KAMA UTANI, IKAZAMA MPAKA NDANI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA 1
Umeshawah kuoa alafu hujui Kama umeoa, au unaenda sehemu unashangaa watu wanakupongeza kwa kufanya kitu ambacho hata wewe mwenyewe hujui Kama umekifanya, hicho ndicho kilichonitokea Mimi sasa…
Nimetoka zangu kazin nikarudi home, nashangaa namkuta mlinzi ananipokea kwa tabasamu na kunipongeza Kisha akanambia ” ila wewe msiri Sana..
Sikumuelewa na Wala sikujali nikaingia zangu ndani Napo nikamkuta baba na mama yangu wakiwa wamekaa kana kwamba wananisubiri, maana akanambia ” yaan Malik wewe Ni wa kuoa bila kuiambia familia yako kama unaoa kweli..
Mama nae hakuniacha ni kunizoga tu “yani wew malick naomba huyo mwanamke aje nyumbni leo nataka kumuon leo maliiiiiiick hatujamliza” mama nae akasema nikaona nyumban pagumu nikatoka kwenda kwenye gari haraka sijakaaa sawa ukaingia ujumbe kutoka kwa myra
” HEART BROKEN 💔” ilisomeka ivoo aisee kichwa kiliwaka moto
Myra Ni mpenzi wangu ambae nilikuwa nampenda Sana na nilipanga kumuoa siku sio nyingi sana
SEHEMU YA 2
Ujumbe wa myra ulinivuruga kabisa yani nikawa wamoto kweli .Kutuma ujumbe nikashindwa kuongea nikashindwa nikabaki tu natetemeka yani nikamuwaza yule mwanamke kwanza nikaona ngoja kabla sijaenda kwa Myra wangu nikaona nikamuone yule mwanamke kwanza nimulize kwann afanye ivii lakini unajua ilikuwaje ngoja nikupe story ya jana
Naitwa malick nadhiru amour wengi wanapenda kuniita mi amour haswa habity wangu myra Baba angu nintajir anamiliki mali nyingi sana na kwetu pesa zipo ila sasa tatzo ni kwamba mama na baba angu walikuwa wanataka mimi nioe nipeleke mke nyumbani na ndo ugomvi wangu kila siku na wazazi wangu .Kwahiyo mimi kama malick nikaona niondoke tu niende nikapige moja mbili pale club
Nikiwa nimekaa akaja mdada mmoja wakati tayar nilishaanza kulewa
“Samahani kaka nina shida naomba unisaidie “
” mmmh mrembo shida gani iyo na ni usiku “
“Kaka angu nilikuwa nashuti movie lakin mmoja wetu hajafika kwahiyo naomba kaka unisaidie ni nikipande kidogo tu jaman” akasema yule mdada mimi sasa napenda kuwa stelling chapu tu nikakubali kwa moyo mkunjufu nikaenda kushut kipande cha ndoa mim nikafunga ndoa na yule binti akiwa kapendeza na mabusu mengi nikampa
Sasa icho kipande ndo kimepostiwa alafu kaandika na maneno ya kwamba yeye ndo mke halali wa malick nadhiru jaman akanitag kabisa bila kujua myra wangu atakuwa kwenye hali gani. Kwenye gari nikiwa na hasira kibao huku nikiapa yani nikimkamata huyu mwanamke aisee ataona mbingu ya saba🤣🤣🤣
Siwezi kukwambia nilijuaje kwake huyo binti ila nilipofika nje ya nyumba yao maajabu nilimkuta huyo bint katulia pale njee nikashuka kwa hasira na ghazabu nikamfata yule mwanamke
” Nilijua tu ungekuja na ndo mana nilikaa hapa nikusubiri” alisema yule mdada
“Kwahiyo kila kitu ni mipango umepanga wew ” nikimwambia huku nikiwa na gazabu kweli
Kwa majina yake kamili aliitwa aliita Minasha chotara wa kiarabu sijui kama kweli alikuwa muigizaji ila kwao kulionekana kuna pesa chafu Sasa akajua kabisa mimi nina hasira hakujari ila alinikumbatia kwa mahaba tele jamanie nyie😍😍😍 nikatulia mwenyew nikasikia sauti
” huyo ndo mgeni ambae tunamsubiri ndani” kheee saut nzito kweli iliuliza wakati mm nimekumbatiwa na Minasha “ndio baba huyu ndo mume wangu””
Mimi nikabaki sielewi nini??????????
SEHEMU YA 3
Macho nikayatumbua jaman sasa sielewi Mina anataka nini kwenye maisha yangu
“Tafadhari malick naomba unisaidie sahiv then tutaongea kila kitu baadae plzz malick”
” kwann niwe mimi lakin ety jaman mim nina mpenzi binti” Minasha aliniomba sana mpka akanza kulia na katika maisha yangu sipendi kuona chozi la mwanamke kwahiyo nikakubali tu nifanyaje sasa jaman😒😒
Nikaingia ndani ya mjengo ule wenye wafanyakazi kila sector jaman kunawatu wanaish maisha matamu mana nikisema mazuri nakosea🤣🤣 .Nikapokewa vizuri bhas baba wa minasha akaniuliza maswali na mimi nikajibu kwa kudanganya ili mina asijisikie vibaya na hapo nikawa nimemsaidia binti huyu mina .Muda ulivoisha nikaaga na kutoka na mina hapo hasira zikaanza upya nikawa namuangalia kwa jicho lingine kabisa
“Malick naomba unisamehe sana najua kabisa unampenz wako anaitwa myra lakini kila kitu mimi nitaweka sawa ” akasema kwa kujiamn kweli mimi nikawa namuangalia tu “utaenda kumuambia nini mwanamke wangu ili akuelew hivi unajua unaniharibia vitu vyangu lakini “
” am sorrie amour jaman”Mina akasema huku akishuka chini kuomba msamaha nami nikawa namtazama tu akaendelea kulia huku akiomba samahani .Mimi sikumjibu mtu nikashika funguo zangu na kuanza kulifuata gari langu tayari kwa kuondoka lakin mina aliniwahi akanishika mkono akarudia tena kusema
“Malick naomba nisamehe sana “lakini sikujari mwamba nikapanda gari tayari naenda kwa myra wangu sikujua hata hali ya moyo wake ipoje nilichochea spidi mpaka nafika nje ya geti la kina myra tayar nilishafanya mazoez namna ya kuomba msamaha nikaandaa na mvua ya machozi mana mwanaume akilia ujue anamanisha😅😅😅 Myra wangu alikuwa amepanga na alikuwa mwanachuo ambae mwaka huu alikuwa anamaliza na tuliahidia kufunga ndoa lakini sasa mambo yameanza kwenda kombo sasa sijui naenda kumwambia nini myra wangu Bhasi bwana mi nikazama mpka ndani nikamkuta myra wangu ametulia anaangalia muvi huku kashika tama pembeni kuna popcorn 🍿 😄 anakula
Mimi nikafika nikakaa pembeni yake “toka kwangu malick sitaki kukuona”
” Baby 👶 wangu nipe walau dakika 3 tu nitakwambia kila kitu”
” malick siwezi kukuelewa kwa chcht mana everything is exposed baba mimi sitaki jaman wew ni sumu kwangu tayari mume wa mtu”
“Noo my wangu mm nakupenda wew yule pale alifanya vile ili kuokoa maisha yake”
“Hapan kwanini ??? Haya kwanini nikusikilize yani najiuliza jaman sijui nimekosa nini ….eeeh au kwa sababu mimi msambaa yule chotara wa kiharabu lakini malick kumbuka uzuri unanunuliwa tu ” alisema hivo huku akiendelea na mambo yake weeee nikaona hapa sitasamehewa bhasi mwanaume nikamwaga machozi hadi kama🤣🤣🤣si huku nikitoa maneno ya huruma ila nyie jaman mwenzenu nikalia pale😭😭😭mpka nikamuona myra anaanza kulegea ” mi amour baba bhas mimi nimekusamehe jaman niiiimekusamehe sasa haya nyanyuka na unyamaze”
“Wew sijui unataka mm niutoe moyo wangu uuone jaman ndo uamini jaman”
” nakusamehe ila kwa sharti moja “”nambie tu mama angu kwako mm sina kipingamiza”
Nikasema ivoo ili nipate msamaha ” nataka unitambulishe kwenu na univalishe pete ya uchumba “mmmh kwanza nikastaki na kutulia mana hili jambo so dogo🤔🤔🤔
” aaaah sasa baby ilo jambo si tulishakubaliana kuwa mapka umalize mama angu”
” unataka msamaha au hutaki ” akasema myra huku ananitazama kwa macho makali daa sina jinsi malick mim nimepatikana bhasi tu ndo nishapenda ” sawa mama angu unataka lini” nikauliza huku nikiwa nasubiri majibu 🫣🫣🫣
“Nataka kesho mimi nataka kesho ilo jambo” 🤯🤯🤯🤯nikashtuka jaman lakini sikuwa na naman kama ndo mam mtu kaamua mimi nani nimpinge .Bhasi bhana mi nikakubali hapo nikaanza kumchoka angalau nipate utamu wa moyo mana kwenye hayo mambo kwakweli myra alikuwa fundi tena hodari .Nilimuona akisimama kisha akaenda kusimama kwenye mlango kisha akaninyooshea mkono akinambia njoo baba tuburudike ..mimi sasa mwee nikataman hata nitambae na miguu mana kunyanyuka nilikuwa kama nachelewa 😂😂😂
IYO KESHO SASA
Kwa uchovu niliokuwa nao ilibidi nilale kwa myra nijilie vitu vyangu mana hata ivo asubuhi yake ilikuwa ni weekend sikuwa na shaka lolote kwa sababu sikupaswa kwenda kazini kwahiyo nilikuwa tu nabilingita na mkewangu wangu myra
Bhasi tukajiandaa wenyew tukavaaa tukapendeza taayari tulipendeza sana tena myra wangu alikuwa ndani ya abaya na alifunga ushungi kwa umalidadi mkubwa nikasema mke si huyu. Tukaingia kwenye gari safari ikaanza kuelekea kwa baba na mama malick. Hatujuchukua muda mrefu tukafika nyumbani kwetu mlinzi akafungua geti tukazama ndani mimi na myra wangu tukazama mpka ndani .Mama na baba walikuwa chumbani nikamtuma mfanyakazi akaenda kuwaita
Mama na baba yangu wakashuka taratibu huku macho yao yakiwa yanamuangalia myra huku nikimuona mama akinongona mbona kama siyo yeye mkewe mama alinongona ila mm sikujari nikamkalisha chini mama na baba kisha myra nikajiandaa kuongea ila kabla sijasema kitu akaja mlinzi wa mlangoni
“Samahan madamu kuna watu wapo hapo njee ” kwa hasira ya kukatishwa maongezi nikamuliza kwa hasira”anadai yeye ni mkwe wa familia hii” alisema mlinzi mmmh nikaguna jamani ikabidi mama anyanyuke na baba waende wakaone hao wageni na mkwe wao
Ile kutoka nje alikuwepo minasha na familia yao wakati huo kavalishwa mavazi ya harusi ya gharama kweli kafunikwa na baba yake akasema “Mr amour tumemleta mkweo “
Mimi nikatamani dunia ipasuke harafu niingie🙆🙆🙆🙆
SEHEMU YA 4
Nilitamani aridhi ipasuke mimi niingie .Niligeuka nyuma kumuangalia myra moyo wangu uliuma sana chozi lake lilivo dondoka niliumia mara 1000 .Wakati huo minasha amefunikwa ety ndo biharusi wangu
“Tumeona tumlete mkweo Mr nadhiru ili muweze kukaa nae “
“Hakuna shida kama kashafika nyumbni bhasi yupo salama kabisa ” bhasi baba na yeye akamuita mfanyakazi wetu wakaenda kumchukua minasha na kumpeleka ndani rena chumbani kwangu kabisa .Nilichokifanya nikamchukua myra wangu na kwenda kumpeleka nyumbani kwake njia nzima myra wangu maskini alikuwa kimya tu huku akifuta machozi aisee mimi kama mwanaume niliumia sana jamani
Nilimfikisha mpaka kwake , lakini hakutaka niingie ndani akanambia ” malick naomba uondoke ila kesho njoo unione baba naomba usichelewe” aliniambia ivoo akanipa moyo mana nilijua atakuwa na hasira sana alinikumbatia na kunipa busu la upendo na akaniomba niondoke nikapumzike
Nikamuomba myra wangu nilale pale lakini aligoma na akaniambia niendee nyumbani kwanza na mimi kwa myra sina kauli nikanywea kama nimemwagiwa maji kisha nikaingia kwenye gari safari ikaanza mimi kurudi nyumbani lakini nilikuwa nina hasira na minasha maana kwa alichokifanya sio sahihi kabisa nikachoma mafuta haraka kuwahi nyumbani
Wakati huo nyumbani minasha alikuwa amepekekwa chumbani kwangu na bado alikuwa amefunikwa sura yake mimi nikipofika nyumbani nikapaki gari nikaingia moja kwa moja mpka chumbani kwangu ndo nikamkuta mina amekaa kafunikwa usoo .Sikutaka kuongea ila nilimuwasha kibao kimoja cha moto sana
“Unahisi wew ni nani kunifanyia ivii au umefurahi baada ya kujeruhi moyo wa mwanamke wangu au unahisi sis hatuna mioyo na maumivu hatupati ety nijibu” niliongea mpaka neno la mwisho lakin binti hakunijibu wala kutia neno nikaona mbona izi ni dharau pro max .Ikabidi nimfunue nilichokikuta aisee moyo wangu ulijaa giza aisee
Nilichokiona ni sawa na unyanyasaji ambao alikuwa amefanyiwa minasha na wazazi wake kwanza mdomoni alikuwa amepigwa gundi ambayo ilimzuia hata kuongea uso wake ulikuwa umejaa kutokana na kwamba alikuwa amepigwa sana niliona uso wake unaalama nyekundu za vidole vyangu kibao ambacho nilikuwa nimempiga .Mina aliniangalia kwa huruma hukua machozi yakimtoka😭😭😭😭 mimi mwenyew nilishindwa kujizuia kudondosha chozi moyoni nikajiuliza mimi nasema naumia kumbe kuna watu maumivu ni chakula
Nilimyanyua kwa upendo kisha nikampeleka bafuni na kumuacha huku nikimwambia aogee ili mwili ukae sawa mana inaonekana alishushiwa kipigo cha maana yani .Nikawa nina maswali mengi ya kumuliza mina yani mpaka nikaona kama kichwa kinapata moto kabisa .Lakini niliona acha nimuache apumzike kesho nitamuliza
Nikatoka haraka haraka mana hata muda ulishaenda sana nikaenda zangu kulala kwenye chumba cha wageni na kumuacha mina akiwa chumbani kwangu .Nililala huku nikiwa natazama dalini nikiwa na maswali kibao kum kichwa hatimaye usingizi ulinichukua nikalala.Asubuhi nilipoamka na kushika simu yangu nikaona ujumbe wa myra sikutaka kukumbuka kabisa kama kuna mina yupo chumbani kwangu nilichofanya nikaoga vizuri nikajiandaa tayari kwenda kwa mchumba wangu myra
Nikatoka bila hata kuliza kama mina ameaka au laa nikachukua gari yangu na kuondoka nikaenda kwa mwanamke wangu nilipofika nikaenda moja kwa moja mpka ndani kwa myra nikapakuta peupe yani hamna hata kijiko aisee myra kaamua kunikimbia jaman …..🙆🙆🙆
SEHEMU YA 5
Myra kaamua kuondoka kabisa yani amehama hata bila kunambia jamani nilihisi kuchanganyikiwa nikatoka mkuku mkuku mpaka kwa dada mmoja ivi alikuwa rafiki yake sana na myra aliitwa hadija nikamfata ili anangalau nimulize nini kinaendelea .Nilimkuta dada wa watu anafua nikamsalimia na kisha maswali yakaanza
“Vip huyu mwenzio amekuaga ” nilimuliza huku namuangalia machoni
“Ndio kaniaga kanambia kwamba umeenda kuhamia kwenye nyumba yenu mpya “
Nyumba mpya nikashangaa nyumba mpya ya wapi jaman
“Mimi ndo kanambia ivoo na kaamisha kila kitu kaondoka hapa”
Duuu nikakuna kichwa iii nayo mpya kweli myra jaman mbona anautesa sana moyo wangu kwann ananifanyia ivii nikatoka pale kwa hasira nikaenda kwenye gari kisha nikachukua simu yangu na kuanza kupiga namba ya myra lakini hakuongea myra ila alikuwa mtu mwingine akusema namba nayojaribu kupiga ipo bizeee
Yaani myra wangu kaamua kuniblock kabisa daa jaman jamanie
Sasa hapo akili ya kwenda kazini ikanijia na chapu nikageuza gari langu na kuondoka kuelekea kazini kwangu
Wakati mimi naangaika na myra huku kuna mtu anaamka akiwa na maumivu mazito sana hakuwa mwingine bali ni minasha bado alikuwa amechoka sana .Aliketi kitandani na kuanza kuwaza hatima ya maisha yake
Ilikuwa kama bahati kuzaliwa kwenye ile familia kubwa ya kitajiri lakini maisha yake yote akuishi kwa amani kabisa kwa sababu ya kuzaliwa nje ya ndoa ndani ya nyumba ya bwana ally minasha alichukuliwa kama mfanyakazi wa ndani kwani familia yake yote ilikuwa ikimchukia kasoro mama yake ndo alimpenda sana mwanae na kumpa moyo kuwa mkakamavu
Mama yakehakuchukua muda mrefu sana dunian bhasi nae aliaga dunia na kumuacha minasha akiwa mpweke .Wakati huo minasha ndo alikuwa anamaliza masomo yake ya chuo na taarifa izooo zilimnyongonyesha sana .Ndugu walipoona kikwazo kimeondoka bhasi wakapanga kumuondoa kabisa nyumbani hapo wakamtafutia mzee wa kiarabu ili aweze kumuoa mina na ilikuwa ni ndoa ya lazima
Mina ndo kuchukua maamuzi ya kwenda kutafuta ndoa kwa nguvu na ndipo akakutana na mimi na tukafunga ndoa ili yeye asiolewe na yule mzee na baada ya hapo ndipo alipoletwa kwetu akiwa tayari ameshushiwa kipigo cha maana kwa kwenda kinyume na ndugu zake
Hayo ndo yalikuwa maisha ya minasha .kitandani pale alitafakari namna ambavyo anaweza kuongea na malick na akamuelewa aliwaza sana .Pia alijilaumu kuvunja na kuharibu mahusiano ya watu yaan myra na malick.Akiwa kwenye dibwi la mawazo mara mlango ulifunguliwa na akaingia mama yake malick
“Mkwe wangu mbona upo tu ndani shida nini?? Na malick yuko wapi hajui kama.leo alitakiwa kubaki na wew ndani ?
“Naona ameamka asubuhi sana nahisi atakuwa ameenda kuninunulia nguo mana sina nguo hata moja”
Aaaaa ni malick kweli ndo kaenda kukununulia izoo nguo au unaniongopea my dear “
“Hapana mama malick mimi namjua ni mtu wa tofauti sana
Wakati wao wanaongea mara wakasikia kitu kimepasuliwa hawajakaa sawa tena kingine wakati huo mm namalizia hasira za kuachwa na myra kwenye vyombo vya ndani .Mama alitoka akiwa na minasha wakishuhudia hasira zangu .Yani myra alikuwa zaidi ya maisha yangu kuondoka kwake kwenye maisha yangu lilikuwa ni pigo kubwa sana kwangu🥹🥹🥹🥹
Inaendelea……….

