Nisaidieni Jamani, Sijawahi Kukutana Na Kitu Kama Hiki Maishani Mwangu
Niko kwenye mahusaino na huyu Kaka hii ni wiki ya pili sasa. Niliunganishwa na rafiki yangu ambaye naye nilikutana naye kwenye mitandao mwaka jana, basi tukawa tunachart mpaka kuaminiana.
Kuna siku akanipost status akaniambia kuna Kaka yake kanipenda anaomba namba. Nilimuambia ampe, akampa, basi huyo kaka anaomba tuonane, tukaonana, tangu siku hiyo, yeye kila siku ni kunipost kwenye mitandao, kuniita mke wangu, ananipigia simu kuniamsha, mchana kuulizia kama nimekula na usiku tunaongea hata masaa 5.
Kaka anaonyesha kunipenda, kashanipa mpaka simu niongee na Mama yake, anawaambia kuwa mimi ndiyo mke wake. Analalamika kuwa haumizwa sana hivyo hataki na mimi nimuumize, anajali mpaka naogopa Kaka.
Juzi alikuja mpaka nyumbani, hakuniambia kama anakuja kujitambulisha ila kwakua nilishamuelekeza alinipigia simu kuwa yuko nyumbani, basi nikamkaribisha na kumtambulisha kwa Mama, anaongea mambo mengi, mipango ya ndoa, ananiambia kuhusu mali zake, anajenga kanipeleka mpaka kwenye nyumba yake ambayo anajenga.
Kanionyesha gari yake kila kitu anasema chetu. Sababu ya kuja kwako Kaka ni hivi, jana tulikua tunaongea, akaniambia anataka tumalizie nyumba yetu ili tuone hataka kwani hataki kuishi nyumba ya kupanga. Ananiambia kuwa anahitajika kama milioni 16, mimi ninazo na anajua kwani kwakaua likua ananiambia kila kitu nilimuambia hiyo ni pesa nilikusanya kwaajili ya gari.
Nikamuambia mimi siwezi kwakua ni kwaajili ya gari basi kakasirika, akaniambia naonekana kama sitaki kuolewa, yaani ananiambia mimi mbinafsi, sitaki kushirikiana naye. ananiambia niko kama X wake aliachana naye kwakua nimbinafsi, sasa hapo Kaka nashindwa nifanye nini, nimeshampenda, anaonyesha kunipenda ananiambia hajali kuhusu pesa hata tukibadilisha kiwanja kuandika majina yangu yeye hajali kwani ananipenda.
Naogopa kwani ndiyo kwanza tuna wiki mbili lakini kashafanya mambo mengi sana Kaka, nisaidie! Ukichelewa kupoke simu basia anumia anaweza hata kulia!


4 Comments
Dah hapo unataka kuumizwa mpaka uchanganyikiwe, wewe mtu kama anakupenda hawezi kulazimisha utoe mil 16 zako et mnajenga anaweza akandanganya hata Kwa kufoji
Hey! This is kind of off topic but I need some guidance from an established blog. Is it hard to set up your own blog? I’m not very techincal but I can figure things out pretty quick. I’m thinking about setting up my own but I’m not sure where to start. Do you have any points or suggestions? Thank you
I love it when people come together and share opinions, great blog, keep it up.
I love it when people come together and share opinions, great blog, keep it up.