NYOKA WA KUTUMWA
Sehemu Ya 6
………………. Ilipoishia …………………………
maana yule nyoka awezi kukubali kuona munaharibu nyumba yake kwahiyo ataanza kuwauma na hatimae mukapata madhara ya kujitakia.
Watu walibaki vivywa wazi maana hawakutegemea kusikia maneno yale kutoka kwa mzee sube, Kikoa kiliendelea na mwishowe wakaamua kufanya kama alivyosema mtu wa kwanza kutoa wazo, wakachaguliwa vijana shupavu mashujaa mahodari kwenye masuara ya utegaji mitego na kuwapa kazi na hatimae kikao kikafika mwisho.Siku ya pili ilipofika wale vijana waliochaguliwa kuifanya kazi wakachukua zana zao za kutengenezea mtego na kwenda nao sehemu ambayo ilisemekana huyo nyoka kufika mara kwa mara. Walitega huo mtego kisha wakamchukua mbuzi na kumuweka ikiwa kama chambo cha kumuitia nyoka, Walipomaliza wote wakaenda kujificha kusubilia nini kitatokea, lakini matumaini makubwa ya kufankiwa yakiwa juu yao, wakaa kimya wakisikiliza kwa makini ili wasikie pindi mtego ukifyatuka. Zilipita dakika kadhaa ghafla mbuzi ambae aliwekwa kwenye mtego akaanza kulia kwa sauti ya kuashiria amepatwa na tatizo, wale vijana wakaa vizuri huku wakiwa wameshika mapanga wakisubilia kusikia mtego ukifyatuka, sekunde kadhaa mbele mtego uliskika, haraka walitoka walipojificha na kuelekea kwenye mtego wao wakiwa na mawazo ya kumkuta nyoka akiwa amenasa kwenye mtego wao. Walishangaa kukuta mtego ukiwa umefyatuka huku yule mbuzi akiendelea kula majani, wakaukagua vizuri na kukuta ukili ukiwa umenasa kwenye mtegeo, wakautoa na kuutupa pembeni na kuanza kuongelea jambo lile.
KIJANA 1: Jamani nini kimetokea hapa maana sielewi mbona mtego umefyatuka na hakuna kitu kilichonaswa.
KIJNA 2: Hata mimi nana shangaa jambo hili, au kuna mtu ametuchezea.
KIJNA 3: Nahisi maana tangu nianze kutega hii mitego sijawai kuona ikifyatuka nyenyewe bila kunasa kitu.
KIJANA 4: labda kuna kitu kiligusa huu mtego . Kama vipi tutege tena alafu tukajifiche na tuangalie kama itatokea tena .
Wakatega tena kisha wakaenda kujificha bila kujua kuwa walifanikiwa kumnasa wakiemtaka na kumtoa wenyewe kwenye mtego na kumuacha huru tena. Walipoenda kujificha tena, Yoka akarudi kwenye umbile lake ya nyoka na kurudi nyumbani kwake.
Walikaa mda mrefu bila mafanikio yoyote na hatimae jioni ikaingia wakarudi mpaka kwa mfalme na kumpa taarifa hukusu kushindwa kwao kumpata nyoka. taarifa ile ilimuhuzunisha sana mfalme maana alitegemea mafanikio makubwa kutokana na wale watu walio wachagua kuwa hodari kwenye kazi kama zile. Lakini mmoja kati ya wale vijana aliongea kitu ambacho kiliwashangaza sana wenzake pamoja na mfalme.
KIJANA: Lakini kuna kitu kinanishangaza kila nikitafakari, hivi ukili una uwezo wa kuufyatua ule mtego, alafu nimeshangazwa na kitu kimoja pale ambapo nilikuwa nimeuhifadhi sikuuona wakati tunatoa ule mtego.
MFALME: Mh! Ukili sijawai kusikia ukifyatua mtego, au kuna mtu atakuwa anatuchezea mchezo hapa kijini, sasa nyie nendeni hili jambo nitalifikisha kwa wazee wa kijiji tutajua jinsi gani tufanye.
Wale vijana wakaondoka na kurudi majumbani kwao huku kila mmoja akifikiria kuhusu ule ukili, mda mfupi mbele mfalme akaita wazee baadhi wenye cheo pale kijijini kisha akamtuma mlinzi wake mmoja aende akamuite mzee sube. Zikapita dakika kadhaa hatimae yule mlinzi akarudi akiwa ameongozana na mzee sube, mfalme alifurahi kuona vile maana alikuwa anampenda sana yule mzee bila kujua yeye ndie chanzo cha matatizo yote pale kijijini. Kikao kiaanza huku wale wazee wakiwa awajui nini wameitiwa hamala pale.
MFALME: Wazee wangu nimewaita hapa kwa ajili ya kuwapa taarifa niliyoipata kutoka kwa wale vijana tuliowatuma kumtega nyoka, lakini kwa bahati mbaya hawakubahatika kumpata lakini kuna jambo wameniambia la kushangaza kidogo.
Mfalme akaeleza kama alivyoambiwa na yule kijana na mwisho akawapa nafasi na wao watoe mawazo yao juu ya kile alichowaambia, ndipo mzee mmoja akaanza kuongea.
MZEE: Mtukufu mfalme kutona na hiyo taarifa moja kwa moja inaonyesha kuna mtu anatuchezea kwahiyo hatuna budi kumtafuta mganga atakae wenza kutusaidia kututatulia hili tatizo.
Mzee sube akamuangalia yule mzee kwa jicho Fulani la kuonyesha kuchukia kile alichokiongea lakini kwa bahati mzuri hakuna mtu ambae alimuona akiwa kwenye hiyo hali.
MFALME: Kweli kabisa mzee wangu maana watu wamekuwa wakikichezea sana hiki kijiji chetu cha mbaka kwahiyo lazima tumtafute huyo mganga na ikiwezekana leo hii hii tumchague mganga na apewe taarifa yake ili kesho aje aianze kazi yake, Au unasemaje mzee Sebe unasemaje kuhusu wazo hili. { Aliuliza huku akimtazama mzee sube usoni na kumwachia nafasi ya kuongea }
MZEE SUBE: Ni wazo zuri na hatuna budi kulifanya maana huyu nyoka sasa hivi amekuwa hatari na endapo tutamuacha aendelea kuzuru watu wa hiki kijiji tutajikuta wote tumepotea.
Mfalme alifurahi sana kuona wote wamekubaliana jambo lile na ndipo akatoa nafasi ya kumpendekeza mganga ambae wao wanaona ataweza kusaidia kutokana na lile tatizo, mzee mmoja akasimama na kumtaja mganga aliehisi yeye kuwa anafaa kuifanya hiyo kazi.
MZEE: Mtukufu mfalme kuna mganga mmoja anaitwa mzee Duba ambae tangu ujana wake amekuwa akiifanya hiyo kazi ya uganga na amesaidia watu wengi sana hapa kijijini na kwa sasa anapatika karibia na msitu wa dawa.
Mfalme akawauliza wale wazee wengine kama kweli kile alichokisema mwenza, kila aliemuuliza aliitikia haraha lakini ilipofika zamu yam zee sube alisita kwa sekunde kadhaa kisha akakubali kuwa yule huyo mzee Duba anafaa kuifanya hiyo kazi. Baada ya wote kukubaliana mfalme akafunga ule mkutano na kuwaruhusu wale viongozi warudi majuimbani kwao ili kesho yake asubuhi wawai kufika kwa ajili ya kumpokea huyo mzee Duba maana yeye alikuwa hamfahamu. Wale wazee walipoondoka akatumwa kijana mmoja aende huko kwa huyo mganga akampe taarifa kuwa anahitajika kufika kwa mfalme kesho yake, kijana akafanya kama alivyo ambiwa akaanza safari ya kwenda huko karibu na msitu wa dawa kumfuata mganga. Sube alipofika nyumbani kwake akaingia moja kwa moja mpaka ndani bila kumwambia kitu chochote mke wake ambae kwa mda huo alikuwa amekaa nje na kumsababishia mawazo mengi, Haraka mke akainuka na kumfuata mumewe ili akajue nini tatizo mpaka awe kwenye ile hali na wakati sio kawaida yake.
BIBI SUBE: Kulikoni mbona upo hivyo.
MZEE SUBE: Mke wangu tupo kwenye wakati mgumu sana, usiku wa leo kuna kazi tunatakiwa tuifanye.
BIBI SUBE: E ! kwani kimetokea nini huko kwa mfalme. { Aliuliza huku akiwa na uwoga }
MZEE SUBE: Kuna mganga kachaguliwa kwa ajili ya kuja kualibu mambo yetu.
Bibi sube aliposikia vile, akaanza kutetemeka huku akimrahumu mume wake juu ya wazo ambalo alilitoa ambalo sasa hivi limeanza kuwatia jamba jamba.
BIBI SUBE: Heeee ! Sasa tutafanyaje si kuhumbuka huku mume wangu. Lakin mimi nilikuambia hiki tunachokifanya yatatukuta kama yaliyomkuta mzee SUI .
MZEE SUBE: Mke wangu wala usiogope haiwezi kutokea kama kilachotokea kwa mzee sui na kila siku nakuambia kuwa mzee sui kilchofanya afe ni uzembe wake yeye pamoja na mwanae. Sasa sikiliza mganga aliechaguliwa ni yule mzee duba kwahiyo leo usiku inatakiwa twende tukapoteze uhai wake maana kama tukimuacha kweli yatatukuta kama ya mzee sui na ama.
BIBI SUBE: Hivi kweli tutaweza kumuua yule mzee maana kaanza mda mrefu sana ile kazi na lazima katuzidi uwezo.
MZEE SUBE: Hahahaha mke wangu unafurahisha sana. Mzee duba hawezi kufurukuta kwangu japokuwa ameanza zamani ile kazi ila mimi ni zaidi kwahiyo awezi kuzuia uchawi wetu hata siku moja.
BIBI SUBE: Hapo sawa mume wangu maana roho yangu ilikuwa hipo juu.
Kwa upande wa yule kijna ambae alitumwa aende kutoa taarifa kwa yule mganga kwa bahati mzuri akabahatika kumkuta yule mganga akiwa anatengeza dawa na wakati huo giza lilikuwa lishaanza kuingia. Alipokelewa vizuri sana na mzee Duba na baada ya kufahamiana akamueleza kilichompeleka pale, Mzee duba alifurahi sana kusikia amechaguliwa kuwa mganga anaetakiwa kutatua lile tatizo lililopo pale kijiji, akamuomba yule kijana ile siku walale pale alafu asubuhi na mapema waanze safari yao ya kwenda kwa mfalme. Wakati huo Duba alikuwa Hafahamu kitu chochote kinachoendelea juu yake. Masaa yalienda na hatimae mda wa kulala ukafika Duba akamuandalia yule kijana sehemu mzuri ya kupumzika, na yeye akaenda kulala sehemu yake, mda huo kwa upande wa sube na mke wao walikuwa wakijiandaa kwenda kuifanya kazi walio ikusudia kuifanya siku ile. Mda wa kazi ulipofika wakakusanya vitu vyao na kuweka kwenye ungo kisha na wao wakapanda na kusafiri mpaka nyumbani kwa Duba na kumkuta akiwa amelala fofofo. Walipofika wakamwaga unga huku wakiizunguka nyumba na mwisho wakashikana mikono na kuingia ndani kwa kutumia ukuta. Ghafla sura zao zikabadili na kuwa tofauti ambazo mtu yoyote isingekuwa rahisi kuwafahamu, Wakaanza kuimba na kucheza nyimbo zao za kichawi huku wakizunguka kitanda cha ukambaa alicholalia Duba, Walipomaliza wakamwamsha kwa mkitikisa mpaka alipozinduka kutoka usingizini. Duba alishtuka sana alipokutana uso kwa uso na wawili wale waliokuwa na sura za kutisha, akakurupuka pale kitandani na kuangukia chini. Wawili wale waliendelea kumfuata mpaka huku yeye akiwa anarudi nyuma nyuma, na mwisho akasimama na kukimbilia nje, Ghafla nje ya nyumba mulipo mwagiwa ule unga mkaanza kuwaka moto na kumfanya Duba ashindwe kuendelea kukimbilia mbali na pale. Akadondoka chini huku akitafuta wapi wale watu walipo, Ndipo sube na mke wakatokea pale pale alipokuwa ameanguka ndipo Duba akaanza kuwauliza maswali wawili wale huku kijasho kizito cha kujuta kikimtiririka.
MGANGA: Kwani munataka nini kwangu kama kuna kitu munakiitaji niambieni mimi nitawapatia.
Yule mganga baada ya kusema vile ndipo mzee sube akaanza kucheka kwa dharahu na kumjibu.
MZEE SUBE: Hahahaha wewe si mganga ambae unataka ukaaribu mambo yangu. Sasa nimekuja kwa ajili ya kupambana, uwezo wako ndio utakufanya uendelee kuishi .
Sube baada ya kujibu vile ndipo Duba akagungua kuwa ni mzee sube, maana walikuwa pamoja zamani kwenye shughuli zao za kichawi lakini baadae Duba akaacha kuloga watu na kuwa mgawa, chapokuwa nae ni mchawi.
MGANGA: Nimekujua wewe sube na mimi nilijua tu lazima hipo siku utanifanyia kitu kama hiki maana umezoea kuwatesa wanakijiji. kama unataka kuniua niue tu ila endapo utaniacha nitasema ukwel kwa mfalme.
Sube alichukia sana kusikia vile, ndipo akajibadirisha na kurudi kwenye sura yake ya kawaida na kusogea karibu na alipo Duba na kuanza kuongea.
MZEE SUBE: Vizur sana kama umegundua mimi nani sasa kwa kuwa unajfanya jeuri basi leo ndio utakuwa mwisho wako wa kuonahuu ulimwengu, kamwe sitakuacha hai.
MGANGA: Sawa wewe fanya utakalo lakini jua kuwa siku za mwizi ni arobaini hipo siku ukweli utajurikana tu hata kama utaniua.
Sube akasimama akamkazia macho Duba ghafla damu zikaanza kumtoka puani mdomoni na masikioni, huku akiangaika kutokana na maumivu makali aliyokuwa anayapata hatimae akakata roho.
Sehemu Ya 7
Bibi sube alishangaa sana kuona Duba akifa kijinga kiasi kile utadhani mtoto mdog asie na nguvu ya kujitetea, wakaondoka mahara pale na kurudi nyumbani kwao na kumuacha Duba akiwa amelala chini huku damu nyingi zikiendelea kumvuja. Walipofika kwao na kubadilisha zile nguo zao, Bibi Sube akaanza kumuuliza mume wake hukusu kilichotokea.
BIIBI SUME: Mume wangu umewezaje kumuua yule mtu kiurahisi vile, maana nilijinga ipasavyo kwa mapambano nilihisi kungekuwa na kurupushani kubwa.
SUBE: Nilikuambia Duba kwangu mimi ni kama mtoto atambaae, anitishi hata kidogo, sisi wakubwa wewe.
Bibi sube alitabasamu kisha wakalala zao na hatimae ile siku ikapita na kuja siku nyingine. Kwa upande wa yule kijana mgeni wa Duba akaamuka mapema sana na kwenda sehemu aliyokuwa amelala Duba, alipoona hayupo moja kwa moja akajua itawa ayari ameamka mapema zaidi yake, akatoka nje akitegemea kukutana na Duba. Hakuamini macho yake baada ya kuoona mganga aliekuja kumchukua akiwa amelala chini huku damu zikiwa zimemtapakaa. Akamsogelea huku akiwa na hofu kubwa nafsi mwake, akamtazama ndipo akagundua ameshakata roho, alishtuka sana na kuanza kupiga mayowe ya kuomba msahada kwa majirani wa yule mzee, na mda mfupi mbele watu wakaja nyumbani kwa Duba huku huzuni kubwa ikitawa kutokana na kuondokewa na mganga wao aliekuwa akiwasaidia. Wakaubeba mwili wa Duba na kuupeleka ndani kisha wakamtuma tena yule kijana apelike ile taarifa kwa mfalme. Kijana akatoka na kuinza safari yake huku akiwa anakimbia na baada ya masaa kadhaa akafanikiwa kufika kwa mfalme na kukuta akiwa na baadhi ya wazee wakiongelea mambo mengi kuhusu kijiji chao. Kabla hata ya salamu yule kijana akaanza kutoa ile taari huku akihema kwa haraka.
KIJANA: mtukufu Mfalme mganga amefariki.
Mfalme pamoja na wale wazee walishtuka maana ile taarifa ilikuwa mbaya kwa upande wao kutokana na umuhimu ambao alikuwa nao Duba kwa kipindi kile.
MFALME: Eeeeeee !!? Amefariki ?
KIJANA: Ndio mtukufu mfalme amefariki.
MFALME: Kwahiyo wewe ulimemkuta ameshafariki au.
Kijana wakati anataka kusimulia mara mzee sube akawasili sehemu ile, ndiupo mfalme akamkatisha yule kijana na kumkaribisha mzee sube na kumpa taarifa ya msiba wa Duba na wakati yeye ndie aliesababisha kifo chake.
MFLME: Karibu sana mzee Wangu .
MZEE SUBE: Ahsante sana mtukufu mfalme.
MFALME: Mzee tumepatwa na tatizo yule mganga ambae tulitegemea atusaidie juu ya lile jambo letu amefarikii.
alipoambiwa hivyo kwa unafiki akajifanya kushtuka na kushanga kama sio yeye aliefanya hilo tukio .
MZEE SUBE: Eeeeee !! Duba amefariki, Tumeangamia.
MFALME: Ndio hivyo mzee sube.
MZEE SUBE: Mh! kwani alikuwa anasumbuliwa na nini mpaka amefariki maana imekuwa ghafla.
MFALME: Hata mim sijui hivi hapa ndio nlikuwa nanimuulza huyu kijina ambae nilimtuma jana akamuite huyo mganga, yeye ndio ameleta hii taarfa za msiba. Haya kijina nambie ilikuwaje.
Akaanza kusimulia huku watu wote wakimsikiliza kwa makini, mda wote mzee sube alikuwa akijifanya kusikitika kuhuzunisha na msiba ule.
KIJNA: Mtukufu mfalme nilipofika nilimkuta yule mzee mzima wa afya tena akitengeneza dawa, nilipomueleza wapi natoka alifurahi sana nikampa ujumbe ulioniagiza, ila yeye akaomba jana nipumzike alafu leo asubuhi tuanze safari ya kuja huku, lakini cha ajabu leo nimeamka nimemkuta nje amekata roho huku damu nyingi ikiwa usoni mwake ususani maeneo ya poani, mdomoni na masikioni.
Aliponyamaza Sube akadakia na kuanza kuongea kabla mfalme ajasema kitu chochote.
MZEE SUBE:Mtukufu mfalme hapo kuna mkono wa mtu ambao unafanya hayo yote tena ni kati yetu sisi wazee maana haiwezekani kila tunachopanga kinaharibika, lazima kuna msaliti kati yetu..
alisema vile ikiwa kama kujisafisha kwa upande wake, wote walikuwapo mahali pale walikubari kile alichokisema mzee Sube na kuamini kabisa kati yao kuna msaliti, Wakiwa kwenye hali ya kuulizana nani msaliti malme akasimama na kuanza kuongea.
MFALME: kweli kabisa ulichokisema mzee sube haiwezekani kila siku mipango yetu ihalibike, sasa ninasema hivi endapo nitamgundua huyo msaliti hukumu ya kifo itakuwa juu yake.
Waliendelea kuongea kwa mda kuhusu lile swala, walipomaliza wale wazee wakaruhusiwa warudi majumbani kwao lakini mzee Sube aliombwa abaki maana mfalme alikuwa anataka kuongea nae. Wazee wote wakaondoka huku wakiulizana nani msaliti, wakati huo maongezi ya mfalme na mzee sube yakaanza.
MFALME:Nimekuambia ubaki kwa sababu katika wazee wote hapa kijijini wewe ndio ninakuamini na kukutegemea, ila kutokana na kile ulichokisema kuna kitu nimekihisi kutoka kwa wale wazee wenzako.
MZEE SUBE: Kitu gani hiko mtukufu mfalme.
MFALME: Katika hawa viongoz wangu kuna mzee mmoja namuhisi kuwa ndie anaetugeuka tunapokuwa tunapanga mambo yetu.
MZEE SUBE: Nani huyo.
Mfalme akamtazama Sube kwa jicho Fulani lililopelekea sube kuogopa na kuhisi labda amejirikana maana hata siku moja mfalme hakuwai kumwangalia kwa jicho kama lile, kisha akaanza kuongea.
MFALME:Nahisi mzee Bugu ndie msaliti.
Sube akashusha pumzi zake taratibu na kuanza kuongea.
MZEE SUBE:Kweli kabisa mtukufu mfalme maana hata mimi nilikuwa ninamuhisi huyo huyo Bugu lakini nilikuwa nashindwa kukuambia niliogopa kuonekana mchonganishi.
MFALME: Kumbe hadi wewe umegundua hilo, sasa tufanyaje.
MZEE SUBE: Kwa kuwa hatuna uhakika bora umtoe uongozi na umpe mtu mwingine unae muamini ili tutakapokuwa tunapanga mambo yeye asiwepo.
Sube alisema hivyo kwa sababu mara kwa mara Bugu alikuwa akipinga maneno yake na kwenda kinyume kabisa na yeye, aliona atamwaribia mambo yake. Mfalme bila kujiuliza wala kutafakari akakubaliana na mzee sube wafanye hivyo.
MFALME: Sawa mzee wangu nimekuelewa na nitafanya hivyo.
Mzee sube akaruhusiwa kuondoka maana walikuwa wamemaliza maongezi, akaenda nyumbani kwake na kumsimulia mke wake kila kitu kilichotea kwa mfale, Bibi sube alifurahi sana na kumpongeza mume wake kwa kazi mzuri aliyoifanya.Badaa ya hapo masaa yalienda na hatimae ile siku ikawa imepita, siku iliyofuata mfalme akaita wale viongozi wote na kufanya nao mkutano wa dharula ambao haukutegemewa na mtu yoyote yule.
MFALME: Nimewaita hapa kuna kitu nataka niwaambie na hiko kitu kinahusu kubadilisha uongozi maana kuna baadhi yenu kwa sasa mme zeeka sana kwahiyo inabidi muwapishe na wenzenu ili nyie mupumzike. Kwahyo leo nimeamua kumtoa uongozi mzee bugu na kumpatia mzee sube.
Mzee sube alishangaa sana kusikia vile maana hakutegemea kama mfalme angempa kile cheo, ndipo akaanza kupiga makofi huku akimshukuru mfalme kwa hatua aliyoichua. wale viongozi wengine baada ya kuona sube akipiga makofi na wao wakajaribisha huku hali ya mshangao ikitawala usoni mwao, maana lile jambo lilikuwa la ghafla na kwa pale kijijinni kwao hakukua na sheria ya mfalme kumtoa mtu uongozi bila kuomba ushauri kutoka kwa wale wazee, lakin kwa upande wa sube furaha ilitawa. Mfalme akaendelea kuongea.
MFALME: kwahiyo kuanzia leo mzee sube atakuwa kiongozi kama nyie wengine.
Kikao kiliendelea kilipoisha na hatimae kikafika tamati ndipo wale wazee wakaondoka na kumuacha sube pamoja na mfalme, wakiwa njiani wakaanza kuwaongelea wawili wale.
KIONGOZI 1: Jamani mwenzenu hata sielewi nini kinaendelea kati ya mzee sube pamoja na mfalme.
KIONGOZ 2: He! Kwahiyo ww ndio umejua leo ?. Sisi wenzako tumeliona hilo tangu zamani sana.
MZEE BUGU: mimi nashangaa kitu kimoja tu. leo mimi na mzee sube naonekana mimi ndio mzee kweli na wakati nimezaliwa nimemkuta mzee sube ndio anajifunza kuongea.
KIONGOZ 1: Bugu pale lazima mzee sube kuna alichokifanya sio bure .
KIONGOZ 2: Hata mimi naona hivyo hivyo, ila hebu tuachane na hizi mada maana sio mzuri.
waliachana na ile mada na kuongea mambo yao mengine na hatimae wakafika makwao. Kwa upande wa vijana wa kile kijiji siku hiyo na wao walifanya kimkutano kidogo wakiongelea kuhusu yule nyoka jinsi gani wafanye ili wafanikiwe kumnasa.
Sehemu Ya 8
waliachana na ile mada na kuongea mambo yao mengine na hatimae wakafika makwao. Kwa upande wa vijana wa kile kijiji siku hiyo na wao walifanya kimkutano kidogo wakiongelea kuhusu yule nyoka jinsi gani wafanye ili wafanikiwe kumnasa.
KIJANA 1: Hivi munajua huyu nyoka tusipomfanyia kazi atatumaliza wote.
KIJANA 2: Kweli unachokiongea maana sisi ndio tunaotegemewa hapa kijijini tukiwa kama vijana na sifa ya hiki kijiji chetu kuwa na vijana mashupavu, mashujaa sasa itakuaje tushindwe kummaliza haka kadudu kadogo kabisa.
KIJANA 3: Jamani kuna kitu nilisahau kuwaambia, Juzi nikiwa natoka msituni kuwinda nikapita nyumban kwa mzee sube maana njia ile ndio urahis mimi kufika nyumbani. Sasa wakati napita mbele ya nyumba ya mzee ghafla alinipta nyoka mmoja nakumbuka alikuwa na rangi ya njano kichwani pamoja na mkiani ila sehemu zingine zote alikuwa na rangi ya blue, baada ya nyoka kunipita akaingia kwenye kile kichaka ambacho kipo karibu sana na nyumba ya mzee sube. nikasogea mpaka pale kwenye kichaka ili nimuue yule nyoka ila cha ajabu wala sikumuona bali nilikuta kijisehemu fulani pakiwa pamemwagiwa unga mweupe na mwekundu pamoja na ukili ukiwa katika ule unga wenye rangi. Nikiwa nashangaa ghafla alikuja mzee sube na kunifukuza eneo lile na kuniambia kuwa nisipite tena njia ile .
KIJANA 4: huyu mzee sube atakuwa anajua ukweli kuhusiana na huyu nyoka.
KIJANA 1:Itakuwa kweli ulichokisema maana nilishangaa sana kuona tabibu wa kijiji anakosa dawa ya kutibu sumu ya nyoka alafu mzee sube awe nayo, wakati yule mzee Chala ameudumia sehemu hii kwa mda mrefu na hakuna ugonjwa ambao alikuwa anashindwa kutibu, na ndio maana yule mfalme wa jirani alikuwa anamuhitaji sana kutokana na umahiri wake wakazi.
KIJANA 5: kama ndio hivyo inabidi tuanze kumchunguza huyu mzee maana asijifanye tabibu kumbe anatuchezea akili zetu.
KIJANA 6: Itakuwa vizuri tukifanya hivyo, kwahiyo tutafanyaje ili tumchunguze.
KIJANA 2: Inabidi tuwe tunazunguka zunguka sana pale nyumbani kwake mpaka tufanikiwe kumuona huyo nyoka, kama tukishindwa kumuona mchana tutaenda kumchunguza tena usiku mpaka tupate ukweli wa jambo hili.
Baada ya kukubaliana vile kila mmoja akarudi nyumbani kwao kwa ajili ya kujiandaa na kazi, ilipoika majira ya saa kumi jioni wakakutana na kuanza kupanga njia watakazo zitumia pindi wakifika nyumbani kwa Sube.
KIJNA 1: Jamani huku tuendako tunatakiwa tuwe makini ili tuifanikishe kazi yetu na itapendeza sana kama Mzee sube hatatuona, maana anaweza kutufukuza. Cha msingi kila mtu ajitoe kwa ajili ya kusaidi mbaka.
Walipomaliza wakaianza safari yao na kuishia kwenye nyumba moja ambayo ilikuwa karibu sana na nyumba ya Sube, ndipo akatumwa kijana mmoja aende kwenye kile kichaka kuangalia kama ataona kitu chochote, ila kabla ajaondoka aliambiwa endapo ataonekana na mzee Sube asirudi tena mule ndani bali atoe ishara, kama amefanikiwa kumuona huyo nyoka au laa kisha aende zake. Kijana akafanya kama alivyo akizwa alitoka mle ndani na kusogea mpaka kwenye kile kichaka na kujifanya anashangaa kitu Fulani, lakini kabla hajaona kitu chochote ghafla mzee Sube akatoka ndani kwake na kumkuta yeye akichakua chakua majiani. Kwa hasira sube aliongea.
MZEE SUBE: Wewe kijana unafanya nini hapo au wewe mwizi eee, ebu toka na ukawaambie wenzako sitaki nimuone mtu akipita shemu hii kwa sababu sio njia.
Kijana baada ya kufukuzwa akatoka bila hata ya kutoa ishara maana Sube alikuwa anaendelea kumuangalia, kwahiyo akaogopa kufanya hivyo asije akagundua kuwa wanamchuguza, wale vijana wengine walishangaa kuona vile lakini hawakuwa na jinsi waliendelea kusubilia labda watoona kitu chochot . Baada ya mda Fulani kupita, nyumbani kwa mzee sube akafika kijana ambae alikuwa ameagizwa kutoka kwa mfalme.
KIJNA: Mzee sube mtukufu mfalme ameniagiza nije nikuite na amesema tufanye haraka maana mke wake wa pili aitwae Mana ameng’atwa na yule nyoka.
MZEE SUBE: Sawa tangulia mwambie ninakuja mda sio mrefu.
KIJANA: Sawa ila amesema usichelewe maana hali yake mbaya sana.
MZEE SUBE: Sawa kijana nimekuelewa ila wewe tangulia.
Kijana akaondoka na kumuacha Sube akijianda, huku akimueleza mke wake kuhusu yule kijana
MZEE SUBE: Mke wangu nahis vijana wa hapa kijijini kama wanachuguza mambo yetu.
BIBI SUBE: He! Kwanini unasema hivyo mume wangu.
MZEE SUBE: Nilipotoka nje nimemkuta kijina mmoja kwenye kile kichaka akichambua chambua kama anatafuta klitu Fulani, aliponiona akashtuka, mimi nikamfukuza, ila leo ni mara ya pili naona kijana akisogea maeneo yale ilaw wala usiwe na hofu mke wangu maana hakuna kitakacho alibika.
BIBI SUBE: Mh! Iwe kweli tu maana mda mwingine huwa naogopa sana nikikumbuka hiki tunacho kifanya.
MZEE SUBE: Usiogope mke wangu haiwezekani kutokea jambo baya lolote lile. Sasa sikiliza mfalme kamtuma kijana aje kuniita, mke wake kang’atwa na Yoka kwahiyo anataka nikamtibu tena amesema nifanye haraka maana hali yake ni mbaya sana. Kwaihiyo nakuomba ukae pale nje ili endapo atakuja kijana yoyote umkataze kusogea wala kupita karibu na kile kichaka.
BIBI SUBE: Sawa mume wangu nmekuelewa.
Sube akaondoka na kumuacha mke wake akijianda kwenda kulinda kile kichaka. Kwa upande wa wale vijanawalipoona Sube ametoka walifurahi sana na kuona kazi yao itakamilika mda mfupi maana aliekuwa akizuia wao kuchunguza kwenye kile kichaka ameondoka, lakini dakika kadhaa mbele walimuona bibi sube akitoka ndani ya nyumba huku akiwa amebeba kitanda cha ukambaa na kwenda kukiweka karibu na kile kicha, huku akifuma mkeka. Kitendo kile kiliwafanya wale vijana wazidi kuamini kuwa wawili wale wana siri kubwa na kwenye kile kichaka kuna kitu wanakificha ndipo wakaanza kuongelea swala lile.
KIJANA 1: Jamani sasa hivi mimi naamini wazee wale kuna kitu wanakifanya haiwezekani wazuie watu kwenda au kupita kwenye kile kichaka, lazima kutakuwa na kitu sio bure.
Maneno ya yule kijana yalikubaliwa na kila mtu pale ndani ndipo wakaanza kutafuta mbinu zaidi za kuwakamata wale watu.
KIJANA 2: Mimi ninaaona bora tukamwambie mtukufu mfalme juu ya jambo hili. Ili tutakapofanya jambo lolote tuwe huru.
.
Wakiwa wanaendelea kuongea mara mwenzao moja akamuona mzee Sube anarudi ndipo akawashtua wenzake na kuanza kumchungulia kupita kidirisha kidogo kilichopo kwenye nyumba hiyo, Sube alipofika akaa alipokuwa mke wake na kuanza kuongea mambo ambayo wale vijana hawakuweza kuyasikia kutoka na wawili wale kuongea kwa sauti ya chini. Giza lilizidi kuingia wale vijana wakaamua kupumzika huku wakisubiria kwa hamu ifike siku nyingine wakampe taarifa mfale wao. Asubuhi ilipofika wakaondoka kwenye ile nyumba na kwenda nyumbani kwa mfalme, walipofika huko walipokelewa na kueleza shida yao.
KIJANA: Mtukufu mfalme tumekuja hapa kuna kitu tunataka tukuambie ukiwa kama kiongozi mkuu hapa kijijini kwetu,kama unavyojua hapa kijijini kwetu tumekubwa na janga la huyu nyoka na mara kwa mara tumekuwa tukitafuta suruisho lakini ilikuwa inashindikana.
MFALME: ni kwel kwahiyo nyie mnahitaji nini.
KIJANA: Kwanza kilichotuleta hapa tumekuja kukuambia kuwa tumemjua mtu ambae anasababsha haya matatizo na ndio maana kila tukivyopanga mambo yetu tulikuwa atufanikiwi kwa sababu huyo mtu amekua akienda kinyume na sisi yani ni msaliti.
Yule kijana baada ya kusema vile moja kwa moja mfalme kichwani mwake akajua wale vijana wanamzungumzia mzee bugu kwa sababu hata yeye amekuwa akimuhisi hivyo. Japokuwa alihisi wanamuongelea mzee bugu ila akaona bora awaulize wale vijana kuwa nani wanamuhisi ili endapo watamtaja mzee bugu atakuwa kapata uwakika kuhusu mzee bugu kuwa kweli ni msaliti.
MFALME: Ehe vijana nani huyo munamuhisi kuwa ni msaliti wa hiki kijiji na ndie chanzo cha haya matatizo.
KIJANA: Ni mzee SUBE mtukufu mfalme.
MFALME: Eeeee !!! Munasemaje nyie vijana ?.
alishangaa sana kusikia vile maana hakutegemea kama wangemtaja mtu anae mwamini kupitakiasi.
KIJANA: Ndio hivyo mtukufu mfalme, mzee Sube ndio chanza cha haya matatizo.
MFALME: Hahaha nyie vijana munanchekesha sana. Mzee sube mimi ninamjua vizuri tena sana, katika wazee ambao nina waamini hapa kijiji mzee sube ndie namba moja alafu leo ndio mje mniambie kuwa yeye ndio msaleti.
Mfalme alicheka sana na kuhisi wale vijana wametumwa na baadhi ya watu pale kijijni kutokana mzee sube kuwa karibu nae.
KIJANA: Tunajua sio rahisi kutuamini kwa sababu mzee sube kwa sasa upo karibu nae kwahiyo uwezi kuona ubaya wake ambae amekuwa akiufanya.
MFALME: Najua mnasema hivyo kwa sababu mzee sube yupo karibu na mimi na nimempa cheo kwahiyo mkaona bora mje kumuaribia ili nisielewane nae au itakuwa mumetumwa nyie ?. Sasa nasema huo mpango wenu mmeshindwa kufanikiwa.
Vijana wliumia sana na kuona mfalme hana nia ya kusaidia kijiji bali yupo kwa ajili ya kumlinda mtu mmoja, lakini hawakukata tama wakaendelea kuongea nae.
KIJANA: Mtukufu mfalme sisi atujatumwa na mtu yoyote kama wewe unavyofikilia bali hiki tunachokuambia ni kweli na ipo siku utakuja kuamini tunachokuambia.
MFALME: Mh ! Leo nimeamini kuwa sio kila mtu anapenda mafanikio ya mwenzake bali kuna watu wanapenda kumuona wenzao wakiwa wanaiishi kwenye maisha ya shida. Sasa nyinyi mumekuja kuniambia hivyo ili mimi nifanye nini.
KIJANA: Kwanza tumekuja kukupa taarifa ya kumgundua mbaya wa kijiji pili tumekuja kuomba ruhusa ya kumchunguza yule mzee.
Mfalme akajibu kwa jeuri..
MFALME: Mkitoka kumchunguza yeye mje kunichunguza na mimi, endapo itaonekana mnamsingizia hukumu ya kifo itakuwa juu yenu .
KIJANA: Sawa mtukufu mfalme ila leo usiku tunaomba uje kwenye ile nyumba ambayo ipo karibu na nyumba ya yule mzee ili uone mwenyewe tabia zake, ila utamapokuja angalia asikuone na mtu yeyote sana sana mzee sube pamoja na mke wake.
MFALME: Sawa nitakuja ila narudia tena ikionekana mnamsingzia hukumu ya kifo itakuwa juu yenu.
Walipomaliza maongezi wakaondoka na kumuacha mfalme akitafakari maneno yao huku akipanga na adhabu ambazo watapata pindi ikijulikana wanamsingizia mzee sube. Kuanzia hapo masaa yalienda na hatiamaemda wa kwenda kwenye kazi ukawadia, wale vijana wakajikusanya sehemu moja na kwenda kwenye ile nyumba waliyokuwa wamekaa siku ya kwanza
Sehemu Ya 9
Baada ya mda kidogo kupita mfalme akawasili sehemu ile na kuwakuta vijana wakiwa wamejianda na kila aina ya dhana kwa ajili ya kupambana na yule nyoka pindi wakifanikiwa kumuona, kijana mmoja ambae ndie alikuwa kama kiongozi wa wale wenzake akamkaribisha mfalme.
KIJANA: Karibu sana Mtukufu mfalme, tumefurahi kukuona maana ukweli utadhihrika mbele yako..
MFALME: Sawa lakini endapo sitaona kitu chochote mahara hapa nawaahidi adhabu ya kifo itakuwa juu yenu sitakuwa na msamaha na mtu, na wala sitaangalia umuhimu wenu hapa kijijini.
Japokuwa mfalme alikuwa akiongea maneno makali, wao hawakuogopa maana waliamua kujitolea kwa ajili ya kijiji chao, waliendelea kuongea nae huku baadhi yao wakiwa makini kuangalia kwenye kile kichaka wakisubilia kuona nini kitatokea. Mda ulienda bila ya mafanikio ya kuona kitu chochote hofi zikaanza kutawala nafsini mwao vijana wale kila walipokuwa wakikumbuka maneno ya Mfalme, baadhi yao walijuta na kujirahumu kwanini walienda kumpa taarifa mfalme lakini walikuwa wameshachelewa. ilipofika majira ya saa sita usiku wale vijana walijishukuru na kuona wameshindwa kuifanya ile kazi na kuhisi walidhania kitu kisichokuwa kweli, ndipo wakaamua kulala wakisubilia adhabu yao ikifika kesho yake asubuhi. Kwa upande wa mfalme hakuitaji kulala alijitahidi kupambana na usingizi ilimradi aone kile walichokisema vijana, japokuwa wenyewe walikata tama na kukili wamekosea. Sasa kwa upande wa Sube na mke wake na wao walikuwa macho wakiongea kuhusu Yoka.
SUBE: Kuna wazo nimelipata kuhusu Yoka.
BIBI SUBE: Wazo gani .
SUBE: Ninaona huyu nyoka tumwamishe tumpeleke msituni awe anaishi huko maana naona kama watu wameanza kutuchunguza.
BIBI SUBE: Sawa sio vibaya kama umeona hivyo, kwahiyo huku kijijini hata onekana tena.
SUBE: Ataonekana ila sio sana, ila sasa hivi ninataka awe anaenda mpaka kwenye kijiji cha Mbui kwa mfalme Koe ilituzidi kujulikana.
BIBI SUBE: Sawa nimekuelewa.
SUBE: Sawa, alafu twende tukamuangalie mdudu mwenyewe maana tuna siku nyingi hatujamwangalia.
Wakanyanyuka kuelekea kwenye kile kichaka, wakikwa awajui hili wala lile linaloendelea zidi yao. Mfalme wakati anaendelea kuangalia angalia huku macho yake yakilazimiisha kufumba, Ghafla akamuona Sube akiwa ameongozana na mke weka, kisha wakatazama pande zote kama mwizi anapoenda kuiba. Mfalme akashtuka na kufikicha macho yake yaliojaa ukungu kutokana na usingizi mzito aliokuwa nao, kisha akatulia na kuangalia kwa makini nini wawili wale wanataka kufanya. Sube alipoona nje hakuna mtu yoyote akaanza kupiga mluzi mara kwenye kile kichaka akatoka nyoka mkubwa mwenye kung’aa na kusogea walipo wawli wale. Mfalme alishtuka sana utadhani yule nyoka alikuwa amemfuata yeye alitamani kupiga makelele kutokana na uwoga lakini akajikaza kiume na kuendelea kuangalia nini kitafanyika. Sube akachuchumaa na kumpaka unga Yoka kisha akaongea maneno Fulani ambayo mfalme hakusikia kisha nyoka akaondoka, wawili wale na wao wakarudi ndani kulala maana walikuwa tayari wamemaliza kazi yao. Mfalme alisikitika sana kisha akawatazama wale vijana alitamani awaamushe ili awaambie kile alichoona lakini moyo wake ulisita, kutokana na ukaribu aliokuwa nao yeye na mzee sube, Ndipo akaamua kulala huku mawazo mengi yakitawala kichwa chake maana alikuwa ajui aanze wapi kuwaambia wanakijiji pamoja na wale viongozi kuhusu swala lile. ilipofika asubuhi na mapema mfalme aliamke na kurudi nyumbani kwake bila kumuaga kijana yoyote pale ndani maana wao walikuwa bado hawajaamka. Alipofika kwao mda wote alikuwa mtu wa kijiinamia, jambo ambalo lilimshangaza sana mke wake kwa sababu haikuwa kawaida yake kuwa vile, ndipo akahitaji kufahamu nini kimemkuta huko atokako.
MKE: Mume wangu mlikoenda mlifanikiwa au wale vijana walikuwa wanamsingizia yule mzee wa watu.
Mfalme kwa kuwa hakutaka mzee sube ajulikane akaona bora amdanganye mke wake japokuwa hakupenda kufanya hivyo.
MFALME: Hapana hatujafanikiwa maana hatukuona kitu chochote kwahiyo sijui kama wanamsingizia au laa.
Mfalme aliongea huku akiwa na wasiwasi na kumfanya mke wake ahisi kitu Fulani.
MKE: Mh! Ila kutokana na unavyoongea naoka kama sio kweli unavyonimbia .
MFALME: Kwanini unasema hivyo mke.
MKE: Nakuona jinsi unavyoongea una wasiwasi sana .
MFALME: Hapana mbona nipo kawaida, na wala sijakudanganya.
MKE: Sawa ila naomba uniambie kwanini tangu umerudi umekuwa mtu wa mawazo wala hauna furaha kuna kitu gani kimekukwaza huko utokako.
Mfalme baada ya kuulizwa vile, akamtazama mke wake na kuamua kumwambia ukweli wa kile kilichotokea.
MFALME: Mke wangu kwanza naomba unisamehe kwa kutokukuambia kweli kuhusu kule nitokako. Ila jambo ambalo walikuja kilisema wale vijina kuhusu mzee sube ni kwel kabisa tena nimeshuhudia kwa macho yangu mwenyewe, na nimegundua kitu kumbe mzee Sube ndie mwenye yule nyoka.
Mke wa mfalme alishangaa sana kusikia vile maana na yeye alitokea kumuamini mzee sube kama alivyokuwa akiaminiwa na mume wake.
MKE: Eeeeeee ! Mume wangu kwahiyo unataka kuniambia kumwamini kote kule kumbe ni mbaya kias hiko. Sasa baada ya kuona hivyo umechukua huamuzi gani.
MFALME: hapa kichwa chote kinawaka moto maana hata sijui cha kufanya kwa mzee yule. Alafu kitu kingine, jambo hili nataka iwe siri yangu mimi na wewe tu maana watu wengene wakisikia wanaweza kudhania kuwa mimi na mzee sube tulikuwa tunashilikiana kufanya jambo hili kutokana na kuwa karibu nae.
MKE: wewe unataka iwe siri wakati wale vijana na wao wamemuona huyu mzee sube.
MFALME: Hapana hawakumuona walikuwa wamelala.
MKE: Sawa ila mume wangu mzee sube inabidi ahukumiwe kama watu wengine wanavyofanya kitu kibaya hapa kijijni kwetu.
MFALME: sawa ila kabla sijafanya hivyo ninataka nimuite ili nimuonye endapo atarudia au ataendelea kufanya vile nitamuhukumu.
MKE: Mh! mume wangu bado unataka kumtetea mzee sube ila basi kwa kuwa wewe ndio mfalme fanya utakalo.
Waliendelea kuongelea jambo lile na mwishoe wakaachana nalo huku mke akimshangaa mfalme kwanini amekuwa akimtetea Sube kiasi kile. Kwa upande wa wale vijana walishtuka sana baada ya kuamku maana hawakutegemea kuona mfalme ameondoka mahara pale bila kuongea na wao, hofu ilitawala kwao, kila mmoja alimuuliza mwenzake nini ameona ule usiku lakini hakuna jibu liliopatikana maana wote walikuwa wamelala fofofo. Wote kwa pamoja wakaanza kupanga mipango jinsi gani wafanye ili mfalme asiwape adhabu ya kifo maana walikuwa awajui, nini mfalme ameona mwishowe wakapanga kwenda kumuomba msamaha endapo atakataa basi watakuwa tayari kupokea adhabu hiyo. Wakiwa wanaendelea kuongea ghafla wakasikia mlango wa ile nyumba ukigongwa kuashiria kuna mtu anataka kuingia humo, mapigo ya mioyo yao yakaanza kwenda mbio maana walihisi wamekuja kuchukuliwa na askari wa mfalme ili wakapewe adhabu yao. Japokuwa walikuwa wanaogopa lakini hawakuwa na jinsi mmoja wao akanyanyuka kwenda kufungua mlango na kukutana na kijana mwenzao anaeshughulika kule kwa mfalme, haraka akaingia ndani. Akasalimiana na wenzake kisha akaanza kuwaeleza nini kimempeleka mahara pale.
KIJANA: Nimeagizwa na mtukufu mfalme nije kuwapa taarifa anawahitaji majira ya mchana mfike nyumbani kwake.
Taarifa ile ilizidi kuwatisha na kujua kuwa mda wao wa kuishi hapa duniani umefika tamani, Yule mtoa taarifa alipomaliza akaondoka zake na kuwaacha wenzake wakiwa wamejiinamia. Waliendelea kukaa mle ndani kila mmoja akiwa na mawazo yake na hatimae mda walioambiwa waende kwa mfalme ukawadia, wakatoka kwenye ile nyumba na kuanza safiri ya kuelekea huko, Kwa kuwa ni vija walitembea kwa mwendo wa kijeshi { haraka } mda mfupi mbele wakafanikiwa kufika huko, na kamkuta mfalme akiwa amekaa pamoja na mke wake, wakawasalimia na kusubilia kuambiwa walichoitiwa, ndipo mfale akaanza kuongea.
MFALME: Nimewaita hapa ninataka mniambie nani kati yenu ameona kitu kwa mzee sube, maana nyie mlisema yeye ndie msababishaji wa mambo yote.
Wale vijana baada ya kuulizwa vile, walijikuta viungo vya miili yao vikifa nguvu na kulegea maana moja kwa moja wakagundua kuwa mfalme na yeye hakubahatika kuona kitu chochote kwa Sube, kumbe Mfalme aliwauliza vile kama kuwatega ili aone kama kuna ambae alikuwa ameona kile alichokiona yeye kwa mzee sube. Wale vijana walikaa kimya na kuinamisha vichwa vyao chini kuashiria hakuna kitu walichokiona, Mfalme alipoona vile akaona bora awaambie ukweli kile alichokuwa amekioa yeye japokuwa alihitaji afanye siri.
MFALME: Najua hakuna hata mmoja ambae ameona kitu kwa kuwa mlilala, ila mimi nilifanikiwa kuona kila kitu kwa mzee sube na sasa naamini yale maneno ambayo nyie muliniambia.
Vijana hawakuamini kile walichokisikia haraka waliinua vichwa vyao na kumtazama mfalme huku furaha ikitawara nafsini mwao na kufukuza huzuni, walipongezana kwa kazi mzuri walioifanya lakini mwisho wakahitaji kufahamu nini mfalme atafanya kwa mzee sube.
Sehemu Ya 10
KIJANA 1: Tunashukuru sana mtukufu mfalme kama umeliona jambo hili maana sisi tulikuwa na wasiwasi tulidhani na wewe haukuona kitu chochote. Ila tunahitaji kujua kitu gani umepanga kumfanyia mzee Sube.
Baada ya kuulizwa vile akaa kimya kwa sababu yeye hakutaka kufanya kama wao walivyokuwa wakidhania atafanya kwa yule mzee, lakini mwisho akaona bora awaambie ukweli jinsi yeye alivyopanga kufanya kwa Sube. Lakini mda huo Sube na mke wake walikuwa awajui chochote kuwa tayari wamefahamika wao ndio wabaya wa kile kijiji bali waliendelea kufanya shughuli yao ya kutibu watu walioumwa na yule nyoka.
MFALME: Mimi sina lengo la kumpa adhabu mzee sube kwa kuwa hii ni mara yake ya kwanza kokosea hapa kijijni. Kwahyo nataka nimuite ili nimuonye na endapo ataendelea kufanya hivi hapo nitampa adhabu.
Jibu la mfalme liliwashangaza sana wale vijana maana wao walijua kama mfalme ameshajua ukweli kilichobaki ni hukumu kwa mzee sube. Lakini vijana hawakukata tama wakaendelea kumuuliza maswali kutokana na uamuzi aliouchukua.
KIJANA 2: Lakini mfalme sheria ya hiki kijiji chetu inasema mtu akifanya jambo la kuhatarisha maisha ya wenzake kwa makusudi anatakiwa kupewa hukumu ya kifo mbele ya wanakijiji. Sasa inakuaje mzee sube unataka kumuonya na wakati yeye inatakiwa ahukumiwe kifo.
MFALME: Ni kwel kijina unachosema ila kwa hili ninaomba mnisamehe maana siwezi kumuhukumu haraka hivi kwa kuwa kwa sasa najua ana mambo mengi hapa kijijini pia amekua akitoa mawazo na ushauri mzuri kwangu jinsi ya kuongoza hiki kijiji. Kwahiyo endapo nitachukua uamuzi wa kumuua nitakuwa nimempoteza mtu muhimu kwangu.
Jibu la mfalme liliwaacha vijana mdomo wazi na kuhisi kitu Fulani kutoka kwake, maana kosa alilolifanya sube hakutakiwa kutetewa na mtu yoyote yule. Kwa kuwa mfalme ameshaamua kufanya hivyo wale vijana ikabidi wakubari kuwa wapole japokuwa waliumia kupita kiasi. Lakini kabla awajaondoka kijana mwingine akauliza swali.
KIJANA 2: Mtukufu mfalme hivi mtu muhimu anaweza kufanya jambo baya na hatari kama hili, hivi unajua nia ya yeye kufanya hivi, inakuaje kama alikuwa anahitaji kukuangamiza wewe. { Kijana aliongea hivyo ili kumjengea chuki mfalme lakini mfalme hakujali }
MFALME: Hayo unayoniuliza ni sahihi ila jua kuwa na yule ni binadamu kuna siku anakuwa anapitiwa na shetani na kujikuta akifanya vitu kama vile. Kwahiyo ni wajibu wetu kumrudisha mzee sube kutoka kwa shetani.
Maneno ya mfalme yalimchukiza sana mke wake pamoja na wale vijana, ndipo mke akadakia na kuanza kuongea maneno ya kumshangaa kwanini anafanya vile.
MKE: Hivi mume wangu kwani huyo mzee sube amekufanyia kitu gani kizuri mpaka umtete kiasi hiko kama washauri si utampata wingine mbona wazee wamejaa hapa Mbaka. Mara ngapi umewahukumu watu ambao ilikuwa ni mara yao ya kwanza kukosea au ndio unataka kubadilisha sheria. Ila kumbuka ulimuhukumu mke wako uliempenda sana pamoja na mkwe wako kwa kosa ambalo lilikuwa la kwanza wao kulifanya hapa kijijini au wale hawakuwa na umuhimu kwako na kwa hiki kijiji. Amka mume wangu huyu mtu unaemtetea leo ni zaidi ya Shetani kwa hiki kitendo alichokifanya kwetu sisi pamoja na hiki kijiji chetu cha mbaka.
Baada ya kusemaa vile kwa asira akaainuka na kuingia ndani na kuwaacha wale vijana wakiendelea kusubilia, Japokuwa maneno ya mke yalikuwa makali lakini hayakuweza kubadilisha msimamo wa mfalme, jambo ambalo lilizidi kuwachukiza wale vijana. walipomaliza kuongea wakaruhusiwa warudi majumbani kwao huku wakiwa wamepewa onyo endapo baya lolote litamkuta mzee Sube hukumu itakuwa juu yao, vijana wakaondoka huku wakisononeka. Baada ya kupita dakika kadhaa Mfalme akachukua walinzi wawili na kwenda nao nyumbani kwa sube na kumkuta akitengeneza dawa, sube akafurahi sana alipoona ametembelewa na Mfalme akamkaribisha vizuri kama sio yeye anaefanya mabaya, akaenda ndani kumuita mke wake, mda huo alikuwa ajui lolote bali alijua mfalme ameenda kumtembelea tu. Wakasalimiana nae ndipo Mfalme akamuomba Sube wasoge pembeni ili waonge kidogo, bila uwoga sube akasogea na kumuacha mke wake akiwa pamoja na wale walinzi, ndipo maongezi yakaanza.
MFALME: Mzee sube nimekuja hapa kwa ajili ya jambo moja ambalo limenisikitsha sana baada ya kufahamu ukweli wake.
Sube alipooambiwa vile hakuogopa maana alijua hilo jambo litakuwa linamuhusu mzee Bugu kwa kuwa yeye ndie alizaniwa kufanya mambo mabaya.
MZEE SUBE: mmmmh !!!. Jambo gani hilo mtukufu mfalme. { Aliuliza bila uwoga }
Sube alipouliza hivyo, Mfalme akaa kimya kwa huku akimtazama na kujiuliza wapi aanze kumwambia, mwishoe akaamua kuongea
MFALME: Kuhusu nyoka anaesumbua hapa kijijni.
MZEE SUBE: Ehe niambie umegundua ukweli gani kuhusu huyo nyoka. { alijifanya kuongea kwa mshangao mkubwa }
MFALME: Sube usijifanye kushangaa wakati wewe ndie muhusika wa jambo hili.
Mlipuko mkubwa mithiri ya bomu la nyukilia ulitokea kwenye moyo wa Mzee sube na kuanza kutetemeka maana hakutegemea kusikia kile alichoambiwa na mfalme, lakini akajitahidi kujikaza na kuendelea kuongea.
MZEE SUBE: Sijakuelewa mtukufu mfalme.
MFALME: Lazima usinielewe kwa kuwa ukweli umejulikana, sasa nataka uniambie yule Nyoka ulieniambia anaitwa Ruka wa nani. { Mfalme aliongea kwa hasira }
Sube alikataa na kusema amfahamu mwenye yule nyoka lakini mfalme aliendelea kum’bana na mwishoe sube akakosa kitu cha kujitetea na kubaki akiwa ameinamisha kichwa chni kuashiria kukubali lile kosa, Mfalme alisikitika sana alipoona jambo lile ndipo akaanza kumuonya.
MFALME: Sube nilikuamini sana na sikufikiria kama wewe ungekuwa muhusika wa jambo hili nimekufanya uwe mshauri wangu na ukanishauri mambo mazuri kumbe ulikuwa ukiniuma huku unapoliza, kwanini uliamua kufanya hivi nimeumia sana nilipofahamu ukweli huu. ujio wangu kwako nimekuja kukupa onyo mzuie huyo yoka wako, na usirudie tena kufanya jambo hili maana sitakusamehe tena bali hukumu ya kifo itakuwa juu yako kama nilivyofanya kwa wenzako waliosababisha matatizo hapa kijijini.
Aliposema hivyo akawachukua walinzi wake na kuondoka nao bila kuaga huku akiwa na hasira, kitendo kile kilimshangaza sana bibi sube na kujiuliza nini kimetokea, haraka akakimbilia sehemu aliyokuwa mume wake na kumkuta akiwa amesimama huku ameinamisha kichwa chini kama mtu alieonewa, ndipo akaona bora amuulize kilichotoekea.
BIBI SUBE: Meme wangu kwani kimetoke nini mbona mfalme ametoka kwa hasira vile.
Sube hakujibu kitu na kuendelea kuinamisha kichwa chake chini, jambo ambalo lilizidi kumchanganya bibi sube.
BIBI SUBE: Mume wangu kwani si ninakuuliza au aunisikii, kimetokea nini kati yako na mtukufu mfalme.
Sube aliopna mke wake ameng’ang’ania jambo hilo ndipo akamjibu huku misuri ya kichwa ikiwa imemsimama kutokana na kuchukia yale maneno ya mfalme.
MZEE SUBE: Mfalme amegundua ukweli kuhusu Yoka nahisi kuna mtu amemwambia.
Bibi sube alishtuka kupita kiasi na kuishiwa nguvu ya kusimama
BIBI SUBE: Eeeeeeeee !! Mume wangu mfalme amejua kweli ?. Sasa itakuaje jamani si kufa huku mume wangu.
aliposema hivyo Sube akajibu huku akiwa na jaziba kama mtu aliefumania ugoni au kuona mtoto wake akipigwa na jirani.
MZEE SUBE: Hafi mtu eti anasema amenisamehe ila nisirudie tena, chamoto watakiona sitajificha tena na nitafanya juu chini mpaka mfalme na yeye nimuangushe madarakani, na huyo alieenda kumwambia nikimgundua lazima arudi kuwa mavumbi, sipendi mtu aingile mambo yangu.
BIBI SUBE: Hapana mume wangu kama tumesamehewa tuachane na mambo haya tutakufa.
MZEE SUBE: Siogopi kufa na leo Mfalme ama zake ama zangu.
BIBI SUBE: Kwahiyo unataka kumfanya nini.
MZEE SUBE: Subilia utaona ikifka usiku.
Sube akatoka na kwenda kusikojulika na kumuacha mke wake bado akiwa amekaa pale pale chini, Bibi sube alisikitika sana na kujirahumu kwanini alikubali wafanye jambo lile lakini alikuwa ameshachelewa kuwaza jambo hilo. Mfalme alipofika nyumbani kwake kama kawaida mawazo yaliendelea kumtawala huku ajirahumu kwanini alimuamini mzee sube haraka vile mpaka inapelekea anashindwa kufanya hukumu inayo mstahiri. alijirahumu kwanini alikuwa akifanya mambo bila kuomba ushauri kwa wazee wengine na kusababisha kuondoa viongozi waaminifu na kumuweka mzee sube. Masaa yalienda hatimae usiku ukafika, Sube na mke wake wakajiaanda vizuri kufanya kazi yao kisha wakaenda nyumbani kwa mfalme kwa nija ya kichawi, na kumkuta akiwa amelala fofofo pamoja na mke wake, Ndipo wawili wale wakaanza kuimba na kucheza zile nyimbo zao za kichawi huku wakizunguka kitanda cha wawili wale. Mda huo Yoka na yeye alikuwa akizini kuuma watu kwa kasi maana Sube aliamua kufanya ubaya zaidi kwa wanakijiji wote. Walipomaliza kucheza Sube akachukua unga na kumlisha mfalme huku akisema maneno ikiwa kama kunuia kile anachomlisha.
MZEE SUBE: Wewe mfalme ninapokulisha unga huu ninataka usiwe na kauli yoyote kwangu na kila nitakachokisema mimi ukakikubali mara moja. Na endapo utaenda kinyume kifo kiwe juu yako.
Bibi sube akachukua maji yaliyokuwa kwenye kibuyu na kumnywesha mfalme, kisha wakatoeka na kutokea nymbani kwao huku wakiwa na furaha kutokana na kufanikiwa jambo lao. Ndipo Sube akaanza kumueleza mke wake vitu gani anatakiwa yeye afanye ikifika kesho yake ili ile dawa ikamilike asilimia zote.
MZEE SUBE: Mke wangu mpaka sasa hivi kazi tulioifanya imefikia asilimia Hamsini kwahiyo bado hamsini zingine ili kazi yote ikamilike kabisa.
BIBI SUBE: Kwanini umesema hivyo.
MZEE SUBE: Hii dawa itakamilika kesho asubuhi inabidi mimi nikamuamushe mfalme kabla ajaamka yeye mwenyewe au kuamshwa na mtu mwingne yeyote na endapo nitafanikiwa kufanya hivyo dawa itakuwa tumeifanikisha kwa asilimia zote..
Bibi sube hakua na chakuongea zaidi ya kumuomba mume wake awe makini atakapoenda huko kwa mfalme, wawili wale wakala. Mfalme akiwa kwenye usingizi alianza kuota ndoto.
Alikuwa yeye pamoja na mzee sube wakiwa wanatembe huku na kule katika kijiji chao huku mzee sube akiwa amebeba ule unga wenye rangi nyeupe na nyekundu na begani mwake alikuwa amembeba yule nyoka anaeitwa YOKA.Wakati wapo katikati ya safari ghafla mzee sube akaanza kurefuka na kuwa mkubwa, hapo hapo mfalme akabadirika na kuwa kama mtoto wa miaka minne au mtano, ndipo Sube akaanza kumcheka na kuongea maneno ya kumdharau.
MZEE SUBE: Hahahaha nahisi jeuri yako imefika mwisho. Siku zote siwezi kuongozwa na mtoto mdogo kama wewe na utakuwa ukifuata kila nitakachokuambia mimi.
Kisha akachukua ule unga na kumlisha,,,,,,, ghafla mfalme akashtuka kutoka usingizini na kukaa kitako huku akiitafakari ile ndoto. Mda mchache mbele mke na yeye akaamka na kumkuta mfalme akiwa amekaa akamuuliza tatizo, mfalme bila kuficha akamwambia nini ameota, mke alisikitika sana na kumwambia itakuwa mizimu imeamua kukuonyesha ubaya wa mzee sube kwahiyo kazi kwake kumuhukumu au kumsamehe kama alivyosema yeye mwenyewe. Maneno ya mke wake yalimgusa na kumfanya abadili ule uamuzi wake, akatoka nje na kuchukua walinzi kadhaa na kwenda nao mpaka nyumbani kwa mzee sube, mda huo ilikuwa yapata majira ya saa kumi na moja alfajiri. Walipofika nyumbani kwa mzee sube ndipo mfalme akafungua mlango na kuingia ndani bila hata hodi na kukuta wawili wale wakiwa bado wamelala. Akaamuru wale walinzi wawachukue,,,, Sube na mke wake walishtuka kuona mfalme amekuja kuwakamata maana hawakutegemea kabisa kutokea jambo hilo. Bila kuchelewa walinzi wakafanya kama walivyoambiwa wakawachukua na kuwapeleka mpaka mbele ya nyumba ya mfalme ambako huko ndiko utolewa hukumu. Kijana mmoja akaenda kupiga ngoma ya dharula ili wanakijiji wasogee sehemu ile washuhudie hukumu itakayo tolewa kwa mzee sube na mke wake. Watu wengi walijiuliza kitu gani kimetokea mpaka ikapigwa ile ngoma maana wengi wao walikuwa awajui nini kinaendelea pale kijijni. Kutokana na shahuku waliokuwa nayo haraka walitoka majumbani kwao na kuwasili nyumbani kwa mfalme na kukuta wawili wale wakiwa wamefungwa kwenye mti uliopo sehemu hiyo. Watu wengi walishangaa kuona sube na mke wake wapo sehemu ile pia wale wazee na wao walishangaa na kujiuliza nini sube amefanya mpaka afikie hatua ile wakati alikuwa mtu wa karibu na mfalme. Lakini maswali ya watu wote waliofika sehemu ile yalijibuwa baada ya Mfalme kueleza kosa la watu wale.
MFALME: Jamani nimewaita hapa kwa ajili ya kuona hukumu ya watu hawa kwa kosa la kutengeneza nyoka ambae ameleta madhara makubwa sana hapa kijijini kwetu na kusababisha vifo vya wenzetu wengi.
Maneno ya mfalme yalisababisha kutokea kimya kisichokuwa cha kawaida kutokana na watu wote kubaki vinywa wazi, kutokana na kuto amini kile walichokisia, mara minong’ono ya chinichini ikaanza ndipo mfalme akaendelea kuongea.
MFALME: Siku zote tumekuwa tukikataza watu kufanya mambo kama waliofanya wawili hawa na hukumu kali tumekuwa tukitoa kila anapopatikana mkosa lakini bado watu wanajifanya awaelewi wanaendelea kufanya mbambo yao, kwahiyo kutokana na kosa walilolifanya wanaukumiwa kifo kwa kupigwa mawe mpaka mwisho wa uhai wao.
Mfalme aliposema vile baadhi ya watu walipiga makofi na kushangilia jambo lile lakini wengine waliwaonea huruma na kutamani wangewasamehe, lakini kwa kuwa hukumu ilikuwa tayari imetoka basi hakukua na jinsi. mfalme akaendelea kuongea.
MFALME: Ila kabla ya yote napenda kutoa shukrani kwa vijana wa hiki kijiji kwa kazi yao kubwa walioifanya mpaka tukafanikiwa kumpata msaliti na hadui kwetu, na kuanzia sasa wale vijana wote walioshiriki kutika kumpata mbaya wetu watukuwa askari wangu. Ila kuna kitu nimejifunza sio kila anaekuchekea ni mwema kwao bali mda mwingine anasubilia ugeuze kisogo ili atoe makucha yake, nilimuamini sana huyu mzee na alikuwa akinipa ushauri mzuri kumbe huyo huyo ndie adui kwangu na kwa wanaichi wangu. ….. kwahiyo kuanzia sasa hukumu itolewe kwa watu hawa.
Ndipo wakaja baadhi ya askari wakiwa wamebeba mawe na kuweka mbele yao, walipomaliza kazi hiyo ndipo waanza kuwarushia. Wakati wanafanya vile, ghafla kwenye kichaka akichoishi Yoka kikaanza kuwaka moto na kutekete Yoka akiwemo ndani yake. Wale askari wakaendelea kuwapiga huku umati wa watu wakishuhudia jambo lile mpaka wawili wale walipokata roho, wakachukuliwa na kwenda kutupwa msituni kuwa chakula cha wanyama na wadudu waishio huko……. Na Huo ndio ukawa mwisho wa Sube, mke wake pamoja na Yoka, kuanzia hapo kijiji kikarudi kuwa na amani kama dhamani na wawili wale wakabaki kuwa kama stori hapo kijijini.
MWISHO


2 Comments
I like this website its a master peace ! Glad I discovered this on google .
Woah! I’m really digging the template/theme of this site. It’s simple, yet effective. A lot of times it’s tough to get that “perfect balance” between superb usability and appearance. I must say that you’ve done a superb job with this. Also, the blog loads very quick for me on Chrome. Outstanding Blog!