NYUMBA YA MAAJABU
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Sehemu Ya 4
Walikaa pale sebleni kwa muda kidogo na hata mchana iliwakutia pale pale, muda kidogo Neema akamwambia Sophia kuwa chakula cha mchana kilikuwa tayari mezani, Sophia alimuangalia na kumuuliza kuwa amekipika muda gani kwani kwa kumbukumbu zake walikuiwa wote hapo sebleni kwa muda wote pamoja.
Neema akatabasamu na kumwambia Sophia,
“Tulikuwa wote ndio ila wewe muda mwingi ulikuwa unasinzia, mimi nimeenda kupika nimekula hata hujajua. Pole dada, ila ni hali yako hiyo ndio imekufanya hivyo”
“Kheee kwani unajua kama mimi nina mimba! Nani kakwambia?”
“Si ngumu kumgundua mwanamke mjamzito tena ikiwa mtu unauzoefu nao ndio kabisa yani, mi hata mtu mwenye mimba ya siku moja namjua sembuse hiyo mimba yako ya miezi mitatu jamani”
Sophia akashtuka kuona kuwa Neema amejua hadi muda wa mimba yake kuwa ina miezi mitatu,
“Khee umejuaje kama mimba yangu ina miezi mitatu?”
“Mimi hata mimba ya siku moja nagundua kutokana na kukaa sana karibu na bibi yangu, tena mimba yako wewe hiyo miezi mitatu ipo wiki ya mwisho maana wiki ijayo itaanza mwezi wa nne. Yani usijali chochote, mimi nilishaisoma hali yako dada nenda kale upate nguvu maana mimba inataka uwe unakula hata kwa kujilazimisha ila uwe unakula ili kumfanya mwanao akue vizuri”
Sophia hakuongea zaidi ila aliinuka na kwenda mezani kula ambapo alikula vizuri sana tofauti na siku zingine ambavyo huwa anakula kwa kujivuta vuta, alikuwa akifurahia tu utamu wa kile chakula kwa muda ule.
Alipomaliza kula alirudi pale sebleni na kukaa tena na Neema ambaye alionekana makini sana katika kuitazama ile Tv kamavile kuna vitu vya maana anavyovitazama kwani alionekana kuwa makini mno.
Sophia akamuuliza tena Neema kuwa anapendea nini kutazama Tv muda wote na kumuuliza kuwa kama hachoki kutazama vile.
“Si nilishakujibu dada kuwa napenda kuangalia Tv kuliko kitu chochote kile kwahiyo wewe usijali, au hupendi niwe naangalia?”
“Hapana, wee angalia tu Neema”
Sophia aliamua kujivunga tu kwa muda huo ingawa kiukweli hakupenda kwavile aliona Tv inakosa muda wa kupumzika.
Ibra aliwahi kutoka kazini siku hiyo kwani alihitaji kuzungumza na Jane na pia kumuomba awe anaenda nyumbani kwake pindi yeye akiwa kazini, kwahiyo moja kwa moja safari yake ilikuwa ni kuelekea kwakina Jane. Alipofika kwa bahati nzuri alimkuta Jane akiwa mwenyewe nje ya nyumba yao na kumuomba kwaajili ya mazungumzo,
“Jane samahani nimekuita kwa pembeni kwavile naogopa mama yako asije akaniona bure. Tafadhali twende wote nyumbani kwangu nataka kuongea nawe kidogo tu”
Jane akaingia kwenye gari ya Ibra bila hata kuhoji maswali ya ziada, kisha Ibra akaendesha gari ambapo alipokaribia na nyumbani kwake alilisimamisha na kuzungumza kidogo na Jane.
“Kwanza unaendeleaje maana mama yako asubuhi alifoka sana hata sijui alijuaje”
“Dunia haina siri, siku ile nimepiga kelele kuna watu walimueleza mama na vile nilivyorudi naumwa mama aliniuliza sana mwisho wa siku sikuweza kuendelea kumficha na nikaamua kumwambia ukweli”
“Sawa hakuna tatizo Jane hata hivyo tulifanya makosa sana, ila kuna kitu kimoja nilikuwa naomba unisaidie”
“Kitu gani hicho?”
“Pale nyumbani tumepata msichana wa kazi ila mimi nimejikuta kutokumuamini kwakweli, sasa nilikuwa naomba pindi nikiwa kazini uwe unaenda pale nyumbani mara kwa mara kumuangalia mke wangu na ikiwezekana hata uwe unashinda pale pale”
Jane akajifikiria kidogo ila hakukataa na kumfanya Ibra afurahi kisha akamuomba kwa muda huo aingie nae ndani ili angalau amfahamu huyo mdada wa kazi waliyempata.
Ibra alisogeza gari yake mpaka getini kabisa kisha akashuka pamoja na Jane kuelekea ndani, na walipofika Ibra alifungua mlango wa ndani na kuingia ambapo Sophia na Neema walikuwa pale pale sebleni.
Ila Jane alipomuona Neema alishtuka sana na kufanya wote wamshangae kilichomshtua kiasi kile.
Ibra alisogeza gari yake mpaka getini kabisa kisha akashuka pamoja na Jane kuelekea ndani, na walipofika Ibra alifungua mlango wa ndani na kuingia ambapo Sophia na Neema walikuwa pale pale sebleni.
Ila Jane alipomuona Neema alishtuka sana na kufanya wote wamshangae kilichomshtua kiasi kile.
Jane alianza kurudi kinyumenyume na kuwafanya washangae zaidi huku Ibra akimuuliza kuwa tatizo ni nini au ni kitu gani kakiona, ila Jane hakusema chochote na alionekana akizidi kurudi kinyumenyume na alipofanikiwa kufika nje alionekana akiondoka kwa kukimbia kabisa eneo lile.
Walibaki wakimshangaa na kutazamana tu, kisha Sophia akamuuliza mume wake
“Umetoka nae wapi Yule na kwanini aogope vile na kukimbia?”
Ibra alikosa jibu ila Neema alionekana akicheka na kisha kuwajibu yeye,
“Hivi unafikiri angeweza kuingia Yule na kukaa pamoja na mimi!”
“Kwanini asiweze?”
“Yule mtoto ni mchawi halafu alikuwa amekuja na vitu vyake vya kichawi, sasa kuniona mimi ameogopa sana sababu mimi ni mtu safi na siwezi kuingiliwa na wachawi. Ndiomana ameshindwa hata kunitazama mara mbili hapa”
Sophia akamuangalia mumewe na kumwambia,
“Umesikia sasa, Yule Jane ni mchawi ila nikisema mimi unaona kamavile namuonea haya sasa leo umesikia kwa macho yako tena licha ya kusikia umeweza kujionea mwenyewe jinsi alivyojawa na hofu hadi kukimbia. Kwakweli Neema amekuja kuikoa familia yetu mume wangu”
Ibra hakuongea chochote kwani hata yeye hakutegemea kabisa lile swala la Jane kumkimbia Neema ambaye wao wanaishi nae ndani, alijikuyta akiwa na maswali pamoja na mawazo mengi sana katika kichwa chake. Ila Sophia alijitahidi kwa muda huo kumuweka mumewe sawa ambapo akamwambia akae ili atulize akili, ila Ibra kabla hajakaa akakumbuka kuwa gari yake alikuwa ameiacha nje ya geti kabisa na hivyo kumwambia mkewe asubiri akaiingize kwanza.
Ila alipotoka ndani tu alikuta ile gari ikiwa imeshaingizwa ndani ya geti huku geti likiwa limefungwa vizuri kabisa, kwakweli akili ya Ibra ilikuwa kamavile inavurugika kwa muda huo kwani alijikuta akiwa haelewi elewi kabisa, kitendo hicho kilimfanya asimame sana pale nje bila ya kuingia ndani ikabidi Sophia amfate nje maana aliona akikawia.
“Si ushaingiza gari, mbona umesimama tu?”
“Hii gari sijaiingiza mimi”
“Sasa nani ameiingiza jamani mume wangu?”
“Hata mimi nashangaa sielewi kabisa”
“Mmh twende ndani bhana itakuwa umejisahau tu”
“Hapana siwezi kujisahau kiadsi hiki Sophy dah! Akili yangu haipo sawa kabisa”
Kisha akaingia ndani na moja kwa moja akaelekea chumbani ambapo Sophia aliamua kwenda kumfata huko chumbani.
Ibra alionekana kujiinamia tu kitandani kwani ilionyesha wazi kuwa alikuwa na mawazo mengi sana, ikabidi Sophia aendelee kumpa moyo mumewe na kuwa karibu naye ili angalau aweze kumsaidia katika kumpunguza mawazo aliyokuwa nayo.
“Ni vitu gani unawaza kiasi hikomume wangu?”
“Wewe acha tu Sophy, kewakweli akili yangu haipo sawa kabisa”
“Pole sana, basi itabidi uoge ili angalau uchangamshe akili. Tafadhali Ibra mume wangu naomba ufanye hivyo”
Ibra alimuelewa mkewe na kuamua kufanya hivyo ambapo moja kwa moja alienda bafuni kuoga. Ila alipokuwa mule bafuni kila akifumba macho inamjia picha ya Yule joka pamoja na picha ya Neema kwakweli akajikuta akipatwa na uoga kupita maelezo ya kawaida. Kitendo hicho kilimfanya atoke bafuni kwa haraka bila hata ya kuoga vizuri.
“Khee mume wangu umetoka hadi na povu sikioni”
“Wee acha tu Sophia, kuna muda nitakueleza na utanielewa vizuri tu”
“Nieleze saizi mume wangu ili tushauriane cha kufanya”
“Hata kama nikikueleza saizi sijui kama utanielewa mke wangu, nitakueleza tu pindi akili yangu itakapotulia”
“Basi twende ukale mume wangu”
“Hiko chakula nani kapika?”
“Amepika Neema”
“Mmh kama Neema hapana, sijisikii kula kwakweli”
“Kheee makubwa, sasa maana ya mdada wa kazi ndani ni nini jamani mume wangu?”
“Mdada wa kazi ni mtu wa kutusaidia kazi za humu ndani ila sio mpaka chakula cha mumeo apike mdada wa kazi”
Sophia alimshangaa sana mumewe kwani hakutegemea kama angeongea maneno kama hayo, aliona kuwa Ibra ni mwanaume asiye na huruma kwani anajua fika hali ya Sophia kuwa ni mjamzito ila bado alihitaji kupikiwa chakula naye, kwakweli Sophia alikuwa amechukia kwa kiasi kisha akainuka na kumwambia,
“Ngoja nikakuandalie chakula mwenyewe basi ili ufurahi”
“Unaenda kuniandalia chakula gani?”
“Wali”
“Sitaki wali, nataka ugali”
Kisha Sophia akatoka mule chumbani na kumuacha Ibra akiwa mwenyewe amejiinamia tu kwa mawazo.
Sophia alienda moja kwa moja jikoni huku akiwaza kuhusu Ibra kutokuwa na huruma na hali yake,kisha akaona ni vyema amsongee tu huo ugali kwa haraka kisha amuandalie na mboga ya haraka aweze kula.
Akabandika sufuria ya kusongea ugali, kisha akaenda kufungua friji ili aangalie kama kuna mboga ya aina yoyote. Alipofungua ile friji alishangaa kwa muda kwa kila mboga aliyoifikiria kichwani mwake ilikuwepo mule akajiuliza kuwa ni Ibra alinunua mboga hizo au imekuwaje, ila moja kwa moja alihisi ni Ibra tu kwani hakuna mwingine ambaye angenunua zile mboga kama sio Ibra.
Akatoa samaki ambao walikuwa wamekaushwa vizuri ili awaunge na kumuandalia Ibra mezani, ila alipokuwa anageuka na wale samaki akashangaa kumuona Neema akiwa ameweka vizuri ugali kwenye sahani na kufanya amuulize kwa mshangao,
“Khee Neema umeingia saa ngapi humu jikoni?”
“Nimeingia wakati wewe unatafuta mboga kwenye friji ndio nikaamua nikusaidie kusonga huu ugali maana maji yalikuwa yanachemka.”
“Umejuaje kama yale maji yalikuwa ya ugali?”
“Kheee dada, ukizoea kupika basi itakuwa rahisi sana kujua kila aina ya pishi na ndiomana nimejua kwa haraka sana kuwa yale maji yalikuwa ya ugali na ugali huo tayari. Lete hao samaki nikupikie haraka wakati unaenda kuandaa huu ugali mezani”
Sophia hakuongeza neno bali alimpa Neema wale samaki kisha akabeba ule ugali na kuupeleka mezani huku akiwaza kuwa neema amewezaje kusonga ugali kwa muda mfupi kiasi kile! Akajiuliza,
“Ingawa ugali ni chakula cha haraka kupika ila mmh ndio kwa muda mfupi vile?”
Hakupata jibu na kurudi jikoni ambapo alimkuta Neema ameshamaliza kuunga wale samaki na alishawaandaa kwenye bakuli, Sophia alishtuka ila alishindwa kuuliza chochote ambapo alichukua ile mboga na kwenda kuweka mezani kisha akaenda kumuita mume wake.
“Chakula tayari Ibra”
“Mmh umepikia kompyuta au?”
“Kwanini?”
“Mbona kimekuwa haraka sana!”
“Nakujali mume wangu na ndiomana nimeharakaisha”
“Sio swala la kunujali Sophia ila umetumia muda mfupi sana”
Kisha Ibra akainuka na kwenda mezani kula ambapo alikula huku akimsifia mkewe kuwa amepika chakula kitamu sana, Sophia alikuwa akitabasamu tu ingawa alielewa wazi kuwa zile sifa alipaswa apewe Neema maana ndiye aliyepika chakula kile, ila hakumwambia mumewe kwavile alikataa kula chakula kilichopikwa na Neema.
Ibra alipomaliza kula alimuuliza Sophia,
“Mbona huyu Neema muda wote namuona akiangalia Tv tu, hivi hachoki?”
“Kasema anapenda kuangalia Tv kuliko kitu chochote kile na ndiomana mimi huwa namuachaga tu aangalie, tena mara nyingine utakuta anaangalia na wala hata hajitingishi yani sijui kukaa vile hachoki”
“Labda hachoki, ila kwa mimi siwezi kwakweli kuangalia Tv muda wote siwezi. Sasa huko kupika na kazi zingine za hapa atakuwa anazifanyaje?”
“Kazi anafanya vizuri ila ndio akishafanya anarudi tena kwenye Tv”
“Mmh basi sawa”
Ibra akainuka na kurudi tena chumbani kwao kwani hakutaka hata kukaa sebleni. Ila Sophia alienda kukaa na Neema ambaye muda wote alikuwa makini kuangalia Tv tena kuna kipindi alionekana kutokupepesa hata macho na kumfanya Sophia ajiulize zaidi kuwa huyu Neema hachoki.
Walikaa pale hadi giza lilipoingia na kuwasha taa za ndani, kisha Sophia akainuka na kuelekea chumbani alipo mumewe.
Alimkuta akiwa amejiinamia tu kama ambavyo alijiinamia mwanzo,
“Kheee hayo mawazo Ibra sasa yamezidi jamani. Tushirikishane hutaki sasa hata sijui ndio nini wakati mimi ndio mkeo”
Ibra muda huu alimuuliza swali Sophia,
“Hivi Sophy una uhakika kuwa Jane ni mchawi?”
“Jane ni mchawi ndio tena ni mchawi aliyekubuhu”
“Mmh sio kwamba anasingiziwa?”
“Hivi mume wangu huyo Jane ana lipi labda la kusingiziwa? Hata kama kusingiziwa ndio watu wote hawa wanamsingizia? Tuseme mimi namsingizia, da’ Siwema je anamsingizia? Yule mganga je? Na Neema je anamsingizia? Yule Jane hata hasingiziwi mume wangu ni mchawi kweli, na bora tumepata kiboko yake humu ndani maana hatokanyaga tena nyumba hii na mauchawi yake”
“Dah! Nashindwa kuamini kwakweli maana mi ninavyomuona Jane ni wa kawaida tu”
“Kwani unafikiri mchawi ukimuona unamjua kwa haraka hivyo? Huwezi kumjua sababu anakuwa ni mtu wa kawaida tu halafu wanajifanyaga wana roho nzuri balaa kumbe roho zao ni za kichawi. Kwakweli mume wangu tunatakiwa kushukuru sana uwepo wa huyu Neema humu ndani”
Kisha Sopy akamuomba mumewe waende sebleni wakapate chakula cha usiku,
“Ila najisikia kushiba sijui kama nitaweza kula”
“Sasa ungependa chakula gani kwa usiku huu?”
“Labda ningepata mkate tu na chai au maandazi tu na chai maana nimeshiba mke wangu”
“Basi twende tukanunue mkate, tuchemshe chai tunywe mume wangu”
Wakakubaliana kufanya hivyo, kisha kwa pamoja wakatoka mule chumbani.
Walipofika sebleni walimkuta Neema akiwa pale pale kwenye Tv ila alipowaona tu akawakaribisha waende mezani, Sophia akamuuliza alichoandaa
“Itakuwa vyema kama mkisogea pale wenyewe muone nilichowaandalia”
Sophia akamshika mumewe mkono na kwenda nae mezani ambapo walikuta Neema amewaandalia maandazi na chai, Sophia akatabasamu na kumwambia mumewe
“Hakuna haja tena ya kwenda dukani mume wangu kwani chakula ulichohitaji kipo tayari”
“Amejuaje kama tunahitaji chakula cha hivi muda huu?”
“Labda kwavile kaona tumekula jioni”
Kisha Sophia akamsihi mumewe akae pale mezani na waweze kula kile chakula ambapo Ibra alifanya hivyo na kukaa pale mezani halafu wakaanza kula ila Ibra alimuuliza Sophia kuwa huyo Neema amekula muda gani,
“Ngoja nimuite umuulize mwenyewe”
Sophia akamuita Neema ambaye aliwafata pale mezani na kuwasikiliza walichomuitia, Ibra akamuuliza Neema
“Mbona huji kula na sisi?”
“Mimi nimekula jikoni kwahiyo sina njaa tena”
“Usije sema tunakutenga, tafadhari siku nyingine tuwe tunakula pamoja umesikia Neema”
“Sawa msijali nimewaelewa tutakuwa tukila pamoja ila tatizo ni kuwa hamtashiba”
“Hatutashiba kivipi?”
Neema akacheka na kujibu kamavile mtu anayetania,
“sababu nakula sana”
Sophia akacheka pia na kumwambia,
“Ungekuwa unakula sana si vyakula vingekuwa vimeisha humu ndani jamani, Neema bhana tuwe tunakula pamoja ndio vizuri”
“Sawa dada nimekuelewa nitakuwa nafanya hivyo”
Kisha akarudi tena kwenye kuangalia Tv na kuwaacha Sophia na ibra wakiendelea kula.
Walipomaliza kula, Ibra akamwambia mkewe kuwa anaona vyema yeye akalale tu kwani amejawa na uchovu sana,
“Sawa mume wangu,na mimi nitakuja kulala muda sio mrefu”
Ibra akaenda chumbani kisha Sophia akaenda sebleni kukaa na Neema huku akijaribu kumuuliza kuwa ameionaje siku,
“Neema siku ya leo umeionaje na maisha ya humu ndani umeyaonaje kwa ujumla?”
“Nimeipenda na kuifurahia sana siku ya leo kwani inaonyesha wazi kuwa maisha yangu humu ndani yatakuwa ni yenye furaha”
“Na vipi ule ujio wa Yule Jane?”
“Yule hawezi kuja tena hapa, popote ninapokuwa hakuna mtu mbaya anayeweza kusogea ndiomana Yule alikimbia mwenyewe maana asingeweza kukaa na mimi karibu”
“Nafurahi kusikia hivyo maana alikuwa ananikera sana Yule binti, ngoja nikutakie usiku mwema ingawa sijui utaenda kulala saa ngapi”
“Muda sio mrefu na mimi nitaenda kulala hata usijali dada”
Sophia akaelekea chumbani ambapo alimkuta mumewe akiwa amelala hoi kabisa kisha nae akajiunga kwenye kulala pembeni ya Ibra.
Usiku wa manane Ibra alishtuka kutoka usingizini ambapo alihisi kamavile tumbo lake limevurugika hivyo akaamka na kukaa kitandani ila aliona ni vyema anywe maji hivyo akainuka na kuelekea jikoni ili akachukue maji. Ila alipofika sebleni alishangaa kumuona Neema akiangalia Tv ila kwavile mkewe alimwambia kuwa Neema anapenda sana Tv hakushangaa zaidi ila aliona ni vyema amuulize kuwa hana usingizi au imekuwaje.
Ibra akamsogelea Neema na kumuuliza,
“Vipi mpaka saizi, huna usingizi?”
Neema aliinua sura yake na kumuangalia Ibra, kwakweli Ibra hakuweza kumtazama Neema mara mbili kwani macho ya Neema yalikuwa yakiwaka moto na kumfanya Ibra apige kelele za uoga kwa mara ya kwanza katika maisha yake.
Neema aliinua sura yake na kumuangalia Ibra, kwakweli Ibra hakuweza kumtazama Neema mara mbili kwani macho ya Neema yalikuwa yakiwaka moto na kumfanya Ibra apige kelele za uoga kwa mara ya kwanza katika maisha yake. Ila kelele zile za Ibra hazikufika popote zaidi ya kuishia mule mule ndani kwani Ibra alianguka chini muda huo huo na kuwa kama mtu aliyepatwa na usingizi mzito sana.
Mtu ambaye alishtuliwa na kelele zile alikuwa ni Sophia ambaye alishtuka usingizini ila alijikuta gafla hajali kuhusu zile kelele na kumfanya ajigeuze na kulala vizuri zaidi ambapo nay eye alipatwa na usingizi mzito kushinda wa mara ya kwanza.
Alipopitiwa na ule usingizi safari hii Sophia alipatwa na ndoto ambapo alijiona mahali na mbele yake alimuona mtoto mdogo ambaye sura yake ilionekana kufanana nae sana kitu kilichomfanya Sophia amwite Yule mtoto ‘mwanangu’ ila alipojaribu kumsogelea Yule mtoto alisogezwa mbele zaidi, kisha kuna sauti ikamwambia Sophia,
“Ni kweli mtoto huyu ni mwanao ila hautaweza kumshika wala kumgusa zaidi zaidi utakuwa unamuona tu wakati umelala”
Sophia akajikuta akihoji kwenye ile ndoto peke yake,
“Kwanini nisiweze kumshika wala kumgusa wakati ni mwanangu mwenyewe?”
“Pole sana Sophia, ila hii ni zawadi yetu sisi. Tunapenda sana watoto”
Sophia alijikuta akiumizwa sana kwani kila alipoitazama sura ya Yule mtoto ilionyesha simanzi kubwa, iliyomfanya Sophia asiweze kukubaliana na ile hali kwahiyo akaanza kumfata Yule mtoto ambapo alishtuka usingizini kabla ya kumkaribia Yule mtoto na tayari palikuwa pameshakucha.
Sophia alikaa kitandani akitafakari kuhusu ile ndoto na je kwake ilikuwa na umuhimu gani, alijikuta akilishika tumbo lake na kusema,
“Uwe salama mwanangu, nakupenda sana”
Kisha akamuangalia Ibra aliyekuwa hoi na usingizi na kumfanya amuamshe kwani muda wa kujiandaa kwenda kazini ulikuwa umewadia, Ibra alishtuka sana ila alionekana kuwa na uchovu uliopitiliza, Sophia akamuuliza mumewe
“Kheee mbona umechoka sana mume wangu?”
“Dah yani hata sijielewi kwanini nimechoka hivi”
Kisha akainuka na kwenda kuoga halafu akarudi kuvaa ila kuna vitu vilionekana kumweka kwenye mawazo sana, alijikuta akijiuliza kuwa alichokiona usiku wa jana kilikuwa ni kweli au ni ndoto tu iliyompitia, akajikuta akisema kwa sauti
“Kama ilikuwa ni kweli basi nilichukua maamuzi gani? Na kama ni ndoto kwanini nilipiga kelele? Au zile kelele nazo zilikuwa ni ndoto?”
Ibra alikosa jibu ila kwavile Sophia alimsikia Ibra anachojihoji aliamua kumuuliza kuwa ni kitu gani ambapo Ibra kabla ya kujibu akamuuliza Sophia,
“Hakuna kelele zozote ulizozisikia usiku Sophy?”
“Kuna kelele nilizisikia usiku tena ilikuwa kama sauti yako hivi”
“Sasa ulipozisikia ulichukua hatua gani na mimi nilikuwa wapi kwa wakati huo?”
“Nilishtuka kutoka usingizini ila wewe nilikuona pembeni yangu ukiwa hoi na usingizi hivyo nami nikajigeuza na kuendelea kulala. Kwani ni vipi mume wangu?”
“Hakuna kitu mke wangu ila akili yangu ikiwa sawa nitaweza kueleza kile ninachofikiria kichwani”
Sophia ilibidi amkubalie tu mumewe kwani kumpinga pinga alishachoka tayari, kwavile Ibra alikuwa kashamaliza kujiandaa akamuomba tu mkewe amsindikize nje kama kawaida yao.
Ibra na Sophia walitoka hadi sebleni ambapo walimkuta Neema kisha kusalimiana nae na Ibra kuwaaga ila Neema akamuomba kitu,
“Kaka kabla hujaondoka itakuwa ni vyema ukanywa chai kwanza, leo nimeamka mapema sana ili nikuandalie chai naona unashinda na njaa kwa muda mrefu”
“Dah asante Neema ila nimechelewa muda huu”
Sophia nae ikabidi aanze kumsisistiza mumewe,
“Kwani kunywa chai inachukua muda gani Ibra jamani, si ungekunywa tu ili uwe na nguvu huko uendako jamani mume wangu!”
“Ni kweli msemayo ila naomba chai nianze kunywa kesho maana leo nimeshachelewa”
“Jamani kaka sio vizuri hivyo jamani, yani nimeandaa kwaajili yako”
“Nisamehe bure Neema”
Kisha Ibra akaenda kufungua mlango na kuondoka kwani hakutaka kuendelea kukaa hapo ili wasije kumpa vishawishi zaidi wakati tayari alikuwa na mawazo yake kichwani.
Ndani alibaki Sophia na Neema ambapo Sophia akasema ni vyema hiyo chai akanywe yeye ila Neema akamkataza na kumwambia yak wake bado hajamuandalia.
“Hakuna shaka Neema ila chai si chai tu!”
“Yeah chai ni chai tu ila kuna chai bora kwa mama mjamzito, tulia nikuandalie. Sitaki unywe hii sababu utashiba na kushindwa kunywa chai bora kwaajili yako, subiri nikuandalie dada na mwenyewe utafurahia”
Sophia hakuhoji sana kisha akaelekea chumbani kwa lengo la kuoga na kuweka chumba chao vizuri.
Ila alipokuwa chumbani alifikiria sana kwani hakuona kama kunakuwa na tofauti ikiwa kuna wajawazito wanaokunywa chai za pamoja na familia zao, akajiuliza sana kuwa kwanini Neema amemkataza kunywa ile chai ila hakupata jibu, kwa upande mwingine alihisi kuwa pengine kuna kitu ambacho Neema ameweka kumdhuru mume wake ila akajiuliza kwanini amdhuru maana hakuona kama kuna sababu yoyote kwa Neema kufanya hivyo, ikabidi apuuzie yale mawazo yake.
Alipomaliza shughuli zake alitoka na kumkuta Neema kama kawaida akiwa amekaa kuangalia Tv, ila kabla nay eye hajakaa kujumuika na Neema akamwambia kuwa asikae kwanza aende mezani kwa lengo la kunywa chai ambapo Sophia alifanya hivyo na kukuta akiwa ameandaliwa chai ya maziwa na chapati psmoja na nyama ya kurosti. Sophia alikunywa kisha akarudi kukaa sebleni na kumuuliza maswali Neema,
“Samahani Neema kuna kitu naomba nikuulize”
“Niulize tu dada hakuna tatizo”
“Hivi maziwa yamenunuliwa muda gani humu ndani? Inamaana Ibra analeta vitu bila ya kuniambia?”
“Mbona maziwa yapo mengi dada ndiomana mimi nimeyapika tena kwa afya yako ni vizuri sana ukinywa mara kwa mara”
“Swala ni kwamba yaliletwa lini? Unajua hujawahi kunidai hela ya mboga hata siku moja ila kila siku tunakula vizuri tu je hizi mboga zinatoka wapi na huyo Ibra kazileta muda gani?”
Safari hii Sophia hakujibiwa chochote ila gafla akapatwa na usingizi na kulala pale kwenye kochi kwani usingizi ule ulikuwa ni usingizi mzito sana.
Ibra alifanya shughuli zake leo huku akiwa na mawazo sana, alijikuta akiwaza mambo mbali mbali haswa lile swala la kuona macho ya Neema yakitoa moto lilimkosesha raha kwani alizidi kujiuliza kuwa ile ilikuwa ni ndoto au ni kitu gani, swala la Jane kukimbia pia lilimpa mawazo na kumfanya awahi kufunga shughuli zake siku hiyo ili aweze kwenda kwakina Jane kuzungumza nae kuhusu kilichomkimbiza kiasi kile.
Alipomaliza tu kufunga, aliingia kwenye gari yake na safari yake ilikuwa moja kwa moja kwakina Jane ambapo alimkuta Jane akiwa ametulia tu nje kwao, kisha akamuita pembeni na kusalimiana nae halafu kuanza kuzungumza kuhusu jambo lililompeleka mahali pale.
“Jane kwanza kabisa samahani kwa kilichotokea jana kwani sikutarajia kama ungekimbia kiasi kile”
“Nisamehe mimi kaka ila kwakweli sikuweza kuendelea kuwepo pale kwenu na sidhani kama nitaweza kuja tena”
“Hebu niambie kwanza kilichokukimbiza wewe ni nini, na kwanini ulishikwa na uoga kiasi kile? Na kwanini useme huwezi kuja tena pale kwetu?”
“Siwezi kuja kwasababu ya Yule mgeni wenu siwezi kabisa yani siwezi”
“Ndio uniambie kwanini?”
“Siwezi tu, nadhani damu yake na yangu haviendani”
“Hebu Jane niambie ukweli maana kwa mujibu wa Yule binti ndani ni kuwa wewe ni mchawi”
Jane akacheka kicheko cha mshangao na kusema,
“Kheee mimi mchawi! Huo uchawi niutolee wapi mimi ikiwa hata mama yangu hajui kuhusu uchawi? Mimi mwenyewe narogwa je mchawi huwa na yeye anarogwa? Hapa nilipo huwa naonekana sijielewi sababu nimesharogwa sana. Na kama amewaambia hayo maneno Yule mgeni wenu basi jueni kwamba yeye ndio mchawi na sio mtu mzuri kabisa.”
“Kwanini unasema hivyo na nipe sababu ya kukimbia kwako”
“Sikia kaka nikwambie kitu, mimi sina akili ya darasani ila nina akili ya maisha, na akili hii nimeipata kwa kuangalia maisha ya watu mbalimbali na kusoma makala mbalimbali. Mimi ni mpenzi wa kusoma hadithi za kutisha na kusisimua ila humo nimejifunza vitu vingi sana. Kuna makala mengi huwa yanaeleza kuwa unapokutana na mtu mbaya kwa mara ya kwanza basi mwili wote husisimka na nywele kusimama. Sasa mimi nilipomuona Yule mgeni wenu hiyo hali ndiyo imenikuta kwa mara ya kwanza katika maisha yangu na aliponiangalia nilihisi kutetemeka mwili mzima ndiomana sikuweza kukaa pale na kuamua kukimbia”
“Kwamaana hiyo Yule ni mtu mbaya?”
“Sijui kwa nyie mnamuonaje ila kwa mie hapana kwakweli Yule si mtu wa kawaida, sijawahi kupatwa na ile hali katika maisha yangu yani ilikuwa ndio mara ya kwanza. Nakumbuka mama alinifundisha kuwa nikikutana na kitu kibaya niondoke eneo lile huku nikiomba Mungu anisaidie maana siwezi jua kuwa kitanipata nini na ndivyo nilivyofanya”
“Bado sikuelewi Jane kwahiyo Yule ni mtu mbaya mule ndani?”
“Mmh kwani nyie mmemtoa wapi kaka?”
Ikabidi Ibra amueleze Jane jinsi yeye na mkewe walivyokutana na Neema na mpaka kumkaribisha nyumbani kwao na kuamua kuwa awe mdada wa kuwasaidia kazi za ndani.
“Mmmh kaka kweli kabisa mnamchukua mdada wa kazi ambaye hamfahamu hata nyumbani kwao je akipata matatizo mtafanyaje?”
“Kwakweli hatuna la kufanya kwani ilikuwa ni katika kumsaidia ukizingatia kasema kuwa ndugu zake hawamtaki, na sijui katokea kijiji gani huko”
“Basi kabla ya yote mlitakiwa mumpeleke kwa mjumbe ili ajue kuwa kuna mtu asiye na kwao mnaishi nae na lolote likiwapata mtakuwa salama maana mlishatoa taarifa. Maisha yanataka umakini sana, unamchukua mtu awapikie, awafulie, aangalie nyumba yenu halafu hamjui kwao mnategemea nini? Kuna mtu duniani asiye na kwao? Mngeenda kwanza kwa mjumbe”
“Ila Jane umeniambia jambo la msingi sana ambalo hata sikulifikiria kabisa, licha ya kusema ni mtu mbaya na nini na nini ila hilo swala la kwa mjumbe ni la muhimu sana ambalo nilikuwa nimelisahau kabisa yani. Asante mdogo wangu.”
“Hata usijali kaka ila mimi kuja kwenu tena hapana, ila ngoja kuna kitabu nikuletee ukakisome unaweza kuwa na mawazo mapya ya maisha”
Jane akaelekea ndani kwao na kutoka na kitabu kidogo kisha akamkabidhi Ibra, kitabu kile kiliandikwa juu yake “Fahamu kuhusu majini” Ibra akashtuka sana na kumuuliza Jane,
“Unamaana gani kunipa hiki kitabu! Hivi unajua kuwa majini ni viumbe wa ajabu sana ambao huwezi kustahimili kukutana nao! Au unamaana kuwa Neema ni jinni? Uliona wapi jini anapika, anaosha vyombo, anafua, analala uliona wapi?”
Kisha Jane akakichukua tena kile kitabu na kumwambia Ibra,
“Hiki kitabu ni tofauti kabisa na unavyokifikiria lakini najua ipo siku utakihitaji na utakisoma na kukielewa, kwa leo acha nikae nacho mwenyewe ila zingatia swala la kwenda kwa mjumbe kwanza”
Jane akamuaga Ibra na kurudi ndani kwao kwani hakutaka kuongea nae zaidi halafu alihisi kama kichwa kikimgonga hivi.
Ibra alirudi kwenye gari yake na kupanda huku akitafakari kwa muda kabla ya kuondoka pale kwakina Jane kwani lile wazo la Jane la kumshauri kuwa wampeleke Neema kwa mjumbe kwanza lilikuwa likifanya kazi katika akili yake, kisha akataka kuondoa gari yake ili aondoke ila kabla ya kuondoka kuna mdada alitoka ndani kwakina Jane na kumfata Ibra na kuanza kumgongea kwenye kioo ambapo ikampasa Ibra afungue kioo cha gari yake ili amsikilize ila Yule dada aliongea kwa kufoka,
“Umemfanya nini Jane?”
“Kumfanya nini kivipi?”
“Katoka kuongea na wewe hapa karudi ndani analalamika kuwa kichwa kinamuuma sana na analia tu”
Ibra akashangaa sana na kumfanya ashuke kwenye gari kisha kuongozana na Yule dada mpaka ndani ambapo Jane alionekana akigalagala chini huku akilalamika kuhusu maumivu ya kichwa, Ibra akatoa wazo kuwa ni vyema wakampeleka hospitali hivyo akasaidiana na Yule dada ili wamkongoje waende nae huko hospitali ili kujua kinachomsumbua Jane ni kitu gani.
Wakati wanatoka akatokea mama Jane na mmama mwingine ambao kwa pamoja walishangaa na wakaelezwa hali halisi ya Jane na kuwa wanamuwaisha hospitali ila Yule mama mwingine alisema Jane arudishwe ndani ili aweze kumfanyia maombi ambapo Ibra hakuweza kupingana nao kisha wakamrudisha Jane ndani kisha Ibra alitoka nje na kuwaacha.
Ibra akiwa nje alijiuliza maswali mengi sana kuwa wale watu wako vipi yani wanathamini sana maombi kuliko afya ya ndugu yao, akatingisha kichwa kwa kusikitika.
“Badala mtu wamuwaishe hospitali eti wenyewe wanataka wamuombee kwanza, ngoja niondoke zangu mie”
Ibra akarudi kwenye gari yake kisha akaondoka eneo lile na kuelekea nyumbani kwake.
Alipofika nyumbani kwake aliona nyumba ikiwa kimya sana kanakwamba ndani hapakuwa na mtu yeyote, kisha akaingiza gari na kufungua mlango wa sebleni ambao ulifunguka kama kawaida na kuingia ndani. Akamuona mkewe akiwa amelala hoi kwenye kiti tena alionekana hajitambui kabisa, kisha Ibra akamuuliza Neema bila hata ya salamu
“Vipi huyo kafanyaje?”
Neema alimuangalia Ibra bila ya kumjibu kitu chochote na kufanya Ibra amuulize tena,
“Neema si naongea na wewe, kafanyaje huyo?”
Safari hii Neema naye alimuuliza swali Ibra ila swali lake lilikaa kibabe sana na alionekana kujiamini kupita maelezo,
“Na wewe unataka?”
Ibra alijikuta akitetemeka kwa uoga huku akihofia kitu ambacho anaweza kufanyiwa na huyo Neema kwani alikosa ujanja gafla.
Neema alimuangalia Ibra bila ya kumjibu kitu chochote na kufanya Ibra amuulize tena,
“Neema si naongea na wewe, kafanyaje huyo?”
Safari hii Neema naye alimuuliza swali Ibra ila swali lake lilikaa kibabe sana na alionekana kujiamini kupita maelezo,
“Na wewe unataka?”
Ibra alijikuta akitetemeka kwa uoga huku akihofia kitu ambacho anaweza kufanyiwa na huyo Neema kwani alikosa ujanja gafla.
Gafla alimuona Neema akicheka kisha akasema kama kwa masikhara hivi,
“Kumbe kaka ni muoga kiasi hiki!!”
Akajichekesha zaidi ila Ibra alikuwa kimya kabisa,
“Kaka usiwe hivyo bhana mi nilikuwa nakutania tu wala sikuwa na maana yoyote mbaya. Dada leo amechoka sana na ndiomana unamuona yupo hivyo”
Ila bado Ibra aliendelea kuwa kimya kwani ilikuwa ni vigumu sana kwake kuamini zile kauli za Neema ukizingatia na yale aliyoambiwa na Jane ndio kabisa yalikuwa yakimchanganya kichwani, ila bado Neema aliendelea kujigelesha ili aonekane kuwa ni mtu mzuri kwani alishauona wasiwasi wa Ibra.
“Kaka jamani usiwe hivyo, ngoja nimuamshe na dada”
Neema alimsogelea Sophia pale alipolala na kumtingisha kidogo ambapo Sophia alishtuka sana tena huku akihema juu juu na kumfanya Ibra ashtuke na kumsogelea mke wake huku akimuuliza kuwa tatizo ni nini, Sophia aliwatazama Ibra na Neema kwa muda kidogo ndipo alipowajibu sasa,
“Nimepatwa na ndoto mbaya sana”
“Pole Sophy, ni ndoto gani hiyo?”
“Nimeotwa nakimbizwa na watu wa ajabu sana, yani walikuwa wanataka kunikamata kabisa. Walipokuwa wananikaribia ndio mmenishtua.”
“Duh pole mke wangu”
Kisha Neema nae akaingilia kati na kuanza kuwaambia tafsiri za ndoto,
“Ndoto ya kukimbizwa sio ndoto mbaya kabisa, nilipokuwa mdogo bibi aliniambia kuwa mtu anapoota anakimbizwa ajue kuwa watu wanamuhimiza kwaajili ya maendeleo yake, na vile anavyokimbia ndio anavyokimbilia maendeleo yake. Kwahiyo ikiwa hadi umeamka wale watu hawajakushika basi ujue kuna maendeleo makubwa sana yanakuja mbele yako”
“Mmmh ndoto ya kukimbizwa ndio inamaana hiyo?”
“Ndio maana yake hiyo kwahiyo hata usiwe na mashaka kwa hiyo ndoto. Halafu kikubwa ni kuwa muende mezani mkajipatie chakula kwani najua wote mmeshachoka tayari”
Ibra sasa ndio akaongea na Neema kwa kumjibu muda huu,
“Asante Neema ila ngoja kwanza tukajimwagie maji ndio tuweze kula vizuri”
Kisha Ibra akamshika mkono mkewe Sophia na kumuomba waende chumbani ambapo Sophia alifanya hivyo.
Walipofika chumbani, kitu cha kwanza kabisa ambacho Ibra alimuuliza Sophia ni kuwa alilala muda gani,
“Unafikiri nakumbuka basi muda niliolala! Hata sikumbuki mume wangu na hata sijui imekuwaje nadhani ni sababu yah ii mimba”
“Itakuwa ni kweli maana mimba nazo zina mambo sana, pole mke wangu ila kuna jambo napenda tuzungumze kidogo”
“Jambo gani hilo tena?”
Ibra aliamua kumueleza Sophia kuhusu kumpeleka Neema kwa mjumbe na umuhimu wa wao kufanya hivyo,
“Mmh umezungumza jambo jema sana mume wangu, kwakweli kuna umuhimu mkubwa wa kufanya hivyo maana akipata matatizo huyu tutakimbilia wapi? Hata sijui kwanini hatukuwa na wazo hilo tokea mwanzo”
“Nadhani kwasababu ya kutingwa na mambo, ila nashukuru kwa kunielewa mke wangu maana sikujua kama ingekuwa rahisi hivi kwa wewe kunielewa.”
Sehemu Ya 5
“Ni vichache ambavyo sielewi ila sio kwa jambo la msingi kama hilo, duniani majanga ni mengi na mtu hujui la mbele bora kutoa taarifa mapema.”
“kwahiyo sasa twende nae lini kwa mjumbe?”
“Linalowezekana leo lisingoje kesho mume wangu bora kwenda nae leo leo”
“Kama leo basi inabidi tuwahi maana nilisikia kuwa mjumbe wa mtaa huu ni mtu wa dini dini sana bora tumuwahi mapema kabla hajaenda kwenye ibada zake”
“Hakuna tatizo, twende basi tukaongee na Neema ili twende naye kwa huyo mjumbe”
Wakakubaliana kwa pamoja kisha kutoka sebleni ambapo leo Neema hakuwa pale sebleni na wakajua wazi kuwa kaenda chumbani kwake na wakaamua kumuita, walipomuita tu Neema aliitika na kwenda pale walipo kisha akakaa kwenye kochi na kuanza kuwasikiliza walichomuitia ambapo Sophia aliamua kuanza kumueleza.
“Neema tumeishi na wewe hapa kwa siku mbili tatu na kwakweli tumependa sana uwepo wako hapa ila kuna jambo moja tulilisahau kabla ya kukukaribisha hapa nyumbani”
“Jambo gani hilo?”
“Neema, unajua sisi ni binadamu na hatujui ya leo wala ya kesho sasa tunapaswa twende na wewe kwa mjumbe ili atambue uwepo wako mahali hapa maana sisi hatuwafahamu hata ndugu zako, mwisho wa siku usije ukapata matatizo bure halafu tukashindwa kujieleza kwa jamii”
Neema akacheka kidogo kisha akawauliza,
“Kwahiyo mnataka mnipeleke mimi kwa mjumbe?”
“Ndio Neema”
“Kwani mkinipeleka kwa huyo mjumbe ndio anaweza kufanya nisipatwe na matatizo?”
“Hapana sio hivyo ila inakuwa vizuri hata ukipatwa na tatizo tunajua wapi pa kuanzia”
“Ila mimi si nilishawaambia kuwa ndugu zangu hawanitaki kwahiyo ni sawa na kusema kuwa sina ndugu kabisa, sasa mnataka nikifika kwa mjumbe nikajieleze tena kuwa nimekataliwa?”
“Neema naomba utuelewe kidogo, Yule mjumbe hautamueleza yote hayo. Tunachotaka sisi atambue ni kuwa tunaishi na wewe humu ndani, ni kweli ndugu zako walikukataa ila kwetu umekuwa kama ndugu tayari kwa hizi siku chache tulizoishi pamoja. Tunahitaji kuishi na wewe kihalali”
“Ila bado sioni sababu ya nyie kunipeleka mie kwa mjumbe, ingekuwa vyema kama mngenipeleka pale mwanzoni ila kwasasa hapana”
Ibra na Sophia wakatazamana kwa muda kisha Ibra akamuuliza Neema kwa ukali kidogo,
“Kwani Neema una nini hadi hutaki kwenda kwa mjumbe?”
“Kwani wewe unaniona mimi nina nini?”
“Hivi unajua kama hapa ni nyumbani kwangu na mimi ndiye mtu pekee mwenye mamlaka na nyumba hii! Unatambua hilo kweli?”
Neema akacheka kwa dharau, kitendo hicho kilimchukiza sana Ibra na kujiuliza kuwa kwanini huyu neema anajiamini kiasi kile kwenye nyumba yake mwenyewe, kisha akamwambia tena kwa hasira
“Unataka kwa mjumbe utaenda, hutaki kwa mjumbe utaenda. Hii ni nyumba yangu siwezi kupangiwa cha kufanya na mgeni kwahiyo kwa pamoja sasa tunaenda kwa mjumbe”
“Unaniamuru hivyo kwa mamlaka ya nani?”
Sophia pia akamshangaa huyu Neema na kumuuliza,
“Kheee hivi ndio wewe Neema tuliyekukuta njiani ukilia kuwa una matatizo? Ni wewe kweli? Mmmh hapana, umekuwaje leo?”
“Ni mimi mwenyewe na hivi ndivyo nilivyo, sipendi kuendeshwa kwa lolote wala chochote”
Ibra alizidi kupatwa na hasira sana na kuzidi kumuuliza Neema kwa hasira,
“Wewe Neema unajiamini hivyo kama nani humu ndani? Unapata wapi kiburi cha kujiamini kiasi hiko?”
Kisha akamuangalia Sophia na kumwambia,
“Mke wangu, umeona sasa madhara ya kuokota okota haya, yani tumeenda kuokota na visivyookoteka”
Neema akawaangalia kisha akawaambia,
“Msijali, ngojeni nikajiandae twende huko kwa mjumbe”
Kisha akaondoka pale na kuelekea kwenye chumba chake.
Sophia na ibra walimsubiri pale seblani ili atoke na waanze kuelekea huko kwa mjumbe, muda kidogo Neema alitoka akiwa vile vile hata wakamshangaa kuwa alichokwenda kujiandaa kilikuwa ni kitu gani, kisha akawaambia kuwa waende huko kwa mjumbe. Walitoka kwa pamoja hadi nje ambapo Ibra alielekea kwenye gari yake ili wapande waende ila Neema aliwauliza
“Kwani huko kwa mjumbe ni mbali?”
“Hapana sio mbali sana”
“Basi hakuna sababu ya kupanda gari, twendeni tu kwa mguu”
Nao wakaafikiana nae kisha wakatoka nje kwa pamoja na kuanza kutembea wakielekea huko kwa mjumbe ila walikuwa kimya kabisa njia nzima kwani hakuna aliyemuongelesha mwenzie.
Walitembea kwa muda mrefu sana bila ya kufika kwa huyo mjumbe hadi Sophia akaamua kumuuliza mumewe sasa maana yeye ndio alikuwa akipajua nyumbani kwa mjumbe
“Khee mbona hatufiki kumbe ni mbali hivi?”
“Hata mimi mwenyewe nashangaa kuwa kwanini hatufiki na wala hata sio mbali, sijui tumekosea njia maana sielewi kabisa”
Neema alikuwa kimya kabisa, walizidi kutembea hata giza liliwakutia njiani wakiwa hawajafika kwa mjumbe wala nini na kufanya Ibra afikirie kuhusu gari yake kuwa ni bora hata wangekuja na gari maana walishachoka tayari.
Baada ya mwendo mrefu na giza kuingia sana wakaona vyema warudi nyumbani kwao kwani walichoka vya kutosha na miguu ilianza kuwauma kwa uchovu, Ibra alimuangalia mkewe na kumuomba msamaha kwa kumtembeza kiasi kile
“Nisamehe mke wangu kwa kukutembeza hivi, hata sijui imekuwaje tumepotea njia”
“Na huko nyumbani tunarudije sasa?”
Wakatazamana tu kwani kiukweli walikuwa wamepotea njia na hata ya kurudia hawakuikumbuka tena. Sophia akamuangalia Neema na kumwambia,
“Tusaidiane mawazo Neema jinsi ya kurudi nyumbani maana tumeshapotea”
“Ndiomana mimi nilikataa hayo maswala ya kwa mjumbe ona sasa kilichotupata yani tumechoka balaa hata mimi mwenyewe sikumbuki njia”
Ibra hakuwa na la kusema zaidi ya kukazana kuwaomba msamaha kwani alijiona yeye kuwa ndio chanzo cha kuwatembeza wenzie kiasi kile, kisha akamuangalia Neema na kumwambia
“Neema samahani maana ningekusikiliza tangu mwanzo basi saizi tungekuwa nyumbani. Tusaidiane tuweze kurudi nyumbani maana ni usiku sana sasa hivi na hatufiki kwa mjumbe wala nyumbani hatufiki, tusaidiane jamani”
Neema akainama kama mtu aliyechoka sana kisha akaanza kucheka huku wao wakimshangaa kinachomchekesha ila wakati wanamshangaa wakajikuta gafla wakiwa nyumbani tena ndani sebleni.
Kila mmoja alimuangalia mwenzie kwani ilikuwa kama ni maajabu hivi kuwa wamewezaje kurudi hapo, ila miguu yao ilikuwa imejaa vumbi balaa na walikuwa wamechoka sana. Ibra akatazama miguu ya Neema haikuonekana kuwa na vumbi kabisa kanakwamba ni mtu ambaye hajatoka hata nje kwa siku hiyo, kwakweli kati ya Ibra na Sophy hakuna aliyeweza kusema chochote kisha wakaamua kwenda chumbani kwao kuoga ambapo walichukua muda mfupi tu kuoga na kutoka bafuni huku kila mmoja akitafakari kivyake. Ila Ibra aliamua kumuuliza mkewe
“Hivi hiki kilichotokea umeelewa kweli mke wangu?”
“Mmh mpaka saa hizi sielewi, hivi tumewezaje kurudi humu ndani”
“Je unakumbuka mara ya mwisho ilikuwaje?”
“Nakumbuka ndio, mara ya mwisho Neema alikuwa ameinama akicheka na sisi tulikuwa tukimshangaa”
“Je unahisi huyu Neema ni binadamu wa kawaida kweli?”
Sophia akasita kidogo kujibu kisha na yeye akamuuliza mume wake,
“Unamaana gani Ibra?”
“Aah wewe niambie tu kwa mawazo yako kuwa je umuonavyo Neema ni mtu wa kawaida kweli?”
“Kama sio mtu wa kawaida je atakuwa ni mtu wa aina gani?”
“Mimi sielewi ila huyu Neema ananipa mashaka sana”
“Sasa tutafanyaje mume wangu?”
“Wazo langu ni kuwa tumtimue”
“Mmh mume wangu, tukimtimua ataenda wapi?”
“Kwani wewe anakuhusu nini huyu? Je ni ndugu yako? Tumtimue bhana kuliko kuongeza balaa ndani tena tumtimue leo leo”
“Usiku huu mume wangu!”
“Kwani usiku kitu gani, waswahili husema heri nusu shari kuliko shari kamili. Huyu tumtimue tu kwani nahisi ni mchawi mkubwa sana”
“Kheee mi sijui kama nitaweza hilo mume wangu maana kuna muda huruma inanijaa juu yake”
“Utajijua na huruma zako maana kila siku zinatuletea mabalaa tu katika maisha haya, ngoja mi nikafanye ninavyojisikia”
“Ila Ibra kwanini tusingesubiri hadi kesho?”
“Kesho mbali bhana, linalowezekana leo lisingoje kesho”
“Haya baba maamuzi ni yako ila mimi namuonea huruma sana”
Ibra hakutaka kupoteza muda katika kujadiliana na mke wake kwani anamtambua ni jinsi gani huwa anaponzwa na huruma yake ambayo badae hugeuka majuto kwani hadi huyo Neema kukaribishwa hapo kwao ni kutokana na huruma ya mkewe.
Ibra akaamua kwenda kufanya kile ambacho roho yake inamwambia.
Akatoka hadi sebleni ambapo aliangaza macho yake huku na kule ili kumuona Neema ila hakumuona na kumfanya ashangae kwani kawaida ya Neema ni kukaa pale sebleni akiangalia Tv, Ibra alipotazama Tv aliikuta ikiwaka na kuona kuwa ile ni sababu tosha ya kumtimua Neema kuwa anaachaje Tv inawaka wakati yeye hayupo pale sebleni.
Ibra akasogea sasa karibu, alipotazama kwenye kochi alishtuka sana baada ya kuona kuna nyoka amekaa juu ya kochi akiwa amejiviringisha na kichwa amekiinua juu.
Akatoka hadi sebleni ambapo aliangaza macho yake huku na kule ili kumuona Neema ila hakumuona na kumfanya ashangae kwani kawaida ya Neema ni kukaa pale sebleni akiangalia Tv, Ibra alipotazama Tv aliikuta ikiwaka na kuona kuwa ile ni sababu tosha ya kumtimua Neema kuwa anaachaje Tv inawaka wakati yeye hayupo pale sebleni.
Ibra akasogea sasa karibu, alipotazama kwenye kochi alishtuka sana baada ya kuona kuna nyoka amekaa juu ya kochi akiwa amejiviringisha na kichwa amekiinua juu.
Kwakweli Ibra aliishiwa na ujasiri gafla na kujikuta akipiga kelele kwani hakujua afanye kitu gani kwa muda huo, kelele za Ibra zilimshtua Sophy na kumfanya atoke mbio ili ajue kuwa mumewe amepatwa na nini ila nae alipofika pale sebleni alipatwa na uoga wa hali ya juu baada ya kumuona Yule nyoka kwenye kochi na kujikuta akimkumbatia mumewe kwa nguvu huku akiita jina la Neema kanakwamba wanamuhitaji Neema aweze kuwasaidia.
Muda kidogo Neema alitokea na moja kwa moja akamuamuru Yule nyoka atoke nje, kisha akaenda kufungua mlango ambapo Yule nyoka alijitoa pale kwenye kochi na kutoka nje kidsha Neema akafunga mlango na kuwatazama Ibra na Sophia ambao walikuwa kimya kabisa kwani walikuwa wakitetemeka kwa uoga.
Kisha Neema akawaambia kwa kujiamini
“Njooni mkae tuzungumze”
Sophia akadakia,
“Hapana Neema, labda utueleze kwanza Yule nyoka katokea wapi?”
Neema akacheka na kuwaambia,
“Yule sio nyoka ni mtu”
Wote wawili wakashangaa kuwa ni mtu kivipi, kisha Neema akaendelea kuwaeleza,
“Yule ni Jane”
Sophia na Ibra wakashtuka sana kwani hawakutegemea kabisa kuwa Yule nyoka anaweza kuwa Jane, kwahiyo wakauliza
“Ni Jane kivipi?”
“Yote kayataka huyu kaka Ibra, aliyekutuma leo uende kwakina Jane ni nani? Na huyu nyoka alikuja kwa lengo la kuwadhuruu, mshukuru sana uwepo wangu.”
Ibra akashangaa kiasi kuwa huyu Neema amejuaje kuwa yeye alienda kwakina Jane na iweje Jane ajigeuze nyoka wakati alishasema kuwa huyu Neema si mtu mzuri, akajikuta akikosa swali wala jibu. Ni Sophia pekee aliyeweza kuuliza zaidi,
“Inamaana hatorudi tena?”
“Hawezi kurudi kwasababu mimi nipo”
Kisha Ibra akamshika mkewe na kurudi nae chumbani huku akiwa na mawazo lukuki.
Wakiwa chumbani Sophia aliamua kumuuliza Ibra,
“Mume wangu huko kwakina Jane ulienda muda gani? Ni nani aliyekushauri uende huko jamani! Mbona unapenda kutafuta matatizo Ibra? Hivi uambiwe na nani kuwa Jane sio mtu mzuri ndio uamini jamani mmh!”
Ibra alikuwa kimya kwanza kwani bado kuna mambo mengi sana yalikuwa yakizunguka akili yake haswa kuhusu huyu Neema na Jane je ni nani wa ukweli kati yao? Ila kwa upande mwingine alimuamini zaidi Jane kuliko Neema, kisha akapanda kitandani na kulala bila ya kuongea ya zaidi na mkewe, hivyo akamfanya Sophia nae apande kitandani na kulala pia.
Wakiwa wamelala, Ibra akajiwa na ndoto ambapo kwenye ndoto ile alikuwa akiona vitu ambavyo vipo kwenye nyumba yao, kwanza kabisa alijiona yupo ndani na kutoka sebleni ambapo akamuona Neema mmoja akiwa jikoni na Neema mwingine akiwa sebleni na gafla Yule Neema wa sebleni akageuka na kuwa nyoka kisha Neema wa jikoni akatoka na kumfukuza Yule nyoka halafu akamuangalia Ibra na kutabasamu kisha akamwambia,
“Mimi ndio Neema, kunikwepa huwezi…….”
Ibra akashtuka kutoka usingizini huku akihema ila akaisikia sauti ya Neema ikiendelea kuongea,
“Na kunifukuza pia huwezi, nimejipa jina hili kwa makusudi kwani huwezi ukaniepuka kamwe”
Kisha akasikia kicheko cha Neema ambapo Ibra akajawa na hofu sana huku akimuamsha mkewe ili nae aweze kusikia ila Sophia alipoamaka hakusikia chochote kwani hata ile sauti ya kicheko haikuendelea tena, Sophia akamuuliza mume wake
“Tatizo ni nini mume wangu jamani?”
“Sophia mke wangu haya ni majanga”
“Majanga! Majanga kivipi?”
“Nimeota ndoto mbaya sana ila yenye uhalisia ndani yake”
“Uhalisia kivipi na ni ndoto gani?”
“Sophia mke wangu, sijielewi sijielewi kabisa. Hebu angalia saa hapajakucha kweli?”
Sophia akaangalia muda na kumwambia mumewe,
“Ni saa nane kamili mume wangu”
“Dah muda hata hauendi pakuche jamani, mimi hata sijui kama nitaweza kulala tena, nitakaa macho tu”
“Hapana usikae macho tulale, hizo ni ndoto tu. Hivi unakumbuka kipindi kile mimi nilipokuwa nikiota ota ulikuwa unaniambiaje Ibra? Basi jua kwamba hizo ni ndoto tu hata zisikupe mawazo tulale mume wangu”
“Tatizo huelewi kuhusu hizi ndoto mke wangu”
“Hata wewe ulikuwa huelewi pia kuhusu ndoto nilizokuwa naota mimi ila napenda kukwambia tena mume wangu kuwa hizo ni ndoto tu zisikutishe”
Sophia alijitahidi kumshawishi mumewe ili waendelee kulala ambapo Ibra nae alijitahidi aweze kulala ila usingizi ulimpiga chenga kwa muda huo.
Kulipokucha kama kawaida, Ibra aliamka na kwenda bafuni kuoga ila kila alipokuwa akioga na kufumba macho aliona sura ya Neema na kumfanya apate hofu kama aliyoipata majuzi yake hivyo akatoka bafuni kwa haraka sana na kumuamsha mkewe ili angalau avae huku akizungumza na mke wake.
Sophia aliamka na kumtazama mume wake ambaye alionekana hata kuoga hakuoga vizuri siku hiyo,
“Ila oga yako siku hizi mume wangu majanga tupu, unatoka na povu jamani”
“Sophia naamini kuna muda utanielewa tu mke wangu”
“Kunieleza hutaki sasa sijui nitakuelewaje”
“Nitakueleza tu hata usijali”
Sophia akamuangalia mume wake kwa makini sana ila hakuweza kumwambia zaidi kwani alijua ni wazi hapendi kuulizwa sana kitu ambacho alisema atamueleza. Kisha Ibra akamwambia Sophia kuwa amsindikize nje kwani ndio alikuwa akienda kwenye shughuli zake ambapo Sophia alifanya hivyo na walipofika sebleni tu ikawa kama jana kuwa Neema alishaandaa chai ili Ibra anywe na akamuomba afanye hivyo kabla ya kuondoka,
“Hapana Neema nimeshachelewa”
“Unajua hata usiku hujala kaka!”
“Naelewa ila hata usijali”
Kisha Ibra akatoka nje na kufuatiwa na mkewe ambaye alitoka nae hadi nje kabisa akimwambia asubiri alitoe gari kwanza, na alipolitoa gari tu alimwambia mkewe apande ili azungumze nae kidogo ambapo Sophia alifanya hivyo,
“Sophy mke wangu, mimi naenda kwenye shughuli zangu ila tu nakuomba kuwa makini sana na huyu Neema, kuwa nae makini kwenye kila kitu kuanzia chakula anachokupikia yani kila kitu. Nakupenda mke wangu, kuna mengi tu nahitaji kuyafatilia kwa undani kuhusu huyu mtu humu ndani”
Kisha akamuaga mke wake na kumbusu kwenye paji la uso, ambapo Sophia akashuka kwenye ile gari halafu yeye akaondoka zake.
Sophia alirudi ndani na kumkuta Neema akiwa kimya pale sebleni ambapo jambo la kwanza kabisa Neema akamuuliza Sophia alichokuwa akizungumza na Ibra,
“Mmh Neema ni mambo ya kawaida tu ya kifamilia”
“Ila hata mimi ni mmoja ya wanafamilia yenu kwahiyo natakiwa kujua vyote vinavyoendelea humu ndani, natakiwa kufahamu kila kitu”
“Hakuna tatizo ila utafahamu taratibu”
“Napenda kuwekwa wazi na kila kinachoendelea hapa ndani, haijalishi amekwambia kuhusu nini ila unapaswa kunieleza”
Kwavile Neema alionekana kumng’ang’ania Sophia amueleze ikamfanya Sophia aamue kuwa kumweleza ukweli vile ambavyo amezungumza na mumewe kwenye gari, Sophia alipomaliza tu kumueleza alishangaa Neema akicheka na kusema,
“Nimefurahi sana kuona Sophia unasema ukweli, basi nakuahidi kuendelea kushirikiana na wewe bega kwa bega na wala usiwe na hofu juu yangu kama unavyoambiwa na mumeo. Tafadhari yapuuzie maneno yake, kinachomsumbua zaidi ni kuwa anafika kwakina Jane na wanamuharibu kisaikolojia”
Sophia akatabasamu tu ingawa kiukweli hakupenda kumwambia Neema kile alichozungumza na mumewe ila ndio hivyo alikuwa ameshamwambia.
Ibra akiwa katika shughuli zake, kuna rafiki yake alipita na kujikuta akizungumza nae mawili matatu kwani hawakuonana kwa kipindi kirefu sana. Pia rafiki yake alimdokeza kuhusu biashara mpya ambayo inaingiza sana faida na kumfanya Ibra atamani kuhusu biashara hiyo kwani alipenda sana kujaribu vitu kwaajili ya kujiongeze kipato tena ukizingatia kuna mambo mengi yaliingia katikati na kufanya pesa yake iyumbe kwahiyo alifurahi sana kuonana na huyo rafiki yake na kuelezewa kuhusu hiyo biashara.
Rafiki huyu wa Ibra alitamani sana kupafahamu nyumbani kwa rafiki yakekwanza kwani toka amehamia huko hakuwahi kufika,
“Utapafahamu tu Lazaro hata usijali”
“Tena ikiwezekana iwe leo ndugu yangu si unajua duniani hapa mambo mengi sana!”
“Yeah naelewa, basi tutapita mara moja upafahamu kisha twende huko kwenye biashara unayosema.”
“Sawa hakuna tatizo na kwa hakika hii biashara utaipenda sana ndugu yangu”
Wakakubaliana na kuondoka mahali hapo wakielekea nyumbani kwa Ibra kwanza kisha waende kwenye hiyo biashara ambayo Ibra aangalie inavyokwenda na kama ataweza kuifanya na kuendelea kujiongezea kipato.
Walipofika nyumbani kwa Ibra kwakweli Lazaro alishangaa sana ile nyumba ya rafiki yake kuwa kapata wapi pesa ya kuweza kumiliki nyumba yote ile,
“Mjini mipango Lazaro”
“Kweli mjini mipango yani kwa stahili hii mmh! Nimeshangaa kwakweli maana sio kawaida kabisa. Nakumbuka nilikuwa na uwezo kukuzidi ila nyumba yangu mimi ni ya kawaida tu ila mwenzangu upo kwenye mjengo wa maana. Hongera sana kaka”
“Nashukuru ndugu yangu, karibu sana”
Walishuka kwenye gari na kisha Ibra akafungua mlango wa ndani na kumkaribisha Lazaro ndani ambapo walimkuta Sophia na Neema wakiwa sebleni wamekaa kama kawaida, Ibra akawasalimia ila Lazaro alimsalimia Sophia tu ambapo Ibra akamshtua kuwa huyu mwingine hajamuona ila Lazaro akahamaki tu,
“Yupi huyo?”
“Inamaana humuoni hapo?”
Ibra alimuonyesha alipo Neema ila Lazaro bado hakuonyesha kama amemuona mtu yeyote eneo hilo na alikuwa akimshangaa tu Ibra huku akimwambia,
“Hebu acha masikhara Ibra unataka nimsalimie nani tena wakati nimemuona shemeji tu”
Sophia akamaliza mjadala kwa kuwakarabisha wakae, ila bado ibra hakulizishwa na hali ile na kufanya ajaribu kumuuliza kitu Neema aone kama kweli Lazaro hajamuona huyu Neema.
“Neema hujamuona huyu mgeni na wewe?”
Neema akamtazama tu Ibra bila ya kumjibu chochote huku maongezi mengine yakiendelea pale sebleni ambapo Lazaro aliwalalamikia kuwa nyumba yao inaonekana kuwa ni nzito sana,
“Hii nyumba ni nzuri ila ni nzito sana”
“Nzito kivipi?”
“Mnatakiwa mtafute watu wa maombi ili muifanyie maombi nyumba yenu ikae sawa”
Sophia akaguna na kuuliza,
“Mmh maombi tena?”
“Ndio maombi ni muhimu sana maana naona nyumba yenu ni nzito jamani”
Ibra akamtazama mkewe kisha akamtazama Neema ambaye alionekana yupo makini sana kutazama Tv, kisha Ibra akamuuliza Neema
“Unasikia kinachoongelewa huku?”
Neema alikuwa kimya tu na alimuangalia kisha akaendelea kuangalia Tv, Ibra akachukia sana na kumfanya ainuke na kwenda kuzima Tv moja kwa moja kwenye soketi ya kuingiza umeme kisha akarudi tena kukaa.
Ila Lazaro nae aliaga na kumuomba aende nyumbani kwake, Ibra akamuuliza kuhusu wao kwenda kule kwenye biashara.
“Sitaweza kwenda tena maana hapa nilipo kichwa kimeanza kunigonga naomba niondoke tu”
Lazaro akainuka na kufanya Ibra nae ainuke ili amsindikize, walipotoka nje Lazaro alionekana kuwa na kizunguzungu kikali sana ambapo ilibidi Ibra ampakie kwenye gari yake na kuitoa nje kabisa huku akitaka kumpeleka hospitali ila Lazaro aligoma na kuhitaji kurudishwa tu nyumbani kwake ambapo ikabidi Ibra afanye hivyo.
Sophia alibaki ndani na Neema huku akijiuliza kimoyomoyo kuwa kwanini Neema alikuwa hamjibu chochote Ibra halafu bado alionekana kimya kabisa ingawa Tv ilikuwa imezimwa na Ibra kwa hasira.
Sophia aliamua kumuongelesha yeye sasa ili aone kama atajibiwa kitu chochote,
“Neema mbona kimya sana mdogo wangu?”
Neema alikuwa kimya tu hakujibu chochote kile na kumfanya Sophia azidi kumshangaa kwani haikuwa kawaida kabisa kwa Neema kufanya hivyo. Sophia akainuka pale alipokaa na kusogea alipo Neema ili kumshtua kwa kumshika kabisa, ila aliposegea ili amguse gafla akashangaa kuwa pale hapakuwa na mtu yoyote yani Neema hakuonekana gafla.
Kwakweli Sophia alipigwa na butwaa kwani muda wote alikuwa akimuona Neema mahali hapo halafu tena gafla Neema ametoweka, alijikuta akitetemeka tu na kuwa kama mtu asiyejielewa.
Neema alikuwa kimya tu hakujibu chochote kile na kumfanya Sophia azidi kumshangaa kwani haikuwa kawaida kabisa kwa Neema kufanya hivyo. Sophia akainuka pale alipokaa na kusogea alipo Neema ili kumshtua kwa kumshika kabisa, ila aliposegea ili amguse gafla akashangaa kuwa pale hapakuwa na mtu yoyote yani Neema hakuonekana gafla.
Kwakweli Sophia alipigwa na butwaa kwani muda wote alikuwa akimuona Neema mahali hapo halafu tena gafla Neema ametoweka, alijikuta akitetemeka tu na kuwa kama mtu asiyejielewa.
Akiwa anajitetemekea pale mara akamuona Neema akitoka chumbani na kuja pale sebleni na ndio hapo uoga ulipomzidia na kujukuta akishindwa kustahimili na kuanguka chini na kuzimia.
Sophia akiwa amezimia alijiona sehemu ya mbali sana, alijiona mahali akiwa amekaa mwenyewe halafu mbele yake aliwaona watoto watatu wakimuangalia kwa huruma sana na kumfanya nay eye apatwe na huruma kisha akainuka pale alipokuwepo na kuanza kuwafata ila kila alipowasogelea nao walizidi kwenda nyumba kisha akajikuta akisogea na kusogea bila ya kuwafikia na kumfanya sura yake ikiingiwa na simanzi zaidi.
Muda kidogo akajikuta ameshtuka na kujiona yupo sebleni kwenye kiti huku pembeni yake akiwepo Neema ambaye alimpa pole baada ya kushtuka, kisha Sophia akamuuliza Neema kuwa ni kitu gani kilitokea
“Sijui ni kitu gani dada ila ulianguka gafla tu”
Sophia alijaribu kuvuta kumbukumbu nyuma ili kuweza kukumbuka kilichomtokea ila hakuweza kukumbuka kitu chochote kile, alijikuta akiangaza tu macho yake huku na kule ila Neema alimuomba anyanyuke na aende kula chakula cha mchana ili kupata nguvu kwavile alikuwa hajala chochote toka alivyokula asubuhi.
Sophia akainuka na kwenda moja kwa moja mezani kula chakula alichoandaliwa na Neema na kuanza kula chakula kile.
Ibra alimrudisha Lazaro hadi nyumbani kwake ambapo walipokelewa na mke wa Lazaro kisha Lazaro akamuomba mkewe amfanyie maombi maana hali yake haikuwa sawa, mke wa Lazaro hakujifikiria mara mbili na moja kwa moja alianza maombi.
Ibra alikuwa kimya kabisa akiwatizama huku yale maombi yakiendelea mpaka kuna muda ambao Lazaro alidai kuwa anajihisi nafuu sasa na anaweza kuzungumza, kisha akamuangalia rafiki yake na kumwambia,
“Ibra pendelea kufanya maombi kwenye nyumba yako”
“Maombi gani ambayo napaswa kuyafanya? Maana mimi sijazoea hayo mambo kwakweli”
“Hivi unajuu ukuu wa Mungu Ibra? Nyumba yako imetawaliwa na mambo mabaya, sio kwamba nakuonea wivu hapana ila kuna vitu nimevihisi kwenye nyumba yako”
Ibra akafikiria kidogo na kumuuliza rafiki yake huyu,
“Hivi wakati naongea na Yule Neema mbona ulikuwa hunisikilizi?”
“Mimi sijamuona huyo Neema ndani kwenu na wala sijakusikia kama kuna muda umeongea nae zaidi ya kuning’ang’aniza nimsalimie mtu nisimuona”
Mke wa Lazaro alisikia yale maongezi na kutamani kujua zaidi kuhusu huyo mtu ambapo Ibra aliamua kuwaeleza kwa kifupi jinsi walivyokutana na Yule Neema hadi kwenda nae nyumbani kwake, ila mke wa Lazaro nae alimuuliza kama kuna taratibu zozote alizofanya ili kumtambulisha huyo Neema kwa mjumbe na kuwafanya wawe huru nae nyumbani kwao,
“Yani hapo ndio kwenye tatizo, Yule Neema hataki kabisa twende nae kwa mjumbe yani kashatugomea kabisa kasema tungetaka kumpeleka kwa mjumbe basi tungeenda nae toka mwanzoni”
“Mmh shemeji poleni sana, lakini katika maisha hakuna kitu kibaya kama kuishi na mtu usiyemfahamu maana huwezi jua hi mtu wa aina gani na ndiomana kuna utaratibu ili kitakachokupata chochote au kumpata huyo binti watu watajua ni jinsi gani wanakusaidia. Kusaidia mtu njiani sio tatizo ila tatizo ni kutofata taratibu”
“Basi labda kama mtaweza shemeji mje siku moja nyumbani kwangu na kunisaidia kumshawishi Yule binti niweze kwenda nae kwa mjumbe maana mie amenikatalia kabisa na nimeshindwa hata kufanya hivyo”
Mke wa Lazaro alimkubalia Ibra ila Lazaro aligoma kwenda tena nyumbani kwa Ibra,
“Ndugu yangu tafadhali nisamehe bure tu ila sitaweza kuja tena nyumbani kwako, kama nilivyokwambia tafuta watu wa maombi kwanza”
“Usijali, mimi nitaenda, siku ukipata muda shemeji njoo unifate niende huko kwako”
“Sawa mke wangu ila ile nyumba inahitaji uwe na umakini wa hali ya juu”
Wakakubaliana pale kisha Ibra akaaga na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwake huku akiwa na mawazo sana kwani hakuelewa kuwa nyumba yake imekumbwa na kitu gani hadi kushauriwa na watu juu ya maombi. Kwanza kabisa alikumbuka maneno ya Jane kisha akakumbuka alichoambiwa na Lazaro pamoja na mke wa Lazaro kwakweli akili yake ilikuwa ikitembea bila ya majibu yoyote yale hadi alipofika nyumbani kwake bado alikuwa na mawazo.
Ibra aliingia ndani na kumkuta Neema akiwa pale sebleni ambapo alimsalimia kisha akamuuliza alipo mke wake,
“Yupo chumbani kalala”
“Mbona kalala mapema sana”
“Labda ni uchovu tu”
“Sawa, ila Neema mbona muda ule wakati yupo mgeni nilipokuwa nikikuuliza kitu ulikaa kimya tu?”
Neema akamuangalia Ibra na kutabasamu hivyo akafanya Ibra azidi kupatwa na maswali mbalimbali kisha akamuuliza tena,
“Mbona unatabasamu?”
“Yule rafiki yako hawezi kurudi tena hapa”
“Kwanini?”
“Sio mtu mzuri Yule na amekuonea wivu sana wewe kumiliki nyumba kama hii kwani hata yeye ametamani ingekuwa yake”
“Kwahiyo ndio ulishindwa kunijibu sababu ananionea wivu?”
“Huwa sipendi kuongea na watu wabaya, nimeshawaambia hili mara nyingi sana mwenzenu siwezi kuzungumza na watu wabaya”
“Sawa, ila kwanini pia hupendi twende kwa mjumbe?”
“Mimi sio kwamba sipendi, nyie mkipata muda tu twendeni sina tatizo juu ya hilo kabisa”
Ibra alishangaa sana leo kujibiwa kirahisi hivi na huyu Neema kwani haikuwa kawaida yake ukizingatia ukizungumzia tu swala la mjumbe alikuwa mkali sana ila leo alionekana kukubali kwa haraka zaidi. Kisha Ibra kaelekea chumbani alipo mkewe na kumkuta kweli amelala na hivyo kumuamsha kwanza, Sophia aliamka kama mtu aliyekuwa amezidiwa sana na usingizi na kumfanya Ibra ampe pole kwa kumuamsha kwa haraka vile.
“Kwani kuna kitu gani mume wangu?”
“Hakuna kitu ila nilikuamsha ili angalau nikusalimie, halafu ndio uendelee kulala”
Sophia hakujibu cha zaidi kwani alijilaza tena pale kitandani na ilionekana usingizi kumchukua kwa muda huo huo. Ibra alitulia akitafakari kisha kuamua kwenda kuoga ambapo alienda kuoga kwa haraka sana na kurudi tena chumbani ila akashangaa pale kitandani hakumuona tena mkewe na kumfanya ashtuke kuwa mkewe atakuwa ameenda wapi kwani alimuacha hapo akiwa maelala fofofo.
Ibra akavaa haraka haraka na kwenda sebleni kumuangalia mabapo alimkuta Neema tu pale sebleni na kumuuliza,
“Dada yako kaenda wapi?”
“Kwani hayupo chumbani?”
“Nilimkuta amelala lakini nimetoka kuoga gafla simuoni tena”
“Aah acha masikhara bhana kaka, sasa atakuwa ameenda wapi?”
“Sijui kwakweli na ndiomana nimekuja kukuuliza wewe labda umemuona kuwa ametoka”
“Hapana mimi sijamuona, na ninachojua yupo chumbani kwenu amelala”
“Chumbani hayupo nielewe hivyo Neema”
“Je unaniruhusu twende pamoja tuakamuangalie huko chumbani”
“Twende ukaone”
Neema alitabasamu kisha akainuka pale kwenye kiti na kuongozana na Ibra hadi chumbani kwao, walipofika tu pale chumbani Sophia alionekana kitandani na kumfanya Neema amwambie Ibra,
“Si huyo hapo amelala jamani, nikusaidie kumuamsha?”
Ibra akatingisha kichwa kwani tayari uoga ulishamjaa moyoni, Neema alisogea kwenye kitanda na kukaa kisha akamgusa Sophia ambye alishtuka kutoka usingizini na kuamka kabisa huku akimshangaa Neema kuwa ameingiaje kwenye chumba chao.
“Usijali dada, ni kaka kaniruhusu kwa lengo la kukuamsha wewe”
“Sawa hakuna tatizo Neema nimeshaelewa”
Sophia alikaaa pale kitandani kisha Neema akainuka na kutoka ambapo Ibra alisogea alipo mkewe na kumuangalia kwa makini sana ambapo Sophia pia alimuangalia mumewe kwa macho makali huku akimuuliza,
“Kwanini umemruhusu Neema aingie chumbani kwetu? Inamaana wewe hukuweza kuniamsha mwenyewe hadi aje Neema?”
“Unanilaumu bure mke wangu, kwa hali ilivyokuwa sikuweza kuacha kumlaumu aingie humu chumbani”
“Halafu badae unaanza kulalamika ooh hatumfahamu vizuri na umemruhusu mwenyewe kuingia mpaka chumbani”
“Nisamehe kwa hilo mke wangu”
Kisha Sophia akainuka na kuelekea bafuni kwa lengo la kujimwagia maji kwanza ili aweze kupata nguvu.
Sophia akiwa bafuni gafla alipiga kelele na kurudi chumbani huku akilia na kumfanya Ibra ashangae sana kuwa ni nini kinamsumbua,
“Vipi mke wangu nini tatizo tena?”
“Sielewi, sielewi, sielewi Ibra”
“Huelewi kitu gani tena Sophy jamani, kwani kuna nini au umeona kitu gani?”
“Sijui hata ni kitu gani kwakweli sijui Ibra”
“Khee sasa makubwa haya, yani ukimbie ulie na usielewe unacholilia wala kilichokikimbiza kweli? Ni kitu gani umeona?”
“Nitakw\mbia tu mume wangu ila naomba unisindikize tu nikanawe vizuri”
Hilo halikuwa tatizo kwa Ibra ila tatizo ni kuwa mke wake amekumbwa na kitu gani huko bafuni ndio kulimkosesha jibu kabisa. Kisha akainuka nae na kuelekea nae bafuni ambako kulionekana kuwa kawaida tu halafu Sophia akajimwagia maji haraka haraka na kutoka nje.
Ibra alikaa huku mkewe akivaa nguo, kisha akaamua kuzungumza nae tena kuwa ni kitu gani kilimtokea bafuni wakati akioga na kumfanya akimbie na hata kuanza kulia,
“Nimekwambia sielewi Ibra yani sielewi kabisa”
“Sasa huelewi kivipi Sophy yani inawezekana vipi mtu kupatwa na jambo usilolielewa?”
“Sijui ila sielewi”
“Basi ngoja nikuulize hivi, umeona nini huko bafuni?”
Kabla hajajibu wakagongewa mlango na Neema ambaye alikuwa akiwaita ili waweze kula chakula ila leo Sophia alikuwa wa kwanza kusema kuwa anajihisi kushiba sana na kumfanya Ibra nae kusema kuwa ameshiba, hivyo Neema hakuwagongea tena na ukimya nao ukatawala ambapo Ibra alimwambia mkewe kuwa ni bora walale tu kwa muda huo.
“Ila leo nimelala sana Ibra hata sidhani kama nitapata usingizi saizi”
“Pole mke wangu ila inatakiwa ulale maana ni usiku huu si unajua tena mambo ya usiku”
“Naelewa ila sina usingizi mume wangu”
Wakiwa wanabishana kuhusu swala la kulala gafla umeme ukakatika na kufanya kuwe na giza la haswaa chumbani kwao na kumfanya Sophia amkumbatie kwa nguvu Ibra kwa uoga aliokuwa nao kwa muda huo,
“Itabidi tuwashe tochi ya simu sasa”
Ibra akaanza kupapasa ilipo simu yake ila hakufanikiwa kuipata na kushangaa kuwa siku hiyo aliweka wapi simu yake, akajaribu kuinuka huku akiwa ameshikiliwa na Sophia na kuendelea kapapasa sehemu mbalimbali na mwisho wa siku hawakuwa na la kufanya zaidi ya kumuita Neema ambaye alienda na kuwapelekea mshumaa pamoja na kiberiti ili ikitokea umeme umekatika tena wawashe tu.
Walimshukuru sana Neema na muda kidogo umeme nao ukarudi, Ibra alikuwa kashika ule mshumaa na kiberiti kisha Sophia akamuuliza mumewe
“Hivi wakati umeme umekatika hadi tukamuita Neema humu ndani, je alifungua mlango wa chumbani kwetu saa ngapi na ametoka saa ngapi?”
“Kwanini umeuliza hivyo Sophy?”
“Maana sikumbuki kama mlango ulifunguliwa ila ninachokumbuka ni kuwa Neema alileta mshumaa na kiberiti, pia sikumbuki muda aliotoka ila tu nimeona umeme umerejea”
“Hata mimi sikumbuki mke wagu ila nakuona sasa ufahamu umeanza kukurudia”
Kisha Ibra akamuomba mkewe kwa muda huo waweze kulala tu kwani hakuona umuhimu wa wao kuanza kumzungumzia Neema kwa muda huo.
Kulipokucha Sophia alikuwa wa kwanza kuamka kwa safari hii, kisha akamuamsha mumewe na kumwambia kuwa angepena siku hiyo amuandalie chai yeye mwenyewe ili aweze kunywa kabla ya kuondoka,
“Leo umeota nini mke wangu?”
“Nimeamua tu Ibra sababu nakupenda na pia naijali afya yako”
Ibra aliinuka na kwenda kuoga kisha Sophia alitoka chumbani kwao, alipofika sebleni alimuona Neema akiwa amekodolea macho kwenye Tv kisha yeye akaenda jikoni ambako alimkuta Neema akiosha vyombo na kufanya Sophia aanze kupiga kelele.
Ibra aliinuka na kwenda kuoga kisha Sophia alitoka chumbani kwao, alipofika sebleni alimuona Neema akiwa amekodolea macho kwenye Tv kisha yeye akaenda jikoni ambako alimkuta Neema akiosha vyombo na kufanya Sophia aanze kupiga kelele.
Ila Neema huyo huyo ndio alimfata Sophia na kumuuliza kuwa tatizo ni nini, ila Sophia alikuwa akitetemeka tu na kushindwa kujibu,
“Jamani dada nini tatizo, niambie tafadhari”
Sophia alizidi tu kutetemeka mpaka pale Ibra alipoingia jikoni pia kwani na yeye alishtushwa na kelele za Sophia, ni hapa Sophia alipomkimbilia mume wake na kumkumbatia ambapo Ibra nae alimuuliza kuwa tatizo ni nini,
“Sielewi, sielewi naomba twende chumbani”
Ikabidi Ibra amshikilie mke wake na kwenda nae chumbani ambapo Sophia alionekana kupooza sana kwani hakuweza kuongea ya zaidi.
“Niambie basi Sophia, tatizo ni nini?”
“Hata sielewi Ibra ila ningependa nikuombe kitu”
“Kitu gani?”
“Leo unapotoka naomba tutoke wote kisha mimi ukaniache kwa Da’Siwema”
“Kheee habari za Siwema zimeanza tena! Haya hakuna tatizo, jiandae basi”
Sophia aliinuka na kwenda bafuni ambapo alioga haraka haraka kisha kuvaa na kumuomba mumewe kuwa waondoke.
Walipokuwa wanatoke, Neema alikuwa pale sebleni ambapo Ibra alimuaga Neema kuwa yeye na mke wake wanatoka
“Mmh kaka leo mnaniacha mwenyewe!”
“Ukiona hivi ujue tumeshakuamini”
Neema akatabasamu kisha wakaondoka na kwenda kupanda gari yao moja kwa moja na safari ikaanza, Ibra alitamani sana kujua kilichompata mkewe jikoni na kumfanya apige kelele kiasi kile ila bado Sophia alikuwa mgumu kusema na kumfanya Ibra akubaliane na hali halisi tu.
Walifika nyumbani kwa Siwema kisha Ibra akamshusha mkewe na kumuaga ambapo moja kwa moja Sophia alienda kumgongea Siwema, haikuchukua muda mrefu akafunguliwa mlango
“Kheee kumbe ni Sophia, karibu sana yani hata sikukutegemea kama ungekuja leo”
“Imenibidi tu kuja dada yangu maana nina majanga ya kutosha tu”
“Majanga? Majanga gani tena? Hebu njoo uingie ndani tukae tuzungumze kwanza”
Wakaingia ndani ambapo walikaa huku Siwema akiwa na hamu ya kujua hayo majanga yanayomsumbua rafiki yake,
“Kwanza kabisa dada yangu, siku hizi mume wangu simuelewi kabisa nyumbani kutokana na mambo anayoyafanya”
“Anafanya mambo gani hayo?”
“Mara agome kula yani mambo shaghalabaghala, kisha kuna kitu kinaendelea ndani kwetu ila huwa hasemi hata nikimuuliza vipi ila na mimi kuna kitu leo nimekiona na nimeshindwa kumwambia kabisa hadi nimekuja kwako”
“Kitu gani umekiona na mambo gani yanayoendelea kwenu?”
Sophia aliamua kumueleza jinsi walivyokutana na Neema njiani na jinsi walivyoenda nae nyumbani kwao na jinsi walivyomshawishi kwenda kwa mjumbe akakataa na kile alichokishuhudia asubuhi,
“Mmh mbona makubwa hayo Sophy, una uhakika kweli kuwa ni yeye aliyekuwepo hapo sebleni na jikoni?”
“Nina uhakika kabisa dada maana nilikuwa na akili zangu timamu kabisa na sikuwa na usingizi kabisa.”
“Sasa mbona nashindwa kuelewa jamani, je kwa fikra zako unahisi ni nini mpaka ikawa hivyo?”
“Kwakweli sijui maana hata mimi nimeanza kutokumuelewa Yule Neema kabisa”
“Je Yule Jane nae huwa anaendelea kuja pale kwenu?”
Ikabidi Sophia amueleze kidogo juu ya kilichotokea kwa Jane alipomkuta Yule Neema na kisha Jane kusema kuwa hatorudi tena pale.
“Mmh inamaana huyo Neema ana nguvu kumshinda Jane?”
“Yani kama Neema ni mchawi dada basi atakuwa ni mkubwa wa wachawi”
“Sasa wewe unataka tufanyaje mdogo wangu”
“Nataka unisaidie Yule Neema atoke pale ndani dada yangu maana ananipa mashaka sana”
“Duh! Ila hebu twende kwanza nyumbani kwako nikamshuhudie huyo Neema mimi mwenyewe”
Sophia akaona kuwa hilo ni swala la muhimu sana, hivyo kukubaliana na Siwema ambaye alienda kujiandaa kisha kutoka na Sophia na kuanza safari.
Walifika nyumbani kwa Sophia na kuingia ndani ambapo Yule Neema alikuwa pale sebleni amekaa tu akiangalia Tv kisha akawakaribisha kwa uzuri sana.
“Karibuni jamani, karibuni sana”
Wakakaa kisha Neema akaenda jikoni na kuwaletea glasi za juisi na kuwaandalia ili waweze kunywa ambapo walikunywa huku wakiendelea na maongezi mengine ila baada ya kunywa ile juisi tu wote wawili yani Siwema na Sophia wakapatwa na usingizi mzito sana na kuwafanya walale pale pale sebleni.
Ilichukua muda mrefu sana wakiwa wamelala bila ya kuwa na habari ya aina yoyote ile, na aliyekuwa wa kwanza kushtuka alikuwa ni Siwema ambapo alimuona Neema akitabasamu tu Ila yeye alikuwa akijishangaa kwani hakutegemea kama angelala kwenye kochi muda ule.
“Dah kumbe nililala”
“Pole sana kwa uchovu dada”
“Asante yani sikutegemea kabisa kama ningelala kiasi hiki”
“Ndio mambo ya uchovu yalivyo, mtu unaweza kujishangaa ukilala sehemu yoyote ile haswa ikiwa na utulivu”
Kisha Siwema akamuangalia Sophia na kujaribu kumshtua,
“Kheee yani huyu ndio hajitambui kabisa”
“Muache tu ataamka mwenyewe si unajua mimba nayo inamsumbua dada”
“Naelewa ila kama amelala sana au ni mimi ndio nililala kabla yake?”
“Ndio ulilala kabla yake, hata hivyo mjamzito anatakiwa apate muda wa kupumzika ndimana nakwambia muache ataamka mwenyewe”
Siwema aliitikia tu huku akijifikicha macho yake, muda kidogo Ibra nae aliwasili kutoka kwenye shughuli zake na kuwakuta pale sebleni ila Sophia akiwa amelala vilevile, ikabidi Ibra asalimiane na Siwema kwanza,
“Ila shemeji una tabia mbaya yani umemleta mwenyewe Sophy nyumbani halafu hata kusubiri tusalimiane imekuwa shida mmh!”
“Nisamehe bure shemeji yangu nilikuwa nawahi kibaruani”
“Sawa, za majukumu lakini!”
“Nzuri tu, ila huyu nae kwanini anapenda kulala sebleni siku hizi”
“Tena amelala muda mrefu balaa”
Ikabidi Ibra amsogelee Sophia na kuanza kumuamsha ila Neema alikazania msimamo wake kuwa wamuache ataamka mwenyewe kwani si vizuri kuwasumbua wajawazito, Siwema akaingilia kati
“Hata kama si vizuri kuwasumbua wajawazito ila huyu amelala muda mrefu sana jamani, tumuamshe tu”
“Nisikilizeni mimi, muacheni alale hadi atakapoamka mwenyewe”
Kwakweli Ibra alikuwa hapendezewi na kauli za huyu Neema kuwa wamsikilize yeye kama nani wakati aliyelala pale ni mke wake, Ibra alimuangalia Neema kwa jicho kali sana kisha akaendelea kumuamsha Sophia, ambapo Neema aliing’ang’ania ile ile kauli yake ya kusikilizwa na kumfanya Ibra aongee kwa hasira sasa,
“Tukusikilize wewe kama nani wakati aliyelala hapa ni mke wangu!”
Neema akamwambia,
“Mdomo uliponza kichwa, endelea kumuamsha”
Siwema alikuwa kimya tu kwani hata yeye kwa muda huu alishindwa kumuelewa huyu Neema moja kwa moja kwani halikuwa jambo la kawaida kwa msichana wa kazi kubishana na bosi wake kamavile ambvyo Neema alikuwa akibishana na Ibra.
Ingawa Ibra alikazana kumuamsha Sophia ila hakuamka, ndiohapo Ibra akashikwa na hasira zaidi na kumuuliza Neema kwa ukali,
“Umemfanya nini mke wangu Neema?”
“Kwani wewe unahisi nimemfanya nini?”
Neema alijibu kwa dharau kabisa na kumzidisha hasira Ibra ambapo alijikuta akinyanyua mkono wake na kutaka kumzaba kibao Neema ila ule mkono kabla haujatua kwenye shavu la Neema tayari alikuwa ameudaka na kumwambia,
“Usithubutu maana utajutia maisha yako yote hadi unaingia kaburini”
Ibra aliutoa mkono wake kwenye kiganja cha mkono wa Neema na kuushusha chini kisha akakaa karibu na mke wake huku akiwa amejiinamia tu.
Ikabidi Siwema aanze kumbembeleza shemeji yake ili angalau apunguze hasira alizokuwa nazo ambapo kwa muda huo kimya kidogo kilitawala mule ndani.
Iliingia jioni kabisa ambapo Sophia alishtuka kutoka katika ule usingizi mzito sana huku akiangaza macho yake na kuwa kama mtu aliyechoka sana, alimuangalia Siwema, akamuangalia mume wake ambapo nao walikuwa wakimtazama tu kisha akajikuta akiwauliza,
“Mbona mnaniangalia hivyo jamani?”
“Umelala kwa muda mrefu sana Sophy hadi ukatupa mashaka ndiomana unaona tukikuangalia tu”
“Kheee kumbe nimelala kwa muda mrefu eeehh ila dah nimechoka sana”
Ibra akamsogelea mkewe na kuanza kumpa pole kwani kiukweli alikwa anaonekana kama mtu aliyechoka sana na kupoteza muelekeo kabisa ila Siwema nae aliamua kuaga kwani ni muda mrefu tu alikuja akingoja Sophia aamke ndipo aage na kuondoka.
“Ila kwanini Da’Siwema leo usingelala hapa hapa?”
“Hapana Sophy sikujipanga kulala, nitakuja kulala siku nyingine”
Kisha Ibra akainuka pamoja na Sophy kwa lengo la kumsindikiza Siwema ambapo Neema nae alimuaga halafu wakaondoka.
Njiani Siwema akaanza kuongelea kuhusu Neema,
“Jamani, mi mwenzenu tatizo kubwa nililoliona kwa Yule binti ni kiburi na huenda hao ndugu zake hawamtaki sababu ya kiburi maana anaonekana kuwa na kiburi cha hali ya juu”
“Sasa unatusaidiaje kwa hilo shemeji?”
“Mmh sijui hata tufanyaje ila ningeprnda siku mje nae nyumbani kwangu kisha mmuache nmkomeshe maana mie watu wenye kiburi vile huwa nawakomesha”
“Hilo wazo zuri shemeji tena ningependa tulifanyie kazi kesho tu maana mie amesha nichosha”
“Jitahidini mfanye hivyo, yani mie nikikaa nae siku mbili tu Yule ananyooka mbona maana huwa sipendi ujinga mie”
Wakaona hilo ni wazo jema sana na wote wakakubaliana kufanya hivyo, kisha Siwema akapanda daladala halafu wao wakaanza safari ya kurudi kwao taratibu.
Sehemu Ya 6
Walifika na kuingia ndani ambapo kwa safari hii walienda moja kwa moja chumbani kwao huku wakifurahia sana lile wazo walilopewa na Siwema.
“Nilikwambia Ibra tukienda kwa Siwema tutapata suluhisho
“Kweli kabisa Sophy ila tusiongee sana ili kesho iwe rahisi kukamilisha mpango wetu.”
“Sawa hakuna tatizo.”
Kichwani mwa Ibra ilikuwa ni kumpeleka Neema moja kwa moja kwa Siwema yani asirudi tena nyumbani kwao ili kama kufukuzwa basi akafukuzwe huko huko kwa Siwema kwahiyo hilo swala lilimfanya atabasamu muda wote kwa wakati huo.
Wakaongea ongea mule ndani, muda kidogo wakagongewa mlango kuwa chakula tayari, kwavile walikuwa tayari na mipango yao kichwani hawakuona tatizo lolote kwa wao kwenda kula kisha wakatoka na kwenda kula ambapo kwa siku ya leo Ibra alimuomba Neema ale nao pamoja,
“Ila mimi nimeshakula jikoni”
“Hata kama umekula jikoni Neema ila ukija na kujumuika pamoja nasi japo kwa kula kidogo tu itakuwa vizuri”
Neema hakuwabishia na akaenda mezani kukaa pamoja nao ambapo akajipakulia chakula chake kidogo tu kisha wote wakaanza kula, ila muda mwingi Ibra alikuwa akimuangalia Neema kwa lengo la kumchunguza ila kwa siku hiyo alijikuta akila huku akimshangaa huyu Neema aliyeonekana akishika shika kijiko tu bila kula ila chakula kilionekana kupungua kwenye ile sahani ya Neema kanakwamba kinaliwa ingawa muda wote aliokuwa akimuangalia hakuna muda ambao aliweka chakula mdomoni.
Kwakweli hiki kitendo kilimstaajabisha sana Ibra ila hakutaka kuongea jambo lolote lile kwani aliona ni kamavile watazua jambo jipya. Walipomaliza kula, vyombo vilitolewa mahali pale kisha Ibra na mkewe wakaelekea tena chumbani ila Ibra alikuwa akijiuliza vitu vingi sana na kujikuta akiamua kumuuliza Sophia,
“Hivi inawezekana vipi mtu kushikashika kijiko huku chakula kwenye sahani kinaisha bila kuliwa, inawezekana vipi? Je mtu huyo ni wakawaida kweli?”
“Unazungumzia nini Ibra?”
“Aaah ngoja tuachane na hayo ila kuna wakati utanielewa zaidi”
Ibra akamuomba mkewe walale ingawa kiukweli alikuwa na mawazo sana ukizingatia hakuuelewa kabisa ule ulaji wa Neema.
Kulipokucha kama kawaida waliamka na kujiandaa kisha kwa pamoja wakatoka hadi sebleni na kumkuta Neema akiangalia Tv kama kawaida kisha Sophia akaanza kuzungumza naye,
“Neema, leo ningependa twende wote kwa yule rafiki yangu wa jana ili ukufahamu nyumbani kwake na iwe rahisi kuwasiliana hata kikitokea kitu chochote nyumbani hapa”
“Kwahiyo ndio twende muda huu dada!”
“Ndio twende saizi ili tuwahi kurudi”
Neema akawaomba wasubiri ajiandae kwanza, na wao wakamruhusu kufanya hivyo huku wakifurahi kwani hawakutegemea kama angekubali kirahisi namna ile. Muda kidogo Neema alitoka akiwa tayari amejiandaa kisha safari ikaanza.
Wakiwa njiani Sophia akakumbuka Yule mtoto ambae walikuwa wakikutana nae njiani,
“Unamkumbuka Yule mtoto mume wangu, hivi siku hivi yuko wapi?”
“Hata sijui alipotelea wapi dah alikuwa ananikera sana”
Sophia akacheka tu huku Neema nae akicheka kanakwamba na yeye amewahi kumuona huyo mtoto.
Walifika nyumbani kwa Siwema na kushuka ambapo kwa muda huo walimkuta Siwema akiwa nje na shughuli zake za asubuhi ambapo aliwakaribisha ndani vizuri sana kisha wote wakaingia ndani. Muda kidogo Ibra akaaga kuwa anahitaji kwenda mahali na mke wake kisha watamfata Yule Neema badae ambapo Siwema aliwakubalia vizuri kwani mpango wao ulikuwa mmoja ila hata Neema nae hakubisha, kisha Sophia na Ibra wakatoka na kurudi kwenye gari yao huku wakifurahi sana na safari ya kurudi ikaanza.
“Nimefurahi sana kuutua ule mzigo”
“Hunifikii mimi mume wangu yani nimefurahi kupita maelezo ya kawaida”
“Sasa cha kufanya tukifika nyumbani ni kufunga minguo yake yote tuitoe nje”
“Halafu hata huwa nashangaa kuwa zile nguo kazitoa wapi wakati tulivyomuokota hakuwa hata na chochote mjinga Yule”
“Ni kweli ila cha msingi tumeutua mzigo”
Waliwasili nyumbani na kuingia ndani ila pale sebleni Tv ilikuwa inawaka tu na kufanya watazamane,
“Hivi tuliondoka bila ya kuzima Tv?”
“Inawezekana mume wangu si unajua tena tulikuwa na furaha ya kuondoa ule mzigo”
Kisha Ibra akachukua rimoti ya Tv na kutaka kuizima, ila kabla hajaizima akasikia sauti,
“Usizime kaka bado naangalia”
Walishtuka na kugeuka, wakamuona Neema akitokea jikoni.
Kisha Ibra akachukua rimoti ya Tv na kutaka kuizima, ila kabla hajaizima akasikia sauti,
“Usizime kaka bado naangalia”
Walishtuka na kugeuka, wakamuona Neema akitokea jikoni tena akiwa hana habari kabisa, kwakweli si Ibra wala si Sophia aliyeweza kustahimili hali ile kwani walijikuta wakitetemeka tu ila walimshangaa huyu Neema kwani naye alionyesha kuwashangaa na wao. Ibra aliamua kujikaza kiume huku akiuliza kwa sauti ya kutetemeka,
“Ne-ne-neema umefikaje hapa?”
“Kivipi kaka”
Neema alijibu kwa kujiamini kabisa, kisha Ibra akajikakamua tena na kusema;
“Si-si-situmekuacha kwa Siwema wewe!”
Neema akacheka kisha akawatazama kwa muda mrefu na kuwafanya wakae chini bila ya kutarajia, Ibra na Sophia walikuwa wakiangaliana tu kwa uoga na bila ya kufanya chochote huku Neema akiendelea na shughuli zake.
Ulipita muda wakiwa pale sableni bila ya kufanya chochote kile, Neema akawafata muda huu na kuwaambia,
“Mnatakiwa kuwa makini sana kwani mimi kabla hamjapanga kitu chochote juu yangu tayari nakuwa nimeshakijua, pia ni nyie wenyewe mlinionea huruma na kunikaribisha nyumbani kwenu kwamaana hiyo siwezi kutoka mahali nilipokaribishwa kwa upendo. Pia nikiingia mahali nimeingia yani kutoka msahau kabisa”
Sophia akamuangalia mumewe kisha akauliza,
“Kwahiyo Yule tuliyempeleka kwa da’Siwema ni nani?”
Neema akacheka na kumwambia Sophia,
“Niulize mimi maana ukimuuliza mumeo ni kama unajisumbua tu, na bata nikiwaambia zaidi nitakuwa nawachanganya tu bora nisiwaambie, au mpigieni simu huyo Siwema wenu awaambie”
Ibra alichukua simu huku akitetemeka na kumpigia Siwema ambapo Siwema alipokea simu ile na kusema.
“Yule mtu wenu mliyemleta hayupo”
“Ameondoka muda gani?”
“Nadhani muda sio mrefu”
Kisha simu ikakatika na kufanya Ibra atazamane tena na mkewe ila walijishangaa sababu hakuna aliyeweza kuinuka wala hakuna aliyeweza kufanya chochote kwani wangeweza kwa mufda huo wangeondoka pale nyumbani kwao. Waliazamana kwa muda ila gafla wakapatwa na usingizi wa ajabu.
Ibra alikuwa wa kwanza kuamka huku akiwa amechoka sana, pembeni yake alikuwepo mkewe Sophia na kufanya Ibra ajaribu kurudisha kumbukumbu za haraka na kweli aliweza kukumbuka mambo yote kasoro tu hakukumbuka wamewezaje kwenda chumbani kulala kwani kwa kumbukumbu zake ni kuwa walilala pale pale sebleni kwao.
Ibra akaona ni vyema amuamshe mke wake ingawa ilikuwa ni usiku, na alipomuamsha mkewe aliamka ila alionekana kuwa na usingizi sana
“Ibra jamani kuna nini tena acha nilale”
“Khee yani Sophy umesahsau yote yaliyotokea mke wangu hadi unapzata nguvu ya kulala kiasi hiko!”
“Nimechoka sana mume wangu jamani”
Sophia akajigeuza upande wa pili na kulala vizuri zaidi, Ibra alimshangaa mkewe ila hakuweza kufanya chochote kwa muda huo zaidi ya kumkumbatia na kulala tena hadi palipokucha.
Asubuhi hii Ibra alikuwa wa kwanza tena kuamka huku akiwa anakumbuka matukio yote yaliyotokea jana yake kasoro tu ni kuwa waliingiaje chumbani na kulala, Ibra alijishika kichwa huku akiwa na mawazo sana, muda kidogo Sophia nae aliamka na kusalimiana na mumewe kisha Ibra akamuuliza;
“Sophy una kumbukumbu yoyote kwa kilichotokea jana?”
“Ndio nakumbuka”
“Unakumbuka nini?”
“Nakumbuka tulikuja na Siwema hapa na ametushauri kuwa tumpeleke huyu Neema nyumbani kwake ili akamfunze adabu kwani anaonekana kuwa na kiburi sana”
“Mmmh Sophy mke wangu hayo ni mambo ya juzi”
“Ya juzi kivipi Ibra wakati ni jana tu. Hebu twende tujiandae tumpedleke au umeghairisha!”
“Kuwa mwelewa Sophy hayo unayoyasema ni ya juzi, ngoja nikueleze ya jana”
Kisha Ibra akaanza kumueleza mkewe kuhusu yale yaliyotokea jana ila Sophia alionekana kustaajabu na kushangaa sana huku akihisi kuwa huenda mume wake anaota kwani yeye hakuwa na kumbukumbu yoyote ile ya jana.
“Ibra unaota au? Huyu Neema bado hatujampeleka kwa da’Siwema yani ndio leo tunataka kumpeleka mume wangu nahisi umeanza kuchanganyikiwa”
“Sophy itakuwa ni wewe ambaye umechanganyikiwa maana nakumbuka ulipiga kelele juzi hadi ikafikia kukupeleka kwa Siwema kisha akaja hapa na kutushauri kuwa huyu binti tumpeleke nyumbani kwake kisha jana tukafanya hivyo na ndio hayo majanga yakatokea. Kwakweli mke wangu huyu Neema sio mtu mzuri kabisa inatakiwa tufanye jitihada za kumuondoa, nadhani atakuwa amekusahaulisha tu”
“Haiwezekani mume wangu, ila ili kuvunja utata basi tumpigie simu da’Siwema ili tujue kati ya mi na wewe nani anakosea”
Ibra alikubali kwani alihisi kuwa ndio njia pekee ya kumsaidia mkewe kurudisha kumbukumbu za jana. Wakampigia simu Siwema naye hakukawia kupokea baada ya salamu tu Siwema akawauliza;
“Mlisema mtamleta huyo Neema huku leo imekuwaje tena mbona kimya?”
Ibra akapatwa na butwaa kuwa hawa watu wamepatwa na nini ikiwa mambo hayo yalikuwa jana, kwakweli Ibra hakuendelea kuongea na kukata ile simu huku akijiuliza maswali lukuki, kisha akainuka na kwenda bafuni kuoga labda aweze kuiweka akili yake sawa.
Ibra alipokuwa bafuni aliwaza sana na kujiuliza vitu vingi huku akijiuliza kuwa kamakweli anaota au ni vipi maana matukio yote ya jana anayakumbuka sasa imekuwaje hawa wenzie hawakumbuki chochote!
Akajimwagia maji huku akiangaza macho yake kulia na kushoto ila alikuwa hajielewi kabisa kwani ilikuwa kama masikhara vile ila ndio hivyo wenzie wote hawakukumbuka kilichotokea, akapata wazo kuwa akimaliza kuoga basi aende kwakina Jane akazungumze nae kwani alihisi huenda akamsaidia kwa mawazo aliyokuwa nayo kwa muda huo.
Alipomaliza kuoga na kuvaa akatoka na kumkuta mke wake sebleni akiwa na Neema tena akionekana hana hofu yoyote ile kabisa, Ibra hakutaka kuongea sana zaidi ya kumuaga mke wake kuwa anatoka kidogo.
“Sawa ila nadhani ule mpango wetu wa kwenda kwa da’Siwema umehairisha”
“Hapana ila tutaongea zaidi nikirudi badae”
Kisha Ibra akatoka na kuwaacha pale ndani Sophia na Neema, muda kidogo Neema akamuuliza maswali Sophia;
“Kwani dada, kaka ana matatizo gani maana hata kunisalimia hajanisalimia”
“Achana nae huyo akili yake huwa inatawaliwana mawazo ya ajabu ajabu tu”
“Kama mawazo gani?”
“Achana nae Yule hata asikuumize kichwa, hebu tufikirie mambo mengine”
Kimya kidogo kikatawala kisha Sophia akakumbuka kitu na kusema;
“Mara nyingi Ibra amekuwa akinikumbushia nikaanze kliniki, naomba kesho nikumbushe niende Neema”
“Hata usijali dada na wala usijisumbue kwenda huko kliniki kwani kipi kipya wanachofanya? Mi ninaweza kukufundisha vyote na ukawa salama zaidi ya kwenda huko kliniki”
“Mmh nasikia ni muhimu, sijui kuna dawa za kunywa na sindano za kuchoma”
“Dada usijisumbue yani usijisumbue kabisa ngoja nitakufanyia kitu wewe mwenyewe utapenda kuliko hata kwenda huko kliniki”
Sophia akatabasamu kwani kuna wakati alihisi kama ni mzigo hivi kwenda kuanza kliniki kwahiyo alivyoambiwa hivyo na Neema akafurahi sana.
Ibra alifika nyumbani kwakina Jane na kumkuta Jane akiwa nje na shughuli zake, akamuita naye Jane hakusita kusogea alipo Ibra na kumsalimia kisha maongezi yao yakaanza,
“Unajua Jane kilichonileta hapa ni kuhusu Yule Yule mdada aliyepo ndani kwetu kwakweli amezidi kutushangaza na kutuonyesha maajabu tu.”
“Eeeh kivipi kaka?”
“Kwanza kabisa kumpeleka kwa mjumbe ilishindikana yani alitufanyia vituko sio vya nchi hii, inakuwa kama ni ndoto hivi lakini ndio ukweli ulivyo. Halafu alichokifanya jana ndio kimenitisha zaidi mpaka nimekuja kwako mdogo wangu kupata ushauri”
“Mmh pole sana, kwahiyo jana ndio kafanyaje tena?”
Ibra akamsimulia Jane vile ambavyo ilikuwa, kwakweli Jane alishangaa sana na kumuuliza kwa makini Ibra kama hayo matukio ni ya kweli au ni ndoto tu.
“Jane, hii sio ndoto yani nina uhakika kabisa na haya matukio ni kweli kabisa ila nadhani Yule mtu amevuruga akili ya mke wangu hata amekuwa haelewi chochote jamani.”
“Dah pole sana, ila mi kwa ushauri wangu nadhani itakuwa vyema ukamchukue mjumbe uende nae hapo nyumbani kwenu”
“Lakini sasa mjumbe wa huku ni nyie ndio mmemzoea labda twende wote ili tumshawishi kwenda nae nyumbani”
“Sawa kaka hakuna tatizo, ngoja nijiandae”
Ibra akatulia pale nje akisubiri Jane amalizie kujiandaa, muda kidogo simu yake ikaanza kuita alipoiangalia kuwa nani anapiga akakuta ni Siwema kisha akaipokea,
“Shemeji nimepata mahali kuna mtaalamu huyo mahili inabidi tumpeleke huko huyo mdada wenu wa kazi ili asitumiwe tena na huyo Jane”
“Samahani Siwema, hivi unaelewa kweli unachokizungumzia?”
“Kivipi shemeji?”
“Kumbuka jana ulivyosema kwenye simu na leo asubuhi ulivyosema”
“Ya jana nakumbuka ndio na ndiomana nimeenda kutafuta mtaalamu ila leo sijawasiliana na nyie yani ndio muda nimekupigia shemeji kukujulisha”
“Mmmh asubuhi si tumekupigia simu wewe na tukaongea!”
“Shemeji acha masikhara basi, simu mmepiga muda gani jamani hadi nisikumbuke? Hatujaongea asubuhi bhana”
“Mmh basi ngoja badae nitakupigia tuongee vizuri”
Ibra akakata ile simu huku akitafakari kwani aliona kamavile Siwema kachanganya mada tu kwani kwa kumbukumbu zake walimpigia simu asubuhi ili kupata uthibitisho kwa mkewe kuwa ilikuwa kweli na si ndoto ingawa majibu ya Siwema kwa hiyo asubuhi ilionyesha kamavile haikuwa kweli. Ibra alitafakari sana bila ya majibu na alihisi kichwa kumuuma tu.
Jane alipotoka ndani wakaanza safari ya kuelekea kwa mjumbe bila ya kupoteza muda zaidi.
Sophia akiwa amekaa na Neema ndani muda huu, Neema akamwambia kuwa anataka kumpima vipimo kama vya kliniki kwahiyo akamuomba aelekee nae chumbani kwake.
“Kwahiyo chumbani kwako ndio vizuri Neema?”
“Ndio dada twende”
Sophia akainuka na kwenda na Neema hadi chumbani kwake, kisha Neema akamwambia Sophia kuwa apande kitandani naye alifanya hivyo. Neema akaanza kushika shika tumbo la Sophia huku akimwambia kuwa nimeshika kichwa cha mtoto, mara nimeshika miguu yake basi Sophia akawa anafurahi tu. Kisha Sophia akamuuliza Neema;
“Je unaweza kuhisia jinsia ya mtoto?”
“Aaah naweza ndio ila subiri ukilala ukiamka nitakwambia jinsia yake, ila mtoto anaonekana kuwa mtamu sana huyu”
“Mtamu!! Kivipi mtamu?”
“Sio utamu utamu, namaanisha ni mzuri sana”
“Sikukuelewa mwanzo”
“Basi ndio nielewe, ila cha kukwambia kwasasa nenda kalale kwanza umpumzishe mtoto”
“Sawa kungwi wangu”
Wote wakacheka, kisha Sophia akainuka na kuelekea chumbani kwake ambapo alipojiweka tu kitandani ukampitia usingizi mzito sana.
Ibra na Jane walifika kwa mjumbe na bahati nzuri walimkuta na kumsalimia kisha Ibra akaelezea shida yake ambapo mjumbe alimsema kwanza,
“Hivi nyie vijana mkoje? Yani unamuokota mtu na kukaa nae siku zote hizo bila ya kutoa taarifa! Kwa mfano akikufia utakimbilia wapi?”
“Nisamehe kwa hilo baba yangu kwakweli nimefanya kosa, ila nakuomba sana twende nyumbani ukamuone”
“Kwanza ni utaratibu wa wapi huo kuwa mimi ndio nije huko badala ya nyie kuja?”
Ikabidi Jane amuombe pale, na mwisho wa siku mjumbe alikubali na kuongozana nao hadi nyumbani kwa Ibra, ila walipofika walishangazwa na ukimya wa ile nyumba kwani ilikuwa ni kimya sana na wakagonga kwa muda mrefu bila ya kufunguliwa;
“Mmmh au wametoka? Na kama wametoka kwanini hawakunipa taarifa jamani!”
Ikabidi Ibra amuombe msamaha pale Yule mjumbe kisha mjumbe akaondoka zake, halafu Ibra akaondoka na Jane na kukaa huko kwa muda ili kuvuta masaa yaende.
Jioni Ibra alirudi nyumbani kwake na kufunguliwa mlango na Neema, swali la kwanza alimuuliza Neema kuwa walikuwa wapi mchana;
“Nilimpeleka dada kliniki”
“Kwahiyo yuko wapi saivi?”
“Nimerudi nae kachoka sana na amepitiliza kulala”
Ibra akaenda chumbani alipo mkewe huku akitafakari mambo mbalimbali bila ya jibu na alimuona akiwa amelala hoi hajitambui kabisa, kisha akasogea karibu yake na kulala nae huku akijipa imani kuwa wakishtuka ndio wataenda kula kwani usiku ulikuwa bado haujaingia.
Ilikuwa ni usiku sana ambapo Ibra alishtuliwa na sauti ya Sophia akilia, alikuwa akilalamika tumbo linamnyonga sana. Ibra alimshika mkewe na kukaa ila walipoangalia kitandani, palikuwa pametapakaa damu na kufanya uoga uwashike.
Ilikuwa ni usiku sana ambapo Ibra alishtuliwa na sauti ya Sophia akilia, alikuwa akilalamika tumbo linamnyonga sana. Ibra alimshika mkewe na kukaa ila walipoangalia kitandani, palikuwa pametapakaa damu na kufanya uoga uwashike.
Kwakweli Ibra ndiye ambaye alishtuliwa zaidi na zile damu, huku akijaribu kumtuliza mkewe kwani yeye alipoona zile damu alikuwa akilia tu.
“Nyamaza mke wangu tujue cha kufanya”
“Inamaana damu zote hizi zinanitoka mimi?”
“Ndio mke wangu”
Sophia akaendelea kulia kwani alijiona kamavile anakaribia kufa, ikabidi Ibra anyanyuke na kuvaa haraka haraka kisha akamnyanyua mkewe na kuanza kukokotana nae ili waende hospitali, kutoka sebleni akamkuta Neema amekaa tena akiwa hana wasiwasi wowote ule ingawa aliona wazi Sophia akitokwa na damu kwani zilikuwa zikichuruzika tu.
Ibra hakumuongelesha Neema na kuendelea kumkokota mkewe ili atoke nae nje, Neema akawaangalia na kuwauliza,
“Vipi usiku huu mnaenda wapi?”
“Hivi wewe huoni midamu inayochuruzika au? Nampeleka mke wangu hospitali”
“Usimpeleke, rudi nae chumbani”
“Hivi wewe una kichaa nini, yani mke wangu anaumwa na damu zinamtoka kiasi hiki halafu unasema nisimpeleke hospitali!!”
Ibra hakumtazama zaidi Neema kwani alitoka na mkewe nje na kuacha Neema akicheka na kusema,
“Utaona faida ya kumpeleka huko, mdomo uliponza kichwa”
Ibra alifika nje na kumpakia mkewe kwenye gari kisha safari ya hospitali ikaanza.
Walifika hospitali na Sophia akapokelewa na manesi na kupelekwa moja kwa moja kwa daktari kwani hali yake ilikuwa mbaya sana, Ibra alikuwa kachanganyikiwa tu pale nje huku akijiuliza,
“Huko kliniki alikoenda mke wangu leo wamemfanya nini jamani? Yani mke wangu kwenda kliniki tu na matatizo juu yamempata dah! Mungu msaidie mke wangu apone”
Alihisi kama akili yake kutokufanya kazi kwa muda kidogo huku akingoja majibu ya daktari.
Ulipita muda akiwa anasubiri na baada ya masaa kadhaa alitoka daktari na kwenda kuongea nae, ila daktari hakusema chochote zaidi ya kumwambia kuwa aendelee kusubiri au kama anaweza basi aende nyumbani kwake na aje kesho yake kwani wao bado waliendelea kumuhudumia, kwakweli Ibra hakuweza kufanya hivyo badala yake alijikuta akizunguka zunguka hapo hospitali hadi panakucha kwani hakuweza hata kusinzia kutokana na mawazo juu ya mke wake.
Bado alikuwa akimngoja daktari amwambie kuhusu mgonjwa wake, muda kidogo daktari alitoka tena na kumfata ila daktari alimkaribisha ofisisni kwake na akaongozana nae hadi huko ofisini.
“Pole sana ndugu yangu”
Neno la pole lilimfanya Ibra presha iwe juu na kuwa kama amechanganyikiwa,
“Nini dokta mke wangu amekufa? Mungu wangu, nitawaeleza nini ndugu zake mimi! Nitabaki na nani jamani? Uwiii bora ningemsikiliza Neema! Dokta niambie ukweli”
“Usipaniki bwana Ibra, tafadhali punguza presha. Mkeo hajafa”
Ibra akapumua kidogo na kuuliza tena;
“Kwahiyo amefanyaje mke wangu?”
“Kwa bahati mbaya mimba yake imetoka……”
“Jamani mwanangu, kwahiyo tarajio la kuitwa baba kwa hivi karibuni halipo tena! Dah mwanangu jamani”
“Jikaze Ibra wewe ni mwanaume unatakiwa kuwa jasiri, mkeo kapoteza damu nyingi sana hata sijui ni kitu gani kilichosababisha mimba yake kutoka. Pole sana”
“Yani mke wangu kuanza kwenda kliniki tu na mimba imetoka? Jamani mambo gani haya?”
“Kwani mkeo kaenda kliniki lini?”
“Jana mke wangu ndio kaenda kliniki”
“Ila mimba yake inaonyesha ilikuwa kubwa tu, kwanini amechelewa hivyo kuanza kliniki? Yani miezi saba kasoro ndio anaenda kliniki!! Ila sidhani kama kliniki ndio wamemsababishia hayo matatizo kwani kule hata kama mimba ipo kwenye hatari huwa wanawapa wajawazito tahadhari ili wawe makini ila kama umekuja na kadi yake ungenipatia labda naweza gundua tatizo”
“Mimi sijui alipoweka kadi yake maana huko kliniki ameanza jana halafu leo mimba imetoka dah mwanangu jamani”
Dokta hakuwa nay a ziada zaidi ya kumpa pole tu Ibra na kumwambia kuwa mkewe hawezi kuruhusiwa kwavile amepoteza damu nyingi sana.
Ibra alitoka kwa daktari akiwa kama amechanganyikiwa kwani hakujua aanzie wapi na aishie wapi.
Alipokuwa nje ya hospitali hiyo, wazo likamjia kuwa awapigie simu ndugu zake na Sophia ingawa alijua wazi kuwa watamlaumu sana kwani hakuwahi kuwaambia habari za mimba.
“Mmh sasa nifanyaje hapo? Nikae kimya tu, mtoto wa watu akipatwa na matatizo zaidi itakuwaje? Lakini watanisema sana hata sijui nifanyaje”
Wakati ameshika simu ili awapigie akashtushwa na sauti ya Neema ambapo alishtuka sana;
“Kheee ulivyoshtuka kama umeitwa na mzimu vile”
“Aaah ahh Neema, aah umejuaje kama tumekuja hospitali hii!”
“Nimejua tu, nimemletea dada chakula ili apate nguvu na tuweze kurudi nae nyumbani”
“Ila dokta kasema ametokwa na damu nyingi sana hawawezi kumruhusu”
“Usijali, watamruhusu tu, ngoja akanywe kwanza huu uji”
Neema aliondoka pale na kuongoza moja kwa moja hadi wodi aliyolazwa Sophia ambapo Ibra alikuwa akimfata tu nyuma hata swala la kuwapigia simu tena ndugu wa Sophia akalipuuzia.
Neema alipofika akamuamsha Sophia na kumpa ule uji, baada ya muda mfupi Sophia alionekana kuchangamka sana kamavile sio Yule mtu aliyekuwa hajiwezi muda mfupi uliopita.
Muda kidogo daktari alikuja na kuwapa ruhusa ya kwenda nyumbani, wakatoka wote na kuongozana mpaka kwenye gari.
Kwakweli Ibra hakuwa na la kusema kwani haya mambo yalikuwa kwa muda mfupi sana, ila akasema tu
“Yani nilijua nampoteza mke wangu”
Neema akadakia,
“Hata usijali, nisingeweza kuacha apotee maana bado namuhitaji sana”
“Unamuhitaji kivipi?”
Neema akacheka tu ila Sophia alikuwa kimya kabisa kwani hata yeye hakujielewa ukizingatia usiku tu wa kuamkia siku hiyo alikuwa hoi akiumwa sana ila leo alikuwa ni mzima kanakwamba hajaumwa chochote kila ila muda wote alikuwa akijidadisi moyoni kuwa imekuwaje hadi mimba yake kutoka.
Walifika nyumbani na kuingia ndani ambapo Neema aliwakaribisha mezani kwa madai kwamba alishawaandalia chakula, Ibra akamuuliza tena Neema
“Ulikuwa na uhakika gani kama tunaweza kurudi leo?”
“Nilikuwa na uhakika kabisa, na ndiomana nikaja kuwafata. Unajua mimi nishazoea kuishi nanyi humu ndani kwahiyo sikuweza kuvumilia kuona mko mbali name, nikiwaambiaga nawapenda huwa hamuamini ila nataka mtambue kwamba nawapenda sana.”
Ibra na mkewe wakakaa mezani na kula kisha Sophia akahitaji kwenda kupumzika, moja kwa moja Ibra akaenda na mkewe chumbani ambapo walioga kisha wakapumzika pamoja ukizingatia hata Ibra hakulala usiku kucha kwani alikuwa na hofu na hali ya mke wake.
Wakati wamelala, Sophia akajiwa na ndoto tena ndoto hii ilikuwa ni ile ile ya watoto watatu ambao walikuwa wakionyesha sura za kuhuzunika ila safari hii kati ya wale watoto watatu kuna mmoja wapo alipunga mkono kama ishara ya kumuaga Sophia ambapo alipoanza kuondoka Sophia alianza kumkimbilia ila hakumfikia. Aliporudi aliwakuta wawili ambao nao kila alipotaka kuwashika walisogea nyuma ila sura zao zilionyesha kusononeka sana na kumfanya Sophia ashtuke kutoka kwenye ile ndoto huku akihema juu juu ila baada tu ya kushtuka, neno la kwanza kulisema ilikuwa “mwanangu” huku akishika shika tumbo lake na machozi kumtoka.
Ibra aliamka pia na kumkumbatia mkewe,
“Tutapata mwingine mke wangu, cha muhimu ni bado una uhai”
“Roho inaniuma sana Ibra yani sana, mtoto alikuwa faraja yangu, tumaini yangu, furaha yangu na ndoa yetu ila hayupo tena na sisi. Nilikuwa nafarijika sana na mwanangu ingawa alikuwa bado yupo tumboni ila ameondoka bila hata ya kumtia machoni”
Machozi yalimtiririka Sophia huku Ibra akiendelea kumbembeleza na kuamua kwenda nae sebleni ili wakaangalie Tv kwa kupoteza mawazo hayo.
Walitoka sebleni ila leo Neema hakuwepo hapo sebleni na Tv ilikuwa imezimwa kwahiyo ni wao ambao walienda na kuiwasha tena ile Tv, moja kwa moja wakakutana na igizo la Kiswahili na ilionyesha lilikuwa la kichawi. Waliangalia kidogo na kujikuta wakijadili,
“Waswahili nao kwa kuhusudu mambo ya kichawi siwawezi”
“Sio kwamba wanahusudu Sophy, ukweli ni kwamba hayo mambo yapo kwenye jamii yetu na ndiomana wanayaigiza”
“Kama ndio hivyo mbona ulinimaindi kipindi kile da’Siwema alivyonipeleka kwa mganga”
“Unajua nini Sophy tatizo hukunishirikisha mapema na ndiomana nilichukia ila hata nisingechukia kiasi kile”
“Ila kiukweli waswahili tunapenda sana kuamini haya mambo ya kishirikina ingawa Yule mganga ameshindwa kuniondolea Jane hadi leo”
“Kheee yani bado unaamini kuwa Jane ni mtu mbaya jamani”
“Ni mtu mbaya ndio, wewe unamtetea bure tu”
“Jane si mtu mbaya kabisa na ipo siku utajua umuhimu wa Jane katika maisha yetu ingawa tumeshindwa kutumia uwepo wake”
Neema nae akaja kujumuika nao pale sebleni, alikuja huku akicheka na kuwaambia
“Huyo Jane msimtetee yani siku mkimjua vizuri mtajilaumu sana”
Ibra akajibu,
“Tutajilaumu ndio kuwa kwanini hatukuwa nae karibu toka mwanzoni”
Neema akabadilisha mada,
“Hivyo mnavyoviangalia mtaenda kuviota vyote”
“Halafu kweli, yani Ibra anatetea hili igizo wakati ni uchawi mtupu”
“Mnataka mkiota muwashike watu ubaya, kuweni makini sana na vitu vya kuangalia”
Kisha Neema akawabadilishia stesheni, Ibra alikaa kimya kwa muda huku akijiuliza kuwa kwanini huyu Neema anajichukuliaga tu maamuzi kamavile yeye ndio mwenye nyumba wakati ni msichana wa kazi tu.
Muda huu Ibra akainuka na kuelekea chumbani kwao, alikaa kitandani akakumbuka kuwa wakati wanaenda hospitali hapo kitandani palikuwa pamejaa damu swali ni kuwa je Neema amefua mashuka yote na mpaka godoro? Maana hapakuonekana hata tone la damu tena, akajikuta akijiwa kama na mawazo kuwa ile damu mule chumbani iliyeyuka yenyewe akashtuka sana kwa uoga, kisha akasema
“Neema si mtu wa kawaida”
Gafla akaona maneno yakijiandika kwa chini ‘Si mtu wa kawaida kweli’
Ibra alitoa macho na kufumba kisha kufumbua tena na kupiga kelele za kumuita mke wake ambapo Sophia hakukawia kwenda chumbani alipo mumewe na kumuuliza kuwa kuna tatizo gani.
“Nini tatizo Ibra jamani, umepatwa na nini tena?”
Ibra akawa anamuonyesha Sophia yale maandishi ila gafla yalifutika na kumfanya Ibra awe kamavile mtu aliyewehuka kwa muda huo, kwakweli Sophia alikuwa akimshangaa tu mumewe kuwa amepatwa na jambo gani kwani alikuwa kama ana matatizo.
“Ibra jamani loh! Tatizo ni nini sasa?”
“Naogopa kila kitu Sophy, naogopa mimi”
Sophia akamkumbatia mumewe kwani alihisi kuwa mumewe pia bado alikuwa na mawazo ya kupoteza kiumbe chao kilichokuwa tumboni.
“Usijali mume wangu, tujipe moyo naamini tutapata mtoto mwingine”
“Sio swala la mtoto tu Sophy bali ni swala la huyu Neema”
“Mmmh mume wangu kwani ana nini jamani? Hebu tuachane nae na tuishi kwa amani, tuangalie jinsi gani tutaweza kukabiliana na mambo yaliyopo mbele yetu”
“Sophia mambo yaliyopo mbele yetu si mtihani mkubwa kama mtihani huu tulionao wa Neema”
“Mume wangu, usijichanganye akili yako kuhusu huyu Neema”
“Unajua Sophy usiwe kama mtu asiyejielewa mke wangu, hebu nikuulize ni nani alikushauri jana kwenda kliniki maana usikute hata swala la kutoka kwa mimba chanzo ni yeye”
Sophia akamuangalia mumewe na kumwambia,
“Sijaenda kliniki jana mie, nilikuwa nyumbani siku nzima”
“Mmh unaona hapo michezo ya Neema eeh!! Mke wangu fungua macho yako, kwani Neema amekufanya nini jana wakati sipo?”
Sophia akajaribu kufikiria kidogo na kukumbuka kuwa jana alipimwa mimba yake na Neema na baada ya hapo akalala usingizi mzito, akakumbuka na jinsi tumbo lilivyoanza kumuuma hadi kupelekwa hospitali.
“Mmh nimekumbuka Ibra”
Kisha akamsimulia vile ambavyo Neema alimpima mimba ile.
“Eeh unaona hapo Sophy unaona yani ni huyu huyu Neema ndio chanzo cha mimba yako kutoka mke wangu. Huyu Neema katuulia mtoto wetu dah ! Sikubali lazima nifanye kitu”
“Kitu gani Ibra?”
“Subiri”
Ibra akainuka na kumuacha mkewe pale kitandani akijiuliza maswali kuwa mume wake anataka kufanya kitu gani.
Ibra alijitoa muhanga na akajitoa ufahamu kabisa kwa muda huo ambapo akaenda moja kwa moja jikoni na kuchukua kisu, kisha akanyata sebleni hadi alipokaa Neema na kumchoma nacho mgongoni ila Neema hakushtuka hata kidogo ingawa damu zilionekana kumtoka.
Ibra alijitoa muhanga na akajitoa ufahamu kabisa kwa muda huo ambapo akaenda moja kwa moja jikoni na kuchukua kisu, kisha akanyata sebleni hadi alipokaa Neema na kumchoma nacho mgongoni ila Neema hakushtuka hata kidogo ingawa damu zilionekana kumtoka.
Ibra alijikuta akiduwaa na kile kisu chake sababu Neema hakushtuka wala kutingishika kanakwamba hakuna alichokichoma mahali pale, akajikuta akishindwa kupiga hata kelele huku ameshika kisu chake mkononi.
Mkewe aliamua kutoka ili ajue mumewe anataka kufanya kitu gani ila alimkuta mumewe sebleni akiwa hajielewi kabisa,
“Vipi Ibra umepatwa na nini mume wangu?”
Ibra akanyoosha kidole alipo Neema ili mkewe aangalie zile damu na amuone jinsi Neema alivyotulia tu bila ya wasiwasi wowote ule.
“Mbona hamna kitu mume wangu unanionyesha nini? Na mbona umeshika kisu mkononi?”
Ibra akaanza kuongea kwa kujiuma uma,
“Ina-ina-inamaana humuoni Neema hapo na damu!”
“Mume wangu hebu acha kuota jamani, Neema yuko wapi hapa?”
Ibra akajifikicha macho na alipoangalia kwa makini hakumuona Neema wala nini na kumfanya apatwe na uoga zaidi ukizingatia mwanzoni alimuona mahali hapo na alimchoma na kisu, akajikuta akianza kutetemeka kwani kile kisu mikononi mwake hakikuwa na damu tena na wale pale chini hapakuwa na damu tena, akajikuta akianza kuongea kwa nguvu sasa
“Hapana sioti, sioti mimi ni ukweli mtupu Neema alikuwa hapa na nimemchoma na kisu. Huyu Neema ni mchawi huyu ni mchawi”
Mara Neema akatokea chumbani na kuuliza kwa dharau,
“Nani anayeitwa mchawi huyo?”
Ibra akajibu kwa hasira huku akitetemeka,
“Wewe hapo Neema ni mchawi”
Neema akacheka sana na kumuangalia Ibra kisha akamwambia,
“Ningekuwa mchawi ningeshawamaliza siku nyingi sana kwa vituko vyenu haswa wewe mwanaume, Ibra kuwa makini sana na mimi huwa sitaniwi”
Kisha akasonya, Sophia akamuangalia Neema kwa mshangao na kusema,
“Neema kuwa na adabu, huyu ni baba mwenye nyumba”
Neema akacheka tena kisha akasema kwa dharau,
“Baba mwenye nyumba awe huyu!!! Kwa uwezo gani alionao? Anauwezo wa kumiliki nyumba kama hii? Mnapotafuta nyumba muwe mnauliza kwanza na waliotangulia kukaa hapo”
“Unamaanisha nini Neema?”
“Sahau nilichosema”
Kisha Neema akampuliza Sophia usoni na muda huo huo Sophia akaanguka kwenye kochi na kupitiwa na usingizi, akamfanyia hivyo na Ibra ambaye pia akapitiwa na usingizi.
Kulipokucha kama kawaida Ibra alikuwa wa kwanza kuamka na walikuwa chumbani wamelala yani yeye na mke wake, Ibra aliinuka na kukaa kitandani ila kichwa chake kilikuwa kizito sana.
Alijikuta akiwaza mambo mengi huku akijaribu kurudisha kumbukumbu zake nyuma na kwa bahati aliweza kukumbuka mambo yote ambayo yalitokea, akasikitika sana huku akijiuliza cha kufanya. Akamuamsha mke wake kwanza ili ajue kama nae anakumbuka chochote, Sophia aliamka na kukaa pia kisha Ibra akamuuliza;
“Unakumbuka kilichotokea jana?”
Sophia akawa kimya kwa muda kisha akamjibu mumewe;
“Kwani kimetokea kitu gani maana sina kumbukumbu kama kuna kitu cha kustaajabisha kilichotokea”
Ibra akataka kumuelezea mkewe kwa kifupi juu ya kilichotokea, ila kabla hajaanza kueleza wakasikia Neema akiwaita, Sophia akamkatisha mumewe na kumuomba kuwa wakamsikilize kwanza Neema
“Ila Sophia mke wangu siku akili yako ikirudi sawa utaelewa kwanini hatupaswi kumsikiliza huyu Neema”
“Jamani mume wangu hata hujui anatuitia nini usikute ni mambo ya maana hebu twende tukamsikilize”
Sophia akawa wa kwanza kuinuka ikabidi Ibra nae ainuke na kumfata mkewe, kisha wakatoka hadi sebleni alipo Neema ambaye aliwasalimia kwa adabu kabisa mpaka Ibra akashangaa kuwa huyu Neema mwenye kiburi leo anajifanya ana adabu kwasababu gani, wakatulia kumsikiliza;
“Jamani kuna jambo nataka kuwaeleza”
Ibra alitulia zaidi kwani alijua ni maajabu mengine kwani Neema alishakuwa tishio tayari kwake, Sophia akamuuliza kwa makini zaidi,
“Jambo gani hilo Neema? Tueleze tafadhali”
“Jana usiku nimejiwa na ndoto mbaya sana, kwanza kabisa alitokea bibi yangu akaniambia anataka kunionyesha maajabu yaliyotokea kwangu kisha akapotea. Mara nikamuona Jane akisema kuwa kuna mambo anayafanya ili mimi nionekane mbaya kwenye macho yenu. Nikashtuka usingizini, kwakweli Jane ni mtu mbaya sana ten asana mnaweza mkachukizana na watu wengi sana kwasababu yake. Nimeamua kuwaita na kuwaeleza haya ili mjue ya kuwa sina ubaya wowote mimi”
“Mmmh!!!”
Ibra aliguna kwanza kwani hakuamini hata kidogo haya maneno ya Neema na wala hakufikiria kama ni maneno ambayo Neema aliyowaitia asubuhi hiyo na kwa haraka haraka akahisi kuwa Neema amefanya hivyo kwavile hataki amsimulie Sophia kile kilichotokea kwa hofu ya kumkumbusha vizuri, Ibra akamuangalia Neema na kusema
“Inamaana na kilichotokea jana ni Jane ndio amefanya?”
“Kipi hicho kilichotokea jana?”
“Yani Neema bila hata ya aibu unajifanya kuuliza kipi kilichotokea? Kwani hujui kilichotokea?”
Sophia naye akauliza,
“Kwani kitu gani kilitokea?”
“Mke wangu Sophy huyu Neema ni mchawi”
“Mchawi? Kivipi? Au na wewe mume wangu ushachanganywa na Jane?”
“Niamini mimi Sophia huyu Neema ni mchawi na ndiye aliyemuua mtoto wetu”
“Kheee kivipi mume wangu wakati ni mimba imetoka!”
“Kwa macho ya kawaida unaona kamavile mimba imetoka ila kiukweli imetolewa na Neema kiuchawi”
Neema alikuwa kimya tu akiwasikiliza na maongezi yao kanakwamba hayupo ila alikuwepo palepale akiwaangalia, Sophia naye akamuangalia Neema na kumuuliza
“Je ni kweli umesababisha mimba yangu kutoka Neema? Je ni kweli wewe ni mchawi?”
Neema akacheka sana, kisha akawaambia
“Ila kweli nyie mtakuwa na matatizo ya akili, yani niliyowasimulia yote yameingia kulia na kutoka kushoto duh! Mtu mwenye akili timamu anaweza kuniuliza maswali kama hayo kweli?”
Neema akamuangalia Sophia kwa msisitizo zaidi ambapo Sophia akainuka na kuelekea chumbani kwao.
Sophia alipokuwa chumbani aliwaza sana na kufikiria kuwa huenda mume wake ana matatizo kichwani kwani halikuwa jambo la kawaida kumuita mtu mchawi bila kuwa na uthibitisho, akainuka tena ili aende sebleni akamuombe msamaha Neema na aweze kumshawishi mume wake ili wamuombe msamaha Neema.
Alipofika sebleni alimkuta Neema akiwa peke yake na kumuuliza alipo mumewe kwanza,
“Ibra yuko wapi?”
“Katoka”
“Kaenda wapi?”
“Hata hajaniaga alipoenda”
“Kheee Ibra ameanza kuchanganyikiwa sasa loh! Yani kaondoka bila hata kuoga tena kifua wazi au alivaa shati gani?”
“Yani hata sijui maana nilichosikia ni kuwa alifungua mlango na kutoka sababu mimi nilikuwa jikoni”
“Khee makubwa haya, tafadhali Neema naomba utusamehe mimi na mume wangu kwa kukushutumu vibaya”
“Hata usiwe na wasiwasi dada, mimi ni mtu muelewa sana.”
“Nashukuru kwa hilo Neema ila huyu Ibra hata sijui ana matatizo gani jamani yani kuondoka bila hata kuoga loh!”
Sophia alifikiria kidogo kisha akaenda tena chumbani na kuchukua simu yake akijaribu kumpigia mumewe ila simu ilianza kuitia mule mule ndani na kugundua kwamba mume wake ameacha simu ndani, akatoka tena na kuelekea sebleni kisha akamwambia Neema
“Kumbe simu yenyewe kaiacha ndani, ila mie nae hata sijui nafikiria nini maana mwanzoni nilipotoka nae hapa hakutoka na simu halafu eti naenda chumbani kumpigia loh! Ila pia alitoka hajavaa shati hata sijui ameendaje huko”
“Labda kaenda kuanua ya kwenye kamba huwezi jua”
“Mmh halafu sijafua siku nyingi”
“Una wasiwasi gani wakati mimi nipo! Yani mimi nikiwepo hutakiwi kuwa na mashaka ya aina yoyote ile sababu nitafanya kazi zote za humu dada”
Kisha Neema akamuomba Sophia aelekee mezani kula huku akimsisitiza kuwa ni muhimu ale sana ili kurudisha afya yake baada ya ile mimba kutoka, Sophia hakujiuliza mara mbili na moja kwa moja alielekea mezani na kula chakula alichoandaliwa na Neema.
Sophia alipomaliza kula akaenda kuoga na kujiandaa kwani alipata wazo la kwenda nyumbani kwa Siwema ili aweze kuzungumza nae kuhusu mume wake na jinsi anavyomshutumu Neema kuwa ni mchawi na anahusika na mimba yake iliyotoka. Akatoka chumbani sasa na kumkuta Neema pale sebleni kama kawaida na kuamua kumuaga,
“Neema, mimi natoka kidogo”
“Unataka kwenda wapi dada?”
“Naenda kwa rafiki yangu mara moja”
“Sawa dada, badae tutaonana”
Akaagana nae pale vizuri kabisa na kuondoka, alipofika getini gafla kichwa kilianza kumgonga yani kamavile mtu anagonga na nyundo, Sophia hakuweza kwenda mbele na kusimama kwa muda kwanza kisha akaanza kurudi na kuingia ndani.
Alipoingia ndani alishangaa kumkuta Neema akicheka sana,
“Mbona unacheka hivyo Neema?”
“Na wewe mbona umerudi?”
“Kichwa kinaniuma sana tena kimenianza gafla tu”
Neema akacheka tena kisha akamwambia Sophia,
“Basi hunabudi kuahirisha safari yako, ni bora ukapumzike tu”
“Ila sasa mbona unacheka Neema?”
“Nacheka vile ninavyoweza kuziendesha akili zenu”
“Unasemaje Neema?”
“Nenda kapumzike na wala sijasema chochote”
Sophia alielekea chumbani kwake huku akiwa na mawazo sana kwani hakuielewa kabisa ile kauli ya Neema kuwa anacheka vile anavyoweza kuziendesha akili zao,
“Mmmh akili zetu anaziendeshaje huyu? Inamaana kuna kitu huwa anatufanyia?”
Wazo lingine likamjia palepale kuhusu Ibra,
“Hivi Ibra anaweza kuondoka bila ya kuniaga kweli! Mbona kamavile ni jambo lisilowezekana kabisa, mmh basi kabadilika sana siku hizi”
Akajilaza kidogo na kupitiwa na udsingizi palepale.
Wakati amelala akajiwa na ndoto, kwenye ndoto yake leo aliona watoto wadogo wawili, sura zao zilionyesha huzuni sana na kufanya nae aone huzuni pia ila alisikia sauti ikimwambia,
“Je, ni yupi atapona kati yao?”
Sophia akashtuka sana na kuamka, akaangaza huku na huko na kuona kuwa giza nalo lilikuwa limeingia, akafikiria kuhusu ile ndoto ila akajikuta akikumbuka kuhusu mume wakw,
“Inamaana Ibra bado hajarudi?”
Akainuka na kuelekea sebleni ambako alimkuta Neema ila kabla hajamuuliza Neema chochote akashangaa Neema akimwambia,
“Umeamka mapema sana tena sana, inatakiwa urudi kulala”
Sophia akajishangaa akirudi tena chumbani na kulala.
Kulipokucha Sophia alikuwa wa kwanza kuamka na kumkuta mumewe amelala hoi pembeni yake na kumuamsha, Ibra naye aliamka kwa upesi sana tena alikuwa ni mtu anayejishangaa kwa wakati huo, kisha kwa haraka akaenda kuoga na kurudi huku akivaa haraka haraka.
“Kheee kukuamsha nikuamshe mie halafu haraka ujifanye unazo wewe loh!”
“Natakiwa niwahi kwenye shughuli zangu kuna wateja niliahidiana nao leo”
“Ndio ulipokuwa jana!”
“Kuwa jana kivipi mke wangu jamani, ngoja niwahi nikirudi tutazungumza”
Ibra alimbusu mkewe kwenye paji la uso na kisha kuondoka zake.
Ibra alifika kwenye shughuli zake ila kila mmoja alionekana kumshangaa kwenye eneo lile,
“Unaonekana umeshiba pesa ndugu yangu yani siku zote hizo ulikuwa wapi?”
“Kivipi jamani mbona siwaelewi?”
Wakabaki kumshangaa tu kisha kila mmoja kuendelea na shughuli zake, Ibra alikuwa akishangaa tu biashara yake kwani ilionyesha haijafunguliwa muda kidogo na kujiuliza kuwa kwanini hakufungua siku zote hizo, wakati akifikiria hayo alifika rafiki yake Lazaro na kumkuta hapo kisha kusalimiana nae,
“Kila siku nikipita hapa sikukuti Ibra, vipi ndugu yangu umekumbwa na nini?”
“Hata mimi mwenyewe sifahamu kuwa nimekumbwa na nini?”
“Au ndio mambo ya Yule msichana wenu wa kazi?”
Kidogo Ibra akaanza kukumbuka baadhi ya mambo na kumuangalia rafiki yake kisha kumwambia,
“Lazaro, nadhani Yule binti atakuwa kanifanya kitu sio bure”
“Pole sana, ila huyo binti sio wa kumuendekeza inatakiwa umwambie ukweli”
Muda huo huo Neema akaja pale kwenye biashara ya Ibra na kuwaambia,
“Haya niambieni huo ukweli”
Ibra na Lazaro waliangaliana kwa mshangao.
Kidogo Ibra akaanza kukumbuka baadhi ya mambo na kumuangalia rafiki yake kisha kumwambia,
“Lazaro, nadhani Yule binti atakuwa kanifanya kitu sio bure”
“Pole sana, ila huyo binti sio wa kumuendekeza inatakiwa umwambie ukweli”
Muda huo huo Neema akaja pale kwenye biashara ya Ibra na kuwaambia,
“Haya niambieni huo ukweli”
Ibra na Lazaro waliangaliana kwa mshangao, kwakweli walitetemeka pia kwani hakuna hata mmoja kati yao aliyemtarajia Neema kwa muda huo. Ibra alijikuta akimuuliza Neema kwa sauti iliyojaa uoga na kutetemeka
“Na-na-nani aliyekuonyesha hapa kwenye biashara zangu?”
“Mkeo ndio kanionyesha hapa”
“Mke-mke-mke wangu mwenyewe yuko wapi?”
“Huyo hapo anakuja”
Kuangalia nje ni kweli alimuona Sophia akisogea pale kwenye biashara yake na kumfanya Ibra azidi kupatwa na mashaka.
Sophia alifika eneo lile na kuwasalimia, Ibra alishindwa hata kuitikia salamu ya mke wake na kujikuta akimuuliza
“Mbona-mbona hukuniambia kama utakuja huku leo?”
“Kwani kuja mahali ambako mume wangu huwa anashinda ni dhambi au ni vibaya?”
“Hapana si vibaya ila mbona hukunitaarifu?”
“Hivi wewe ulivyokuwa na haraka vile ile asubuhi ningekutaarifu vipi? Kwakweli mimi sijakuelewa kuhusu ulipoelekea jana ndiomana leo nimekuja kuhakikisha kama kweli umekuja kwenye shughuli zako isije kuwa napigwa changa la macho”
Lazaro akaingilia kati yale maongezi kwa kumuuliza Sophia,
“Sasa shemeji, change la macho upigwe na Ibra au huyo msichana wenu wa kazi?”
Neema alimuangalia Lazaro kwa jicho kali sana na kumwambia,
“Na wewe hayakuhusu, fanya yako”
“Unaniambiaje wewe?”
“Kama nilivyokwambia na kama ulivyosikia”
“Wewe usionichezee mimi sio hao wakina Ibra unaowachezea mimi ni mtu mwingine wa tofauti”
Neema akamsonya Lazaro kisha akamwambia,
“Kwa utofauti gani ulionao wewe!”
Kisha akamsonya tena, kwavile Lazaro alikuwa ni mtu wa hasira kwakweli hasira zilimpanda palepale na kumnasa kofi Neema huku akisema,
“Mke wangu mwenyewe hajawahi kunisonya sembuse wewe kikaragosi”
Neema akacheka na kumwambia Lazaro tena kwa dharau zaidi ya mwanzo,
“Yani umenipiga mimi kibao eeh!! Sasa nakwambia hiki kibao ulichonipiga kitakutesa wewe na familia yako na hapo ndio utaujua ukikaragosi wangu mbweha wewe”
Ikabidi Ibra aingilie kati kwani aliona kamavile mzozo ungekuwa mkubwa zaidi na kumsihi rafiki yake apunguze hasira ila Neema aliendelea kuongea,
“Tena umsihi sana ten asana maana hanijui vizuri huyo, sasa nitamuonyesha kuwa mimi ni nani”
Kisha akamshika mkono mke wa Ibra na kumwambia,
“Tuondoke”
Kabla hata Sophia hajasema chochote alijikuta akifatana tu na Neema na kuondoka eneo lile.
Ibra na Lazaro walibakia mahali pale kisha Lazaro akamwambia rafiki yake kuwa awe makini sana,
“Kuwa makini Ibra haiwezekani wanawake wakatupanda kichwani namna hii”
“Ndugu yangu, kuna wanawake wa ukweli na wanawake wa uongo, sio kila mwanamke ni mwanamke kweli. Wewe mwenyewe ulisema kuwa nyumbani kwangu si pa kawaida na umegoma kuja tena, basi pale nyumbani kwangu toka amekuja huyo Neema ndio kumekuwa na matatizo sasa utasema ni mwanamke wa kawaida Yule???”
“Ila Ibra ngoja nitamuagiza mke wangu aje akupe ushauri wa kiroho maana bila ya hivyo huyu Neema atakusumnbua tu na uchawi wake”
Ibra akatulia kwanza na kutafakari uchawi wa Neema bila ya jibu ukizingatia wanafanyiwa vioja kila leo, akawaza kuwa hata anavyoulizwa na mkewe kuhusu jana huenda kuna kitu kilitokea ingawa hakuwa na uhakika zaidi.
Lazaro aliamua kumuaga pale rafiki yake na kuondoka huku akimsisitiza kuwa ni lazima wapate msaada wa matatizo ya huyo Neema, Ibra aliitikia huku akiendelea na mawazo yake.
Akajaribu kurudisha kumbukumbu zake kwa siku ya jana ili aweze kujua kuwa alikuwa wapi, akakumbuka alivyotoka chumbani na mke wake muda Neema amewaita na jinsi alivyomsema Neema kuwa ni mchawi mbele ya macho yake, kisha akakumbuka jinsi mkewe alivyoinuka na kuelekea chumbani kanakwamba hakuna ya maana yanayozungumzwa pale. Halafu akakumbuka kuwa mkewe alivyoinuka kuna kitu alipuliziwa na Neema na kumfanya aanguke chini ndio hakukumbuka kulichoendelea hadi asubuhi yake alipoamshwa na mkewe,
“Mmmh kwakweli huyu Neema ni mchawi tena mchawi kabisa aliyekubuhu, hivi tunawezaje kuishi na mtu mchawi kiasi kile kama Neema jamani yani hadi nyumba yangu naiona chungu”
Wakati akiwaza hayo, alikuja rafiki yake ambaye ni mfanyabiashara mwenzie wa eneo lile aliyejulikana kama baba John ambaye kwa muda huo ndio alimshtua toka kwenye yale mawazo.
“Vipi wewe umeanza kuchanganyikiwa au?”
“Hapana ndugu yangu ila kuna mambo yananitatiza bhana”
“Mambo gani hayo?”
“Msaidizi wetu wa kazi nyumbani ni mchawi kwakweli anatutesa sana yani sina raha”
“Si umtimue jomba, kwanini uendelee kufuga maradhi?”
“Kumtimua si kazi rahisi, tushajaribu mara nyingi imeshindikana baba John yani nachanganyikiwa hadi sijui cha kufanya”
Baba John akafikiria kidogo kisha akamwambia Ibra,
“Eeeh nimekumbuka kitu, kuna mganga wa kienyeji huyo ni khatari ndugu yangu yani huyo mtu mbona ataondoka bila kuaga”
“Dah itakuwa vyema sana kama utanipeleka huko ndugu yangu kwakweli nimechoka, au kamavipi tufunge unipeleke hata muda huu”
“Dah kweli umechoka ndugu yangu pole sana, ngoja nimuite dogo abaki pale dukani twende”
“Sawa, mimi nipo tayari ndugu yangu”
Baba John akatoka na kumuacha Ibra akifunga funga ile biashara yake ili aende huko kwa mganga wa kienyeji.
Ibra na baba John waliongozana hadi kwa huyo mganga ambaye baba John alimueleza Ibra, walikuta kuna mtu ndani kwahiyo wakasubiri atoke kwanza, baba John aliendelea kumsisitiza Ibra kuwa hapo wapo mahali sahihi na tatizo lao litafika mwisho.
Yule mtu alipotoka waliingia wao na moja kwa moja Yule mganga alianza kuwaeleza matatizo yao;
“Naona baba Jumatano umekuja na mwenzio, unahuruma sana wewe yani angekuwa ni mtu mwingine asingeweza kushirikiana na huyu kumleta huku. Sasa kijana matatizo yako tumeshayajua ila ni mazito kidogo sema tutajitahidi hivyo hivyo tukusaidie”
“Nashukuru sana wazee, kwakweli naomba mnisaidie sana yani mambo yamenifika kooni sina raha sina amani wala sina furaha naomba tu mnisaidie niondokane nayo”
“Sawa, sisi tutakupa dawa ila inatakiwa ufate masharti ya dawa yetu”
“Nipo tayari kwa masharti yenu”
“Hii dawa, ukiwa umefika nyumbani kwako yani kabla hujaingia ndani ilambe kisha ingia ndani ila ukishaingia ndani usiongee na kiumbe yeyote Yule….”
“Hata mke wangu!!”
“Elewa maana ya kiumbe yeyote Yule, yani usiongee chochote wewe fanya mambo yako kimya kimya tu mpaka muda wa kulala ilambe tena na ulale. Pakikucha ilambe tena yani nakwambia kile kitendo cha wewe kutoka kwenda kwenye shughuli zako ndio muda huo huo Yule kiumbe nae atafungasha virago vyake na kuondoka”
“Asante sana ndugu mganga kwakweli nitafata masharti vilivyo sitakosea hata kidogo”
“Jitahidi sana usikosee masharti, maana ukikosea yatakayokupata mimi simo”
“Yani siwezi kukosea hata kidogo kwahiyo usijali kuhusu hilo”
Wakamuaga Yule mganga na kuondoka eneo lile, wakiwa njiani ikabidi Ibra amuulize baba John;
“Ndugu yangu vipi Yule mganga kakuita baba Jumatano wakati mwanao anaitwa John??”
“Ibra, kwenye maisha kuna siri nyingi sana ila ngoja nikwambie kuhusu mwanangu John.”
“Eeeh niambie ndugu yangu”
“Mke wangu mimi alikuwa hashiki mimba ndio tukaenda kwa Yule mganga, akatufanyia dawa hadi mke wangu akapata mimba halafu mganga akasema siku mke wangu atakapojifungua huyo mtoto basi tunatakiwa tumuite huyo mtoto jina la siku hiyo, sasa mke wangu akajifungua siku ya Jumatano hapo ndio ikawa kimbembe maana sijawahi hata siku moja kusikia mtu akiitwa Jumatano ndipo tulipoamua kumuita mtoto John ila jina lake halisi ni Jumatano yani tumemuita John ili watu wasiulize ulize sana. Bora hata tungempata Jumanne wakina Jumanne wapo kuliko hiyo Jumatano. Kwahiyo huyu mganga siku zote huniita baba Jumatano sababu anajua siri iliyojificha kwa mtoto wetu”
“Dah ila huyu mganga atakuwa vizuri sana, ngoja nimalize haya halafu nije tena labda anisaidie na matatizo yangu mengine”
“Hata usiwe na shaka Yule mzee ni kiboko”
“Basi ngoja tuzunguke kidogo hata nikirudi nyumbani muda uwe umeenda enda niweze kufata masharti vizuri”
Baba John akamshauri warudi kwenye biashara ili wakamalizie muda huko, kwahiyo walikubaliana na kuongozana kwenye biashara zao.
Sophia alishtuka usingizini na kuamua kwenda sebleni huku akijishika kichwa na kulalamika kuwa kinamuuma sana, Neema alimpa pole na kumwambia kuwa anywe maji mengi kitapoa.
“Unajua nimeota ndoto ambayo siielewi hadi sasa”
“Ndoto gani hiyo dada”
“Nimeota eti mimi na wewe tumetoka hapa nyumbani na kuelekea kwenye biashara ya Ibra, halafu tukamkuta na rafiki yake ambaye uligombana nae na akakupiga kibao kisha wewe ukanishika mkono kuwa tuondoke. Nimeshangaa kuamka najikuta kitandani kumbe ni ndoto loh!”
Neema akacheka na kumwambia Sophia;
“Kweli hiyo ni ndoto dada yani mimi nipigwe kibao halafu nimuangalie tu huyo mtu nimechanganyikiwa au!”
“Kwahiyo ingekuwa kweli ungemfanyaje?”
“Ningemrudishia, yani nisingeweza kukubali kupigwa kizembe namna hiyo.”
“Ila leo inaonekana nimelala sana yani hata sikumbuki muda gani nimekula”
“Dada jamani itakuwa mimba nyingine hiyo inakunyemelea”
“Dah bora iwe kweli maana nimemiss kushika shika tumbo langu na kuongea na mwanangu angali tumboni yani nimemkumbuka sana ungawa sikuiona sura yake”
“Usijali dada, utampata mwingine tu, ila hata hivyo nakuhisi kama una mimba vile”
“Mmmh Neema ndio fasta hivyo jamani, ila natamani niipate nitafurahi sana”
“Ila ili uwe salama usionane kabisa na Yule Jane dada yangu.”
“Nani aonane na Yule shetani yani siwezi kabisa, sijui Ibra vipi maana ndio anaonanaga nae”
“Mumeo ana matatizo sana, ila dada una mimba”
“Mmmh kweli Neema?”
“Ndio ni kweli nimeona bora tu nikwambie”
“Uwiiii Ibra atafurahi sana nikimwambia, unajua mimi huwa naamini sana maneno yako Neema. Sina hata haja ya kupima”
Muda kidogo Ibra akaingia ndani ila hakuwasaliia wala nini na kupitiliza chumbani, Sophia na Neema wakaangaliana kisha Neema akamuuliza Sophia;
“Kwani shemeji ana matatizo gani dada?”
“Hata naelewa basi, yani kama hajatuona vile”
“Hebu mfate umuulize, asipokujibu basi jaribu kumwambia swala lako la mimba na kama akiwa kimya jifanye unaumwa”
“Sawa sawa, ngoja niende”
Sophia akainuka pale na kuelekea chumbani alipo Ibra.
Alimkuta Ibra akiwa amejilaza kitandani, Sophia akamuamsha na kumuuliza tatizo ni nini ila Ibra alikuwa kimya tu,
“Jamani mume wangu nani kakuudhi jamani? Ibra wa kuninyamazia mimi wewe?”
Ibra alikuwa kimya tu hakumjibu kitu chochote mke wake na wala hakuonyesha kujali vile alivyokuwa akiulizwa na Sophia.
Kwakweli Sophia alikuwa anapatwa na hasira tu vile mumewe alikuwa hamjibu, kisha akamwambia
“Ibra, mwenzako nina mimba”
Ibra bado yupo kimya tu.
“Jamani mume wangu hata kufurahia jamani, inamaana hutaki mtoto tena mume wangu!”
Ibra hakujibu chochote na kuzidi kumsononesha Sophia kwani alikosa raha kabisa vile ambavyo alikuwa hajibiwi na mumewe.
Kimya kikatawala mule ndani, muda kidogo Sophia alijitupa chini na kuanza kulalamika kuwa tumbo linamuuma sana huku akijinyonga nyonga na kulia, Ibra akataka kumuinua mkewe ili amuwaishe hospitali ila Sophia alikuwa anagoma kuinuka na kuendelea kujinyonga nyonga tumbo, kwakweli Ibra alihisi kuchanganyikiwa kwani alitamani kuongea Ila akikumbuka masharti aliogopa kuongea ila akiangalia hali ya mkewe alitishika zaidi, mara gafla Sophia akawa pale chini kimya kabisa na kumfanya Ibra uoga umshike zaidi na kuanza kumsukuma sukuma mkewe kama ishara ya kumuamsha ila wapi yani hakushtuka hata kidogo na kumfanya Ibra azidi kupatwa na hofu.
Akaamua kumnyanyua, ila alipomnyanyua tu alishangaa damu zikimtoka Sophia kama maji, yani hapo Ibra alichanganyikiwa kupita maelezo ya kawaida na kutoka nje na mke wake. Wakati anapita sebleni alimkuta Neema amekaa huku akicheka sana ila Ibra bado aliendelea na msimamo wake wa kutokuongea chochote ila wakati anatoka akajikwaa mlangoni na kufanya yeye na mkewe waanguke chini.
Akaamua kumnyanyua, ila alipomnyanyua tu alishangaa damu zikimtoka Sophia kama maji, yani hapo Ibra alichanganyikiwa kupita maelezo ya kawaida na kutoka nje na mke wake. Wakati anapita sebleni alimkuta Neema amekaa huku akicheka sana ila Ibra bado aliendelea na msimamo wake wa kutokuongea chochote ila wakati anatoka akajikwaa mlangoni na kufanya yeye na mkewe waanguke chini.
Kwakweli kile kitendo cha kujikwaa na kuanguka kilimpa maumivu sana Ibra na kumfanya augulie kwa muda kidogo kisha kuinuka na kumuingiza mkewe kwenye gari akielekea nae hospitali.
Walipofika hospitali walipokelewa ila kwavile Sophia hakuwa na ufahamu wowote ikabidi daktari azungumze na Ibra ili ajue nini chanzo,
“Vipi wewe ni bubu?”
Ibra aliangua kilio kwakweli kwani alijiona wazi zoezi likimshinda,
“Una matatizo gani wewe? Una kichaa au? Una mahusiano gani na mgonjwa na ugonjwa wake umeanza vipi? Sema basi ili tumuhudumie mgonjwa au la tutampoteza huyu”
Ibra alijikuta akiongea kwa huzuni sana,
“Kwani wale wagonjwa wanaoletwa na mabubu mnawahudumiaje?”
“Mabubu huwa wanafanya vitendo na wanaeleweka sasa wewe unatulilia halafu sisi tutafanye, haya sasa elezea matatizo ya mgonjwa”
“Hata sijui kwakweli ameanza gafla tu”
Daktari akamuhoji hoji pale Ibra kisha akaandika maelezo na kuendelea kumshughulikia mgonjwa, kwakweli Ibra aliwaza sana;
“Amakweli ng’ombe wa masikini hazai yani kujitahidi kote kule na sharti nililopewa na mganga mwishowe yamenishinda dah!”
Ibra aliumia sana rohoni na kukosa raha kabisa ila ndio hivyo ilishatokea.
Ibra aliitwa na daktari na kuelezwa kuwa Sophia alikuwa na mimba ila hiyo mimba imetoka.
“Ila dokta unajua siku si nyingi tulikuwa hospitali mke wangu mimba yake ilitoka sasa kumbe alishapata nyingine tayari nayo imetoka dah!!”
“Usishangae sana, mwanamke ambaye mimba imetoka au kuharibika mara nyingi kizazi chake kinakuwa wazi sana na kinakuwa tayari kubeba mimba nyingine kwa wakati wowote ule. Mimba ya mkeo imetoka ila ilikuwa changa sana yani haikuwa hata na wiki ila ndio hivyo imetoka. Kwasababu alishawahi kupatwa na matatizo ya hivi ndiomana ameumwa sana. Pole sana ndugu yangu kwa kuipoteza hii mimba”
“Ila sababu ni nini dokta hadi mimba ya mke wangu kutoka?”
“Sababu huwa ni nyingi ila nadhani alianguka, maana mimba ikiwa changa namna hii inakuwa bado haijajishikilia vizuri”
Ibra aliishia kusikitika tu huku akijiuliza kuwa huenda pale walivyojikwaaa na kuanguka ndio kumesababisha yote yale ila alijiuliza kuwa mbona mkewe alianza kutokwa damu kabla ya kuanguka pale na kukosa jibu la moja kwa moja.
Karibia na alfajiri Sophia alizinduka na kuitiwa mumewe ambapo alipewa taarifa za kutoka kwa mimba yake, kwakweli Sophia alijikuta akilia sana na kumuuliza Ibra kuwa kwanini imekuwa vile.
Mwisho wa Season 1
SEASON 2 inakuja

