KAMA UTANI, IKAZAMA MPAKA NDANI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA 16
Nilipomsogelea karibu ndipo nikatambua yule ni myra .Myra aliponiangalia akatabasamu kisha akanikumbatia kwa mahaba . Maskini minasha alivoona hivo hakutaka kuona mengi alipiga hatua akaenda zake chumbni akabadili nguo akatoka lakini bado akanikuta nimekumbatiwa na myra
Hata hakuniambia wapi anaenda akafungua mlango akatoka huku namuangalia nikabaki nimekumbatiana na Myra , hata hivo imrani nae akaamua kutuacha ili tuweze kuzungumza
“Baby utaendelea kunikumbatia tuu jamani …….najua umenimiss sana lakini hapa sio mahala pake”
” sawa ….. tukae hapa kwenye sofa tuongee”
” Jamani mume wangu kwanini tusiendee chumbani …. baby nimekumiss sana”
” Myra …..emu myra tuongee mambo ya maana mana sahivi siko sawa kabisa”
” sawa baby” Tukasogea mpka kwenye masofa tukakaa nikamwambia akae sofa lingine ili kila mtu ajitegeme vizuri mana mambo ya kuegemeana sahivi mimi siyapendi kabisa πππ akaguna tu kisha akakaa pembeni yangu tukaanza maongezi
” Haya nambie kimekurudisha nini kwangu …. si ulisema hunitaki , hutaki hata kuolewa na mimi sasa nini kimekurudisha “
“Hapana baba…..unajua zile zilikuwa hasira tu wala haikuwa akili yangu …kwahiyo nimerudi kwako baba sina kimbilio” alisema hivo huku akijishusha na kunipigia magoti kwa lengo la kuomba msamaha. Lakini mimi wakati huo mimi nilikuwa namuwaza tu minasha kwa jinsi alivoondoka afu ukizingatia na hali yake ilivoo yani nilikuwa nawaza sana
“Emu nyanyuka mama …… mimi kwa sasa siwezi kuwa nawe “
” unamaana gani kusema huniitaji ….. au kwa sababu ya minasha “
“Minasha hayupo hapa kwahiyo tusimuongelee sawa ” nilisema hivo kisha nikageuka pembeni akanigeuza kisha akanambia
” achana na minasha mimi hapa ndo mkeo harisi achana …. nyama yako tamu usiochoka kuila”
“Nyama gani hiyo….. mimi sitaki chochote kutoka kwako na sitaki unipigie simu wala unitafute kwa sasa nimeamua kuwa na minasha kama mke wangu “
” mmmmmmh nilijua tu toka ile siku mina alikuwa anakunyemelea usidanganywe na uarabu wake muongooo huyo ….. mimi nakupenda sana malick “
Wakati huo tunaongea mimi na myra , chumbni kwake imrani alikuwa anaongea na minasha yaani alikuwa akimbembeleza asichukue maamuzi magumu sana
“Shemeji bora ungerudi tuu …… sasa wew unamuachaje mume wako emu njoo bhna”
“Hapana shemeji mi na hali yangu nguvu za kuongea hata sina yeye mwenyew ataamua na ataonesha thamani yangu iko wapi mimi kuongea siwez”
” shemeji nakuomba mimi huyo myra namjua myra hamfai kaka kabisa fanya uje bhana …. mi nakuelewa wew”
Minasha hakumjibu alikata simu kisha imaran nae akatoka na kuja sebleni akanikuta bado nipo na myra .
” kaka samahani kwa usumbufu …. ila natoka kidogo naenda kumchukua shemu pale nje” myra na mimi tukashangaa shemeji gani
” nani minasha au …. kwani kapatwa na nini”
“Hajanambia ila kasema tu nimfate mana anakupigia wew simu yako hushiki so kanambia mimi bhasi” imrani akaongea hivoo kisha akaondoka zake
Myra akaniangalia kwa huruma kweli huku akimsindikiza imrani ambae alikuwa anamwita shemeji yake leo amemkana aliumia sana π’ π’π’ Mimi hata siwazi kabisa nachowaza minasha wangu atakuwa na hali gani
Mara mlango ukafunguliwa akaingia minasha akiwa na imrani tena amechoka kweli nilipomuona moyo wangu ulipasuka paaa nikatamani kujua nini kimemsibu minasha wangu nikajaribu kujikaza ila uvumilivu ukanishinda ikabidi tu nimfate minasha nikamshika
” Mkewangu shida nini mama ….. umeondoka kwa hasira hata hujaniaga “
” hali yangu haiku….” kabla hajamalizia myra akadakia kwa huku akinilaumu
” Hivi malick unanichukuliaje mimi wew….. unaongea na huyo tapeli “
” samahani malick naomba niende ndani mana huu ugomvi mimi haunihusu kabisa ” akiwa anaenda zake chumbani nikamzuia
“Unaenda wapi wakati wew ndo mwanamke wangu , mkewangu, mama kijacho wangu” hapo ndipo nilipomuona myra akishangaa “kumbe minasha anamimba!!! ?
SEHEMU YA 17
Mina akaniangalia kwa mshangao asiamini kama ndio mimi nimeongea .Alijua kama kweli nampenda lakini sio kufikia hatua ya kuongea vile kwa ujasiri tena mbele ya minasha . Myra akabaki anatutazama sasa
” Emu ondoka bhana nataka kumuhudumia mkewangu ” nilimwambia myra kisha nikamkumbatia mke wangu
” Malick hii vita bado mbichi yaani ndo kwanza imeanza …. hivi tu minasha nimuache akumiliki kitu kama hicho hakiwezi tokea” alitamka hivoo myra kisha akawa anaondoka
” Myra hayo ni maneno ya mkosaji ….. kwendra”
Sikujari kabisa kuhusu myra akaondoka huku namuangalia na viapo vyake vya kijinga .Nikamchukua mkewangu nikampeleka chumbni . Nikamwingiza bafuni na kumuogesha mana nilijua alikuwa na hasira sana juu ya mimi kuwa pale na myra
” mume wangu mzuri …. naomba usifanye hivo kwa kunipunguzia hasira baba mimi sina hasira kabisa”
“Najua minasha huwezi sema ila nimekukosea sana “
” Hapana baba ….. mimi sijachukia niko na furaha nina furaha kiukweli mana kwanza leo mbele ya myra umenisaminisha nimefurahi sana “”
“Minasha naomba nikwambie mama ….. mimi nakupenda sana tena nakupenda sana na sijawahi kuwaza kukupoteza mama angu kitu nachokihitaji kwako naomba uniamini amini tu kuwa malick mume wako nakupenda sana “
Bhasi bhana nikaendelea kumbembelezana na minasha wangu kipenzi cha moyo wangu huku tukicheka na kufurahi mwenyew na kwa muda huo sikuipa nafasi akili yangu kumuwaza kabisa myra. Hatimaye mimba ya minasha ilifikisha miezi nane ikabaki tu mwezi mmoja ajifungue hapo ndipo alipokuwa amechoka hata vitu vingi alisimama kufanya . Akawa mama wa nyumbni lakini wakati huo sikujua kama rehema alijuwa na mahusiano
Bhasi siku moja nikiwa na mke wangu tuliweza kuwafuma lakini minasha alisimama upande wa imrani akimwambia kama wamependana bhasi tuwaache lakini kulitokea mrumbano kidogo kati yangu na minasha . Minasha aliongea sana kitu ambacho kikamfanya hata apoteze fahamu
Haraka nilimchukua mke wangu na kumpeleka hospitali na daktari alivomfanyia vipimo alinambia kuwa ni hali ya kawaida tu na atakuwa sawa bhasi nikamuacha imrani pale mimi nikaenda nyumbni kuleta nguo za kubadilisha na baadhi ya vitu ambavyo angetumia akiwa hospitali
Nikiwa nyumbani natafuta tafuta vitu gafla imrani akanipigia simu
” kaka kaka shemeji huku”
“Shemeji kafanyaje …. emu sema haraka “
” shemeji ….. shemeji kaka kaweuka ” mmmh nilipata mshituko mpka nikashika moyo moyoni mwangu niliwaza nini kimemfanya mke wangu kuwa chizi
Sikutaka kuamini moja kwa moja nikaenda mpka hospitali na nilipoingia mahali alipolala nikamkuta amelala imrani nae akaja nae
” Nini hiki mbona ….. mbona umenambia vitu vya ajabu na sahivi namkuta minasha amelala”
Imrani hakuongea ila alinipa tu simu niangalie jamani sikuamini ambacho nilikiona aisee nilimuona minasha akifanya fujo kama mweu sikutaka kuamini kwanza nikacheka sana
” unataka kunambia kuwa …..ety kuwa huyu ndo minasha wangu ” nilimuuliza huku nikimtazama minasha aliekuwa kitandani amelala
” kaka najua huwezi kuniamini ila sasa huu ndo ukweli…..na huyo hapo ndo shemeji “
Mimi sikuwa hata na uwezo wa kufanya chochote ila nilikosa nguvu na nikaanza tu kulia nikiwa nalia pale akaja daktari na kuniambia nimfate ofisini .Bhasi ikabidi nimfate Daktari mpaka ofisini tulivofika tukakaa na kuanza kuongea
” malick hivi unatambua kama mkeo ni kichaa yaani kichaa chake inabidi apelekwe kwenye kituo cha vichaa”
Daktari alinambia kitu ambacho kilinishangaza sana
SEHEMU YA 18
Maneno ya daktari yalinifanya nichanganyikiwe maana sikuwahi kusikia au minasha kunambia kama alikuwaga na ugojwa wa uchizi . Kitu hichi kiliniumiza sana kwani ukizingatia ana watoto wangu wawili ndani ya tumbo lake sasa inakuwaje anakuwa kichaa wa akili kitu hichi kiliniumiza sana akili na roho
Sikuweza kukubali ety minasha apelekwe milembe ila nilimchukua na kumpeleka nyumbani ningemchukulia uangalizi mwenyew si mkewangu bhana
Lakini nilizan ni kazi nyepesi sana kuishi na kichaa lakini ilikuwa ni kazi ngumu sana kwani alikuwa kama mtoto na alihitaji uangalizi mkubwa sana π’
Siku moja wakati nimetoka kwenda kumtazama hali yake yaani clinic kwenye gari akawa analalamika kuwa kiu imembana ikabidi nisimamishe gari kisha nikashuka na kwenda kutafut maji dukani .Ila cha kushangaza nilipofika pale dukani nilishangaa sana kumkuta muuzaji wa duka lile alikuwa myra kwanza nilistop kununua maji kisha nikageuka kwenda kutafuta duka lingine
” malick ” myra aliniita
” nini …….nini unataka kutoka kwangu “
” nothing …… ila kama utahitaji msaada wowote mi nipo tayari kukusaidia najua na taarifa zako zote ninazo “
” kwahiyo unafatilia maisha yangu kwamba chochot ninachokifanya wew unakijua “
” yeah ….. kumbuka wew ndo uliniacha ila mimi bado nakupenda sana na siwezi kukuacha kabisa”
” siwezi ….wala stakuja kuwahi kukuomba wew msaada wa aina yoyote ile sawa “
” hahahaha unajitia kiburi … bhasi dunia yote itakapo kutenga utakuja kwangu ukitambaa na kuniomba msaada “
Aliongea kwa kujigamba kana kwamba anafahamu kitu kuhusu mke wangu
” nini kinachokupa kiburi wew mwanamke “
” tulia baba mambo mazuri hayataki ila kumbuka mkeo kwangu ni kama moto nikiamua namuwasha na nikiamua namzima sasa emu fika nyumbni leo moto nitaumwagia maji na utaacha kufuka moshi “
Akaniachia hio kisha akaondoka zake .Sikumtilia maanani sΓ na nikaenda kwenye gari nikamkuta minasha wangu tayari amelala .Nikaona hii ndo nafasi ya mimi kuendesha gari kwenda nyumbani .nilipofika bado alikuwa amelala nikambeba na kumuingiza ndani nikamlaza kitandani kisha nikaingia chooni kuoga mana nilikuwa nimechoka sana
Lakini nilipotoka chooni wakati navaa nikasikia
” Malick mume wangu naomba maji ya kunywa”
Mmmh kwanza nilishangaa hii ilikuwa sauti ya mwanamke wangu minasha nilimuangalia kwa muda nikawaza au naota nikamshika lakini bado alihitaji maji nikampatia maji akanywa
“Malick kichwa kinaniuma sana na pia sikumbuki chochote mwili wangu unauma sasa “
” usijari mama utakuwa sawa sawa njooo hapa karibu yangu”
Bhasi nikamkumbatia yaani siamini mpaka machozi yananitoka mara simu yangu ikaita kuangalia mpigaji namba ilikuwa ngeni ikabidi nipokeee kujua nani ananipigia
“Baby wangu malick”
” myra…. myra unataka nini kwenye maisha yangu”
” Nataka urudi kwenye maisha yangu ….. malick wew ni wangu hakuna mtu anayeweza kututenganisha “
“Hahahhahaha acha kuota ndoto za mchana binti …. minasha nampenda na nimwanamke wangu “
“Sasa huyo minasha atakufa kwa ajiri yako “
“Kivipi …na unamaana gani “
” namanisha maisha ya mkeo yapo mikono mwangu yaani ukicheza vibaya tu unapompoteza “
” hunitishi wew” “aaaah unakiburi subir nikuonesheee ” alivosema hivo nikasubiri nionee nini atafanya mara gafla hali ya minasha ikachenji pale pale akaanza kuongea mambo ya ajabu ajabu
” sasa kama hutanisikiliza mimi huyo minasha atakuwa chizi daima ” akanambia hivoo kisha akakata simu .Maswali yakabaki kwangu ?????
SEHEMU YA 19
Nikaacha kuwaza kisha nikamfata minasha na kuanza kummbembeleza mana mara nyingi waga ananisikiliza sana mimi pamoja na ukichaa wake bhasi nikamlaza kwenye mapaja yangu nikaanza kumbembeleza ili aweze kulala
Baada ya yeye kulala nikamwita imrani mdogo wangu ili niweze kumwambia kitu ambacho kilitokea leo
“Unajua kaka malick…. kwa sas inapaswa tumuangalie myra kwa jicho la pili “
” Unamanisha nini”
” Namanisha kwamba….. huenda anahusika kwa namna moja au nyingine kuhusu ukichaa wa shemeji”
” usinambie huenda amerogwa na myra “
“Haswa ….. kabisa nahisi amemroga shemeji”
” daaa hapo nimeelewa … ndo maana kumbeee sasa nimeelewa”
“Umeelewa nini braza.. kwanini tusimpeleke kwa bwana ramadhani akafanyiwe maombi “
” hapana …. emu subiri nakuja hakikisha minasha anakuwa salama na unamuwekea uangalizi”
Kaka nakujua sana unatak kwenda kumvaa myra lakini huu si wakati bora emu tuliza hasira na fanya maamuzi sahii”
” hapana imrani hivi unamuona namna minasha anavoteseka ….. tena anaujquzito kabisa myra moyo wa huruma amepeleka wapi”
” sasa yule pale sio wa kumfata na kwa hasira …. cha muhimu shemeji kwanza awe salama harafu mengine yatafata”
Hapo machozi yameshanitoka kama mvua ” nambie sasa imrani nifanyee nini eeety kaka …mwenyew unajua kuwa minasha na watoto wangu ndo kila kitu kwangu staki kumpoteza yoyote kabisa “
“Sawa kaka lakini sasa unahasira huwezi kufanya chochote” imrani aliongea na kujaribu kunituliza . Nilichoamua ni kumualika myra nyumbni kwangu niweze kuongea nae kwa kina
Nae hakukataa alikubali na kusema siku ya jumapili angekuja nyumbani kwangu kuja kuitikia uwito wangu . Bado nilikuwa nikihangaika na mke wangu minasha .Kumuogesha ilikuwa ni mimi kumvalisha kumlisha hata kumbembeleza alale ilibidi nifanye mimi. Lakini pia hata clinic nilimpeleka mimi na tulichoshukuru hali ya mama na watoto ilikuwa njema sana
Alikuwa msumbufu tena haswa alipokuwa akitoloka na kwenda mabarabarani au kwenye majalala ya uchafu . Kitu hichi kilinifanya nimuweke kwwnye chumba ambacho hakina kitu mana hata chumbni kwangu vitu ambavyo vinapasuka nilivitoa kwa ajiri yake
Huu ulikuwa mtihani kwangu na mateso makubwa kwa minasha . Fikiria mtu ni chizi na lakini hapo hapo ni mjamzito wa mimb ya miezi nane kiukweli nilikuwa nikimuonea huruma sana mke wangu
Siku iliyofuata alikuja mtu wa kumtengeneza nywele mke wangu alimtengeneza vizuri japo alikuwa akisumbua lakini akiwa karibu yangu waga anatulia . Pamoja na hayo bado imrani alikuwa akiomba sana tumpeleke kwa mzee ramadhani lakini mimi nilisubiri kuja kumsikiliza myra kwanza
Lakini kumbuka mimi nilikuwa mwanaume.hisia nazo zilikuwa zikinisumbua sana tena hasa pale nilipokuwa nikimuogesha hisia zilikuwa zikinipanda . Muda mwingine niliwaza au nimuombee myra anipe tu anitibu lakini huenda angeniona zaifu sana
Kwahiyo kwa hap nilipambana na hali yangu . Usiku wa kuamkia jumapili nikiwa nimelala na minasha usiku nilishituka baada ya kuota ndoto mbaya sana nilipoangalia upande wangu wa kulia nikashangaa kutokumuona minasha na ilikuwa yapata kama saa 11 alfajiri. Nilinyanyuka na kuanza kumuangalia kama chooni lakini hakuwepo . Nikaendelea kumtafuta mpaka sebuleni lakini hayupo
Sasa nikaanza kuchanganyikiwa sehemu zote sikuona mke wangu harafu nakuja kuingia getini nakuta geti lipo wazi harafu mlinzi amelala . Hapo ndo nikaanza kuona presha ikinipanda nikatoka pale getini kisha nikaanza kumtafuta kwa kumuita kwa sauti mke wangu na kama unavojua mda huo watu walikuwa wengi sana wakienda katika mihangaiko yao
Simu yangu iliita sana π’ na sikuwa hata nampango wa kuipokea ila kwa kuwa iliita muda mrefu ikabidi niangalie nani ananipigia ndo kukuta alikuwa ni myra . Kwanza nilichukia sababu yeye ndo sababu ya mke wangu kuwa hivi . Bhas ikabidi nipokee niweze kumsikiliza anataka nini
” kwani muda wa kuja kwangu umefika mpka unipigie simu sahivi “
” Punguza hasira babe …. naona unahangaika sana kweli kumtafuta huyo kichaa wako emu acha bhana huyo kichaa wako nimemuona huku kwetu anazurura zurura nikawa nimemchukua so yupo salama ” Alisema hivo kisha akakataa simu yani mimi nilikasilika sana .Kwanini anakuwa mtu wa hivi lakini daaaa aiseee
SEHEMU YA 20
Nilijisikia vibaya sana kuona mkewangu nashindwa kumuwekea uangalizi mpaka anakutana na maadui zangu aisee nilijiona mwanaume useless sana . Taratibu nilianza kurudi nyumbani huku nikiwa mnyongee sana π’ kiukweli kuumfanya mkewangu kuwa chizi asiyejielewa na huku akiwa mjamzito wa miezi nane ilikuwa inaniumiza sana
Unajua kuna muda niliwaza labda nimvizie nimuuwe myra ili mke wangu awe sawa lakini nashindwa naona kama nitafany kitu ambacho kitagharimu sana maisha yangu na familia yangu mana hata kama nitamuua myra vipi kuhusu mkewangu na watoto wangu nani atawasimamia au ndo wanangu watalelewa bila baba
Nilifika nyumbani na kumkuta rehema na imrani wamegawana majengo wanamtafuta minasha
” imrani unafanya nini mdogo wang”
” Namtafuta shemeji ndani hayupo ndo mana tuko hapa tunamuangaza “
” Acheni na muende mkaendelee na mambo yenu”
“Mbona kaka sikuelew yaani tusimtafute …. kwanin sasa”
” Nisikilize mdogo wangu …. minasha yupo sehemu japo siamini kama atakuwa salama au la ila mungu atamlinda” Nilisema hivo kisha nikaenda zangu ndani mpka chumbani kwangu
Nilipofika nilichukua kanga ya minasha kisha nikaanza kulia kwenye ile kanga kwa uchungu sana . Nilifikiria sana kuhusu maisha ya minasha wangu yaani kiukweli anateseka sana
Hatimaye muda uliwadia wa myra kuja pale nyumbani. Nilichokuwa nawaza ni kuhusu mwanamke wangu tu na mwanangu ambae ni minasha na mimba yangu Niliwaza huenda myra akafanya jambo baya kwa minasha wangu . Lakini myra akafika akiwa na minasha tena akiwa amemfunga kamba na akiwa na mlinzi wangu wanamwingiza ndani
Nilimpokea mke wangu na kumfungua kamba zile na kumpeleka chumbani . Nilimuacha myra akiwa amekaa sebleni mimi nikaingia chumbni na mke wangu nikamvua nguo kisha nikaingia bafuni na kumuogesha vizuri . Kisha nikatoka pale chumbni nikaenda jikoni nikachukua chakula na kupeleka chumbani . Nikampa chakula minasha wangu na kuanza kumbembeleza ili alale
Myra alichukizwa sana tabia yangu ya kutokumjari na kuendelea kufanya mambo yangu tena namuhudumia malikia wangu . Nilipomaliza na kuona kabisa minasha ametulia na kulala na kichaa chake ndo mwanaume nikatoka na kumkuta myra yani amewaka kweli kajaa hasira yani ile nafika tu sebuleni nae anasimama
” hivi malick unanichukuliaje yani ….. unaniweka mimi hapa kama mapambo ya sebuleni” Aliongea lakini mimi sikumjibu nilienda nikakaa kwenye sofa kisha nikampa ishara ya kwamba akae tuongee kwa amani kabisa
” Malick unazalau sana si ndio… hivi unajivunia nini wew lakini”
” Kitu ambacho najiuliza … kwanini hukunichawia mimi ukamfata mke wangu ambae hana hata hatia yaani natamani sana kujua “
” yote nafanya kwa sababu yako malick …. mimi namchukia sana minasha ndo mana nimempa adhabu kama ile”
” stop it sawa … mbingu zitakuadhibu myra naomba muache minasha”
” unataka minasha awe salama”
” ndio fanya hivo na hio azabu nipe mimi” nilisema hivo bila kujua myra anawaza nini kichwani mwake
” Mimi siwezi kukuadhibu wew mana nakuhitaji sana ila kitu kimoja nataka”
” unataka nini wew mwanamke”
” ili huyu mwanamke wako malikia wako awe salama naomba unioe mimi hapa ……” alisema hivo kisha akatabasamu kwanza mpka rehema alitoka jikoni imrani alishituka mimi ndo nilitumbua macho nisiamini hivi ni kweli au naota????????
Inaendelea…….

