KWA UTAMU HUU SIKUACHI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Episode 12
Kweli bana lucia akaanza ukaribu na huyo kijana alikuwa anaitwa japhet, kweli siku ya kwanza Boniface kaenda kumpelekea chakula lucia akamkuta na japhet wapo wanakula zao, alipanic sana, ila hakusema na mtu, akarudi nyumban kwake kama mtu ambae alie changanyikiwa, kisha akawa anajiambia “ licha ya kuwa na mimba yangu bado anahangaika na wanaume wengine, au ndio kweli mimba sio yangu ni ya huyo jamaa, ila hakuna uwezekano huo maana mimi lucia huwa namfuatilia sana, hawez kuwa na mwanaume mwingine zaidi yangu..
Akachukua simu yake akampigia, akashangaa simu inapokelewa na mwanaume, ambae alijua fika ndio Yule boya ambae alikuwa nae, kichwa kikaanza kumuuma, akaenda kuchukua bunduki akataka kujiua, bahat nzuri dada yake alikuwa pale, maana aliitwa kuwa mdogo wako anaanza kuwehuka huku..
Kuna nyimbo huwa anamuimbiaga kuanzia wakiwa wadogo ndio akaanza kuiimba tena kwa sauti tamu, ilikuwa inasema ..
“Boniface mr handsome, namna ambavyo ulivyo na moyo wa kipekee hautakiwi kuwa na hasira..
Maana hasira zako huwa zinaleta madhara
Bony dada yako nakupenda sana
Hata kama dunia itakupinga ila mimi dada yako Brenda kwa ajili yako nitapambana..
Nitahakikisha lile tabasamu limerudi bila udhia
Nitakaa pemben yako mpaka utakaposinzia
Nitakuwa faraja yako mpaka utakapo tulia..
Usifanye jambo lolote lile la ajabu maana name nitaumia
Usijidhuru maana mwili wako sio wako pekee yako
Maumivu yako ni yangu pia
Nakupenda sana kaka yangu Boniface, na daima sitokuchoka wala kukukimbia..
Brenda akamalizia hivyo, Boniface akakaa chini kisha akaanza kulia na kusema “ naumia dada naumia sana, nampenda sana lucia ila ananiambia kuw aile mimba yake sio yangu na sasa hivi yupo na mwanaume mwingine anatembea nae kila sehemu, dada nifanye nini maana naumia sana dada yangu, akaanza kulalamika Boniface..
Dada yake akamuangalia kwa sekunde kadhaa kisha akamuambia kuwa “ wewe ni wa thamani sana na thamani yako kamwe haiwezi kushuka kwa sababu ya mwanamke, nitahakikisha kuwa unamsahau huyo mwanamke na utapata mwanamke bora sana ambae anajua thamani yako..
“ hapana dada hapo ndipo ambapo unakosea sasa, ikabidi asema Boniface ..
“ sikuelewi, unamaanisha nimekosea wapi?, ikabidi Brenda aulize..
“ sitaki uongelee kuhusu mimi kumsahau lucia maana sitaki kumsahau, kama ni kiuteseka niacheni niteseke ila sitaki kumsahau, maana kila ninapomfikiria najisikia vizuri sana, hivyo dada naomba sana kama unanipenda kama mdogo wako au kaka yako, usiongelee kabisa habar za mimi kuachana na lucia na wala kumsahau maana na wewe unaweza ukageuka adui yangu, na badala yake wewe ni mwanamke unatakiwa kunifundisha mbinu ambazo zitasaidia mimi kuwa na lucia, na sio vinginevyo ..
Brenda akashusha pumzi kisha akasema “ nimekuelewa bony, ila naomba uzingatie kila ninachokisema kwa makin ili upate kilicho bora zaidi..
“ hayo ndio maneno sasa ya kuniambia dada yangu kipenzi, akasema Brenda..
“ kwanza usimsogelee wala asikuone one na ikiwezekana usimtafute kwa sms wala kumpigia simu.,.
Boniface akatoa macho kama fundi saa akaona kweli dada yake hamtakii mema, yaan anamaanisha kuwa asimtafute lucia na wakati anapoteza muda wake na mwanaume mwingine akaona kama dada yake anamchanganya hivi maana ukweli ni kwamba hawez kufanya hivyo hata kama dada yake amesema..
Episode 13
“sikuambii kama uachane na mwanamke wako hapana, nataka muendelee kuwa pamoja, ila yale maneno yako ya kila siku na vitendo vyako ndio vinampa jeuri unatakiwa umpe nafasi ya kukumiss ili ajue wewe ni wa thamani kiasi gani, yaan unachokifanya cha kumfata kila wakati ndio kinachosababisha akuone kama mtu wa kawaida sana kitu ambacho sio kweli kabisa, wewe sio wa kawaida kwa kiwango hicho ambacho unajiwazia nay eye anakuwazia, wewe ni mwanaume jasiri sana ila ni dhaifu sana kwake, ameshazoea maneno yako kuna namna yatakuwa yanamtesa ukikaa mbali nae kwa muda mfupi, sijakukataza kwenda kumuona sijakuzuia kuumia, ila hakikisha hayaoni maumivu yako hakikisha kuwa anaishi maisha akijua kuwa umeshampuuza na jambo zuri zaidi ni kuwa anamimba yako, atazunguka wee ila mwisho wa siku lazima atakutafuta maana wewe ndio baba halisi wa mtoto wake, akasema Brenda, kuna namna haya maneno ni kama yakamuingia kidogo Boniface maana alishakuwa chizi mapenzi..
Dada yake siku hio alilala pale maana bado hakuwa anaamin akili ya ndugu yake, hivyo akasema amuangalie mpaka asubuh kisha kulipopapambazuka dada yake qliuondoka..
Siku hio Boniface hakutoka kabisa, ila kuna muda akili yake ilikuwa inakataa maana alimmiss sana lucia, alitaman walau amuone hata kidogo maana alikuwa anahisi kupagawa, mara akapata wazo maana anajua lucia ni mjamzito nan i ujauzito wake kabisa, basi akaingia jikoni kisha akapika, akaenda mpaka maeneo ya hospital akamkuta mfanya usafi mmoja alikuwa ni mmama, akamuomba akampen chakula lucia kisha akamlipa na kumuomba afanye afanyavyo lucia ajue kuwa Yule mama ndio ameandaa kile chakula..
Yule mama akakubali kweli akampelekea chakula na lucia alimshukuru sana akaanza kula mwenyewe bila kulazimishana na mtu, maana kwanza hakutaka kumkera Yule mama, na kingine alikuwa ana njaa balaa, yaan mimba yake ilikuwa inamtuma kula kula tu yaan…
Basi bana baada ya Boniface kupewa hizo taarifa kuwa lucia pamoja na mwanae ambae yuko tumboni wamekula vizuri alijisikia vizuri sana yaan, akaona kumbe angetumia hii mbinu muda mrefu huenda lucia angekuwa anakula vizr tu bila kuvurugana nae, akiwa kwenye gari akiwa anajianda akuondoka, akamuona lucia ameshikana mkono na Yule mwanaume ambae ni mfanyakazi mwenzake, akaanza kupanic maana anampenda sana lucia, akataka kushuka ili akalete vurugu ila akakumbuka dada yake amemuambia kuwa awe mtulivu na ampe lucia muda wa kumkumbuka na asiwepo pemben yake kila wakati…
Basi akajikaza na kuondoka zake ingawa ilikuwa ni kishingo upande maana moyo wake haukuwa unataka kabisa kuondoka ila akili yake ikamuambia ondoka utengeneze thamani yako wewe sio dhaifu kiasi hicho, basi bana hata kama alikuwa anaondoka eneo lile ila alimuweka mtu ambae atakuwa anamfuatilia lucia kwa kila hatua maana hakuwa anamuamin mtu kwenye mali yake hata kidogo…
Episode 14
Basi akaja kupewa taarifa kuwa lucia alikuwa anataka kutolewa kupata chakula cha jion pamoja na Yule mfanyakazi mwenzake, akahisi kuwehuka, akaomba apewe location, akapewa hata hakujiangalia maskin akatoka na ndala za chooni mpaka kwenye gari kisha akaenda mpaka kwenye hio sehemu ambayo lucia alitakiwa awepo, akaambiwa kuwa wameelekea chumban, akaenda mpaka kwenye chumba ambacho ameelekezwa ila akakuta pamefungwa akarudi mapokezi na kutaka funguo..
“ samahan hatuna mamlaka ya kumpa funguo ,mtu ambae hatumfahau hata kidogo, hii ni hotel na sio nyumba ya mtu ambayo kila mtu anaweza kuingia popote pale kwa namna anayotaka yeye, mmoja wa wahudumu akasema ambae alikuwa amesimama pale mapokezi..
“ mnajua mnachokizungumza nyie kweli, yaan mke wangu ni mjamzito na Yule mtu sio salama kwa mke wangu na mwanangu, nawaapia kwa jina la mungu yaan jambo lolote lile likimkutra mke wangu mtalipa kwa kweli, maana nyie ndio mtakuwa mmesababisha..
Wale watu wa mapokezi wala hata hawakujali waliona kama anaongea tu na huenda vitu anavyoongea havina maana wala mantiki yoyote ile ni kama anaongea ili kujifurahisha tu, mara akaja meneja Alikuwa anapita mara akamuona Boniface, alipomuona akashtuka kisha akasogea mpaka alipo kisha akasema “ mr boaz imekuwaje mpaka ukafika hapa, kuna lolote lile ambalo naweza kukusaidia?..
Wale watu wa mapokezi wakashangaa namna ambavyo boss wake anamuheshimu na kumpapatikia Boniface na wakati wao walimdharau..
“ nataka funguo ya chumba namba kumi na mbili kuna mtu anataka kumfanyia uhalifu mke wangu, akasema kwa sauti ya kujiamin na wakati huo huo Yule meneja akatoa amri kuwa apewe ufunguo kweli alipewa na baada ya kupewa akaenda moja kwa moja mpaka kwenye hicho chjumba na kufungua mlango, akakuta lucia anapurukushana na Yule mfanyakazi mwenzake, ni kama Yule kijana alikuwa anamtaka kimwili ila lucia hakuwa anataka mpaka wakachaniana nguo, lucia aliingia akampiga sana Yule mwanaume kisha akaamrisha watu wamchukue na kuondoka nae..
Kweli wakamchukua na Boniface akabaki na lucia, akamuangalia kwa sekunde kadhaa kisha akasema “ najua kuwa ulishwah kunambia kuwa kuliko uwe na mimi ni bora uwe changudoa, naona namna ambavyo umeamua kuwa changudoa lucia, na najua unafurahia maisha yako ya uchangudoa ukiwa na kiumbe changu tumboni, akasema kisha akasita kidogo na kusema “ sijui hata najiaminisha nini na wakati ulishasema kuwa hio mimba sio yangu…
Lucia hakuwa na namna zaidi ya kulia tu, akawa analia sana, mwisho akasema “ Boniface naomba nisamehe..
Boniface akacheka sana kisha akasema “ haya nambie natakiwa nikusamehe kwa sababu gani, labda nikusamehe kwa sababu nimekukuta na mwanaume chumban mkiwa mnataka kufanya faragha yenu, au nikusamehe kwa kuniumiza kipindi chote hichi, au nikusamehe kwa kutokuona juhudi zangu na moyo wangu wa dhati wenye upendo wa kweli kwako, au nikusamehe kwa lipi maana naona kama umenikosea sana..
“ huyu mwanaume hakuwa mpenzi wangu Boniface na sikuwah kufikiria kama anaweza kunifanyia hivi maana ni mtu ambae tunaheshimiana sana, akawa anajitetea lucia..
“ hakuwa mpenzi wako ila ni mwanaume ambae unakubali kuingia chumban kwake na unajua kuwa una ujauzito au ndio kama unavyosema kuwa una mimba ya mwanaume mwingine labda ndio miomba yake mlikuwa mnataka kumzibua mtoto wenu maskio, sio mwanaume wako ila ni mwanaume ambae unataka kuniumiza nae, ni kweli nimeumia na naumia mpaka sasa hivi, akasema Boniface kisha akawa anamsogelea lucia wakati huo lucia anatetemeka balaa, ila Boniface hata hakumfanya kitu na badala yake akashika mkono wa lucia na kuuweka kwenye moyo wake kisha akasema “ moyo unaniuma, moyo unaniuma sana mamaa, naumia sana lucia, ni kweli hauoni upendo nilionao kwako, ni kwamba huelewi kama nakupenda au laa, nakupenda sana na ndio maana unaniumiza lucia..
“ unanihukum bure sikuja chumban kwa kutaka, nilipigiwa simu kuwa ana dharura na anahitaji huduma ya kwanza, angalia, akawa anasema lucia akiwa anamuonesha Boniface sindano na kiboks cha huduma ya kwanza na kweli alikuwa amevaa gloves, Boniface akamkumbatia kwa nguvu na kusema “ afadhal umejitetea mamaa, maana nilikuwa nahisi kupasuka ndani kwa ndani…
Episode 15
Nilikuwa naanza kupagawa mamaa, ukiwa unajua umenikosea ni bora hata unavyonielewesha angalau uweze kunitolea mashaka moyoni mwangu..
“ nakuomba mamaa usiwe karibu na Yule mwanaume kwa namna yoyote ile maana utaniua kwa pressure nitakufa mamaa, nakupenda sana na sitaman kukuona upo karibyu na kiumbe chochote kile ambacho kina jinsia ya kiume, maana najijua namna ambavyo nina wivu sana, nina wivu sana na wewe mamaa..
Lucia akamuangalia Boniface kisha akaangalia chini kwa aibu, Boniface akamshika mkono kisha akatroka nae nje, na alipotoka nae, akaenda nae mpaka kwake, kwa kuwa lucia alikuwa mkosaji akawa anatii kila ambacho alikuwa anaambiwa na Boniface , wakaenda mpaka kwake, lucia akajua leo naliwa, ila haikuw ahivyo Boniface alikuwa anamuonea huruma sana na mimba yake, basi akampikia akala kisha akampeleka chumban akalala…
Akawa anamuangalia mpaka alipopitiwa na usingizi, alipolala nay eye akapita nyuma yake kisha akalala pemben yake akiwa amemkumbatia mpaka kulipopambazuka ndio akaamka na kwenda kumuandalia chai , lucia aliamka akiwa mnyonge sana, maana amemkosea sana Boniface ila bado anapambana kuhakikisha kuwa yupo pamoja nae kwenye kila kitu, kuna namna chozi likamtoka lucia kwa upendo mkubwa ambao Boniface alikuwa anauonesha kwake..
“ unalia mamaa, au nimekukwaza, nambie kama nimekukosea nikuombe msamaha kipenzi changu, sitamani kukuona una huzun mamaa hata kwa bahati mbaya, naomba unambie nimekufanya nini mpaka unakuwa na majonzi kiasi chote hicho akawa analalamika Boniface…
“ wala haujanikosea mimi nalia kwa furaha, mapenzi unayo nipa sijawah kupata, akasema lucia kana kwamba anaimba ile nyimbo ya kyleen, mpaka Boniface akanikuta anatabasamu bila kupenda maana hakutegemea kama kuna siku lucia ataongea nae kwa namna ile..
Akamsogelea na kumbusu kwenye paji la uso kisha akamuambia “ nakupenda sana mamaa, naomba usije ukaniumiza tena..
Lucia akatabasamu tu bila kusema lolote, maana bado hakuwa na uhakika na moyo wake kama amempenda Boniface au ndio alikuwa anamuonea huruma tu..
Basi wakaenda kunywa chai na mara baada ya kumaliza kunywa chai, bony akaondoa vyombo na kutaka kumsindikiza lucia kazin, kweli wakaenda mpaka kazin kwa lucia na alipohakikisha ameingia pale hospital anapofanya kazi yeye akaondoka zake, akaja kurudi tena mchana na chakula cha mchana kwa sababu hakuwa anataka kumuona mwanamke wake anateseka na njaa hata kwa bahati mbaya kwa sababu kwanza alikuwa ana vidonda vya tumbo na pili alikuwa ana kiumbe chake tumboni…
Basi bana baada ya kuhakikisha lucia amekula akaondoka zake kwenda kuendelea na shughuli zake, na muda wote huo Boniface alikuwa anamtaman sana lucia ila hakuwa anajua atamuanza vipi na pili alikuwa anamuonea huruma na mimba yake..
Siku moja lucia akaenda kumsalimia mama yake maana bado alikuwa hospital na hakuwa anajua kama Boniface ndio alikuwa ana shughulika na matibabu ya mama yake, na wakati wote yeye ambao yupo busy basi Boniface ndio alikuwa bega kwa began a wazaz wake..
INAENDELEA …..

