MKE WA DUNIA
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU 01
Kwa Majina naitwa Mamy. Ni mtoto wa pili katika familia ya watoto wa tatu. Upande wa malezi Nimelelewa na mama baada ya baba kufariki dunia na kuniacha nikiwa na umri mdogo. Mama alipambana kutulea na kutupa nahitaji muhimu kama kula, mavazi, malazi, elimu.
Maisha ya nyumbani kwetu yalikuwa ya kawaida tu. Mama yangu alikuwa anafanya kazi ya kuuza genge barabara kubwa, biashara ilikuwa nzuri na ndiyo ilivyokuwa inakidhi nahitaji ya nyumbani.
Nakumbuka nilipofika form two ndipo nilianza wenge baada ya kuvunja ungo tu. Nilibadilika gafla na kuwa mtoto mbaya, navyosema mtoto mbaya mnielewe. Yaani nilikuwa sisikii siambiliki, sishauriki. Nilijiona ndo nimekuwa najua Kila kitu na nayajua maisha kuliko wakubwa zangu.
Nikiludi shule ni kudhurura mtaani, sikuwa na muda wa kushika daftal kabisa, naludi shule saa kumi nitakula na kufua nguo za shule baada ya hapo ni kuzurura tu mtaani mpaka saa tatu au saa nne usiku.
Mama alishanipiga mpaka alichoka. Dada yangu alishanisema mpaka alichoka alibaki kuniangalia tu nifanye navyotaka. Kwenye malezi watoto wanaolelewa bila baba tunawapaga tabu sana mama zetu. Na asilimia kubwa watoto wanaolelewa pasipo uwepo wa baba zao ndiyo wanaoongoza kwa baadili mabovu.
Mtaani nilikuwa sishikiki. Marafiki zangu mie walikuwa wakiume tu. Shule napo kesi hazikuisha, sikuwa na akili na pia nidhamu ilikuwa zero.
Nilivuka kidato Cha pili nilifaulu ila nilikataa shule, hapo na bwana wangu ananionga vihela na Kwa kipindi icho nilikuwa nilipewa elfu kumi naona kama laki Moja. Akili za kitoto ni shida jamani. Hata kabda ya miaka kumi na Saba nilikuwa nishatolewa usichana wangu, bwana mwenyewe aliyenitoa usichana wangu aliniacha Kwa dharau kama zote.
Basi baada ya kukataa kuendelea na shule mama alijionea nafuu maana kufahuru kwenyewe ilikuwa bahati mbaya tu na hata ningesema nikomae nimalize form 4 nisingefaulu Kwa akili zile mie nilikuwa nazungusha tu kwenye mitihani ni zero tu. Nikifanya vizuri kwenye mtihani ni marks 20 sijawai kufika 30 hata huo mtihani wa taifa wa form two sijui nilifauli vipi.
Basi baada ya kuacha shule nikawa mtoto wa mtaani ni kigulu na njia Kila sehemu. Hakuna mtaa nilikosa bwana. Nilikuwa Malaya mbwa na hapo hata miaka 18 sijafika ndo kwanza nilikuwa na miaka 16. Kwetu nishashindikana na mara kwa mara niliambiwa ipo siku ujanja wote utaingia mfukoni ila hata sikujali maneno Yao.
Leo nipo mtaa huu kesho nipo mtaa ule, nilijiona mie ndo mie na Kwa uzuri tu MUNGU aliniumba. Mamy nilikuwa mamy kweli.
Basi bwana nikapata bwana wa kunituliza. Alikuwa mvuta Bangi tu alafu ni mvulana mdogo tu wa miaka 20 Hana maisha yoyote, anaishi kwao ila hapo ndo nikapenda kweli kweli na kutulia kabisa. Nikaachana na mabwana zangu wote nikalidhika na huyo mvuta Bangi Abdul. Abdul alikuwa Hana kazi ya maana kiufupi hakuwa na Hela, kipindi nipo na Abdul ndipo nilianza kutafuta kazi ya kufanya. Nilipata kazi ya kuuza duka la vyakula basi nikageuzwa chuma ulete na bwana Abdul( nyie mapenzi ni uchizi haswaaa.
Basi bwana Abdul alikuwa Kila alinifuata dukani usiku wakati wa kuludi nyumbani namfungashia unga, mchele, sukari na maharage anampeleka kwao. Mpaka duka la watu likaanza kupukutika. Nilifanya kazi miezi mitatu tu duka likafilisika mwenyewe alikuwa mstarabu tu sijui alinichukulia akili za kitoto maana hakunilipisha chochote zaidi ya kunilipa yeye mshahara wa mwezi wa tatu na kufunga duka lake.
Nikawa mtu wa home tu na nilikuwa sishindi home kwetu, mie huyo kwa kina Abdul nitashinda huko mpaka usiku saa mbili ndo naludi nyumbani. Kipindi icho mama yake Abdul alikuwa ananijua basi nikajiona ndo mke Tena. Nitawafanyia makazi yote nikiludi kwetu nimechoka nalala kama mfu. Yote hayo kisa nipendwe.
Basi bwana siku hiyo dada yangu alikuja nyumbani maana alikuwa na familia yake yaani mke wa mtu. Baada ya kuja home nikawa nashinda nae. Siku mbili tu nilizoshinda nae dada alihisi kitu.
Ilikuwa asubuhi baada ya kunywa chai nilienda chumbani kupumzika kidogo. Dada alinifuata alikaa kitandani na kuniambia niinuke nikae ana mazungumzo na Mimi. Nilimtii nikainuka na kukaa kitandani.
“Mamy una mimba?”.
“Mimi!”. Nilishangaa na kumuuliza huku najishooshea kidole.
“Ndiyo, niambie mimba ya nani?”
“Khaaa! Dada mie Sina mimba”.
“Subili nakuja”. Dada aliyasema hayo na baada ya hapo alitoka chumbani, dakika 20 saa aliludi Tena chumbani alinikuta nimekaa nipo mbali kimawazo.
“Shika hichi kikopo twende chooni wote, nataka nikusimamie mwenyewe nione unavyokojoa”.
“Khaaa! Kwanini sasa dada unifanyie hivyo?”.
“Nataka nikupime mimba”. Nilikubali shingo upande na hofu ulishanijaa. Tuliingia wote chooni. Nilikojoa huku dada akiwa amenisimamia. Mkojo wa mwisho mwisho niliukingia kile kikopo baada ya hapo tulitoka chooni. Dada alichukua kipimo Cha mimba na kupima.
“Umeona Sasa?”. Dada alinionyesha kile kipimo, mie sikuuelewa chochote kwanza hata sijawai kuvitumia.
“Nini dada?”. Nilimuuliza ila nilishtuka bonge la Kofi la shavu.
“Niambie mimba ya nani mshenzi wewe?”.
“Dada kwani na mimba?”.
“Inamaana ujuo?. Mamy niambie nani aliyekupa hiyo mimba na Sasa hivi mguu wangu mguu wako mpaka kwa uyo bwana ako.
Niliinamisha kichwa chini mapigo ya moyo yalikuwa juu, muda huo mama alikuwa kwenye biashara zake huko barabarani.
“Ya Abdul”.
“Abdul ndo nani, anakaa wapi?”.
“Anakaa hapo mtaa wa tatu dada”. Hapo naongea nimekuwa mdogo utadhani sio Mimi mamy mcharuko.
“Haya simamisha ngwala zako twende kwa huyo Abdul”. Dada alikuwa amepanik kweli kweli. Akili yangu ilifanya kazi kwa haraka, nikajisemea hapa kumpeleka dada kwa kina Abdul na ikiwa hata Abdul mwenyewe hajui kama na mimba yake naweza nikakataliwa kweupe.
“Dada Abdul amesafiri hayupo Kwa Sasa”. Dada aliniangalia kwa hasira na kutoka chumbani.
Haraka nilichukua simu yangu na kumpigia Abdul kumpa taarifa ya mimba. Alipopokea simu nilimueleza kuwa na mimba yake. Wala hakukataa alikubali na kuniambia Kwa Sasa nisiwalete home mpaka aongee na wazazi wake kwanza. Tulikubaliana hivyo.
Usiku mama alipoludi alipewa taarifa na dada. Alisikitika sana aisee. Alinionea huruma maana umri wangu Bado. Miaka 16 tayari na mimba, hakusema lolote zaidi ya kuniambia ndicho nilichokuwa nakitaka Sasa nimekipata.
Basi niliendelea kuwazunfusha nyumbani kwa kuwaambia kuwa Abdul Bado hajaludi. Mimba ilifikisha miezi 3 nilifaa kuanza kliniki ndipo Abdul alijitokeza kwetu. Familia haikuwa na namna zaidi ya kumpokea tu maan hata wangemkataa mimba ndo hiyo nishapewa.
Basi aliambiwa kuhusu kunitolea barua ili kumstili mama yangu. Maana ni aibu kwa familia hasa upande wa baba yetu wangemuambia Hana malezi mazuri ndo maana nimeaeubikiwa kumbe ni mimi tu mwenyewe.
Abdul alikubali kunitolea barua na kuahidi ataileta siku flani. Mpaka mimba inafikisha miezi Saba hakuna Cha barua Wala kishika uchumba na kila nilipomwambia aliniambia kuwa kwa sasa hana Hela ila atatoa tu. Haikuwa Siri tena ndugu wote walijua kuwa Mamy ni mjamzito.
Miezi tisa ilifika. Nilijifungua mtoto wa kiume Kwa njia ya kawaida. Namshukuru MUNGU nilijifungua kwa njia rahisi kabisa tofauti na matarajio ya wengi kutokana na umri wangu. Baada ya kujifungua nilikula uzazi kwetu.
Abdul Hana maisha yupo yupo tu, mama yake ndo akawa na kazi ya kununua vitu vidogo vidogo vya mtoto…Mamy mimi nilikonda, nilipauka uzuri wote kwisha, sina Tena Cha kulingia mjini…..
SEHEMU 02
Mtoto alifikisha miezi mitatu. Abdul alianza kunishawishi nikaishi nae kwao. Nilipomwambia kuhusu kuleta barua nyumbani aliniambia hajajipanga bado. Twende kwanza nyumbani kwao tukaishi wote barua itafuata baadae.
Kwakuwa nilikuwa nampenda sana nilikubali kwenda kuishi nae japo nyumbani hawakuridhia mimi kwenda kuishi ukweni na ikiwa mwanaume Hana ishu yoyote mjini analishwa tu na wazazi wake.
Nilienda nyumbani Kwa kina Abdul Kwa mabavu pasipo nyumbani kuridhia nilifika huko na kuanza maisha mengine nikiwa ukweni. Ikawa mimi ndiye mfanya kazi wao. Jamani nilikuwa natumikishwa kama kijakazi.
Nilivumilia yote kwasababu nilikuwa nampenda baba mtoto wangu. Abdul alianza kujichanganya na Vijana wenzie na kufanya kazi ndogo ndogo. Baada ya muda kidogo baba mkwe alitupa chumba tujitegemee wenyewe kwa Kila kitu. Hapo nimefubaha na nimekonda Kwa mawazo na kumnyonyesha mtoto. Natamani hata kuludi kwetu ila nilifikilia namna nilivyoindoka Kwa mabavu nashindwa.
Tulianza kuishi kwa kujitegemea ndo hapo nilianza kuona Kila rangi kutoka Kwa Abdul baba wa mtoto wangu. Jamani alikuwa muhuni hamna mfano. Unakuta anafanya kazi na analipwa vizuri ila pesa huiyoni kula ya shinda inafikia hatua mpaka naenda kushinda nyumbani kwetu kuanzia asubuhi mpaka usiku ili nipate kula na mwanangu, Abdul alivyo wa ajabu Sasa na aliyokosa hata haya mimi nikienda kwetu na yeye anakuja huko huko kula. Atakuja mchana atakula baada ya hapo ataondoka na kuludi tena usiku kula na baada ya hapo tutaondoka wote kwetu.
Anakuja kwetu hajui kubeba Cha unga Wala sukari. Hali hiyo ilikuwa inaniumiza alifanya kazi Hela hauioni akikosa kazi tutakuja kushinda wote nyumbani. Na mbaya zaidi alikuwa mbahili hajui kuacha matumizi hata kama akiwa na Hela yeye ndo atakayeenda dukani kununua mafuta, unga, nyanya na kila kitu, ilikuwa ni aibu hata mtu atokee aseme anaomba nimuazime mia mimi hiyo mia sina labda ya kuchora.
Yote hayo nilivumilia na kuamini ipo siku atabadilika ila ndo nilizidi kufumaa acheni tu, ilifikia hatua hata pesa ya kunyoa nywele ni shida jamani elfu Moja tu kunipa ili nikanyoe nywele anasema Hana eti mwanamke hapendezi kunyoa. Nikimwambia anipe ya kusuka basi ataniahidi kunipa ila ndo usahau kabisa.
Siku Moja dada yangu mkubwa alikuja nyumbani kusalimia. Nilienda kumsalimia alishangaa baada ya kuniona nilivyo. Alinikalisha chini na kunihoji nini tatizo.
“Umepatwa na nini mamy mbona umekonda hivyo, alafu mtoto hamumpi lishe huyu?”. Niliinamisha kichwa chini, ni kweli mwanangu hakuwa na lishe na tayari alifikisha miezi 9, mtoto mkavu yaani mwembamba sema uzuri alikuwa mchangamfu sana.
“Niambie shida nini mdogo wangu?”.
“Amna dada sema maisha tu magumu acha tu. Nilimueleza dada maisha nayoishi na mwenzangu alibaki mdomo wazi”.
“Khaaa! Kwaiyo mpaka anakufukuza jamani jamani”.
“Ndiyo ananifukuza ananiambia niludi kwetu ila dada mtoto Bado mdogo mimi siwezi peke yangu. Nimechoka ila navumilia kwaajili ya mwanangu tu”.
“Unataka kuludi nyumbani ila mtoto ndiye anayekukwamisha?”. Dada aliniuliza.
“Ndiyo dada. Natamani kuludi ila mtoto kama unavyomuona. Bado mdogo sitoweza kumlea mwenyewe. Sina Hela sina kazi pia”.
“Kama tatizo ni mtoto basi Wala sio shida kabisa. Mtoto atakuwa tu ila manyanyaso hayavumiliki mdogo wangu. Wewe fikilia hapo hajakuoa anakunyanyasa hivyo na kukusimamga. Najua unanyonyesha na mtoto hana lishe anategemea maziwa Yako sana sana huo uji wa Dona ushamkataa mtoto hakui alafu Bado anakusimanga unakula sana na maneno kibao”.
Yaani Abdul alikuwa ananisimanga acheni tu. Mala mchafu, mala unakula sana, si uludi kwenu kwani umefukuzwa , hapo Bado Malaya mbwa.
“Hapana mdogo wangu. Ni sawa ulikosea mwanzo ila mtoto akinyea mkono huwezi kuukata. Ludi nyumbani tu. Yaani Mamy uzuri wote umeisha umekuwa kama mstimu jamani. Alafu si ni yeye aliyelazimisha mkaishi wote kwao?, Sasa Kwanini akutese hivyo. Dada aliongea kwa masikitiko.
“Kama mtoto tutapambana kumlea na atakuwa tu. Umri wako Bado mdogo na unayopitia hustahili. Naamini imejifunza na siku nyengine utakuwa makini”.
Tuliongea sana na dada aliniambia mama akiludi ataongea nae na siku hiyo nililala kwetu. Majira ya usiku mama aliludi na baada ya chakula Cha usiku ndipo dada alimueleza mama maisha yangu. Mama alisikitika sana na kupitisha maamuzi ya mimi kuludi nyumbani.
“Unafukuzwa umeng’ang’ania tu kwani hapa tulikufukuza Mamy wewe”. Mama aliongea mwa masikitiko.
“Kesho uende ukachukue nguo zako na Kila kitu chako na Cha mtoto uludi hapa nyumbani”. Mama alichukua haswaa. Yaani Abdul na kumvumilia kote ila Bado alikuwa ananifukuza loooh!.
Kesho nilienda kuchukua nguo zangu, sikumkuta abduli. Nilibeba Kila kilicho changu na mwanangu huyo nikaondoka nyumbani kwetu. Usiku Abdul alipoludi hakukuta nguo zangu Wala za mtoto. Alinipigia simu nilipokea na kumwambia nimeamua kuludi kwetu tu, atafute kwanza maisha. Alipaniki mpaka nilishangaa, unaweza sema sio yule aliyekuwa ananifukuza.
Usiku huo huo alikuja nyumbani kunifuata akakutana na dada yangu. Dada mchambaji yaani dada yangu anachamba haswaaa!. Walimkaribisha vizuri na baada ya Salam ndipo Abdul alianza kuongea.
“Mamy amekuja huku bila kuniaga na naona ameamua kubeba nguo zake zote sijui ana maana gani?”.
“Kwanza samahani. Nikuulize tu swali dogo. Ulimchukua mdogo wangu akiwa hivi alivyo sasa?”. Dada alimuuliza swali abdul alinyamaza kimya”.
“Wewe mbona umependeza?, mbona umenyoa vizuri?, muangalia Mamy kichwani alivyo. Mamy ebu vua huo mtandio”. Nilivua mtandio. Jamani manywele yalikuwa marefu na yameshonana kichwani kama mchwa na ilifikia wakati kuchana ilikuwa shida maana zilikuwa zinauma balaa. Nikawa navaa mtandio.
Abdul aliona aibu aliinamisha kichwa chini. Dada alimchamba siku hiyo. Jamani alichambwa mpaka nilimuonea huruma.
“Yaani hata akiomba umnulie juice ya mia tano utaanza kumsimanga sijui hauna malengo na maisha. Juice ya mia tano inakuzuia nini wewe kununua kitanda. Haya tangu ubanie kumuuhudumia na kumnywesha hata juice au soda umefanya maendeleo gani. Hutoi Kodi unakaa bule”.
“Nenda tu si umesema huwezi kumlisha aludi kwao?. Ndo ameludi Sasa. Ukiona unaweza kumlisha njoo umuoe kabisa na sio sogea tukae, na wewe Mamy ole wako nikuone unatoa ngoko zako kwenda kule tena. Kama mtoto tutamuhudimia wenyewe na atakuwa kama utashindwa kutoa matumizi”.
“Abdul aliomba msamaha maana sio Kwa vichambo vile, dada na mama walimsamehe ila walimwambia akatafute maisha na yakimkaa sawa basi aje na Nia ya kunioa kabisa na sio kuishi kihuni na alishindwa basi nitaolewa na wanaoweza”.
Aliondoka kinyonge, hakutegemea kama ipo siku nitayasema kwetu aliyokuwa ananifanyia. Alikuwa ananifukuza akiamini siwezi kuondoka na hata nikitaka kuondoka kwetu hawawezi kunipokea…..
SEHEMU 03
Familia yangu ilijitoa kunisaidia kwenye nahitaji ya mwanangu. Baada ya mtoto wangu kufikisha mwaka mmoja nilianza kutafuta kazi. Kipindi icho nilikuwa nishaachana na Abdul maana sikuona mabadiliko yeyote kwake kinaendelea zaidi ya kuwa mtu wa wanawake tu na Bangi ndo ilizidi kumkolea kichwani.
Nilijuta na kusema laiti ningemsikiliza mama na dada yangu haya yasingetokea. Sema ndo hivyo majuto ni mjukuu. Nilipata kazi ya kuuza duka la nguo kaliakoo mshahara ulikuwa laki mbili na nusu kwa mwezi Kila kitu kwako, yaani kula na nauli juu Yako.
Nilianza kufanya kazi kwa juhudi zote nikiwa nasaidiana na wafanya kazi wenzangu. Duka lilikuwa kubwa sana kwaiyo tulikuwa wahudumu watatu na msimamizi mmoja jumla wanne.
Kidogo maisha yalienda vizuri baada ya kupokea mshahara wangu wa kwanza. Nilimnunulia mtoto wangu baadhi ya mahitaji muhimu na nyengine kuweka akiba ya nauli maana mwezi wa kwanza mama ndiye alikuwa ananisave nauli.
Abdul aliposikia Nina kazi alianza kujiludi na kutaka tuludiana tulee mtoto wetu. Nilimkatalia kabisa maana hata ningekubali kuludi ningekaa wapi. Hana chumba Wala chochote, kiufupi Hana akili ya maisha. Nilimkatalia kata kata kuwa simuhitaji Tena tubaki kama wazazi tu.
Niliendelea na kazi. Nilijituma sana na kuwa muaminifu. Kama mjuavyo kazi za maduka wanaangalia na kujituma kwako na uaminifu. Wengi wanashindwa na kuishia kufukuzwa au kuacha wenyewe. Upande wangu nilijituma haswaa na kuwa muaminifu hali iliyompelekea boss kunipenda na kuniongezea mshahara kutoka laki mbili na nusu mpaka laki tatu.
Nilifanya kazi mwaka mmoja ndipo nilipata wazo la kupanga. Kipindi icho mwanangu alikuwa amefikisha miaka miwili. Nilinunua godoro nikaweka ndani. Nilimuomba mama mkubwa mwanae niishi nae ili awe anabaki na mtoto maana kipindi Cha nyuma mama alikuwa anaenda nae gengeni.
Mama mkubwa alikubali. Alimsafilisha mwanae kutoka mkoani mpaka Dar. Sarah alikuwa Binti wa miaka 16 alipishana na mimi miaka mitatu tu maana kipindi icho nilikuwa na umri wa miaka 19.
Nilimpokea Sarah na kuanza kuishi nae kwaajili ya kunisaidia kumlea mwanangu. Sarah hakuwa na shida kabisa. Alikuwa mlezi mzuri wa mwanangu na nijilitahidi kumuonyeshea upendo wote ili aweze kuishi na mwanangu vizuri pale ambapo sipo.
BAADA YA MIAKA 4.
Mamy nilikuwa na maisha mazuri. Nilipendeza sana na kunawili sio mimi tu hata mwanangu na Sarah. Nilikuwa nimepanga chumba na Sebule. Hapo nishanunua fenicha za ndani za muhimu zote. Kula hainipigi chenga.
Bado nilikuwa nafanya kazi ya kuuza duka la nguo ila haikuwa kaliakoo. Boss aliinamisha kariakoo baada ya kufungua tawi jengine makumbusho. Mimi ndiye nilikuwa msimamizi wa duka hilo. Mshahara wangu ulikuwa laki nne kwa mwezi. Kiasi maisha yalikuwa mazuri. Sikuacha kuwasaidia nyumbani kwetu pia.
Kipindi chote hicho sikuwai kuwa na mahusiano akili yangu yote iliwaza kumtengenezea maisha mazuri mwanangu. Na mpaka muda huo Abdul alikuwa anaishi kwao Hana nyuma Wala mbele.
Weekend Moja tulitoka na familia yangu, yaani Mimi, Sarah na mwanangu Aquram. Tulienda mwenge mlimani city kula bata kidogo.
Nilimpeleka mwanangu kwenye michezo ya watoto. Huko alikutana na mtoto mwenzie wa kike na gafla tu walizoeana Kwa dadika ,si mnajua tabia za watoto Huwa hawana ubaguzi Wala ubinafsi tofauti na sisi wakubwa, wao wanavutana Kwa upendo tu kutoka mioyo mwao.
Nilimuacha Sarah Aquram mie niliingia super market kununua baadhi ya vitu.
Baada ya kumaliza kununua vitu nilitoka nje ya super market nikiwa na mifuko yangu mkononi natembea sina hili Wala lile. Hata sijui ilikuaje mpaka nikapalamiana na mtu.
Baada ya kupalamiana na mtu yule nilidondosha mifuko yangu na mtu yule alidondosha simu yake ya Bei mbaya na kujifunika upande wa kioo.
“Sorry”. Niliyasema hayo huku nikiwa nimeinamisha kichwa chini. Nilichuchumaa na kuiokota Ile simu , baada ya kuigeuza Ile simu nilitoa macho. Simu ilikuwa imepasuka kioo Ni iphone 15. Nilitoa macho.
“Mshenzi wewe. Unatembee huangalii mbele, alafu wanawake wengine bhna ni matatizo matupu. Ona Sasa umeniharibia simu yangu”. Kijana yule alifoka kwa sauti na kusababisha watu walio karibu na eneo lile wasikie na kubaki kutushangaa.
“Samahani kaka, sijafanya makusudi. Wote hatukuwa makini ndo maana tumepalamiana maana kama wewe ungekuwa makini basi ungenikwepa pembeni.
“Kwaiyo unataka kuniambiaje wee Binti?”. Aliendelea kuongea kwa paniki na mpaka muda huo Bado nilikuwa nimeishikilia simu yake mkononi mwangu hakutaka kuipokea.
“Wanawake wapumbavu na wazembe kama nyie ndo maana mnazalishwaga na kukimbiwa shenzi kabisa. Sasa simu yangu utailipa nakwambia”. Kaka yule alipaniki balaa. Nilimuangalia muonekano wake ulikuwa wa kishua sana. Yaani anaonekana sio mtu wa njaa kabisa ila namna alivyopaniki mpaka nilibaki nashangaa ni simu mpaka anitukane na kunidhalilisha hivi mbele za watu au Kuna mengine?”. Nilijiuliza mwenyewe huku namtazama yule kaka ambaye hakuonyesha hata repe la utani.
“Kuna nini kwani?”. Mbaba wamakamo alitusogelea na kutuuliza. Yule kaka alimueleza yule baba Kwa hasira.
“Huenda hajafanya makusudi”.
“Ni makusudi kabisa, watu wasikini wanakuwaga na roho mbaya sana, anaweza akakufanyia jambo makusudi ili akuingize hasara sasa mie sijawai kuingiwa na hasara kizembe. Simu yangu atalipa”.
“Kwani simu yenyewe shilling ngapi?”. Nilimuuliza kwa paniki sana baada ya kunitolea maneno ya kashfa na yasiyo na utu hata kidogo.
“Bei ya simu hauiwezi mtu masikini kama wewe ila kwa huruma yangu utailipa theluthi yake milioni Moja na nusu”. Nilichoka baada ya kuniambia Bei . Ni sawa na mishahara yangu ya mienzi mi nne.
Pesa ilikuwa nyingi sana ila kwa dharau zile za kuitwa masikini na maneno kibao nilijisikia vibaya na kuapia lazima nimlipe tu hata kwa awamu. Nilikuwa tayari kwenda kutoa pesa kwenye account yangu ya bank niliyoweka ilikuwa takribani laki 6. Nilikuwa najidunduwiza mwenyewe ili ninunue kiwanja ila ndo hivyo bahati haikuwa kwangu kwa wakati huo.
“Kwa Sasa Sina hiyo milioni Moja na nusu. Ila naweza nikakulipa kwa awamu.”. Nilimwambia yule Kijana, alikataa ila yule baba aliniombea . Peni na karatasi vililetwa kwaajili ya kuweka Saini na pia anuani ya makazi nilitoa mpaka namba za baba mwenyenyumba na mjumbe pia. Kijana yule hakutaka mzaa. Aliwapigia baba mwenye nyumba na mjumbe kwa uthibitisho zaidi……..
SEHEMU 04
Baada ya kujiridhisha kwa kila kitu tuliingia bank nilitoka laki tano nikampa yule Kijana roho iliniuma mno jamani daaah. Hela zenyewe za mawazo.
Baada ya kumlipa Kijana yule alinipa muda wa mwezi mmoja nimlipe Tena lako tano na yaani ndani ya miezi miwili niwe nimemaleza deni .Tulikubaliana hivyo Kwa unyonge. Niliondoka kuwafuata wakina Sarah nikiwa nimechoka kimwili na kiakili kabisa. Pesa iliyobaki bank haikufika hata laki mbili.
Nilifika niliwakuta wapo busy kucheza. Nilitafuta sehemu nilikaa. Uvumilivu ulinishinda niliangua kilio japo nilijitahidi kulia kimya kimya ili nisiwakusanye watu walio eneo hilo.
Nikiwa nalia Kwa kuinamia meza nilishtuka baada ya kushikwa bega langu. Nilijifuta machozi haraka na kunyanyua kichwa. Nilishangaa baada ya kukutana macho kwa macho na mtoto mzuri wa kike Marika sawa na mwanangu Aquram, mtoto yule alininyooshea mkono alinipa kitambaa nijifute machozi vizuri.
Bado niliendelea kushangaa, kwanza amejuaje kama nilikuwa nalia. Nilijiuliza mwenyewe pasipo majibu. Nilikipokea kitambaa kile na kujifuta machozi.
Nilimpakata yule mtoto. Alikuwa ananiangalia machoni kwa hudhuni sana.
“Mama usilie, ukilia unakuwa mbaya. Ebu Cheka kidogo maa”. Yule mtoto aliongea hayo huku nyuso zake zikipambwa na tabasamu Bomba.
“Nilimuangalia yule mtoto na kuachia tabasamu. Kidogo moyo wangu ulikuwa umepoa. Yule mtoto alianza kunifuta usoni Kwa viganya vyake huku akiwa anatabasamu.
“Unaitwa nani mtoto mzuri’. Nilimuuliza yule mtoto.
“Naitwa Amara Fredrick”. Kalinitajia jina lake na la baba yake juu.
“Waoooh! Una jina zuri Amara. Umekuja na nani huku?”.
“Na bibi na baba. Alafu nimepata rafiki mzuri anaitwa Aquram”. Alivolitaja jina la Aquram nilijua ni mwanangu Moja Kwa moja.
“Rafiki Yako yupo wapi?”.
“Yule pale analuka luka luka”. Alituonyeshea kidole Aquram wangu. Nilitabasamu na muda mchache alikuja mmama mtu mzima wa makamo.
“Mtoto unazurura wewe, mie naangaika kukutafuta kule kumbe upo huku”. Yule mmama alilalamika.
“Mie nipo na mama. Bibi nimepata mama mzuri si unanamuona eeeh. Alikuwa analia mie nimembembeleza”. Amara aliongea Kwa sauti ya kitoto ila alielekewa alichokuwa anaongea.
“Ni muongeaji mno, Kuna muda mpaka anaboa”. Yule mama aliniambia.
“Nimempenda bule. Ni mtoto mzuri sana na ana huruma. Ni kweli nilikuwa nalia na yeye ndiye aliyeninyamazisha na kulejesha tabasamu usoni mwangu”.
“Ndivyo alivyo. Hapendi kuona mtu analia na usipo nyamaza basi yeye atalia zaidi Yako na pia huyo aliyekuliza akimjua atamchukia sana”.
“Ni mtoto mzuri. Amara mamaa mimi naitwa Auntie mamy”.
“Mama chimama sio auntie”. Nilimshangaa Amara alivyo mdogo ila maneno yote mdomoni eti mama chimama. Nikakumbuka ya whozu na wema sepetu pamoja na mtoto Lola.
Aquram na Sarah walikuja nao Amara baada ya kumuona Aquram aliinuka mbio akaenda kumkumbatia. Wakakumbatiana wenyewe na kuanza kuruka ruka kwa furaha.
Baada ya kuachiana mwenye kumbato walishikana mikoni.
“Mama chimama, huyu hapa rafiki yangu”. Amara aliyasema hayo mie nilikuwa ntabasamu tu.
“Mama nimempata rafiki mzuri”. Aquram aliniambia hayo huku wakiwa wananisogelea kwa ukaribu.
“Ni mwanao?”. Bibi yake Amara aliniuliza.
“Ndiyo ni Kijana wangu”. Bibi Amara alinishangaa kwa mshangao wa wazi wazi. Ni nadhani hakutegemea kama tayari naitwa mama kwani sura yangu Bado ilikuwa ya kitoto kiasi japo nilikuwa na mwili wa wastani.
“Basi mjukuu wangu amempenda kweli kweli mwanao. Tangu wamekutama hakauki mdomoni mwake”. Bibi Amara aliyasema hayo huku akiwa anatabasamu. Ni mmama mzuri aliyevalia mavazi ya ghari na mwili wake ulipambwa na nakshi nakshi, cheni, hereni, Pete, sanaa vya gharama viliupamba mwili wake.
Simu ya mwana mama yule ilianza kuita, alipokea na kuweka sikioni. Nilisikia tu alisema tunakuja.
Baada ya hapo aliniaga na kumshika mjukuu wake mkono. Masikini Amara alianza kulia anataka aondoke na Aquram mwanangu.
Mtoto alicharuka kulia huku akiwa ameng’angania Aquram mkono. Wote tulibaki kuwashangaa. Ilibidi tukae Tena kwenye viti.
“Samahani mama Aquram. Jina lako Halisi ni nani eti na jee umeolewa?”. Aliniuliza maswali mawili Kwa wakati mmoja.
“Naitwa Mamy, sijaolewa naishi mwenyewe na mwanangu na huyu mdogo wangu”.
“Onhooo! Baba mtoto wako yupo wapi?”
“Ni story ndefu mama ila kiufupi tumetengana na Kila mtu na maisha yake Kwa Sasa”.
“Pole na hongera. Kumbe naongea na Malkia wa nguvu. Wewe ni mwanamke jasiri mwenye usubutu matumaini yangu utafika mbali sana”.
“Asantee mama”.
“Naomba nikuulize kama hutojali unaweza kuniambia”.
“Bila shaka, uliza tu mama”.
“Kwanini ulikuwa unalia?”. Yule mama aliniuliza kwa sauti tulivu. Nilifikilia kwa dakika kadhaa ndipo niliamua kumueleza ukweli kilichotokea dakika kadhaa zilizopita.
“Pole jamani. Kuna watu hawajui bahati mbaya na wanamidomo michafu kama vile wamezaliwa chooni”
“Acha tu mama yangu. Maisha yenyewe haya yakuungu. Bado nadaiwa milioni Moja. Nafikilia nitailipaje”.
“Usijali. Nipe namba Yako ya simu. Tutawasiliana zaidi nijue nakusaidia vipi maana baba Amara anatusubili huko muda hauluhusu kuendelea kuwepo hapo mwanangu”. Nilimpa namba za simu bibi Amara kimbembe kilikuwa kuwatenganisha hao watoto wawili waliotokea kupendana kwa muda mchache tu.
Amara Alilia kweli kweli ilibidi aondolewe kinguvu. Bibi yake alimbeba na kutokomea nae. Aquram mwanangu alikuwa mnyonge gafla, nilishangaa upendo wao jamani sijawai kuona watoto kuliliana kiasi icho. Nilipowaza deni Tena nilikuwa mnyonge gafla……
SEMEHU 05
Tuliludi nyumbani mimi na familia yangu ndipo, baada ya Sarah kunigundua kuwa sipo sawa aliniuliza shida nini ndipo nilimueleza yaliyonikuta.
“Kwaiyo tunafanyaje dada?”.
“Hata sielewi ila ntalipa tu sina jinsi”.
“Pole, Kuna watu hawana bahati mbaya kabisa”.
“Hata hivyo simu ni ya gharama sana ni ngumu mtu kasamehe bule. Ana haki ya kudai kama ameona nimefanya makusudi. Kilichoniuma tu ni namna alivyo nidhalilisha. Amejua kunidhalilisha jamani. Hakika tutafute pesa umasikini ni mbaya daaaah!”. Niliongea hayo Kwa unyonge.
Siku iliisha kesho ilifika na kwenda kazini. Akili yangu ilikuwa imetawaliwa na msongo wa mawazo. Milioni Moja sio mchezo daaaah!. Majira ya saa tano simu yangu ilianza kuita namba ni ngeni. Nilipokea na kuiweka sikioni.
“Hello!”. Baada ya kupokea Ilisikika sauti upande wa pili ya mwanamke.
“Hello, naongea na nani?”.
“Ni mimi wa Amara. Mnaendeleaje?”.
“Anhaa!, shikamoo mama”.
“Marahaba hali zenu?”.
“Huku salama tu sijui huko kwenu?”
“Tupo salama pia MUNGU ni mwema, Jana sikuwa na muda mzuri wa kuzungumza na wewe. Unaweza kuniambia saivi nini kilikusibu Jana ili nijue nakusaidia vipi kama mwanamke mwenzangu?”.
“Ndiyo mama”. Nilianza kumueleza yule mama namna ilivyokuwa.
“Ooooh! MUNGU wangu, pole sana mama Aquram”.
“Asantee mama, yatapita tu”.
“Sawa. Basi usijali sana nitakutafuta acha niangalia namna y kukusaidia maana kama ulivyosema pesa Yako kulipa itakuwa ngumu kutokana na kipato chako na familia Yako”.
“Nitashukuru mama hata ukinikopesha tu, nitakuwa nakulipa taratibu. Naomba unistili kwa hilo. Kijana yule ni mkorofi ndo maana naumiza kichwa. Sipendi masimango ila ndo hivyo maisha tu haya”.
“Usijali na pia ondoa shaka”.
Nilimaliza kuwasiliana na bibi Amara nlkidogo nilipata matumahini maana aliahidi kunisaidia. Majira ya usiku alinipigia simu.
“Weekend unaweza kuja nyumbani maana pesa ishapatikana. Nataka uje weekend ili umlete na Aquram. Unajua mjukuu wangu bado anamtaja mwanao mpaka leo?, naomba uje weekend mapema tu ili watoto wapate muda mzuri wa ku enjoy”.
“Sawa mama hakuna shida”. Tulikubaliana hivyo na bibi Amara japo sikumuamini Kwa asilimia zote.
Niliendelea kupambana kujituma kazini huku nikiwa nasubilia weekend ifike. Jumapili iliwadia. Nilijiandaa Mimi na mwanangu Sarah alienda nyumbani kwetu siku hiyo kumsalimia mama.
Tulipokuwa tayari nilimpigia simu bibi Amara ili anipe ramani ya kufika anapoishi.
“Chukuani Taxes, mwambie awalete Africana mtaa wa majengo nauli nitalipia mimi”.
“Sawa”. Tuliondoka na mwanangu kama alivyoniambia nilifanya hivyo. Tulifika Africana mtaa wa majengo nilimpa taarifa kuwa nimefika.
“Sawa namtuma mdada anakuja na Amara nauli ya taxes anayo usilipe sawa?”
“Sawa”. Baada ya dadika kweli nilimuona Amara kwa mbali ameongozana na Binti wa marika yangu. Nilishangaa tu mwanangu kaniponyoka mkononi alianza kumkimbilia Amara na Amara alianza kumkimbilia Aquram. Walipofikiana walikumbatiana Amara alimbusu Aquram shavuni, wote tulikuwa eneo hilo tulibaki tunashangaana tu.
Yule Binti alitufikia alinisalimia na kumlipa dereva Hela yake. Baada ya hapo tuliongozana huku watoto hao wakiwa wameshikana mikono.
Tuliingia kwenye mjengo mkubwa, ni gorofa Moja lililojengwa kisasa, nyumba ukiitazama tu kwa nje ni mzuri sana huko ndani sijui inakuaje. Niliyawaza hayo mwenyewe.
“Bibi, bibi” Amara alianza kupaza sauti kumuita bibi yake hapo hata ndani hatujaingia.
Tuliingia ndani, humo ndani bwana kizuri sio powa. Kila kitu kwangu kilikuwa kigeni.
“Waoooh!, karibuni”. Bibi Amara alitukaribisha kwa uchangamfu.
“Asantee mama tumekaribia”. Tulisalimiana, muda huo Amara na Aquram walikuwa busy na yao. Wanaongea wenyewe mala watekwnyane kama mjuavyo michezo ya watoto.
“Twende kwa baba yangu ukamsalimie”. Amara alimshika mkono Aquram na kumuongo kupandisha juu gorofani.
“Daddy huyu hapa Aquram”. Baada ya kuingia tu Amara alimwambia hayo baba yake. Aquram alimuamkia baba yake Amara. Yule baba alishangaa furaha aliyokuwa nayo mwanae baada ya kuwa karibu na Aquram. Aliwapakata wote miguuni na kuongea nao kwa furaha.
Huku chini tulikuwa tumekaa mimi na bibi Amara tunapiga story za hapa na pale.
“Si unaona mjukuu wangu anavyopagawa pale anapomuona mwanao?, hali hii inanipelekea kuvutiwa na wewe zaidi na kutamani hata uwe mkwe wangu”. Bibi Amara aliongea hayo Kwa sauti tulivu. Niliinamisha tu kichwa chini na kutabasamu.
“Kwani mama yake yupo wapi?”.
“Unmzungumzia mama yake Amara?”
“Ndiyo”.
“Hayupo nchini na ni muda mrefu sana, ni story ndefu sana ila ukinipa umuhimu nitakueleza. Unaonekana ni Binti mzuri sana na Amara amevutiwa sana na wewe, unaweza pia kuwa mama Bora kwake”.
“Ni kweli mimi ni mama Bora kwa Kila mtoto”.
“Nimependa majibu Yako, unaonekana una roho safi kabisa”.
Tuliendelea na maongezi y hapa na pale huku nikiwa nakunywa juice iliyotengenwzwa Kwa ustadi wote.
“Acha nikufatie Hela chumbani”. Bibi Amara aliyasema hayo na kuelekea juu gorofani.
“Umeona watoto wanavyopendana?”.
“Kwakweli mama mpaka nawashangaa ujue”.
“Basi ndo hivyo. Alafu mama Aquram ni mrembo sana anaweza kuwa mkeo na akamlea vizuri mwanao”.
“Umeanza hivyo Sasa”.
“Sio nimeanza wewe njoo umuone kwanza, ni binti mpole na mzuri wa sura mpaka umbo na kwa muda mchache niliofahamiana nae hata tabia yake hainipi mashaka kabisa. Naamini anatabia njema sana”.
“Mmmh aya”.
Bibi Amara alitoka chumbani alimuacha mwanae anajiandaa kutoka na watoto. Alifika sebleni alinikabidhi zile pesa na kuniambia ni million Moja kamili.
“Nimekupa kwa mapenzi yote na Wala sijakukopesa. Ni milion Moja kamili”.
“Asantee sana mama, MUNGU akubariki zaidi”.
“Usijali ila wakuahukuriwa na wakupewa hizo baraka zaidi ni baba Amara mama yeye ndiye ametoka hizo pesa. Alafu ujue nini mwanangu, baba Amara anakuja saivi anataka mfahamiane naomba naomba uonyeshe utulivu zaidi sawa?”. Nilikubali na baada ya muda niliwasikia wakina Amara wanakuja kupitia sauti zao za vicheko.
Walifika sebleni mimi nilikuwa nimeinamisha kichwa chini.
“Baba huyu hapa mama chi mamy”. Amara aliongea hayo ndipo baba yake alinisogelea na kuninyooshea mkono kwa lengo la kusalimiana kwa ukarimu.
Nilimpa mkono na kunyanyua sura yangu, wote tulipigwa na mshangao baada ya Kila mmoja kumtambua mwenzie……
INAENDELEA……

