NILIENDA SAFARI YA KIKAZI, NIMERUDI NIMEMKUTA MKE WANGU ANA MIMBA YA MWANAUME MWINGINE
Habari ndugu syaga james?? Ninaomba ufiche jina langu, kisa changu ni Kama ifuatavyo: Mim ni mwanaume wa miaka 37 ni baba wa watoto watatu, wawili wakiume wa mwisho ni wa kike. Kidogo mimi na mke tuko mbalimbali kulingana na utafutaji wa maisha, namaanisha mke wangu yuko mkoani kwetu yaani nyumbani, na mimi niko nje ya mkoa huo, ila huwa ninawasiliana na mke wangu kuhusu familia na mambo yanaenda vizuri tuu. Kikawaida kila mwezi huwa nakuja mara moja, ila kuna kipindi nilikaa muda mrefu bila kurudi kama miezi miwili hivi ni kutokana na mapambano ya kazi, ilipopita miezi miwili nikarudi nyumbani na kuwakuta wote wako salama.
Ila nikimuangalia mke wangu naona kabadilika sana, yaani yuko kama mjamzito, nikamuuliza mbona sikuelewi??mbona uko kama mjamzito?? Hapo akashtuka misamaha ikaanza kuwa mingi, akaanza niambia naomba unisamehe kwani kuna siku nilitoka nje na sikujua kama niko kwenye hatari.
Akaendelea kusema baada ya kukutana na huyo mwanaume kumbe mimba ilikamata na pia akadai hakuwa na roho ya kikatili ya kuitoa ile mimba, jamani nilichoka isitoshe niliumia mnoo kitu ambacho sitakaa nisahau maisha yangu yote, nikamwambia kama uliamua kunichiti ndio uniletee mpaka mimba ndani kweli??
Ameishia kulia na kuomba msamaha, pia uvumilivu ulinishinda nikaamua kumrudisha kwao na kuwaeleza wazazi wake juu ya kile kilichotokea, akiulizwa mimba ni ya nani anasema huyo mtu hakumjua jina vizuri, wala hakumpa namba za simu, hivyi kweli unaweza date na mtu bila kumjua na kuwa na namba yake??
Hapa wazazi wake na ndugu zake wamebaki kunibembeleza kumuombea msamaha ila mimi binafsi nimekataa na kumuona huyu mwanamke kama muuaji na anaweza niuwa nikiendelea nae kwa hichi alichonifanyia, je ingekua ni wewe ungefanyaje?? Ungesamehe ulee mtoto wa mtu maisha yaendelee?? Maana naambiwa nipige moyo konde kitanda hakizai haramu ila mimi nimeshindwa nikikaa na kufikiria naumia mnoo, kwani hakuna alichokua anahitaji akakosa jamani.

