KIUTANI NIMEINGIZWA UKUBWANI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Chapter 11
Wakati prisca anaangalia hiyo taarifa na jimmy nae alikuwa anaangalia.
“Hiki nini jamani? Prisca alijiuliza na mara simu yake ikaanza kuita.
Unaona hii napigiwa simu na watu wengi kwaajili ya hizi taarifa zilizozagaa.
“Tulia prisca nitajua jinsi ya kumaliza hili.
“Yani najuta kukufahamu yani umekuja kwenye
maisha yangu na kuniharibia maisha yangu.
“Prisca hii sio inshu kubwa sana….
Achana na mimi bwana. Unasema sio inshu kubwa wakati Inasemekana umeowa mwanafunzi tena ndoa feki ili upate cheti vcha ndoa kwaajili ya mambo yako? Hii ni kashfa kubwa sana…. Kabla prisca hajamaliza kuongea Patrick aliingia bila hata kubisha hodi.
“Huu sio muda wa kugombana mnatakiwa kufikiria njia ya kujisafisha maana lazima waandishi wa habari watamtafuta jimmy na hata wewe Prisca unaweza kufuatwa na kuhojiwa kuhusu hili?
“Mimi sitaki kuhusishwa na skendo za ajabu. Jimmy nataka ufanye jambo moja ili tumalizie hili mapema sana na kila mtu aishi maisha yake kwa amani.
Sotoi talaka na hii ndoa umekubalika kisheria ila nita dili na huyu aliyesababisha haya. Aliongea Jimmy kwa hasira na Patrick akajibu.
“Ni mr Kenedy, kalipiza kwa kile kilichotokea jana usiku.
“Ni yule mwanaume mpumbavu?
“Ndio.
Prisca alivuta pumzi na kushusha kwa nguvu.
Kimnya kilitawala baada ya muda Patrick
alimgeukia Prisca. “Prisca naomba kitu kimoja kutoka kwako. “Kitu gani?
“Naomba uwe bega kwa bega na Jimmy ili hili liishe na Jimmy aendelee na maisha yake.
Prisca alimuangalia Jimmy, wakati huo Jimmy alikuwa akimuangalia huku akitoa huruma.
Japokuwa alikuwa ana hasira sana na Jimmy kutokana na mambo aliyofanya lakini alikubali kumsaidia.
“Sawa.
“Asante, nenda kajiandae kuna kitu nataka tufanye
Patrick alitoa simu yake na kumpigia simu akampa maelekezo ya kufika nyumbani kwa Jimmy.
Simu ya Jimmy na prisca hazikuacha kuita na messege ziliingia za kutosha.
Walikaa pale sebleni wakiwa kimnya wakisubiri. Baada ya dakika kadhaa walifika vijana wawili waandishi wa habari.
Kama nilivyo waambia nataka mrekodi mazungumzo ya hawa watu.
“Sawa kama wapo tayari tuanze.
Walianza kufanya mahojiano huku wakirekodi, walianza kumuhoji Prisca.
Dada prisca hili swala lilizuka na kutrend mitandaoni unalichukuliaje?
Kabla prisca hajajibu alimuangalia Jimmy, jimmy nae alikuwa kamkazia macho huku akiwa na
hofu hakuwa na imani kama prisca anaweza kumtetea kutokana na mambo aliyokuwa amemfanyia.
Prisca alimuangalia yule aliemuhoji na kuanza kujibu.
Ndugu mimi sina presha na maneno ya watu jimmy ni mume wangu wa halali na ndoa yetu niya amani sana kabisa.
Prisca aliweka kituo kisha akamuangalia jimmy na kuushika mkono wake.
Jimmy alijihisi amani. Vipi kuhusu tetesi za kuolewa ukiwa
mwanafunzi?
“Kumbuka kuwa mimi ni mwanafunzi wa chuo sheria inaruhusu mimi kuolewa.
Asante sana kwa maelezo yako.
Yule kaka alihamia kwa Jimmy.
kwaajili ya manufaa yako ya kibiashara? “Vipi mr Jimmy inasemekana hii ni ilikuwa ndoa
Sio kweli ndoa yangu na mke wangu imetokana na mapenzi yetu haihusiani na mambo yangu binafsi. Kilichotokea ni hila na watu wanaotaka kuniharibia sifa yangu.
Ila nasema haya maneno hayawezi kuathiri mambo yangu wala ndoa yangu, ndoa yangu itadumu miaka mia kwa uwezo wa Mungu. Nampenda mke wangu.
Alisema Jimmy huku akimuangalia prisca kisha wakatoleana tabasamu. Walionekana kama watu walio kwenye mapenzi ya dhati
na kuwaacha wao wawili. Baada ya mahojiano kuisha wageni waliondoka
“Asante Jimmy alishukuru lakini prisca hakujibu kitu aliondoka na kwenda chumbani kwake.
Chapter 12 & 13
Kuanzia siku hiyo kitu kilianza kuzaliwa moyoni na kichwani kwa jimmy alijikuta anampenda zaidi na kutamani kuendelea nae kwenye maisha.
Siku moja Jimmy aliamua kwenda nyumbani kwakina prisca kujitambulisha rasmi alienda akiwa kajiandaa kwa kila kitu lakini prisca hakuwa anajua chochote.
“Mama naomba nisamehewe kwa kilichotokea ndio hapa kwa kupata ridhaa yako ili niwe mume wa Prisca rasmi.
“Unajua ukikosea sana kwa tamaduni za kwetu unatakiwa kulipa faini pia ulipe mahali. “Nipo tayari kufanya mnachotaka.
Kwakuwa mimi ni mama na hakuna ndugu wengine siwezi kutoa tamko ila tutazungumza na ndugu wote alafu tutakujulisha.
Sawa mama. Jimmy aliondoka huku akiwa amemuachia kiasi cha pesa mama prisca kama kuimba msamaha.
Baada ya wiki moja Jimmy akiitwa na kupangiwa mahari pamoja na faini. Hakuchukua muda alilipa palepale na wazazi wakatoa tamko kuwa wamekuwa mke na mume ila unatakiwa kufungwa ndoa ya kidini hapo badae.
Jimmy alikubali baada ya hapo alirudi nyumbani akiwa na amani pia alikuwa huru kusema prisca ni mke maana alifuata taratibu zote.
Aliporudi nyumbani alimkuta prisca amekaa anaangalia movies.
“Vipi mpenzi wangu leo umepika nini?
Prisca alimuangalia kwa mshangao. Umeanza lini kuniita mpenzi na
kutakanikuandalie chakula?
Sikiliza prisca kuanzia sasa wewe ni mke wangu rasmi ndugu na wazazi wako
wanaotambua hill na wamenipa ridhaa ya kukumiliki. Sasa tunatakiwa kuishi kama mume na mke, unatakiwa kunipigia na kunipa huduma nyingine, chumba changu ndio kutakuwa
chumba chako cha kulala.
“Hivi mbona kila siku unakuja na mbinu mpya
unampango gani na maisha yangu? haya yote ni kwasababu nakupenda mke wangu.
Unapenda sana kuniharibia siku. Prisca alinyanyuka na kuondoka kabisa pale sebleni. Ilipofika usiku Prisca alikuwa chakula za chumbani kwake mara akasikia kitanda cha mlango kinafunguliwa alijua lazima atakuwa Jimmy.
“Unataka nini tena?
“Fungua mlango.
“Unajua wewe ni msumbufu.
“Fungua tafadhali kuna jambo la muhimu.
Prisca alinyanyuka kitandani akaenda kufungua
mlango huku akiwa na Night dress tu. Alipofungua mlango alishangaa kumuona jimmy akiwa na mto mkononi.
“Mbona hivyo?
“Nimekua kulala na wewe mke wangu. Prisca alifyonza na kutaka kufunga mlango lakini Jimmy alizuia akaingia ndani.
“Hebu kuwa na haiba ya kike basi, acha ubishi. “Hebu niache huko.
Jimmy aliushika mkono wa Prisca akanvutua kitandani, waligaragazana pale kitandani prisca alitaka kutoka pale chumbani lakini Jimmy aliweza kumdhibiti wakalala wote kitandani huku
Jimmy akiwa kamkumbatia. Prisca hakuwa na njia ya kujinasua mikononi kwa Jimmy ilimbidi atulie lakini alikuwa kakasirika
“Alafu unajua nini mke wangu kesho naomba unipigie pilau zuri nitakuwa na mgeni wangu jioni, usiniangushe tafadhali.
Prisca hakujibu ndio kwanza alifumba macho na kujifanya amepigiwa na usingizi.
Jimmy alipoona hivyo alimuachia na kumfunika vizuri huku akimuangalia usoni na kumlaza nyusi
zake.
Kila siku jimmy alikuwa mtu wa kulazimisha mambo ili kumfanya Prisca azowee kuwa nae
lakini kwa upande wa Prisca nae alikuwa alimfanyia makusudi na kudai kuwa hayupo kama mke wala msichana wa ndani bali yupo pale kwasababu ya kifungo cha dili haramu.
Hayo unasema wewe ila mimi najua katika maisha yangu mke wangu ni mmoja tu ambae ni wewe.
Kuna wakati Prisca alitamani kukubali kuwa na Jimmy lakini kila alipokumbuka mambo ya nyuma alivyofanyiwa na Jimmy ikiwa kutoka na wanawake tofauti na kumuingilia bila ridhaa yake akajikuta anakata tamaa na kuendeleza chuki zake.
Siku moja usiku prisca alikuwa amekaa kitandani jimmy aliingia na kwenda kujilaza kitandani.
“Prisca mke wangu njoo ulale huu ni muda wa kutafuta watoto. Prisca aligeuka kumuangalia na Jimmy
akamkonyeza. Prisca alifyonza kisha akanyanyuka na kwenda sebleni. Alichukua wine
akaweka kwenye grass na kuanza kunywa taratibu. Baada ya muda Jimmy alimfuata.
Unakunywa ili upandishe hisia zako unipe kama siku ile?
Prisca alimuangalia huku akiwa kakunja sura. “Hivi kwanini unanifuata fuata hivyo? Nenda
Kalale huko ndani.
Siwezi bila wewe na kuhusu kufuata sitaacha mimi ni kama kivuli chako.
Chapter 14
Prisca alizidi kuwa mtu wa mabishano, kila siku alikuwa akitaka uhuru wake wa kuivunja ndoa. yao bandia na hiyo ilileta kutokuelewana.
Kila Jimmy alipomweleza kuhusu majukumu ya ndoa, Prisca alikuwa wa kwanza kukunja uso na
kupinga.
Hakutaka kupika, hakutaka kufanya usafi, na hata kutamka neno mume kwake ilikuwa swala zito Ilifika mahali hata jina la Jimmy hakulitamka kwenye midomo yake alikuwa anakuita wewe.
Jimmy hakujali aliendelea kumpa muda pla alitafuta mtu wa kufanya kazi pale ndani.
Siku moja Prisca aliamua kwenda kwao.
Aliingia chumbani kwa mama yake alisalimia na kukaa pembeni ya kitanda. Wewe bona umekuja asubuhi hivi huko ni
kwema? “Mama, naomba nikae hapa wiki mbili tu nipumzishe akili.
Mama yake alimuangalia kwa mshangao. “Umechoshwa na nini? Si uko kwa mumeo
wewe?
“Mama, siyo kila ndoa huwa unakuja kwa uzuri. Mimi Moyo wangu haupo huko. Unamaanisha nini kusema hivyo?
Ndoa hii ilikuwa ya dili haikuwa rasmi.
Kila siku nakwambia kosa umelifanya mwenyewe unafanya mambo makubwa bila kufikiria madhara yake.
na ukumbuke huyo mwanaume ameshakutolea mahari anatambulika kwenye familia *Mama hujui tabia za yule mwanaume
Lakini anakupenda kama angekuwa hakipendi basi asingekupokea tangia mwanzo wala kulipa ada ya chuo. Alafu angalia ulivyobadilila ni wazi anakuhudumia vizuri.
Prisca alinyamaza, akainama. Mama yake akaendelea kusema
“Mwanangu, unajua kwenye ukoo wetu ukishafunga ndoa huna tena nafasi ya kurudi ya kudai talaka, Hakuna kurudi hapa kama wewe ni mke wa mtu, rudi kwa mumen.
“Mama…”
“Hakuna cha mama. Rudi kwa mumeo na ujifunze kuvumilia. Mapenzi ya kweli hujengwa kwa uvumilivu na upendo. Huwa hayaji kwa. kuokotwa barabarani.
Niangalie mimi mama yako nimeishi miaka 22 na marehemu baba yenu nimevumilia mengi. Prisca hakuwa na la kusema alijiinamia tu.
Wakati unakuja huku umemuaga mume wako? Prisca alitingisha kichwa akimaanisha hapana. “Huo sio utaratibu kwenye ndoa kila inapotokea unatakiwa kumuaga mumeo na akirudi kutoka kazini alikuta nyumbani.
Mama inatisha bwana mimi sitaki hayo. mambo. Hutaki wakati umeyakimbilia?
Prisca alirudi kwa Jimmy jioni akiwa na hasira ya kukataliwa hata na mama yake na kuonekana mama yake kuikubali ndoa yao na kuimwagia
baraka zote.
Alipofika nyumbani Jimmy alimfungulia mlango kwa tabasamu, kama kawaida yake.
“Karibu mke wangu, nilikumiss sana “Hebu nipishe hakunaga upendo wa kulazimisha, Prisca alijibu huku akiweka pochi mezani. “Lakini kuna ndoa ya kujenga kwa maamuzi mke wangu. Jimmy alijibu kwa upole.
“Maamuzi hayo unayo wewe mimi bado sina
maamuzi juu yako.
Bado sijakata tamaa. Prisca alimuangalia usoni kisha akaondoka na kuelekea chumbani..
Usiku ule Jimmy aliandaa chakula mwenyewe baada ya hapo alimuita Prisca kuja kula lakini prisca hakutaka kwenda kula alijifungia. chumbani na kuwasha muziki akachukua headphone na kuweka masikioni. Jimmy aliamua kumuacha akaenda kula kisha
alipomaliza akaenda chumbani kulala.
Jimmy hakukata tamaa. Asubuhi aliamka
mapema akaandaa chai, akampelekea Prisca
kitandani.
“Najua si rahisi kunielewa lakini maisha haya lazima yajengwe kwa upendo wa aina hii Nitakupenda mpaka mwisho wa maisha yangu, sita kufukuza ila Ukitaka kuondoka kwangu utaondoka kwa mapenzi yako mwenyewe. Prisca alimuangalia kwa jicho kali lakini ndani ya moyo wake kulikuwa na kulikuwa na hisia flan. Aliwahi kutamani mwanaume wa aina hio mpole, mwenye subira, lakini sasa hataki kukubali kwa sababu tayari aliingia katika ndoa kwa mazingira yenye utata, dharau na kutokuelewana. Jimmy alinyanyuka na kuondoka priscal alimuangalia kile chakula kwakuwa alikuwa na
njaa alianza kula.
Jioni baada ya muda wa kazi kuisha Jimmy alikutana na Patrick lakini alionekana kuwa mpole sana tofauti na siku zote. *Vipi unawaza nini?
“Mapenzi… Alijibu Jimmy kwa mkato na kusababisha Patrick acheke sana. “Kweli nimeamini mapenzi hayana ubabe.
“Prisca anaumia sana akili yangu, nampenda lakini hanielewi sijui nitafanya nini kaka. “Kanuni ni ileile kaka zidisha mapenzi pale anapokosea akija juu wewe kubembeleza pia. usisahau vizawadi wanawake wengi huo ndio ugonjwa wao.
Siku iliyofuatailikuwa siku ya jumamosi Jimmy alikuwa anataka kutoka, alimfuata prisca na kumwambia.
Natoka ila ningependa leo unipikle pilau.
Prisca alimuangalia kisha akatoa tabasamu. Unataka pilau ya ngamia au ya kuku? Jimmy aliachia tabasamu kisha akajibu.
Ya kuku inatosha mke wangu.
Sawa. Jimmy alimuangalia kisha akatoa kicheko kidogo cha kebehi.
Mida ya mchana jimmy alirudi nyumbani akiwa kaongozana na shemeji yake Deo. Waliingia
ndani wakutane prisca ameandaa hotpot na sahani mezani yani kiliandaliwa kila kitu wakisubiri watu wale. Karibu ndani shemeji.
Asante. Naona dada yako wameshaandaa chakula
tuksruble mezani. Wakiongozana mpaka dinning mara prisca. alifika lakini alipomuona kaka yake ni kama alipata mshituko.
Jimmy na Deo walikaa mezani jimmy alivuta hotpot iliapakue chakula lakini kwenye hotpot ya kwanza hakukuwa na kitu. Jimmy alishusha pumzi na kumwambia Deo.
Shem chukua hiyo hot pot upakue. Deo alivuta hotpot alipofungua alikuta maji.
Alimuangalia Jimmy usoni. “Hiki ni kitu gani? Hii michezo gani shem?
Hayo ndio mapishi ya dada yako Deo alimgeukia prisca na kumuangalia huku akiwa amekunja uso.
Hiki nini umefanya? Haya ndio huwa unamfanyia mume wako ambae akitokea mahali na kujijali familia yako? Au kisa ni kwamba haukufanywa kitchen part? Unataka nikutafutie. mwalimu wa kufundisha nini maana ya ndoa? Nasema hivi kama unafanya haya kwa makusudi ili uondoke kwa huyu jamaa basi tafuta sehemu
ya kwenda sitaki kukuona pale nyumbani. Mimi
nina njaa zangu nikajua nakuja kula kumbe
najuta huu upumbavu. Aiseee pole sana ila kwakuwa ni chaguo lako basi pambana nalo. Deo alimuaga kisha akamsindikiza na Jimmy. Baada ya kumtoa mpaka getini jimmy alipitia kwenye gari lake akachukua mfuko na kuingia ndani.
Alimkuta prisca akiwa bado kasimama palepale, Alimsogelea na kumpatia ule mfuko. Prisca alisita kupokea jimmy alimshika mkono na
kumkabidhi kisha akaondoka akaenda. chumbani. Prisca alifungua ile mfuko alikuta
zawadi tena zawadi za thamani. Priscal alishusha pumzi na kujiuliza. Huyu mtu ana moyo wa aina gani namfanyia mabaya ananilipa haya.
Chapter 15
Taratibu mambo yalianza kubadilika kidogo kidogo kwa upande wa prisca.
Siku moja Jimmy aliporudi kutoka kazini akakuta
nyumba safi.
Chakula kilikuwa mezani, na jikoni ilisikika sauti ya mchiriziko wa maji.
Alisogea hadi jikoni na kukuta Prisca amevaa apron huku akiwa anatengeneza juice. Alisogea karibu zaidi na kumuangalia usoni, prisca pia alimuangalia na kusema
“Leo kuna mgeni mkubwa anakuja hapa?” Jimmy aliuliza kama utani
Prisca alimuangalia kwa jicho kali, kisha akajibu kwa sauti ya chini:
“Unaishi kwa mazoea?
“Sio kawaida ndio maana nashangaa.
“nimefanya kwa sababu nimejisikia kufanya, sio kwa sababu Deo alisema au natumikia ndoa feki.
Jimmy alitabasamu alafu akasema.
“Sawa mke wangu Hata hiyo ni hatua. “Nenda kaoge uje ule.
Jimmy alimuangalia huku akiwa na wasiwasi
hakuwa anamuamini sana Prisca.
“Hili ni kweli au kuna utani unaendelea
“Tena utani wa leo ni mbaya sana. Alijibu prisca
huku akiendelea na kazi zake. Jimmy alitoka jikoni akaenda mpaka dinning kwenye meza akasimama na kuangalia yale maandalizi.
“Kwa nje safi sasa sijui huko ndani kuna nini maana hashindwi kuniwekea mawe kwenye hotpot na kuifunga vizuri kama hivi.
Taratibu alinyoosha mkono na kufungua moja la hotpot kweli kulikuwa na chakula tena kilikua kinanukua vizuri.
Waoooo…. Mara jimmy akahisi kuguswa begani kiligeuka alimuona prisca kasimama nyuma yake.
“Wewe unafanya nini hapa si nilikwambia uende ukaoge kwanza ndio uje hapa mezani. “Sikuwa naamini kama kuna chakula cha kweli. “Nimeshamwambia usiishi kwa kukalia na hayo
yote nimefanya kwakuwa nimejisikia.
Jimmy alimgeukia akamuangalia usoni kwal muda huku akiwa kashika kiuno, tabasamu kwa mbali ambalo lilikuwa linagoma kujitokeza kisha kwa sauti ya chini kasema.
Kweli inaonekana kuna kitu kumekuchal ambacho kinaonekana kwa macho ila kwa maneno ni uwongo sababu mdomo imezoea kutamka maneno ya uongo.
Prisca alikuwa ameshika upawa mkononi kwake akaanza kuipiga piga kwenye kiganja cha mkono wa kushoto.
“Unamaanisha nini kusema hivyo?
Mmmmh acha niache mambo kama yalivyo. nisije nikaivuruga hii siku iliyoanza vizuri. Jimmy waliondoka akaenda chumbani akaoga na kubadili nguo kisha akashuka kwenda kupata chakula. Siku hiyo alikula huku akiwa anakusudia kile chakula kwa utamu.
Maisha yakizidi kubadilika kati yao amani ilianza kutawala waliweza kukaa na kuongea pamoja wakicheka na kufurahi, walitoka pamoja na kwenda sehemu mbali mball,
Siku moja majira ya jioni prisca alipokuwa jikoni
akiandaa chakula cha jioni alianza kunisikia vibaya ghafla alihisi kichefuchefu akachukua limao lakini hakikukeata alitoka haraka na kwenda kutapika. Baada ya kumaliza kutapika alisimama na
kujiuliza.
“Sina homa na imekuwaje ghafla hivi nitaoike na hii kwangu huwa ni ngumu sana. Huwa natapika nikiwa nasoma kali sana.
Prisca alijiuliza maswali huku akiwa ana hisia
kuwa ana ujauzito. Alishika tumbo lake. “Hivi inawezakuwa ni ujauzito? Ujauzito wa Jimmy. Akiwa bado anajiuliza alisikia anaitwa na Jimmy. Alitoka chooni haraka na kumfuata sebleni alimkuta Jimmy kasimama sebleni huku akiwa kabeba mfuko wa zawadi kama kawaida yake.
Prisca alipokuwa kasimama pale sebleni alisikia harufu.
“Mungu wangu nimeunguza. Alisema prisca huku akitaka kukimbilia jikoni lakini Jimmy akamdaka mkono.
“Nimeshazima huko ulikuwa unafanya nini huko ndani?
“Aaa.. ni… Nilishika na tumbo la ghafla. Prisca aliongea kwa kigugumizi.
“Pole.
“Asante
Hii ni zawadi yako. Prisca alipokea na kushukuru.
“Acha niende nikaandae chakula kingine. “Haina haja, twende tukajiandae tutaenda kula nje.
Sawa. Walipandisha wote chumbani wakajiandaa kisha wakatoka na kwenda kwenye mgahawa wa paradise, mgawa maarufu wenye
huduma safi. Walifika hapo wakaagiza chakula, jimmy aliagiza
samaki mkubwa na ndizi.
Yule samaki alipoletwa Prisca alishindwa kujizuia alinyanyuka haraka na kuondoka lakini Jimmy alikuwa kwenye mshangao hakuelewa kwanini prisca alinyanyuka na kuondoka haraka.
Alikaa kwa muda lakini prisca alikuwa hajarudi. Jimmy aliamua kunyanyuka na kumfuata kule alikoenda. Alisimama akawa anaanza macho upande wa chooni lakini hakuona mtu lakini alipo geuka upande wake wa kushoto alimuona.
prisca akiwa amesimama na kijana mmoja
wakiwa wanaongea, wakicheka na kushikana
mikono. Jimmy alishusha pumzi huku moyo
wake ukidunda wivu ukianza kumnyemelea. Mara aliona Prisca anatoa simu yake kwenye pochi yake ndogo na yule mwanaume alikuwa akiandika namba za prisca.
“Yani anampa namba ili wawasiliane? Hapana
huyu ni mwanamke wangu lazima watu waheshimu na kujua mipaka yao. Jimmy alienda pale walipo.
“Jimmy umenifuata huku?
“Kwahiyo ulikuwa unamuwahi huyu jamaa yako? “Hapana huyu ni rafiki yangu tulisoma pamoja sekondari…
“Ilikuwa ni wakati huo prisca sasa hivi ni mrs Jimmy Jimmy alimgeukia yule kijana na
kumuuliza
Kijana sijui unajua kuwa huyu ni mke wa mtu sasa?
“Hakunismvia lakini ni rafiki tu.
“Ndio nimeshakwambia mimi.
“Sawa nimekuelewa.
“Haya futa hiyo namba ya simu sasa hivi. “Jimmy unafanya nini lakini mbona unakuwa sio
muelewa na kufikiria mambo ambayo siyo.
Jimmy hakutaka kuongea zaidi alichukua simu ya yule kijana na kufuta namba ya prisca kisha akamshika Prisca mkono wakaondoka.
INAENDELEA

