MUME WANGU ALINIKATAA, NIKAAMUA KUANZISHA MAHUSIANO NA RAFIKI YAKE
Kaka mimi nashida ninaomba ushauri wako mimi mwaka juzi nilipata mchamba akanitolea mahari tukaanza kuishi wote tukakaa Kama mwezi mmoja akawa ameondoka Maana anafanya nchi za nje na akiondoka anakaa muda mrefu Sana
Sasa kipindi yeye alipoenda Kazi mimi nilienda nyumbani kwetu tutakubaliana wakati nipo kule akanipgia simu na kusema tuachane mimi ni malaya kiukweli niliumia Sana na ukiangalia mimi nimekuwa muaminifu Sana kwa mume wangu alinitukana Sana na kusema mimi kwetu masikini bais mimi nikawa Sina Budi kukubaliana na maamuzi yake
Sasa Kuna siku rafiki yake alinitafuta na kuniuliza kuhusu mahusiano yetu nikamuelezea mwanzo mwisho na akajaribu kuongea nae Maana alipoongea nae akamwambia kuwa hawezi kurudiana na mimi na nikipata mume niolewa basi shemeji yangu ambae Ni rafiki yake Alinifariji Sana hicho kipindi
Alikuwa na .mimi bega kwa bega basi baada ya muda yule shemeji aliomba tuwe wapenzi mimi pasipfikiria nikamkubalia tukaanza mahusiano hicho kipindi mimi nikiwa bukoba yeye Yupo dar kiukweli alikuwa ananipenda kila ninachokitaka alinipa Tena pia tukaanza kufanya kilimo akatumia gharama nyingi Sanaa basi wakati nikiwa nipo nae kwenye mahusiano yule mume wangu aliomba turudiane na aliomba msamaha Sana pia kwa family na kuahidi kumaliza mahari iliyobakia
Mimi nikaamua nirudiane nae na akanitumia nauli nikarudi dar Sasa kilichonileta Ni hiki hapa yule shemeji yangu ameomba tuonane na mimi nimesharudi kwa mume Wangu na mimi naogopa kumwambia ukweli kuwa nimerudi kwa mume Wangu na Kuna baadhi ya vitu ameviwekeza kwangu na ametumia pesa nyingi na nakumbuka Kuna siku aliniambia kwamba nikimsaliti atanifanya kitu kibaya please naomba ushauri nifanye nini?


1 Comment
Spot on with this write-up, I actually think this website wants way more consideration. I’ll most likely be again to read far more, thanks for that info.