BABA YAO ALINIOA ILI APATE WATOTO WA KUWATOA KAFARA
Kaka mimi nina Watoto wawil,Nilizaa na baba fulani nilikaa naye miaka 9 baadae alinitelekeza,lakini alitumia njia mbaya mno aliniita mahali akiwa na mke mwingine akaniambia yeye hakuwa na mpango na mimi yeye alifuata kwa sababu zake tuu? nikamuuliza kwa hiyo nyumbani kwetu mlifata nini hadi kufata taratibu zote? akatulia tuu huyo mama aliyekuja nae ni mke waliyeachanaga zamani,
Naomba nifupishe,YULE MAMA ALINIAMBIAGA MAMBO MABAYA SANA NILILIA KWA UCHUNGU SANA HIYO SIKU MAANA NALIKUMBUKA WALIPOENDAGA NYUMBANI YEYE NA WAZAZI WAKE BABAANGU MKUBWA ALIWAHOJI SANA AKAWAAMBIA KAMA HAMNA MPANGO NA BINTI YETU BORA MUMWACHE WAKASEMA TUNA NIA NJEMA.
Sasa baada ya kulia nikaambiwaga unapiga makelele ya nini hayatakusaidia, mtoto wangu alikuwa na Miaka 4 akaja akanifuta machozi akaniambia nyamaza mama yangu,nilipoona Majungu yamezidi kutoka kwa huyo mama nikasimama nikaondoka,Nikafika nyumbani mtoto mkubwa akawa kama kachanganyikiwa akawa anajiongelesha na kuzunguka zunguka,Kiujumla alipata shida ya kipsycholojia ndugu zangu wakaangaikaa nae akaja akakaa sawa baada ya muda,tulipokaa kama miezi 3 mtoto akapata matatizo makubwa sana haikukaa sana mtoto mdogo nae yakampata yaliyo mpata kakaake,
BAADAE KATIKA KUHANGAIKA MAKANISANI NILIKUJA KUAMBIWA NA MTUMISHI AMBAE HATA HANIJUI KUWA BABAAKE ALITAKA KUWATOA KAFARA,
NiIilia sana nikaunganisha na ile KAULI YA KWAMBA NILIKUFATA KWA SABABU ZANGU TUU,SASA NIMEKUJA KWAKO KWA VITU VIWILI.NAOMBA UNISHAURI MIMI WATOTO WAMEKUWA KIDOGO KWA SASA LAKINI Sina hamu ya kuolewa kabisa sina hamu hata ya mwanaume
Wakati mwingine natamani kuwa na rafiki tuu wa kupiga story lakini nikiona mwanaume wa kabila la huyo baba hata huyo rafiki naona Sihitaji,Jamani mwanaume alinifanyia kitu kibaya yule alinitelekeza nyumba ya kupanga Kodi ikawa imeisha,Mtoto ni mchanga huyo wa 3 halafu nina mshono halafu mtoto ni Pre mature Jamani mwacheni tuu Mungu aitwe Mungu.
LA PILI NISAIDIE NIMSAIDIEJE MWANANGU AWE SAWA MAANA YEYE ANASEMAGA BABAAKE ASHAKUFAGA hata Shuleni anasemaga hivyo hivyo nimemuonya na kumbembeleza sana lakini habadiliki nikamwambia Mungu anapenda watu wenye Moyo safi hataki anasema sintosahau ile siku ulivyolia kwa uchungu,
Nisaidieni nilimwambia akisema tena babaake amekufa Nampeleka Polisi akasema kama hajafa yuko wapi sasa Mara aseme matatizo yote yale tuliyopata alishindwa hata kutuma meseji aseme pole,Yaani ananishinda kwa Point lakini mimi nataka asamehe amekataa,nisaidieni nimfanyeje?
Na huyu mtu hajawahi kuuliza Watoto wanaendeleaje ni mwaka wa tano huu,sikuwahi kujua kuna Wachaga wako hivi kweli.

