KAMA UTANI, IKAZAMA MPAKA NDANI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA 21
Sikuamini kama myra angeongea vile na kunipa mashariti kama yale
” mmmmmh ndo nilivoamua kama unataka minasha na wanao wawe salama unapaswa kunioa … harafu nitaruhusu minasha awe salama” nilimsogelea myra kisha nikamnasa kibao kikubwa ambacho kilimpeleka mpka chini kish nikaita walinzi
“Mtoeni huyu … huyu mwanamke shetani atake nje 😢 staki kumuona ” wakati myra analia huku ananitazama kwa hasira kweli
” malick unathubutu kunyanyua mkono wako na kunipiga ..kwa sababu ya huyo mwanamke kichaaa” Sikutaka anitawale na maneno yake nikamnasa kibao kingine chamoto zaidi
” nitaendelea kukupiga kama utaendelea kumtukana minasha sawa …. chunga sana kauli zako myra sawa”
” nakwambia malick utajutia sana 😢 najua utakuja kwangu ukiwa unalia na kuomba msamaha na mimi nitakuadhibu sana ” alisema maneno yale kisha akanyanyuka na kuondoka zake mimi nikabaki namuoangalia kwa hasira sana 😒😒😒 nilitamani hata kumuua
Wakati myra anapiga hatua kuondoka nilikuwa nawaza mambo mengi sana nilikumbuka vingi sana jinsi ambavyo alikuwa mwanamke mwema sana kwangu . Alikuwa mwanamke wa ndoto zangu mwanamke ambae niliwaza angekuwa mama wa watoto wangu mwanamke ambae niliwaza familia yangu ingekamilika kama ningekuwa nae
Mpaka sasa nilikuwa nawaza sana kwanini gafla tu alibadilika na kuwa shetani akawa mwanamke ambaea anathamini sana pesa na sio upendo . Sikuamini kama ni yeye ambae aliniacha pale nilipo mwambia kwamba sina fedha za kumpa ni anivumilie lakini alishindwa kabisa kunivumilia hili swala lilikuwa likiniumiza sana
Lakin pia mkono wangu ulikuwa ukitetemeka sana kwa kumpiga mtu ambae aliwahi kulala kwenye ubavu wangu na kulala na mimi kama mwanaume wake na akiniita mume wangu .Kiukweli chozi lilinidondoka nikajikuta nalia na muda mwingine nikiamin huenda haya yalikuwa makosa yangu lakini mimi kosa langu ni lip au chanzo alikuwa ni huyu minasha mpka sasa sikuwa na majibu au mimi ndo nilisababisha haya baada ya kushindwa kuzuia hisia zangu na kusaini taraka aisee pale nilipokuwa nimesimama nililia sana
Nikiwa nawaza na kujionea huruma mwenyew gafla nikaona mama ynagu mzazi akiwa na baba tena mkononi akiwa amemshika myra akirudi nae ndani sasa nikashangaa nini tena kinaendelea lakini tena hapo hapo minasha alikuwa amezinduka na alikuwa akipiga kelele ndani na kuvunja vitu mule chumbni
” mbona umeganda gafla unashida gani ….ooooh mwanamke wako tayari amenza kelele si ndio”
” mama kwani hiyo ndo salamu”
” salamu gani unataka wakati umempiga myra bila kujar chochote…. hivi malick lini utabadilika nakuliza”
” kwani mama yangu mzazi umepatwa na nn mbona unaongea mambo ambayo mimi siyaelew”
” wew ni mjinga sana malick unawezaje kuishi na mwanamke kichaa… myra hapa karudi mwenyew lakini unampiga kweli hivi ukoje wew
Imrani akaingilia kunisaidia” mama , minasha na mkweo anaumwa na kumbuka mungu atamponya tu hawezi kuwa hivi milele na kwanini gafla uwe upande wa myra hivi unajua myra kafanya nini kwa minasha”
“Icho kitu ambacho myra kafanya kwa minasha sitaki kujua ila nachojua myra anampenda sana malick na ndo mwanamke bora kwa malick naamini hivo minasha ilikuwa kwa bahati mbaya tu kwahiyo malick ni bora angekuwa na myra tu”
” mama …. lak..” kabla imrani hajamalizia mama yangu alimkatisha
” Nyamaza kimya unajua nini wew .. bora hat ungekuwa umeoa lakini maisha yalishakushinda huna hata mtoto wa kusingiziwa emu acha kuropoka matope”
Aiseee ndani kulikuwa na taharuki sana maana kulikuwa na majibizano juu ya mimi kumuacha myra aondoke na kumpiga myra , sasa hapa ndipo mama yangu alipotoa tamko ambalo lilimshangaza kila mtu
” sasa nasema hivi … malick utake usitake utamuoa myra na huyo kichaa ataenda kwao ” alisema hivo huku akimshika myra na baba akimuunga mkono mama
SEHEMU YA 22
“Sasa nasema hivi…. malick utake usitake utamuoa myra na huyo kichaa ataenda kwao ” alisema hivo huku akimshika myra na baba akimuunga mkono mama
” Mama ….. mama unaongea nini laiki mbona sikuelew “
” ukishamuoa myra bhasi ndo utanielewa sawa”
” Mama nasema hivi …. kama mimi imrani niko hai sitaruhusu kabisa kaka yangu amuoe myra siwezi kabisa kuruhusu ” mdogo wangu alisimama kunitetea
Lakini sasa nilikuwa sielew kabisa hivi wazazi wangu hizo ni akili zao au nawew wamelogwa na myra mbona mwanzo hawakuwa hivi jamani mawazo yakaanza kuwaza huenda tayari hata wazazi wangu wamelogwa na myra mana haiwezekani tu gafla ety wamekuwa upande wa myra na wanamsapoti sana myra
Nilimsihi mdogo wangu anyamaze kimya ili aache watu waende lakini walitamka kwamba myra atabaki hapa mpaka pale mtakapo funga ndoa .Kisha wao wakaondoka na kumuacha myra pale . Kiukweli leo ndo niliona kuwa imrani waga anahasira sana bora hata mimi mana aliwaka sana
Mimi nikaondoka zangu nikamuacha myra kasimama nikaenda kwa mwnamke wangu kwenda kumtuliza minasha wangu ambae tayari alishakiwasha . Nikafungua mlango nikakuta vitu vimevunja vunja yani minasha kafanya uaharibifu mpka kachoka na akapitiwa na usingizi . Nilifika pale nikaanza kumuangalia mwanamke wangu , kiukweli alikuwa mrembo sana mwarabu alafu ameumbika sana
Taswira ya mahaba aliyokuwa akinionesha kama mumewe niliyakumbuka pia tena nilivunia kuwa na mke mwarabu mwenye heshima na kujari . Minasha nilimpata, lakini kwa sasa ni mtu ambae haelew hata anafanya nini hanitambui mim ni nani kwake daaa nilikuwa naumia sana
Mara nikasikia mlango ukigongwa haraka nikaenda kufungua ndipo nikakutana na sura ya myra akiwa mbele yangu
” malick chakula kipo mezani twende ukale “
” sijisikii kula “
” malick ni wew kweli ambae unakataa chakula changu kwa ajiri ya minasha ….. unakumbuka kipind kule nilipokuwa nikikupikia chakula ulisema kwamba radha yake ni ajabu kwani hata mikono yangu pia ni ajabu lakin why leo chakula changu ukikatae malick”
“Naomba nikulizee kitu myra”
” uliza”
” Kipi kilikubadilisha mpaka ukawa mwanamke wa maslay harafu sahivi unamroga minasha ety unataka kuolewa na mimi “
“Najua …. najua nilifanya makosa kipindi kile na ndo mana nimerudi kuja kurekebisha pale ambapo nimekosea “
“Lakini my tayari ushachelewa kwani huoni kama moyo wangu ulifunguka kwa minasha “
” naposema nakuhitaji tafadhari baba nikubalie …. na nipo tayr kulekebisha pale ambapo nimekosea kwa gharama zozote malick”
” najua unachokitaka ni fedha ila mimi ….ila mimi myra pesa sina mimi sina za kukupa nenda tu ukatafute wanaume wenye fedha ila kwangu hazipo”
” Kwako sihitaji pesa tena nataka kuwa nawe katika maisha yangu nakupenda sana malick “
” sikia icho chakula hata sikiamini wew nenda ukale tu chakula chako”
Nilimwambia hivo kisha nikaingia ndani na kufunga mlango sikutaka kumsikiliza kabisa huyu mwnamke nilimuacha akiita tu malick aaah lakini mimi nilipanda kitandani kisha nikamkumbatia minasha wangu tukalala . Asubuhi na mapema watu wote tuliamka reheme akatuandalia chai pale watu wote tukiwa pale mezani tunakunywa chai mara akafika myra kila mtu alipomuona alimtolea macho sana . Imrani akanyanyuka na kudai hawezi kula meza moja na mchawi badae nikamuona rehema akanyanyuka bila kuchoka imrani akamfata na minasha akawa ameondoka nae nikabaki mimi na myra tunatazamana na mimi bila huruma nikanyanyuka na kumtakia chai njema akabaki mwenyew mchawi yule???????
SEHEMU YA 23
Myra aliona tunamfanyia dharau kubwa na yeye aliamua kuondoka na kuacha meza ikiwa tupu . Kiukweli roho yake ile ya kinyama na kichawi ndo ilifanya sisi tuweze kumtenga . Na tulienda kunywea chai jikoni huku tukicheka kwa furaha na amani lakini bado imrani alingangania tumwite shekhe aje amuombee minasha anaimani atakuwa sawa bhasi mimi nikawa nimekubali
Lakini tukiwa tumeketi pale mlango uligongwa na rehema akaenda kufungua na kukutana na babu yake na minasha .Nilishangaa kumuona na yeye aliponiona alinikumbatia kisha akanambia
” mwanangu nyakati ngumu waga hazidumu hili jambo litapita” lakini mimi sikumjibu nilibaki nalia tu kwenye mabega yake “Punguza kulia mwanangu, minasha ni jasiri anaweza kuvumilia kila kitu na atakuwa sawa , hili swala niachie mimi sawa mwanangu”
Nilitingisha kichwa kisha akaniomba nikamwandae minasha bhasi na mimi nikawa nimeenda kumuandaa ili aweze kuondoka na babu yake .Nilimuona tu myra akitabasamu baada ya minasha kuondoka
” sasa mume wangu mtarajiwa …. kwakuwa huyu kichaa hayupo basi ndoa yetu itakuwa yenye amani kabisa”
” Hivi unahisi mimi ntakuoa wew….. endelea kuota ndoto za mchana ” mara na imrani nae akawa amefika akasema
” hata mimi pia siwezi kukubali kabisa kuona kaka yangu anamuoa mchawi ….. shemeji yangu ni minasha tu na ndo namjua”
Myra alisikia hasira sana akaondoka kwa hasira sana na kwenda chumbani kwake . Ikabidi leo niende kazini nikapoteze mawazo mana kukaa ndani na kumuona myra anakatiza tu ndani mwangu nilikuwa napandwa na hasira sana . Nilipofika kila mtu alinipa pole nilimwita secretary wangu na akanipa mrejesho wa kila kitu
Nikatuliza akili ili niweze kufanya kazi zangu, nikafanya mikutano mbali mbali ya kibiasharaa baada ya hapo nikatoka na kwenda kuangalia biashara za minasha maana bado nilikuwa nasimamia mimi . Vitu hivi vilinifanya nimkumbuke sana 😢 minasha wangu
Nilipomaliza kila kitu nikaanza safari ya kurudi nyumbni nilivofika njian nilipaki gari kisha nikaingia supermarket nikanunua chocolate 🍫 kisha nikatoka nikapanda gari nikawa naenda nyumbani , nikafika nikaingia mpaka getini nikashuka kwenye gari nikatoka na kwenda ndani .Chakushangaza nafungua mlango nakutana na myra yupo mlangoni ananisubiri
“Karibu sana mwanaume wangu “
” Asanteee….. harafu mimi sijawahi kuwa mwanaume wako”
” sawa lakini …… leo nimekuandalia chakula kizuri sana … oooh baby umejuaje kama napenda chocolate 🍫 ” bhasi akaishobokea akaichukua mimi nikawa namuangalia tu nikaamua kuingia ndani lakini palikuwa kimya sana ikabidi nimulize
” wameenda sokoni ….. kwahiyo leo tupo mimi na wew tu malick wangu ” alinijibu huku ananipapasa , Nikamuangalia kisha nikamtoa mkono wake afu nikamwambia kama ni chakula cha mezani nitapika mwenyew na hata hicho cha chumbani ni mwanamke mmoja tu anaestahiki kunipa hichi kitu kisha nikamuacha na hiyo code nikaenda zangu
Nikaenda zangu ndani mpka chumbani kwangu nikavua nguo nikaingia bafuni , wakati naoga mara gafla mlango wa chooni ukafunguliwa akaingia myra akiwa uchi jamani haya si majaribu kabisa
” wew unataka nini humu “
” kwani kipi ambacho huelewi mimi nimekuja kuoga na wew mume wangu mtarajiwa”
” toka… emu toa vimifupa vyako hivooo “
” mmmh yani leo unaniona mimi namifupa au sio ety …. sasa mimi humu sitoki” akanambia kisha akawa ananisogelea karibu kabisa
” haya si unataka kuoga …… hata oga bhasi mimi nimemaliza ” kisha nikatoka nikamuacha bafuni nikavaa nguo haraka haraka nikaingia zangu jikoni kwenda kuandaa chakula changu nile wakati naandaa chakula nikampigia simu imrani
” wew mbona hurudi kaka …. au ndo umeenda kupunguza uzito”
” hapana kaka yaani niliyoyajua huku nimakubwa sana kuhusu myra”
” Nini tena …. emu nambie”
” hapana kaka emu subiri kwanza nifike nyumbni ila kaka hakikisha unakaa mbali na myra sio mtu mzuri kabisa ….. sawa kaka”
” namjua si mchawi huyu”
” kaka sio uchawi tu kaka …. myra anamengi sana wew kuwa nae mbali mimi nikija tutaongea” mmmmh nikabaki na mguno hakunipa nafasi ya kuuliza chochote kisha akakata simu
SEHEMU YA 24
Maneno ya imrani yalianza kunitisha nikaogopa sana tena ukizingatia nimebaki mimi na myra ndani nikachukua chakula changu haraka haraka nikakimbia chumbni kwangu mana hata muda ulikuwa umeenda nikaufunga na funguo nikabaki chumbni kwangu .Nikiwa namalizia kula nikasikia myra anagonga mlango
” Malick baba fungua mlango ” alikuwa anaomba myra
” wew si uingie ” ” malick mlango umeufunga napitaje”
” aaaah wew tena ….. kuna kitu ambacho kinakushinda kweli wew si mchawi fanya upite ” nilimwambia hivo afu nikacheka kwa dharau na kujifunika shuka langu nikalala mpka asubuhi kuna kucha nililala kwa amani bila kusikia makelel ya myra, asubuhi nikaamka na amani nikaingia bafuni kuoga kisha nikajiandaa nikafungua mlango na kutoka ,ndo hapo nikakutana na mama na baba yangu wakiwa mezani wanakunywa chai tena wanatengewa na myra
Nikashangaa wamekuja sangapi hawa ukizingatia sikuwa na taarifa na ujio wao lakini so kesi ni wazazi wangu niKasogea mpaka walipo kisha nikaakaa
” shikamoo mama……. ” niliwasalimia huku nikiwatazama usoni huenda hata hawa sio wazazi wangu myra kaniletea madondocha
” Hivi malick ni nani aliekuzaa wew” mama aliniuliza lile swali
” mama ni wew hakuna mwingine ……”
“Sasa kama ni mimi mama ako mbona hutaki kunisikiliza mwanangu au unataka nikulambee na miguu ndo ujue kwamba namanisha naposema wew umuoe myra “
” Mama mimi siwezi kumuoa kabisa myra …… kwanini nimuoe huyu mwanamke shetani mimi Simpendi kwanza “
Mama yangu aliinama chini nikamuona analia kabisa , yaani mama angu analia kisa mimi kutokumuoa myra kweli au kuna lingine ” malick mwanangu kama kweli mimi na mama yako utamuoa myra kivyovyote vile na tena jambo hili litafanyika kesho usiku”
” Mama staki kukuvunjia heshima ….. na nasemaje hapa sifungi ndoa na kahaba huyu myra ” nilisema hivo nikachukua funguo yangu ya gari nikawa naenda zangu kuufata mlango
” kama dharau zimefikia kiasi hichi bora nizalilike tu ” mama yangu akawa anavua nguo kunitengenezea laana , baada ya kuona hivo niliwahi haraka nikaenda kumshika mama asifanye kitendo kile” mama kwanini lakini mama”
” Tafadhari mwanangu malick funga ndoa na myra nakuomba mwanangu”
” Bhasi mama ….bhasi mama angu inatosha jamani kama ni hivoo tu unataka bhasi mimi nitafanya nitamuoa myra” nilimwambia hivoo mama, sikutaka mama yangu ajizalilishe kwa ajiri yangu sikuwa nataka kabisa japo ilikuwa kinyume na matakwa yani maana sikuwa na mpango wa kumuoa myra kabisa
Mama yangu alinikumbatia na kuniambia kama ningemuoa myra kila kitu kingekuwa sawa , kwahiyo ikawa hivo na ndoa ikawa imepangwa ifanyike kesho usiku itakuwa na hafla ya kawaida tu na sio kama harusi za uswazi .Wazazi wa myra walikuja nyumbni kwangu mida ya jioni na kuelewana kisa mahali na my akaulizwa anataka kiasi gani ila yeye akasema hataki mahali kwakuwa ananipenda sana watu wote walimsikiliza yeye na harusi ikawa imepitishwa kufanyika kesho . Lakini mpka muda huo bado sikuwa nimemuona rehema wala imrani harafu kingine simu ya yule mzee ilikuwa pia haipatikani hapo napo nilishindwa kuchanganua mambo nikaanza kufikiri au labda imrani kajua siri za myra , harafu myra kamteka mdogo wangu
Nikapiga kimya kutulia tuone ambacho kinaendelea . Lakini bado nilikuwa na wasiwasi sana kuhusu familia yangu , maandalizi ya harusi yalipangwa vizuri na kila kitu kilienda sawa . Pia myra alienda na yeye kupambwa saluni . Hatimaye usiku wake ndo ilitakiwa kuwa ndoa yangu maandalizi yote yalikuwa yamewekwa sawa kabisa
Maskini mimi jaman nilishindwa hata nifanyee nini mana nilikuwa naenda kuoa bila kurizia tena mwnamke ambae mdogo wangu amenitaafharisha kwamba nisiwe karibu nae . Zoez la ndoa lilianza kuandaliwa na hata wakaalikwa watu baadhi kutoka kwenye ukoo wetu
Bhasi bhana zoezi la ndoa likaanza nikakalishwa pale na mashekhe na mashahidi na chumbani alikuwepo myra mama yangu na mama myra nikakalishwa na kushikwa mikono tayari kuanza kula viapo
” malick unakubali kumuoa myra na kumchukulia kama mkeo” niliulizwa hilo swali lakini ile nanyanyua mdomo niseme kitu gafla tukasikia ” nilisema hii ndoa haiwezi kufungwa kama nipo hai” daa alikuwa ni mdogo wangu imrani pembeni yake alikuwa rehema amemshika minasha ambae alikuwa analia ndani kwa ndani nje yalikuwa ni machozi tu
SEHEMU YA 25
“Malick unakubali kumuoa myra na kumchukulia kama mkeo” niliulizwa hilo swali lakini ile nanyanyua mdomo niseme kitu gafla tukasikia ” nilisema hii ndoa haiwezi kufungwa kama nipo hai” daa alikuwa ni mdogo wangu imrani pembeni yake alikuwa rehema amemshika minasha ambae alikuwa analia ndani kwa ndani nje yalikuwa ni machozi tu
Malick mimi nilisimama na miguu yangu ilikuwa ikiwasha kwenda kumlaki minasha mana moyo wangu ulikuwa unaniambia kuwa ameshakuwa poa . Uvumilivu ulinishinda ilibidi nimuwai na kumlaki minasha wangu , hapo sasa mimi na yeye tulikaa chini na kuanza kulia kwa uchungu mambo ambayo tunapitia yalikuwa magumu mnoo
Mama nae alikuja mbio akiwa na myra akashangaa kumuona minasha akiwa amepona kabisa hata yeye alikuja mahali tulipo na kutukumbatia .Ikawa sio harusi tena bali ni vilio ndipo imrani na rehema wakachukua jukumu la kuwatawanyisha watu ili tubaki familia kama familia tuyaongeee haya mambo na kuyamaliza
Myra akawa kama amechanganyiki yaani mana kupona kwa minasha kulimchanganya sana . Nikamuona imrani baba mahasira anamfata myra, akaenda akamshika mkono kisha akamleta pale ukumbini ili kila mwanafamilia amuone
” aaaah myra ujanja wako na uchawi wako vimeishia wapi….. kabla sijasema kitu kuhusu mpango wako wote wa kufa na kaka yangu anza kutubu mwenyew ” Mimi nikashituka mpango tena wa kufa na kaka yangu yaani anamanisha myra alipanga kufa na mimi kivip yani ” myra ongea sasa kwanini ulimfanya shemeji yangu chozi badala ya kumuuua …. sema acha kukaa kimya”
Mambo ya kusutana humu nilizoea kuyaona kwenye tamthiliya jamani lakini leo namuona myra kama gaidi wa filamu na mimi na minasha tunasimama kama mastelling ” myra sema mama na baba yangu uliwatishia nini mpaka wakawa upande wako wakitaka wew uolewe na kaka yangu ” myra hakujibu hata kimoja alikuwa amenyamaza kimya huju akilia tu kimya kimya ” myra naomba tujibu kulikuwa na haja gani ya kufanya yote haya ilhali wew mwenyew ulimuacha malick ” alizidi kuongea imrani
” YOTE NILIFANYA KWA SABABU NAMPENDA SANA MALICK” alisema hivo kisha akavuta pumzi ndefu na kuendelea ” nilirudi kwake ili kulipa wema alionifanyia toka nikiwa nasoma , sikutaka kabisa malick akae mbali nami lakini namlaumu sana shoga yangu alinambia malick hafai , kiukweli yote haya nafanya kwa sababu nakupenda sana malick “
” hahahahahahahaha ” alicheka sana imrani sasa namimi nikashangaa hivi imrani huyu mdogo wangu anajua nini kuhusu myra ” unanichekesha myra ….. unajua unaleta utani mbona hujasema kama wew unau UKIMWI na umekuja kufa na kaka mbona hujasema kama ulitumia udhaifu wa mama yangu kumpenda minasha na wajukuu zake kumfanya akae upande wako ….. kwanini myra uli blackmail mama yangu”
Mambo machafu yalikuwa mengi sana aliyofanya myra kumbe huko mbeya alienda kujiuza na ndipo alipopata ukimwi na kuamua kuja kufa na malick.Akiwa amesimama pale kabla hajajibu chochote bhasi pale pale alikohoa gafla na damu zilianza kumtoka mdomoni ,Mama yake alimuwahi haraka kabla hajadondoka chini
” namchukia sana minasha sababu yeye ndo chanzo cha yote …. niliweka kiapo kwa mganga kama ndoa hii ingekamilika bhasi minasha na watoto wake wangekufa ama lasi hivo angepona na mimi ku..fa” aliendelea kukohoa huku mama yake akilia kuhusu mwanae .Sasa hapa ndo nikaelewa kumbe ningemuoa myra ningeua familia yangu aisee nilichoka sana nilimuangalia pale myra akiwa katika hatua zake za mwisho nilimchukia sana
Ilipita kama mwaka mmoja hivi toka lile tukio la mimi na myra . Hatimaye sasa ninamiliki vivuruge wawili ndo minasha alikuwa amenizalia watoto wangu wazuri nilikuwa nawapenda sana . Minasha alianza kazi pia na alikuwa mama bora kwa wanangu na mke bora kwangu . Lakini bila kusahau imrani mdogo na ukali wake wote na kujifanya kote kule lakini kwa rehema alikuwa hana kauli
Walipendana na hata ndoa yao nilisimamia mimi na minasha wangu na pale nyumbani alikuja mdogo wangu tukawa tunakaa nae pale nyumbani . Kiufupi amani ilirejea tena nyumbani japo mikwaruzano ya hapa na pale kununiana haviwezi kukosa kwenye familia lakini siku moja mimi na minasha baada ya kuzagamuana nikamuliza
” hivi mina unajua wew ni mwarabu wa tofauti sana kwanza una shepu zuri so kama wenzako kwanini au wew ulichanganywa na wabongo”
” Hahahahaha ila malick …. mimi mama yangu alikuwa mnyamwezi we alikuwa na huo mshepu mpaka baba angu akachanganyikiwa yani “
” sasa hapa ndo nimeelewa kwanini ulikuwa unapiga kazi kama warembo wa kinyamwezi … yaani wanyamwezi bhana wale ni wanawake na nusu daaa aisee ndo mana huishiwi utamu mama nakupenda mpka kufa”
” lioneee tamaa tu ” ” hiii …..sasa mkewangu unataka niwe na tamaa na nani “
” malick wew ni mzeee sahivi, punguza speed ya umeme utaniua humu ndani siku moja “
Aaaaaaah wapi wew … wew mali yangu nasambaza umeme kuleta nuru, ma mpenzi tuendelee na kazi yetu bhana…….
MWISHO

