KIUTANI NIMEINGIZWA UKUBWANI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Chapter 16
Jimmy alimshika mkono wakaondoka huku yule kijana aliwasindikiza kwa macho na kutingisha
kichwa
Daaa kuna watu hawajiamini na wanawake zao.
Jimmy na Prisca walienda kukaa kwenye meza
yao. “Jimmy unachofanya ni wivu au huniamini?
“Prisca nina wivu na wewe kupita maelezo sitaki
ukaribuaha na wanaume hovyo, najua una julikana kutokana na mambo yako ya mtandaoni lakini unatakiwa uwe na mipaka wewe ni mke wa mtu na ulikutana bao huko watambue kabisa maana ipo siku nitapasua kichwa cha mtoto wa mtu kwa bastola.
Prisca alimuangalia na kushindwa kuongea Jimmy hakujali aliendelea kula.
“Siwezi kuendelea kukaa hapa…..
“Unataka kuondoka bila kula?
“Sipendi harufu wala kuona huyo samaki.
“Una tatizo gani?
“Sijui ila sitaki.
“Mmmh haukosi sababu wewe mwanamke.
Prisca alinyanyua sahani yake na kuhamia meza ya pili.
“Khaaaa wewe mwanamke
Please Jimmy nilichokwambia namaanisha kama ukija hapa nitaacha hiki chakula na kuondoka hapa.
Ilibidi jimmy amuelewe kwakuwa alikuwa anamuona basi alitulia wakala walipomaliza wakarudi nyumbani kwao.
Baada ya wiki moja kupita prisca aliamua kwenda hospitali kupima ilinikupara majibu ya uhakika.
Alipima vipimo vingi ikiwemo mimba.
Baada ya muda Prisca alirudi kwa daktari kuchukua majibu ya vipimo vyake.
“Majibu ya vipimo ulivyoona yanasema hauna ugonjwa wowote. Alisema daktari kisha akatulia.
“Doctor kwa hali ninavyojisikia sina tatizo kweli? “Huna ugonjwa ila una ujauzito wa wiki sita.
Hongera sana.
Prisca alimuangalia daktari usoni hakuonyesha furaha wala huzuni alikuwa akimshangaa daktari usoni.
Upo sawa dada? Sauti ya daktari ilimfanya prisca atoke kwenye mawazo.
“Nipo sawa doctor, asante.
Kwa ushauri nikushsuri uwazi kuanza clinic mapema kwaajili ya usalama wako na mtoto.
“Sawa doctor nitafanya hivyo. Prisca aliondoka kwenye chumba cha daktari akiwa anawaza amwabie jimmy au amuache
kwanza?
Akiwa anawaza hivyo akipishana na Kayden bila kumuona. Kayden walipomuona anatoka kwenye chumba
cha daktari akiwa vile akahisi lazima kutakuwa na tatizo. Alienda kwenye kile chumba cha daktari.
“Doctor willy kuna binti ametoka hapa muda sio mrefu anaitwa prisca ana shida gani?
Kwakuwa willy na Kayden wanafahamiana willy alimwambia ukweli.
“Ni mjamzito lakini anaonekana hana furaha. Kayden akicheka kidogo kisha akatoka kwenye chumba cha daktari.
Siku zilienda prisca alikuwa akipata tabu na harufu za vyakula na kutamani vyakula ambavyo
alikuwa hali hapo mwanzo hii ilianza kumpa wasiwasi Jimmy. Siku moja usiku wakiwa wamekaa sebleni Prisca alinyanyuka na kuelekea jikoni. Baada ya muda alikuja akiwa
kakasirika mfano wa mbogo aliyejeruhiwa. “Niliweza kitu changu kwenye kabati la jikoni kiko wapi?
“Kitu gani?
Kuna udongo kiliweka pale na sasa siuoni utakuwa umechukua wewe.
“Kwanini unakula udongo?
Sasa swali gani hilo? Nitakupa kwasababu napenda nipe udongo wangu bwana. “Nimeutupa.
“Unasemaje wewe? Utaenda kuununua sasa hivi sitaki utani na vitu vyangu.
Muda huo ulikuwa ni saa tano usiku. Jimmy alipo ona prisca anakuwa mkali sana alinyanyuka na Prisca akamfuata nyuma
walienda jikoni akafungua kabati lingine na kumpatia ule udongo. Prisca aliuchukua haraka
na kuula kama mtu aliekuwa na njaa sasa amepata chakula. Baada ya hapo alishusha na
kikombe cha maji ya kunywa. Hapa sasa roho yangu imetulia unaweza kuongea jambo nikakuelewa.
Jimmy aliendelea kumuangalia lakini badae akauliza.
“Prisca una mimba? Prisca alitingisha kichwa akimaanisha ndio.
Tabasamu lilianza kuchomoza midomoni kwa Jimmy, alimsogelea na kumkumbatia prisca kwa furaha.
“Asante prisca kwa kunihifadhia mbegu yangu hatimae naenda kuwa baba sasa.
furaha ilizidi kwenye nyumba yao, Jimmy
alizidisha mapenzi alimpa kila kitu prisca pia alimnunulia gari kama zawadi na kuahidi kumfanyia mambo mengi.
Siku Jimmy alipokuwa nyumbani alipenda kumpigia mke wake chakula walikaa pamoja huku alimshika tumbo na kusema.
Mtoto wangu, damu yangu, mrithi wangu, nitamuita Junior akiwa wakiume akiwa wakike nitamuita Jenista.
Wakati Jimmy anapanga ndoto zake Kayden alikuwa anapanga mipango yake ya kulipiza kisasa kwa ule usiku aliyopigwa, moyo wake ulijaa chuki na kutaka kumuona jimmy alipitia kwenye wakati mgumu kwa kuvunja uhusiano wao uliokuwa ukichanua siku hadi siku.
Chapter 17 & 18
Siku moja Mida ya saa mbili usiku Kayden alikuwa amekaa kwenye bar moja akipata kinywaji huku akiwa anamsubiri mtu.
Baada ya dakika kadhaa alifika kijana mmoja anayejulikana kwa kina la Brown. Walisalimiana na Kayden kisha akavuta kiti na kukaa. Waliungana pamoja wakaendelea kunywa huku wakiendelea na maongezi yao.
“Brown nimekuta hapa kwaajili ya kukupa kazi moja tu.
“Lete kazi boss wangu.
Kayden alinyanyua grass ya kinywaji akanywa kwanza fundi moja kisha akaendelea kusema.
“Nataka yule Jimmy ajutue kwa kisa la kunipiga ngumi mbele za watu. Naona nilimchafua mtandaoni lakini wakajisafisha sasa hivi nataka kumuweka mbali na yule mwanamke najua ataumia sana sababu mwanamke wake ni mjamzito.
“Sawa unataka nifanye nini ili kuvunja ndoa yao?
“Prisca amemaliza chuo anatamani sana kupata kazi sasa hii ndio njia nzuri ya kumkamata. Nataka umtafute kama boss wa kampuni fulani alafu mwambie mkutano sehemu hapohapo utamaliza mchezo na taarifa zitafikia jimmy.
“Hiyo imeisha boss wangu subiri majibu mazuri.
Baada ya siku mbili kupita Prisca alikuwa njiani anaelekea nyumbani kwa mama yake mara simu yake ilianza kuita na ilikuwa namba ngeni. Alipokea na kusikia sauti ya kiume ambayo hakuitambua.
“Prisca
“Ndio sijui naongea na nani?
“Brown ceo wa kampuni ya VW.
“Ndio mr Brown
Namba yako nimepewa na mtu moja hivi ameniambia kuwa ulikuwa unahitaji kazi na mimi nilikuwa nahitaji mtu wa masoko kwenye kampuni yangu.
Kwakuwa prisca alikuwa anatamani sana kupata kazi alikubali.
“Sawa nipo tayari.
“Basi naomba tuonane kwaajili ya maongezi “Unataka tuonane lini?
“Sioni kama kuna haja ya kupoteza muda hata muda huu naweza kukuelekeza sehemu ukaja tutaongea.
“Sawa.
“Njoo Golden hill hotel.
Sawa baada ya dakika chache nitakuwepo hapo.
Baada ya kukubaliana wakakata simu na Prisca akatafuta namba ya Jimmy na kuipiga III amwambie taarifa aliyopokea kutoka kwa Brown Alipiga simu iliita mpaka ikakata, iliita mara kadhaa bila kupokelewa aliamua kuachana nae na kuelekea Golden Hill.
Alipofika hotelini aliipiga ile namba kumjulisha Brown kuwa amefika,
Baada ya dakika chache Brown alitoka na kumfuata moja kwa moja.
“Habari yako miss Prisca.
“Salama. Brown?
“Ndio, tunaweza kwenda kuongea?
Sawa. Waliongozana mpaka ndani ya hoteli walikaa kwenye meza huku wakinywa vinywaji na kuzungumza mambo ya kazi. Baada ya muda macho ya Prisca yalikuwa mazito kama mtu mwenye usingizi mzito Brown alikuwa akimuangalia mpaka Prisca alipokuwa hajiwezi alinyanyuka na kwenda kumchukua akaenda nae mpaka kwenye chumba cha hotel ambacho alikuwa kachukia kabisa Alimkata kitandani kisha akampigia simu Kayden na kumwambia. “Boss kazi yako imeisha.
Kayden alicheka kisha akasema.
“Sawa ngoja tumalizie mchezo.
Kayden alichukua simu yake nyingine na kutuma ujumbe kwa Jimmy.
“Mke wako yupo na mwanaume kwenye hotel ya Golden hill hotel chumba namba 45.
Wakati huo Jimmy alikuwa anatoka kwenye kikao akiwa ameongozana na Patrick.
Messege ilipoingia aliisoma mara mbili mbili na macho yake hakijatoa kwenye simu yake pla alikuwa kakunja sura kama vile kapona kitu kilichompa maudhi.
“Vipi kwema? Patrick aliuliza.
Chapter 19
Jimmy bado alikuwa akishikilia simu yake, Patrick alichukua ile siku na kuusoma ile ujumbe.
“Huyu aliyetuma huu ujumbe ni nani?
*Sijui ni nani.
*Twende hotelini tukashuhudie.
*Vipi kama ni mtego?
*Tumejipanga.
Waliondoka haraka na kwenda kupanda kwenye gari ya Jimmy wakaelekea moja kwa moja hotelini.
Walifika mapokezi na kuomba kuonyeshwa chumba namba 45..
Kwema jamani? Muhudumu wa mapokezi aliuliza
“Kwema.
Muhudumu bado alikuwa na wasiwasi.
“Samahani ngojeni kwanza.
“Hatuna muda wa kusubiri.
Aliongea Jimmy kwa ukali, Patrick akamtuliza.
Tulia jimmy jazba na hasira hazitasaidia hili Patrick swala linataka twende taratibu. alimgeukla yule muhudumu na kumwambia
“Tunaweza kuonana na meneja?
“Ndio.
*Tukutanishe nae tafadhali.
Yule muhudumu alipiga simu kwa meneja akamuelezea kuna watu wanataka kumuona
wapo pale mapokezi. Baada ya dakika chache meneja alifika Jimmy na Patrick wakiongea nae kwa utulivu mpaka akawaelewa wakapandisha pamoja mpaka chumba namba 45.
Walipofika mlangoni meneja aliwakumbusha kile walichokuwa wamekubaliana.
*Jamani sitaki fujo wala ugomvi.
Kama tulivyo kwamba tupo hapa kwaajili ya kuhakikisha tu.
Sawa. Meneja aligonga mlango mara mbili mara mlango ulifunguliwa na Brown ambae alikuwa kifua wazi.
Jimmy na Patrick walimpatia macho usoni, meneja akauliza.
Samahani kwa usumbufu hapa ndani upo na nani?
*Ni swali gani hilo mkuu alafu mbona kama nimevamiwa?
Jimmy aliona kama wanachelewesha na kupoteza muda kwa maswali mengi alimaukuma Brown kisha akaingia ndani.
Alipofika ndani alisimama huku macho yake yakiwa kitandani, alimuona prisca akiwa amelala usingizi tena hajitambui. Alisogea karibu na kumuamsha lakini Prisca alikuwa haamini alimfuata browz na kumshika kwa nguvu “Wewe ni nani?
“Niachie bro.
“Kwanini upo hapa na mke wangu?
*Mke wako? Brown by aliuliza kwa mshangao. Huyu ni mwanamke wangu wa siku nyingi sana na hapo alipo ana mimba yangu.
alihisi kuishiwa nguvu lakini Jimmy hakumuachia aliendelea kumshikilia kwa nguvu. * Haiwezekani Prisca hawezi kunifanya hivi. Na nitaanza na wewe. Jimmy alimtwisha ngumi ikabidi Patrick na meneja waingilie walimtia Jimmy nje. Na muda huo huo Brown alichukua shati lake akaondoka huku akiwa anavaa.
Jimmy na Patrick wakiwa nje jimmy alikuwa akilalamika.
“Umeona tabia za huyu mwanamke kumbe alikuwa amenipa mimba ambayo sio yangu.
aliniambia anaenda kwa mama yake na sasa yupo kwenye chumba cha hotel na mwanaume. Sidhani kama Prisca amefanya hili.
“Ghaaaa Patrick wewe ni kipofu, huoni, haijaona Prisca amelala pale kitandani na yule mwanaume Kalori kuwa ni mwanamke wake na
mtoto wa tumboni ni mtoto wake? *Haitoshi kuamini nataka kuongea na Prisca. Mimi sitaki hata kumuona huyo mwanamke
nenda kamwambie sitaki kumuona nyumbani
kwangu. Aliongea Jimmy kwa katiba kisha
akapanda kwenye gari yake na kuondoka. Patrick alirudi chumbani akamkuta Prisca akiwa bado Kalala kitandani pia alikuwa anatokea na jasho jingi sana. Alijaribu kumuamsha lakini Prisca hata hakujitingisha wala kufumbua macho.
Hili sio jambo la kawaida mtu hawezi kulala
usingizi mzito kiasi hicho. Alisema meneja ambae alikuwa kasimama pembeni
akimuangalia Prisca.
“Hili ni kweli acha tumpeleke hospitali. Meneja na Patrick walisaidiana, wakambeba
Prisca na kwenda kumpandisha kwenye gari wakamkimbiza hospitali.
Alipokelewa na kufanyiwa vipimo ikaonekana kapewa dawa ya usingizi hivyo wakampumzisha kwa muda huku Patrick akiwa pembeni yake akisubiri.
Baada ya saa moja kupita Prisca alizinduka kutoka kwenye usingizi mzito sana.
*Prisca upo sawa? Patrick aliuliza lakini Prisca
hakujibu alikuwa bado anawenge pia alishika kichwa chake ni kama vile alikuwa akihisi maumivu.
*Mpe muda kidogo apumzike. Alisema kesi. Patrick akiwa
Anasubiri Prisca akae sawa ili waongee mara anapigiwa simu na kupewa taarifa kuwa Jimmy amepata ajali mbaya sana.
“Mungu wangu imekuwaje tena?
Kwakuwa Patrick ndio kama ndugu na rafiki mkubwa wa Jimmy ilimbidi aondoke haraka
kwenda kumuangalia.
“Kapelekwa hospitali ya rufaa.
Alifika hospitali akamkuta Jimmy ana hali mbaya hajitambui
Chapter 20
Patrick akifuatilia matibabu ya Jimmy huku aliuliza kichwa chake kwani haya yote yanatokea.
Hii haipo sawa kabisa lazima kuna mchezo
mchafu unaendelea nahitaji kufanya jambo.
Akiwa amekaa kwenye benchi la hospitali alijaribu kuvuta taswira ya Brown jinsi alivyo.
Alinyanyuka haraka na kuondoka pale hospitali akaenda kwa mtu ambae anachora picha
alimuelekeza jinsi ya kuchora hatimae ilitoka picha ya Brown.
Patrick alishika ile picha aliangalia huku akitoa tabasamu. Huyu ni yeye, asante sana.
Alilipia pesa aliyoambiwa kisha akaondoka Alienda sehemu akatafuta vijana na kuwapa kazi
ya kumtafuta Brown.
Baada ya hapo alienda hospitali kwenda kuonana na Prisca, alimkuta prisca akiwa anajiandaa kuondoka pamoja na mama yake.
Vipi?
Zimetuhumiwa tulikuwa tunarudi nyumbani sasa
Sawa. Acha niwapeleke
Patrick, jimmy yuko wapi? Mampigia simu hapokei. Prisca aliuliza Acha niwapeleke nyumbani kwa mama tukifika huko tutaongea.
Kuna tatizo?
Hapona kuwa na amani.
Basi waliondoka pale hospitali wakaenda mpaka nyumbani kwa kina Prisca.
Prisca na Patrick walikuwa wamekaa chumbani maana Prisca bado hakuwa sawa.
Patrick alipokuwa amekaa kando ya kitanda moyo wake ulikuwa na maswali mengi. Alimuangalia kwa muda mrefu kabla ya
kumwuliza swall lolote.
“Prisca, nataka unieleze ukwell wote. Ni Nani yule mwanaume ulikuwa nae kwenye chumba
cha hotel? Nini kinaendelea kati yako na Jimmy? Mimba ni ya nani?”
Prisca alishangaa maswali ya Patrick. Maswali yako siyaelewi Chumba cha hotel
nilikuwa nafanya nini?
Patrick alihisi huenda Prisca hajui kinachoendelea akamuelezea kila kitu Prisca akawa anashangaa
Prisca alilia kimya kimnya huku machozi yakimtiririka mashavuni.
“Patrick, Jimmy ndiye baba wa huyu mtoto
Sijawahi kuwa na mwanaume mwingine tofauti
na Jimmy na yeye ndio mwanaume wangu wa
kwanza pia natamani awe wa mwisho. Yule mtu
alinipigia simu na kusema ni CEO wa kampuni ya VW anataka kunipa kazi akataka tuonane hotelini tuongee. Nilipofika nikawa nakunywa
juice lakini baada ya hapo sijaelewa kilichokuwa kinaendelea.
Patrick akaanza kuunganisha matukio. Hakika huu haukuwa mzozo wa mapenzi tu kulikuwa na mchezo mchafu. Alimuahidi Prisca kuwa atatafuta ukweli wote, hata kama ni kwa
gharama
Jimmy amenikasinksa?
Ndio alikasirika na yeye hayupo sawa alipata ajali mbaya yupo hospitalini Mungu wangu Alisema Prisca huku
akiendelea kulia kwa sauti.
Hapana Prisca haitakiwi kulia jimmy atakuwa sawa pia jangalie hiyo hali yako,
Alimbembeleza mpaka Prisca akawa sawa Kabla ya kuondoka Patrick valimuomba kitu
Prisca.
Prisca naomba usije hospital wala kuwasiliana na Jimmy mpaka mambo yatakapokuwa sawa Sawa.
Siku chache baadaye Patrick akiwa hospitalini, alipokea ujumbe kutoka kwa chanzo chake cha kuaminika.
Kayden ndiye aliyepanga mtego huo kumchafulia Jimmy jina na kuharibu ndoa yake. Alimlipa mtu aitwaye Brown kumteka Prisca na
kumnywesha dawa ili aonekane kuwa na
uhusiano nae. “Asante kwa taarifa namtaka huyo Brown mara moja.
Tupo nae godawn
Nakuja hapo sasa hivi.
Unaenda wapi? Jimmy aliuliza kwa sauti ya chini.
Kuna kazi naenda kufanya ila nitarudi
Patrick aliondoka na kuelekea godawn alimkuta Brown akiwa kuvishwa kwa kipigo Alichuchumaa na kumuangalia vizun
Wewe kijana mjinga ni kweli ulifanya vile? Ulitumwa na Kayden?
Brown hakujibu.
Oooh kumbe jeuri hebu mshitueni kidogo. Vijana walianza kumshambulia kama vile wanauawa nyoka.
Jamani nasema, nasema niacheni.
Hebu muacheni.
Walimuacha Brown akaanza kuongea huku kijana mmoja akimrekodi.
Baada ya hapo Patrick aliondoka na kutoa ruhusa ya kumuachia aondoke.
Patrick walirudi hospitali na kumuonyesha ile video.
“Unamkumbuka huyu? Jimmy allangalia lakini hakuweza kumtambua
haraka kutokana Brown alikuwa kavimba na damu zilitanda mwilini kwake.
“Ni nani na mbona yupo kwenye hali hii? Ni Brown yule mwanaume aliekuwa hotelini na
Prisca
Sitaki kusikia habari za hawa watu,
“Punguza hasira msikilize.
Jimmy alisikiliza jinsi Brown alivyokiri kutumwa
na Kayden pia alikiri kuwa sio mimba yake na hakumfanya chochote Prisca Kayden ni shetani kwanini anafuatilia maisha
yangu?
“Nilijua hilo tangia mwanzo kuwa ni michezo ila wewe kukuelewa
Prisca alipewa dawa nyingi za usingizi Mke wangu yuko wapi? Mbona hakuja kumuangalia?
Nilimzula sababu ulikuwa na hasira nae
Nataka kumuona mke wangu. Sio sasa mpaka mambo yatakapokuwa sawa.
Patrick aliendelea kumuuguza jimmy mpaka
akawa sawa Lakini bado alikuwa hajapona vizun, alitembea kwa msaada wa magongo, lakini hasira na uchungu vilimpa nguvu mpya.
Siku moja Jimmy alikuwa anafanya mazoezi ya
kutembea na Patrick
“Ninataka huyo mtu ajutie alichonifanyia. Ulipobakiza nitamaliza Patrick nataka kumfanya Kayden ajutie alilofanya.
“Umepanga kufanya nini?
“Usijali utaona.
ikihitaji msaada unakaribishwa.
Baada ya hapo, Jimmy alipanga kisasi chake kimya kimya. Alitumia jina tofauti, akaanza kununua hisa za kampuni ya Kayden kupitia
mawakala. Mwezi mmoja baadaye, Kayden alishtuka kuona kuwa amepoteza nafasi ya kusimamia kampuni yake Jimmy ndie alikuwa msimamizi wa kampuni ya
Kayden. Kayden akiwa hana mamlaka hata ya kuamua mkutano wa wafanyakazi
Siku moja Jimmy alimtembelea Kayden ofisini, alimkuta akiwa hana furaha, amechoka na
kukata tamaa Jimmy alisimama mbele yake, akasema kwa sauti ya kujiamini
“Huwa sigombani kwenye mambo ya ujinga, fimbo ya kuadhibu ni hii niliyokuchapia.
Unatakiwa kupambana kiume, si kwa majungu na visasi visivyo na akili.”
Kayden allinama kidogo, akatabasamu kisha akatoka bila hata kutoa jibu. Hili ni fundisho kwa wengine.
Baada ya kumaliza mambo yake, Jimmy alikwenda nyumbani kwa mama mkwe wake, mahali Prisca alikuwa akiishi tangu mzozo ulipotokea. Aligonga mlango, Prisca
alipofungua, alimtazama mume wake kwa mshangao na wasiwasi. Jimmy alipiga hatua moja mbele, akaushika
mkono wa mke wake kwa upole:
“Nisamehe mama turudi nyumbani. Tukae pamoja, tulee mimba na badae mtoto wetu
katika familia yenye upendo na amani. Nilikosea
kwa kukuhukumu bila kusikia upande wako. Prisca alimuangalia kwa macho yenye machozi, kisha akasema kwa sauti ya utani:
“Ila hil dili yenu imenizamisha ukubwani bila
kutarajia
Jimmy alicheka kisha akamvuta na kumkumbatia kwa upendo. Lilikuwa ni kumbatio lililojaa majuto, msamaha na matumaini. Baada ya hapo
Wallagana na mama mkwe, wakaondoka wakiwa wameshikana mikono wakirudi kwenye ndoa yao mpya iliyoimarishwa na mitihani ya
maisha
Maisha hayakosi mitihani, lakini upendo wa kwell huwa haukatiki kama mfano wa kamba inavyokatika. Prisca na Jimmy walirudi pamoja,
mpaka Prisca alipojifungua mtoto wa kike wakalea mtoto wao kwa amani, huku Patrick akiendelea kuwa rafiki wa dhati.
MWISHO


1 Comment
Together with everything which seems to be building within this area, many of your viewpoints are relatively stimulating. Having said that, I beg your pardon, but I do not give credence to your whole strategy, all be it exhilarating none the less. It looks to everyone that your comments are actually not entirely validated and in simple fact you are generally yourself not even thoroughly certain of your argument. In any case I did take pleasure in reading it.