Baba Alikuwa Anatuvutisha Bangi, Kisha Anatufanya Matusi
Nina miaka 25 katika familia yangu tupo watoto wa 3 kipindi naanza kupata ufahamu nilikuwa naona baba na mama yangu Wanatupenda sana maana walikuwa hawatukatazi kufanya chochote kwa mfano inaweza ikawa siku ya sikukuu baba anatuambia tutoke twende tukatembee. Tukifika bar anatuagizia safari na varuu tunakunywa ikaenda hivyo mpaka mama yangu akawa mlevi kabisa mlevi wa vilabuni akawa anatuacha sisi na baba yeye analala vilabuni
Kipindi hicho Mimi nipo darasa la 3 Kuna siku tulilewa sana nimelala usiku mkubwa nikashtuka nikakuta tumefungiwa mlango wa chumbani kwa nje maana tulipopanga tulikuwa na chumba na sebule lakini tupo Mimi na mama ndo tumelala dada yangu hayupo kuchungulia kwenye kitobo Nakuta baba anafanya uchafu na dada yangu
Nikawa sina amani hata tukiambiwa kunyweni Mimi najifanya nakunywa kumbe namwaga basi mama akaja kujua kama baba anatembea dada yangu lakini hakufanya chochote basi tukahama pale baba akajenga nyumba tukahamia kwetu basi kule ukawa ndo uhuru akaanza kutuvutisha na bangi lakini mama aliona ni sahihi hakulipinga hilo tukawa walevi wa bangi na pombe sigara
Yaani baba akawa haogopi ikifika usiku anakuja chumbani akahama kwa dada yangu akaja kwangu akawa anataka aniingilie nikahama nyumbani nikahamia mitaani nikawa nalala nje mama yangu akaja akachanganyikiwa akarudishwa kwao hatujakaa sawa dada yangu kajinyonga kafa baba kaowa mke mwengine
Kwa hiyo nikawa Sina msaada katika kuhangaika kwangu nikapata bwana akanistili japo Hana maisha mazuri lakini Nina uhakika wa kula nalala pazuri na sikosi hela mama yangu tokea aondoke ni miaka 12 Sasa Sina msaada wowote anaendelea na mambo yake hajui nakula wapi Wala nalala wapi
Sasa juzi baba kanipigia simu anasema mama kachanganyikiwa tena na Mimi ndo mtoto wake niliobakia ndo natakiwa nimsaidie maana Hana makazi Wala malezi Naombeni mnishauri jamani nimechanganyikiwa sielewi nifanye Nini
Kwa huyu mwanaume nimestirika lakini Kuna changamoto za Kila aina kipindi nafikiria nipange chumba nianzishe maisha yangu ya kujitegemea naambiwa nimsaidie mama sielewi namsaidiaje maana Mimi mwenyewe Sina msaada nimechoka kwa huyu mwanaume nakula nalala lakini akiamua kunipiga, ananipiga mpaka na panga
Yaani hapa nina makovu usoni kwa ajili ya kipigo nishaurini jamani nifanye nini?

