NYOKA WA KUTUMWA
Sehemu Ya 1
Katika kijiji kimoja kulikuwa na mzee mmoja aitwae mzee sube , Pia mzee sube alikuwa na mke ambae alikuwa anaitwa Dae { Bibi sube }. Mzee sube pamoja na mke wake walikuwa wanajishughulisha na kilimo maana awakuwa na uwezo, Maisha ya mzee sube pamoja na mke wake yalkuwa ni magumu japokuwa walikuwa wanajishughulisha na kilimo. Mzee sube pamoja na mke wake walikuwa ni wachawi wakubwa sana hapo kijijini kwao ila watu wa hiko kijiji walikuwa awafahamu kuhusu jambo hilo. Siku moja mzee sube alimuita mke wake na kuaanza kuongea nae kitu fulan kuhusu maisha yao.
MZEE SUBE: Mke mimi nimekuita hapa kuna kitu nataka tuongee.
BIBI SUBE: Kitu gani hiko mume wangu.?
MZEE SUBE: Kuna wazo nimelipata maana naona aya maisha tunayoishi sio mazur hata kidogo na wakati sisi ni watu wakubwa sana hapa kiijini.
BIBI SUBE: Ni kwel mume wangu yani hata mimi aya maisha nimeyachoka kabisa.
MZEE SUBE: Basi leo ndio itakuwa mwisho wa haya maisha magumu.
BIBI SUBE: Aya basi nambie hilo wazo lenyewe mume wangu .
MZEE SUBE: Mke wangu kuna kitu nataka tukifanye na kitu kitatufanya sisi tujulikane na tuwe watu wakubwa sana hapa kijijini na kila mtu ajue kuwa sisi ni wakina nani na huo ndio utakuwa mwanzo wa kujulikana kwetu na kufanikiwa pia.
Bibi sube baada ya kuambiwa vile akajikuta akiwa anashauku kubwa ya kutaka kujua hiko kitu chenyew kitakacho wajulisha wao katika kile kijiji chao.
BIBI SUBE: Bas niambie kitu chenyewe mume wangu maana unafanya niwe na furaha hata kabla sijambiwa kitu chenyewe.
MZEE SUBE: Mimi nataka kutengeneza nyoka ambae atakuwa anang’ata watu .
BIBI SUBE: Heee!! Ili kiwe nini mume wangu?
Bibi sube alishangazwa kidogo na lile wazo la mume wake maan akutegemea kama angesema wazo kama llile.
MZEE SUBE: Na mimi nilijua tu kuwa nikikuambia lazima ushangae kwa kuwa aujajua faida yake hapo baadae. nataka kumtengeneza nyoka na awe anauma watu na endapo utakuwa umeumwa na huyo nyoka itabidi uje uchukue dawa kwangu na hiyo dawa sitatoa bure bali nitakuwa naiuza kwa kubadilisha na chakula, je hilo sio wazo zuri ?
Bibi sube baada ya kuulizwa vile alikaa kimya kidogo na kisha akajibu.
BIBI SUBE: Unajua mume wangu mimi wala sikufkilia kama unataka kufanya hivyo nilidhani unataka kuwakomoa wanakijiji ili wakujue kuwa wewe ni nani ila kama ndio hivyo basi ni vizur tu mume wangu.
MZEE SUBE: Na ndio maana nakupenda sana mke wangu kwa kuwa ni muelewa na unapenda sana kusikiliza mawazo yangu na kuyafanyia kazi.
BIBI SUBE: Sawa nashukuru mume wangu kwahiyo hyo kaza ya kumtengeneza uyo nyoka itaanza lini?
MZEE SUBE: Inatakiwa tufanye leo hii hii tena usiku katika ule mda wetu wa kazi.
BIBI SUBE: Aha sawa nimekuelewa mume wangu na nitafanya utakalo wewe.
Basi baada ya kukubaliana vile kila mtu akaendelea na shughul zake za kila siku. Masaa yalipita na hatimae ukafika ule mda ambao mzee sube pamoja na mke wake walipanga kufanya shughuli yao ya kumtengeneza huyo nyoka wako. Mda ulipofka mzee sube alivaa kaniki na kichwan akajifunga kitambaa chekundu, pia bibi sube alikuwa amevaa kitambaa chenye rangu nyekundu na kichwani akajfunga kaniki. Mzee sube alikuwa ameshika ukili pamoja na nyumbu huku bibi sube akiwa amebeba vibuyu viwili vyenye unga wenye rangi ndani yake, kibuyu kimoja kiliwa na unga mweusi na kibuyu kingne kIlikuwa na unga mwekundu. Baada ya hapo wakatoka na kwenda nyuma ya nyumba yao ndipo mzee sube akachukua ule ukili na kuuweka chini kisha akachora chini kitu chenye umbile la nyoka likiwa limeizunguka ule ukil. Baada ya hapo bibi sube akachukua ule unga mweusi na kuanza kutia kwenye ule ukili, baada ya hapo ndipo mzee sube akaanza kuongea maneno fulan ya kichawi na baada ya kumaliza ndipo bibi sube akachukua unga mwekundu na kumiminia tena kwenye ule ukili. Baada ya kufanya vile mzee sube akachukua ule ukili na kwenda kwenye kichaka ambacho kilikuwa karibu sana na ile nyumba yao. Wakaanza kukizunguka kile kichaka huku wakiwa wanaimba nyimbo zao za kichawi. Sasa wakiwa wanafanya vile ghafla waliona manyasi ya kile kichaka yakiwa yanatikisika kumaanisha kuwa ule ukil alikuwa ushabadilika na kuwa nyoka kama walivyodhamilia wao. Mzee sube alienda kwenye kile kichaka na kumtoa yule nyoka. Kiukwel alikuwa ni nyoka mkubwa sana mwenye rangi ya blue yenye kung’aa huku mkian kwake pamoja na akichwan akiwa na rangi ya njano. Mzee sube baada ya kumchukua yule nyoka akaenda kumuweka sehemu ya wazi na kuanza kumnuia maneno fulani ya kumuongoza yule nyoka.
MZEE SUBE: Wewe nyoka nimekutengeneza kwa ajili ya kazi moja tu ya kuwadhuru watu wa hiki kijiji cha MBAKA. Pia nataka ufanye kile nitakachokuambia ufanya na mimi ndio nitakae kuongoza na hiki kichaka ndio itakuwa nyumba yako na kuanzia leo nakupa jina lako ni YOKA .
Alipomaliza kumnenea, akambeba yule nyoka na kumrudisha tena pale kwenye kichaka ila alipomuweka tu ghafla yule nyoka akabadlika na kurudi tena kuwa ukili. Jambo lile lilimfurahisha sana mzee sube maana aliona kuwa kafankiwa kwa asilimia mia katika kumtengeza yule nyoka. walipo maliza kufanya vile ndipo mzee sube pamoja na mke wake wakaondoka na kwenda ndani kupumzika huku wakiwa wanafuraha sana ya kufanikisha jambo lao, kwahiyo ile siku ikapta na kuja siku nyingne. Iipofka asubuhi mzee sube aliamka mapema sana na kuelekea kweye kile kichaka kwa ajili ya kumuangalia yule nyoka wake. Alipofika kwenye kile kicha aliukuta ule ukili kama alivyouacha jana usiku. Baada ya kuona vile ndipo mzee sube akasema maneno na kuuambia ule ukili.
MZEE SUBE: Usibadilike mpaka nitakapo kuruhusu mimi na endapo utakimbizwa na mtu wowote kimbilia hapa nyumban kwako.
Baada ya kusema vile ghafla ule ukili ukabadilika na kuwa nyoka na mda huo huo ukubadilka tena na kuwa ukili. Kitendo kile kilmfurahsha sana mzee sube maana alijua moja kwa moja kuwa Yoka amekubali kile kitu alichoambiwa. Baada ya hapo mzee sube alitoka pale kwenye kichaka na kurudi zake ndan. Alipofka alimkuta mke wake akiwa anachemsha uji kwa ajili ya kupasha tumbo joto ila waendelee na majukumu mengne. Mzee sube alipofka akaanza kuongea na mke wake.
MZEE SUBE: Habar yako mke wangu.?
BIBI SUBE: Mzuri tu mume wangu.
MZEE SUBE: Umeamkaje?
BIBi SUBE: eeee mume wangu kwani tulilala pamoja jaman ila maswal unayo niulza utazan nilienda kulala kwa jirani ( bibi sube aliongea kwa kumdhihaki mumewe )
MZEE SUBE: Hata kama tumelala pamoja je kama umeamka huku ukiwa unaumwa?
BIBI SUBE: Si ningekuambia mume wangu kipenz.
MZEE SUBE: Aya mama umeshinda wewe maana uking’ang’ania kitu ukubali kushindwa.
BIBI SUBE: Hahahaha sawa. Ehe mume wangu tuachane hii mada vipi ulienda kumuangalia YOKA?
MZEE SUBE: Ndio tena sahizi ninatoke huko huko kumuangalia.
BIBI SUBE: Ehe anaendeleaje?
MZEE SUBE: Nimemkuta yupo kama tulivyomuacha jana usiku kwahiyo inaonesha kuwa ile sehemu ni salama.
BIBI SUBE: Mh afadhali maana usiku wala sikulala kwa amani maana nilikuwa nahofia sana ile sehemu maana siunajua ni njiani pale ?
MZEE SUBE: Basi ndio hivyo pale ni sehemu salama japokuwa n barabarani .
BIBI SUBE: Basi kushukuru.
MZEE SUBE: ndio hivyo ila leo tuna kazi ya kwenda msituni kuchimba dawa ya kuwatibia watu baada ya kubanwa na YOKA.
BIBI SUBE: Alafu ni kweli basi ngoja nipike haraka haraka twende.
Basi baada ya hapo bibi sube alipika haraka haraka kama alivyo sema alipomaliza walikula na baada ya kumaliza ndipo safari ya kwenda msituni ikaanza. Sasa wakiwa njia mzee sube alianza kumwambia mke wake dawa ambayo inatafaa kumtibia mtu ambae ameng’atwa na yoka.
MZEE SUBE: Ehe unaijua dawa ambayo tunatakiwa tukaichukue kule msitun?
BIBI SUBE: Ndio naijua si ile dawa ya kuondoa sumu ya nyoka mwilini.
MZEE SUBE: Hapna sio hiyo, dawa inayotakiwa ni ile inayoweza kumrudisha Yoka kwenye ile hali ya ukil. Hiyo ndio dawa ya kuitafuta na ndio itaponyesha mtu.
BIBI SUBE: e kumbe mimi nilikuwa sifahamu.
wawili wale waliendelea kupiga stori na hatimae wakafika msitun, mzee sube alielekea moja kwa moja mpaka kwenye mti mmoja mkubwa na kuanza kuchimba mizizi ya ule mti. Bibi sube alipoona kuona vile na yeye akaanza kuchimba ile mizizi ya ule mti. Mda wote wakati wanachimba ule mti akukuwepo na hata mmoja wa kumuongelesha mwenzake wote walikuwa bize na kuchimba ile mizizi pia ilikuwa ni sheria ya ule msitu, endapo unaenda kuchimba mizizi ya dawa hautakiwi kuongea na mtu wowote wala kitu chochote pale msituni. Wakati wanachimba ile mizizi ghafla bibi sube aliona mti fulan mbele yake ambao ulitokea kumvutia sana, kwahiyo alipomaliza kuchimba ule mti wa kwanza ndipo akaenda kuchimba mizizi miwili ya ule mti alio uwona . Jambo lile llmshangaza sana mzee sube na kumfanya awe na maswali mengi sana maana ule mti akiochimba mwenzake sio ambao ukitakiwa. Kitendo kile kilmfanya mzee sube atamani kumuulza maswali mke wake lakini alishindwa kumuuliza kwa sababu ya taratibu ziliZopo pale msituni . Bibi sube aliendelea kuchimba ule mti na hatmae akamaliza Ndipo wakachukua vile vifaa vyao na kuanza kurudi nyumbani kwao. Walitumia mda mrefu kidogo kutoka nje ya ule msitu maana huo mti ulikuwa katikati na mara baada ya kutoka ndipo mzee sube akaanza kutoa lile dukuduku lake kutaka kujua kwanini alikuwa anachimba ule mti na wakati alikuwa lengo lao kufanya vile.
MZEE SUBE: nataka nikuulze kitu.
BIBI SUBE: Mh kitu gani hiko ( bibi sube aliongea kwa wasiwasi )
MZEE SUBE: Hivi unaweza kuniambia kuwa kwanini ulikuwa unachimba ule mti mwingine na wakati aikiwa lengo, Tena nilitamani nikulize pale pale ila sheria za mzimu ndio zilinibana.
BIBI SUBE: Na mimi nilijua tu lazma uniulize maana nilikuona jinsi ukivyoniangalia kwa kunishangaa ila ule mti mimi nlikuwa nataka kufanyia kazi yangu Fulani tofauti na hii.
MZEE SUBE: Aha maana nilishangaa sana kuona vile.
Sehemu Ya 2
BIBI SUBE: Na mimi nilijua tu lazma uniulize maana nilikuona jinsi ukivyoniangalia kwa kunishangaa ila ule mti mimi nlikuwa nataka kufanyia kazi yangu Fulani tofauti na hii.
MZEE SUBE: Aha maana nilishangaa sana kuona vile.
Walipomaliza kuongelea ile mada, waliendelea na safari yao huku wakiendelea kupiga stor zingine za hapa na pale. Walitumia masaa mawil kutembea na hatimae wakafika nyumban kwao na moja kwa moja wakaanza kuitengeneza ile dawa yao. Wakati wanatengezea ile dawa ndipo bibi sube akaanza kumuongelesha mume wake juu ya ile jambo lao.
BIBI SUBE: Mume wangu hivi wewe unajisikiaje tunavyofanya jambo hili .
MZEE SUBE: Ninafura kupita kiasi maana najua siku sio nyingi na sisi tutakuwa tunaishi kama wafalme hapa kijijini.
BIBI SUBE: Ni kweli lakini kwa upande wangu nusu nafurahia ila nusu nyingine sifuriha. Maana unakumbuka kilchompata mzee sui pamoja na mtoto wake Ama { mzee sui na Ama ni wahusika katika simulizi ya kwanza ihusuyo hiki hiki kijiji cha mbaka }. Sasa mimi naogopa sana maana isije ikatutokea kama yaliyowapata wenzetu na kama unavyojua jinsi sheria za hiki kijiji chetu cha mbaka zinavyowabana watu wabaya.
MZEE SUBE: Sawa ila siku zote kwenye maisha ukitanguliza kufikiria hasara hauwezi kufankiwa kamwe.
BIBI SUBE: kwahiyo unamaanisha nini maana sijakuelewa.
MZEE SUBE: Nina maanisha ukitaka kufanya jambo lolote usianze kufikilia madhara au matatizo yanayoweza kukupata katika utendaji wa hilo jambo na kuhusu mzee sui na mwanae ule ulikuwa ni uzembe wao wenyewe na ndio maana wakauawa. Ila mimi sitakuja kufanya uzembe kama ule.
BIBI SUBE: Sawa nimekuelewa.
Waliendelea kutengeneza ile dawa na hatimae wakafanikiwa kumaliza ndipo mzee sube akaanza kumwambia mke wake juu ya jambo ambalo wanatakiwa kulifanya ifkapo usiku.
MZEE SUBE: Kama unavyoona dawa ipo tayari kwahiyo leo usiku tunatakiwa tuanze kumruhusu Yoka kufanya kazi yake maana dawa iko tayari.
BIBI SUBE: Sawa.
MZEE SUBE: Sawa basi ngoja nikuache ninaenda kule mwemben kucheza bao.
BIBI SUBE: Sawa mume wangu ila usichelewe kurudi maana mda sio mrefu chakula kitakuwa tayari.
MZEE SUBE: sawa nmimekuelewa.
Mzee sube akaondoka na kumuacha mke wake akiwa anaanda chakula cha mchana ila baada ya kuona mume wake ameondoka ndipo akachukua ile dawa yake ya mti mwingine na kuanza kuitengeneza na hatimae akamaliza akaichukua na kwenda kuificha ndani sehemu ambayo mzee sube asingeweza kuiyona. Baada ya hapo akaendelea na mapishi na hatimae akamaliza na mara mume wake akarudi nyumban kwa ajili ya kula. Bibi sube akapakuwa kile chakula na kuanza kula walipomaliza wakaenda kupumzika huku wakisubiria kwa hamu usiku uingie ili wakaifanye ile kazi yao. Kuanzia hapo masaa yalinda haraka hatimae ikafika usiku, Ndipo mzee sube pamoja na mke wake wakavaa zile nguo zao za kichaw na kwenda nyuma ya nyumba yao huku bibi sube akiwa amebeba vile vtu alivyokuwa amebeba ile siku ya kwanza. Walipofika ndipo mzee sube akaanza kumuita yule nyoka kwa jina ambalo alikuwa amempatia, ila alikiwa anaita kwa sauti ya chini huku akipiga na mluzi. Alipofanya vile ghafla ule ukili kule kichakani ukabadilka na kuwa YOKA na kuelekea nyuma ya nyumba ambako alikuwa ameitwa. Alipofika ndipo mzee sube akaanza kuongea na yule nyoka wake.
MZEE SUBE: Nimekuita hapa kwa ajili ya kukupa ruhusa ya kuanza kuifanya kazi ambayo imefanya mimi nikutengeneze yani ni kuwadhuru watu wa hiki kijiji cha mbaka. Ila kumbuka kitu kimoja kile kichaka ndio nyumba yako na kila ifikapo saa kumi na moja alfajiri unatakiwa uwe usharudi pale kichakani .
Baada ya kusema vile akachukua unga mweusi ambao alikuwa ameushika mke wake na kuanza kumpaka huku akimnuia maneno fulani.
MZEE SUBE: Huu unga niliokupaka utakuwa unakusaidia wakati ukiwa katika matatizo, utakusaidia kupotea au kubadilika na kuwa ukili.
Aliposema vile akachukua unga mwekundu na kumpaka kinywani huku akimnuia maneno mengine.
MZEE SUBE: Huu unga nakupaka kwa ajili ya kukufanya uwe mkali na uwe na hasira mda wote na kwa kila mtu unaemuona kasoro mimi pamoja na mke wangu.
Baaada ya kufanya vile akamruhusu aende.
MZEE SUBE: Aya sasa uko huru kwenda kokote ila usisahau kila kitu nilchokuambia.
Baada ya kusema vile akamalizia kuongea maneno ya kichawi na ndipo Yoka akaondoka na kwenda kuianza kazi yake aliyotumwa. Yoka baada ya kuondoka ndipo mzee sube pamoja na mke wake na wao wakaelekea ndani kwa ajili ya kupumzika maana walikuwa washamaliza kazi yao kwa siku ile. Sasa Yoka akiwa akatika mawindo yake akapita karibu na nyumba moja ambayo ilikuwa karibu sana na nyumba ya mfalme na kubahatika kumuona kijana mmoja akiwa anatoka ndani ya nyumba yao, ndipo akaanza kummendelea { kumvizia } yule kijana ili akamuume. Huyo kijana bila kujua akasogea mpaka karibu na sehemu ambayo Yoka alikuwa amekaa akimvizia, ndipo yoka akaruka na kumbana yule kijana mguuni , kijana aligumia sana na kuanza kuangalia chini ili aone ni kitu gani ambacho kilikuwa kimemng’ata ila kwa bahat mbaya akufanikiwa kuona maana yoka baada ya kufanya vile tu akapotea. Ndugu wa yule kijana baada ya kusikia ile sauti ya ndugu yao ikipga kelele walitoka nje haraka na kwenda kuangalia kilichompata. Walipofika walimkuta ndugu yao akiwa amekaa chini huku akiwa amejishika mguuni, wakaanza kumuuliza maswali nini kimempata ndipo akaanza kueleza kilichomtokea.
NDUGU 1: Kaka kwani umepatwa na tatizo gani?
KIJANA: Mimi sijui jamani ila nahisi kuna mdudu ameniuma lakini sijajua ni mdudu gani nilipoangalia chini sikumuona.
NDUGU 2: sasa itakuwa nini hiko?
KJNA: hata sijui . { alijibu huku akiwa analia kutokana na maumivu makali ambayo alikuwa anayapata }
NDUGU 1: Basi tumpeleke ndani ili tuone hiyo sehemu aliyobanwa maana hapa atupaoni kutokana na hili giza.
Ndugu yake mwingine alitoa hilo wazo baada ya kushindwa kuona sehemu alipokuwa ameumia kutokana na giza nene lililope sehemu ile. Walimchukua yule kijina na kumpeleka ndani kuangalia hiyo sehemu ambayo alikiwa ameng’atwa, wakamuweka karibu na taa na kuanza kumkagua wakabahatika kupaona sehemu ambayo yule ndugu yao alikuwa ameng’atwa maana ilikuwa inamatobo manne pia ilikuwa nyeusi kama amepaka masizi. Kutokana na ile hali walioina kwenye kile kidonda moja kwa moja wakagundua ndugu yao alikuwa kabanwa na nyoka tena mwenye suma kali, ndipo wakaanza kutafuta dawa za kumsaidia kupunguza maumivu na kufanya ile sumu isiendee kumletea matatizo zaidi mwilini mwake. Waliangahika huku na kule kwa majirani zao wakitafuta dawa ya kumsaidia ndugu yao hatimae wakafanikiwa kuipata kisha wakampatia. Kwa mawazo yao walidhani kama wamefanikiwa kumsaidia ndugu yao kwa kumpatia ile dawa kumbe ilkuwa tofauti kabisa maana siku iliyofuatia asubuhi walimkuta ndugu yao akiwa ana hali mbaya na kile kidonda kikiwa kimechimbika na nyama ya ile sehemu kuoza. Jambo lile liliwashangaza sana wale ndugu zake maana ile dawa ambayo walimpatia usiku ilikuwa mzuri kwa kutibia sumu ya nyoka. Walipoona vile wakamchukua ndugu yao na kwenda nae kwa tabibu wa kijiji kwa ajili ya kupata dawa ambayo ingezeweza kumsaidia ndugu yao, walipofika wakamuelekeza kila kitu kilichompata ndugu yao.
NDUGU 1: Tabibu tumekuja tumemleta huyu ndugu yetu kapatwa na matatzo.
TABIBU: Matatizo gani ? { Aliuliza huku akimtazama mgonjwa }
Baada ya kuuliza vile ndipo wale ndugu wa yule kijina wakaanza kumsimulia.
NDUGU 1: Hayo matatizo amepata usiku wakati ameenda kujisadia na mwenyewe amesema kuna mdudu amemng’ata na sisi baada ya kumuangalia vizuri tukagundua kuwa kabanwa na nyoka. Kwahyo tukamtafutia ile dawa ya kutulizia maumivu pamoja na kupunguz a makali ya sumu tukampatia tukiamini kuwa tumemsaidia ndugu yetu cha ajabu leo asubuhi tumeamka tumemkuta akiwa kwenye hii hali.
Walipomaliza tabibu akaanza kuangalia kile kidonda cha yule kijana na kuwaeleza alichokiona yeye.
TABIBU: Jamani nimekiangalia kile kidonda inaonyesha ni kweli kang’atwa na nyoka tena mwenye sumu kali ila sasa kinacho nishangaza, kama mulimpa dawa kwanini awe kwenye hali kama ile maana mimi ninavyoijua dawa ile hata kama ukabanwa na nyoka wa aina gani endapo utaitumia lazima upate uafadhali sasa imekuaje kwa huyu mwenzenu ? { Aliongea kwa mshangao mkubwa }
NDUGU 1: Na ndio maana hata sisi tumeshangaa.
TABIBU: Alafu mbona kile kidonda chake kimechimbika vile na nyama yake naona imekuwa nyeusi sana imekuwaje ?
NDUGU 2: Hata hatufahamu na ndio maana tumekuja kwako ili utusaidie.
TABIBU: Mh hili ni tatizo kubwa na mimi wala sina dawa ya kumsaidia kutokana na tatizo lake maana dawa niliyonayo mimi ndio kama mliotumia huko kwenu.
Walipojibiwa vile waliumia sana na kuanza kumuangalia ndugu yao kwa huzuni, lakini hawakukata tama waliendelea kumuuliza tabibu maswali zaidi ili wapate msaada kwa ndugu yao.
NDUGU 2 : Kwahiyo tufanye nini maana sisi tunakutegemea wewe.
TABIBU: Mimi ninaona bora tumpeleke kwa mfalme ili atangazie watu kama kuna mtu atakaweza kumsaidia kabla ajapata madhara makubwa.
Aliposema vile wote walikubali na kumchukua yule ndugu yao na kumpeleka nyumbani kwa mfalme kwa ajili ya kuwatangazia watu ili wamsaidie kumpa dawa za kumponyesha.
Walipofka kwa mfalme wakasalimiana nae kisha tabibu akaanza kumwambia mfalme juu ya tatizo lililomkuta yule kijana.
TABIBU: mtukufu mfalme huyu kijina kapatwa na matatizo jana usiku.
Mfalme alishangaa kusia vile maana hata siku moja yule tatbibu hakuwai kumpeleka mgonjwa pale kwake,.
MFALME: Matatizo gani hayo tabibu?
TABIBU: Jana usiku huyu kijana alitoka nje kujisahdia ila kwa bahati mbaya aling’atwa na mdudu na baada ya kumchunguza vizuri tukagundua aling’atwa na nyoka. Ila cha ajabu amepewa ile dawa ya kuzuia sumu ya nyoka ila hali yake bado imekuwa mbaya zaidi.
MFALME: Sasa wewe ndio tabibu wa hiki kijiji cha mbaka unamsaidiaje huyu kijana?
TABIBU: Kusema kweli mtukufu mfalme mimi nimeshindwa kumsaidia kwa sababu dawa niliyonayo mimi ndio ambayo amepewa na haikumsaidia ndio maana nikaona bora nimlete kwako ili uwatangazie wanakijiji wengi waje kumsaidia.
MFALME; Sasa kama wewe umeshindwa nani ataweza kumsaidia na wakati wewe ndio unategemewa hapa kijijini.
TABIBU; Ni kwel mtukufu mfalme ila kwa hili lpo nje ya uwezo wangu na ndio maana nikaona bora uwatangazie watu wengine ili waje wamsaidie kama wao wataweza.
MFALME: Sawa nmekuelrwa.
Mfalme akamuagiza kijina apige ng’oma ya dharula kwa ajili ya kuwaita wanakijiji katika ule uwanja wao wa mkutano, kijana akafanya kama alivyo agizwa. Wakati inapigwa ile ng’oma mzee sube pamoja na mke wake walibahatka kuisikia ile sauti na moja kwa moja wakahisi kuwa labda Yule nyoka wao mwenye jina la YOKA alikuwa kafanya kazi yake ambayo alikuwa ametumwa, mzee sube akamuomba mke wake abaki pale nyumbani na yeye aende huko kwa mfalme.
MZEE SUBE : Mke wangu hiyo ng’oma inayopigwa huko nahisi kunatatizo limetokea kwa mfalme alafu kichwani mwangu naona hilo tatizo kama kalisababsha Yoka.
BIBI SUBE: Yani kama ulikuwa kichwani mwangu hivi maana hata mimi ninmehisi hivyo hivyo
MZEE SUBE: Sasa tufanye kitu kmoja mimi ngoja niende alafu wewe baki hapa nyumbani chochote kitakachotokea kule nitakuja kukuambia.
BIBI SUBE: Sawa safari njema ila kuwa makini.
MZEE SUBE: Wala usijari mke wangu.
Mzee sube akatoka nje na kuanza safari ya kwenda nyumbani kwa mfalme, alijtahi kutembea haraka sana na hatimae akafika na kuwakuta watu wengine wameshafika pale uwanja ndipo mfalme akasimama akawasalimia wanakijiji na kuanza kuongea juu ya jambo ambalo limfanya awaite pale.
MFALME: Jamani wananchi wa hiki kijiji cha mbaka nimewaita hapa kwa ajili ya jambo moja na ninahitaji msaada wenu juu ya jambo hili.
Mfalme baada ya kusema vile ndipo wanakijiji wakaanza kutazamana huku wengine wakiwa wananong’ona wakiulizana Ila kwa upande wa mzee sube moyo wake ulikuwa unaenda mbio na hakutaka kuongea na mtu yoyote bali alikuwa makini kusikiliza anachokisema mfalme, wanakijiji waliponyamaza mfalme akaendelea kuongea.
MFALME: Jambo lenyewe ni hili , hapa kuna kijana ameletwa ameumwa na nyoka na alipewa ile dawa ambayo huwa tunaitumiaga kuuwa sumu ya nyoka ila bado hali yake mbaya .Kwahiyo mimi sipo tayari kumpoteza huyu kijina kama kuna mtu anadawa ya kumsaidia naomba ajitokeze ila iwe tofauti na ile dawa ya kijiji iliyotengenezwa na mababu zetu.
Mzee sube aliposikia vile moyo wake ulilpuka kutokana na furaha ambayo alikuwa nayo, haraka bila uwoga akapita mbele na kumueleza mfalme kuwa yeye anaweza kumsaidia yule kijana, Mfalme alifurahi sana kusikia vile mda huo wananchi walikuwa wakinong’onezana kutoka na mzee sube kujitokeza.
MZEE SUBE: Mtukufu mfalme mimi ninaweza kumsaidia huyo kijana.
MFALME: Kweli mzee ?
MZEE SUBE: kweli mtukufu mfalme.
MFALME: Aya mzee anza kazi na endapo utafanikiwa kumsaidia huyu kijana nitakupatia zawadi.
MZEE SUBE: Sawa mtukufu mfalme ila naomba uniruhusu nikachukue dawa yangu nyumbani ninakuahidi huyu kijna atakuwa mzima kabisa.
MFALME: Sawa fanya haraka kabla hatujampoteza huyu kijana.
Baada kuruhusiwa akakimbia haraka na akafanikiwa kufika nyumbani kwake na kumkuta mke wake akiwa amekaa kwenye mkeka ajui hili wala lile linaloendelea kwenye mkutano kule kwa mfalme. Alipofika alikuwa anahema haraka haraka kutokana na kukimbia kwa speed { haraka } Baada ya kukaa sawa ndipo akamsimulia mke wake kwa ufupi kilchotokea kwa mfalme.
Sehemu Ya 3
MFALME: Sawa fanya haraka kabla hatujampoteza huyu kijana.
Baada kuruhusiwa akakimbia haraka na akafanikiwa kufika nyumbani kwake na kumkuta mke wake akiwa amekaa kwenye mkeka ajui hili wala lile linaloendelea kwenye mkutano kule kwa mfalme. Alipofika alikuwa anahema haraka haraka kutokana na kukimbia kwa speed { haraka } Baada ya kukaa sawa ndipo akamsimulia mke wake kwa ufupi kilchotokea kwa mfalme.
Alipofika alikuwa anahema haraka haraka kutokana na kukimbia kwa speed { haraka } Baada ya kukaa sawa ndipo akamsimulia mke wake kwa ufupi kilchotokea kwa mfalme.
MZEE SUBE: Mke wangu tumefanikiwa tena kwa asilimia elfu kumi maana mia ni ndogo.
BIBI SUBE: Kwanini maana umenishtua sana ulivyokuwa unakuja nilihisi unakimbizwa.
MZEE SUBE: Sio nakimbizwa ila hii ni furaha maana mfalme amekubalia nikamtibu mtu ambae kang’atwa na yoka.
BIBI SUBE: Heee! Mume wangu kweli ?
MZEE SUBE: Kweli Hivi hapa unavyoniona nimekuja kuchukua dawa na kuondoka.
BIBI SUBE: Kama ndio hivyo na mimi ninakuja huko huko.
MZEE SUBE: Yani hata kama utataka kuibeba mpaka nyumba uje nayo wewe beba twende, Kwanza ngoja nikachukue dawa ili twende kabla sijachelewa.
Akaingia ndani na kwenda kuichukua ile dawa yake, alipotoka bibi sube na yeye akaenda chumbani akuchelewa akatoka wakaanza safar yao ya kwenda kwa mfalme. Kutokana na mwendo wa haraka waliokuwa wanatembea wakafanikiwa kufika mapema nyumbani kwa mfalme na kuwakuta watu wakiwa wanasubiria. Ndipo mzee sube akamuweka vizur yule mgonjwa huku akisaidiwa na mke wake, akachukua ile dawa yake na kumtia kwenye kidonda na nyingine akamnywesha. Walikaa kwa dakika kadhaa wakisubilia yule kijina apate afadhali ila cha ajabu hali yake ilizidi kuwa mbaya jambo ambalo lilimshangaza sana mzee sube. Bibi sube alipoona vile akatoa ile dawa yake na kumpatia mume wake ili amnyweshe yule mgonjwa, Sube akachukua ile dawa na kumnywesha zikapita dakika kama mbili yule kijina akazinduka maana alikuwa kama mtu aliezimia. Jambo lile llmshangaza sana mzee sube na kujikuta akimuangalia mke wake kwa jicho la mshangao kumaansha kuna kitu alihitaji kumuuliza lakini alishindwa kutokana na kuwepo kwa watu karibu yao. Wanakijiji pamoja na mfalme walifurahi sana kuona yule kijana amepona, ndipo mfalme akaanza kuongea na wanakijiji huku akiwa anamshukuru sana sube pamoja na mke wake.
MFALME: Wakijiji kwanza nina furaha sana juu ya uponyaji ambao kaupata huyu kijna pia napenda kutoa shukrani zangu nyingi kwa huyu mzee pamoja na mke wake maana jambo ambalo wamelilifanya sio kwamba limemsaidia huyu kijana tu bali na wanambaka wote. Maana huyu kijina anaweza kuwa askari au mfalme na akasaidia hiki kijiji chetu huko mbeleni. Kwahyo jambo alilolinya huyu mzee la kupongezwa sana na kila mtu.
Mfalme aliposema hivyo wanakijiji wakaapiga makofi kwa ajili ya kumpongeza mzee sube, Lakini wakatii wanakijiji wanapiga makofi, Sube alikuwa mbali sana kimawazo kutokana na kile kitendo ambacho amekifanya mke wake. walipoacha kumpongeza, mfalme akamtangaza rasmi mzee sube ndie atakaekuwa tabibu mkuu pale kijijini kutokana na ule msahada ambao alikuwa ameufanya.
MFALME: Sasa baada ya kumpongea kwa maneno na kwa kumpigia makofi, mimi nataka nimpe zawadi nyingine nampa cheo cha kuwa tabibu mkuu hapa kijijini kwetu maana inaonesha anazijua dawa nyingi ambazo zitaweza kutusaida.
Maneno ya mfalme yalimfanya mzee sube afurahi sana maana aliona malengo yake yamekwisha timia. Mfalme alihailisha ule mkutano na kuwaambia watu wakaendele kufanya shughuli za zingine za kuleta maendelea pale kijini kwao, Wanakijiji baada ya kuondoka ndipo akamuita mzee sube na kuanza kuongea nae.
MFALME: Mzee wangu kutokana na cheo ambacho nimekupa unatakiwa ukae karibu na hapa nyumbani kwangu ili wanakijiji wakipatwa na matatizo iwe rahisi kukupata.
Wazo la mfalme na maneno yake yalikuwa ni mazur sana ila kwa upande wa Sube alikuwa wazo zuri hata kidogo maana aliona kama angeamia karibu na mfalme ingekuwa rahisi kumgundua kuwa yeye ndio msababishaji wa yote maana asingekuwa na sehemu ya kumtunza yule nyoka wake.
MZEE SUBE: Ni wazo zuri mtukufu mfalm ila mimi ninaona bora nibaki kule kule maana ni karibu na msituni kwahiyo nitakuwa napata dawa kwa urahisi kuliko nikija kukaa huku itakuwa mbali na msituni.
Sube baada ya kupinga wazo lile, mfalme alimlazimisha lakini haikuwezekana alizidi kupinga na kutoa sababu zake nyingine ambazo zilifanya mfalme akubali kumuacha aendelee kukaa kule nyumbani kwake.
MFALME: Sasa kama ukihitaji dawa utakuwa unawatuma vijana ambao watakuwa wakikusaidi.
MZEE SUBE: Sawa ila kwa hizi kazi sio rahis kumtuma mtu akakuchukulie dawa msituni na akakuletea kama unayohitaiji wewe. Kwahiyo usijari mtukufu mfalme nitafanya kazi kwa ufasaha zaidi japokuwa nitakuwa naishi mbali na eneo lako na mda wowote utakao nihitaji haraka nitawaslii.
MFALME: Sawa nimekuelewa.
Walipomaliza maongezi yao sube akamchukua mke wake na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwao, wakiwa njiani ndipo akaanza kuuliza kuhusu ile dawa.
MZEE SUBE: Ehe mke wangu nimekumbuka kitu nataka uniambie ile dawa wewe uliipata wapi?
BIBI SUBE: Hahaha wewe unajifanya kujua dawa sasa ilikuwaje ukashindwa kuigundua ile, tena bila mimi leo ungeumbuka. { Aliongea kwa kumdhihaki huku akiwa anacheka }
MZEE SUBE: Yani bila wewe mwanamke leo mimi sijui ningekuwa mgeni wa nani sijui na jinsi kijijini wasivyo tupenda mh.
BIBI SUBE: Na ndio maana nimekuwa mke wako ili endapo utakwama na jambo lolote nikusaidie.
MZEE SUBE: Mmmmh mwanamke una maneno mazuri wewe ila shida yangu kubwa nataka kujua ile dawa umeipata wapi?
BIBI SUBE: Nliipata kule msituni na ilitokana na ule mti mwingne.
MZEE SUBE: Haaaa kumbe sasa uliujuaje ule mti ni dawa.?
Bibi sube baada ya kuulizwa vile ndipo akaanza kutoa histori juu ya kuufahamu ule mti na kazi yake.
BIBI SUBE: Bibi kabla ajafariki siku moja alinchukua kule msituni kwa ajili ya kumsaidia kuchimba dawa zake, tukiwa msituni kwa bahati mbaya mimi nikang’atwa na nyoka ambae aliniambia kuwa ana sumu kal,. Akaniambia kuna mti mmoja tu ambao mizizi yake ndio itaweza kunisaidia kupona. Kutokana na uadimu wa ule mti ilfanya bibi kuangaika huku mimi hali yangu ikizidi kuwa mbaya zaidi. Alijitahidi kuutafuta ule mti bila ya kukata tamaa maana akupenda aone mimi nikipoteza maisha nikiwa bado mdogo tena mbele macho yake, Katika kuangaika sana akafanikiwa kuupata ule mti na kunitengenezea dawa, nilipoitumia mda mfupi mbele nikaanza kurudi kwenye hali ya kawaida.
MZEE SUBE: Mh! Sasa ikawaje baada ya hapo maana hiyo hstoria yako nimeipenda.
BIBI SUBE: mmmh na wewe kwa kupenda hadithi. {akaendelea kusimulia} Mda ukivyozidi kwenda na mimi nilizidi kupata uafadhari na hatimae nikapona kabisa, ndipo bibi akanichukua na kunipeleka kwenye ule mti na kuniambia ndio ulio nsaidia endapo nitapata ugonjwa wowote au kuumwa na mdudu wowote awe wa kutumwa au sio wakutumwa lazima nipone na hiyo sio kwangu tu bali kwa watu wote. Ila aliniambia kuwa ule mti una kawaida ya kupoteapote na huwa unaletwa na mzimu kwa mda fulani na hatimae unatoka pale ulipo na kwenda sehemu nyingine na tangu niuone wakati nipo mtoto ndio nimeuona tena ile siku na nilishindwa kukuambia chochote kutokana na sheria za pale msitu.
MZEE SUBE: Hapa nilipo kichwa chote kinawaka moto maana huo mti kama una kawaida ya kupotea sasa itakuwaje na wakati ule mti ndio dawa ya kuzuia sumu ya YOka ?
BIBI SUBE: Ndio hivyo ila nakumbuka aliniambia kitu kingine kama unataka uupate ule mti kwa urahisi inabidi uende usiku tena ukiwa umevaa zile nguo za kazi na unatakiwa uombe ile mzimu ikuonyeshe ule mti ulipo kwa mda ule.
MZEE SUBE: haaa! Kama ndio hivyo basi leo usiku inatakiwa twende kule msituni kwa ajili ya kuutafuta huo mti Maana Isije Yoka akamng’ata mtu tukashndwa kumsaidia kwa sababu dawa tayari imeisha.
SIMULIZI YA KICHAWI : Nyoka Wa Kutumwa
Sehemu Ya 4
MZEE SUBE: haaa! Kama ndio hivyo basi leo usiku inatakiwa twende kule msituni kwa ajili ya kuutafuta huo mti Maana Isije Yoka akamng’ata mtu tukashndwa kumsaidia kwa sababu dawa tayari imeisha.
BIBI SUBE: Sawa mume wangu.
Waliendea na safari yao huku wakiendelea kuiongelea ile dawa na hatimae wakafanikiwa kufika nyumbani kwao na kuanza kupanga dhana ambazo watazitumia hapo usiku kule msituni. Walipomaliza wakaendelea kufanya shughuli zao za kila siku huku wakiwa wanasubiria kwa hamu ufike usiku ili wakachukue ile dawa. Masaa yakapita na hatmae usiku ukafika na ndipo mzee sube pamoja na mke wakaanza kujiaanda kwa ajili ya safari yao ya kwenda msituni. Walipomaliza Sube akatoka nje na kwenda kwenye kile kichaka na kumruhusu Yoka akafanye kazi yake, ndipo na wawo wakaanza safari yao ya kwenda msituni mda huo ilkiwa yapata saa sita usiku. Walitembea kwa miguu kutoka kwao mpaka karibu na kutoka nje ya kijiji kisha wakasimama na kushikana mikono huku wakiwa wanaangalian wakiwongea maneno fulani ya kichawi ghafla wakapotea pale ambapo walikuwa wamesimama na kutokea moja kwa moja ndani ya msitu huku wakiwa bado wameshikana mikono.
Wakaachana mikono na kuanza kuimba na kucheza nyimbo zao za kichawi, Sasa wakati wao wanafanya mambo yao, Yoka na yeye alikuwa kazini. Baada ya kutoka kichani akaanza kuzunguka katika kile kijiji akitafuta mtu wa kumng’ata. wawili wale walipomaliza kuimba nyimbo zao ndipo bibi sube akaanza kuongea na mizimu ili wapate kuuona ule mti kwa urahisi.
BIBI SUBE: Mababu na mabibi zetu sisi ni wajukuu zenu tumekuja tunashida tunaomba mutusaidie.
Akanyamaza na kuanza kusikiliza nini mizmu itasema kama itawapokea au laa, lakini kwa bahati mbaya kimya kilitawala na hakuna ishara yoyote ambayo ilijionyesha kuashiria mizimu kukubari ombi lao ndipo bibi sube akarudia tena.
BIBI SUBE: Mababu na mabibi sisi ni wajukuu zenu tumekuja tunahitaji msahada wenu.
Baada ya kurudia ghafla akatokea bibi yake ambae alimuonyesha ule mti kipindi ameng’atwa na nyoka, alikuwa amevaa kaniki na kujifunika kitambaa chekundu kichwani, aliwatama na akaanza kuongea na wawili wale huku wakiwa wameinamsha vichwa vyao chini.
BIBI: Karibu wakuju zangu karibuni sana. Mizimu imekubari kuwasikiliza na imejua nini shida yenu na ipo tayari kuwasaidia ila hii iwe siri yenu.
Alipomaliza kuongea ghafla akapotea ndipo mzee sube na mke wake wakainua vichwa vyao na kuanza kuangalia huku na kule wakiwa wanamtafuta yule bibi, wakiwa kwenye haraka za kumtafuta bibi sube akauona ule mti uikiwa mbele yao. Akamshtua mzee sube kisha wakaenda kuuchimba mizizi ya ule mti. Walipomaliza waliiaga mizimu na hatamae wakashikana mkono na kupotea pale mstuni na wakatokea nyumbani kwao huku wakiwa na furaha sana. Mara baada ya kufika walisikia mtu akipiga hodi kwa nguvu kwenye mlango wa nyumba yao. Kitendo kile kiliwatisha sana walikaa kimya kwa mda kigodo huku wakiwa wanabadirsha zile nguo zao za kazi ambazo walikuwa wamevaa kule mstuni na kuvaa nguo zao za kawaida ndipo wakaende kufungua mlango. Walimkuta baba mmoja akiwa analia kwa uchungu kama mtu aliefiwa na mwae mpendwa au mke wake, mzee sube alipoona vile ikabidi amuulize kulikoni maana ni kitu cha ajabu kidogo mwanaume kulia kama mtoto mdogo
MZEE SUBE: Heee! kulikoni mbona upo hivyo?
BABA: Nina shida baba yangu ninahitaji msahada wako.
MZEE SUBE: Shida gani hiyo mwanangu na mbona usiku sana?
BABA: Mwanangu kang’atwa na nyoka nimempa dawa ya kuua sumu ila hali yake bado mbaya.
MZEE SUBE: Pole sana mwanangu ila usijari mwanao atapona na atakuwa mzima kama kawaida.
BABA: Nitashukuru sana kama utayasaidia maisha ya mwanangu.
MZEE SUBE: Basi subilia kidogo nitengeneze dawa.
BABA: Sawa.
Akaingia ndani na kumsubili mzee sube atengeneze hiyo dawa, mzee sube akachukua ile mzizi ambayo walikuwa wamechmba katika ule mti na kuanza kuipondaponda kwenye jiwe ambalo alikuwa anatumia katika kutengenezea dawa zake. Alipomaliza kuitengeneza akaongozana na yule baba kwenda nae nyumban kwake. Waliwakuta watu wengi kidogo wakimuangalia yule mtoto ambae kwa mda huo hali yake ilizidi kuwa mbaya zaidi, ndipo mzee sube akaanza kufanya mambo yake na hatimae yule mtoto akapona kabisa tena kwa mda mfupi sana. Kitendo kile kiliwafurahisha sana wanakijiji ambao walikuwa pale na kumuona mzee sube ndio mtu anae faa sana pale kijijini kwao na kumbe walikuwa awajui kuwa yeye ndie chanzo. Alipomaliza kazi yake akarudi nyumbani kwake huku akiwa na furaha kubwa sana, ile siku ikawa imepta. Siku iliyofuatia asubuhi habari zilimfikia mfalme juu ya jambo ambalo amelifanya mzee sube juu ya kumtibu yule mtoto, habari hiyo ilimfurahisha sana mfalme na kumfanya amuite mzee sube nyumbani kwake kwa ajili ya maongozi fulani. Mzee sube baada ya kupata taarifa ya kuitwa kwa mfalme haraka aliwasili na kumkuta mfalme akiwa amekaa pamoja na viongozi wengine wa kile kijiji, walisalimiana na ndipo mfalme akaanza kumuambia lengo la kumuita pale.
MFALME: Nimekuita hapa kwa ajili ya kukupa pongezi kwa jambo ambalo umelifanya jana kumtibu yule mtoto. Pia nimejuita kwa ajili ya kukupa zawadi kutokana na wema ambao umekuwa ukiufanya kwa hawa wanakijiji wenzako.
MZEE SUBE: Lazima nifanye hivyo mtukufu mfalme.
MFALME: Sawa, kwahiyo nimeona bora nikupe zawadi ya eneo ambalo utakuwa unafanya shamba lako pia nitakupa na watu ambao watakuwa wakulimia hilo eneo na nina fanya hivi kama shukrani zangu kwako.
Mzee sube baada ya kusikia vile alifurahi sana na kumshukuru mfalme kutokana na zawadi ambayo amempatia.
MZEE SUBE: Nashukuru sana mfalme wangu hata sijui nsfanye nini ili nionyeshe hii furaha yangu. Ila mimi nakuahidi nitakuwa bega kwa bega na wanakijiji na nitatoa msahada wangu kadri niwezavyo.
MFALME: Sawa na mimi nakuahidi kuwa karibu sana na wewe katika kuwasaidia awa wanakijiji. Ila mzee unaweza kuniambia huyo nyoka atakuwa ni wa aina gani mpaka awe na sumu kali kiasi kile maana sijawai kusikia wala kumuona nyoka wa aina hiyo.
Mzee sube alishtuka kidogo maana alihisi kama mfalme ataweza kuhisi kitu juu ya huyo nyoka ikabidi amdanganye.
MZEE SUBE: Huyo nyoka hatari sana mfalme pia nyoka kama huyu mara nyingi huwa anaishi mistun na kuonekana kwake ni nadra sana na ndio maana wewe umeshindwa kumfahamu na hata kusikia habari zake maana watu wamekuwa wakimsahau mara kwa mara.
MFALME: Heee kumbe sasa huyo nyoka anaitwa jina gani.
MZEE SUBE: Huyo nyoka anaitwa RUKA.
MFALME: Ahaa sasa tunatakiwa tufanyaje ili tumkamate.
MZEE SUBE: aa huyu nyoka huwa awindwi maana ni mkali sana ila huwa anakaa sehemu moja na baadae anatoka yeye mwenyewe bila ya kufukuzwa na mtu.
MFALME: Kwahiyo ataendelea kuwadhuru watu mpaka atakapotoka yeye mwenywe.
MZEE SUBE: Ndio hivyo mtukufu mfalme maana atuna jinsi.
MFALME: Mh! Sawa.
Jibu lile lilimfanya mfalme akose raha maana aliona kuwa kijiji kipo katika wakati mgumu juu ya jambo lile, Walipomaliza Kuongea na waliagana ili kila mtu akaendele kufanya shughur zake, ila ajaondoka alimsihii mfalme asimwambie mtu kuhusu yule nyoka wala kupanga mipango ya kumtafuta.
MZEE SUBE: Mtukufu mfalme nakuomba usimwambie mtu yoyote kuhusu huyu nyoka maana tutakuwa tumevunja miiko ya mababu na mabibi zetu. Pia usisubutu kumtafuta RUka maana utasababisha matatizo makubwa zaidi hapa kijijini.
Mfalme alishangaa kidogo maana aliona kama mzee sube amekuwa akimlinda yule nyoka asiuawe lakini kutokana na ukubwa wa mzee sube, mfalme ilibidi akubari tu maana aliona kuwa inawezekana kuwa kweli kama atafanya vile atakuwa amevunja miiko ya kijiji chao. Baada ya hapo ndipo mzee akarud nyumban kwake huku akiwa na furaha kubwa maana amefakiwa kumdanganya mfalme pia kapewa shamba pamoja na wafanyakazi wa kumlimia hilo shamba . Alipofika nyumbani alimkuta mke wake akiwa anapika uji kwa ajili ya kupasha matumbo moto, mzee sube akamuita mke wake huku akiwa na furaha na kuanza kumsimulia kilichotokea kwa mfalme. Wakati huo mfalme na yeye alikuwa akiwaza na kuwazua njia gani atumie kulitatua lile tatizo lililoingia kijijini kwao, ila aliishiwa nguvu kila alipokuwa akiyakumbuka maneno yam zee sube.
MZEE SUBE: Mke wangu akuna siku ambayo nina furaha kama leo .
BIBI SUBE: Ehe nambie unafuraha ya nini?
MZEE SUBE: Yani hauwezi amini hapa tulipo tumepewa shamba na mfalme isitoshe ametupatia mpaka na wafanya kazi wa kulima hilo shamba.
BIBI SUBE: Hee ! Mume wangu kweli au unantania tu?
MZEE SUBE: Sikudanganyi alafu kuna kitu hicho yani da hata sijui nisemaje hivi unajua kuwa mfalme akitafuta ya njia ya kumuangamiza YOKA?
BIBI SUBE: Aaaaa! Sasa imekuaje mbona naogopa.
MZEE SUBE: Sasa unaogopa nini wewe mfalme hawezi kufanya kitu chochote kusuhu yoka maana jinsi nlivyomwambia nahisi wala hata taka kumtafuta.
BIBI SUBE: Kwahiyo kasitisha hilo zoezi?
MZEE SUBE: Ndio hvyo yan leo ni siku ya kufuraha alafu kuanzia leo Nimataka nimruhusu yoka afanye kazi mpaka mchana.
BIBI SUBE: Mume wangu hauoni kma itakuwa hatari kwa upande wetu pamoja na yoka?
MZEE SUBE: wala usiogope mke wangu nakuahid nitakuwa makini juu ya jambo hli .
Aliposema vile akanyanyuka na kwenda mpaka kwenye kichaka na baada ya kufika akaangalia kushoto na kulia kwake il aone kma kuna mtu anakuja au anamuona na baada ya hapo ndipo akaanza kusema maneno fulani huku ukiwa ameinamia kile kichaka. Baada ya kufanya hivyo mara akatoka nyoka kwenye kile kichaka na kuanza kutembea pale kijijini, Mzee sube alifurahi sana akarudi tena kwa mke wake na kuendelea kupiga story huku wakiwa wanasubiria uji uive il wanywe. Siku hiyo watu waliumwa sana na nyoka maana aliruhusiwa afanye kazi mpaka mchana Kwahyo watu wengi walikuwa kwa mfalme wakisubilia dawa ifike il wapone. Hali hiyo iliendelea kwa siku kadhaa na watu wengi walidhurika na wengine kupoteza maisha kutokana na kukosa kupata dawa kwa wakati. kwa upande wa mzee sube na mke wake wao walijitahidi kwa nguvu zao zote kusaidia wana kijiji lakini ile speed ya nyoka kuuma watu ilikuwa kubwa na kupelekea kushindwa kuwasaidia watu wote. Wazee wa kijiji baada ya kuona lile tatizo limezidi kuwa kubwa walikusanyana na kwenda kuzungumza na mfalme juu ya yule nyoka maana alikuwa amezid balaa.
MZEE.1: Mfalme tumekuja hata tunashida ya kuzungumza na wewe.
MFALME: kuweni huru wazee wangu mimi ninawasikiliza.
MZEE 2: Mtukufu mfalme sisi tumekuja hapa kwa ajil ya kuongelea kuhusu hili tatizo lilokumba hiki kijiji chetu cha mbaka kwasasa.
MFALME: Tatizo gan tena ?
MZEE 3: kuhusu huyu nyoka ambae amekuwa akisumba sana hapa kijijini kwetu.
MFALME: kweli huyu nyoka kwa sasa amekuwa tishio hapa kijiji kwetu ila mimi nimepata maelezo yote kuhusu huyu nyoka.
MZEE 2: Kwahiyo umeamua kufanya nini baada ya kujua kuhusu huyu nyoka.
Mfalme kabla ajajibu mara mzee sube akafika maana alipelekewa taarifa kuhusu kikao kilichopo kwa mfalme, mfalme baada ya kumuona mzee sube alijkuta na yeye akiwa anamtete yule nyoka.
Sehemu Ya 5
MFALME: KwelI huyu nyoka ni hatari sana ila hatakiwI kuwindwa maana atakuwepo hapa kwa mda tu na baadae ataondoka.
Maneno ya mfalme yaliwashangaza sana wale wazee maana wao walitarajia kuambiwa yule nyoka atafutwe na hauawe ila mfalme alisema kinyume kabisa na mawazo yao. Ila kwa upande wa mzee sube alifurahi sana kusikia mfalme akisema vile alijua moja kwa moja kafankiwa kuteka ufahamu wa mfalme. Wale wazee waliendelea kuongea huku mzee sube akiwa anawahudumia wagonjwa.
MZEE 1: Kwahiyo itabidi tuvumilie tu. angaliania mtukufu mfalme watu wanavyo umia ila kwa kuwa umeamua hivyo sawa sisi tumekulewa.
Wakamuaga mfalme na kuondoka zao huku wakiwa wamesononeka kutokana na jibu ambalo alikuwa ametoa mfalme. Siku hiyo mzee sube aliendea kufanya kaz yake na hatimae akamaliza na kurudi kwao na ile siku ikawa imepta. Siku kadhaa zilipita huku watu wakiwa wanaendelea kupata tabu na nyoka aitwae yoka ambae katumwa na mzee sube kwa ajili ya kijtafutia umaharufu pale kijijini kwake. Siku moja mchana kulikuwa na vijana kama watano wakiwa wanatembea wakielekea shambani kwao ghafla mmoja wao akang’atwa na yoka. Kitendo kile kiliwakasilisha sana wale vijana wengine na ndipo wakaanza kumkimbiza Yoka huku wakiwa wameshika fimbo na wengine panga pamoja na mawe. Vijana hao walijitahidi sana kumkimbiza lakini baada ya kumkaribia ghafla yoka akaingia kwenye kichaka Fulani, wote kwa pamoja wakakizunguka hiko ili nyoka asitoke sehemu ile na kuanza kuishambulia kwa kupiga mawe pamoja na zile fimbo walizobeba. walipomaliza kufanya hivyo mmoja kati yao akaanza kukatakata kile kichaka wakiamini wamefanikiwa kumuua yoka lakini kwa bahati mbaya waliambulia patupu. Walijiuliza mda gani nyoka ametoka maana hawakutegemea kuona kile walichokiona, lakini halikupatikana jibu zaidi ya kutazamana na kusikitika kumkosa adui wao mkubwa. Wakaondoka na wakarudi mpaka kwa yule mwenzao kisha wakamchukua na kumpeleka nyumbani kwa mzee sube kwa ajili ya kumfanyia matibabu, walipokelewa vizuri ndipo mzee sube akaanza kuwauliza tatizo japokuwa alikuwa anajua alifanya hivyo ikiwa kama kuwapumbaza na wasihisi kitu chochote kuhusu yeye na yule nyoka.
MZEE SUBE: Vijana huyu mwenzenu kapatwa na nini.
kijana mmoja akaanza kumsmulia jinsi ilivyokuwa.
KIJANA 1: Tulikuwa tunaenda shamban ila kwa bahati mbaya akatokea nyoka na kumbana mwenzetu, tukajitahidi kumkimbiza ili tumuuwe lakini kwa bahati aliingia kwenye kichaka na kutupotea kwa mzingra ya kutatanisha ndipo tukamchukua huyu mwenzetu na kumleta huku kwako kwa ajili ya kumfanyia matibabu.
Mzee sube alichukia sana aliposikia wale vijana walihitaji kumuua nyoka wake, akaingia ndani kuchukua dawa na kumpatia mgonjwa, Wale vijana walifurahi sana wakitegemea kumuona mwenzao akirudi kwenye hali yake ya kawaida. Mda mfupi wakielekea majumbani kwao hali ya mwenzao ikabadilika na kuwa mbaya zaidi ya mara ya kwanza, haraka waligeuza na kurudi nyumbani kwa Sube na kumkuta akiwa amekaa na mke wake, wakamueleza jinsi hali ya mwenzao ilivyobadilika, mda huo mgonjwa alikuwa amelazwa chini huku akipwitapwita kama kuku aliepigwa jiwe kichwani au kuchinjwa. akiwa kwenye hali ya kuangaika na maumizu makali ghafla alimuona nyoka mkubwa akiingia kwenye kichaka kilichokuwa karibu na nyumba ya mzee sube. Alitamani awaambie wenzake lakini kwa kuwa alikuwa mahututi alishindwa kuongea na kubaki akimuangalia Yoka kwa hasira mda mfupi mbele akakata roho, kumbe mzee sube aliwapa dawa tofauti ya kutibu sumu ya nyoka, alifaya hivyo ikiwa kama adhabu kutokana na kitendo walichokifanya cha kutaka kumuua Yoka. Jambo hilo liliwaumiza sana wale vijana na kuwa na hasiri ya kumtafuta yule nyoka kwa hudi na uvumba bila kujua kuwa mda ule alikuwa karibu yao. Wakamchukua yule mwenzao na kwenda kumzika kisha wakaenda mpaka kwa mfalme kwa ajili ya kuomba kufanya mkutano wa kijiji kizima kwa ajli ya kupanga mipango ya kumuangamiza yule nyoka. Walipofika wakamueleza shida yao na hatimae mfalme akawakubari ndipo ikapangwa siku rasmi ya kufanyika huo mkutano. Siku hiyo ilipofika watu walikusanyika kwa wingi nyumbani kwa mfalme maana kila mtu alipata taarifa ya kuwepo kwa hiko kikao na alichoshwa na matatizo wanayoyapata kutoka kwa huyo nyoka. Mda ulipofika kikao kikaanza huku viongozi wote wa kijiji wakiwemo bila kumsahau mzee sube, Mfalme akasimama kuanzisha mkutano rasmi.
MFALME: Ndugu wanakijiji cha mbaka tumekutana hapa kwa ajili ya kujadiri hili swala lilitupata ambalo limekuwa likitunyima raha pia limetufanya tusiishi kwa maani . Nahisi wote munajua nini tatizo lilipo hapa kijijini kwetu kwa sasa kwahiyo kuanzia sasa hivi nafungua mkutano rasmi na nani ruhusu mtu kutoa wazo pia na ruhusu mtu kupinga wazo ila kwa viongozi tu.
Mfalme akaa chini huku watu wakiwa wanampigia makofi kutokana na kile alichokiongea, mzee mmoja akasimama na kuanza kutoa mawazo yake.
MZEE: Mtukufu mfalme nina wazo moja kama litakuwa zuri naomba lifanyiwe kazi. Mimi ninaona bora huyu nyoka tumtengeneze mtego ambao utamnasa kama tulivyofanya kwa baadhi ya watutu hatari ambao walikuja hapa kijijini kwetu, hilo ndio wazo langu.
Mzee aliposema vile watu wote walipiga makofi mpaka na mzee sube mwenyewe, zamu za viongozi kukubali au kupina ikafika, kila kiongozi aliko mbele aliongea na kulikubali lile wazo mpaka mzee sube maana alikuwa anajua hakuna awezae kumtega Yoka akafanikiwa kumpata, lakini mke wake alishangaa kuona Sube akilikubali lile wazo maana yeye alikuwa afahamu nini mume wake aliwaza. Mtu mwingine akasimama kutoa wazo lake.
KIJANA: Mtukufu mfalme wazo langu ninaona bora ikifika usiku tuanze kumtafuta maana yeye uwa anadhuru sana usiku kuliko mchana kwahiyo inamaansha kuwa usiku ndio rahisi kumpata, hilo ndio wazo langu.
Mzee sube baada ya kusikia vile akasimama na kuanza kuipinga lile wazo la ya yule kijana maana aliona wakifanya hivyo itakuwa rahisi sana kumkamata yoka maana huwa anaenda mbali sana na eneo lake majira ya usiku kwahiyo wanaweza kumkimbiza na hatmae wakamkamata. Baadhi ya watu walishangaa kuona mzee sube amepinga lile wazo ila mfalme aliona kawaida maana alikuwa anamsikiliza sana mzee sube.
MFALME: Jamani wanakijiji huyu ndie tabibu wetu pia ni mzee wetu kwahiyo yeye anajua mambo mengi kuliko sisi ni vizuri endapo akisema kitu tumsikilize maana hata mimi nimeona hilo wazo sio zuri kwetu.
Vijana wengi walisikitika kusikia mfalme akiumuunga mzee sube, ndipo kijana mmoja akasimama na kuanza kutoa wazo lake.
KIJANA 2: Mtukufu mfalme pamoja na wanakijiji wote wazo langu naona tungepita kila sehemu kwenye kichaki tuviondoe maana tukifanya hivyo nyoka hatakuwa na sehemu ya kakaa na atakuwa anazunguka zungika na ndio itakuwa rahis kumuua.
Wazo la huyo kijana lilipendwa na kila mtu mahara pale mpaka mfalme mwenyewe lakini ilikuwa tofauti kwa mzee sube, maana hakupiga makofi kuonyesha kuunga mkono lile wazo wala kutabasamu jambo ambalo liliwashangaza sana viongozi wenzake. Mfalme akasimama na kumpongeza lile wazo lilitolewa.
MFALME: Kijana hongera sana kwa kutoa wazo zuri kiasi hiki nimefurahi sana na tutaanza kulifanyia kazi wazo lako ili tuone mafanikio yake.
Mfalme akaa na kupisha viongozi wengine waonge kuhu lile wazo, kila aliesimama alilipongeza na kushauri lianze kufanyiwa kazi wazo hilo lakini ilikuwa tofauti ilipofika zamu yam zee sube kutoa maoni yake juu ya wazo lile.
MZEE SUBE: Jaman mimi nilikuwa sijui kuwa vijana wa hiki kijiji chetu ni wajinga na wapumbavu kiasi hiki yani wanapitwa mawazo na wazee. Hivi unaonaje mtu aje nyumbani kwako kuaribu nyumba yako utamuacha kweli hata kama atakuwa na upanga lazama utajitahidi kadri uwezavyo kumzuia kufa hivyo hii ndio itakavyokuwa kwa hiyo siku mutakayo anza kuondoa hivyo vichaka . maana yule nyoka awezi kukubali kuona munaharibu nyumba yake kwahiyo ataanza kuwauma na hatimae mukapata madhara ya kujitakia.
INAENDELEA

