Nilipogonga Mlango, Alitoka Mwanaume, Akiwa Amejifunga Khanga Ya Mke Wangu
Ndugu mabibi na mabwana habarini za Leo kwa jina naitwa Lameck nina umri wa miaka 40 ni baba wa watoto wawili mwaka 2007 nilinunua eneo langu nikajijengea kijumba changu nikahamia na mwaka 2008 nikapata mchumba na mwaka 2009 nikafunga ndoa kanisani maaana tuliokoka na mimi na mke wangu tukaanza maisha ya ndoa kwenye kile kibanda changu alichokuta nimekijenga na mwaka 2010.
Tulipata watoto wetu wawili hawa ni mapacha ambao kwasasa wapo fom one tuliendelea na maisha ya ndoa tukiwa na maisha ya kawaida tu mimi sikuwa na kazi maalum ila nilikuwa mchakarikaji sana na yeye mke wangu nilimuwekea kibanda cha. Kiduka hapo nyumbani tulipojenga pia mke wangu alikuwa mwanakwaya mzuri tu. Pia alikuwa mwalimu wa kwaya ila sasa mwaka 2015 nilipata boss mzungu nikawa nafanya vijikazi kwake na anailipa vizuri tu na tukafanikiwa kujenga tena nyumba ya vyumba vitatu maisha yakaendelea badae boss mzungu akanifanya kuwa dereva. Wake tukisafiri huku nakule
Lakini nikiwa safarini na boss wangu nikawa napata tarifa kuwa ndani kwako tumekuwa tuona mke wako akiingia na mwanaume wakati wa mchana watoto wakiwa shule au usiku watoto wakiwa wamelala
Hiyo hali ikanistua sana ila mimi sikumuuliza mke wangu nilikaa kimya nikaendelea na uchunguzi wangu kimya kimya nikiwa nipo kwenye uchunguzi wangu na nikiwa nipo safarini nilipata tena tarifa kwa mtu mwingine kabisa akinipa tarifa ile ile ya mke wangu anaingiza mwanaume ndani kwangu nilipata presha lakini nikajikaza ili tu safari yangu iwe salama maana mimi ndio dreva
Baadae nikaja kubaini kuwa anaetembea na mke wangu ni ndugu moja. Wa kanisani ambae ni rafiki wa mchungaji sana na mara nyingi huyo ndugu akisafiri nje ya nchi uwa anamletea mchungaji zawadi na pia aliwa kumnunulia mchungaji gari nilipogundua nilikaa kimya nikitafuta ushahidi zaidi ya nilioupata
Lakini wakati huo mimi nimeanza kuendesha maisha yangu binafsi bila ya kumshirikisha mke wangu nilibahatika nikapata pesa nzuri tu nikanunua eneo kibaha la kekari 3 na nikajenga nyumba kubwa tu na nikanunua kila kitu ndani na nikanunua na gari ya kutembelea nikaiweka tu ndani kwangu. Kibaha na pia nikanunua Costa 3 nikazifanya dala dala hapa mjini dar na nilimuweka mama mzazi kwenye nyumba yangub nilimleta toka kijijini na dada wa kazi hivi vyote mke wangu hakuvijua
Mwaka 2023 kipindi cha likizo za watoto shule niliwasafirisha watoto kijijini na nyumbani alibaki mke wangu peke yake na siku moja nilimuaga nasafiri kwa muda wa wiki moja lakini kiukweli mimi sikusafiri. Nilienda tu nikakodi nyumba ya wageni nikala tu peke yangu nikamtafuta boda boda ambae ni jirani yangu nikampa kazi hiyo kwamba nitamlipa afatilie muda wote hata kama ni usiku wa maneno awe macho nilimuahidi laki 2 hiyo siku ikapia bila kuambiwa chochote na huyo boda alikesha akifatilia
Siku ya pili.yake saa tano za usiku aliona mwanaume akielekea kwangu na huyo mwanaume alipokaribia ndani kwangu akamuona na mke wangu akitoka ndani na kwenda kumpokea huyo mwanaume na alimpokea kwa kumrukia kifuani na kuanza kunyonyana ulimi hapo nje baadae wakaingia. Ndani
Mimi nikiwa huko nyumba ya wageni nikitafakari usaliti ninaotendewa na mke wangu huyu mtumishi. Wa MUNGU na nikiwa naiangalia pete yangu ya NDOA aliyonivalisha yeye gafla niliona simu ikiita. Muda. Huo ni saa sita ya usiku akaniambia popote ulipo njoo haraka sana tembea mwendo wa ngiri maneno ya Boda hayo tayari mgoni wako ameingia ndani kabisa nilitoka nje ya hiyo gest kwa bahati tu wakati natoka nje ya gest nikaona boda anapita nikamuita akanipeleka fasta nyumbani kwangu maana hata hivyo hakukua mbali sana kwa boda dakika 5 tu nilipofika kwanza nilinyata nikazunguka nyuma ya nyumba yangu yani my GOD nilisikia sauti za mahaba chumbani kwangu. Kitandani kwangu nikarudi mlangoni nikagonga mlango nikiwa na boda wangu akiwa amevaa kofia iliyyofunika. Uso mzima huwezi kumjua
Nilipogonga mlango alitoka mwanaume akiwa amejifunga khanga ya mke wangu na kifua wazi aliponiona alikimbilia chumbani wakati huo nina panga sina nia ya kumzuru mtu ila ni kujilinda tu maana niliona nimevamiwa ndani kwangu
Tuliingia mpaka ndani chumbani mke wangu akiwa uchi nikamwambia vaa kanga tukawatoa wote sebuleni na wote wamejifunga kanga tu hawana nguo ndani
Nilimpigia cm baba na mama yake mzazi nikawaomba waje haraka na nilimpigia cm baba. Yangu mdogo na binamu yangu na wao wakaja na nilimpigia cm wazee wakanisa watatu wawili wa kiume na mmoja wakike wote wakaja na nilimipigia cm mchungaji wetu nae akaja japo mchungaji alitaka kukataa kuja nilimsihi sana akaja walipofika kwa macho yao walijionea na nilitaka waje watu wote wa karibu yangu ili tu ushahidi ukamilike
Baba wa mke wangu Alilia sana kuona mtoto wake alichokifanya ila mchungaji akasema haoni kama mgoni wangu kafanya kosa nilishangaa mno ila wazee wakanisa wakasema hili ni kosa na watengwe na kuomba msamaha ila mchungaji akasema haoni kosa la kuwatenga
Ndugu zangu mabibi na mabwana mimi niliongea pale nikasema yote kwa yote nina mshukuru MUNGU amenionyesha nimeona na nyinyi mmeona mimi mke wangu sitamfukuza ila mimi ndio naondoka
Nilichukua nguo zangu tu na nguo za watoto nikaondoka niliacha vyote nikamuachia nikaondoka
Usiku huo wote tuiondoka tukawaacha watatu tu mke wangu na mgoni wangu na mchungaji. Walichoongea hatujui jumapili ilipofika nilienda kanisa ila mke wangu na mgoni wangu sikuwaona wale wazee wa kanisa walijiuzulu wakabaki washirika tu wa kawaida ila mimi. Nilimsihi MUNGU anipe tu amani ya moyo
Ndugu zangu mabibi na mabwana
Baada ya miezi miwili kupita niliitwa na mchungaji nikaambiwa kuna barua yako unahitajika ukachukue mahakamani nilienda nikaambiwa nisaini karatasi ya talaka nikiwa na Pete yangu ya ndoa niliomba kuja kesho kusaini sikurudi tena mpaka Leo
Sasa kanisani kila mtu amepata tarifa mimi nipo nahudhuria kanisani najifanya sijui kitu. Na nina Pete yangu ya ndoa mkononi baada ya miezi mitatu mbele nikasikia inatangazwa ndoa ya mke wangu na mgoni wangu nilishangaa mno ila nikakaa kimya nikasemea sihami hapa kanisani mpaka nione mpaka mwisho ila watoto niliwahamisha kanisa wakawa wanasali kanisa la…. kibaha
Ndugu zangu mabibi na mabwana ndoa ilitangazwa wiki hii wiki ijayo ndoa ikafungwa na nilifika kanisani ndoa ikifungwa nikiwa na Pete yangu mkononi ya ndoa ndoa ikafungwa na hakukua na tangazo la pingamizi na hata kama lingetolewa nisingesimama maana mimi vyooooote nilishafikabidhi mbele za MUNGU nilifanyiwa ukatili sana na mke wangu na mgoni wangu na mchungaji wangu siku ndoa inafungwa washirika walisusia ilikuwa na jamaa na marafiki wa mwanaume tu na watu baadhi
Ndoa ikafungwa maaharusi wakaenda nyumbani kwa bwana harusi sinza na kesho yake walisafiri kwenda afrika kusini fungati maisha yakaenda nikiwa na Pete yangu ya ndoa sijaivua bado na ninaendelea na maisha yangu na wanangu kibaha
Baada ya miezi 6 ya ndoa yao na mwanamke akiwa na mimba sasa ya ndoa yake mpya yule mgoni wangu alikamatwa uwanja wa ndege wa Dar es salaam akitokea Vietnam akiwa na kilo 5 za madawa ya kulevya hapo ndio kila kitu kiliharibika maishani mwao
Yule mgoni wangu alikamatwa akawa na kesi kila kitu kilitaifishwa kumbe yeye pia alikuwa anabebeshwa madawa na alipangishiwa nyumba sinza waliokuwa wanambebesha madawa wote hawakuonaneka tena mchungaji pia alimkana ndugu wa mgoni wangu wakamwambia mke wangu kuna wanasheria wapo ila hela za kuwapa hakuna uza nyumba ili tuwape watusaidie ndugu yao atoke mke wangu akauza nyumba sikupewa hata hamsini mbovu na ela zote zikaliwa na hakutoka gerezni ukonga na mke wangu sasa ni mjamzito walipokuwa wanaishi sinza akafukuzwa na wenye nyumba kodi iliisha mchungaji alikataa kumpokea akasema atasumbuliwa na polisi mke wangu pakukaa hana baba yake hamtaki na kwao maisha ni ya chini kula kwa shida na mimba yake ikatoka mwanamke huyu akalazwa hospital baba yake na mama yake wakauza kieneo wakamlipia bili ya matibabu akatoka
Ndugu zangu mabibi na mabwana baada ya miezi 3 yule mgoni wangu akiwa gerezani ukonga alifariki dunia ndugu zake wakachukua mwili wakazi mke wangu sasa akiwa amedhoofika na ugumu wa maisha na anaishi kwa rafiki yake ambae ni. Mama ntilie vingunguti siku moja nikiwa naingia kanisani niliona mtu ameniangukia miguuni akilia na kuomba msahamaha akisema anakaribia kufa anaomba nimsamee ili tu awe salama mbinguni ndio maneno yake NIKAMWAMBIA NILIKUSAMEE TOKA ILE SIKU YA KWANZA UWE NA AMANI MAANA NA MIMI NINA AMANI SASA baada ya wiki mbili mke wangu alifariki tumezika miezi minne iliyopita nikachukua mwili nikalipa garama zote nikatafuta mahali tukamuhifadhi nikaleta watoto wakamuona mama yao kwa mara ya mwisho .
Ndugu zangu mabibi na mabwana
NIKANAWA MIKONO NIKAMSHUKRU MUNGU NIKAVUA PETE YA. NDOA NIPO NAMGONJWA BWANA
NILIAMUA KUCHAGUA AMANI NA USHINDI NIKAWAACHIA WAO NA MWISHO WA SIKU NI MUNGU NDIO ALIYONISHINDIA

