majibu!! akazipiga hatua kulifuata begi lake,, akalifungua akazitoa picha za mama yake,, akazitazama kwa muda mrefu kiasi,,kisha akaitazama ile picha ya mama yake aliyoikuta kwenye mkoba wa Shamy! akatabasamu kisha akajisemea moyoni,, “sasa mbona kaichagua picha hii!? bila shaka kaipenda kuliko picha hizi zote! Zack akahisi huenda shami alofungua begi lake akatoa picha hiyo,, hakujua kuwa Shamy kaitoa wapi picha hiyo,, punde si punde simu ya Shamy ikaita tena,, Zack akajisahau kuirudisha picha ile ndani ya mkoba wa Shamy akaichanganya kwenye picha nyingine za mama yake na kuzirudisha ndani ya begi lake! kisha akalifunga na kuzipiga hatua kuufuata mlango akaufungua na kutoka chumbani akaelekea kule jikoni alipokuwepo Shamy,, akamkabidhi Shamy simu yake.. kisha yeye akaelekea sebuleni,, akawasha Runinga na kuanza mutazama vipindi! ya kwenye Runinga.
Baada ya lisaa limoja kupita Shamy alimaliza kuandaa chakula akakiweka kwenye meza ya chakula.. akamkaribisha Zack wakaanza kula…
Zack hakuuliza kotu fhoxhote kuhusu ile picha kwa sababu aliamini Shamy hakuichukua kwa lengo baya!
Siku zilizidi kusonga,, lakini simu Shamy ikawa inaita mara kwa mara,, tena ni namba moja pekee iliyokuwa ikimpigia mara nyingi, hata nyakati za usiku wakati Zack na Shamy wamepumzika!!! Zack akaanza kuingiwa na wasiwasi kuhusu namba hiyo lakini hakumwambia Shamy kitu chochote,, akawa anafanya uchunguzi kudadisi mawasiliano ha Shamy na pamoja na hiyo namba inayompogia mara kwa mara!
Siku moja nyakati za usiku,, wakati Shamy yumo bafuni anaoga, ghafla ukaingia ujumbe mfupi wa maneno, kwenye simu ya Shamy!
Zack akaangaza macho yake ili aone kama Shamy anashuhudia anachotaka kukifanya.
akaona hakuna dalili zozote za Shamy,, kuja muda huo kutokea bafuni.
akaufungua ujumbe huo,, alipousoma akashtuka! ujumbe huo ulisomeka hivi; habari ya usiku huu! nimekukumbuka,, na nomefurahi sana mchan wa leo tulivyokuwa pamoja! pia nakutakia usiku mwema,, ewe mwanamke nikupendae!
Zack akahisi kuishiwa nguvu,, jasho likamtoka! akajisemea moyoni,, ” Shamy ananisaliti? kosa langu ni lipi? je!? huyu ni nani anayetaka kuvuruga uchumba wangu mimi na Shamy? Zack akaamua kuufuta ujumbe huo Shamy asiuone..
Shamy alipotoka bafuni akapanda kitandani,,lakini akamuona Zack akionekana hana furaha,akauliza,,”Mbona kama unamawazo! nini kinakutatiza?
Zack akaqmua kudanganya kwa kusema hakuna kitu,, nahisi uchovu tu.
Shamy akazima taa wakaanza kuutafuta usingizi!
********************************
Siku zilizidi kusonga,,Shirima hakuacha kumsumbua Shamy,, kwa kuendelea kumchombeza maneno ya kimapenzi kila siku!
Shirima akaamua kumbadilishia Shamy muda wa kufanya kazi,,akamuweka kwenye orodha ya madaktari wa zamu ya usiku (night shift) ..Shamy hakuwa na kipingamizi kwa sababu Mkuu wake wa kazi!
Shirima aliamja kufanya hivyo kwa lengo moja tu,, aweze kuwa na Shamy muda mwingi,, huenda Shamy akashawishika na kumkubalia!
kitendo hicho kilimfanya Zack awe mnyonge sana,, akikumbuka na ule ujumbe mfupi wa maneno(sms) aliyouona kwenye simu Shamy,, anakuwa mnyonge kabisa..
Sikumoja Zack akaomba ushauri kwa rafiki yake kipenzi,, akamueleza yote aliyoyasnhuhudia..
Rafiki yake huyo akamshauri kuwa aende kwa mganga,, Zack akashawishika akaona ni ushauri mzuri na unafaa!
Zack akamuaga rafiki yake kisha akaingia ndani ya gari na kurudi nyumbani.
akiwa njiani,,wazo likamjia,,akajisemea moyoni,, “kwa nini nisimuangamize kabisa huyo kinyago anayetaka kuingilia mapenzi yangu!
*******************************
INAENDELEA

