NI WEWE TU (ONLY YOU)
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Sehemu Ya 4
Ilikuwa ni kama alikuwa akiingia vitani, alijua dhahiri kwamba Jackline alikuwa na mpenzi lakini alihitaji kushinda vita hivyo na kumpata.
Alijua udhaifu wa wanaume wanapokuwa na wanawake kwa kipindi kirefu, alijua jinsi walivyokuwa wakichoka na hata kule kujali kunavyopungua, kwa kuwa alilifahamu hilo, alitaka kumuonyeshea Jackline kwamba yeye alikuwa mwanaume wa kipekee sana, aliyemsikiliza, aliyemchekesha na hata kumfariji.
Alichokifanya ni kumpa Jackline usumbufu, kila wakati alikuwa akimpigia simu na kuzungumza naye, wakati mwingine alikuwa akichati naye huku akimwambia mambo mengi kuhusu maisha.
“Jackline, nikuulize swali?” aliuliza Daniel baada ya wiki ya kwanza kupita tangu waanze kuwasiliana.
“Niulize!”
“Unaijua picha halisi ya mapenzi moyoni mwako?” aliuliza.
“Unamaanisha nini?”
“Yaani nguvu ya mapenzi ilivyokuwa kubwa moyoni mwako!”
“Ndiyo! Naijua.”
“Unakumbuka siku za kwanza ulipokutana na mpenzi wako na kuanza uhusiano?” aliuliza.
“Nakumbuka!”
“Mapenzi yake yalikuwaje?”
“Mmh! We acha, yalikuwa ni balaa…”
“Bila shaka alikuwa akikutafuta kwa siku kila dakika!”
“Exactly” (kabisa)
“Mpaka meseji mia mbili mliziona chache!”
“Yaani we acha tu!”
“Na sasa hivi? Yapo vilevile?”
“Mmh! Hapana kwa kweli!”
“Unahisi kwa nini?”
“Labda tumezoeana!”
“Kwa hiyo mkizoeana mapenzi yanapungua? Kujali kunapungua? Na mawasiliano yanapungua pia?” aliuliza.
“Mh! Maswali magumu hayo,” alisema Jackline huku aitoa tabasamu.
“Jackline! Mapenzi yana nguvu sana, unapoambiwa kwamba mtu anajiua kwa ajili ya mapenzi, usichukulie kawaida, mapenzi yanaleta stress, picha ya mapenzi ni kubwa mno.
“Siku ya kwanza ulipoanza kumpenda mpenzi wako, ile ndiyo picha halisi ya mapenzi, ile ndiyo nguvu ya mapenzi, baada ya kuzoeana, mapenzi yanapungua na mwisho kuondoka kabisa. Sisi ndiyo tunayafanya mapenzi yapungue, ila nguvu ya mapenzi ipo vilevile,” alisema Daniel.
“Inaonekana unafahamu mengi kuhusu mapenzi!”
“Mimi ni masta! Yaani kama chuo cha mapenzi nina PhD,” alisema Daniel na wote kuanza kucheka.
Walizungumza mambo mengi siku hiyo, alichokuwa akikitaka Daniel ni kumteka msichana huyo, alitaka kuwa mtu wa kwanza kumpigia simu asubuhi, na wa mwisho kumpigia simu usiku, alihitaji kuwa mtu wa kwanza kumtakia kula chakula cha mchana na usiku, kwa kifupi, alitaka kumuonyeshea kwamba alikuwa akimjali sana.
Upande wa pili moyo wa Jackline ulianza kubadilika taratibu, kile alichokuwa akikifanya Daniel kilionekana kuanza kumuingia. Kwa siku, Daniel alikuwa akimpigia simu zaidi ya mara kumi, mara kumjulia hali, mara kumtakia chakula chema, mara kumuuliza ni nguo gani alikuwa amevaa siku hiyo, yaani kila kitu alichokuwa akikifanya kilianza kumtenganisha na mpenzi wake.
“Mungu! Naomba unisaidie, sitaki mwanaume yeyote auchukue moyo wangu kutoka kwa Peter,” alisema Jackline.
“Mungu! Naomba unisaidie, sitaki mwanaume yeyote auchukue moyo wangu kutoka kwa Peter,” alisema Jackline.
Wakati mwingine mpenzi wake, Peter alipokuwa akipiga simu alikuwa akiiangalia tu, aliipokea na kumsikiliza. Mwanaume huyo hakuwa mchangamfu kama Daniel, hakuweza kumchombeza kwa maneno matamu kama kijana huyo, aliongea naye na alipokata tu, simu iliyofuata ilikuwa ni ya Daniel.
“Umekwishakula?”
“Leo sijisikii kula!”
“Kwa nini?”
“Nahisi kama naumwa!”
“Pole sana! Labda nikutoe lunch, unaonaje?”
“Lunch? Wapi?”
“Manzese, kuna mama ntilie mmoja anapika chakula safi sana,” alisema.
“Kwa mama ntilie? Manzese?”
“Yeah!”
“Are you serious?”
“Nakutania, naomba tuonane hapo Mlimani City!”
“Marry Brown au KFC?”
“KFC.”
“Sawa. Ndani ya nusu saa nitakuwa hapo,” alisema.
Siku zote hizo walikuwa wakiwasiliana kwenye simu tu, hawakuwa wameonana, kitendo cha kusema kwamba waonane Mlimani City kilimpagawisha Daniel, akakurupuka, akaingia bafuni kuoga harakaharaka na kujiandaa kisha kuondoka.
Daniel hakukisahau kikaratasi kile alichokiandika kwa mara ya kwanza alipomuona Jackline, alikichukua na kukiweka mfukoni, alihitaji kumuonyeshea msichana huyo ili ajue ni kwa kiasi gani alikuwa amempenda tangu siku ya kwanza alipomtia machoni mwake.
Tangu alipoanza kuoga, ni ndani ya dakika ishirini tayari alikuwa Mlimani City katika Mgahawa wa KFC akimsubiria Jackline ambaye aliingia baada ya dakika kadhaa. Haraka Daniel akasimama, akamkaribisha na kumkumbatia, wakakaa.
“Nimechoka sana kukwambia kitu kimoja kila siku,” alisema Daniel.
“Kipi?”
“Kwamba unapendeza sana! Yaani kila siku nikikwambia hivyo, nachoka, basi hata siku nyingine vaa kawaida,” alisema Daniel, Jackline akatoa tabasamu.
“Nashukuru!”
“Na unanukia vizuri sana! Kama Muingereza!”
“Hahah! Una maneno!”
“Sure! Jackline, wakati mwingine nahisi ni kama ndoto kufahamiana na wewe! Najiona muda wowote ule nitaamshwa na kuambiwa niende chuo,” alisema.
“Mimi mbona wa kawaida tu!”
“Najua! Hata Bill Gates anajiona ni mtu mwenye hali ya kawaida kiuchumi!”
“Jamani! Unanifanya nasikia aibu.”
“Hebu angalia macho yako, angalia lipsi zako, angalia mashavu yako, Jackline, nina uhakika hujazaliwa kama sisi, wewe umeshushwa kutoka juu,” alisema Daniel huku akimwangalia Jackline machoni.
“Jamaniiiiiii…”
“Na kama umezaliwa, basi si hospitalini, umezaliwa supamaketi kule Dubai!”
“Hahah! Jamani Daniel!”
“U mzuri sana mpaka unaboa!”
Daniel hakuacha kumsifia Jackline, uzuri wake ulikuwa ukionekana dhahiri, watu wengi waliokuwa mahali pale walikuwa wakimwangalia msichana huyo.
Alipendeza, alivutia na kikubwa zaidi alionekana kama msichana kutoka katika ulimwengu mwingine kabisa. Waliongea mambo mengi mahali hapo, Daniel hakutaka kumwambia kuhusu suala la uhusiano wa kimapenzi, alichokihitaji ni kumuonyeshea jinsi alivyokuwa akimpenda tu.
Daniel hakutaka kuchelewa, alichokifanya ni kuingiza mkono mfukoni na kukitoa kile kikaratasi alichokuwa amekiandika siku ya kwanza alipomuona Jackline na kumgawia.
Jackline akakichukua na kuanza kukisoma, alishangaa, alimwangalia Daniel, akatoa tabasamu, hakuamini kama kweli kijana huyo alikiandika kikaratasi kile siku ya kwanza alipoonana naye.
“Hii ilianza tangu siku ya kwanza, nilikuona kuwa wa tofauti sana,” alisema Daniel huku akiachia tabasamu.
“Kipi kimekuchanganya?”
“Uzuri wako, unatisha sana, yaani kama ni kuumba, nadhani siku hiyo Mungu alitulia sana, alihakikisha hakuna kazi yoyote anayoifanya siku nzima, ni kukuumba wewe tu,” alisema Daniel na wote kuanza kucheka.
“Jamaniiiiiiii!”
Walipomaliza kula, akamchukua na kumpeleka kwenye sinema ambapo kulikuwa na filamu nzuri ya mapenzi na kuingia. Walikuwa pamoja, walitembea pamoja na kukaa pamoja.
Jackline alijihisi tofauti kabisa, alikuwa huru na wakati mwingine hata Peter alipokuwa akipiga simu, aliifunika simu yake, hakutaka kuongea kwani alamini kwamba kama angeipokea, angemvurugia umakini wake kwa mwanaume huyo. Filamu ilipokwisha, wakatoka!
“Tutaonana siku nyingine! Ahsante kwa chakula na ahsante kwa filamu!” alisema Jackline.
“Usijali! Ila na wewe ahsante kwa kukubaliana nami kuja hapa,” alisema Daniel wakati huo walikuwa wamesimama pembeni ya gari alilokuja nalo Jackline.
“Usijali!”
“Kwa hiyo kuonana mpaka Yesu arudi au?”
“Hahaha! Tutaonana tu!”
“Lini? Mwaka kesho?”
“No! Hivi soon. Kuna vitu nitakuwa navyo bize kidogo, ila tutaonana.”
“Sawa. One last thing!” (kitu cha mwisho)
“What is it?” (kipi hicho?)
“Umependeza sana! You look stunning!” (unang’aa)
“Ahsante! Ila usichoke kuniambia hivyo!”
“Haina shida!”
“Sawa. Bye!”
“Bye!” alisema Jackline, akaingia ndani ya gari, Daniel akabaki amesimama nje huku akimwangalia kwa uso wenye tabasamu.
“Mbona huondoki?”
“Nataka mpaka uondoke, nisije kuondoka halafu watu wakakuiba! I have to keep you safe” (natakiwa kukulinda) alisema.
“Ooh! Sawa. Nashukuru kwa kunijali!”
“Nashukuru kwa kuniruhusu kukujali!” alisema Daniel, Jackline akawasha gari na kuondoka mahali hapo huku mwanaume huyo akibaki akiwa amesimama akimwangalia msichana huyo alivyokuwa akiondoka.
***
Japokuwa moyo wa Jackline ulianza kutekwa na kijana Daniel lakini hakutaka kuonyesha ishara yoyote ile. Kwake, alikuwa na mpenzi mmoja aliyekuwa akimpenda kwa moyo wake wote, mwanaume ambaye aliamini kuwa kuna siku angekuja kumuoa, mwanaume huyo alikuwa Peter.
Peter ndiye alikuwa mwanaume wake wa kwanza, walionana nchini Afrika Kusini walipokuwa wakisoma katika Chuo cha Pretoria kilichokuwa nchini humo.
Walipendana! Kwa uzuri aliokuwanao Jackline, wanaume wengi walimfuata na kumtongoza lakini hakutaka kukubaliana nao, kwake, mwanaume ambaye alionekana kuuteka moyo wake alikuwa mmoja tu.
Wakawa pamoja, wakafanya mambo mengi huku wakiwa wanatoka kwenda sehemu mbalimbali. Peter alikuwa na muda wa kuyafurahia maisha yake na mpenzi wake huyo.
Walipokuwa wakirudi Tanzania, walikuwa pamoja, walionyesheana mapenzi kemkem kiasi kwamba mpaka wazazi wa pande zote mbili walijua kile kilichokuwa kikiendelea.
Walipanga mambo mengi maishani mwao na kuahidi kwamba wangeishi pamoja mpaka pale ambapo wangefukiwa ardhini. Walikuwa na imani hiyo na kila mtu aliyekuwa akiwaangalia alijua dhahiri kwamba watu hao wangeishi pamoja siku moja.
Kwa kuwa walikuwa watoto wa matajiri, kila walipokuwa wakirudi nchini Tanzania, walikuwa wakiondoka kwenda Misri katika mapiramidi yaliyokuwa Giza na sehemu mbalimbali kuyafurahia maisha yao.
Hakukuwa na mtu aliyekuwa radhi kumuacha mwenzake, walipenda kupita kawaida. Walipambana, kulipokuwa kukitokea vishawishi vingi, walihakikisha wanashikama na kuvishinda ilimradi tu mwisho wa siku waendelee kuwa pamoja.
Huku maisha yakiendelea kama kawaida, Peter akaanza kuona tofauti kwa mpenzi wake, hakuwa kama alivyokuwa kipindi cha nyuma, yale ambayo hakuwa akitaka kuyaona kwa mpenzi wake, yakaanza kuonekana kitu kilichomtia hofu ya kumpoteza msichana huyo.
Alipokuwa akimpigia simu, msichana huyo hakuwa akipokea na wakati mwingine simu yake ilikuwa ikitumika kwa kipindi kirefu na kila alipokuwa akimuuliza, alimwambia kwamba alikuwa akizungumza na ndugu zake.
Hilo likamfanya Peter kukosa amani, akahisi kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea ambacho Jackline hakutaka kukiweka wazi.
Hakutaka kuliona penzi lao likipotea, alichokifanya ni kuwasiliana na Jackline na kumwambia kwamba walitakiwa kuonana kwani kulikuwa na mambo kadhaa walitakiwa kuyazungumza kama wapenzi.
“leo?” aliuliza Jackline.
“Ndiyo!”
“Mbona umenishtukiza sana mpenzi?” aliuliza msichana huyo kwa sauti nyembamba.
“Dakika kadhaa tu bebi!”
“Jamaniiii!”
“Basi nakufuata!”
Ni ndani ya dakika kadhaa tu tayari Peter alikuwa ndani ya eneo la nyumba ya mzee Mwamanda. Akateremka kutoka kwenye gari lake la kifahari na kuufuata mlango wa kuingilia sebuleni na kuingia ndani.
Kila mtu aliyemuona alifurahi, kijana huyo alionekana kuwa sahihi kwa Jackline, alipendwa kwa kuwa tu alionekana kuwa na penzi la dhati ambalo mwanaume alitakiwa kumuonyeshea mwanamke.
Jackline alikuwa chumbani kwake, aliposikia kwamba Peter amefika, kitu cha kwanza kilikuwa ni kuchukua simu yake na kuzifuta meseji zote alizokuwa amewasiliana na Daniel.
Hilo lilimuuma kwa kuwa kila alipokuwa akimkumbuka kijana huyo alichukua simu hiyo na kuanza kuangalia jinsi walivyokuwa wakichati lakini kwa kuwa hakutaka kuona mpenzi wake akihisi kitu chochote kibaya, akaamua kuzifuta meseji hizo.
Sehemu Ya 5
Hilo lilimuuma kwa kuwa kila alipokuwa akimkumbuka kijana huyo alichukua simu hiyo na kuanza kuangalia jinsi walivyokuwa wakichati lakini kwa kuwa hakutaka kuona mpenzi wake akihisi kitu chochote kibaya, akaamua kuzifuta meseji hizo.
“Mmh! Asije akanipigia simu bure,” alisema Jackline, alichokifanya ni kuibloke namba ya Daniel, yaani kwa kifupi hakutaka kupokea ujumbe wala meseji kutoka kwa mwanaume huyo wakati akiwa na Peter.
Alipohakikisha amerekebisha kila kitu kwenye simu yake, akavaa nguo zake na kutoka chumbani kwake, alipofika sebuleni, akamkumbatia mpenzi wake na kutoka.
Ndani ya gari Jackline akajifanya kuwa na furaha isiyokuwa na kifani. Alitaka kumuonyeshea mpenzi wake kwamba hakukuwa na kitu chochote kilichokuwa kikiendelea upande wa pili.
Kile kikampa upofu Peter na kuona kwamba hakukuwa na kitu chochote kibaya kilichokuwa kikiendelea kwa mpenzi wake. Waliendelea na safari mpaka walipofika katika mgahawa wa kishua wa Brown Dolphin uliokuwa Masaki, wakaingia na kuanza kupata chakula.
“Kuna kitu gani kinaendelea mpenzi?” aliuliza Peter huku akimwangalia Jackline, wakati huo walikuwa wamekwishamaliza kula.
“Kivipi mpenzi?”
“Yaani naona kama kuna mabadiliko yameanza kujitokeza, kuna nini?” aliuliza Peter huku akimwangalia mpenzi wake huyo.
“Hakuna kitu!”
“Una uhakika?”
“Yeah! Kwani kuna lolote lile?”
“Kama hakuna haina shida. Unajua wakati mwingine nakuwa na wasiwasi sana,” alisema Peter na kuanza kucheka.
Mwili wa Jackline ulikuwa mahali hapo lakini akili yake ilikuwa kwa Daniel. Ni kweli Peter alikuwa kijana mzuri, tajiri lakini kila alipokuwa akiongea naye, alionekana kuwa tofauti kabisa.
Mwili wa Jackline ulikuwa mahali hapo lakini akili yake ilikuwa kwa Daniel. Ni kweli Peter alikuwa kijana mzuri, tajiri lakini kila alipokuwa akiongea naye, alionekana kuwa tofauti kabisa.
Alikuwa mwanaume wa usiriazi kila walipokuwa, alikuwa mwanaume ambaye hakutaka kumfurahisha, hakupenda utani tofauti na Daniel ambaye alijua kumfanya mwanamke kucheka na kujiona wa thamani katika dunia hii.
Walizungumza na walipomaliza, wakaondoka. Jackline alipofika nyumbani kwao, akajifungia chumbani kwake na kulala kitandani, kitu alichokisubiri kilikuwa ni simu kutoka kwa Daniel tu.
Alisubiri, wakati mwingine aliichukua na kuangalia jina lake, alitamani kumpigia lakini akasita, hakutaka kabisa kumuonyeshea mwanaume huyo kwamba hata na yeye alikuwa ameanza kuzimika.
Alimmisi Daniel lakini hakutaka kumpigia simu, alihisi kama angeonekana dhaifu hivyo kusubiri simu ya mwanaume huyo. Muda ulizidi kusogea, dakika, saa lakini bado simu yake haikuita, na mpaka analala, hakupokea simu kutoka kwa Daniel.
Hakulala kwa raha, usiku ulikuwa ni wa mang’amung’amu, kila wakati alikuwa akishtuka na kitu cha kwanza kabisa kuangalia kilikuwa ni simu yake, alihitaji hata kuona meseji ya salamu ili moyo wake uridhike.
Hakuwa amepigiwa simu wala kutumiwa ujumbe wowote ule. Moyo wake uliuma kupita kawaida, hakujua ni kitu gani kilitokea kwa Daniel, na mbaya zaidi hakutaka kumpigia kwa kuwa angekuwa ameonyesha udhaifu kwa mwanaume huyo.
Alikaa siku ya pili, kimya, siku ya tatu ikaingia, napo kukawa kimya. Moyoni aliumia lakini alivumilia, ilipoingia siku ya nne bila kupokea simu wala ujumbe kutoka kwa mwanaume huyo, akaamua kumpigia, hata kama angeonekana dhaifu, alikuwa radhi. Alipopiga tu, simu ikaita na kupokelewa.
“Halo Jackline,” alisikia akiitwa, moyo wake ukapata faraja kubwa kupita kawaida, mtu aliyeongea alikuwa daniel.
“Halo!”
“Nini kinaendelea huko! Naona umeifunga simu yangu, nakutafuta tangu majuzi, sikupati, meseji haziji, tatizo nini? Kuna lolote baya nililokufanyia?” aliuliza Daniel.
Hapo ndipo Jackline alipokumbuka kwamba siku ambayo alikwenda kuonana na Peter aliamua kuifunga simu ya Daniel ili isiweze kuingia kwa kupiga wala meseji, kwa siku zote alizokuwa akisubiri simu ya mwanaume huyo, si kwamba hakuwa akimtafuta, alimtafuta ila simu haikuwa ikiingia.
Alijiona mjinga, alihuzunika, hakuamini kama angesahau kama ilivyokuwa hivyo kuanza kumuomba msamaha kwamba alifanya hivyo kwa kuwa kuna mambo alikuwa akihitaji kuyafanya.
“Ndiyo unibloku?”
“Samahani sana mpenzi!” alisema Jackline, kwa kile kilichotokea, aliamini akimuita mpenzi ingesaidia, alivyofikiria ndicho kilichotokea, moyo wa Daniel ukaburudika na kujisikia faraja.
“Usijali! Nahitaji kukuona!”
“Leo?”
“Ndiyo!”
“Haina shida! Wapi?”
“Unaweza kuja nyumbani?”
“Wapi? Mwenge?”
“Yeah!”
“Sawa haina shida!”
Baada ya kukubaliana, Jackline akakata simu na kuanza kujiandaa. Moyo wake ulikuwa na shauku kubwa ya kukutana na mwanaume huyo, aliumia baada ya kuona kwamba kipindi chote hakuwa amewasiliana na kijana huyo kwa sababu ya uzembe wake.
Kipindi hicho, hakumfikiria tena Peter, kwake, Daniel ndiye alikuwa kila kitu. Alipomaliza kujiandaa, akatoka, akachukua gari na kuondoka nyumbani hapo kuelekea Mwenge alipokuwa akiishi Daniel.
Hakuchukua muda mrefu akafika Mwenge Mataa ambapo akawasiliana na Daniel na kumuelekeza mahali alipokuwa akiishi na kwenda huko. Alipofika, akaelekezwa kuliingiza gari ndani ya nyumba ya akina Daniel na kuteremka.
Wakasogeleana na kukumbatiana kwa furaha, kila mmoja hakuamini kumuona mwenzake mahali hapo. Moja kwa moja Daniel akamchukua na kuelekea naye ndani.
Kwa jinsi Jackline alivyovaa, Daniel alichanganyikiwa, kwake, siku hiyo alionekana kuwa msichana mrembo kuliko wote aliowahi kukutana naye.
Alivalia gauni refu jekundu, nywele zake alikuwa amezibana, chini alivalia viatu virefu kidogo na alikuwa amebeba mkoba wa rangi ya damu ya mzee.
Alikuwa akinukia vizuri kiasi kwamba alipoingia ndani ya nyumba hiyo, n harufu ya manukato yake tu ndiyo iliyokuwa ikisikika kila kona. Walikaa sebuleni kwa dakika chache huku akimtambulisha msichana huyo kwa wadogo zake na dada wa kazi kisha kuelekea chumbani kwake.
Macho ya Jackline yalikuwa yakiangalia huku na kule, kiukweli kwa jinsi Daniel alivyokuwa akiishi na familia yake, walikuwa wakiishi katika maisha ya kawaida sana, hayakufanana na maisha ya akina Peter lakini moyoni mwake hakutaka kuyafikiria maisha hayo kwa sana, kwake, kitu alichokuwa akikifikiria ni kuwa na mwanaume huyo tu.
Waliongea, wakachombezana, wakashikana hapa na pale mwisho wa siku wakabaki watupu kitandani, kilichosikika baada ya hapo ni sauti ya kitanda iliyokuwa ikilalamika.
Jackline hakutegemea kufanya mapenzi na Daniel lakini akajikuta akifanya naye kwa kuwa hakuona kama kungekuwa na mwanaume mwingine ambaye angestahili kufanya naye kwa kipindi hicho.
“Jackline! How do you feel,” (Unajisikiaje, Jackline?) aliuliza Daniel huku akimwangalia msichana huyo usoni.
“Normal!” (kawaida) alijibu msichana huyo huku akionekana kusikia aibu.
“Do you really love me?” (unanipenda kweli?)
“I need some time to answer such a question,” (nahitaji muda kulijibu swali kama hilo) alisema Jackline.
“Why?” (kwa nini?)
Jackline hakulijibu swali hilo, alibaki akiangalia pembeni tu, Daniel hakutaka kumuacha hivi hivi, alichokifanya ni kumvutia tena kwake na kuanza kubadilishana mate.
Wakati huo walikuwa watupu kabisa, kilichotokea ni kuanza kufanya tena mapenzi kitu ambacho kwa Jackline kilimfanya kumpenda zaidi Daniel lakini hakuwa radhi kumwambia ukweli kwamba alikuwa akimpenda mno.
Mtu ambaye alikuwa kichwani mwake ni Peter, aliona kabisa kwamba kulikuwa na kazi kubwa kuachana na Peter lakini kwa jinsi Daniel alivyokuwa akija kwa kasi kichwani mwake, aliona dalili zote kwamba hakuwa na muda mrefu wa kuwa na mwanaume huyo.
Walipomaliza kila kitu, tayari ilikuwa ni saa moja usiku, wakaenda kuoga, walipomaliza, msichana huyo akaaga na kuondoka kurudi nyumbani kwao.
Njiani, akachukua simu yake na kuiangalia, kulikuwa na missed calls nyingi kutoka kwa mpenzi wake, Peter, alikuwa amemtafuta zaidi ya mara kumi lakini hakuwa amepokea kwa sababu simu ilikuwa kwenye ‘silent’ lakini pia hakutaka kuishika kuogopa simu yoyote ya Peter kuonekana.
Alitamani kumpigia lakini akasita, kuzungumza na Peter ilikuwa ni lazima afike nyumbani kwanza ndipo ampigie. Akaiacha na kuendelea na safari yake.
Alimfikiria Daniel, ni kweli aliwahi kufanya mapenzi na Peter lakini kwa mwanaume huyu wa leo alikuwa balaa. Alijua kuuchezea mwili wake, alijua kuzishika sehemu zilizokuwa zikimchanganya, alijua kumlamba sehemu zote mwili mwake, kwa kifupi, kwake, Daniel alikuwa fundi zaidi ya mkandarasi.
“Daniel! You are the man,” (Daniel, wewe ni mwanaume) alijisemea Jackline huku safari ya kurudi nyumbani ikiendelea kama kawaida.
Kutokana na foleni kubwa iliyokuwa njiani, alichukua dakika arobaini mpaka kufika nyumbani, akaliingiza gari ndani, alipolipaki, akateremka na kuelekea sebuleni.
Alipoingia tu, macho yake yakagongana na macho ya Peter aliyeonekana kuwa na hasira mno, mbali ya mwanaume huyo, pia kulikuwa na wazazi wake, wao walikuwa wakimwangalia kwa jicho la kusikitisha, kwa jinsi hali ilivyoonekana, kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea.
“Umetoka wapi?” aliuliza baba yake baada ya salamu!
Jackline alibaki kimya, aliogopa, mahali hapo hakukuonekana kuwa na amani, kuwaambia kwamba alitoka kwa akina Daniel lilikuwa jambo gumu, alibaki akiwaangalia watu wote waliokuwa humo kwa zamu.
“Nimekuuliza umetoka wapi?” aliuliza mzee Mwamanda huku akionekana kukasirika.
Akainuka kwenye kochi na kumsogelea Jackline pale alipokuwa amesimama, alipomfikia, akamzaba kibao. Mzee huyo alikasirika, si kwamba Peter alikuja mahali hapo tu bali msichana huyo aliondoka pasipo kuaga.
Peter alikuwa kimya, moyo wake ulimuuma kupita kawaida, alimpigia simu msichana huyo mara kadhaa lakini haikuwa ikipokelewa, alichanganyikiwa na kuhisi kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea na hivyo kuelekea nyumbani kwao.
Hapo nyumbani alipofika, hakumkuta, roho ilimuuma na kitu ambacho kilikuja kichwani mwake ni kwamba msichana huyo alikuwa na mwanaume sehemu fulani. Aliwaelezea wazazi wake kilichotokea na hivyo kumsubiri.
“Ulikuwa wapi?” aliuliza mzee Mwamanda lakini bado Jackline hakujibu kitu.
Jackline alikasirika, kwa hasira zake, akaondoka sebuleni hapo na kuelekea chumbani kwake ambapo akajifungia na kuanza kulia.
Peter aliyekuwa sebuleni akasimama, akaondoka kuelekea chumbani kwa Jackline, alijaribu kuufungua mlango lakini ulikuwa umefungwa kwa ndani hivyo kuanza kugonga akimtaka msichana huyo amfungulie.
Hakukubali, hakutaka kuzungumza na mtu yeyote kwa kipindi hicho, aliendelea kubaki chumbani huku Peter akiendelea kugonga kwa takribani dakika arobaini na tano lakini msichana huyo hakufungua mlango.
“Mama! Naondoka, nitazungumza naye kwenye simu,” alisema Peter huku akionekana kunyong’onyea.
Akaondoka huku moyo wake ukiwa na huzuni tele, alitegemea kwamba angezungumza na mpenzi wake na kumuuliza kilichokuwa kimetokea lakini ilishindikana.
Akaondoka nyumbani hapo, njiani, Peter alikuwa na mawazo tele, kichwa chake kilifikiria kuhusu kusalitiwa tu jambo ambalo hakutaka kuona likitokea katika maisha yake yote kwa kuwa tu alimpenda Jackline.
Alipofika nyumbani, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kumpigia simu msichana huyo, hazikupokelewa, alipojaribu kumtumia meseji pia hazikujibiwa kitu kilichomfanya kuwa kwenye wakati mgumu kupita kawaida.
Wakati yeye akihuzunika, Jackline alikuwa chumbani kwake akilia, hakupenda kuona baba yake akimpiga kibao mbele ya mpenzi wake, kwake, ile ilionekana kuwa dharau kubwa.
Alikaa chumbani huku akilia, katika kipindi kigumu kama hicho alihitaji jambo moja tu, kufarijiwa na mwanaume, tena asiwe mwingine zaidi ya Daniel ambaye ndiye aliyekuwa moyoni mwake kipindi hicho. Wakati akiwa kwenye huzuni huku akisubiria faraja, mara simu yake ikalia mlio kuashiria kwamba kulikuwa na meseji iliyokuwa imeingia, akaichukua simu, ilitoka kwa Daniel.
“Ulifika salama mpenzi?” aliuliza Daniel kwenye simu kwa njia ya meseji.
“Yeah! Ila nilipigiwa!”
“Na nani?”
“Baba!”
“Kisa?”
“Niliondoka bila kuaga!”
“Pole sana mpenzi!
“Ahsante sana!”
“Nije nikuone?”
“Sasa hivi?”
“Yeah! Umepigwa, sidhani kama ni jambo zuri nikibaki nyumbani na wakati msichana nimpendaye amepigwa!” aliandika Daniel.
“Hapana! Ni usiku sana sasa hivi!”
“Hata ingekuwa saa kumi alfajiri, bado ningeweza kuja kwa ajili yako, naomba uniruhusu mpenzi!” aliandika Daniel.
“Hapana! Kesho mpenzi!”
“Sawa.”
Walichati tu mpaka ilipofika majira ya saa saba usiku. Moyo wa Jackline ulichanganyikiwa kabisa, kwake, Daniel alionekana kuwa kila kitu, yule Peter ambaye alikuwa kwenye moyo wake kwa kipindi kirefu alianza kuondoka na mwanaume huyo mpya kuanza kukalia kiti moyoni mwake.
Daniel alijua kila kitu, kuanzia kujali na hata kufanya mambo mengine ya kumdatisha msichana kama yeye. Hakumfikiria tena Peter na kitu pekee alichokuwa akikifikiria ni kumwambia mwanaume huyo ukweli kwamba hakutaka kuwa naye tena kwa sababu kulikuwa na mwanaume mwingine aliyeingia moyoni mwake.
Hakujua ni kwa jinsi gani angeanza kumwambia ukweli wa kilichokuwa kikiendelea. Alijaribu kufikiria njia nzuri, akawaza kumpigia simu, akaona njia hiyo si sahihi, akafikiria kuhusu kumtumia meseji lakini napo akagundua kwamba jambo hilo si zuri, alichokifikiria mara ya mwisho ni kumwambia kwamba waonane halafu amwambie ukweli kile kilichokuwa kikiendelea.
“Mmh! Nitaweza kweli?” alijiuliza.
Ilikuwa ni lazima afanye hivyo, moyo wake haukuwa na uwezo wa kuwaweka watu wawili na kuwapenda kwa upendo sawasawa, ilikuwa ni lazima mmoja aondoke, na huyo mtu aliyetakiwa kuondoka alikuwa Peter.
Hakutaka kuchelewa, akachukua simu yake na kumpigia, ilipopokelewa, akamwambia kwamba alitaka kuonana naye hivyo watafute sehemu kwani kulikuwa na mambo mengi waliyotaka kuzungumza.
“Kuna tatizo?” alisikika Peter akiuliza.
“Hapana! Ninataka kuzungumza nawe,” alisema Jackline na kukata simu.
Baada ya saa moja, wawili hao walikuwa katika mgahawa wa Jumanji uliokuwa Mbezi Beach, Jackline alionekana kuwa na hofu juu ya kile alichotaka kumwambia Peter. Ni kweli mapenzi kwake yalipungua lakini upande mwingine alimuonea huruma mwanaume huyo.
Alianza naye mbali, alimpenda, alimpa zawadi nyingi, alimfanya kuwa mwanamke mwenye furaha lakini hayo yote yalikuja kutoweka baada ya kumpata Daniel ambaye hakuwa na pesa sana, hakuwa na kitu chochote cha kumpa lakini mapenzi aliyomuonyeshea, jinsi alivyomjali ilikuwa ni tofauti na Peter.
Peter alionekana kuwa na wasiwasi, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea kwa mpenzi wake, alimwangalia, kwa jinsi Jackline alivyoonekana, alionekana kuwa na kitu fulani alichotaka kumwambia mahali hapo.
Walikula na kunywa kwani Jackline aliamini kwamba kama wasingekula, baada ya kuzungumza kusingekuwa na mtu ambaye angekuwa na hamu na chakula.
“Jack mpenzi, kuna nini?” aliuliza Peter huku akimwangalia msichana huyo usoni.
“Peter! Naomba usinielewe vibaya,” alisema Jack, akameza funda la mate na kuendelea:
“Nimekaa na kufikiria sana, naomba usipingane na uamuzi wangu kwa kuwa unaweza kupingana nao na baadaye kujuta,” alisema msichana huyo maneno yaliyomfanya Peter kuwa na hofu zaidi, mapigo yake ya moyo yakaanza kudunda kwa nguvu.
“Peter! Naomba usinielewe vibaya,” alisema Jack, akameza funda la mate na kuendelea:
“Nimekaa na kufikiria sana, naomba usipingane na uamuzi wangu kwa kuwa unaweza kupingana nao na baadaye kujuta,” alisema msichana huyo maneno yaliyomfanya Peter kuwa na hofu zaidi, mapigo yake ya moyo yakaanza kudunda kwa nguvu.
“Kuna nini?” aliuliza huku kijasho kikimtoka.
“Naomba tuachane! Naomba kila mtu aangalie maisha yake,” alisema Jackline kwa sauti ndogo.
Ilikuwa ni sentensi ndogo lakini iliyobeba maumivu makali mno. Peter alimwangalia Jackline, alitaka kuhakikisha kwamba kile alichokisikia ndicho alichokizungumza au alisikia vibaya.
Sehemu Ya 6
“Nimekaa na kufikiria sana, naomba usipingane na uamuzi wangu kwa kuwa unaweza kupingana nao na baadaye kujuta,” alisema msichana huyo maneno yaliyomfanya Peter kuwa na hofu zaidi, mapigo yake ya moyo yakaanza kudunda kwa nguvu.
“Kuna nini?” aliuliza huku kijasho kikimtoka.
“Naomba tuachane! Naomba kila mtu aangalie maisha yake,” alisema Jackline kwa sauti ndogo.
Ilikuwa ni sentensi ndogo lakini iliyobeba maumivu makali mno. Peter alimwangalia Jackline, alitaka kuhakikisha kwamba kile alichokisikia ndicho alichokizungumza au alisikia vibaya.
Akamkazia macho, alihitaji kuona kama msichana huyo alikuwa akimaanisha au alikuwa akimtania, mbali na hiyo pia akafikiria tarehe na mwezi kwani alihisi kwamba ilikuwa ni tarehe ya Siku ya Wajinga dunini, ilikuwa ni tofauti kabisa.
“Unasemaje?” aliuliza Peter huku akionekana kushtuka.
“Peter! Naomba tuachane, nimefikiria sana kuhusu uhusiano wetu, mahali unapokwenda ni kubaya zaidi, kabla hatujafika huko, naomba tuachane,” alisema msichana huyo.
“Tatizo nini? Kuna nini mpenzi? Kama kuna tatizo naomba tulirekebishe,” alisema Peter, alionekana kuwa na hofu, hakuamini kabisa kile alichokuwa akikisikia kwa msichana huyo.
“Hakuna tatizo, ukweli ni kwamba nahisi moyo wangu ukimpenda mtu mwingine zaidi. Najua unaumia kwani najua sana jinsi unavyonipenda na kunijali. Ila Peter, moyo wangu umetekwa na mtu mwingine kabisa, naomba tuachane kwani naamini huko mbele kuna mambo mengi makubwa na mabaya yanaweza kutokea kama tu nitaendelea kuwa nawe,” alisema Jackline, alijipa ujasiri kwani ndicho kilikuwa kitu pekee ambacho kingemfanya kuachana na Peter kwa usalama.
“Tatizo nini?”
“Nimeangukia katika penzi la mwanaume mwingine!”
“Ni nani huyo?”
“Si lazima umjue lakini kuna siku utamjua!”
“Ni tajiri? Ana pesa zaidi yangu? Ni mzuri zaidi yangu?” aliuliza Peter.
“Ni masikini, hana pesa, si mzuri wa sura kama wewe lakini anajali, anasikiliza, ni mcheshi zaidi yako. Wakati mwingine mapenzi hayahitaji pesa Peter, hayahitaji uzuri wa mtu, mapenzi yanahitaji muda, yanahitaji kujaliana Peter,” alisema Jackline.
“Kwa hiyo tatizo ni kwamba sikuwa na muda na wewe?”
“Inawezekana ikawa sababu! Wakati wewe ukiniambia upo bize, kuna mtu alikuwa akinihitaji, hakuwa bize, alinijali sana. Peter, siwezi kuendelea na wewe,” alisema Jackline.
Kwenye kila neno alilokuwa akilizungumza mahali hapo lilionekana kuwa mwiba mkali moyoni mwa Peter. Ni kweli alichokisema, Peter hakuwa na muda naye, alijifanya yupo bize na kazi aliyokuwa ameianza, Jackline alihitaji muda wa kuwa naye, kuongea naye kwenye simu na hata kuchati lakini hakuwa akipata nafasi hiyo.
Akampata Daniel ambaye alimfurahisha, kila alipokuwa akiamka, ilikuwa ni lazima kukuta meseji zake kwenye akaunti yake WhatsApp, mwanaume ambaye alizichukua picha zake nyingi mtandaoni na kumtumia yeye mwenyewe na kumwambia jinsi alivyokuwa mzuri, alivyokuwa na lipsi tamu, jinsi alivyokuwa akimpenda kwa kila kitu.
Jackline hakutaka kubaki mahali hapo. Alifanya kitu ambacho katika maisha yake hakuwahi kufikiria kwamba kuna siku angekifanya. Aliumia kumpoteza Peter lakini aliamini kwamba mwanzo wake na Daniel usingekuwa mbaya kwa kuwa walikuwa wakipendana mno.
Peter alibaki kwenye kiti kama mtu aliyepigwa shoti ya umeme, kile alichokisikia kutoka kwa mpenzi wake hakikuaminika, wakati mwingine alihisi kama alikuwa akiota ambapo baada ya muda fulani angeamka kutoka usingizini.
Alimwangalia Jackline jinsi alivyokuwa akiondoka, hakutaka kukubali, akasimama na kuanza kumfuata, alihitaji kuzungumza naye zaidi kwani kwa maneno yale aliyokuwa ameyazungumza yalimvunja nguvu na kumuumiza mno.
“Jackline mpenzi! Siwezi kukuacha, kama sikukupa muda wa kutosha, naomba unipe nafasi ya pili, naomba unielewe, nipe nafasi ya pili nikuonyeshe jinsi ninavyokupenda,” alisema Peter huku akiwa amemshika mkono Jackline, wakati huo hata watu waliokuwa pembeni walikuwa wakiwaangalia.
“Umechelewa Peter!”
“Never too late.” (sijachelewa)
“Peter! Maumivu unayoyasikia sasa hivi ni madogo kulinganisha na yale ambayo utayasikia hapo baadaye. Naomba tuachane, huu ni uamuzi wangu ambao siwezi kuubadilisha. Mtu akiniuliza kuhusu wewe, nitamwambia kwamba nakupenda lakini naomba tuachane kwa sababu sitaki kumuona mtu ninayempenda akiumia kama ambavyo utaumia baadaye,” alisema Jackline.
“Lakini naomba nafasi ya pili!”
“Hapana! Peter, kwa hilo hapana,” alisema Jackline kwa sauti ndogo, akajitoa mikononi mwa Peter, akalifuata gari lake, akaingia, akaliwasha na kuondoka mahali hapo.
Peter alibaki akiwa amesimama tu, aliliangalia gari la Jackline jinsi lilivyokuwa likiondoka mahali hapo. Alihisi kama mwili wake umepigwa ganzi, kila kitu kilichokuwa kikiendelea kilionekana kuwa kama mchezo fulani wa kuigiza.
Watu walikuwa wakimwangalia, wasichana walishangaa, kijana mwenye sura nzuri kama Peter hakutakiwa kuachwa, alitakiwa kunyenyekewa na mwanamke yeyote yule lakini kilichoshangaza ndiyo kwanza aliachwa.
Peter hakutaka kuendelea kubaki mahali hapo, akalifuata gari lake, akaingia na kuondoka. Alichokifikiria kilikuwa ni kwenda nyumbani kwa akina Jackline na kuonana na wazazi wa msichana huyo tu.
Alihitaji kuwaambia ukweli, kila kitu kilichokuwa kimetokea ili hata kama ingekuwa ni rahisi kuzungumza nao, wafanye hivyo lakini si kumkosa Jackline.
Moyoni mwake, ndani kabisa alikiri kwa kile alichokuwa ameambiwa na Jackline. Hakuwa na muda na msichana huyo, hakumuonyeshea kumjali, hakumuonyeshea upendo ule ambao alitakiwa kumuonyeshea kama mpenzi wake.
Hakumpa muda ambao alistahili kumpa, alijifanya kuwa bize na mambo yake, alijisahau na mwisho wa siku alikuwa akivuna kile alichokuwa amepanda.
Ndani ya gari mawazo yake yalikuwa kwa msichana huyo, alikumbuka nyuma kabisa alivyokuwa ameanza naye uhusiano wa kimapenzi, alimuahidi kila kitu kwamba angempenda mpaka kifo chake, angemjali, angempa muda wake lakini siku chache zilizopita, akayasahau yale aliyomuahidi na kuwa bize na mambo yake.
Hakuchukua dakika nyingi akafika nyumbani kwa akina Jackline, akaliingiza gari ndani, katika sehemu ya maegesho, hakuliona gari la msichana huyo na kuhisi kwamba alikuwa amekwenda sehemu fulani.
Akateremka na kuelekea ndani, akafungua mlango na kuingia. Alipazoea nyumbani hapo, palikuwa kama kwao, alikuwa akija muda wowote aliokuwa akiutaka na hakukuwa na mtu aliyemuuliza lolote lile.
Bahati nzuri kwake ni kwamba aliwakuta wazazi wote wawili. Kwa jinsi alivyoonekana tu, wote wakahisi kwamba kulikuwa na jambo baya lilikuwa limetokea, akawasalimia na kukaa kwenye kochi.
Hakutaka kupoteza muda, akawaambia wazazi wa Jackline kila kitu kilichotokea, jinsi msichana huyo alivyoomba muda wa kuonana naye na kumwambia yake aliyokuwa amemwambia kwamba walitakiwa kuachana kwa kuwa alimpata mwanaume mwingine aliyejua kupenda, aliyejua kujali zaidi yake.
“Yaani Jackline ndiye amesema hivyo?” aliuliza mzee mwamanda.
“Ndiyo baba! Nimechanganyikiwa. Nyie wenyewe mnajua ni kwa jinsi gani ninampenda binti yenu. Moyo wangu umeumizwa mno, wakati mwingine siamini kile alichokuwa ameniambia!” alisema Peter, machozi hayakuacha kutiririka mashavuni mwake.
“Au kuna jambo baya ulimfanyia?” aliuliza mama yake Jackline.
“Hapana mama! Sikumfanyia jambo lolote baya!”
“Sasa inakuwaje awe ameamua uamuzi mgumu namna hii?”
“Hata mimi nashangaa!”
“Basi sawa, tutazungumza naye, tuachie sisi,” alisema mzee Mwamanda.
Moyo wa Peter kidogo ukaridhika, akasimama, akaaga na kuondoka. Akiwa njiani ndani ya gari, akachukua simu yake na kumpigia Jackline, simu haikuwa ikipokelewa. Moyo wake uliuma kupita kawaida, alichoamua ni kumtumia meseji.
“Naomba unisamehe kwa kila kitu!” aliandika.
“Usijali Peter! Nimekusamehe! Najua wewe ni binadamu, wakati mwingine unakosea na unahitaji msamaha pia,” alijibiwa meseji yake.
“Nashukuru kwa kunisamehe!”
“Haina shida!”
“Kwa hiyo?”
“Kuhusu?”
“Kurudiana nami?”
“Hilo ni vigumu Peter. Siwezi kufanya jambo kama hilo!”
“Lakini si umesema umenisamehe?”
“Ndiyo! Nimekusamehe lakini si kurudiana nawe tena. Naomba unielewe Peter. Huu ni uamuzi mgumu sana kuufanya katika maisha yangu, kumuacha mtu unayempenda ni jambo gumu sana, ninahuzunika, ninalia lakini naamini kuna siku nitapata furaha kwa huyu niliyekuwanaye. Nakutakia siku njema,” ulisomeka ujumbe aliouandika Jackline.
Peter aliusoma zaidi ya mara kumi na tano, machozi yaliendelea kutiririka mashavuni mwake, aliumia kupita kawaida, hakuamini kama mtoto wa tajiri kama yeye, mwenye elimu yake alikuwa akipitia maisha yale.
Aliamini katika pesa na elimu kwamba unapokuwa na pesa, hakuna kitu kigumu mbele yako, unapokuwa na elimu hakuna mwanamke yeyote ambaye anaweza kukubabaisha, muda huo ndipo akagundua kwamba pesa si chochote kile, kulikuwa na uwezekano mkubwa wa tajiri kuachwa na kufuatwa masikini.
Elimu aliyokuwanayo haikuweza kumsaidia katika suala la mapenzi, alisononeka, alilia lakini hayo yote hayakubadilisha kile kilichokuwa kimetokea.
Baada ya kufika nyumbani, akaliingiza gari ndani, akalipaki na kuelekea sebuleni. Alihitaji kuzungumza na wazazi wake na kwa sababu hawakuwa wamerudi, akawasubiri mpaka ilipofika majira ya saa mbili usiku ambapo wakarudi na kuanza kuwasimulia kile kilichokuwa kimetokea.
Wao wenyewe hawakuamini, alimfahamu Jackline, alikuwa msichana mrembo ambaye alimpenda mtoto wao kwa mapenzi ya dhati. Alikuwa tayari kufanya kitu chochote kile lakini si kumuacha Peter.
Wakahisi kulikuwa na kitu kilichokuwa kimetokea ambacho hakikuwa sawa, walichokifanya ni kumpigia simu msichana huyo, akapokea na alipoulizwa kuhusu jambo hilo, hakutaka kuwaficha, aliwaambia ukweli kwamba aliachana na mwanaume huyo.
“Kwa nini?” aliuliza baba yake kwa sauti ya chini.
“Baba! Sitaki kumuumiza Peter,” alisikika Jackline.
“Unamaanisha nini na wakati tayari ushamuumiza?” aliuliza mzee huyo.
“Kwa maumivu ambayo atayapata baadaye, ni bora aumue sasa hivi. Baba! Ninatamani Peter awe na furaha, sipendi kumuumiza zaidi ya anavyoumia sasa hivi ndiyo maana ninahitaji awe peke yake, huru kutafuta msichana yeyote yule,” alisema Jackline.
Mzee huyo akaona kabisa Jackline alikuwa mgumu kuingilika, alichohisi ni kwamba kulikuwa na tatizo kwani kwa mtu kama Jackline ambaye alijielewa asingeweza kuchukua uamuzi wa ghafla kama huo.
Akamwambia Peter awaambie ukweli wa kila kitu kilichokuwa kikiendelea, yaani waambiwe sababu yote. Hakuwa na jinsi, huo haukuwa muda wa kuficha ugonjwa, alichokifanya ni kuwaambia maneno yaleyale ambayo Jackline alimwambia.
“Kwamba hukumjali?” aliuliza baba yake.
“Ndivyo alivyoniambia!”
“Hukuwa unampa muda?”
“Hilo nalo aliniambia!”
“Na kweli hukuwa ukifanya hayo yote?” aliuliza mzee huyo.
“Baba! Yaani nashindwa nizungumze nini!” alisema Peter.
Hilo lilikuwa tatizo kubwa kwenye mahusiano, kumpa mwenza muda wa kuwa naye lilikuwa jambo zuri mno ambalo kila mtu alikuwa akilihitaji.
Mapenzi hayakutaka ubize, mapenzi hayakutaka kujificha, ili uwe na mpenzi wako kwa kipindi kirefu ilikuwa ni lazima umpe muda wa kuwa naye.
Peter hakuwa akiyafanya hayo, alimuona Jackline kuwa msichana wa kawaida kwamba hata kama asingemfanyia vile alivyokuwa akitaka bado msichana huyo angeendelea kuwa naye.
Moyo wa Jackline ulichoka na hatimaye akampata mwanaume aliyempa kila kitu, muda na nafasi ya kumsikiliza japokuwa hakuwa mzuri wa sura kama peter wala pesa alizokuwanazo mwanaume huyo.
Peter hakulala, usiku mzima ulikuwa ni wa maumivu makali, alikuwa akijifikiria ni kitu gani alitakiwa kufanya. Hakutaka kumpoteza Jackline lakini kwa kile kilichotokea kilionyesha kwamba yeye na msichana huyo wasingeweza kuwa pamoja tena.
“Ni lazima nipambane! Ni lazima nilirudishe penzi la Jackline kwangu kwa mara nyingine. Kama ni muda, nitampa, nitamjali na kumfanyia kila kitu,” alisema Peter ambaye hakujua kama vile vyote alivyoahidi kumpa msichana huyo, tayari alikuwa akipewa na Daniel.
Mapenzi yalikuwa motomoto, kila mmoja alimuonyeshea mwenzake jinsi alivyokuwa akimpenda. Japokuwa mara kwa mara Daniel alikuwa akienda nyumbani kwa akina Jackline lakini mzee Mwamanda hakugundua kwamba kijana huyo ndiye aliyemchanganya binti yake na kumuacha Peter.
Kwake alimchukulia kama daktari ambaye mara nyingi alikuwa akifika nyumbani hapo na kumwangalia mtoto wake. Muda ambao Daniel alikuwa akienda ni ule ambao mzee huyo hakuwa nyumbani hapo.
Alikuwa akipigiwa simu na Jackline na kuambiwa kwamba mzee hakuwepo hivyo kwenda huko. Hakukuwa na mtu aliyegundua kitu chochote kile mpaka siku moja ambapo mama yake aliwafuma chumbani kwa Christopher wakiwa wamekumbatiana.
Mwanamke huyo alishtuka, ni kama aliona kitu cha ajabu mbele yake, kile kilichokuwa kimetokea kiliuchanganya kchwa chake na kuhisi kama alikuwa akiota.
Hakuamini kuwaona wawili hao wakiwa wamekumbatiana, alichokuwa akikijua ni kwamba hawakuwa na mazoea ya karibu sasa iweje wafikie hatua ya kukumbatiana kama ilivyokuwa.
Hata kabla hajazungumza kitu chochote, haraka sana Jackline akajitoa mikononi mwa Daniel na kumsogelea mama yake, kwanza akamuomba msamaha kwa kile alichokishuhudia lakini pia akamwambia ukweli kwamba huyo ndiye alikuwa mpenzi wake.
“Unanichanganya! Yaani kujuana juzi tu?” aliuliza mwanamke huyo huku akionekana kuchanganyikiwa.
“Hatukuanza kuonana juzi!”
“Kumbe lini?”
Jackline akaanza kumwadithia mama yake kila kitu kilichokuwa kimetokea nyuma. Wakati huo Daniel alikuwa kimya, aliangalia chini kwa aibu, akahisi kabisa alivuruga kila kitu mahali hapo.
Jackline alichukua dakika kadhaa kumuhadithia mama yake kilichokuwa kimetokea, mwanamke huyo alikuwa kimya tu. Kwa maelezo ya Jackline yalionyesha ni kwa jinsi gani Daniel alikuwa na mapenzi ya dhati kwa binti yake.
Hakuamini kama kungekuwa na mwanaume ambaye angeweza kujitoa kama ilivyokuwa kwa Daniel ambaye alikuwa radhi kupoteza kila kitu lakini si kumuacha Jackline.
“Daniel! Anachokiongea ni kweli?” aliuliza mama yake huku akimwangalia Daniel.
“Ndiyo mama!”
“Una uhakika kwamba unampenda binti yangu?” aliuliza tena huku akiwa amemkazia macho.
“Ndiyo mama! Ninampenda Jackline!” alijibu Daniel kwa kujiamini kabisa.
Hiyo ilitakiwa kuwa siri, hawakutaka mzee Mwambanda ajue kitu chochote kwa wakati huo kwani miongoni mwa watu ambao walikataa katakata kuona Jackline akiachana na Peter alikuwa yeye.
Mara nyingi wawili hao walikuwa pamoja, walikuwa wakitoka na kwenda sehemu mbalimbali kuyafurahia maisha. Kwao, hakukuonekana kuwa na watu wengine waliokuwa wakipendana kama walivyokuwa.
Walibadilishana mawazo na muda mwingi Jackline alimwambia Daniel kwamba angempenda mpaka kufa kwake.
Uhusiano wao haukuwa siri nyumbani kwa akina Daniel, aliwaambia wazazi wake kwamba Jackline alikuwa mpenzi wa maisha yake na alikuwa tayari kumuoa muda wowote ule ambao msichana huyo angependa.
“Daniel!” aliita baba yake huku akimwangalia.
“Naam!”
“Unanishangaza sana. Unamwamini vipi mtu kama huyo msichana, ni msichana wa maisha mazuri, si ndiyo?” aliuliza baba yake.
“Ndiyo!”
“Unadhani hajawaona watoto wa vibosile wote na kukufuata wewe? Hivi Daniel, una akili kweli?” alihoji baba yake.
“Lakini baba…”
“Daniel! Unatakiwa kukua na kuufahamu vema ulimwengu wa mapenzi.” Alisema mzee huyo.
Hakumwamini kabisa Jackline, kwake, wasichana waliotoka katika familia bora walikuwa watu wa tofauti kabisa, wanaoringa na ambao wanaweza kuchukua uamuzi wowote muda wowote ule.
Hakutaka kumuona kijana wake akipotea, alimwambia wazi kwamba huyo Jackline hakuwa na akili ya kuwaacha watoto wa matajiri na kumfuata yeye wa maisha ya chini.
Kwa Daniel hakutaka kuelewa lolote lile, kwake, aliamini kwamba Jackline alikuwa msichana wake wa maisha yake yote hata kama kungetokea kitu gani, angekuwa na msichana huyo maisha yake yote.
Bado Daniel alikuwa akiendelea na masomo yake chuoni, mapenzi yalichukua sehemu kubwa ya maisha yake lakini hakutaka kabisa kuona akimpoteza msichana mrembo kama Jackline.
Aliwaambia marafiki zake kuhusu msichana huyo na mipango mingi aliyokuwanayo kwake, kila mtu alipomwangalia aliamini kabisa kwamba Daniel alikuwa kwenye penzi la dhati kwani kwa jinsi alivyokuwa akiongea, penzi halikujificha hata kidogo.
Siku zikaendelea kukatika. Baada ya miezi kadhaa Daniel akaanza kujisikia hovyo mwilini mwake, akaanza kusikia maumivu makali ya mgongo huku wakati mwingine akijisikia kizunguzungu.
Hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, alichokifanya ni kumwambia mpenzi wake. Jackline aliposikia, moyoni mwake aliumia mno na kumwambia kwamba alitakiwa kwenda kupima.
Hilo halikuwa tatizo, siku iliyofuata akaelekea huko na kupima kawaida, hakukutwa na ugonjwa wowote ule na kuona kwamba inawezekana kulikuwa na tatizo jingine au kama ni ugonjwa ulikuja na kuondoka.
“Ulipima nini?” aliuliza Jackline.
“Maralia, typhord, sina chochote,” alisema Daniel.
“Hivyo tu?”
“Ndiyo!”
“Kingine?”
“Sikupima!”
“Na sasa hivi unajisikiaje?”
“Kidogo afadhali! Nahisi ilikuwa ni ugonjwa wa kupita,” alisema Daniel huku akionekana kudharau alichokuwa akiumwa.
Akapuuzia, hakutaka tena kwenda hospitalini, akajisikia vizuri kabisa hivyo kuendelea na maisha yake kama kawaida. Penzi likawa penzi, wakati mwingine Jackline alikuwa akitoroka nyumbani kwao na kwenda kwa akina Daniel na kulala huko.
Hiyo ilikuwa ni siri kubwa, baba yake hakujua ila mama yake ndiye aliyekuwa akifahamu kila kitu. Hakuwa na cha kufanya, alishindwa kabisa kumzuia binti yake kwenda huko.
Baada ya miezi sita, Jackline akaanza kujisikia tofauti mwilini mwake, akaanza kutapika na mwili kuwa na uchovu mkubwa. Hakutaka kujiuliza hicho kilikuwa kitu gani, jibu lililokuja kichwani mwake ni kwamba alikuwa na mimba.
Hakutaka kubaki na jibu hilo moyoni mwake, ilikuwa ni lazima kwenda kuthibitisha hospitalini, akaenda huko, akapima na kile alichokuwa akikifikiria ndicho ambacho alikutana nacho, akapewa majibu yake, akayachukua na kuangalia, ni kweli alikuwa na mimba.
“Ahsante Mungu,” alijikuta akisema huku akitabasamu. Hakumfikiria baba yake, hakujua ni kwa jinsi gani mwanaume huyo angebadilika na kuwa mbogo, alichokuwa amekiangalia ni kuzaa na mwanaume aliyekuwa
akimpenda, Daniel tu.
***
Moyo wa Peter haukuwa katika hali ya kawaida, bado alikuwa amechanganyikiwa kutokana na kuachwa na msichana Jackline. Alimpenda msichana huyo na kwenye maisha yake hakuona kama angetokea msichana mwingine ambaye angempenda kama ilivyokuwa kwa huyo.
Alichokihitaji sana ni kuonana na mwanaume aliyekuwa amempokonya Jackline kutoka mikononi mwake, alifikiria namna ambayo alitakiwa kuanzia kwani hata kwenda nyumbani kwao alijisikia aibu, hivyo kitu pekee ambacho alikiona kufaa sana ni kumpigia simu ndugu yake na Jackline, Erick.
Simu ikaanza kuita, iliita na kuita lakini haikupokelewa mpaka ilipokatika. Hakutaka kuishia hapo, akapiga tena na tena mpaka simu ilipopokelewa na mwanaume huyo.
Cha kwanza kilikuwa ni kushtaki kwa kile kilichokuwa kimetokea, alimwambia Erick kuwa aliachwa na Jackline kwani aliamua kuwa na mwanaume mwingine kabisa.
Kwa Erick, hakuamini alichokisikia, alihisi kama Peter alikuwa akimdanganya. Alimfahamu kijana huyo, alimpenda mno ndugu yake na muda mwingine alimwambia kwamba kwenye maisha yake hakukuwa na kitu kilichokuwa na nguvu kama mapenzi waliyokuwa wakipendana watu hao.
Sehemu Ya 7
Kwa Erick, hakuamini alichokisikia, alihisi kama Peter alikuwa akimdanganya. Alimfahamu kijana huyo, alimpenda mno ndugu yake na muda mwingine alimwambia kwamba kwenye maisha yake hakukuwa na kitu kilichokuwa na nguvu kama mapenzi waliyokuwa wakipendana watu hao.
Mbali na hayo akaanza kuyakumbuka maneno ya dada yake, aliyakumbuka vilivyo jinsi alivyokuwa akimwambia kwamba kwake, Peter alikuwa ni mwanaume wa ndoto ambaye alikuwa tayari kuolewa naye, kuishi naye mpaka siku ambayo Mungu angemchukua katika dunia hii.
Leo, alikuwa akishtakiwa kwamba Jackline alimwacha Peter, haikumuingia akilini mwake na muda mwingi alihisi kama alikuwa akitaniwa.
“Peter! Hivi unachoniambia ni kweli au?” aliuliza Erick huku akiwa amemsikiliza mwanaume huyo kwa muda mrefu alivyokuwa akijielezea.
“Erick! Siwezi kukuficha! Jackline ameniacha,” alisema.
“Hebu tuonane!”
“Sawa.”
Ni ndani ya nusu saa wakaonana maeneo ya Mlimani City ambapo wakaingia katika mgahawa wa Marry Brown na kuanza kunywa kahasa. Hapo ndipo Peter alipoanza kumuhadithia mwanaume huyo kila kitu kilichokuwa kimetokea.
Erick alikuwa kimya, alimsikiliza Peter kwa umakini kabisa. Kwa jinsi alivyokuwa akiongea, ilikuwa ni rahisi kubaini kwamba mwanaume huyo alikuwa na maumivu makali moyoni mwake.
Aliongea kwa sauti iliyokuwa na uchungu huku macho yake yakimlenga machoni mwake. Alitumia dakika kadhaa, alipomaliza, akanyamaza, akachukua kitambaa chake na kuanza kufuta machozi yaliyoanza kumtiririka.
“Tatizo hasa ni nini?” aliuliza Erick huku akimwangalia Peter.
“Sijajua! Ni maamuzi ya ghafla sana,” alijibu Peter.
“Peter! Dada yangu ana akili sana, hawezi kufanya maamuzi ya kipuuzi ndani ya muda mchache, nahisi kuna kitu, hebu niambie,” alisema Erick.
“Erick! Kama ningekuwa najua chochote, ningekwambia!”
“Unanidanganya! Kama hutaki kuniambia sababu, unadhani mimi nitakusaidia vipi? Hata wakili wako ni lazima umwambie kila kitu kilichotokea ili akusaidie,” alisema Erick.
Peter alipoambiwa hivyo, kwanza akatulia, alichokisema Erick ndiyo ulikuwa ukweli wenyewe, ili ajue ni wapi pa kumsaidia ilikuwa ni lazima amwambie kila kitu kilichotokea.
Hakuwa na jinsi, akamwambia ukweli sababu ya msichana huyo kumuacha kwamba hakuwa akimjali, akimpa muda wala kumsikiliza.
Erick aliposikia hivyo, kwanza akashusha pumzi ndefu na kumwangalia Peter. Alichokisema kilikuwa sahihi kabisa, alimjua dada yake, alimpenda mtu aliyekuwa akimjali na kumsikiliza, kama peter alishindwa kufanya hivyo basi ilikuwa ni lazima kuachwa kama ilivyokuwa.
“Nikusaidie nini hapo?” aliuliza Erick.
“Nahitaji kumfahamu mtu aliyekuwanaye kwa sasa!” alisema Peter.
“Nitamfahamu vipi?”
“Erick, yule ni ndugu yako, sidhani kama kuna ugumu wowote ule,” alisema Peter.
Huo ndiyo msaada pekee aliokuwa akiuhitaji kutoka kwa Erick, alijua kwamba Jackline alikuwa kwenye uhusiano na mwanaume mwingine, alihitaji kumfahamu kwa sura, alihitaji kukutana naye na kuzungumza pamoja ili kama itawezekana basi amwache Jackline ili awe naye.
Hilo lilikuwa gumu kufanyika kwa Erick, alikataa lakini akabembelezwa sana na mwisho wa siku kukubaliana na Peter na hivyo kuanza kumfuatilia dada yake, hasa kwenye suala la namba ya simu.
Aliamini baada ya kuipata namba hiyo ingekuwa ni rahisi sana kwake kumsaidia Peter, alimfuatilia na siku ambayo aliisahau simu yake, haraka sana akaichukua, akaenda sehemu ya simu zilizotoka, akaliona jina lililoandikwa Hubby, hakutaka kujiuliza, alijua kuwa huyo ndiye mwanaume aliyekuwa akitoka naye kimapenzi, akaichukua namba ile.
Haraka sana akawasiliana na Peter na kumpa namba hiyo. Kwa mwanaume huyo ilikuwa ni furaha tele, hakukuwa na kitu alichokuwa akikihitaji zaidi ya namba hiyo.
Haraka sana akampigia simu na kuanza kuzungumza naye. Aliumia kuongea naye lakini hakuwa na jinsi, alijitambulisha na kumwambia kwamba alihitaji kuonana naye kwani kulikuwa na kitu muhimu alitaka kuzungumza.
“Kuhusu nini?” aliuliza Daniel.
“Naomba tuonane!”
“Sawa, ila ninahitaji kufahamu ni kuhusu ninI!” alisema Daniel.
“Kuhusu Jackline!”
“Amefanyaje?”
“Naomba tuonane na tuzungumze. Cha muhimu ni kwamba hutakiwi kumwambia kama tunaonana,” alisema Peter.
Kwanza Daniel akahisi kitu, aliona kabisa kama kulikuwa na mchezo uliotaka kuchezwa, alianza kwa kukataa lakini kwa kuwa Peter alikuwa na ushawishi mkubwa, hakuwa na jinsi, akakubaliana kuonana naye.
Jioni ya siku hiyo wakaonana katika mgahawa wa The Prince uliokuwa Masaki na kuanza kuongea. Hakutaka kumficha, alimwambia kuhusu uhusiano wake na Jackline ulivyokuwa, alivyompenda na mpaka siku ya mwisho alipoachwa na msichana huyo kuwa na Daniel.
Kwa jinsi alivyokuwa akizungumza ilikuwa ni rahisi kuona ni kwa namna gani Peter alikuwa ameumia moyoni mwake. Daniel alikuwa kimya tu akimsikiliza mwanaume huyo alivyokuwa akiongea kwa hisia kali.
“Nimekusikiliza sana, unataka nikusaidie nini?” aliuliza Daniel baada ya Peter kumaliza kuzungumza.
“Ninahitaji uniachie Jackline wangu,” alisema Peter.
Daniel akashtuka, hakuamini kile alichokisikia kwa mwanaume huyo. Mpaka kufikia hapo akagundua ni kwa jinsi gani mwanaume huyo alivyokuwa amekufa na kuoza kwa Jackline.
Kwake, kumuacha Jackline lilikuwa suala gumu mno, alimpenda kupita kawaida na kitu ambacho kilimpa furaha ni kwamba msichana huyo alikuwa na ujauzito wake.
“Peter! Hilo ni jambo gumu sana, unazungumzia kitu kigumu kufanyika,” alisema Daniel huku akimwangalia Peter.
“Daniel! Nakuomba, najua unampenda sana Jackline, naomba uniachie msichana wangu, ninampenda, bila yeye siwezi kuishi, naomba unionee huruma, Daniel, naomba unionee huruma,” alisema Peter huku akiikutanisha mikono yake juu ya meza kama kumuomba mwanaume huyo.
“Siwezi kumuacha! Jackline ana mtoto wangu tumboni,” alisema Daniel.
“Daniel! Si tatizo, nitamlea mtoto wako, ila ninaomba sana uniachie Jackline wangu,” alisema Peter huku akiendelea kumuomba mwanaume huyo.
Daniel hakukubali, alijua kabisa kwamba Peter alikuwa akimpenda Jackline lakini hakudhani kabisa kama alikuwa akimpenda msichana huyo kama alivyokuwa akimpenda yeye.
Hawakufikia muafaka japokuwa Peter aliahidi kumgawia kiasi cha shilingi milioni ishirini kama tu angekubaliana naye kuachana na Jackline.
Baada ya kuongea kwa dakika kadhaa, Daniel akaaga na kuondoka mahali hapo huku akimuacha Peter akiwa kwenye maumivu makali.
Alipofika kwenye Bajaj tu kitu cha kwanza kilikuwa ni kumpigia simu Jackline na kumsalimia. Alitamani kumwambia kuhusu kile kilichokuwa kimetokea lakini alisita, hakuona kama kulikuwa na umuhimu wa kufanya kitu kama kile.
“Upo wapi? Kwenye daladala?” alisikika Jackline akiuliza.
“Nipo kwenye Bajaj! Upo nyumbani?”
“Ndiyo mpenzi!”
“Naomba nije nikuone!”
“Nyumbani?”
“Ndiyo! Kwani baba yupo?”
“Hayupo!”
“Basi nakuja!”
Hakutaka kuelekea nyumbani kwao, alichokifanya ni kumwambia dereva Bajaj kwamba safari ilibadilika na hivyo walitakiwa kuelekea Mbezi Beach. Hilo halikuwa tatizo, dereva akakata kona na kuanza kuelekea huko.
Moyo wake ulikuwa na mawazo kuhusu Peter, aliogopa kwa kuona kuwa kama mwanaume yule alikuwa akimpenda Jackline kiasi kile basi kama asingeongeza nguvu ya kumpenda zaidi basi angeweza kupokonywa kitu ambacho hakutaka kabisa kuona kikitokea.
“Nitapambana! Siwezi kushindwa kulilinda penzi langu, nitapambana mpaka mwisho, yaani mpaka namuoa,” alisema Daniel wakati Bajaj ilipokuwa ikikaribia kwao.
Daniel akaonana na Jackline, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kumsogelea msichana huyo, alipomfikia, akamkumbatia na kumpiga mabusu kadhaa mashavuni mwake.
Moyo wake ulikuwa katika amani kubwa, kila alipokuwa na msichana huyo alijihisi kabisa kuwa huru, amani na furaha kubwa moyoni mwake. Alimwangalia Jackline, alionekana kuwa msichana mrembo mno, alimpenda kwa mapenzi ya dhati yaliyokuwa moyoni mwake.
Walikumbatiana kwa dakika nzima na ndipo wakakaa chini na kuanza kuzungumza. Muda mwingi msichana huyo alikuwa akilishika tumbo lake, alifurahi kujiona akiwa mjamzito, kwake, kubeba mimba ya Daniel kilikuwa kitu kikubwa alichokuwa akijivunia nacho.
Walibaki sebuleni huku wakiongea mambo mengi, mama yake Jackline alikuwa akiwaangalia tu, moyo wake uliridhika kupita kawaida. Katika maisha yake alikuwa akipamba kila siku kuhakikisha watoto wake wanakuwa na furaha, kama kitendo cha Jackline kuwa na furaha kuwa na Daniel, kwake ilikuwa ni furaha tele.
“Daniel, nadhani ni muda wa kumwambia baba,” alisema Jackline maneno yaliyomshtua Daniel.
“Kumwambia baba! Kuhusu nini?”
“Hiki kinachoendelea!”
“Mmh! Unahisi ni jambo jema?” aliuliza.
“Ndiyo! Hata kama sitomwambia, jua kwamba kuna siku atajua kuwa mimi ni mjamzito!” alisema Jackline.
“Mh! Atasemaje? Anaweza kuniua!”
“Hawezi!”
“Baba yako si mkorofi?”
“Ni mkorofi kiasi lakini haimaanishi kwamba atakuua, niachie mimi, nitazungumza naye zaidi,” alisema Jackline huku akimwangalia Daniel.
Daniel akashusha pumzi ndefu, moyo wake ulikuwa na hofu tele, aliogopa kupita kawaida na muda wote alikuwa akihisi kuwa mzee Mwamanda angemchukia kwa kile kilichokuwa kimetokea.
Jackline hakuishia hapo, akamwambia pia mama yake kuhusu ule uamuzi aliokuwa amefikia. Mama yake alianza kupinga lakini baada ya kumwambia kwamba ipo siku mzee huyo angejua kwa kuwa mimba hakikuwa kitu cha kujificha, akakubaliana naye na hivyo yeye kutakiwa kumwambia mzee huyo jambo hilo.
Wakaendelea kuzungumza kuhusu mambo mengi, Daniel hakutakiwa kuondoka mahali hapo, alitakiwa kusubiri mpaka mzee huyo atakapofika na kuzungumza naye huku yeye mwenyewe akiwa hapohapo.
Alikuwa na hofu kubwa, alikuwa akitetemeka na wakati mwingine kijasho chembamba kilikuwa kikimtoka. Alihofu kwa kuwa aliheshimiana na mzee huyo na hakujua ni kitu gani kingetokea kama tu angemwambia kile kilichokuwa kimetokea.
“Unaonekana kuogopa sana,” alisema Jackline huku akimwangalia Daniel.
“Wewe acha tu! Yaani natamani hata kukimbia,” alisema Daniel huku akililazimisha tabasamu kuonekana usoni mwake.
“Hutakiwi kuogopa kitu! Hebu piga moyo konde,” alisema Jackline.
Waliendelea kupiga stori mpaka muda ambao mzee huyo alipofika nyumbani hapo. Hofu ikazidi kuongezeka kwa Daniel, alikuwa akitetemeka, alisalimiana na mzee huyo huku akitamani hata kukimbia.
“Karibi sana dokta,” alisema mzee Mwamanda huku akionekana kuwa na furaha tele.
“Nimekwishakaribia,” alijibu huku tabasamu lake bandia likiwa usoni mwake.
Mzee huyo akaelekea chumbani kwake ambapo akapitiliza mpaka bafuni na kuoga. Muda huo sebuleni hakukuwa na amani, Daniel alikuwa akitetemeka kiasi kwamba alitamani hata kuaga mahali hapo.
Alimwangalia Jackline kwa macho yaliyoonyesha hofu kubwa, alipokumbuka kwamba aliambiwa mzee huyo alikuwa mkorofi, alitamani hata kuondoka mahali hapo.
“Jackline, naomba niondoke,” alisema Daniel huku akimwangalia msichana huyo.
“Hapana! Hili jambo ni lazima tulimalize leo,” alisema msichana huyo.
“Anaweza kukuua!”
“Kama akikuua, basi atuue wote, ila hakuna kuondoka mpaka hili jambo tulikamilishe,” alisema Jackline.
Waliendelea kukaa sebuleni pale mpaka baada ya dakika kadhaa ambapo mzee huyo akarudi sebuleni hapo na kuanza kuongea.
Alionekana kuhisi kitu, haikuwa kawaida kwa Daniel kuwa nyumbani hapo mpaka muda huo, aliona kabisa kulikuwa na jambo lililokuwa likiendelea hapo nyumbani.
Mama yake Jackline hakutaka kunyamaza, huo ndiyo ulikuwa muda wa kumwambia mume wake kile kilichokuwa kimetokea.
Hakutaka kujiuliza mara mbilimbi, akamwambia ukweli wa kila kitu. Mzee mwamanda alikuwa kimya, alimwangalia mke wake alivyokuwa akielezea na muda mwingine alikuwa akiyahamisha macho yake na kumwangalia Daniel ambaye aliuinamisha uso wake chini.
“Mungu nisaidie,” alijikuta akisema Daniel huku akiwa ameinama.
Mama yake Jackline alimwambia mume wake kila kitu, mzee huyo akashusha pumzi nzito, ndita zikaanza kuonekana usoni mwake, alionekana kushtushwa na kusasirishwa kwa kile alichokuwa ameambiwa.
“Dokta…” aliita mzee huyo.
“Naam baba!”
“Ni kweli umempa binti yangu mimba?” aliuliza.
Daniel akanyamaza, swali hilo lilikuwa jepesi kujibika lakini halikutakiwa kujibika kwa pupa. Akanyamaza kwa sekunde kadhaa na kumjibu mzee huyo kwamba kweli alikuwa amempa mimba binti yake.
“Ndiyo mzee!”
“Ulikusudia nini hasa?” aliuliza mzee huyo.
Daniel akanyamaza, hakutakiwa kulijibu swali hilo. Mama yake Jackline alipoona ukimya umetawala akaingilia na kumwambia mume wake kwamba wawili hao walikuwa wakipendana na lingekuwa jambo jema kama wangewaruhusu kuwa wawili na kuishi pamoja.
Mzee huyo hakuzungumza kitu, akasimama na kumsogelea Daniel pale alipokaa na kumuuliza swali moja tu.
“Unadhani nimefurahi kumuona binti yangu akipata mimba kabla ya ndoa?”
Ilikuwa ni rahisi kusikia mapigo ya moyo wa Daniel kwa jinsi yalivyokuwa yakidunda. Kijasho chembamba kilikuwa kikimtoka huku akizidi kutetemeka.
“Kama kweli umeamua kuwa na binti yangu, usiuumize moyo wake,” alisema mzee huyo, alipomaliza kusema maneno hayo, akaondoka kuelekea chumbani kwake.
Daniel akabaki kimya, alikuwa akisikilizia hatua za mzee huyo jinsi zilivyokuwa zikilia wakati akiondoka kuelekea chumbani kwake.
Mzee huyo alipoondoka kabisa, Daniel akamgeukia Jackline na kumwangalia huku tabasamu likionekana usoni mwake, akajisikia nafuu, mwili ukarudi katika hali ya kawaida.
“Vipi?” aliuliza Jackline huku naye akitoa tabasamu.
“Mh! Unaweza kufa!” alisema Daniel na wote kuanza kucheka.
Waliendelea kukaa mahali hapo huku mama yake Jackline akionekana kuwa na furaha tele, kitendo cha mume wake kukubaliana na Daniel kulimfurahisha kupita kawaida.
Ilipofika majira ya saa mbili usiku Daniel akaaga, akatoka nje, wakati wakiingia ndani ya gari, akaanza kujiskia kizunguzungu, akashindwa kupanda, akaushikilia mlango, kuunyanyua mguu tu akashindwa, hapohapo akaanguka chini.
Jackline akashtuka, haraka sana akachomoka upande aliokuwa na kwenda upande ule wa Daniel. Akamuinua pale alipokuwa huku akimuita.
“Daniel…Daniel…” aliita Jackline, Daniel alikuwa kimya.
Jackline alichanganyikiwa, akaanza kumuita mama yake kwa sauti kubwa, mwanamke huyo akafika nje, akamuona mlinzi akiwa amemshika Daniel pale chini alipoangukia, akauliza tatizo, akaambiwa alianguka ghafla.
Hawakujua kilichokuwa kikiendelea, haraka sana wakampakiza ndani ya gari. Kabla hawajaondoka, mzee Mwamanda akatoka ndani, akaanza kuwaangalia huku akionekana kushangaa.
“Kuna nini?” aliuliza mzee huyo.
“Ameanguka!” alijibu Jackline huku akianza kulia.
“Ameanguka?” aliuliza mzee huyo huku akiwasogelea, akamgusa Daniel, haraka sana akawaambia waondoke kuelekea hositalini kwani hali ya Daniel ilionekana si ya kawaida.
INAENDELEA

