MWANAFUNZI MCHAWI
Sehemu Ya 21
Wakati huo mlinzi yule alikuwa akiwaza vitisho alivyotishwa na mwanamke yule pindi alipofika nyumbani pale.
‘Mh kumbeee ni mchawii’ aliwaza mlinzi.
“Ukweli upi” aliuliza Mr Aloyce kwa mshangao kwani katu hakujua kama kuna kitu kinaendelea nyuma ya pazia…
Mr Aloyce bado hakumuelewa vizuri mkewe kwa kauli aliyoisema. Kauli ile iliibua utata mkubwa kichwani mwake na kumtaka mkewe amueleze ukweli.
“Niambie mke wangu… Nini kinaendelea? Maana Mimi sielewi!” Alisema Mr Aloyce kwa sauti ya upole ili mkewe amweleze ukweli wote. Lakini kwa bahati mbaya sana Maimuna alisita kueleza ukweli ambao alitaka kumwambia Mr Aloyce.
Viboko mfululizo vilivyosikika kwa sauti kubwa vilimshukia Maimuna na kumfanya ahangaike kupita kupita kiasi. Aligalagala pale chini kama nyoka aliyepondwapondwa kichwa chake. Sauti na yowe la kilio viliibuka kwa Maimuna kwani alishindwa kuvumilia maumivi ya viboko alivyochapwa na MTU asimfahamu.
“Nasemaaa!nasemaaa!” Alisema Maimuna huku akilia.
Mr Aloyce na Mlinzi wake walibaki na mshangao kwani kila walichokiona walihisi ni muujiza tu. Walibaki kimya huku wakimshangaa mwanamke yule.
“Aloyce… Mimi ni mchawiiii..” Alisikika Maimuna na kwa bahati mbaya sana alishindwa kuongea kwa sauti ndogo hivyo sauti ilipaa sana na kuwafanya wapita njia na majirani kujazana sana nje ya geti kwa Mr Aloyce. Kwa uzito wa adhabu alioipata Maimuna ilimbidi tu aseme ukweli wote uliomwacha mdomo wazi Mr Aloyce.
“Naitwa Maimuna.. Sio mama yake Eddy kama ulivyodhani…” Alisema Maimuna na kumfanya Aloyce ahamaki. Alichanganyikiwa sana na kushindwa kuzungumza.
“Nisamehe Aloyce… Nilikuja kuiteketeza familia yako…. Mkeo alishaliwa nyama … Mimi nilikuja kumlinda Eddy ili sehemu zake za siri zibaki mikononi mwa Doreen”
“What? Ati nini? Kwanza Doreen ni nani?” Mr Aloyce alijikuta anauliza maswali matatu mfululizo huku hasira zikiwa zimempanda kupita kiasi. Alitamani achukue jiwe zito na kumponda nalo mwanamke yule.
“Ni mchawi… Alikuwa anasoma na Eddy…” Alisema Maimuna huku akilia kwa sauti kubwa.
“Oh! Shit!” Alisikika baba Eddy.
Watu waliokuwa pale nje walizidi kutafuta upenyo wa kuingia mle ndani. Lakini geti lilikuwa limefungwa, kelele nyingi kutoka nje zilizidi kusikika.
“Mchawiiiiii! Mchawiii! Tufungulie tumwadhibu huyo mchawiiii!! Funguaa! Mwanamke mchawi hafai kuishi!!” Sauti zile kutoka nje zilimhamasisha mlinzi kufungua geti na kuwaruhusu watu waingie. Cha ajabu watu wale waliingia wakiwa wameshikilia silaha za aina mbalimbali. Wengine mawe wengine visu huku wengine wakiwa wameshikilia fimbo na mapanga. Hali ilichafuka sana pale ndani.
Umati wa watu ulikuwa uvamia uwanja wa Mr Aloyce tayari kwa kumwadhibu mchawi aliyesababisha kilio na majonzi katika familia ya ile iliyokuwa imejaa upendo na amani hapo awali.”Tuue tu… Afe Huyo” walisema. Ghafla Maimuna akabadilika na kuwa kiumbe tofauti na vile anavyofahamika wote wakashtuka.
*****
Doreen aliendelea kushangaa kwa hofu sana ndani ya chumba kile. Upepo mkali uliovuma chumbani mle na kuangusha baadhi ya vitu vilivyokuwa vimewekwa vizuri ulimfanya Doreen ajione mdogo kama sisimizi juu ya janga lile.
Akiwa bado haelewi la kufanya ghafla sura ya MTU aliyemfahamu ikatokea mbele yake na kumfanya Doreen apigwe na mshangao wa hali ya juu.
“Haa! Dorice!” Alisikika Doreen akiita kwa mshangao.
“Mimi hapa! Sema nikusikie!” Alisema Dorice kwa sauti iliyojaa dharau kupita kiasi. Kisha kabla hajaendelea na lolote akanyoosha kidole chake ukutani na ghafla kikatokea kama runinga pana iliyoonesha siku ambayo Doreen alimpaka kamasi usoni kiuchawi ili asipendwe na Eddy. Kisha akaonekana Doreen akimkata Eddy sehemu zake za siri.
“Ulikuwa mjanja sana sio?” Alisema Dorice. Doreen hakuamini macho yake alitetemeka kwa hofu kupita maelezo.
“Do..Dor…Dorice… Umepata wapi huo ujasiri wa kunitisha kiasi hicho?” Aliongea Doreen kwa kigugumizi sana. Dorice alimtazama Doreen na kucheka kidogo huku akitembeatembea ndani ya chumba kile.
“Ulininyang’anya penzi langu kinguvu kwa mtu nimpendae sana.. Cha ajabu ulitaka kumharibia yeye na familia yake… Kwanini wewe in katili na mbaya kitabia kuliko sura yako?” Aliuliza Dorice.
“Tafa..Tafadhali Dorice
nisamehe..”
“Nimekusamehe tangu zamani… Ila nataka kukufunza adabu. Umeua wengi sana wasiokuwa na hatia umewaharibu wengi sana bila kosa.” Alisema Dorice na kutoweka machoni mwa Doreen.
Doreen alichanganyikiwa mno, lakini kilia alipotaka kupotea na kumtoroka Dorice hakuwa na nguvu, kwani Dorice alikuwa na nguvu nyingi mno ambazo zilimsaidia kufanya kila alichokitaka. Na hakuna mchawi ambaye angeweza kumshinda Dorice kwa wakati ule.
Ghafla bin vuu! Kichapo kikali kikamshukia Doreen. Alihisi mawe mazito yanamshukia kichwani mwake na kumpiga kwa nguvu. Alihisi maumivu makali mno. Akapiga ukunga mkali baada ya kushindwa kuvumilia maumivu Yale. Hakuona sababu ya yeye kuendelea kukaa ndani ya chumba kile huku akitaabika akaamua kufungua mlango na kutoka nje ya chumba huku akilia kwa sauti kali . kilio chake kiliwashtua wengi na kuwafanya watoke njee kutazama kulikoni.
Umati wa watu ulifurika kumtazama Doreen pale nje. Alikuwa uchi wa mnyama huku akipiga kelele sana.
“Naacha uchawiii… Mimi si mchawi…uwiiiii… Nisaidieni” alilalama huku akipiga mbio bila kujali kuwa hajavaa nguo yoyote.
Watu walianza kumfuata huku wakipiga kelele “mchawii! Mchawiiii” “masikini we! Binti mzuri hivi kumbe ana mambo ya uchawi?” Walisikika watu wakiongea vikundi vikundi.
Watu walikazana kupiga picha huku wengine wakiokotw mawe na kumfukuza Doreen huku wakimtupia mawe.
Doreen alikimbia sana huku akipiga kelele sana.
Ghafla mama mmoja alipiga kelele sana
“Huyu mtoto aliinibia pesa zangu mgahawani kumbe ni mchawi! Alaaniwe!”
“Mimi alikuja dukani kwangu akataka aniwangie Leo ameumbuka” walizungumza yule mama wa mgahawa ambaye alitapeliwa na Doreen kwa mazingira ya kutatanisha sana ndipo alipojibiwa na mwanaume mwingine ambaye Doreen alijaribu kumuwangia ili aibe pesa.
Doreen alizidi kupiga mbio sana huku umati ule wa watu mjini Iringa ukizidi kumfata kwa kasi wakiwa wameshika mawe na wengine viboko.
*****
Baba Pamela alikuwa ametulia kidogo huku akimtazama binti yake kwa masikitiko makubwa.
“Daddy najisikia hasira hata kumtazama mama” alisema Pamela huku akilia.
“Hutakiwi kuwa hivyo… Nataka tufanye jambo hapa!”
“Jambo gani mume wangu?” Aliuliza mama Pamela.
“Nataka tumwombe Mungu mpaka atujibu juu ya binti yetu”
“Hakuna tatizo mume wangu..” Alisema mama Pamela kwani tayari maneno ya mumewe yalimpa nguvu hata ya kuzungumza.
“Pamela una amini kama Mungu anaweza kutenda mambo ambayo sisi hatuwezi?”
“Ndio naamini… Lakini…”alisema pamela
“Lakini nini? Ukiwa na imani hutakiwi kutilia shaka..”
“Sawa baba niombee tu..”
Baba Pamela aliwataka wote wapige magoti kisha wakaanza na nyimbo na baada ya hapo akaanza kufanya maombi. Aliomba sana akiwa anataka Mungu amrudushie mwanae titi lake.
Radi Kali zikaanza kupiga katika nyumba zilipiga radi nyingi wakati baba Pamela akiendelea kusali kwa bidii na imani sana. Ghafla akawaambia watoke nje wote.
“Roho wa Mungu ananiambia kuna kitu kimefukiwa pale nje ili kutuangamiza” alisema baba Pamela kisha wote wakatoka nje. Baba Pamela aliongoza njia mpaka Pale ambapo Mama Pamela alifukia sahani iliyokuwa na kinyesi. Wakafukua.
Cha ajabu akatokea nyoka mkubwa sana ambaye hakuna aliyetarijia kama angekuwa pale.
“Mungu wangu!” Alisikika Mama Pamela akizungumza kwa woga. Baba Pamela alizidi kumwomba Mungu mpaka yule nyoka alipobadilika na kuwa na sura ya Doreen lakini mkiani akabaki kuwa nyoka. Wote walistaajabu sana huku wakitetemeka kwa woga…
….”Ina maana Doreen ni mchawi kiasi hiki?” Alijikuta anaropoka kwa mshangao mama Pamela. Pamela alizidi kushangaa huku akimtazama mama yake kwa mshangao kisha akimtazama chatu yule mwenye sura ya Doreen. Baba Pamela aliendelea na maombezi yake kwa imani kali. Yule chatu alijigeuza geuza kwa vitisho vikali sana huku akijaribu kupambana Na Baba Pamela kwa kujitoa kwenye lile shimo dogo.
Sehemu Ya 22
….”Ina maana Doreen ni mchawi kiasi hiki?” Alijikuta anaropoka kwa mshangao mama Pamela. Pamela alizidi kushangaa huku akimtazama mama yake kwa mshangao kisha akimtazama chatu yule mwenye sura ya Doreen. Baba Pamela aliendelea na maombezi yake kwa imani kali. Yule chatu alijigeuza geuza kwa vitisho vikali sana huku akijaribu kupambana Na Baba Pamela kwa kujitoa kwenye lile shimo dogo.
Lakini kwa bahati njema chatu yule alipigwa na radi Kali sana iliyoharibu uso wake na kuweka mipasukopasuko iliyoacha damu ichuruzike kirahisi. Baba Pamela hakuacha kuomba na kuithibitisha imani yake thabiti. Ghafla ukatoka moshi mkali kutoka kwenye mdomo wa sura ya Doreen iliyopo kwa yule chatu.
Moshi ule ulikuwa wa ajabu sana Kwani ulikuwa katika mstari ulionyooka mpaka kifuani kwa Pamela, na hata Pamela alipojaribu kukimbia moshi ule ulimfuata kila alipoenda na kumfanya Pamela aogope zaidi. Pamela alipoona hawezi kuukwepa moshi ule akasimama wima akisubiri kuona kitakachotokea huku akihema nguvu sana.
Moshi ule ulitua taratibu kifuani kwa Pamela kisha ule mstari uliokuwa umejitengeneza ukapotelea kifuani kwa Pamela taratibu sana. Pamela alijishangaa sana Kwani alihisi mabadiliko Fulani mwilini mwake. Alitulia kimya huku akimtazama baba yake.
Baba Pamela alipohitimisha maombi yake yule chatu alipigwa radi Kali kisha akatoweka machoni kwa wanafamilia wale.
“Jina la Bwana lihimidiwe kwani ametenda tulichokitaka.. Amejidhihirisha mbele yetu.. Oh asante Bwana wa Majeshi” alisikika baba Pamela huku akiinua macho yake na mikono yake juu ili kumshukuru Mungu kwa ajili ya maombi yake.
“Pamela hebu jitazame kifuani kwako” alisema Baba Pamela huku akitabasamu na kutoa kitambaa laini mfukoni na kujifuta jasho lililokuwa limetapakaa usoni kwake kama chemchem ya maji.
Mama Pamela alimsogelea mwanae na kumsaidia kushuhudia kilichotokea kifuani kwake. Walisogea pembeni kidogo, kisha Pamela akajifunua shati lake na kujitazama kwa umakini. Wote hawakuamini kilichotokea kwani titi lake lilikuwa limerudi kama lilivyokuwa. Pamela alishtuka sana na kupiga kelele za shangwe huku akiruka kama ndama. Akamkimbilia baba yake na kumkumbatia kwa nguvu.
“Baba! Nashukuru baba! Asante!” Alisema Pamela kwa furaha kuzidi kiasi.
“No Pamela! Mshukuru Mungu sio mimi” alisema Baba Pamela huku akitabasamu.
Pamela alimuachia baba yake na kumfuata mama yake, chozi likamdondoka kwa uchungu huku akimkumbatia mama yake
“Nisamehe sana mama! Naomba unisamehe kwa kukufanya ukose amani na kujisikia vibaya kwaajili yangu. Nakupenda sana mama.. Nisamehe mama!” Alisema Pamela huku akilia kwa uchungu.
“Pamela mwanangu! Usijali kwa yote yaliyotokea nilishakusamehe” alisema mama Pamela huku akimkumbatia kwa mahaba mazito binti yake mpenzi.
Baba Pamela alisimama pembeni yao kisha akapiga hatua za taratibu na kuwasogelea.
“Mke wangu… Familia yetu ingekuwa pabaya sana kwaajili ya yule adui! Lakini ni funzo kwako kuwa usimwamini kila mtu pia jifunze kumcha Mungu kwa moyo wote”
“Ashukuriwe Mungu sana! Tangu Leo wote tutamcha Mungu” alisema Mama Pamela.
“Kweli kabisa.. Mungu ni mkuu” alisema Pamela kisha Wote wakakumbatiana kwa furaha, ile furaha ya mwanzo ikawa maradufu. Kila mmoja alionekana kufurahi sana ule umoja uliotaka kuvurugika ukarejea tena katika familia ile ikazidi kung’ara na kuwa familia bora.
“Hakuna wa kumfananisha na Mungu!” Walisema kwa pamoja huku wakiwa na furaha ya ajabu.
*****
Leyla alipokea ugeni kutoka kanisani kwake ambapo wanamaombi watano walitia timu nyumbani kwake na kuiikuta familia ile ikiwa imepoteza furaha kabisa.
Leyla aliwakaribisha wageni wake vizuri na kuwakaribisha viti.
Mwalimu John na Judith walikuwa wapo kimya tu ingawa moyoni mwao walifurahia ujio wa watu wale.
Leyla akaamua kuwaambia kila kitu kilichotokea ndipo Walipoanza maombi yao. Walijtahidi kusali kwa imani kubwa sana. Baada ya maombi ya kama SAA zima ndipo maombi yao yalipoanza kujibiwa. Mambo ya ajabu yalianza kutokea ambApo mwalimu John alianza kuzungumza lakini cha ajabu funza walianza kutoka tena miguuni.
“Kuna mtu ni mchawi hapa” alisema Mwalimu John na kuwafanya wote wastaajabu.
“Tulia mume wangu watu wanakusaidia…” Alisema Leyla akimwambia mumewe.
“Nasema kuna Mtu anaroga hapa… Atoke..” Maneno hayo ya Mwalimu John yaliwafanya wote watazamane na kusitisha maombi kwa muda. Mwalimu John aliendelea kuongea.
“Wewe acha kuroga maombi ya wenzako… Wewe! Nikuseme?” Alisikika mwalimu John wakati huo wote walikuwa wameinamisha sura zao chini wakiogopa kutajwa. Baada ya dakika kadhaa kupita Mwalimu John alimsogelea mwanamke mmoja na kumshika bega.
“Sema ukweli la sivyo hawa funza wanahamia mwilini mwako..” Alisema mwalimu John huku akimkazia macho mwanamke yule.
“Mi..mimi..nime.. Mimi..” Alibabaika yule mwanamke.
“Ukidanganya tu funza wanakuhamia…”
“Ahm..aah.. Kweli.. Nilitaka..nilikuwa naroga msiendelee na maombi..” Alisema yule mwanamke akiwa anaona aibu kupita kiasi.
“Haya tokaa” aliamrisha mwalimu John na yule mwanamke akaondoka haraka huku kila mtu akimtazama kwa mshangao.
Hawakupoteza muda maombi yakaendelea na hawakutumia muda mrefu sana funza kwa mwalimu John wakapotea wote. Na mara ile Judith aliona ulimi wake ukiwa mwepesi sana na akaweza kuongea. Mwalimu John alikuwa kama aliyetoka usingizini alishtuka mno kuona kila kinachoendelea.
“Jamani.. Doreen ulitaka kuniua? Kwanini Doreen?” Alisema mwalimu John.
“Doreen ni nani?” Aliuliza mwanamaombi mmoja.
“Ni mwanafunzi wangu… Ni mchawi sana alitaka kuniua na alinifanyia mambo ya aibu sana” mwalimu John akasimulia kila kitu kuhusu Doreen.
Judithi pia akaeleza kila kitu kilichompata Mwalimu Jason ambaye tayari alishafariki dunia.
“Oh poleni sana watumishi Mungu ni mwema… Cha msingi mumrudie yeye!”
“Amen!”
Hatimaye mwalimu John na Judith wakarudia hali ya kawaida na furaha yao ikarejea tena. Walimshukuru sana Mungu.
Mwalimu John alimsogelea mkewe na kumbatia kwa dhati na upendo.
“Asante kwa upendo wako wa dhati uliokufanya uwe mvumilivu mno kwangu… Nakupenda!” Alisema mwalimu John na Leyla akatabasamu tu.
Wanamaombi wale walishukuru Mungu na kuwasihi familia ile pamoja na Judith kutomuacha Mungu. Kisha wakaondoka zao.
*****
Doreen alipokuwa anakimbia ndivyo kadri kipigo kilipomzidia. Kwani aliadhibiwa sana na Dorice na wakati huohuo Mungu alikmwadhibu kupitia maombi ya watumishi wake waaminifu.
Doreen alihisi mwisho wake umefika. Alilia kwa uchungu huku akipiga hatua za kichovu kuelekea nyumbani kwa kina Eddy kama Alivyoambiwa na Dorice ili akajisalimishe na kuombs msamaha.
Safari ilikuwa ndefu kwa binti yule aliyeuwa watu wengi shuleni kwao na kuwadhuru walimu wake wasiokuwa na hatia
Hakuwahi kufika nyumbani kwa akina Eddy lakini alifika bila kupenda.
Umati wa watu uliokuwa nyumbani kwa mr Aloyce uliongezeka zaidi baada ya Doreen kufika pale.
Kulizuka hali ya tafrani katika eneo lile.
“Mimi ndo Maimuna halisi… Sio mama Eddy kama ulivyodhani..” Alisema Maimuna akiwa na sura mbaya kupita kiasi. Alikuwa ni mweusi mithili ya mkaa wa chunya, macho makubwa makali, mekundu kama pilipili, alikuwa na tumbo kubwa sana lililojaa michiriz, nywee zilikuwa chafu tena zimesokotana sana huku midomo yake mipana myeusi ikiyasitiri meno yake yaliyokaa hovyohovyo kinyani mwake.
Mr Aloyce aliishiwa nguvu, alishindwa kulia akadhindwa kuongea akabaki kimya amejiinamia.
Ujio wa Doreen na umati mwingine wa watu ukawa utata mwingine kwa Mr Aloyce.
“Nisamehe Eddy..
Alisikika Doreen akilia kwa sauti na wakati huo Eddy alikuwa anatembea taratibu kutokea ndani na kuja kymushuhudia kinachoendelea. Waandishi wa habari walikuwa wengi wakipiga picha tukio lile la ajabu.
…Eddy alisimama kwa muda huku akiyashangaa yote yanayoendelea. Alishindwa kuamini kama kinachoendelea pale kilikuwa na ukweli ndani yake. Alifuta macho yake na kutazama tena, safari hii macho yake yalitua moja kwa moja kwa Doreen aliyekuwa amepiga magoti mbele yake huku akilia kwa uchungu na majuto mengi.
“Nisamehe Eddy kwq kukufanyia ukatili huu. Nimekutesa sana wewe na familia yako… Nisamehe tafadhali” alisema Doreen huku akilia kwa uchungu hali iliyodhihirisha majuto aliyokuwa nayo moyoni mwake. Hata hivyo Eddy hakuweza kuzungumza chochote zaidi ya kumtazama Doreen kwa hasira huku machozi yakimtiririka machoni mwake.
Aliumanisha meno yake kwa hasira huku akitamani kuiondoa roho ya Doreen kwani mateso aliyompa maishani mwake ilikuwa ni vigumu kusahaulika. Mateso aliyokuwa nayo yalijaa fedheha na aibu isiyositirika. Machozi yalimshuka taratibu machoni mwake huku akimtazama Doreen.
“Naomba unisamehe Eddy ili adhabu ninayopata ipungue walau kidogo… Nateseka Eddy” Doreen alizidi kumsihi Eddy lakini maneno yake ilikuwa ni kama kujilisha upepo kwani Eddy hakuukubali msamaha wake.
Wanawake waliokuwepo eneo lile walijisikia aibu kwa kuona wanawake wenzao wapo uchi wa mnyama. Wakatoa khanga zao na kuwapa akina Doreen wazivae lakini hata hivyo ilikuwa vigumu kwa akina Doreen kupokea khanga zile kwani maumivu yalikuwa Makali mno kwenye miili yao. Kila Mara walihisi moto ukiwawakia katika ngozi zao. Ikawabidi wanawake wale wawafunike kwa lazima ili kuwasitiri.
Ghafla mwili wa Maimuna ukaanza kubadilika na kuwa mweusi kama mkaa. Akajiviringa viringa kama nyoka pale sakafuni huku akitoa mlio kama wa mbuzi kisha akatoweka mbele ya macho ya watu. Wote waliogopa sana, baadhi ya watu walijikaza kisabuni na kuendelea kubaki pale huku wengine wakikimbia sana na kuondoka eneo lile.
Doreen alibaki pale huku akiendelea kumsihi Eddy amsamehe. Lakini Eddy alikuwa na moyo mgumu sana wa kumsamehe kiumbe yule.
“Hustahili kuishi Doreen… Kufa tu..” Alisikika Eddy kwa sauti iliyojaa hasira.
“Kweli! Afe tu huyu! Tumuue!” Walisikika Raia waliokuwepo eneo lile.
“Nitakufa ndio ila naomba unisamehe.. Najua nimekukosea sana… Sitaki nife kabla hujanisamehe!” Alisema Doreen.
“Kwa mateso uliyonipa siwezi kukusamehe… Umenitesa sana… Sijui nani amekuadabisha namna hii na kukudhalilisha hivi… Amenifurahisha sana” alisema Eddy kwani hakujua lolote linaloendelea kuwa Dorice ndiye aliyefanya yote hayo.
“Na kwa jinsi ulivyonifanyia.. Daima siwezi kumwamini mwanamke! Naapa!” Alisema Eddy lakini kuna sauti ilimnong’oneza masikioni mwake
“Usiseme hivyo… Niamini Mimi” Eddy alishtuka sana akaangaza macho huku na kule pasipo kuona mtu aliyemnong’oneza. Sauti ile haikuwa ngeni sana masikioni mwake ila alishindwa kujua ilikuwa ya nani. Akatafakari kwa muda kisha akaipotezea sauti ile na kuendelea kumtazama Doreen.
“Eddy hutaki kunisamehe?” Aliuliza Doreen kwa sauti ya upole. Eddy akatafakari kidogo, akagundua kutomsamehe binadamu mwenzake ni kosa kubwa kwani yeye hutenda dhambi nyingi lakini husamehewa na Mungu.
“Nimekusamehe.. Ila sitokusahau!”
“Asante…”
Wakati akizungumza hivyo ghafla haja ndogo ilimbana sana Eddy, hakuielewa hali ile kwani tangu sehemu zake za siri ziondolewe hakuwahi kubanwa na haja ndogo hata Mara moja. Eddy alijishangaa sana akaamua kukimbia na kwenda msalani ili kuona kama angeweza kutoa taka mwili inayojulijana kama mkojo.
Alipofika chooni alishusha kidogo suruali yake na bila kutarajia akakuta sehemu zake zimerudi. Eddy hakuamini macho yake, akataka kujihakikishia kama kweli zitafanya kazi. Akakojoa na kweli jaribio lake likazaa matunda kwani alifanikiwa kukojoa kwa Mara ya kwanza.
“Mungu wangu! Mbona siamini!” Alisema Eddy kwa mshangao na furaha ya ajabu. Akajikuta anaruka ruka kule chooni shangwe kuu. Ghafla akahisi kuna mtu nyuma yake, Eddy akageuka haraka na bila kutarajia akakutana na uso uliojaa tabasamu wa Dorice.
“Eddy mpenzi nakupenda sana.. Nimefanya yote Haya kwaajili yako… Ili uone thamani ya upendo wangu.. Narudia tena niamini Mimi! Nakupenda!” Alisema Dorice. Eddy alibaki kimya akiwa ametoa macho kwa mshangao.
“Wewe ni jini”
“Hapana!”
“Sasa umefikaje hapa”
“Sina nia mbaya.. Nilitaka tu nikusaidie kwa tatizo lako… ” alisema Dorice.
“Asante sana… Nashukuru Dorice… ” alisema Eddy na kumkumbatia Dorice bila woga.
“Unanipenda?”aliuliza Dorice.
“Nakupenda sana!” Alisema Eddy kisha wakakutanisha midomo yao na kupeana mabusu. Licha ya kwamba Dorice alifahamu fika kuwa kufanya vile lilikuwa kosa kubwa sana kwa Mansoor lakini hakujali hilo kwani upendo wake wote ulikuwa kwa Eddy, alimpenda kupita kiasi.
“Wewe ndo mwanaume wa maisha yangu Eddy… Tangu nimekutana nawewe siku ya kwanza na ukanambia unanipenda sikutamani uniache hata kwa sekunde moja” alisema Dorice kwa sauti iliyojaa huba.
“Nakupenda pia Dorice… Wewe ni mwanamke pekee uliye kwenye ndoto zangu” alisema Eddy.
“Asante Eddy nitakuja wakati mwingine” alisema Dorice na kupotea.
“Doriiiiiice! Usiache kuja” alisema Eddy kwa sauti lakini Dorice alikuwa ameshaondoka.
Eddy alitoka nje akiwa na furaha sana. Alitamani hata kumwonesha kila mtu sehemu zake za siri ili ajue kuwa anazo.
Alipofika pale nje alikuta Doreen anavuja damu sana kwani wananchi walishaanza kumtupia mawe. Polisi walikuwa wamefika tayari eneo lile na kumchukua Doreen ili asiumizwe zaidi. Kwa mbali alionekana Dorice akimtazama Doreen na kumwambia kuwa yeye ndiye aliyefanya yote Yale. Lakini alipokuwa akizungumza hakuna aliyemwona zaidi ya Doreen na Eddy.
Doreen alichukuliwa na gari ya polisi na kupelekwa hospitali ili akatibiwe majeraha yake.
Lakini hata hivyo watu wengi walifika mpaka hospitali ingawa hawakuruhusiwa kuingia.
Doreen alianza kusaidiwa na madaktari , na baada ya kufungwa majeraha yake aliwaomba kitu madaktari.
“Kabla sijafa naomba mniitie mchungaji pamoja na waandishi wa habari” alisema Doreen kwa sauti ndogo iliyosikika kwa shida.
“Bado haupo vizuri… Unatakiwa kupumzika…” Alisema daktari mmoja.
“Tafadhali dokta nitajitahidi tu… Lakini cha kwanza nataka nikutane na hawa watu kabla sijafa…” Alisisitiza Doreen.
“Unataka kuwambia nini?”
“Kwanza nataka nitubu.. Pili Nataka niwaambie watu siri nzito kuhusu maisha yangu” alisema Doreen na kuwafanya madaktari wale washawishike na kufanya kama walivyoambiwa.
Alitwa mchungaji wa kanisa Fulani kisha wakaitwa waandishi wa habari wa vituo vya televisheni pamoja na radio ili warekodi kile alichotaka kuzungumza Doreen. Wote walikuwa na hamu ya kusikia kile wanachotaka kuambiwa na Doreen.
Na wakati huohuo taarifa za kilichomtokea Doreen zilikuwa tayari zimesambaa nchi nzima kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
MWISHO…


9 Comments
Some really interesting points you have written.Aided me a lot, just what I was looking for : D.
Very interesting information!Perfect just what I was searching for!
Great line up. We will be linking to this great article on our site. Keep up the good writing.
I have learn several excellent stuff here. Certainly value bookmarking for revisiting. I surprise how so much attempt you set to make such a magnificent informative website.
Thanks , I have just been searching for info about this topic for ages and yours is the greatest I have discovered till now. But, what about the conclusion? Are you sure about the source?
Great write-up, I am regular visitor of one’s web site, maintain up the nice operate, and It is going to be a regular visitor for a lengthy time.
I like this site very much, Its a rattling nice position to read and obtain info . “Do pleasant things yourself, but unpleasant things through others.” by Baltasar Gracian.
You really make it appear really easy together with your presentation but I to find this matter to be really one thing that I feel I might by no means understand. It kind of feels too complex and very extensive for me. I am having a look ahead in your next post, I?¦ll attempt to get the dangle of it!
Very interesting info !Perfect just what I was searching for! “The whole point of getting things done is knowing what to leave undone.” by Lady Reading.