MAMA ALIPOSHIKWA TAKO MBELE YANGU
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Sehemu Ya 1
Nilikuwa na Umri wa Miaka mitano lakini akili ilikuwa imekomaa vya kutosha kuona yale ambayo nakumbana nayo kwenye Maisha yangu. Nilikuwa na uwezo wa kutambua na kung’amua kinagaubaga bila hata ya Kuomba ushauri.
Katika mambo yote ambayo sina wasiwasi nayo kwenye akili yangu ni kwamba nilikuwa nampenda sana Mama yangu, hili sina wasiwasi nalo hata kidogo kwani hata wakati alipokuwa anaumwa nilikuwa naingia chumbani kwangu kimya kimya na kuanza kupiga magoti nisali kumuomba Mungu asiuchukue uhai wa Mama yangu.
Endapo Mama angejua ninavyojisikia ndani ya moyo wangu ama kwa hakika hata siku moja asingediriki kusema mbele yangu kwamba anaumwa kwani nilikuwa nikiteseka sana.
Ukweli ni kwamba Mama yangu alikuwa ni kati ya akina mama ambao walikuwa hawaheshimiki kwenye jamii kwa sababu ya aina ya Maisha aliyokuwa anaishi, japo mimi nilikuwa namuheshimu sana kama mama yangu.
Nakumbuka vizuri sana siku ambayo walikuja wanaume wawili na wote walikuwa wanadai kuwa mimi ni mtoto wao, pamoja na hayo yote lakini Mama aliwaambia kuwa kati yao hakuna ambaye ni Baba yangu, hii ilikuwa na tafsiri kwamba Mama alikuwa na mahusiano na wanaume wengi kwa wakati mmoja na kuna uwezekano kwamba hata yeye hamjui vizuri Baba yangu halisi ni nani.
Pamoja na hayo yote lakini Mungu alinipa kipaji cha kumpenda na kumheshimu Mama.
Kuna jambo labda watu hawaelewi lakini ni kweli kwamba Mungu ndie anaamua mambo yote Duniani na hata Kokote Kule, Endapo Mungu aliamua kunilea tumboni mwa mama yangu kwa miezi tisa na hatimaye akaruhusu nizaliwe baada ya miezi tisa na mama huyu huyu basi ni dhahiri kuwa Mungu alikuwa na mpango mkuu sana kwangu na kwa Mama huyu ndio maana akaruhusu anizae yeye na si mwanamke Mwingine. NAKUPENDA SANA MAMA YANGU.
Mama yangu alikuwa anauza baa na alitulea Mimi na mdogo wangu wakike kwa kuuza baa, tulikula tukashiba na tukalala na tukaenda shule kwa hiyo hiyo kazi yake ya kuuza baa.
Alitupenda na alitujali kwa kidogo alichokuwa anapata na ndio maana hadi leo namkumbuka mama yangu na kuishia kusema “acha Mungu akuhukumu na sio wanadamu waliokuona mama mbaya, Kwangu ulikuwa mama ‘Jembe’”
Nikiwa tayari nina Miaka sita nilijiunga shule ya Msingi japo ulikuwa ni umri mdogo kuanza shule kwa wakati ule lakini uwezo wangu uliwashawishi walimu wakaruhusu niingie darasa la kwanza huku nikiwaacha waliokuwa na umri mkubwa wakikosa nafasi.
Katika kipindi ambacho sitakisahau maishani mwangu ni kipindi hiki nilipokuwa hasa darasa la kwanza, lapilli na latatu. Uchokozi kuhusu Mama yangu ulikuwa Mkubwa sana na mara kwa mara nilikuwa nashitaki kwa walimu mpaka wakanichoka, sitamsahau Mwalimu Greyson siku moja alinifukuza huku akiniambia “Nenda zako tumechoka mashitaka yako kila siku wewe tu, kwani hujui kuwa mama yako Malaya kweli!”
Kauli hii iliniuma kupita kiasi, sikuweza kuvumilia nilikimbia moja kwa moja mpaka nyumbani nikamkuta mama anakunywa chai, nilipomuona tu nikaanza kungusha kilio, mama aliacha chai na kunifwata kisha akaanza kunibembeleza huku akiniuliza ninini kimenisibu.
Huku nikiwa ninalia nilimwambia mama kila kitu kilichotokea….
“Nini? Wameniita Malaya?…”
Sehemu Ya 2
“…Manina zao wamewahi kunit..ba mimi hata siku moja, sasa subiri twende huko watanikoma”
Mama aliporomosha matusi makubwa mbele yangu hadi nikashtuka lakini sikujali sana, aliacha chai na kuingia chumbani ambapo alivaa suruali na flana kisha chini akapiga raba nyeupe na kunishika mkono kwa safari ya shuleni.
Mwendo tuliokuwa tunatembea njiani kila mtu alikuwa anashangaa, wanaume wa vijiweni walikuwa wakipiga Miluzi walipotuona huku wakimuita Mama kwa majina yasiyo na adabu lakini mama hakujali yeye aliongoza njia tu.
Tulifika shule ikiwa ni mda wa mapumziko na walimu walikuwa ofisini wanakunywa chai, Mama alizama bila hodi na kuanza kukagua meza moja baada ya nyingine, pamoja na ukaguzi wote lakini Mwalimu Greyson hakuwepo pale ofisini, Walimu walikuwa wameshikwa na butwaa wakituangalia sisi.
Wakati tunataka kutoka Mwalimu Greyson aliingia na kukutana uso kwa uso na mama yangu.
“wewe Mse..ge nimekufwata leo na utanitambua”
Mama aliokota mafimbo yaliyokuwa juu ya meza na kuanza kumchapa nayo Mwalimu Greyson huku akimporomeshea matusi.
“Wewe hanisi nimekunyima ku..m.. alafu unanitangazia mimi Malaya sio? Ningekuwa Malaya si ningekupa nawewe”
Maneno aliyokuwa anayaporomosha mama hadi aibu, nilijuta kwanini nilienda kumleta.
Walimu walianza kuamua lakini Mama alikuwa amemkaba Mwalimu Greyson huku akiwa anamng’ata na kumkwaruza na makucha yake, Mwalimu Greyson alikuwa amechaniwa nguo zake huku damu zikiwa zinamchuruzika kila sehemu sana sana usoni.
Mpaka mama anakuja kumuachia Mwalimu Greyson tayari wanafunzi walikuwa wamejazana nje ya ofisi wakipiga makelele hadi wanakijiji wakaja pale shuleni.
Walifanikiwa kumkamata mama na kumpeleka kwenye Sero ndogo iliyokuwa iko chini ya Mgambo wa Kata ambapo Mama alifungiwa pale.
ha kushukuru ni kwamba wajomba zangu walikuwa maarufu sana eneo hilo hivyo baada ya masaa machache Mama aliachiwa na kuwa nje isipokuwa alishtakiwa na kesi ikawa inaendelea.
Tangu siku hiyo sikuwa na amani tena ya kwenda Shule kwani walimu walikuwa wakinichukia mno, kitendo hiki kilinifanya nikawa Mtoro wa Shule huku roho ikiniuma sana na kila wakati nilikuwa nikisoma madaftari ya wenzangu kujua ni nini walichokuwa wanafundishwa huko shuleni.
Swala langu la kutokwenda shule halikumshtua mama sana isipokuwa alikuwa akienda na mimi pale kwenye baa anayouza na kuwa akiagizwa kinywaji ananituma mimi nikalete huku akiwa yuko na wanaume wake.
Siku moja ambayo sitaisahau alikuja mwanaume mmoja ambaye nilikuwa namfahamu kama dereva wa Basi moja lililokuwa linafanya safari zake kutoka kule kijijini kwetu ambapo sitapataja kwa jina kwenda Arusha na kuongea na mama kidogo kisha nikawaona wakiingia chumbani.
Kilichofwata ni kelele za mahaba alizokuwa anatoa Mama akiwa huko chumbani nikajua kabisa kuwa Mama yangu alikuwa akifanya Mapenzi, roho iliniuma kiasi ambacho nilijikuta natokwa na machozi tu.
Nikiwa nimejiinamia pale kwenye kiti alikuja mwanaume mwingine ambaye aliniuliza mama yangu yuko wapi nikamwambia sijui, nilivyomjibu hivyo akaniambia nimletee Safari Lager ya Moto Nami nikaenda kumletea akawa anakunywa.
Alikunywa ya kwanza akaniambia nimuongezee mpaka zilipofika nne, kuna wakati alikuwa akisikia zile kelele za chumbani na kutega siko kwa umakini kisha akacheka na kuniangalia kisha akaniambia…”Mama anahudumiwa kweli huko”
Nilikasirika sana lakini nikakaa kimya tu, kitu ambacho sikukitambua ni kwamba Yule jamaa Roho ilikuwa inamuuma sana kwani kumbe nae aliahidiwa penzi muda uleule.
Baada ya muda kidogo mama alitoka sambaba na Yule mwanaume kisha akaketi na Yule mwanaume akaaga na kuondoka zake.
Alinyanyuka Yule mwanaume na kumfwata mama ambaye alikuwa anaelekea stoo ya pombe kisha akamshika makalio na kumfokea “Wewe Malaya kwanini umenizengua na kumpa Yule fala”
Mama aligeuka kwa hamaki na kumtukana Yule mwanaume….
“ wewe mshenzi mbona huna adabu hata kwa mwanangu? Ku..m nini”
Kitendo cha mama kusema vile nilikamata bia aliyokuwa anakunywa Yule jamaa na kumtandika nayo Yule mwanaume ambaye alianguka chini kama gunia na kuanza kutiririsha damu kichwani kisha akanyooka.
Kitendo changu cha kuwa mtoro shuleni kiliniuma sana na kilikuwa kikinikosesha raha kwa mda mrefu sana.
Nashukuru Mun…gu kwamba pamoja na kuchukiwa na walimu pale shuleni lakini yupo Mwalimu mmoja ambaye mpaka leo sitomsahau, yeye alikuwa akiumizwa sana na swala langu hadi siku aliponitumia mtu na kuniita kwake.
Ukweli niliogopa sana ila ikanibidi tu kwenda, nilifika kwake nikabisha hodi nikamkuta mdogo wake ambaye alikuwa anachambua mchele pale nje lakini ndani ya uzio wa nyumba yao.
Huyu alikuwa ni Mwalim Josephine Karia ambaye alikuwa ni Mwalimu mgeni kabisa na inaonekana ndio alikuwa ametoka chuoni kwani alikuwa bado ni Msichana.
Nilimuulizia Mwalimu Josephine akaniambia kuwa ametoka kidogo ila atarudi mda sio mrefu hivyo niketi nimsubiri. Alinipa kiti nikakaa kisha baada ya robo saa Mwalim Josephine alirudi akiwa amebeba mfuko wenye mkaa.
Haraka haraka niliamka na kumpokea ule mfuko na kuuingiza ndani, alinisalimia kwa kunishika mkono namimi nikamjibu salamu kwa adabu zote kisha akaniambia niketi nimsubiri akachukue madumu yake ya maji bombani.
Nilimkatalia nikamwambia aketi naenda kuyachukua mimi, japo alikataa lakini pamoja na kukataa kwake nilikuwa tayari nimeshaamka na ninaelekea Bombani, nilifika Bombani nikakuta watu wanachota maji nikawauliza yaliko madumu ya Mwl Josephine wakanionyesha madum mawili, Niliyabeba yote kwa pamoja nikaenda nikamimina maji kwenye jaba kisha nikarudia mara tano zaidi hadi nilipomjazia vyombo vyake vyote.
Alinishukuru sana huku akiniambia tuingie sebleni namimi nikamfwata, alinikaribisha chini kwenye kapeti kwasababu pale sebuleni kwake hapakuwa na makochi nadhani kwasababu ndio alikuwa anayaanza maisha.
Nilipomtazama vizuri Mwalimu Josephine niligundua kuwa alikuwa akilengwa na machozi na hatimaye yakamdondoka kabisa.
Nilijikuta nikipata unyonge kwani sikujua ninini kinamliza Mwalimu wangu, sikupenda kuendelea kumtazama machoni nikajikuta nikitazama kando ili tusigongane macho.
Aliniita jina ambalo sitataka kulitaja hapa ila nitatumia jina la kubuni ‘SAM’ nilimuitikia na kugeuka upande aliokuwa kisha nikamsikiliza anachotaka kusema.
“Nakupenda sana Sam, kila nikikuangalia naona vitu vingi sana kwenye maisha yako”
“Nimejaribu kufwatilia maisha yako kwa ukaribu nimegundua kuwa una changamoto kubwa sana lakini lazima ufanye kitu ili ndoto zako zitimie maana nakuona u mtoto mdogo lakini mwenye ndoto”
Muda wote aliokuwa anaongea nilikuwa namsikiliza kwa makini sana na japo nilikuwa mdogo lakini niliweza kumuelewa.
“Unaishi maeneo gani Sam?”
“Naishi pale sokoni nyuma ya ile Guest yenye uzio wa mbao”
“Sawa si ni ile pale kwa Mlungwana?”
“Ndio”
“Unaishi na nani”
“Mini na mama na mdogo wangu”
“Baba yako yuko wapi?”
“Kwakweli simjui”
“Pole sana, umewahi kumuuliza mama yako kuhusu Baba yako”
“Ndio nimewahi ila anaishia tu kunitukana”
“Msamehe bure mama yako, ipo siku utamjua baba ila kwa sasa sio muhimu sana”
“Sawa mwalimu”
“Sasa Sam nataka unisikilize kwa umakini, nimekuuliza tu lakini najua mengi sana kuhusu wewe na familia yako, ninataka kukushauri kuwa uondoke pale kwenu uende kwa ndugu yako yeyote ukakae huko na usomee huko”
Nilikuwa namsikiliza kwa makini sana huku nikijiuliza ntaenda kwa ndugu gani hasa ambaye anaweza kuishi na mimi.
“Lakini Mwalimu mbona sina ndugu wa kuishi namimi”
“Sio kweli, namjua Yule Bibi yako ambaye ni Mwalimu wa ile shule ya Jumuia kule kata ya Jirani”
“Aaaa, sawa ila sidhani kama atakubali kukaa namimi”
“Sasa wewe hilo niachie mimi, kesho kuna kikao cha walimu wote ndani ya hii kata mimi nitaonana nae ntaongea nae uhamishiwe huko”
“Sawa mwalimu”
Tulimaliza maongezi kisha akanipa mahindi ya kuchemsha nikala kisha nikaondoka zangu kwenda nyumbani.
Usiku mzima wa siku ile nilikuwa natafakari maneno ya Mwalimu ambayo yaliniingia kweli akilini, nilijiuliza Mwalimu ameona nini kwenye maisha yangu lakini nilijikuta tu nikijisikia vibaya kwa kuona kuwa kumbe nimefikia hatua ya watu kunihurumia, nilijua kuwa huenda nina maisha ya kutia huzuni.
Siku zilisogea mpaka ikafika siku ya Jumamosi ambayo ni siku ya sabato na huku kwetu familia nyingi zinakuwa ziko kanisani isipokuwa kwa familia za watu wachache sana.
Nilipata wito mwingine wa kwenda pale kwa Mwalimu kisha nikaenda, nilipofika nilimkuta anafua , nilifurahi sana kumuona nikaenda kuketi pale pembeni yake alipokaa.
Tulisalimiana kwa kupeana mikono japo yakwake ilikuwa imeloana maji ila aliifuta kwanza kwenye kanga aliyokuwa amejifunga ndipo akanipa mkono wake.
Nilichukua beseni lililokuwa pembeni nikatia maji na kuchukua baadhi ya nguo alizoweka pale chini nikaanza kufua, Mwalimu alishtuka sana akinikataza nisifue lakini kazi ilikuwa imeanza na nilikuwa nafua kwa kasi sana.
Sehemu Ya 3
Kusema ukweli siku ile nilifua mpaka nguo za ndani za Mwalimu hadi nikamuona anaona aibu lakini kwangu mimi sikujali, nilimaliza kufua ndani ya nusu saa kisha nikaenda nikachota maji japo ilikuwa sabato lakini mbona hata kule baa anakouza mama nilikuwa naagiziwa kuwahudumia wateja vinywaji siku ya sabato…sembuse kufua potelea mbali!
Nilijaza vyombo maji kisha nikaketi sasa kwa ajili ya kumsikiliza Mwalimu wangu ambaye muda mwingi alikuwa akiniangalia bila kunimaliza.
“Nakuhakikishia Sam…Kuna kitu kikubwa sana ambacho Mungu amekiweka ndani yako na huko mbeleni watu watakishuhudia, wewe ni kijana mzuri, una heshima una adabu, una akili na ni mchapa kazi, usije ukakata tama hata kama utakutana na changamoto kiasi gani”
Hakuna nilichoweza kumjibu Mwalimu Josephine zaidi ya kusema tu Akhsante…. Alinikaribisha ndani kwake tukaketi kisha akaniambia kuwa Yule Bibi yangu Mwalimu atakuja mda sio mrefu hivyo tumsubiri.
Nikweli baada ya Muda kidogo Yule Bibi yangu alikuja nikamuamkia kwa adabu zote kisha nikampokea kibegi chake na kukishikilia mimi.
Mwalimu alimwambia mambo mengi sana kuhusu mimi pamoja na tabia na maendeleo yangu ya shule na kuahidi kuwa atanichukua na wiki ijayo nitaenda kukaa kwake na kuanza kusoma huko hata kama uhamisho haujakamilika hakuna shida kwani mme wake ndio Mwalimu mkuu wa ile shule.
…………………………..
Nilishukuru sana kwani pamoja na kumbamiza yule jamaa na chupa akadondoka chini, badae aliamka na kuondoka zake na hakurudi pale kwa zile wiki nilizokuwa bado pale na mama.
……………
Hatimaye japo mama alikuwa mbishi sana lakini mwisho alikubali kuniachia nikaenda kukaa kwa Bibi yangu na kuanza masomo kwenye shule Mpya.
Kukaa pale kwa Bibi yangu ilikuwa ni mwazo wa Changamoto nyingine ambazo nimezipitia na nitaanza kuzielezea kwenye toleo lijalo.
*******
Maisha mapya yalikuwa yameanza kwenye nyumba ya Bibi yangu ambaye alikuwa Mwalimu wa shule ya Msingi hali kadhalika Mme wake… ambaye alikuwa Mwalimu mkuu wa ile shule.
Huyu Bibi yangu alikuwa ana watoto nane ambao alizaa na mumewe, Watoto sita walikuwa wakiume Huku wawili walikuwa wakike.
Mkubwa kabisa alikuwa msichana ambaye wakati huu alikuwa akisoma shule ya Bweni kidato cha tatu, Wa Mwisho ambaye alikuwa ni mwanamke pia alikuwa hajaanza shule kwani alikuwa kama sikosei ana miaka minne.
Waliobakia wengine walikuwa ni wa kiume japo hakuna hata mmoja ambaye nilikuwa nae darasa moja, Mmoja alikuwa form one shule ya kutwa, mwingine alikuwa darasa la sita na mwingine darasa la tano, mwingine alikuwa darasa la tatu na mmoja darasa la kwanza.
Wakati natoka kwenye ile shule niliyokuwa nilikuwa tayari niko darasa la tatu lakini kuhamia huku ilinilazimu kurudi darasa la Pili kwani darasa la tatu lilikuwa halina nafasi.
Kwangu haikuwa shida kwani lengo lilikuwa ni kusoma na si vinginevyo,
Namshukuru Mungu kwani katika ile nyumba walinionyesha kunipenda sana hasahasa siku za mwanzo ambapo nilipewa mapenzi makubwa sana.
Kule shuleni nilipata marafiki wengi sana ambao tulikuwa tunashirikiana katika mambo mbalimbali kuanzia ya darasani mpaka yale ya nje ya darasa.
Siku zote mimi ni mchapa kazi, nafanya kazi tena bila ya kusubiri kutumwa, siwezi kuona uwanja mchafu alafu nisiufagie siwezi kuona vyombo vichafu alafu nisioshe, kiufupi nilikiwa sichagui kazi iwe ya kike ama ya kiume mimi nilikuwa sina uchaguzi wa kazi.
Nadhani hii ndio sababu iliyonifanya kila nikienda kukaa kwa mtu huwa sichokwi, tabia hii niliendelea nayo hasa pale kwa Bibi yangu japo ilinifanya nikawa mtumwa.
…………………………….
Mwaka wa kwanza ulikatika na hatimaye nikaingia darasa la tatu kwa mafanikio kwani nilishika nafasi ya kwanza.
Walimu walinipenda sana na wengi walidiriki kusema kuwa mimi nilikuwa na tabia njema tofauti na watoto wengine wa ile nyumba ambao wengi walikuwa hawana nidhamu njema.
Katika nyakati ambazo zilikuwa ngumu kwangu zilikuwa na hizi za kipindi hiki nikiwa darasa la tatu,
Ukweli ni kwamba pale kwa Bibi yangu walikuwa wanafuga Ng’ombe ambao walikuwa watano, walikuwa na Mbuzi kama ishirini hivi na Kuku pamoja na Nguruwe kama Kumi hivi.
Kwakuwa nilikuwa mchapakazi sana nilitafuta Sungura nikaanza kufuga palepale, niliwajengea banda wakazaliana na kuwa wengi sana mpaka wakafika hamsini.
Nilikuwa nawapenda sana kwani licha tu ya kuwa ni kitoweo na Biashara nzuri ila walikuwa wanapendeza sana machoni.
Walikuwa wana madoa doa, wengine weusi na wengine weupe pee! Mara zote kila nikitoka shule ilikuwa ni lazima niwatafutie kwanza majani ndio niende nayo nyumbani, na mara nyingi nilikuwa nawapa mchunga ama majani ya viazi vitamu ambavyo kule vilikuwa vingi sana.
Ilifika wakati msichana wa kazi aliondoka pale nyumbani hivyo ikatubidi kazi zote za nyumbani tuzifanye sisi.
Katika hali ambayo ilianza kumea kama utani ni kwamba nilianza kutegewa kazi za nyumbani, ilikuwa kila asubuhi lazima Ng’ombe wakamuliwe ndipo tuende shule, na si kukamua tu bali kufanya usafi wa nyumbani pamoja na mabanda ya mifugo.
Wenzangu walikuwa wanaamka muda wa kujiandaa kwenda shule tu na walikuwa hawajali kazi za nyumbani.
Mwanzoni nilikuwa najitahidi kuzifanya zote mwenyewe lakini mwisho nikashindwa, nilianza kutegea baadhi ya kazi kwani nisingeweza kuamka asubuhi nifanye usafi wa nyumba, nifagie mabanda ya mifugo, nikamue Ng’ombe alafu nijiandae kwenda shule, ilikuwa kazi ngumu sana
Nilichokuwa ninafanya ni kuamka na kufagia mabanda ya Ng’ombe na kuwakamua, lakini cha ajabu nilipoacha kufanya hizo kazi wenzangu hawakuzigusa na mbaya zaidi wakati wa kufokewa mimi ndio nilikuwa nafokewa zaidi.
Mbaya zaidi Yule Bibi yangu alikuwa anatoa maneno makali kama vile
“hakuna kukaa na kula bure hapa”
Maneno kama haya niliona kabisa kuwa yalikuwa yananihusu kwani mimi ndio nakaa bure kwani sio kwetu pale, na ndio maana wenzangu hawakuonekana kujali kwani haya maneno yalikuwa hayawahusu.
Pamoja na kuwa mimi ni mchapa kazi sana lakini kazi za hapa zilikuwa nyingi sana na ukweli nisingeziweza mwenyewe.
Kushindwa kufanya baadhi ya kazi kulinifanya nianze kuchukiwa kwenye hii nyumba, ilifika hatua hata daftari liishe sinunuliwi lingine, wenzangu siku za sikukuu wananunuliwa nguo lakini mimi ilifika hatua navaa nguo iliyochanika na kuyaacha matako wazi.
Hakuna wakati mbaya ninaoukumbuka kama wakati wa kuumwa, hata kama homa initingishe vipi, nilikuwa sibembelezwi nile wala kuambiwa niende hospitali zaidi ya kununuliwa dawa tu na kuendelea kutumwa kazi.
Nakumbuka kuna wakati nilikuwa nafagia banda la ng’ombe nikashikwa na kizunguzungu kilichonidondosha baada ya kukanyaga utelezi wa mavi ya N’gombe na hatimaye nikadundiza kichwa chini na kupoteza fahamu.
Hii ndio siku pekee ambayo niliweza kupelekwa hospitali na kuambiwa nina malaria sugu pamoja na typhoid.
Nililazwa takribani wiki nzima lakini nilikuwa naletewa chakula ambacho sio stahili ya mgonjwa kabisa, namshukuru sana mama yangu ambaye baada ya kusikia ninaumwa alikuja nikakaa nae pale hospitali huku akinipikia na kuniogesha.
Ugonjwa ulipopona nilirudi nyumbani na kuendelea na maisha ambapo nilikuta Sungura wangu wakiwa wamekonda sana kuonyesha kuwa walikuwa hawalishwi, vilevile Mazingira ya nyumba yalikuwa machafu mno huku mifugo nayo ikiwa haijahudumiwa.
Ukweli kazi zote zilikuwa kama zinanisubiri Mimi kwani nilianza kutumwa kazi ambazo zilikuwa zimelimbikizwa.
Nilikuwa nafanya kazi kama mtumwa mpaka ikafika wakati nikazoea na kuona ni kama kawaida tu na ninashukuru kuwa walinijengea mazingira haya ya kunionea lakini hawakujau kuwa wananijenga na kunifanya nifikie mafanikio haya niliyo nayo
………………
Mtu pekee ambaye alikuwa ananionea huruma ni Yule Babu yangu ambaye ndie alikuwa ni Mume wa Yuke bibi yangu.
Japo hakuwa Babu wa Damu lakini yeye ndie alikuwa rafiki yangu mkubwa, kuna wakati alikuwa anawachapa watoto wake akiwaona wamekaa alafu mimi nafanya kazi, huwa alikuwa anapenda kuwaambia “Mnadhani huyu kaja kuwafanyia kazi hapa Pumbaavu kabisa”
Kwakuwa nilikuwa nimeshazoea kazi nilikuwa nikiwaona wanafanya kazi kwa manung’uniko nawaambia waache pindi tu Baba yao akiondoka.
Ratiba yangu ya kuamka ilikuwa ni saa kumi alfajiri, nikiamka huwa nadeki na kufagia uwanja na kudeki vyoo vyote sambamba na kuosha vyombo.
Nikimaliza nawasha moto nachemsha chai na maji ya kukamulia, kisha naanza kusafisha banda la Ng’ombe.
Nikimalizana na banda naenda kukata majani ambayo yalikuwa yamepandwa kwenye mashamba yaliyopo jirani na nyumba na kisha nawapa ng’ombe na sungura huku nikiwa ninakamua.
Nikimaliza kazi hizo ndio unakuta wale ndugu zangu wanaanza kuamka na kuchukua maji ya moto na kuoga, mimi nilikuwa sijali kwani nilishaona ni kawaida tu.
Ajabu ni kwamba mimi nilishaombewa ruhusa kule shuleni kwamba nitakuwa sihesabu namba kwahiyo mimi nilikuwa nafika mda wa darasani tu.
Ninachoshukuru ni kwamba kwa swala la chakula ilikuwa sio haba kwani ile nyumba ilikuwa ina vyakula vingi sana, vya kununua na vile vya shambani vilikuwa vingi sana kuanzia ndizi, viazi, mahindi, maharage, karanga, mayai, mihogo, magimbi vyote vilikuwa sio lazima kununua.
Sehemu Ya 4
Kwakuwa mimi ndio nilikuwa mpishi nilikuwa nakula ninavyotaka na hata hivyo kila siku lazima ninywe nusu lita ya maziwa na hii ikanifanya pamoja na kuwa nafanya kazi nyingi lakini nikawa na mwili mkubwa na wenye nguvu huku misuli ikiwa imechanua vyema.
……………
Mpaka nafika darasa la saba nilikuwa nimeshakuwa na mwili mkubwa kiasi ambacho wasichana wengi walikuwa wananitaka wakinisifia kuwa Mimi mzuri lakini akili yangu ilikuwa haiwazi mambo hayo.
Nilipomaliza darasa la saba nilifaulu kuingia sekondari tena ya mbali tofauti na wenzangu ambao walikuwa wanapangiwa shule za kata.
Nakumbuka nilichaguliwa kwenda kujiunga UMBWE sekondari ya Mjini Moshi lakini cha ajabu niliambiwa kuwa haina haja ya kwenda huko isipokuwa nihamishiwe shule ya kata.
Bibi yangu ndiye alikuwa kinara wa hili jambo ambalo Babu alikuwa haliafiki kabisa na kujikuta akizidiwa nguvu kwani Bibi ndie alikuwa amenileta pale.
“Najua mnamng’ang’aniza asome hapa karibu ili aendelee kuwafanyia kazi, Angekuwa ni Mashaka wako ungekubali asiende huko UMBWE?”
Alisema Yule babu yangu na hata mimi mwenyewe nilijua nakatazwa kwenda huko ili nibaki nifanye kazi.
Mungu si Atumani nilijiunga na Shule ya Kata na kumaliza kidato cha nne katika mazingira ya pale nyumbani.
Matokeo ya kidato cha nne yalivyotoka nilikuwa nimepata Division III ambayo hata hivyo haikubalansi kombi hivyo sikuchaguliwa kidato cha Tano.
Hapa ndipo maajabu mengine nilipoyaona, wale ndugu zangu pale wote walikuwa wamepata Division IV lakini walikuwa wametafutiwa shule na vyuo na walikuwa wanasoma huko lakini mimi ulikata mwaka siambiwi chochote.
Hapa ndipo nlipoanza harakati zangu Binafsi ambazo ndio zilinifanya nifike Nyumbani kwa RPC wa mkoa wa MBEYA simulizi ambayo itafuatia toleo lijalo.
Dalili za kuondoka pale nyumbani zilikuwa hazipo kwani hakuna aliyeonekana kuwa tayari kunisaidia, kilichokuwa kinaniuma ni kuona hata wale watoto wa bibi yangu ambao walikuwa nyuma yangu wanamakiza form four alafu wananiacha mimi pale nyumbani sina ishu huku wao pamoja na kufeli lakini wakawa wanatafutiwa vyuo.
Niliumia sana nikagundua kuwa hapa sio kwetu na nisipoangalia nitiashia kutumikishwa kama mfanyakazi wa ndani.
Nawashukuru sana kwa kunipokea na kuishi na mimi kwa kipindi chote lakini sasa ulikuwa umefika wakati binafsi, wakati wa mimi kuondoka na kwenda kutafuta future yangu, kutafuta maisha ya wanangu na mke ntakayemuoa, kutafuta maisha nimsaidie na mama yangu, wakati ulikuwa umefika.
Nilimtafuta tena Yule askari nikaongea nae kwa kina ambapo alinipa namba za Yule rafiki yake ambaye yuko Dar ili nikaonane nae anisaidie.
“yani huyu ukionana nae mbona fasta tu, wewe mwambie tu kwamba umetumwa na mimi na wewe ni ndugu yangu”
Yale maneno ya Yule askari yalinipa faraja sana, nilijikuta nikianza kuamini kuwa tayari mimi ni askari, nilikuwa nafanya mazoezi ya pushap, kukimbia, kuruka kichura yani ili mradi tu nikifika kule wanione ni mkakamavu.
Siku hiyo nilichukua nguo zangu chache nikachagua zile nzurinzuri nikaanza kuzifua vizuri, zilipokauka nilikunja nikatia kwenye begi.
Nauli yangu niliyoipata baada ya kuuza sungura wangu wote nikaiweka kwenye begi vizuri kabisa huku nikisubiria masaa yaende fasta.
Siku hiyo nilifanya kazi kama jambazi hadi kila mtu akawa anashangaa, hawakujua kuwa mimi nina akili yangu kichwani na kuanzia kesho zile kazi watafanya wenyewe.
Usiku ulipoingia watu walikula chakula na kila mtu akaenda kulala kwake, mimi na mtoto mmoja wa babu tulikuwa tunalala kwenye chumba cha nje ambacho kilikuwa kimepakana na jikoni.
Kwakuwa kule milimani magari huwa yanaanza safari saa kumi usiku mimi saa nane nilikuwa niko macho najiandaa.
Nilichukua kibegi change nikakirushia mgongoni alafu mkanda ukapita begani, nilifungua mlango taratibu nikatoka nje, wakati nakata kona ya nyumba ili niibukie kwa nyuma nilisikia sauti ikiniita.
“we Sam unaenda wapi”
Ile sauti ya Babu ilinishtua lakini nikajikaza nisionyeshe wasiwasi.
“Naenda kukojoa babu”
“Sasa choo kiko huko? Na hilo begi la nini”
“Lina nguo chafu nataka niziloweke,”
“Usiku huu uloweke nguo”
“Ndio babu nataka nikiamka nizifue chap nikakate majani”
“Haya hembu njoo kwanza unichotee maji nimetapika hizi dawa za malaria zinanichefua sana”
Moyoni nilikuwa naumia kwani nilihofia kukosa magari, sikuwa na budi nilifanya alivyoniambia.
“Sasa Sam naomba tukae wote hapa nje, sijisikii vizuri kabisa”
Aliposema hivyo nilisikia kitu kama kisu kikikata tumboni kuanzia kulia kwenda kushoto, mambo yalikuwa yanaharibika.
“sawa babu, usijali”
Nilikuwa ni mtu mwenye huruma na utii sana, tabia yangu hii ilinifanya nisiweze kumkatalia babu, niliweka kibegi pembeni nikakaa nae pale nje.
Alikuwa akitapika sana na kwakweli nilimuonea huruma mno, kuna wakati nguvu zilikuwa zinamuishia mpaka nafanya kumshikilia wakati anatapika.
Ilipofika saa kumi na moja kasoro babu alipata nafuu nikamuingiza ndani, alipofika kwenye mlango wa chumba chake alinigeukia akaniambia
“najua unaondoka, chukua hii itakusaidia njiani, Mungu akutangulie”
Maneno yake yalinishtua kwa mara nyingine nikijiuliza amejuaje kuwa naondoka, nilipigwa na butwaa sana nikakosa cha kujibu lakini hata hivyo alikuwa ashazama chumbani kwao.
Taratibu na kwa unyonge nilianza kuondoka na hatimaye nikawa niko barabarani, kwa muda ule hata iweje nisingeweza kukuta gari, nilichokifanya nikaamua kutembea kwa miguu mpaka mji ulioko huko bondeni kabisa ambapo ningeweza kupata magari.
Mpaka kufika huko kwenye huo mji masaa matatu ya kutembea kwa mwendo wa kasi ni lazima yaishe, sikuwa na budi, kwasababu nilikuwa naenda kwenye mafunzo ya jeshi nikatumia nafasi hiyo kufanya mazoezi ya kukimbia.
Nilikimbia kwa mwendo wa lisaa limoja nikawa nakaribia kufika. Nilikuwa nimechoka nikakaa kidogo huku kiu ikiwa imenibana, kwakuwa hapa njiani kulikuwa na chemchem nyingi za maji nikakinga mikono nikanywa maji, ile namaliza tu kunywa maji nilisikia kama kitu kinavunja majani.
Kunyanyua uso nilishtuka vitu kama majimaji yakinirukia usoni, nilipotazama mbele niliona nyoka mkubwa akiwa anajiandaa kutema mate mengine.
Nilichukua kibegi change nikakimbia haraka sana, uzuri ni kwamba nilishawahi kusikia habari za hawa nyoka ambao wakikutemea mate ngozi inaoza.
Nilitafuta majani flani ambayo tulishawahi kuambiwa kuwa ni dawa nikaaza kuyatafuna na kuyagandisha pale usoni, haya majani yananyonya sumu yote na yakiisha nguvu yanadondoka chini kisha unaweka mengine.
Nilifanya hivyo kwa zaidi ya mara nne hadi nilipoona yale majani hayagandi tena nikajua sumu imeisha, kilichokuwa kinaendelea ni ile sehemu kuwasha, sikujali nikaendelea na safari.
Hatimaye lisaa limoja mbele nikawa nimefika pale stendi na kukuta watu wanakata tiketi za magari ya kwenda dar es salaam.
Nilizama kwenye kibegi ili nitoe nauli lakini nilianza kusikia miguu ikilegea na kunyong’onyea. Nauli ilikuwa haipo.
Baada ya kuwaza sana niligundua kuwa niliidondosha wakati nilipokuwa natoa sweta kwani ilikuwa katikati ya nguo.
Machozi yalianza kunitoka taratibu baada ya juona harakati zangu zinakwama. Pesa niliyokuwa nayo ni shilingi elfu tano tu ambayo alinipa babu wakati ananiaga.
Nilipiga akili haraka haraka nikajisemea lazima niondoke.
Maisha yangu yote Nilikuwa sijawahi kwenda dar es salaam lakini siku hiyo nilidhamiria kwenda tena bila nauli.
……………………….
K’ondakta alikuwa akipta kwa mtu mmoja baada ya mwingine akikagua tiketi, kijasho kilikuwa ‘kinanichuruzika maana nilikuwa nimekaa alafu sina tiketi wala nauli sina, ile elfu tano niliapia kuwa sitaitoa kwani itanisaidia kwenye kula.
Wakati konda anakaribia kwangu nikaanza kujitapisha, nilijitapisha huku nikisaidiwa kwa kupewa mfuko, konda alimaliza kukagua tiketi ikawa imebaki mimi tu.
Sikutaka kumpa nafasi niliendelea kutapika mfululizo kwa masaa matano kisha nikajifanya nimelegea nikajilaza kwenye kiti.
Baada ya nusu saa konda alinitingisha akaniuliza tiketi iko wapi, nilizuga kwa kupapasa mifuko huku konda akiwa amenikata jicho kali.
“kwani ulilipa nauli?”
“ndio”
“Ulilipa wapi maana hapa kwenye chati yangu sioni kwamba hii siti ililipiwa”
“Nililipa lakini”
“Usinizingue nataka nauli yangu, unafikiri sijui kwamba ulikuwa unajitapisha”
“Sio hivyo broo”
“Sio hivyo nini…oya Salimu hebu simamisha gari kuna fala hapa analeta kujuana”
Gari lilisimamishwa nikawa naambiwa nitoe nauli na mimi sina, gari ilitembea hadi tukafika segera ambapo kuna polisi walikuwa pale wamepiga kambi.
Hapa ndipo niliposhushwa na kuachwa pale kisha gari likawashwa na kuondoka, huzuni niliyopata sitaweza kuisahau maisha yangu yote.
Baada ya muda kidogo lilipita basi lingine nikapanda, huko mbele wakaanza kunidai nauli nikawaambia wasubiri kidogo, lengo langu ilikuwa nisogezwe mbele hata nikishushwa niwe nimeshafika mbali.
Kumbe Yule konda alishanishtukia, kama kawaida alimuamuru dereva asimamishe gari ili nishushwe na nikashushwa kweli. Wakati nafika chini Yule konda alinisindikiza na kofu la kichogo hadi nikasikia kizunguzungu.
Katika sehemu zote hii hapa ilinitisha kwani ilikuwa ni porini kweli, nilitafuta sehemu yenye mti nikakaa humo nikitafakari.
Kitendo cha kuachwa pale njiani kilinisononesha sana, nilijisikia kama vile dunia ilinitenga, niliumia sana kuona lile basi likiondoka kwa kasi huku nikilishuhudia likikunja kona na kupotea mbele ya macho yangu.
Nilianza kupiga hatua kwenda pembeni ya barabara nitafute sehem yenye kivuli nikae lakini kila nilipokuwa nakata hatua nilikuwa najisikia unyonge sana, miguu ilianza kuwa mizito huku nikisikilizia maumivu ya lile kofi nlilopigwa na Yule konda.
Jua lilikuwa kali sana na tayari nilikuwa nasikia kiu mno, sehemu hii ilikuwa ni vichaka tupu na hakuna gari iliyokuwa inasimama kwani hakukuwa na kituo wala nyumba za watu.
Nilipiga macho mbele nyuma na pembeni nikashuhudia vichaka vya miti mikavu kuonyesha kuwa hii sehemu hakukuwa na makazi ya watu, sikuona hata dalili ya mtu kupita isipokuwa magari yaliyokuwa yanapita kwa kasi sana.
Sehemu Ya 5
Katika hali ambayo sikuitegemea nilishuhudia majimaji yakishuka kwenye mashavu yangu nikaaanza kuyafuta, kumbe yalikuwa ni machozi.
Nilikuwa najihisi hali ya upweke sana, nilijiona kutengwa na wanaonijua na wasio nijua, mbaya zaidi sehemu hii sikuijua, nilitamani bora ningebaki kule kwa Bibi kwani nilianza kukosa matumaini ya huko niendako.
Baada ya kukosa kivuli niliamua kutembea taratibu kuifwata barabara, jua kali lilinichoma huku nikiwa sioni hata mtu wa kuongea nae, isipokuwa ngedere ambao walikuwa wengi wakikimbizana vichakani, nilipomkumbuka Yule nyoka aliyenitemea mate kule mlimani nilianza kuogopa nikijua kuwa kwa eneo nililopo inawezekana pia kuna chatu kabisa.
Sikuogopa kifo, nilikuwa tayari kwa lolote mbele yangu kwani maisha yangu tayari ni ya mitihani, pamoja na ujasiri niliojivika bado nilikuwa namwamgikwa na machozi usoni, ilifika hatua nikawa nalia kwa kwikwi kabisa kwani nilikuwa najisikia unyonge, upweke na nilikuwa na njaa na kiu.
Nilitembea kwa zaidi ya lisaa limoja lakini sikuona nyumba wala kituo lakini ghafla nilipokunja kona niliona gari aina ya Semi trela likuwa limeinama upande wa pembeni ya barabara. Nilijikuta nikipata matumaini mapya kwa kuona tu watu.
Pembeni ya lile gari nilimuona jamaa mmoja ameshikilia dumu la maji ya Uhai la kama lita kumi hivi anajimiminia kinywani, kwa kiu niliyokuwa nayo nilijikuta nayamezea mate yale maji, asikwambie mtu kiu inatesa kuliko njaa ya chakula.
Nilitamani nimfwate hata nimpokonye yale maji lakini nikaamua kumfwata kistaarabu.
“Broo naomba maji kidogo nina kiu sana”
“we fala nini, unadhani hapa mtoni, hata salam hutoi unataka maji tu…kwendaaaa mse..ge wewe”
Kitendo cha Yule jamaa kunijibu vile nilijikuta nikimwagikwa na machozi kama chem chem, sikuweza kugeuza shingo yangu niliangua kilio kama nimefiwa, sikuwa naigiza, nilijikuta tu nafsi yangu ikitaka kulia, nilijaribu kujizuia lakini sikuweza kila nilivyokuwa nakata hatua ndio kilio kiliongezeka.
Hatimaye miguu haikunyanyuka tena nikakaa chini huku kilio kikiongezeka mara dufu, nilishtuka nikishikwa bega, nilipotupa macho yangu nikakutana nayule jamaa aliyenifukuza.
“We dogo una nini”
Alivyoniuliza lile swali ndio alizidisha machungu yangu kwani nilijikuta unyonge ukizidi na hali ya kutengwa ikanisononesha zaidi. Hapa ndipo niligundua kuwa kumbe ukitaka mtu anaelia anyamaze hutakiwi kumbembeleza, ukimbembeleza utamliza zaidi.
“Dogo hebu simama basi, mbona sikuelewi”
Yule konda alizidi kuniongelesha huku wale wenzie wakija usawa ule tuliopo, nilitaka nisimame lakini miguu ilikuwa imenyong’onyea kwa uchovu wa kutembea kuanzia kule mlimani lakini pia machungu yaliyokuwepo moyoni.
“Siwezi kusimama broo, niacheni tu muendelee na mambo yenu”
“Tukuacheja dogo hebu simama uje hapa”
Nilishikwa mkono nikanyanyuliwa huku akiwa amepitisha mkono wake kwenye bega langu na kufanya kama amenikumbatia huku akiniongozea kwenye gari.
Tulizunguka nyuma ya gari ambapo kulikuwa na kivuli cha gari kisha akatoa maji kwenye dumu na kumimina kwenye chupa tupu ya litamoja na nusu kisha akanipa.
Kwa kiu niliyokuwa nayo niliyapokea yale maji lakini koo langu halikuruhusu kupitisha maji,, kulikuwa na kitu kama fundo limenikaba, nilijikaza sana na mwishowe nikafanikiwa kunywa yale maji.
Niliyanywa yote mpaka yakaisha, yalipoisha tumbo likaanza kuniuma nikajua kuwa ni kwasababu nimekaa na kiu mda mrefu alafu nikanywa maji kwa pupa.
Halikuuma sana, lilipoa kisha Yule jamaa akanipa keki za kwenye pakti na juisi, nilipokea nikanywa pia haraka haraka.
Alianza kunihoji mambo mengi na mimi sikusita nilimueleza kila kitu nikamuoana akisikitika sana ila akaniambia.
“ wala usijali, we komaa tu maisha nikutafuta na siku zote mtafutia juani hulia kivulini, usichoke.”
………………………
Ilikuwa ni usiku wa saa kumi tukiwa tunakatiza mto wami tuko ndani ya semi trela scania lililobeba cemet likielekea Mbeya.
Sehemu hii ya dereva ilikuwa inatosha kukaa watu watatu lakini kuna chemba iko kwa juu kidogo ambayo ina kitanda, walininitaka nipande nilale nami sikusita kwani nilikuwa nimechoka sana.
Nilishtuka nikiamshwa nishuke, nilipokata jicho kulikuwa kumepambazuka, hapa tulikuwa kwenye mizani ya challinze na gari lilikuwa linaacha njia ya dar es salaam likielekea mbeya hivyo ilibidi mimi kushuka hapa.
Yule Konda alinishika mkono akaniambia nimfwate, tulielekea kwenye zile ofisi za mizani tukaingia ndani, Yule konda aliwasalimia wale jamaa wa pale mizani kisha akamuulizia jamaa mmoja aliyemtaja kwa jina Mapunda.
“Mapunda saivi yuko Mikese Morogoro, amehamishwa, kama unaenda huko utakutana nae pale”
Yule konda aliachana nao akaniambia tuondoke.
“Yani huyu Mapunda angekuwepo angukusaidia sana, ni mshkaji wangu sana”
Aliniongoza mpaka kwenye Coaster iliyokuwa inaenda Dar es salaam kisha akanipakia. Nilipokaa kwenye kiti alimuita konda wa ile Coaster na kumlipa nauli yangu kisha akaja na kunipa shilingi elfu tatu.
Alinipa namba zake za simu akaniambia nikifika Dar nimtafute, aliniaga akaondoka zake na muda sio mrefu gari ile nayo ikaondoka.
Miaka mitano baadae nilipata taarifa zilizonihuzunisha kuwa Yule jamaa alifariki kwa kukanyagwa na ile Scania alipokuwa anarekebisha kitu chini ya uvungu wa gari ambalo liliserereka na kumpondaponda na kufariki hapohapo, roho iliniuma sana na namuombea maisha mema huko aliko.
Gari liliingia Ubungo mida ya saa sita mchana, niliangaza macho pale Ubungo sikuelewa A wala B, Bahati nzuri kulikuwa na vibanda vya kupigisha simu kila kona, watu waliofika ama kuishi dar kwa siku za nyuma kidogo watakuwa mashuhuda wa hili.
Nilikifwata kibanda kimoja kilichokuwa na msichana mrembo nikamuomba huduma ya simu akaniambia ni shilingi elfu moja kwa dakika, nilimlipa kisha nikampa namba akaipiga.
Hapa nilikuwa nampigia rafiki yangu niliyesoma nae msingi japo alinitangulia lakini alikuwa rafiki yangu sana.
Wakati huu yeye alikuwa anasoma Mlimani Chuo kikuu. Aliniuliza niko wapi nikamwambia niko Ubungo.
“Uko Ubungo upande gani”
“Kaka sielewi chochote hapa mimi ni mgeni”
“Mpe huyo mwenye simu hapo kibandani”
“Eee unaona hilo Bango hapo la BUZZ ni Bomba, …kwa pembeni kuna mabasi ya kwenda Morogoro, Dodoma na Mbeya, njoo hapa kibanda changu kiko kwa jirani tu”
Ndani ya dakika sihirini nilimuona Joshua akija pale akiwa ameongozana na Rafiki yake mmoaja, nilishangaa sana kumuona akiwa vile, alikuwa amependeza sana na kunawiri mno, alikuwa mweupe siku zote lakini saivi weupe wake ulizidi na alikuwa amenona mno, alikuwa amevalia kisasa sana na kuonekana kijana wa mjini wakati tulikuwa tunacheza nae mpira wa manailoni kwenye Vumbi.
Alinifwata akanikumbatia tukasalimiana fresh sana, tulipiga story mbili tatu kisha akaniambia tuondoke, wakati tunaondoka Joshua alirudi kwa Yule dada akampa mkono akiwa anamuaga.
“Dada kwaheri sana, naondoka lakini ntakukumbuka daima, mgeni wangu umemkaribisha vizuri kaniambia na soda ulimpa bure kabisa, hakika wewe ni wife material, hivi umeolewa? Hebu chukua hii namba na wewe unipe yako…”
Joshua aliongea maneno mengi sana huku dada wa watu akijitahidi kuutoa mkono wake lakini Joshua alikuwa kaung’ang’ania vilivyo.
Walipeana namba za simu kisha tukaondoka, tilikunja kona mbili tatu huku nikishuhudia magari mengi yanavyopita kwa kasi huku wenyeji wakionekana hawayaogopi kabisa.
Tulipanda Daladala zilizokuwa zinaenda Mwenge zikipitia Chuo kikuu cha Dar es Salaam kisha hatimaye tukawa kwenye hosteli anazoishi Joshua.
Jambo la historia kwangu ni kwamba hii ndio ikawa siku yangu ya kwanza kupanda lifti, japo hata nilipopanda sikujua kuwa ile ndio lifti. Niliona tu tukiingia kwenye gorofa refu mno alafu tukaingia kwenye kijichumba kidogo ambacho kilijifunga milango na nikaona Joshua akibonyeza vitufe flani na hatimaye tukajikuta ndani ya sekunde ile milango ikifunguka tena kisha tukatoka.
Nilibaki na maswali kichwani kuwa tuliingia hapa kufanyaje na hatukikaa wala kufanya chochote, nilipojikuta naona mji wa Dar es salaam kwa chini nikajua tuko juu ghorofani na lazima ile ilikuwa ni lfti
Maisha ya pale Mlimani yalinivutia sana, yalikuwa ni maisha yasiyokuwa na stress hata kidogo, nilijikuta nikimtamania Abeid kuwa mwanafunzi wa chuo.
Kilikuwa na mazingira mazuri, mahusiano yalikuwa poa sana na zaidi wanafunzi wa pale walikuwa wanaishi kijamaa sana, utani na masihara mengi yalisababisha wawe wanacheka mara kwa mara.
Nilittamani angalau na mimi ningekuwa mwanafunzi pale lakini ilikuwa haiwezekani kwa wakati ule.
Usiku ulipoingia tulilala japo kwa kuchelewa kwani watu walikuwa hawaishiwi na story, mara wengine wanaangalia movie kwenye tv na PC zao ili mradi kila mtu alikuwa huru kufanya anachotaka.
Kulipokucha asubuhi niliamshwa nikaenda kuoga nikapiga na mswaki kisha tukaenda canteen kwa ajili ya kunywa chai.
Binafsi nilikunywa chai ya maziwa na vitumbua vitatu kisha tukarudi hostel, ukweli ni kwamba nilikuwa na nguo chache sana na zilikuwa za kishamba, sikufanana na watu walionizunguka pale chuoni nikaamini ule msemo wa Kuku mgeni ………
Abeid aliliona hili akanipa flana yake na pensi na sendoz akaniambia nivae tutoke, siku hii ilikuwa ni jumapili hivyo hakuwa na vipindi vya darasani.
Tulitoka akanizungusha maeneo mbalimbali ya jiji la dar es salaam, kuanzia kariakoo, Mnazi Mmoja, Posta mpaka Baharini tukapanda pantoni mpaka kigamboni.
Hii ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuiona bahari…asante sana Abeid, nakuombea Mungu akuzidishie mafanikio kwenye ualimu wako uje kufika mbali zaidi ya hapo ulipo.
……………………..
Ilikuwa ni jumatatu tuko na Abeid tunaelekea Posta karibu kabisa na BoT ambapo ziko ofisi za wizara ya Mambo ya Ndani nikimtafuta Yule niliyeambiwa nijitambulishe kwake anisaidie kupata nafasi ya mafunzo ya uaskari.
Abeid alikuwa ni mjanja sana maana kwa jinsi tulivyofika pale wizarani na maswali tuliyoulizwa na wale walinzi basi ningekuwa peke yangu ningesharudi kwa kuogopa lakini tofauti ni kwamba Abeid kila alipokuwa anajibiwa vibaya yeye alikuwa anatabasamu na kuonyesha kutoshtuka.
Ilifika hatua mpaka wale walinzi wakawa wanacheka kwa jinsi alivyokuwa anawajibu kistaarabu lakini na utani ndani yake.
INAENDELEA

